Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  1. Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa na Waziri wa Elimu kuchunguza njia mbalimbali za udanganyifu katika mitihani ya kitaifa. Andika kumbukumbu za mkutano uliofanyika kuwasilisha uchunguzi huo.
  2. Serikali ndiyo ya kulaumiwa kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya. Jadili.
  3. Andika kisa kitachodhihirisha maana ya methali ifuatayo: Mchuma janga hula na wa kwao
  4. Andika insha itakayoanza kwa maneno yafuatayo.
    Mahakama ilikuwa imejaa furifuri. Jamaa na marafiki walikuwepo. Nilisimama kizimbani. Mashahidi walikuwa wamekamilisha kutoa ushahidi wao. Jaji aliinua uso wake akaniangalia kwa ukali kisha…


MARKING SCHEME

  1. Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa na Waziri wa Elimu kuchunguza njia za udanganyifu katika mitihani ya kitaifa. Andika kumbukumbu za mkutano wa kuwasilisha uchunguzi huo.
    Tanbihi:Mwanafunzi asiandike insha ya Ripoti.
    Hii ni insha ya kumbukumbu.Mtahiniwa azingatie vipengele muhimu.
    1. Kichwa
      • Jina la mkutano
      • Mahali pa mkutano
      • Siku ya mkutano
      • Tarehe ya mkutano
      • Saa
    2. Utangulizi
      • Waliohudhuria
      • Waliotuma udhuru
      • Waliokosa kuhudhuria
      • Waalikwa
    3. Mwili
      • Ajenda
      • Kufunguliwa kwa mkutano
      • kusoma na kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliotangulia
      • Yaliyotokana na kumbukumbu hizo
        (Ajenda zinazohusu njia mbalimbali wanafunzi wanatumia kuiba mtihani)
      • masuala mengine
      • kufungwa kwa mkutano
    4. Hitimisho
      Sehemu za katibu na mwenyekiti kuachwa wazi na tarehe.
      Mwili/Maudhui
      Njia za udanganyifu
      1. Matumizi ya rununu. Kuwasiliana na wengine wa mbali kuhusu maswali ya mtihani.
      2. Walimu kuwasaidia kufanya mtihani kisha wanawapatia majibu.
      3. Wanafunzi wa vidato vingine kuwafanyia mtihani.
      4. Kusaidiana kwa watahini wenyewe katika cha mtihani n.k
      5. Kusoma kutoka vitabuni na vijikaratasi walivyovitiyarisha mapema.
      6. Kutoa majibu mtandaoni.
      7. Kupiga maswali na majibu picha
  2. Serikali ndiyo ya kulaumiwa kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya. Jadili.
    Hii ni insha ya mjadala. Iwe na muunda ufuatao;
    1. Kichwa- Mtahiniwa abuni kichwa mwafaka kulingana na swali
    2. Utangulizi- Mtahiniwa atangulize insha yake kwa kufafanua suala la kupanda kwa gharama ya maisha na mchango wa serikali katika kuishulikia.
    3. Mwili- Maudhui yajitokeze hapa. Mtahiniwa aandike hoja za kuunga mkomo kauli hii na zile za kupinga.
      1. Kuunga mkono( serikali imechangia vipi)
        1. Kuongeza bei ya bidhaa ya kimsingi k.m mafuta.
        2. kufutilia mbali ada za huduma za kimsingi kama vile matibabu, elimu, n.k
        3. Kuruhusu wengine kukwepa ulipaji wa ushuru.
        4. Kutopanua nafasi za kazi/ajira.
        5. Kulegea katika kupambana na tatizo la ufisadi.
        6. Kukosa kuhimiza wananchi na mashirika mbalimbali kubuni nafasi za kazi.
        7. Kuongeza wafanyikazi kupita kiasi katika idara mbali mbali za serikali kuu na kaunti.
      2. Kupinga ( sababu zingine kando na jukumu la serikali)
        1. Mabadiliko ya tabia nchi. k.m hali ya anga
        2. Kuzorota kwa uchumi duniani
        3. Kuzembea kwa wananchi huku wakitegemea usaidizi na misaada.
        4. Majanga yasiyozuilika k.m Korona
  3. Mchuma janga hula na wa kwao
    1. Hii ni insha ya methali
    2. Chuma ni kufanya kazi na kupata faida/ tungua matunda kutoka mtini.
    3. Janga-balaa /baa / shida / hatari / taabu
    4. Ajitafutiaye shida huathirika na jamii / jamaa yake .
    5. Mtahiniwa asimulie kisa /visa vitakavyoafikiana na methali.
    6. Asipinge methali.
    7. ;Ruwaza zifuatazo zinaweza kujitokeza;
      • Mhusika kushiriki raha za kilimwengu, akaambukizwa magonjwa yasiyotibika,hatimaye anarejea nyumbani anakougua , mzigo wa kumtunza unakuwa kwa familia yake.
      • Mhusika aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni au shirika fulani,
        Anafutwa kazi labda kutokana na uzembe au utovu wa maadili ya kikazi, anarejea nyumbani kwa familia yake; kule hana chochote hivyo basi anaishia kutegemea jamaa zake, huu unakuwa mzigo mkubwa kwa watu wake.
      • Mtoto ambaye anatokea kuwa mhalifu, anafikishwa kortini na kutozwa faini kubwa.Hii inakuwa gharama kwa familia yake kwa vile ndio wanaotakiwa kulipia.
      • Mwanafunzi ambaye anakosa kuwajibika masomoni shuleni , anafeli mtihani, maisha ya halafu yanakuwa magumu kwa hivyo jamaa zake wanalazimika kuingilia kati ili kumuauni kwa mahitaji ya kila siku
        Mtahini akadirie kisa cha mwanafunzi.
        Tanbihi
      • Mtahiniwa aandike kisa kuthibitisha matumizi haya ya methali
      • Pande zote za methali zishungulikiwe. Anayeshughulikia upande mmoja asipate zaidi ya alama C – 08/20
      • Anayekosa kulenga katika kisa chake amepotoka kimaudhui alam D -03/20
      • Kichwa kisiwe cha methali tofauti.( ondoa alama 4)
  4. Swali la nne
    1. Hili ni swali la dondoo.
    2. Mtahiniwa aanze kisa kwa maneno aliyopewa.
    3. Mtahiniwa anaweza kusimulia kuhusu mhusika aliyepatikana na hatia, asimulie kuhusu maisha ya jela.
    4. Mhusika aliyepatikana na hatia anaweza akasimuliwa alivyojipata mahakamani.
    5. Mhusika wa kisa anaweza kuwa hana hatia akaachiliwa huru. Asimmulie maisha ya uhuru, uhusiano wake na walionshtaki na walioshuhudia au tahadhari aliyochukua.
    6. Mhusika asiye na hatia anaweza kuelezewa jinsi alivyojipata katika hali hiyo (mahakamani).
    7. Mtahiniwa pia anaweza akasimulia hali kabla ya kushtakiwa na baada ya hukumu katika kisa kimoja.
    8. Mwanafunzi asipoanza kwa dondoo hajapotoka, amepungukiwa kimtindo akadiriwe alivyotimiza matarajio ya swali pamoja na vipengele vingine vya utahini.
      Tanbihi
    9. Akikosa kuanzia kwa dondoo alilopewa lakini kisa kiafikiane nalo, amepungukiwa kimtindo
    10. Akiongezea maneno baada ya dondoo au katikati achukuliwe kuwa ana upungufu wa kimtindo
    11. Lazima kisa kimhusu yeye mwenyewe. Asipojihusisha amepotoka kimaudhui na atuzwe D – 03/20

USAHIHISHAJI

Karatasi hii imedhamiria kutahini uwezo wa mtahniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mwanafunzi, kwa mfano kutunga sentensi sahihi, zenye utiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawázo asilia. Ubunifu rnwingi na hati nadhifu. Kutegemea maagizo ya swali lenyewe na lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa
mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.
Mtahini lazima asome insha yote ili aweze kukadiria viwango rnbalimbali vilivyopendekezwa.

KIWANGO CHA D
01-05

  1. Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile anachojaribu kuandika.
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahill kwa njia inayofaa.
  3. Lugha imevurugika, uakifishaji usiofaa na insha ina makosa ya kila aina ya kisarufi, kimaendelezo, mtindo mbovu u.k

VIWANGO TOFAUTI VYA D
D- (KIWANGO CHA CH1NI)
Maki 01-02

Insha haina inpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile. Kama vile kunakili au kujitungia swali na kulijibu,..

D WASTANI
Maki O3

Utiririko wa mawazo haupo, na insha haieleweki. Makosa ni mengi

D+ (KIWANGO CHA JUU)
Maki 04-05

Ingawa insha hii ina lugha dhaifu ya Kiswahili na makosa mengi ya kila aina, unaweza kutambua kile ambacho anajaribu kuwasilisha.

KIWANGO CHA C
Maki 06-10
Kiwango hiki kina makosa yafuatayo.

  1. Mtahiniwa anaweza kuwasilisha mawazo yake lakini kwa kiwango kisichoeleweka kikamilifu.
  2. Hana uhakika wa matumizi ya lugha.’
  3. Mada huwa haikukuzwa au kuendelezwa kikamilifu.
  4. Mtahiniwa anaweza kupotoka hapa na pale
  5. Kujirudiarudia ni dhahiri.
  6. Mpangilio wake wa kazi ni hafifu na hauna mtiririko
  7. Hana matumizi mazuri ya lugha.
  8. Mtahiniwa ana athari za lugha ya kwanza ambayo huonekana dhahiri, kama vile
    “papa” badala ya “baba”“chakura” badala ya” chakula”, “juki” badala ya “chuki”, “tata” badala ya “dada” u.k

C- ( KIWANGO CHA CHINI)
Maki 06-07

Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha mawazo yake.
Hana msarniati ufaao wala muundo wa sentensi.
Ana makosa mengi yamsamiati, hijai na matumizi mabaya ya sarufi.

C (WASTAN1) Maki 08

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwä njia hafifu.
  2. Hufanya makosa mengi ya sarufi.
  3. Hana ubunifu wa kutosha.
  4. Katika sentensi ndefu uakifishaji wake ni mbaya.
  5. Ana makosa kadha ya hijai na msamiati.

C+ ( KIWANGO CHA JUU)
Maki 09- 10

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri Iakini kwa njia isiyo na mvuto sana
  2. Dhana tofauti hazijitokezi
  3. Anatumia misemo, methali, tashbihi, tanakali za sauti n.k kwa njia isiyofaa.
  4. Utiririko wa mawazo bado haujitokezi wazi.
  5. Kuna makosa machache ya sarufi na hijai.

KIWANGO CHA B

  1. Katika kiwango hiki, mtahiniwa anoiomyesha kijjimudu lugha vilivyo.
  2. Mtahiniwa hudhihirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kujieleza.
  3. Hutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
  4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha kama vile kuandika sentensi kwa njia tofauti na ikaleta maana sawa.
  5. Mada huwa imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.

VIWANGO TOFAUTI VYA B
B- (KIWANGO CHA CHIN1)
Maki 11 - 16

  1. Mtahiniwa huwasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti..
  2. Kuna mtiririko mzuri wa mawazo.
  3. Ana uwezo Wa kutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi.
  4. Makosa machache yanaweza kutokea hapa na pale

B (WASTANI)
Maki 13

  1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
  2. Anawasilisha ujumbe wake waziwazi kwa mawazo
  3. yanayodhihirika.
  4. Matumizi ya lugha ya mnato huweza kudhihirika.
  5. Anatumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
  6. Matumizi ya tamathali za semi yanaanza kudhihirika.
  7. Makosa ni machache hapa na pale.

B+ (KIWANGO CHA JUU)
Maki 14- 15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa njia 4yovutia kwa urahisi.
  2. Kuna makosa ya hapa na pale ambayo mtahiniwa hakudhamiria kuyafanya
  3. Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri.
  4. Sarufi yake ni nzuri•
  5. Uakifishaji wake ni mzuri.

KIWANGO CHA A
Maki 16-20

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato. Ana ubunifu wa rnawazo yanayodbihirika na kutiririka.
  2. Ana uwezo wa kutumia tamathali za lugha ili kutoa hisia zake kwa njia iliyo bora na kwa urahisi.
  3. Uumbuji wake hudhihirisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hali ya kumvutia msomaji wake.

VIWANGO TOFAUTI VYA A
A- (Kiwango cha chini) - maki 16-17

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha
  2. Ana utiririko mzuri wa mawazo kulingana na mada
  3. Ana pamba lugha kwa kutumia tamathali za usemi
  4. Anazingatia matumizi mazuri ya msamiati na sarufi
  5. Uakifishaji wake ni mzuri zaidi
  6. Makosa ni machache yasiyokusudiwa

A WASTANI - Maki 18

  1. Mawazo yanadhihirika wazi.
  2. Makosa ni machache mno.
  3. Hutumia lugha ya mnato.
  4. Hutumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia.
  5. Sarufi yake ni nzuri
  6. Hutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi
  7. Hujieleza kikamilifu

A+ (KIWANGO CHA JUU)
Maki 19-20

  1. Mtahiniwa huwasilisha ujumbe kuiingana na mada
  2. Hutiririsha mawazo yake vizuri zaidi
  3. Hujieleza kikamilifu bila shida.
  4. Hutoa hoja zilizokomaa.
  5. Msamiati wake ni wa hali ya juu
  6. Makosa ya aina yoyote yasizidi matano
 A  A+
 A
 A−
 19 −  20
 18
 16 − 17
 B  B+
 B 
 B−
 14 − 15
 13
 11 − 12
 C  C+
 C
 C−
 09 − 10
 08
 06 − 07
 D  D+
 D
 D−
 04 − 05
 03
 01 − 02
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?