KISWAHILI - KCPE 2020 PREDICTION 1 SET 4

Share via Whatsapp

Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa

Tulipiga doria__ 1__ . Tulikuwa na silaha za kila aina mishale, mikuki, rungu, __2__ na ngao. __3__ ndizo zilizokuwa silaha zetu. Mipango yote ilikuwa imepangwa ikapangika. Tulimngoja nduli yule kwa tahadhari kubwe waama__4__ Usiku wa manane tulisikia vishindo. Tulizingira eneo hilo __5__ uangalifu. Wacha pazuke purukushani. Wezi wale_ 6_ kwa kuona maji yamezidi unga. Waliweka silaha chini na kuanza __7__. Hatukuwa na huruma. Tuliwatia pingu __8__ zilikuwa imara kama chuma. Tuliwasukuma __9__ hadi kituo cha polisi ambapo walifunguliwa mashtaka. Elewa kuwa uhalifu haulipi chochote.

Ufisadi si jambo __10__ kwetu sisi wakenya hata kidogo. Tangu_ 11_ umerudisha maendeleo nyuma. Ni jukumu __12__ kuukomesha. Kwa wale wapendao kutoa __13__ wafikishwe mahakamani na kufunguliwa mashtaka __14__ liwe funzo __15__ na wenzao wenye tabia kama hizo.

Kutoka swali la 16 hadi 30 chagua jibu sahihi

  1. Maneno yafuatayo yanafuatana vipi katika kamusi?
    (i) gingisa
    (ii) giniza
    (iii) gingiza
    (iv) gingizo
    A. (ii), (i), (iii)
    B. (iii), (iv), (i), (ii)
    C. (i), (ii), (iii), (iv)
    D. (i), (iii), (iv), (ii)
  2. Chagua orodha ya nomino zinazopatikana katika ngeli ya U-YA pekee.
    A. Ugonjwa, upweke, uchafu
    B. Uwele, upishi, uwaji
    C. Uto, ufa, upishi
    D. Ude, upweke, uchovu
  3. Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa
    "Uuwi! Nafa,” mkala alipiga unyende.
    A. Mkala alisema kuwa alikuwa anakufa
    B. Mkala alipiga unyende ati yuafa
    C. Mkala alipiga unyende akisema kuwa alikuwa akifa
    D. Mkala alilia kwa uchungu akisema kuwa anakufa
  4. Mahali au sehemu ya nchi kavu iliyozungukwa na maji pande zote huitwa
    A. kisima
    B. nchi
    C. bandari
    D. kisiwa
  5. Nomino kutokana na kitenzi husudu ni
    A. hasidi
    B. uhasama
    C. hasimu
    D. uhusudu
  6. Hamisi alikuwa na thuluthi ya muhogo. Aliugawa sawasawa kwa kakaze wawili kila mmoja alipata
    A. Sudusi
    B. Thuluthi mbili
    C. Tusui
    D. Subui
  7. Chagua sentensi yenye kwa ya kuonyesha jumla
    A. Niliandika kwa kalamu
    B. Tulienda kwa shangazi
    C. Watoto watano kwa saba ni wasichana
    D. Wazee kwa vijana walifika shereheni
  8. Rangi ya maji ya kunde ni sawa na:
    A. rangi ya hughurungi
    B. rangi ya machungwa
    C. rangi ya samli
    D. rangi ya zambarau
  9. Angebisha angefunguliwa. Hii ina maana:
    A. akibisha hatafunguliwa
    B. asipobisha atafunguliwa
    C. hakubisha wala kufunguliwa
    D. si sharti abishe ili afunguliwe
  10. ____! Nimeziacha funguo zangu nyumbani tafadhali nisaidie.
    A. Afanaleki!
    B. Pukachaka!
    C. Ole wangu!
    D. Shabash!
  11. Mwenye pupa hadiriki kula tamu ni sawa na
    A. Mvumbika mbichi hula mbivu
    B. Kinolewacho hupata
    C. Mwenda pole hajikwai
    D. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
  12. 'Po' imetumika katika sentensi
    Alipoenda alimkuta akila
    A. Kiwakikishi cha mahali
    B. Kiwakilishi cha ngeli
    C. Kiwakilishi cha nafsi
    D. Kiwakilishi cha wakati
  13. Sayari kubwa sana kuliko zote ni:
    A. Mshtari
    B. Zebaki
    C. Zohali
    D. Utaridi
  14. Udogo wa sentensi: Lango la jitu lilifunguliwa ni:
    A. Malango ya majitu yamefunguliwa
    B. Jilango la majitu lilifunguliwa
    C. Kilango cha kijitu kulifunguliwa
    D. Kilango la kijitu kilifunguliwa
  15. Meno amemwoa Susi. Mamaye Meno anaitwa
    Pendo. Pendo atamwitaje Susi?
    A. Mkazahau
    B. Wifi
    C. Mkazamwana
    D. Mpwa

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali kutoka 31 - 40

Bibi ni gwiji wa kutamba hekaya, nilipomtembelea likizo iliyopita alinihadithia kisa cha kusisimua sana. Alianza kwa paukwa nami bila kusita nakamjibu "Pakawa" mwongo wahedi uliopita katika kaya ya laleni paliishi aila ya Bwana Maseto, alikuwa na wana wawili walioshahibiana kama reale kwa ya pili. Wote walikua wakiwa
waadilifu, wenye nidhamu na heshima.

Hata hivyo, mmoja wao aliyekuwa kifunguamimba alipohitimu umri wa kubaleghe alianza kubadili mienendo. Heshima ikamtoka nako kumsemesha na kumpa nasaha kukawa sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Alitoroka shuleni pasi na idhini ya mdarisi akaenda kustarehe kwenye vilabu kule madukani. Jioni aliporudi baitini wavyele walimshika sikio lakini tangu lini sikio la kufa likasikia dawa? Alizidi kupotoka kimaadili na mwishowe nyumbani pakawa hapamweki tena. Alifunganya virago vyake na kuelekea mjini huku akijisemea kuwa kule angeenda kuponda raha. Alienda akaandamana na wenzake waliokuwa wawepoka maadili vilevile. Kufika mjini, mji ulimkaribisha kwa mahaka mwema. Baada ya kujifahamisha na huku wakizitumia pesa zao vibaya ndipo
wakaamua kuibuni njia ya kutafuta riiki. Wakaanza kuwa walanguzi wa mihadarati.

Muda si muda wakapata pesa. Donge nono. Hata hivyo njia ya mwongo ni fupi. Haukupita muda mrefu kabla hawajakamatwa na mkono mrefu wa serikali. Walitiwa mbaroni na kuhukumiwa kifungo cha nusu mwongo, kazi ngumu kila siku na viboko viwili kila juma Nyanya alipumua na kuniambia, mjukuu wangu yafuate maagizo ya wakuu wake la sivyo utayaona makuu." Baadaye sote tulienda kulala.

  1. Nyanyake mwandishi ni bingwa wa
    A. Kupika
    B. Kuhadithia ngano
    C. Kutunga ngano
    D. Kuwapa watu mashauri
  2. Mwongo mmoja ni miaka kumi ilhali karne moja ni miaka.
    A. 50
    B. 1000
    C. 20
    D. 100
  3. Wana walishahibiana kama reale kwa ya pili.
    Fani hii ya lugha huitwa.
    A. Tanakali
    B. Takriri
    C. Tashbini
    D. Msemo
  4. Wana wa Bwana Maseto walikuwa na sifa hizi zote awali ila___
    A. Wenye staha
    B. Wenye haki
    C. Wenye adabu
    D. Wenye husuda
  5. Kifungua mimba kama ilivyotumika ni aina gani ya nomino?
    A. Nomino takuzi
    B. Nomino jamii
    C. Nomino ambata
    D. Nomino maalum
  6. Kushika sikio ni semi inayomaanisha?
    A. Kumrudi mtoto
    B. Kumstahi mtoto
    C. Kumwandama mtoto
    D. Kumsema mtoto
  7. Mji ulimkaribisha kwa mahaka mwema Kisawe cha mlahaka ni
    A. Mapokezi
    B. Muungano
    C. Msafara
    D. Mwendo
  8. Wahusika wale walianza kulangua dawa za kulevya. Ipi si dawa ya kulevya kati ya hizi?
    A. Bangi
    B. Miraa
    C. Sharubati
    D. Kokeini
  9. Methali njia mwongo ni fupi kama ilivyotumiwa inaweza kulinganishwa na
    A. Mhini na mhiniwa njia yao ni moja
    B. Siku ya nyani kufa miti yote huteleza
    C. Mgaagaa na Upwa hali wali mkavu
    D. Ujanja wa nyani huishia jangwani
  10. Makala haya ni aina ya
    A. Hotuba
    B. Mjadala
    C. Hadithi
    D. Mazungumzo

Soma kufungu kifuatacho kisha uyajibu maswali ya ufahamu 41 - 50

Kipindi cha pili kilifika, wachezaji wakawasili uwanjani wakiwa wamefukaa, maana kila upande haukujua nini kitakachokuwa matokeo ya kipindi kile cha mwisho. Naam, kipindi cha lala salama kilimtia kila mmoja roho mikononi. Punde si punde refa au mwamuzi alikipuliza kipenga, Prrr! Patashika zikaanza kindumbwendumbwe cha kukata na shoka. Nyasi illumia. Nazo shangwe zilihinikiza na kujaa hewani. Akina yahe walishangilia kwa mayowe hamrere. Hata hivyo, mambo hayakuwa rahisi kamwe. Katika kukurukakara zote hizo, bado timu zilikuwa sare,
bao moja kwa moja hadi mwisho wa kipindi cha pili. Ahaa! Hapakuwa na budi kuongeza muda wa ziada.

Mapambano yalipamba moto mara moja. Matokea yalikuwa yale yale. Kumbe juhudi si pato. Mtangazaji Kaka Jos aliwika uwanjani si haba. Laiti asingalikuwa janadume, barubaru lenye nishati, angalizimia zi uwanjani. Na si ajabu mimi nisingalijinusuru kuyaaandika makala haya. Mungu zibariki roho zenye ghera na hamasa. Muda wa ziada ulipoyeyuka katika baridi ya yabisi, hapakuwa na cha nini wala nani. Kaa alipaswa kuinua gando. Naye akiinua gando, mambo yamekatika. Refa na wainua vibendera wake, waliamua penati zipigwe Magwiji wa mikwaju kutoka katika timu zote mbili walijabari na kujitenga. Wakakaa ange kama wanajeshi tayari kwa mikwaju. Waoga waliyafumba macho. Lakini hapana marefu yasiyokuwa na ncha. Hatimaye, timu ya
uitaliano ilibuka na ushindi dhidi ya ufaransa.

Ama kweli, mchezo ulikuwa kizaazaa makombora ya hapa na pale; shangwe, vifijo na hoihoi pamoja na makofi yalichanganyika na mbija, nilihitimisha ushindi wa mwitaliano na kukata kilemba cha Mfaransa. Waama, asiyekubali kushindwa si mshindani katika mchuano, hakosekani mshindi. Hapo ndipo pakawa mwisho na hatima ya kinyanganyiro cha kombe la dunia, mwaka elfu mbili na sita nchini Ujerumani.

  1. Katika kipindi cha kwanza:
    A. Wachezaji hawakucheza vizuri
    B. Timu zote mbili zilitoka sare suluhu bin suluhu
    C. Timu zote mbili zilifungana mabao matatu kwa mawilil
    D. Timu moja ililemea timu nyingine
  2. Punde si punde refa alikipuliza kipenga
    A. Ili kukikamilisha kipindi cha pili
    B. Akamalizia mchezo wa awamu ya mwisho
    C. Mpira ukaanza awamu ya mwanzo
    D. Mchezo ukaanza awamu ya pili
  3. "Akina yahe" hapa inarejelea
    A. Wadau wa kandanda
    B. Watangazaji wa kambumbu
    C. Wachezaji na akiba
    D. Watazamaji na washangiliaji
  4. Timu zilifungana sare bao moja kwa moja
    A. Wakati wa mikwaju ya penalty
    B. Kwenye kipindi cha pili
    C. katika muda wa ziada
    D. Mnamo kipindi cha kwanza
  5. Katika muda wa ziada
    A. Matokeo yalibadilika mabao yakaongezeka
    B. Mtangazaji kaka jos alichoka akaacha kutangaza
    C. kasi ya mapambano ilipungua
    D. Timu zilizidi kulingana nguvu
  6. Muda wa ziada ulileta matokea gani katika mapambano haya?
    A. Kupigwa kwa makombora ya penalty
    B. Kushindwa kwa wafaransa
    C. Kaa kuinua gando
    D. Kuenda sare hadi mwisho wa mchezo
  7. Shangwe na shamrashamra za hapa na pale ziliashiria
    A. Ushindi wa wafaransa
    B. Ushindi wa wataliano
    C. Nderemo na ushindi wa wafaransa
    D. Nderemo na ushindi wa wataliano
  8. Kwa nini waoga wakayafumba macho yao
    A. Sababu ya kiwewe na dukuduku
    B. Waliogopa mikwaju ya penalty
    C. Hawakutaka kuona matokeo
    D. Waliogopa kushindwa
  9. Mashindano ya soka ya kombe la dunia mwaka 2006 yalifanyika katika nchi ya
    A Wafaransa
    B. Wataliano
    C. Wajerumani
    D. Wareno
  10. Anwani mwafaka kuhusu taarifa hii ni
    A. Kandanda ya kombe la dunia
    B. Kandanda
    C. Mashindano ya kombe la dunia
    D. Finali ya kandanda ya kombe la dunia

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Malizia insha yako kwa maneno yafuatayo huku ukiifanya iwe ya kusisimua Zaidi.

....… ni vyema wazazi kushauriana na wana wao na kuwaelekeza ipasavyo ili kuepuka mambo kama haya yaliyomfikia kijana huyo.



MAJIBU

KISWAHILI SET 4 MARKING SCHEME

Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI - KCPE 2020 PREDICTION 1 SET 4.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest