Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Bunamfan Post Mock 2021 Exams

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Jibu maswali manne pekee.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani: Riwaya, Ushairi, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.
 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

SEHEMU YA A: TAMTHILILA
(Kigogo – Pauline Kea)

 1. Swali la lazima.
  1. ‘’Yaani umenonaje wewe? Waona mimi ni ganda la muwa la juzi.’’
   1. Eleza muktadha wa dondo hili. (al. 4)
   2. Tambua mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili. (al. 2)
   3. Fafanua jinsi wahusika walivyogeuzwa ganda la muwa katika tamthilia. (al. 6)
  2. ‘’ Niko tayari kuwaweka pahali pao mmoja baada ya mwingine.’’ ‘’…
   Wamesahau vipi wasilolijua?’’
   Eleza umuhimu wa matumizi ya mbinu rejeshi ukirejelea dondoo hili. (al. 12)

SEHEMU YA B: RIWAYA
(Chozi la Heri – Assumpta Matei)
Jibu swali la 2 au 3

 1.  
  1. Baba, umewahi kumwona mtoto wa miaka hamsini ambaye hajasota ;
   sikwambii kusimama dede?’’
   i. Eleza jazanda iliyotumika katika dondoo hili. (al. 2)
   ii. Thibitisha kuwa mtoto anayerejelewa hajasota wala kusimama dede.(al. 8)
  2. Eleza umuhimu wa mazungumuzo baina ya Tila na Ridhaa. (al. 10)
 2.  
  1. Eleza umuhimu wa barua aliyoiandika Bwana Kalima kwa Lunga. (al. 10)
  2. Soma kifungu hiki kisha ujibu swali.
   Mkuu wa shule, walimu na wanafunzi wenzangu, swala la uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu. Tumeona jinsi misitu imevamiwa na viongozi wenye mate ya fisi. Nasikia baadhi ya vinara wa taasisi mbalimbali ya umma wamewaacha wanyama kama mayatima kwa kuwapoka makazi yao. Maelfu ya maekari ya misitu yamefyekwa na kujengwa viwanda. Badala ya mibambakofi na miti mingine inayosafisha hewa, michai imetwa nafasi yake. Wanaohusika na matendo haya wanapoulizwa hudai kuwa michai si adui wa mazingira! Wengine wanasema kwamba misitu haina budi kukatwa ili kupanda mimea inayotoa chakula. La kuhuzunisha ni kwamba hawa hawa wanaosema hivyo ndio wanakita majengo ya kifahari katika maeneo yanyofaa kutengewa upanzi wa chakula! Wengine wamediriki kunyakua hata madhabahu kwenye Mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli kubwa za kitalii. Wazee wetu hawana hata pahali pa kuchomea kafara! Tunakata miti bila kupanda mingine. Tazameni shuleni humu! Hata mabustani ya maua tunashindwa kuyastwisha! Tukiendelea hivyo, bila shaka sehemu sehemu yetu itakuwa jangwa!
   Fafanua maudhui yoyote kumi yanayojitokeza katika dondoo hili. (al. 10)

SEHEMU YA C: USHAIRI
Jibu swali la 4 au 5

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  Sikilizeni wimbo huu:
  Niliokuwa mtoto nilitwa chacha
  Kwa matamshi yangu ya sasa
  Nilipokuwa mtu mzima niliitwa Manywele
  Nilipokuwa mwalimu nikaitwa Bure.

  Huu utakuwa wimbo wako Utakapostaafu urudipo nyumbani Umelewa kangara na
  nyayo zako
  Zikishindwa kulenga njia nyembamba vijijini.
  Utakuwa kichekesho cha watoto Watakaoukuita,
  Ticha! Popote upitapo.

  Kumbuka mwalimu utakapostaafu, Mijusi
  watataga mayai ndani ya viatu Vyako
  vilivyokwisha visiginino.
  Na ndani ya sidiria chakavu
  Zilizoshikizwa Kamba kwa pini
  Mende watazaliana ndani ya chupa tupu Za
  marashi na za bia.

  Na manyigu yatajenga ndani ya kofia
  Zilizosahaulika kutani
  Utakapokufa nge watazaliana Chini
  ya jiwe juu ya kaburi lako, Na mlevi
  fulani akipita atapenga
  Na kupangusa vidole kwenye jiwe pweke
  Mwanzo na mwisho wako ndio huo.

  Lakini wakati ungali hai
  Unaweza kubadilisha mkondo wa maji Lakini
  kwanza mzungumze. Wewe na mimi. Acha
  mioyo yote izungumzwe
  Baada ya kunyanyaswa Na
  kisha nusu mshahara.

  Utafundisha tena nyimbo kuwasifu viongozi?
  Utafundisha tena ngonjera?
  Utapeleka tena wanafunzi asubuhi
  Wakajipange barabarani kusubiri Mgeni
  afikaye saa kumi na apitapo
  Apunga tu mkono kuwatia kichaa cha shangwe Na
  huku nyuma mwasambaa na njaa?
  Tazama hilo runda madaftari mezani
  Utalimaliza kwa mshahara mkia wa mbuzi?
  Tuzungumze. Ninyi na mimi.
  Acha mioyo yetu izungumze
  Mkiwa waoga na kujikunja kama jongoo
  Mtawekwa kwenye vijiti na kutupwa Nje ya
  ua, ndani mtawaacha
  Wacheza ngoma wakitunga nyimbo mpya

  Sikilizeni walimu,
  Anzeni kufundisha hesabu mpya
  Mjinga mmoja kujumlisha na wezi ishirini Ni
  sawa na sifuri. Hapana utawala Fundisheni
  historia historia mpya
  Hapo zamani za sasa
  Hapakuwa na serikali.

  Sikilizeni kwa makini
  Umoja hatuna
  Twasambaratika kama nyumba
  Tulicho nacho ni woga,
  Na kinachotuangusha ni unafiki. Lakini
  tusikate tamaa kama mbuni. Tukiupata
  umoja bado tunayo silaha. Kura.

  Maswali
  1. Fafanua sifa za shairi huru zinazojitokeza katika shairi hili. (al. 5)
  2. Eleza jinsi maudhui ya utamaushi yanavyojitokeza ukimrejelea nafsi-nenewa. (al. 4)
  3. Nafsi-nenewa anapaswa kujilaumu kwa masaibu yake. Thibitisha. (al. 2)
  4.  
   1. Bainisha nafsi-neni katika shairi hili. (al. 1)
   2. Taja toni ya shairi hili. Toa mfano. (al. 2)
  5. Eleza matumizi mawili mawili ya usambamba na jazanda katika shiri hili.(al. 4)
  6. Eleza maana ya kufungu kifuatacho:
   Mjinga mmoja kujumlisha na wezi ishirini ni sawa na sufuri. (al. 2)
 2. Soma shairi kisha ujibu maswali.
  Leo ‘mekuita,                                  Nikupe ya moyo
  Kwa upole nitanena,                       “Kayatiye masikiyo
  Tabiya hii yako mwana                   Si yetu tujuwapo

  Uli wa kulaza damu,                       Na uzembe uzidiyo
  Pahala nawe hudumu,                    Uchaoni mbiyombiyo
  Hutufai nawe humu,                        Na hiyo shambiroyo

  Wapendani naumi,                          Uniizia gange
  Hulimi na walimi                             wataka ukajitenge
  Haya sijaona mimi,                         Nakuasa ujichunge

  Mwiza kazi yu wa chira                   Ni andewaye tenge
  Asiyeta ajira                                    Wala hashiki shilange
  Ndiye muja wa hasara,                   Hubomoa asijenge

  Unavitaka vya bure                         Hulitoa jasho lako
  Lako ndizo hamurere                      Umebaki mitiko
  Uchao ‘wa ‘tuza bure.                     Sizo zetu nyendo zako

  La mno lako ni ung’are                   Uzirembe nyele zako
  Uturi ujirashire                                Ukatembee kwa deko
  Hukosi kuzua ghere                        Na marashi ya mnuko

  Unazani utaoa?                               Utamwoa wa nani?
  Jasho nalo hujatoa,                         Utachokishika nini?
  Utaithibiti ndoa?                              Wa kukubali nani?

  Unafaa kujitoa,                                Fanye kazi kwa manani
  Na mali ukayazoa,                          Hamadi i kibindoni
  Ndipo utapopoa                              Ukamtafute mwendani

  Si mambo ya kutanga,                    Fi na huhu fi na yule
  Chunga utajikaanga                        Umetujile uwele
  Mchumba chumbiya mwenga         Na yule ukamuole

  Utafanyani kiwatunga                      Himila wakahimile
  Na hilo likawe janga,                       Na lije likulemele
  Mwanangu hutochenga                   Na wote wakikujile

  Kisomo ndiyo unayo,                       Shahada umejitwaliya
  Ujuzi unao kocho,                            hutaki kuutumiya
  Upate ukitakacho                             Kile cha kukufaiya

  Mwana wa ‘ntiya kichocho               Kwona umejiachiya
  Umekuwa kitumiwacho                    Kidhani wawatumiya
  Unawapa wapendacho                    Na wanachokutakiya

  Komu mwanangu ukome                 Usinifishe mveyeleo
  Usombombi uukome,                       Ukome kwanzia leo
  Sitakwita te’niseme                          Ishapita hii leo

  Ukware si kuwa dume                      Dume ni ajira
  Wa itaha ndiye dume                        Anakheshimu nafseo
  Muungwana ja kimeme                    Fikira nokwelezeo

  Mradi unayo masikizi                       Haya umenisikiya
  Kazituwe nyendo hizi,                      Ukawe wa kutuliya
  Ukasuhubiye kazi,                           Halafu itakufaiya

  Nakoma zaidi s’ezi                            Yametosha mekwambiya
  Nimekuweko na juzi,                         Miyaka menipitiya
  Nimejizolea ujuzi,                              Na ndiyo ha ‘nakupa haya

Maswali

 1. Fafanua sifa za kiarudhi za shairi hili. (al. 3)
 2. Kando na kigezo cha idadi ya mishororo, chambua bahari nyingine tatu za shairi hili. (al. 3)
 3. Huku ukitolea mifano mwafaka, fafanua mambo mawili aliyofanya mshairi ili kukidhi mahitaji ya kiarudhi. (al. 2)
 4. Andika ubeti wa nane kwa mtindo tutumbi. (al. 3)
 5. Tambua mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa na mshairi. (al. 2)
 6. Eleza dhamira ya shairi hili. (al. 1)
 7. Tambua nafsi-nenewa katika shairi hili. (al. 1)
 8. Ni nini toni ya shairi hili? Eleza. (al. 2)
 9. Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama iliyotumika katika shairi hili. (al. 2)
  1. ghere

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
(Tumbo Lisilodhiba na Hadithi nyingine –A. Chokocho na D. Kayanda) Jibu swali la 6 au 7

 1. ‘’Dunia we’ duinia. Dunia ya mwenye nguvu, si ya mimi dhaifu wa nguvu. Dunia ya msumari moto juu ya donda bichi.’’
  1. Thibitisha jinsi dunia ilivyokuwa msumari moto juu ya donda bichi kwa mhusika katika dondoo hili. (al. 10)
  2. Eleza jinsi maudhui ya ushirikina ulivyojitokeza katika hadithi ya Tulipokutana Tena. (al. 10)
 2. Shibe Inatumaliza
  ‘’Mh! Ati kama mimi. Kwani wewe umekula nini?’’
  ‘’Mimi? Hata sikutazama. Nimekomba tu. Wewe je?’’
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al. 4)
  2. Tambua mbinu zozote mbili za uandishi zilizotumika katika dondoo hili. (al. 2)
  3. Eleza jinsi wahusika mbali mbali walivyokomba rasilimali bila kutazama. (al. 8)
  4. Tambua umuhimu wa DJ katika hadithi ya Shibe Inatumaliza. (al. 6)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

 1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
  Wekamaya ndiye aliyemuumba binadamu wa kwanza akamwita Omwami. Jina hili Wekamaya alipewa kwa sababu wanajamii wa Omukwasi waliamini yeye ni mungu mwenye wema. Kwa sababu hii, siku moja alipokuwa akitembea katika bustani yake, Wekamaya alijiambia, ‘’Singependa Omwami wangu wawe wakifa kabisa, nataka afufuke.’’

  Wakamaya alikuwa na wake wawili, Shiswitswi na Ngoitsi. Katika ndoa yao, Wamukaya aliweza kungamua kuwa Ngoitsi alikuwa mke aliyependa kutia chumvi katika maneno na hata kusema kinyume ya aliyoambiwa. Pia, alikuwa kigeugeu kama kinyonga. Kwa upande mwingine, Shiswitswi alikuwa mwadilifu na aliyejawa na busara kedekede. Alikuwa mkweli.

  Wamukaya alipoona kuwa wakati umefika wa kumpasha Omwami habari ya uzima, alimwita mkewe Shiswitswi na kumwambia, ‘’Nenda bustanini na umwambie Omwami kuwa atakayekufa atafufuka.’’ Shiswitswi akaiitika na kusema, ‘’Ndio Wakamaya!’’ Katika harakati hizi, kumbe Ngoitsi alikuwa kasikia alivyotumwa Shiswitsi. Akajiambia mwenyewe, siwezi kugeuzwa ganda la muwa, ujumbe huu ntaipeleka mimi, ndiyo Omwami aniheshimu. Kwa kuwaza, akakumbuka udhaifu wa mke-mwenza wake ambao ulikuwa kuwa mpole. Akala yamini kuutumia.

  Shiswitswi alianza safari na kuwaaga kwenda kwa bustani. Akatembea, akatembea, akatembeaaaaa! Alipofika baada ya siku mbili alishangaa kumpata Ngoitsi tayari bustanini. Tayari keshampa Omwami ujumbe, ‘’Wamukaya amesema kwamba watakokufa wataangamia milele’’ na Omwami kwa mshutuko tayari alishatoweka kutoka bustanini kwa kilio.
  Na huu ndio mwisho wa hadithi yangu.

  Maswali
  1. Tambua kipera hiki cha hadithi. (al. 2)
  2. Kwa nini mtambaji anatumia maneno ‘’Na huu ndio mwisho wa hadithi yangu.’’ (al.4)
  3. Tambua sifa zozote sita za kimtindo zinazojitokeza katika hadithi hii. (al. 6)
  4. Fafanua njia zozote nne ambazo unaweza kutumia kukusanya data kuhusu kipera hiki. (al. 6)
  5. Eleza njia zozote nne zinazoweza kutumika katika jamii ya kisasa kuendeleza kipera hiki.   (al. 4)

MARKING SCHEME

Sehemu ya A: Tamthilia

 1. Swali la lazima
  1.  
   1. Haya ni maneno ya Tunu kwa Majoka. Wako ofisini na Majoka. Ni baada ya Majoka kumwambia Tunu kwamba anapanga kumposa kwa Ngao Junior.
   2. Mbinu ;
    • Swali balagha – Yaani wewe umenionaje?
    • Mdokezo wa methali – waona mimi ni ganda la muwa la juzi.
    • Jazada – Ganda
   3. Jinsi wahusika walivyogeuzwa ganda la muwa.
    1. Jamii ya kina siti kutishwa na vijikaratasi ya kuwataka Wahome Sagamoyo hata baasa ya kuishi na wanasangamoyo kwa muda mrefu.
    2. Kombe mkerekeliwa wa Majoka kuwa miongoni mwa wanaohitajika kuhama Sagamoyo.
    3. Mamapima anamwagiwa pombe hatimaye baada ya ukereketwa wake.
    4. Kenga anamgeuka Majoka baada ya faida zote alizopata na kujiunga na Mrengo wa Tunu.
    5. Ashua anamgeuka Sudi baada ya muda mrefu wa ndoa. Anasema amechoka kupedwa Kimasikani.
    6. Ngurumo anageuzwa ganda la muwa. Baada ya kukawa chatu uongozi wa Majoka ambao amekuwa akinyonga mkono ……………….. bila
    7. Chopi ambaye amekuwa akitumiwa na Majoka kukawa na kuwaangaisha Wapinzani wa Majoka anapangiwa kifo na uongozi ua huo ambao amekuwa akihudumia.
    8. Kingi anaambiwa na Majoka kuwa amefutwa kazi.
     (Zozote 6 x 1)
  2. Umuhimu
   1. Kichimuza matuko ya awali – inatuarifu kuhusu kifo cha Jabali.
   2. Majoka na Kenga in watu wenye kuweka siri – wamesahau vipi wasilolijua
   3. Kuonyesha mfumo wa siasa uliopo, kuna vyama vingi – chama cha mwenye
   4. Kuwaangizia Majoka na Kenga kama watu wanweza kufanya lolote ili kujidumisha mamlakani.
   5. Kusisitiza ukatili ulivyokithiri katika uongozi wa Majoka.
   6. Kuonyesha imani ya kidini katika jamii – wameamini uwepo wa akhera.
   7. Kuangazia umaarufu wa vyama vya upizani na ufuasi mkubwa wa vyama hivyo – ukitaka kufurusha ndege, kata mti.
   8. Kuangaza jududu za wanaharakati katika kupigania haki. Tunu amapanga kuleta wanchanguzi wapya wa kifo cha Jabali.
   9. Kuendelea mbinu zingine za kimtindo – balagha, takriri n.k.
   10. Kuendeleza ploti.
   11. Kuonyesha uhasama uliopo baina ya wapinzani wa kisiasa.
    (Zozote 8 x 1)

Sehemu ya B: Riwaya

 1.  
  1.  
   1. Jazanda
    Mtoto wa miaka hamsini ambaye j=hajasita – mataifa ya bara la Afrika yaliyo na uhuru wa miaka hamsini lakini hayajapiga hatua Kimaendeleo (2 x 1)
   2. Mtoto anayerejelewa hajasota wala kusimama dede.
    1. Waafrika hawajarudishiwa mashamba yao hata baada ya uhuru – mashamba ya Theluji Nyeusi bado ni milki ya wakoloni.
    2. Waafrika ambao ni wenyeji bado ni maskwota katika eneo la Kisiwa bora.
    3. Waafrika bado ni wategemezi kiuchumi hakuna wanaomiliki.
    4. Waafrika hawajitoshelezi kwa chakula.
    5. Kuna uhaba wa ajira.
    6. Mshahara wanaolipiwa waafrika ni wa kijungujika
    7. Waafrika hawana mbinu za uzalishaji hawezo kesaga kaliawa.
    8. Waafrika wanaendeleza Wazungu kiuchumi – wananunua maziwa yao yaliyoganda na kwenda kwa shopping mall yao.
    9. Makampuni ya kigeli kupewa kandarasi ya kuchimba madini.
     (Zozote 8 x 1)
  2. Umuhimu wa mazungumzo baina ya Tila na Ridhaa.
   1. Kumekuwa na mifumo tofauti za kiuchumi zilizotumika kuzalisha mali kwa mfano ujima, ukabaila, ubwanyenye, ujamaa.
   2. Kuonyesha ufaraguzi uliopo baina ya kazi za kifasihi – Mazungumzo haya yanalinganisha viwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Mashetani Kimaudhui.
   3. Yanaonyesha nafasi ya utawala katika kuboiriesha na kudoresha uchumi. Utawala huendeleza mfumo wa kiuchumi.
   4. Yanaangazia wimbi la mabadiliko katika jami. Wanajamii wako tayari kumchagua Mwekevu Tendakazi bila kuzingatia jinsia yake.
   5. Nafasi ya wasichana katika jamii inaimarika. Ridhaa anakiri kumpa nafasi Tila – nafasi ya kusoma kama alivyompa mwangeka.
   6. Mazungumzo haya yanamsawsiri Tila kama mwanafunzi mwenye upevu wa mawazo na mdadisi wa mambo. Anasema kuwa uongozi mzuri ni ule unaoboresha uchumi.
   7. Changamoto ambazo zimewakumba Waafrika tangu uhuru ni umaskini, ujinga na magonjwa wa nafasi za kazi na ufisadi.
   8. Serikali imefanya juhudi kuboresha maisha ya wananchi. Waasiriwa wa magonywa kama ukimwi wanapewa dawa kwa bei nafuu kuna elimu bila malipo, teknolojia inatumika shuleni, tume za kuchunguza ufisadi zimebuniwa.
   9. Kuna umaskini uliokithiri Raia hawawezi hata kumudu gharama ya matatizo yao.
   10. Ujinga wa wananchi umechangia matatizo yao. Hawajui hata mbinu za kujikinga na magonjwa.
   11. Nafasi ya elimu inawafunza vijana kuhusu nafasi yao katika kuboresha uongozi uliopo.
   12. Juhudi za wananchi kujiboresha kiuchumi zimelemazwa na hali ya anga – kiongozi.
   13. Kuna mbinu mpya ya ukulima – kutumia maji ya bomba.
   14. Kazi zilizopo ni za mishahara ya kijungujiko.
   15. Ukoloni mamboleo bado umekithiri – kampuni zinazochimba migodi ni za kibinafsi.
   16. Kuna ushirikiano wa kiuchumi – hizi kampuni za kibinafsi zimewaajiri wananchi.
   17. Udhaifu katika mahakama – kesi kucheleweshwa.
 2.  
  1. Umuhimu wa barua ya Bw. Kalima kwa Lunga
   1. Inaonyesha unafiki uliopo miongoni mwa viongozi wa mashirika – anazingizia kupanda kwa gharama ya uzalishaji ila ana njama ya kumstaafisha tu lunga.
   2. Barua hii inamsawiri Bw. Kalioma kama mbinafsi. Anamfuta kazi lunga kwa sababu za kibinafsi na hajali maisha na taaluma ya lunga.
   3. Mbinu za kuzalisha mali katika mataifa machanga yanapanda kia uchao jambo linalosamabishwa mashirika ya umma kukosa fedha.
   4. Wafanyikazi katika mashirika ya umma wanaweza kufutwa wakati wowote. Hakuna mpango maalum wa kuwastaafisha.
   5. Barua hiyo inamsifia Lunga kuwa mwajibikaji kazini.
   6. Lunga alifanya kazi kwa bidii/alifanya bidii kuendeleza shirika la maghala ya nafaka.
    (Zozote 5 x 2 = 10)
  2. Maudhui
   1. Tamaa – Viongozi wenye mate ya fisi wanavamia misitu.
   2. Upungufu wa utu – Viongozi wanawacha wanyama bila makao.
   3. Uharibifu wa mazingira – misitu inafyekwa na kujengewa viwanda.
   4. Uchafuzi wa mazingira – hakuna mimea inayosafisha hewa.
   5. Ujinga – Wanaosema michai si adui ya mazingira
   6. Mapumza – Wakulima wa michai wanapuuzilia umuhimu wa miti inayosafisha hewa.
   7. Ubinafsi – Wanaopenda mimea kwenye misitu ili kujinufaisha.
   8. Unyakuzi wa ardhi – watu wanaitwa maeneo ya misitu ili kujengea hoteli.
   9. Ushirikina – dhahabu/kafara
   10. Anasa – Kuna hoteli za kitalii.
   11. Elimu – Shule
    (Zozote 10 x 1= 10)

Sehemu ya C: Ushairi

 1.  
  1. Sifa za shairi 
   1. Haizingati idadi kwa mistari/mishororo katika kila ubeti.
   2. Idadi ya vipande hailingani katika mstari.
   3. Halizingatii mpangilio maalum wa vina.
   4. Halizingatii ulinganifu wa mizani katika kila mstari.
   5. Idadi ya vipande vya mishororo ni sawa.
   6. Halizingatii ukamilifu wa mishororo
  2. Utamaushi
   1. Mwalimu hathaminiwi – anaitwa bure/duni
   2. Mwalimu analewa na kupepesuka barabarani.
   3. Watoto kumcheka mwalimu wao apitapo.
   4. Viatu vya mwalimu kuisha visigino
   5. Sidiria ya mwalimu ni chakavu.
   6. Mwlaimu hawezi kumudu bei hya marashi baada ya kustaafu.
   7. Mwalimu atakufa na kuzikwa bila kusherekewa.
   8. Hata mlevi anamdharau mwalimu
   9. Mshahara duni.
    (Zozote 4 x 1 = 4)
  3. Jinsi mwalimu anapaswa kulaumiwa
   1. Yeye ndiye anatunga wimbo wa kuwasifu viongozi wasiotaka kubadilisha taaluma yake.
   2. Yeye ni mwoga – Anajikunja kama jongoo.
   3. Walimu hawana umoja.
  4.  
   1. Nafsineni-Mwalimu
   2. Toni-utamaushi(kutaja al.1, mfano-al.1)
  5.  
   • Usambamba-Utafundisha tena
                         -Sikilizeni
   • Jazanda –Bure, chacha,Mkia wa mbuzi
  6. Mjinga na wezi ishirini hawana manufaa yoyote.
 2. Shairi la pili
  1. Sifa za Kiarudhi
   1. Limepangwa kwa beti
   2. Beti zimegawanywa kwa mishororo mitatu
   3. Vipande ni viwili viwili
   4. Idadi ya mizani imetosheleza
   5. Vina betini vimepangwa kwa njia maalum
    (zozote 3x1=3)
  2. Bahari
   1. Mathnawi- lina vipande viwili katika kila mshororo
   2. Ukara-vina
   3. Mandhuma- upande wa mmoja kutoa hoja na mwingine kukamilisha
   4. Sabilia- mshororo wa mwisho unabadilikabadilika
  3. Uhuru wa kishairi
   1. Kuboronga sarufi- mno lako badala ya lako mno
   2. Inkisari=- mekuita badala ya nimekuita
   3. Tabdila chumchumbiya badala ya chumbia
  4. Lugha tutumbi
   • Unafaa kujitolea kufanya kazi kwa bidii ile uwe tajiri kwa sababu mbinu za mali unazo ndiposa uanze kumtafuta mchumba
    (3x1)
  5. Mbinu za lugha
   • Nahau- kulaza damu
   • Jazanda –jasho
   • Methali- Hamadi kibindoni
   • Tashbihi-muungwana ja kimeme
    (zozote 2x1)
  6. Dhamira
   • Kuhimiza bidii miongoni mwa vijana
    (1x1)
  7. Nafsi-nenewa- Kijana
  8. Toni-ushauri
  9. Ghere-wivu

Sehemu ya D: HADITHI FUPI
(Tumbo Lisilishiba na Hadithi Nyingine)

