Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mincks Group of Schools Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp
MAAGIZO
  1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani.
  2. Tia sahihi yako kasha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  3. Andika insha mbili
  4. Swali la kwanza ni la lazima
  5. Kasha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizoakia.
  6. Kila insha isipungue maneno 400.
  7. Kila insha ina alama 20
  8. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE.

SWALI

UPEO

ALAMA

1

20

 
 

20

 

JUMLA

40

 

MASWALI

  1. LAZIMA
    Wewe ni mhariri wa gazeti la Angaza.  Andika tahariri kuhusu umuhimu wa wanafunzi kushiriki katika michezo na masomo mengine yasiyokuwa ya kiakademia.
  2. Maovu ya kijamii yamekithiri sana miongoni mwa vijana.  Eleza chanzo na upendekeze hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kusitisha maovu haya.
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha matumizi methali ifuatayo:
    Jifya moja haliinjiki chungu
  4. Andika kisa kinachoanza kwa maneno haya.
    “Umeletwa hapa na wasamaria wema.” Sauti ikanieleza.  Nikavuta kumbukizi

MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA

KIDATO CHA NNE
Mwongozo - insha 102/1

  1. Hii ni insha ya tahariri
    Sura ya tahariri idhihirike
    GAZETI LA ANGAZA
    ALHAMISI, OKTOBA 10, 2022
    TAHARIRI KUHUSU UMUHIMU WA MICHEZO NA MASOMO YASIYO YA KIAKADEMIA
    Maudhui
    Baadhi ya maudhui/hoja
    1. Huimarisha afya ya wanafunzi
    2. Huwasaidia kutumia muda wao vizuri
    3. Huwawezesha kukuza vipawa vyao
    4. Huwachangamsha baada ya siku nzima ya masomo hasa darasani
    5. Huwakutanisha na wanafunzi wa shule nyingine
    6. Huimarisha uhusiano kati ya wanafunzi na walimu wao.
    7. Huwafungulia milango ya ajira
    8. Hukuza uwajibikaji na uongozi miongoni mwa wanafunzi
    9. Huwasaidia kuwasilisha jumbe hasa kupitia mashindano ya muziki na drama
    10. Huwasaidia kuimarika kimasomo hasa kupitia mashindano ya sayansi na teknolojia.
      Mtahini aeleze angalau hoja nane.
  2. Maovu ya kijamii yamekithiri sana miongoni mwa vijana. Eleza chanzo na upendekeze hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kusitisha maovu haya
    1. Maovu ya kijamii.
      1. ndoa za jinsia moja
      2. Kuavya mimba
      3. Wizi wa mabavu
      4. Ubakaji
      5. Uasherati/usinzi
      6. Ndoa za mapema
      7. Wanafunzi kuchoma shule
    2. Chanzo cha maovu ya kijamii
      1. Uhaba wa kazi
      2. Ukosefu wa maelekezi
      3. Shinikizo la hirimu
      4. Umaskini /ukata
      5. Changamoto katika ndoa
      6. Ukengeushi
      7. Matumizi ya dawa za kulevya
      8. Ukosefu wa mbinu za kufidia muda mwingi walionao vijana
      9. Uigaji wa kiholela , tabia hasi
      10. Ushawishi potovu kutoka/kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
    3. Mapendekezo
      1. Ushauri nasaha utolewe kwa vijana kupitia asas mabalimbali za kijamii.
      2. Kuchukuliwe hatua kali za kisheria kama vile vifungo virefu , kutozwa faini.
      3. Kubuniwe jipo maalum la kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.
      4. Mtaala wa elimu uhusishe mafundisho maalum kuhusu tamaduni zenye umuhimu.
      5. Wazazi na asasi nyingine kuwaonya vijana dhidi ya kushiriki mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa.
      6. Kubuniwe sera za kudhibiti matumizi ya mitandao hasa miongoni mwa vijana.
      7. Viongozi wa kidini waadilishe jamii kupitia mafundisho maabadani.
      8. Vyombo vya habari vidhibitiwe na kuchuja yale ambayo vinawasilisha.
  3. Jifya moja haliinjiki chungu.
    Hii ni insha ya methali
    Mtahiniwa abuni kisa kitakachodhihirisha maana ifuatayo: hamna mtu anayefanya mamabo pekee akafaulu.
    Hivyo anaweza kutunga kisa kinachosimulia:
    1. Mtu aliyekataa kushirikiana na wengine kufanya mambo fulani na mwishowe akashindwa kufaulu.
    2. Ushirikiano katika jamii k.v shuleni, kijijini, nyumbani n.k ulioleta faida.
  4. Kisa kilenge kuokolewa kwa mkasa k.v ajali, ndoa za mapema, tohara n.k
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mincks Group of Schools Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?