KISWAHILI - KCPE 2020 PREDICTION 1 SET 1

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa maneno hapo chini. Chagua maneno yafaayo zaidi kujaza nafasi zilizo wazi:

Miji__ 1__nchini imekumbwa na__2__ la uchafu.__3__ wengi wamelalamikia jambo__4__.Wauzaji mboga wana__5__ la kufungwa kwa soko lao. Ukarabati__6__ masoko haya__7__ na ufisadi mwingi. Vita vya__8__. na askarikanzu__9__. Mambo haya yamerudisha biashara__ 10__.
KISWA 1

Salamu au__11__ni matendo __12__maneno ya __13__hali na kutakiana __14__ katika harakati za kila siku__15__.
KISWA 2

Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kila swali kulingana na maagizo yake:

  1. Neno karatasi liko katika ngeli gani?
    A. Li – Ya
    B. I- Zi
    C. U – Zi
    D. I-I
  2. Chagua sentensi iliyo na kiambishi po cha
    wakati.
    A. Kipofu huyo alifika saa sita.
    B. Alipopajenga ni pachafu.
    C. Alipofika alimpata akilala.
    D. Maegeshoni hapo panapendeza
  3. Maneno yenye maana sawa huitwaje?
    A. Vitawe
    B. Vitate
    C. Vitatanishi
    D. Visawe
  4. Jumla ya miaka mia moja huitwa
    A. mwongo
    B. alfeni
    C. karne
    D. kikwi
  5. Kamilisha sentensi kwa kiunganishi sahihi
    Kwetu kuna kila kitu_ _meli
    A. wala
    B. ila
    C. sembuse
    D. ingawa
  6. Badili katika kauli ya kutendeshwa;
    Wapangaji hutoa kodi.
    A. Wapangaji hutoshwa kodi.
    B. Wapangaji hutolezwa kodi.
    C. Wapangaji hutozwa kodi.
    D. Wapangaji hutolesha kodi.
  7. Chagua kielezi cha wakati;
    Hapo mwakani tutajiunga na shule mbalimbali
    za upili.
    A. hapo
    B. mwakani
    C. mbalimbali
    D. tutajiunga
  8. Katika sentensi "Aliniita kwa kunijuza", kwa
    imetumika kuonyesha
    A. nia
    B. mahali
    C.jinsi
    D. kifaa
  9. Kikembe cha nyuki ni
    A. kiluwiluwi B. buu
    C. jana D. kisui
  10. Kusema, "Tuliwatuza nao wakatutuza" ni
    kuonyesha kuwa
    A. walitutuza B. tulituzana
    C. tulituziana D. tulituzwa
  11. Andika ukubwa wa
    Mlango wake umefungwa
    A. Malango yake yamefungwa
    B. Jilango lake limefungwa
    C. Kilango chake kimefungwa
    D. Lango lake limefungwa
  12. Chagua kifaa ambacho hakifai kwenye orodha
    A. Mbuzi . B. Susu
    C. Dohani D. Fuawe
  13. Chagua sentensi sahihi kisarufi.
    A. Mtoto yule ni msafi.
    B. Mwindaji mhodari huwa hakosi windo
    C. Mwanafunzi aliyetuzwa ni huyu
    D. Kazi zenyewe inapendeza
  14. Adhuhuri ni wakati ambao
    A. watu hula kishuka
    B. watu hula chajio
    C. watu huamka
    D. watu hula staftahi
  15. Mtu ambaye hutunza na kuendesha farasi huitwa
    A. Saisi
    B. Chotara
    C. Mhazigi
    D. Mhazili

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali ya 31 - 40:

Kwa miaka mingi, jiji la Nairobi limekuwa likikumbwa na changamoto ya misongamano ya magari. Changamoto hii imeweza kuenea hadi miji mingine nchini hasa kutokana na ongezeko la idadi ya watu wanaohamia mijini. Hali hii huathiri vibaya uchumi wa taifa kwani muda mwingi hupotezwa katika msongamano, muda ambao
ungetumika vyema kwa shughuli za kuendeleza uchumi wa taifa.

Hivi majuzi Kaunti ya Nairobi ilichukua hatua kwa kuongeza ada ya kuegesha magari katikati ya jiji na maeneo mengine ambayo hukumbwa na misongamano ya magari. Hatua hii ililenga kupunguza idadi ya magari ya kibinafsi yanayoingia jijini kila siku.

Imedaiwa mojawapo ya sababu za misongamano ni kuwa kuna magari mengi yanayoingia jijini ilhali utakuta mengi kati yao huwa yamebeba mtu mmoja au watu wawili. Katika mataifa yaliyoendelea, uimarishaji wa mbinu za uchukuzi wa umma umechangia kupunguza misongamano ya magari. Mbinu bora za uchukuzi zimesababisha wasafiri wasiwe na tatizo kuacha magari yao nyumbani au nje ya mji na kutumia mbinu za uchukuzi wa umma kama vile basi na treni kuingia katikati ya jiji. Imedhihirika wazi hadi sasa
kwamba hata ada ya kuegesha magari ikiongezwa kwa kiwango kipi, walio na magari ya kibinafsi wataonelea
heri walipe ada hiyo kuliko kutegemea uchukuzi wa umma.

Hivyo basi, ni wajibu wa wataala katika serikali ya taifa na zile za kaunti kuanza kufikiria jinsi watakavyoshawishi wananchi kutumia mbinu za uchukuzi wa umma. Hii haitafaulu ikiwa bado magari ya umma yako jinsi yalivyo sasa ambapo hakuna uaminifu kati ya wasafiri na wahudumu wa magari hayo. Unaposafiri kwa magari haya roho yako i mikononi kwani utakuwa umejawa na hofu kutokana na jinsi yanavyoendeshwa kiholela. Ni sharti washikadau wote katika maeneo yote nchini wapanue mawazo yao ili kukabiliana na swala hili

  1. Kulingana na kifungu, msongamano wa magari
    A. umesababishwa na treni na magari ya kibinafsi
    B. umesababishwa na wasafiri
    C. umesababishwa na wahudumu wa magari
    D. umesababishwa na ongezeko la watu
  2. Maana ya 'roho mkononi' ni
    A. kutia moyo mkononi
    B. kuwa jasiri
    C. kuwa na woga
    D. kuwa na ushujaa
  3. Hatimaye, suluhisho la msongamano jijini ni
    A. abiria kutumia treni
    B. abiria kutohamia jijini
    C. kuimarisha uchukuzi wa angani
    D. kutumia mbinu badala ya usafiri kama treni
  4. Kwa nini jijini kuna msongamano wa magari?
    A. Kwa sababu ya utumizi wa treni
    B. Kwa sababu ya utumizi wa magari ya kibinafsi
    C. Kwa sababu ya uchumi wa taifa
    D. Kwa sababu ya mbinu bora za uchukuzi
  5. Kinyume cha kuhama ni
    A. kutoroka
    B. kuondoka
    C. kuhamia
    D. kukimbia
  6. Kauli ipi si sahihi kulingana na kifungu hiki?
    A. Wakazi wengi wa Nairobi hutumia treni kwa uchukuzi
    B. Magari ya kibinafsi huchangia mno msongamano
    C. Muda mwingi hupotezwa kwenye msongamano
    D. Ada ya kuegesha magari jijini iliongezwa
  7. Maoni ya mwandishi katika aya ya mwisho ni kuwa
    A. washikadau wawajibike
    B. wasafiri mara nyingi huwa na roho mkononi
    C. basi na treni huingia ndani ya jiji.
    D. mbinu bora za uchukuzi hupunguza msongamano wa magari.
  8. Kauli gani iliyo sahihi kwa mujibu wa taarifa?
    A. Wanaohamia mijini hupunguza msongamano.
    B. Kuacha magari nyumbani kutapunguza msongamano.
    C. Uchukuzi wa umma kwa treni unatumiwa na wengi..
    D. Ada ya kuegesha magari ni nafuu.
  9. Manufaa ya kutokuwa na msongamano ni
    A. wenye treni watafaidika.
    B. uchumi wa taifa utadhoofika.
    C. uchumi wa taifa utakuwa vyema.
    D. wasafiri na wahudumu watafurahia.
  10. Wenye magari ya kibinafsi
    A. wanapendezwa na hatua za serikali,
    B. hawaogopi ada mpya.
    C. ni wamiliki wa treni.
    D. huwabeba abiria zaidi ya watano

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 41 - 50:

Kuna wakati kasha kubwa lenye chupa za divai lilitumika kuingiza kokeini nchini Afrika Kusini. Kasha hilo kubwa lilikuwa na chupa 11600 za divai kutoka Amerika Kusini. Divai hiyo ilikuwa imechanganywa na kilogramu 150 hadi 180 za kokeni. Yaaminika kuwa hicho ndicho kiasi kikubwa zaidi cha kokeni kuwahi
kuingizwa nchini humo.

Ijapokuwa huenda ugunduzi huo ukaonyesha kwamba pambano dhidi ya dawa za kulevya linafaulu, ukweli ni kwamba polisi hupata asilimia kumi hadi kumi na tano tu ya dawa haramu za kulevya ulimwenguni. Hilo linasikitisha kwa sababu ni sawa na mkulima anayekata majani machache ya gugu hatari linalomea haraka na
kuacha mizizi yake ardhini.

Jitihada za serikali za kukomesha utengenezaji na uuzaji wa dawa za kulevya huzuiwa na faida kubwa inayotokana na uuzaji wa dawa hizo. Inakadiriwa kwamba dawa za kulevya zenye thamani ya mabilioni ya dola zinauzwa na kununuliwa kila mwaka nchini Marekani peke yake. Kwa sababu ya pesa nyingi zinazohusika, si ajabu kwamba polisi na maafisa wa serikali, hata wale wenye vyeo vya juu kutumbukia katika ufisadi.

Baadhi ya watu huteta ili dawa fulani za kulevya zihalalishwe kwa sababu wanajua kwamba vizuizi vya kisheria haviwezi kudhibiti dawa hizo. Kwa ujumla, wanataka kiasi kidogo cha dawa hizi kwa matumizi ya kibinafsi. Wanahisi kwamba hatua hiyo itasaidia serikali kudhibiti dawa hizo kwa urahisi na itapunguza faida kubwa za
wafanyabiashara maarufu wa dawa hizo.

Huku nchini Kenya, matumizi ya dawa za kulevya huchangia katika kulemaza uchumi. Hii ni kwa sababu vijana wengi ni waraibu wa dawa hizi za kulevya. Wengi wao huchukua muda wao mwingi katika ulevi badala ya kufanya kazi. Kunao wale ambao siha yao imedhoofika kutokana na matumizi ya dawa hizi za kulevya. Hatima ya vijana hawa huwa ni kuishi maisha ya uchochole na mwishowe huenda jongomeo wakiwa bado na umri mdogo.

Kuna vituo vilivyofunguliwa kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya. Waraibu hawa hupelekwa katika vituo hivi ili wasaidiwe kuacha kutumia dawa hizi za kulevya. Lakini, inasikitisha kwamba mara tu mraibu arejeapo nyumbani, kuna uwezekano mkubwa wa kwamba huenda akashawishiwa kuanza tena kutumia dawa za kulevya.

  1. Walanguzi waliweza kuingiza kokeini nchini Afrika Kusini kwa sababu
    A. waliweka chupa zilizokuwa na kokeni ndani ya kasha
    B. walisaidiwa na maafisa wa polisi
    C. walichanganya kokeini na divai
    D. kiasi cha kokeini kilikuwa kikubwa
  2. Kulingana na aya ya kwanza, ni bayana kuwa
    A. Kokeini iliingizwa Afrika Kusini mara moja tu
    B. ulanguzi wa dawa za kulevya katika Afrika Kusini haujawahi gunduliwa
    C. walanguzi wa kokeini duniani huishi katika nchi ya Afrika Kusini
    D. kokeini imewahi kuingizwa nchini Afrika
    Kusini zaidi ya mara moja
  3. Divai ilikuwa na umuhimu gani kwa walanguzi?
    A. Kuficha chupa zilizokuwa na kokeini
    B. Kufanya wasitambuliwe kuwa wanasafirisha kokeini
    C. Kupata darahima
    D. Kufanya kasha lisionekane
  4. Pambano dhidi ya dawa za kulevya halijafaulu kwa sababu
    A. polisi hajahawahi fanikiwa kunasa dawa zozote za kulevya
    B. kiasi cha dawa za kulevya zinazolanguzwa kinaongezeka
    C. kiasi cha dawa za kulevya kinachopatikana na polisi ni kidogo mno ,
    D. polisi wote ni wafisadi
  5. Katika aya ya pili, mkulima amemithilishwa na
    A. maafisa wa idara ya usalama
    B. walanguzi wa dawa za kulevya
    C. waraibu wa dawa za kulevya
    D. madhara ya dawa za kulevya
  6. Jambo linalofanya jitihada za serikali za kukomesha utengenezaji na uuzaji wa dawa za kulevya kutofanikiwa ni
    A. faida kubwa inayotokana na uuzaji wa dawa za kulevya
    B. uuzaji wa dawa hizi kwa njia ya siri
    C. ukosefu wa vifaa bora vya kugundua dawa hizi
    D. uchache wa maafisa wa polisi
  7. Polisi na maafisa wa serikali wanatumbukia
    katika ufisadi kwa sababu
    A. kuna pesa nyingi zinazohusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya
    B. wanashurutishwa na walanguzu wa dawa za kulevya
    C. hawalipwi mshahara wa kutosha
    D. wanataka watajirike haraka
  8. Kila mtu akiruhusiwa kuwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya basi
    A. thamani ya dawa hizo itaongezeka
    B. walanguzi wa dawa hizo hawataweza kupata faida kubwa
    C. matumizi ya dawa hizi itaongezeka
    D. watu wengi sana watakuwa waraibu wa dawa hizi za kulevya
  9. Maisha ya uchochole ni
    A. maisha ya uharibifu
    B. maisha ya uhalifu
    C. maisha ya umaskini
    D. maisha ya ubadhirifu
  10. Sababu haswa ya kufunguliwa kwa vituo vilivyotajwa katika aya ya mwisho ni
    A. kuimarisha matumizi ya dawa za kulevya
    B. kuidhinisha matumizi ya dawa za kulevya
    C. kuwagandamiza waraibu wa dawa za kulevya
    D. kupunguza matumizi ya dawa za kulevya

INSHA

Ufuatao ni mwisho wa insha. Ianze na uikamilishe huku ukifanya iwe ya kusisimua Zaidi.

……………. Hapo ndipo nikagundua ya kuwa mgema akisifiwa tembo hulitia maji.



MAJIBU

KISWAHILI SET 1 MARKING SCHEME

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI - KCPE 2020 PREDICTION 1 SET 1.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest