Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sunrise Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  • Insha zote sharti ziandikwe katika nafasi ulizoachiwa kwenye kijitabu hiki cha maswali.

 

  1. Suala la Afya ya akili ni suala nyeti na telezi na ambalo halijapewa umakini ufaao na wanajamii kutokana na unyanyapaa unaohusishwa nalo. Ukiwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mzalendo, andika tahariri kuangazia vyanzo vya changamoto hii na kupendekeza suluhu mwafaka.
  2. “Vijana ndio nguzo kuu katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa”. Thibitisha.
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha matumizi ya methali ifuatayo:
    Jifya moja haliinjiki chungu
  4. Tunga kisa kitakachokamilika kwa maneno yafuatayo:
    Kweli nimetambua kuwa, familia ni nguzo muhimu katika ujenzi wa jamii.

MARKING SCHEME

  1. Suala la Afya ya akili ni suala nyeti na telezi na ambalo halijapewa umakini ufaao na wanajamii kutokana na unyanyapaa unaohusishwa nalo. Ukiwa Mhariri Mkuu wa Gazeti  la Mzalendo, andika tahariri kuangazia vyanzo vya changamoto hii na kupendekeza suluhu mwafaka.
    Sura ya tahariri idhirike mfano;
    GAZETI  LA  MZALENDO         APRILI 1, 2023
    AFYA YA AKILI
    Au
    GAZETI  LA  MZALENDO
    ALHAMISI, APRILI 1, 2023
    AFYA YA AKILI
    Takwimu zinaonyesha kuwa takriban watu 3000 hujitia kitanzi kote duniani kila siku.
    Matatizo ya kiakili yanaweza kumfanya mtu kukosa kuona thamani ya maisha.
    Pana haja ya kila mja kulivalia njuga na kulitafutia suluhu tatizo hili.
    Ikumbukwe kuwa mja mwenye siha njema ni lulu kwa jamii
    VISABABISHI
    • Baadhi ya matatizo ya kiakili huweza kurithishwa kutoka kizazi hadi kizazi
    • Mama anapotumia dawa za kulevya katika ujauzito wake huweza kuzipitisha kwa mtoto aliye tumboni
    • Mama mjamzito anapokabiliwa na changamoto za kisaikolojia katika ujauzito wake
    • Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake-kutoumbika kwa vitivo vya akili
    • Utumizi wa dawa za kulevya. Mfano,kokeni,bang ink
    • Uwepo wa historia ya matatizo ya kiakili katika familia ya mhusika
    • Mhusika kuzongwa na lukuki ya changamoto  za kiuchumi,kumpoteza mpendwa, talaka nk
    • Mhusika kushuhudia au kuhusika katika shambulizi la kigaidi
    • Mhusika anayeugua ugonjwa  usio na tiba kwa muda mrefu-magonjwa yasiyopona k.v ukimwi,kisukari kifua kikuu na kadhalika
    • Mhusika aliyepitia dhuluma au kutelekezwa utotoni mwake na wazazi au walezi wake
    • Kukosa au kuwa na marafiki wachache
    • Hali ya kutengwa na marafiki,wanafamilia au wanajamii kwa ujumla

      SULUHISHO
    • Waathiriwa wanashauriwa kumuona daktari kwa matibabu
    • Haja ya kuandaa vikao vya ushauri-nasaha kwa waathiriwa
    • Daima watu wanaoonyesha dalili za kuwa na msongo wa mawazo wasiachwe kukaa peke yao
    • Waathiriwa wanashauriwa kuwatembelea wataalamu wa masuala ya kiakili kwa ushauri-nasaha ( psycho-social  support)
    • Viongozi wa kidini wanashauriwa kuwazungumzia na kuwaelekeza waumini
    • Watu washauriwe dhidi ya kujitenga na wanajamii wengine
    • Watu wanaopitia changamoto mbalimbali maishani wahimizwe kuyazungumzia kwa uwazi mambo yanayotanza ili wasaidiwe
    • Serikali inafaa kujenga vituo zaidi vya ushauri nasaha nchini ili kukabiliana na ongezeko la visa vya msongo wa mawazo
    • Mazoezi ya mara kwa mara ya viungo vya mwili
    • Kampeni ifanywe na wadau katika sekta ya afya kupitia kwa vikao vya umma ili kuhamasisha umma kuhusu masuala ya afya ya kiakili
    • Watu waonywe dhidi ya utumizi wa dawa za kulevya

      TANBIHI
    • Katika kulijibu swali hili,mtahiniwa aangazie kwa ukamilifu, visababishi na suluhu kwa matatizo ya kiakili miongoni mwa waja
    • Atakayeangazia visababishi pekee,atakuwa amepotoka,atuzwe D 03/20
    • Atakayejadili suluhu pekee bila kuangazia visababishi atakuwa amejibu swali ila atakuwa amepungukiwa kimaudhui. Asipite kiwango cha C 10/20
    • Atakayejadili visababishi na suluhisho atakuwa amejibu swali
    • Hili ni swali la kiuamilifu,hivyo basi sura ya tahariri ikikosa,mtahiniwa aondolewe alama 4S (sura)
    • Mkwaju wa hoja utiwe pambizoni kushoto mwa ukurasa hoja inapokamilikia
    • Mkwaju wenye kikia utumiwe kuonyesha hoja za visababishi
    • Mkwaju kamili utumiwe kuonyesha hoja za suluhisho
  2. “Vijana ndio nguzo kuu katika kuimarasha mshikamano wa kitaifa”
    Ni insha elekezi
    1. Mtahiniwa aeleze nafasi ya vyama katika utangamano wa kitaifa
    2. Anaweza kueleza/kuonyesha mambo ambayo vijana wanaweza kufanya ili kuleta mshikamano wa kitaifa
    3. Mtahiniwa anaweza kuonyesha hatua ambazo vijana wamechukua  kuleta mshikamano wa kitaifa
    4. Mthahiniwa ataje hoja na kutolea ufafanuzi na asitoe kisa

      Baadhi ya hoja
      1. Waepuke kutumiwa na viongozi kuleta uhasama miongoni mwa raia
      2. Wajisajili katika vyuo ndivyo katika maeneo mbalimbali nchini ili watagusane na raia wa makabila tofauti tofauti
      3. Wakubali kufanya kazi katika maeneo mbalibali nchini ili waingiliane na watu tofauti tofauti
      4. Watumie lugha yao kwa mfano sheng kuunganisha raia au kueneza hisia za kizalendo
      5. Wasajiliwe katika vikosi vya kulinda usalama ili waweze kudumisha usalama kwa njia ya amani badala ya vita
      6. Wahimizane kuchagua viaongozi kutoka katika makabila mbalimbali ili kukomesha ubaguzi wa kikabila na kinasaba
      7. Kushiriki katika shughuli za kiusomi pamoja kama vile makongomano ili kuhimiza mshikamano watahisi kama raia wenye maazimio sawa.
      8. Kushiriki katika mradi wa kazi kwa vijana unaowaleta vijana wa usuli tofauti pamoja
      9. Wafunzwe mbinuishi za kukabiliana na matatizo au changamoto kisha waziwasilishe mbinu hizi kwa wenzao vijana wawaelimishe wenzao
      10. Vijana wathaminiane na kuaminiana, kwa hivyo ni rahisi kuwashawishi wenzao kutangamana
      11. Ndoa mseto: kuoana kutoka makabila tofauti.
      12. Kushiriki kwenye michezo
      13. Kushiriki katika sanaa na maonyesho.
      14. Mtaala wa elimu kuhusisha masuala yanayohimiza umoja na ushirikiano wa kitaifa.
      15. Vijana washirikishwe katika masuala ya uongozi. Hasa masuala yanayoleta utangamano
      16. Hazina ya vijana itengwe ili kuhimiza ujasiriamali.
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha matumizi ya methali ifuatayo:
    Jifya moja haliinjiki chungu.
    Hii ni insha ya methali.
    Mtahiniwa abuni kisa kitakachodhihirisha maana ifuatayo: Hamna mtu anayefanya mambo pekee akaweza kufaulu.
    Hivyo anaweza kutunga kisa kinachosimulia:
    1. Mtu aliyekataa kushirikiana na wengine kufanya mambo fulani na mwishowe akashindwa kufaulu.
    2. Ushirikiano katika jamii k.v. shule, kijijini, nyumbani n.k. ulioleta faida.
  4. Tunga kisa kitakachokamilika kwa maneno yafuatayo:
    Kweli nimetambua kuwa, familia ni nguzo muhimu katika ujenzi wa jamii.
    Mwanafunzi anahitajika kutunga kisa kinachoonyesha nafasi ya familia katika kujenga jamii. Visa vifuatavyo vinaweza kudhihirika:
    1. Kisa cha familia kinachosomesha wana wao na kuwapa wosia ya kuishi vyema. Familia hiyo ikawa taa katika mazingira ambayo yalikuwa na matatizo awali.
    2. Kisa cha familia inayopuuza majukumu yake. Hivyo, wanafamilia hiyo kuwa tatizo sugu kwa jamii pana.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sunrise Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?