Kiswahili Paper 1 Kenya High Post Mock Exams 2020 - Questions and Answers

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Andika insha MBILI. Insha ya KWANZA ni ya LAZIMA.
 • Chagua insha moja nyingine kutoka tatu zilizobaki.
 • Kila Insha isipungue maneno 400.
 • Kila Insha ina alama 20.
 1. Lazima :
  Wewe ni mwenyekiti wa jopo lililoteuliwa kuchunguza chanzo cha utovu wa usalama kijijini Sokoto. Andika ripoti maalum /rasmi kuhusu jambo hili.
 2. Magonjwa mengi yanasababishwa na mitindo ya kisasa ya maisha. 
  Jadili.
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mchagua nazi hupata koroma.
 4. Andika insha itakayoanza kwa maneno haya:
  Milipuko mikubwa ilisikika pu! Pu! Puu! Kisha niliwaona watu wakikimbia kuelekea pande zote…


MARKING SCHEME

 1. Atambue kuwa ni swali la ripoti rasmi. Lazima insha hii iwe na anwani iliyo wazi, yaani iwe na neno ripoti, ya nani, kuhusu nini na wapi ?
  Sharti sura ya ripoti maalum au rasmi izingatiwe:Kichwa, utangulizi, taratibu/yaliyoshughulikiwa, mwili/matokeo ya uchunguzi,hitimisho,mapendekezo na sahihi.
  Baadhi ya hoja:
  Insha iwe na maudhui yasiyopungua matano. Baadhi ya hoja ni kama vile:
  1. Ulevi
  2. Ukosefu wa kazi
  3. Wanyama wa pori kama vile ndovu
  4. Watoto kutopelekwa shule
  5. Utepetevu wa vyombo vyombo vya usalama
  6. Adhabu nyepesi zinazotolewa na mahakama
  7. Wazazi kutotekeleza wajibu wao kwa watoto
  8. Tamaduni zilizopitwa na wakati kama tohara, wizi wa mifugo n.k

   Sharti mtahiniwa atoe mapendekezo ya kutatua tatitizo hili k.v
   1. Kupiga marufuku utengenazaji na unywaji wa pombe haramu
   2. Kuanza miradi ya kuajiri vijana
   3. Watoto wote kupelekwa shule
   4. Vyombo vya usalama kuwa macho na kupigana na uhalifu
   5. Adhabu kali kutolewa kwa wahalifu
   6. Wazazi kutekeleza wajibu wao wa kutunza watoto
   7. Kukabiliana vikali na makundi haramu
   8. Kutupilia mbali tamaduni zilizopitwa na wakati
    Asiyezingatia sura ya ripoti aadhibiwe kwa kuondolewa 4s
    Makosa ya sarufi na hijai yaadhibiwe yanapotokea
 2. Mtahiniwa aandike insha ya hoja
  1. Sharti ataje hoja, kuifafanua na kuitolea mifano
  2. Lazima aunge mkono hoja aliyopewa
  3. Pia aonyeshe upande wa pili wa hoja aliyopewa.
  4. Aeleze mitindo ya maisha ya kisasa.
  5. Hoja zake ziwe tano au zaidi
   Hoja za kuunga mkono:
   1. Baadhi ya vyakula hasa vyenye mafuta, madini,sukari na chumvi husababisha magonjwa kama vile msukumo wa damu na kisukari
   2. Kukosa mazoezi ya mwili hasa kwa sababu ya matumizi ya magari ya usafiri na ya kibinafsi na watu hawatembei kwa miguu.
   3. Matumizi ya pombe huleta madhara mengi kwa mwili yanayosababisha magonjwa ya akili.
   4. Mienendo mibaya hasa kushiriki mapenzi ovyo ovyo husababisha magonjwa ya ukimwi, kisonono na magonjwa mengine ya zinaa.
   5. Uchafuzi wa mazingira husababisha magonjwa kama vile ya pumu,malaria ,kipindupindu n.k
    Hoja za kupinga:
    1. Atetee kwamba magonjwa hayasababishwi tu na mitindo ya maisha ya kisasa.
    2. Baadhi ya magonjwa hurithishwa katika familia.
    3. Kuna magonjwa yanayoletwa na wadudu kama vile mbu, konokono n.k
    4. Magonjwa kama vile mafua husababishwa na hali ya anga na si hali ya maisha.
    5. Hali za kimaumbile kama vile mafuriko husababisha magonjwa kama vile kipindupindu.
 3. Sharti aelewa kuwa ni methali.
  • Atunge kisa ambacho kinaoana vizuri na maana ya matumizi ya methali hii.
  • Kisa chake kiwe cha kuvutia.
  • Sharti aonyeshe pande mbili za methali.Aonyeshe mhusika anayechagua kitu au jambo zuri lakini analikosa na kupata lingine la kiwango cha chini.
  • Anatakiwa kuonyesha kuwa tusiwe watu wa kuchagua vitu bali tufanye bidii kupata tunachokihitaji.
  • Makosa ya hijai na sarufi yaadhibiwe yanapotokea
 4.  
  • Ni sharti mtahiniwa aanze kwa maneno aliyopewa.
  • Anatakiwa kuanza kwa maneno yale bila ya kubadilisha wala kuyapunguza.
  • Kisa chake kiwa cha kuvutia na aonyeshe ni matukio yapi yaliyosababisha milipuko ile, kulikuwa na majeruhi na watu walitoroka kwenda wapi? Ni nini kilichotokea baada ya hapo?
  • Asipoanza kwa maneno aliyopewa atuzwe alama ya bakshishi

USAHIHISHAJI KWA JUMLA

 • Sharti mtahiniwa ajibu maswali mawili pekee.
 • Kazi ya mtahiniwa iwe nadhifu na ipangwe vizuri kiaya.
 • Makosa ya hijai na sarufi yaadhibiwe yanapotokea.
 • Baada ya kusahihisha kazi ya mtahiniwa, awekwe kwenye viwango ya A-D vilivyowekwa na baraza la kitaifa la mitihani K.N.E.C
 • Mtahini atakayepotoka, atakayejitungia swali au atakayetumia lugha isiyo Kiswahili atuzwe alama ya BK01.
 • Urefu wa insha sharti uzingatiwe (maneno 400) ¼Urefu ukadiriwe hivi:
   Maneno   100   200   300   400 
   Kiwango  ¼insha  ½insha  ¾insha   Kamili 
           

Tanbihi:

 1. Hizi ndizo alama za juu iwapo mtahiniwa ameandika kiwango hicho cha maneno . Kisha aadhibiwe makosa mengine.
 2. Mtindo wa zamani wa kuondoa alama 2U ulitupiliwa mbali.

Alama zifuatazo zitumiwe katika usahihishaji.

✓Msamiati unaofaa
×Msamiati usiofaa
−Kosa la hijai
═Kosa la sarufi
^Alama ya achwa – neno linapoachwa katika sentensi


Download Kiswahili Paper 1 Kenya High Post Mock Exams 2020 - Questions and Answers.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest