Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda High Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ni alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili

Lazima

  1. Wewe ni kiranja Mkuu shuleni wenu. Andika memo ukiwaonya wanafunzi dhidi ya visa vya utovu wa nidhamu shuleni.
  2. Ukiwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Wosia. Andika tahirir kuhusu umuhimu wa mitandao ya kijamii nchini.
  3. Tunga kisa kitakachoafiki maana ya methamli ifuatayo;
    'Mpanda ngazi hushuka'
  4. Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno;
    Mwanzoni mambo yalimwia magumu na majukumu mazito aliyopewa hadi alipokutana na .....................................

MARKING SCHEME

  1. Kuandika Memo.
    Mtahiniwa ajikite katika mambo yafuatayo:
    Muundo
    Sura iwe ya memo.
    Kichwa
    Kichwa kionyeshe kuwa ni memo
    Kutoka kwa
    Kwenda kwa Tarehe
    Mada/kiini
    Mwili
    Mtahiniwa ataje usuli wa mada memo.
    Mathalan; kumekuwa na visa vingi vya utovu wa nidhamu...
    Maoni
    – kuhusu visa vya utovu wa nidhamu mwiongoni mwa wanafunzi
    • Matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi
    • Wizi wa mitihani
    • Kupigana shuleni
    • Kurudia chakula katika bwalo
    • Kutowaheshimu viranja
    • Kuchelewa darasani
    • Kuchelewa kufika shuleni baada ya likizo
    • Kupiga kelele darasani
    • Wizi wa vitabu n.k
      Hatua zitakazochukuliwa
    • Kutumwa nyumbani waje na wazazi
    • Kupewa ushauri nasaha kuhusu madhara ya daa za kulevya
    • Kupimwa kwa wanafuzi kuhakikisha hawatumii dawa za kulevya
    • Kuwatuma kwa daktari wa kiakili
    • Wezi wa mitihani kurudia kufanya mitihani hiyo
    • Wezi wa vitabu kununua vitabu maradufu
    • Kupiga kelele darasani, wanafunzi wapewe kazi ya kufanya kuwaadhibu
    • Kurudia chakula –wataosha bwalo mara mbili kwa wiki
    • Kuchelewa kufika shuleni- mwanafunzi arudi na mzazi n.k
      Hitimisho
    • Sahihi
    • Jina
    • Cheo
  2. Kuandika tahariri.
    Mtahiniwa ajikite katika mambo yafuatayo:
    Muundo
    Sura iwe ya tahariri.
    Kichwa
    Kichwa kionyeshe kuwa ni Tahariri ya gazeti la Wosia.
    Mahali
    Tarehe
    Wakati
    Anwani iwe moja, ile ya Gazeti la Wosia.
    Mwili
    Mtahiniwa ataje usuli wa mada ya tahariri.
    Umuhimu wa mitandao ya kijamii
    Baadhi ya hoja ni kama;
    • Mitandao imesaidia katika mafunzo na utafiti wa kielimu wa mtandaoni • Burudani
    • Kuwaunganisha wasomi kutoka mataifa mbali mbali
    • Matangazo ya biashara
    • Urahisi wa kupata habari
    • Kuunganisha jamii
    • Kupunguza gharama za kuandaa mikutano
    • Kulipa kutumia simu na kupunguza matumizi ya pesa hai
    • Kununua na kuuza bidhaa miitandaoni kwa mfano Jumia, kilimall n.k
    • Huduma za benki za mitandao n.k
      Hitimisho
    • Msimamo wa gazeti utolewa hapa
    • Idhibati
    • Jina
    • Cheo
  3. Mpanda ngazi hushuka
    Hii ni insha ya methali
    Mwanafunzi aandike kisa kitakachoafiki methali hii.
    Maelezo ya methali:
    Mhusika alipanda ngazi mathalani kupata cheo au kazi. Sehemu ya pili mhusika akafutwa au kuachishwa kazi.
    Kisa kiwe na sehemu mbili mathalan, kupanda ngazi na sehemu ya kushuka. Kisa kioane na maelezo ya methali hii.
    Baadhi ya visa.
    • Mhusika aliyepata kazi baadaye akafutwa
    • Mhusika, biashara yake ilinawiri baadaye ikaporomoka.
    • Mchezaji aliyevuma baadaye akaporomoka n.k
  4. Insha ya mdokezo
    Hii ni insha ya mdokezo. Mwanafuzi aandike insha itakayoanza kwa mameno aliyopewa. Baadhi ya visa;
    • Mhusika aliyekubwa na shida fulani kisha akabahatika kupata mdhamini
    • Mwanafunzi aliyekumbwa na ugumu wa maisha shuleni kulipa karo kisha akapata mdhamini
    • Mwanafunzi aliyepata shida na somo fulani hadi alipopata rafiki aliymwelekeza n.k
      Tanbihi ya usahihishaji.
    • Mtahiniwa akikosea sura ya insha akadiriwe ila aondolewe 4S
    • Akikosa anwani asiadhibiwe- anwani sio lazima.
    • Hoja zilenge mada
    • Katika swali la kwanza, hatua zitakazochukuliwa zitolewe (huu ndio mtego)
    • Hakikisha kwamba urefu wa insha unazingatiwa (kadiria)
    • Insha ya methali iwe na pande mbili.
    • Tusome kazi za wanafunzi tafadhali. Tusipeane BAKISHISHI bila kusoma na kuandika udhaifu huo kwa karatasi ya mwanafunzi.
    • Iwapo ni lazima BAKISHISHI ni alama 03/20
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda High Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?