 1.  
  1. Jinsi dunia ilivyokuwa msumari moto juu ya donda bichi kwa Sara
   1. Sara ako na ukiwa na udhaifu. Amejilaza chumbani mwake kwa kite
   2. Ameathirika kisaikolojia. Taswira ya jinsi alivyobakwa limekwama akilini mwake
   3. Amepata ujauzito kutokana na ubakaji huo
   4. Amevunjiwa ujanajike na janadume liliolombaka
   5. Tendo la kubakwa limemsabbbishia aibu na uduni
   6. Anahofia kutengwa na kusutiwa na jamaa yake
   7. Ana hofu ya kufukuzwa kwao ikiwa wazazi wake wangeng’amua ujauzito wake
   8. Angetengwa na kuachiswa shule kwa ajili ya ujauzito
   9. Wazo la aliyembaka kuwa huru lilikeketa maini
   10. Angesimangwa
   11. Anahofia kusomewa na babake mzazi. Angemwita kisirani
    (zozote 10x1)
  2. Ushirikina katika hadithi Tulipokutana Tena
   1. Inasemekana Wamate wana uwezo wa kupaa anagani kutumia uchawi
   2. Mkasa wa chatu lililotambaa kutoka mashariki hadi magharibi na watu tumboni
   3. Utabiri wa kisa cha chatu ullikuwa na msingi wa kichawi
   4. Kwa Wamate , mapakacha yanaaminiwa kuongea yakipigwa teke
   5. Sebu ameamini uchawi upo ja[pot u hauonekani. Yeye ni mshirikina
   6. Kuna uchawi wa kurushwa –mizungu ya kuzugwa na kuondoshwa
 2.  
  1. Dondoo
   Kauli ya kwanza ni Mbura. Kauli ya pili ni ya Sasa. Wako shereheni kwa mzee Mambo. Wanbishania upakuzi na shibe
  2.  
   1. Nidaa-Mh!
   2. Swali balagha-Mimi? Wewe umekula nini? Wewe je?
   3. Takriri-Mimi
  3. Jinsi wahiusika mbalimbali walivyokomba rasilmali bila kutazama
   1. Mzee Mambo ni waziri kivulimwenye vyeo viwili japo hana kazi maalum. Analipwa na rasilmali ya umma
   2. Anachota , kupapia na kuifakamia mshahara bila kufanya kazi
   3. Sherehe ya watoto wa Mambo inarushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya kitaifa inayoendeshwa na rasilmali ya umma
   4. Sasa na Mbura wanalipwa kufanya kazi katika wizara moja
   5. Magari ya serikali yanatumika kuendesha shughuli katika sherehe ya watoto wa mzee Mambo
   6. Sherehe ya kufana- vyakula vya aina mbalimbali inaandaliwa kwa gharama ya serikali
   7. DJ analipwa mabilioni ya fedha kucheza muziki kwa sherehe. Hela hizi ni za umma
   8. DJ anamiliki duka kubwa la dawa ambalo mtaji wake ni bihari kuu ya dawaza serikali
   9. DJ anapata huduma za maji, umeme na matibabu bila malipo ilhali yeye ni mfanyikazi wa Serikali
    (zozote 8x1)
  4. Umuhimu wa DJ
   1. Anaonyesha jinsi wananchi wanavyochangia matatizo yanayowakumba- yeye ni raia anayeshirikiana na viongozi kupora mali ya wananchi
   2. Anaangazia ufisadi ulivyokithiri uongozini-analipwa japo ni mfanyikazi wa serikali
   3. Ametumika kuonyesha uozo uliopo katika idara yay a matibabu- anaiba dawa katika bohari ya serikali na kuziuza katika duka lake
   4. Wimbo anoucheza wa sijali lawama inajenga sifa za viongozo kama wenye mapuuza . Hawajalimalalamiko ya wananchi
   5. Anaonyesha jinsi uongozi katika mataifa yanayoendelea umewatelekeza wananchi- DJ anapata huduma za bure wasizopata wananchi wengine
   6. Anaendeleza ploti- amewakilishi wananchi fisadi katika hadithi
   7. Kuendeleza mtindo-wimbo

Sehemu ya E: FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1. Kisasili- Inaeleza kuhusu chanzo cha kifo
  2.  
   1. Huashiria mwisho wa hadithi
   2. Hutangaza funzo kwa wasikilizaji
   3. Huwapa wasikilizaji changamoto za kuwa watambaji hodarib wa ngano
   4. Humpisha mtambaji anayefuata
   5. Huwatoa wasikilizaji kutoka ulimwengu wa ubunifu na kuwarejesha katika ulimwengu halisi
   6. Hupisha shughuli zinazofuata
   7. Ni kitulizo kwa hadhira inayowacha kuwa makini baada ya kiishio
    (zozote 4x1)
  3. Sifa za kimtindo
   1. Majazi-wakamaya
   2. Nahau-tia chumvi
   3. Tashbihi-kama kinyonga
   4. Nidaa-Ndio wakamaya!
   5. Mdokezo wa methali- siwezi kuwa ganda la muwa
   6. Uzungumzi nafsia-Ngoitsi anajizungumzia
   7. Takriri/ Urudiaji-akatembea
   8. Taharuki-hatujui tukio la baadaye
    (za kwanza 6x1)
  4. Mbinu za ukusanyaji data
   1. Kusikiliza
   2. Kushiriki
   3. Kurekodi
   4. Kutazama
   5. Hojaji
   6. Mahojiano
    (zozote 4x1)
  5. Njia za kuendeleza fasihi simulizi katika jamii ya kisasa
   1. Tamasha za uigizaji/muziki
   2. Sherehe za harusi, Jandoni
   3. Vyombo vya habari-redio, runinga
   4. Kutafiti na kuandika kuhusu kipera hiki
   5. Utambaji wa hadithi
    (za kwanza 4x1)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Bunamfan Post Mock 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest