MOKASA Joint Evaluation Examination Kiswahili Karatasi ya 3 2016- Pre MOCK

Share via Whatsapp

A. HADITHI FUPI: DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE

  1. Swali la lazima.
    Kanda la Usufi

    “Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo”

    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

      Haya ni maelezo ya mwandishi.
      Ni kumhusu Sela.
      Sela alikuwa ametambua kuwa amekuwa mjamzito angali mwanafunzi.
      Sela alikosa utulivu darasani.
      Alipomweleza Masazu hali hiyo, yeye alimkana.

    2. Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili. (alama 4)

      Msemo
      mzo wa majuto
      Sela alishindwa atakavyofanya baada ya kutambua kuwa ni mjamzito na haypo mawazo yakamnyima utulivu masomoni. Alipomweleza rafikiye Masazu alikana na kumlaumu kuwa yeye hakujikinga.
      ( Kutaja tamathali alama 1, kuandika tamathali yenyewe alama 1, maelezo ya tamathali hiyo alama 2)

    3. Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika. (alama 12)

      Masazu anamkana Sela baada yake kumpachika mimba. Anamlaumu kwa nini hakujikinga.
      Wanafunzi wenzake Sela waliangua vicheko vya chini kwa chini majina ya kian Sela yanapotajwa wamwone mwalimu mkuu- kwao hilo sio tatizo lao.
      Mzee Butali anaona kuwa jukumu la kuwaelekeza wanafunzi ni la walimu pekee anapomuuliza mwalimu mkuu mbona wao huwaleta wanao shuleni.
      Mzee Butali kumwachia mkewe jukumu la kumshauri Sela. Anamlaumu kwa kutomwelekeza vizuri.
      Mzee Butali kumfukuza Sela na mamake kwake nyumbani. Aliona kuwa tataizo la Sela kuwa mjamzito halikufaa kumletea aibu kijijini na hivyo kuamua kumfurusha.
      Baada ya Masazu kupata kazi Dafina hakushughulika kumtafuta Sela ili amsaidie ulezi wa mtoto wao Kadogo . Ni Sela anayemtafuta.

      B. SEHEMU YA RIWAYA
      Kidagaa Kimemwozea: Ken Walibora

      Jibu swali la 2 au la 3

  2. “Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?"
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

      Haya ni maneno ya askari
      Alikuwa anamweleza Imani
      Imani na Amani walikuwa wamefugiwa kizuizuni
      Imani na Amani walikuwa wamesingiziwa mauaji ya kitoto uhuru.

    2. Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza. (alama 16)

      Maudhui yanayodokezwa ni udhalimu/ukatili- Askari hapa wanawanyanyasa kina Imani kisaikolojia/kiakili kwa kuwataja kama wauaji. Aidha wanawatesa wakiwa kizuizini.
      (Kutaja na kuyatolea mfano maudhui kwenye dondoo hili alama 2x1=2)
      Mifano kwenye riwaya
      Mtemi anapanga njama ya kuuawa kwa Chichiri Hamadi ili anyakue ardhi yake.
      Mtemi anamsingizia Yusufu mauaji ya babake na hivyo anafungwa jela bila hatia.
      Mtemi kuwanyang’anya maskini ardhi yao kwa mfano mamake Imani
      Mtemi kumpiga vibaya Amani kwa kisingizio cha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe kisha kumtupa kando ya Mto Kiberenge.
      Mwalimu Majisifu kuwaibia waandishi chipukizi miswada yao kisha kuichapisha kwa jina lake kama mwandishi
      Majisifu kumwachia mkewe jukumu la kuwalea watoto wao walemavu huku yeye akishiriki ulevi.
      Mtemi kumtumikisha Amani kazi nyingi huku akimlipa mshahara mdogo.
      Mtemi kukataa kumpeleka DJ zahanatini licha ya kuumwa na mbwa wake aliyekuwa akiugua.
      Mtemi anaendeleza dhuluma kwa wanyama mfano anamburura paka kwa gari lake jipya na kumuua.
      Mtemi kuamrisha Matuko Weye kutiwa kizuizini kwa kumkashifu hadharani wakati wa siku ya wazalendo
      Majisifu kumtumikisha Imani kazi nyingi pale nyumbani kwake kisha anamlipa mshahara wa kijungu jiko.
      Wakoloni kuwakataza waafrika kushiriki kilimo cha kisasa cha mimea na ufugaji katika eneo la Sokomoko.
      Wakoloni kuwaua waafrika waliopigania uhuru wao na kisha wanawarusha ndani ya Mto Kiberenge.
      Matajiri katika mji wa Sokomoko kuwatumikisha watoto katika ajira ya mapema. kwa mfano, DJ alikuwa maeajiliwa uchungaji na Bwana Maozi.
      Mtemi kumnyanyasa Lowela kimapenzi licha ya umri wake mdogo.
      Mtemi kumwacha mkewe katika upweke kwa kisingizio cha kwenda kuishughulikia migogoro ya ardhi kila wakati ilhali alikuwa akishiriki mapenzi nje ya ndoa.

  3. Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua. (alama 20)

    Kukutana kwa Imani na Amani kando ya ziwa Mawewa ni kwa kusadifu. Sadfa hii inayaokoa maisha ya Imani ambaye alikuwa amekusudia kujitoa uhai. Pia wawili hao wanajenga uhusiano unaoishia katika ndoa.
    Amani na Imani kukutana na DJ kando ya Mto Kiberenge. Mkutano huu unakuwa ni mwanzo wa uhusiano wao . DJ anawasaidia hawa wawili kupata kazi.
    Amani na Imani wanafika Sokomoko na kupata Mtemi na nduguye wakihitaji wafanyakazi . Sadfa hii inafanikisha wao kupata ajira japo za kijungu jiko.
    Amani na amu yake Yusufu kukutana jelani kisadfa. Hali hii inamwezesha Amani kutambua aliyewaibia familia yao mali yao pamoja na kumuua babu yake.
    Inasidifu kwamba Amani atokapo kibandani anakutana na DJ akipita hapo nje. Sadfa hii inamwezesha Amani kumtuma DJ amwite Amani aje amsaidie katika malezi ya mtoto Uhuru.
    Sadfa ya Majisifu kurejea na gazeti lenye taarifa kuhusu Chwechwe Makweche ambalo Imani analisoma.Sadfa hii inakuwa ni mwanzo wa mchakato wa kumrejesha Chwechwe nyumbani.
    Sadfa inawakutanisha Amani na Oscar Kambona gerezani. Huu unakuwa ni wanzo wa kujengekakwa urafiki baina yao.
    Amani anakutana na Oscar Kambona akiwa maemshika mateka mtemiakinuia kumuua. sadfa hii ndiyo inayookoa maisha ya mtemi Amani amteteapo.
    Mtemi anarudi nyumbani pasi na kutarajiwa na kumfumania amani chumbani mwake. Sadfa hii inasababaisha amani kupigwa kitutu na mtemi na kutalikiwa kwake Bi,. Zuhura.
    Sadfa ianwaleta pamoja Amani na Majisifu. Majisifu anaamua kumtunza baada yake kutoka zahanatini alikokuwa amelazwa. Sadfa hii inamwezesha Amani kumtambua mja aliyemwibia kazi yake.
    Siku ambayo Amani anarudi nyumbani baada ya miadi ya daktari mtemi anampita kwa gari lake bila kujali. sadfa hiui imetumiwa kubainisha ukatili wa mtemi.
    Ni sadfa kuwa Amani na Imani wanapokutana wamewapoteza wazazi wote na kutenganishwa na jamaa zao. Si ajabu wanasuhubiana sana kwa kufahamu hawakuwa na wengine wa kuwategemea ila wao wenyewe.
    Amani na Imani kukatiza masoma yao bila hiari yao. Imani analazimika kuacha shule kwa uchochole ilhali Amani anasingiziwa uchochezi na kufungwa jela alipokuwa chuoni.
    sadfa inabainika wakati Madhubuti na Amani wanakuwa na nia zinazooana kuhusu kumwondoa mtemi na kutetea haki. Usambamba wa nia zao unafanikisha kufichuliwa kwa uozo wa mtemi na watu aliowadhulumu kupata haki.
    Ni sadfa Madhubuti kumtembelea Amani pasi na kutarajiwa akapata akisoma kwa ufasaha na kwa sauti nzuri. sadfa hii inawezesha ugunduzi wa ukweli kuwa Amani ni mwanazuoni ambaye alikatiziwa masomo yake kwa njia haramu.
    Sadfa kubwa inaonyesha kuwa mtemi kuhusiana kimapenzi na Lowela ilhali mwanaye –Mashaka- kwa wakati huo huo alikuwa akihusiana kimapenzi na Ben Bella nduguye Lowela. Sadfa hii inafichua ouzo wake mtemi. Pia inamfanya Mashaka kuwehuka uhusianao wao na Ben Bella unapoisha baada ya ukweli kufichuka.
    Sadfa ianabainika wakati Majisifu anasafiri Wangwani na wakati huo huo Madhubuti anarejea nchini kutoka Urusi.Jamaa hawa wanapitana uwanja mmoja asifahamu mwenzake alikuwa pale pale wakati ule.
    Sadfa iandhihirika kwa Fao kumringa mwanafunzi wake na dadaye pia kuringwa na mwanaye Waziri wa Mifugo.
    Ni sadfa kuwa Fao ambaye anatoka katika familia inayojiweza kifedha anafaidika kwa ruzuku iliyotengewa wachochole swasa na Madhubuti kusomea Urusi kwa mtemi kuwashikia shokoa wanasokomoko kumchangia. sadfa hii ya kimatukio imetumiwa kuonyesha ukatili wa wenye uwezo.
    Sadfa inabainika kwa “mtoto wa kupanga” wa Imani (Uhuru) kufa kwa wahudumu zahanatini kupuuza kumshughulikia sawa na nduguye Imani aliyefariki akiwa mtoto mdogo kwa hali hizo hizo za kupuuzwa zahanatini. sadfa hii inashadidia kutowajibika kwa mfumo wa kutoa huduma za afya.

    C. SEHEMU YA TAMTHILIA
    MSTAHIKI MEYA
    : Timothy Arege

  4. Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

      -Msemaji ni mhubiri.
      -Msemewa ni Meya.
      -Wako katika ofisi ya Meya.
      -Walikuwa wakiomba kwa kelele na askari wakaingia wakidhani Meya kavamiwa.

    2. Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa “ walifanya vizuri kuja” katika tamthilia hii. (alama 4)

      Ni Askari
      Wanatumika kulinda baraza la Cheneo.
      Wanatii maagizo ya Meya bila maswali.
      Wanatumika kuzima migomo ya wafanya kazi.
      Wanageuka Meya na kumkamata mwishowe.
      Wanawasaliti wanacheneo kwa kuwalinda viongozi dhalimu.

    3. Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili. (alama 12)

      Migogoro yenyewe
      Meya na wafanyakazi
      -Wafanya kazi walitaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi.
      -Suluhisho: Migomo
      Meya na Siki
      - Meya hakutaka ushauri wa Siki.
      - Suluhisho: Siki aliendeleza mapambano
      Meya na Diwani III
      - Meya alikataa ushauri wa Diwani III
      - Suluhisho: Diwani III kuungana na wafanyakazi kudai haki.
      Meya na Wanajamii wote
      - Wanajamii walikosa huduma bora kutokana na uongozi mbaya wa Meya.
      - Suluhisho: Waliungana kumtoa Meya mamlakani.
      Askari na Meya
      - Askari walimgeuka Meya baadaye.
      - Suluhisho: Kumtia meya mbaroni.

  5. Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii. (alama 20)

    Maana: Mbinu hii hujitokeza wakati ambapo dalili Fulani hutokea kabla ya tukio Fulani.
    Mifano:
    Tunamwona Meya akiwa ameinama chini akiwa ameshika tama. Hii inaweza kuashiria kusambaratika kwa uongozi wake/ pingamizi zinazomkabil kama kiongozi
    Tunamwona Meya akipanga mafaili yake pamoja ofisini. Hii inaweza kuashiri kule kujaribu kutafuta ufuasi kwa kuunda kamati barazani kuwatuza marrafikiye.
    Ndege zinazowabeba mameya wageni zinaelekezwa uwanje wan chi jirani. Inaashiria kule kuharibika kwa hali Cheneo- kuzorota kwa taasisi muhimu kama vile sekta ya mafuta, usafi nk.
    Propaganda na hila hazikubaiki tena ma umma kwa mfano kupitia nyimbo bandia za “kizalendo”. Hii ni dalili za mwanzo wa mapinduzi.
    Harufu mbaya inayotokana uchafu mjini ni ishara ya mambo kwenda mrama. Hakuna mshahara, mafuta hakuna , kuna njaa.
    Meya anashindwa kunywa maji. Hii inashiria kushindwa kutekeleza wajibu wake. Kwa mfano kulipa mshahara, kusitisha ufisadi nk.
    Mayai madogo pia yanaweza kuashiria udunifu wa hali kama vile: umaskini umeenea, njaa, kiwango cha elimu kimeenda shule.
    Sauti za wafanyakazi ni ishara tosha ya kuwa wafanyakazi wamezinduka na wako tayari kutetea maslahi yao barabara.
    Kuwacha kazi kwa Waridi kunaweza kuashiria kuchoshwa na uongozi dhalimu wa Cheneo.
    Vifo vya wagonjwa vinaweza kuashiria ubovu au kusambaratika kwa taasisi muhimu za serikali kwa mfano sekta ya afya, elimu nk.

    D. SEHEMU YA USHAIRI

  6. Nitafukuzwa mbinguni
    Kwa ushairi wangu mbaya
    Lakini hata motoni nitaimba:
    Wanasema Wanasiasa ni kama jizi
    Lililosukuma mtoto pembeni
    Na kunyonya ziwa la mama
    Wakati amelala usingizi usiku.

    Wanasema
    Mwanasiasa afapo
    Tumejikomboa na domo
    Moja pana lizibwalo na mchanga
    Na kilima cha simenti ngumu
    Lisikike tena hadharani.

    Wanasema pia
    Kusema haki
    Kwa kawaida
    Wanasiasa hatuwapendi.
    Kupiga kura ni hasira za mkizi
    Ni basi tu. Ni Ah!
    Ah!
    Wanamalizia
    Nchi mmefiilisi waacheni walimu
    Wakajenga taifa jipya.

    Kama hamwezi kuona mbali
    Bure kuweka mkono usoni,
    Bure hakuna kichwa
    Kama hamwezi kufikiri.

    Ng’ombe amekamuliwa na wazungu
    Waarabu, wahindi na wao
    Sasa anatoa damu
    Vilivyobaki ni chai ya rangi
    Na madomo mapana zaidi
    Yaliyo bado hai.
    Kuimba nimeimba 



    1. Maswali
      Mshairi ana dhamira gani? (alama 2)

      Kuonyesha madhara ya uongozi mbaya
      Wanasiasa watahadhari dhidi ya tamaa.

    2. Shairi hili ni la kukatisha tama, tetea rai hii. (alama 2)

      Kuna umaskini—nchi mmefilisi…
      Dhuluma- wanasiasa ni kama jizi…linanyonya ziwa la mama, wakati mama amelala usiku
      Kuna wizi/ unyang’anyi…linasukuma mtoto pembeni…na kunyonya ziwa la mama.

    3. Onyesha matumizi mawili ya mishata. (alama 2)

      Ah! … wanamalizia…nchi mmefilisi waachieni walimu…wakajenge taifa. (tathmini majibu mengine kutoka kwa shairi)
      Nitafukuzwa mbinguni…kwa ushairi wangu mbaya…lakini hata motoni nitaimba.
      Wanasiasa ni kama jizi…lilosukuma mtoto pembeni…na kunyonya ziwa la mama.

    4. Eleza mbinu zozote nne za lugha zilizotumika katika shairi hili. (alama 4)

      Tashbihi- wanasiasa ni kama jizi.
      Nidaa- Ah! Ah!
      Msemo- hasira za mkizi.
      Jazanda – motoni- maskini. Ng’ombe – Raia maskini/ Raslimali
      Takriri – bure, bure

    5. Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi. (alama 4)

      Ng’ombe amekamuliwa na wazungu, warabu na wahindi. Sasa ng’ombe sasa ng’ombe anatoa damu na vilivyobaki ni chai ya rangi na wanasiasa walafi zaidi walio hai. Kuimba nimeimba.

    6. Fafanua umbo la shairi hili. (alama 3)

      Vina vinabadilika kutoka mshororo mmoja hadi mwingine
      Mizani inatofautiana kutoka ubeti hadi ubeti.
      Mizani inatofautiana ubeti hadi ubeti mwingine katika shairi.
      Kuna wingi wa matumzi ya mishata.

    7. Eleza maana ya mafungu ya maneno ya maneno yafuatayo: (alama 3)
      1. kupiga kura ni hasira ya mkizi

        kutekeleza amri

      2. kuweka mkono usoni

        kuona aibu/fedheha/soni

      3. ng’ombe amekamuliwa.

        raia/wananchi kufilisishwa.

  7. SABUNI YA ROHO

    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
    Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.

    Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao ‘mefufua, wanazuru kila njanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
    Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Maswali
    1. Taja nafsi nenewa. Thibitisha. (alama 2)

       Nafsi nenewa ni pesa/fulusi- waja wanazitumiwa kusuluhusha matatizo mbalimbali kama vile kununulia vifaa kulipa madeni.

    2. Eleza toni ya nafsi neni. (alama 1)

      Toni ya nafsi neni ni ya kulalamika. Analalamika kuwa pesa zimemkimbia.
      Toni ya kusifia – ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    3. Eleza arudhi zozote nne zilizozingatiwa katika utunzi wa shairi hili. (alama 4)

      Beti nne
      Mishororo mine katika kila mshororo
      Vina vinabadilika katika kila ubeti isipokuwa kibwagizo
      Mshororo wa mwisho ni kibwagizo- sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    4. Mshairi anawasilisha ujumbe gani katika mleo wa ubeti wa sita? (alama 1)

       Pesa zimeteka nyara roho za wapendanao na kuwafanya kuuana majumbani mwao.

    5. Ukitoa mfano eleza mbinu zozote tatu za lugha alizotumia mshairi. (alama 3)

      Balagha – ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
      Tashbihi – sinilipe ja bomu.
      Jazanda – jehanamu ni tatizo.
      Tashhisi – fulusi zinazoombwa kumwondoa mnenaji jehanamu, zina uchoyo.
      Takriri – ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    6. Andika ubeti wa nne katika lugha nathari. (alama 4)

      Mshairi anamsihi mvunja mlima (pesa) kuwasaidia maskini na mayatima ambao hali zao duni. Awabebe waliokwama na kuwainua walio chini. Ndiye sabuni ya roho na mvunja mlima (mtimiza yote).

    7. Jadili jinsi mshairi anatumia ruhusa ya mshairi. (alama 2)

      inkisari – mfano; sinilipue – usinilipue‘mefufua – umefufua
      kuboronga sarufi - mfano wema wako wameonja badala ya wameonja wema wako,Naondoka wangu moyo badala ya naondoka moyo wangu.

    8. Kwa kurejelea mpangilio wa vina eleza bahari ambamo shairi hili linaweza kuainishwa. (alama 1)

      ukaraguni – kila ubeti una vina tofauti na vya ubeti

    9. Fafanua maana ya:
      1. ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima

        - ni wewe ambaye hufurahisha na kusuluhisha matatizo yote

      2. jehanamu (alama 2)

         -  tatizo

        E. FASIHI SIMULIZI

    1. Eleza maana ya mivigha. (alama 2)

      Ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalum cha mwaka. Kwa mfano sherehe za jando, ya mazishi.

    2. Fafanua sifa zozote nne za mivigha. (alama 8)

      - huwa na kiongozi maalum
      - huwa na mahali maalum
      - huhusisha ulaji wa kiapo
      - mawaidha hupeana na watu mahususi
      - huandaliwa katika kipindi Fulani cha wakati

    3. Taja hasara zozote nne zinazohusishwa na mivigha. (alama 4)

      - huhusisha ushirikina
      - baadhi ya mivigha huenda kinyume na sheria na hukuika haki za binadamu
      - mivigha hugharimu pesa nyingi

    4. Eleza njia zozote tatu unazoweza kutumia kukusanya data kuhusu mivigha. (alama 6)

      - kuwepo kwa njia za kuburudisha
      - kutoweka kwa wataalamu wa kupitisha fasihi simulizi
      - kutokuwepo kwa njia bora ya kuhifadhi fasihi simulizi

Join our whatsapp group for latest updates

Download MOKASA Joint Evaluation Examination Kiswahili Karatasi ya 3 2016- Pre MOCK.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest