Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp
Maagizo
  • Jibu maswali yote katika nafasi ulizopewa.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  1. UFAHAMU (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

    Suala la mahusiano ya wanadamu katika jamii, uainishaji wake na udhihirikaji wake limewashughulisha wataalamu wa elimu jamii kwa dahari ya miaka.  Suala hili huwatafakarisha wataalamu hao kutokana na umuhimu wake katika maisha ya binadamu.

    Msingi mkuu wa uainishaji wa mahusiano hayo ni kukichuza kipindi cha mahusiano yenyewe.  Yapo mahusiano baina ya waja ambayo yanachukua muda mfupi, kwa mfano saa au dakika chache na mengine ambayo huenda yakachukua miaka ayami.

    Mahusiano ya muda mrefu kabisa ni yale yanayojulikana kama mahusiano ya kudumu.  Inamkinika kudai kuwa miundo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi huweza kuyadhibiti mahusiano hayo kwa kiasi kikubwa.   Watu wengi huitakidi kuwa uhusiano uliopo baina ya mtu na Jamaa yake utachukua muda mrefu, na kwa hiyo ni uhusiano wa kudumu.  Hali hii hutokana na uhalisi kuwa tunahusiana na Jamaa zetu kwa kipindi kirefu labda tangu ukembe hadi utu uzima wetu.  Uhusiano huu hautarajiwi kuvunjwa na umbali wa masafa baina yetu; tunaendelea kuwasiliana kwa barua au, katika enzi hii ya utandawazi, kwa kutumia nyenzo za teknohama kama mtandao na simu za mkononi na kudumisha uhusiano wetu wa  kijamaa.  Hata hivyo, inawezekana baadhi ya mahusiano ya kijamaa yasiwe ya kudumu.  Mathalan, uhusiano uliopo baina ya mke na mume, na ambao unatarajiwa kuwa wa kudumu au wa kipindi kirefu, unaweza kuvunjwa kwa kutokea kwa talaka.  Talaka hiyo inavunja ule uwezekano wa uhusiano wa kudumu unaofumbatwa na sitiari ya pingu za maisha.

    Katika ngazi ya pili, mahusiano ya kipindi cha wastani, kuna mahusiano yanayohusisha marafiki zetu maishani, shuleni au kwenye taasisi zozote zile, majirani zetu, wenzetu katika mahali mwa kazi, washiriki kwenye sehemu za ibada au za burudani na wenzetu kwenye vyama tofauti na makundi ya kujitolea.   Inawezekana kudahili kuwa baadhi ya mahusiano haya hususan baina ya marafiki na majirani huweza kuwa ya miongo na daima.  Hali hii huweza kutegemea muundo na mfumo wa jamii.  Kwa mfano, kwa wanajamii wanaoishi kwenye janibu fulani mahsusi, na kwa miaka tawili bila kuhajiri, uhusiano wao na majirani huweza kuwa wa kudumu.  Hali hii inasigana na hali iliyoko kwenye maisha ya mijini.

    Maisha ya mijini yana sifa ya kubadilikabadilika.  Isitoshe, kutokana na mfumo wa maisha ya  kibepari yameghosi ubinafsi mwingi.  Mawimbi ya mabadiliko na ubinafsi huweza  kuumomonyoa ukuta wa uhusiano wa kudumu.   

    Mwelekeo wa maisha ya siku hizi ya uhamaji kutoka maeneo au viambo walikoishi watu unasababisha kupombojea kwa mahusiano ya kudumu baina yao na majirani zao.   Uhusiano  kati ya wenza katika mazingira ya kazi unahusiana kwa kiasi fulani na ule wa majirani.

    Vimbunga vya ufutwaji kazi, ubadilishaji wa kazi, hali zisizotegemewa na mifumo ya kimataifa pamoja na hata mifumo ya kisiasa huweza kuathiri mshikamano wa wanaohusika kazini.

    Kiwango cha mwisho cha mahusiano ni uhusiano wa mpito au wa muda mfupi.  Mahusiano ya aina hii hujiri katika muktadha ambapo pana huduma fulani.  Huduma hizi zinaweza kuwa za dukani, kwenye sehemu za ibada, kwenye kituo cha mafuta, kwa kinyozi, kwa msusi na kadhalika.  Kuna sababu kadha zinazotufanya kuyazungumzia ya aina hii kama ya mpito.  Kwanza, uwezekano wa mabadiliko ya anayeitoa huduma hiyo ni mkubwa.  Si ajabu kuwa unaporudi kwa kinyozi au msusi unatambua aliyekushughulikia hayupo.  Hata hivyo, kuna vighairi hususan pale ambapo mtoa huduma anayehusika ni yule yule mmoja.

    Mahusiano ya mpito yanatawaliwa na uhusiano wa ‘chembe chembe.’ Uhusiano wa chembe chembe, bidhaa ya mfumo wa kibepari, unamaanisha kuwa kinachoshughulisha mtu ni chembe ndogo tu ya mwenzako.  Chembe hiyo inaweza kuwa huduma, kwa mfano, gazeti analokuuzia mtu, viatu anavyokushonea, nguo anazokufulia, ususi anaokufanyia na kadhalika.

    Mahusiano ya aina ya aina hii yametovukwa na hisia za utu na ni zao la mifumo ya kisiasa ya kiuchumi na kijamii.  Mtu anayehusiana na mwenzake kwa misingi ya chembe ndogo tu, huenda asijali kama mwenzake amekosa chakula, amefutwa kazi, amefiwa, ameibiwa na kadhalika.

    Suala kuu tunalopaswa kujiuliza ni:  je, tunahusiana vipi na Jamaa zetu, marafiki zetu majirani zetu? Je, uhusiano wetu na raia wenzetu ni wa aina gani? Je, uhusiano wetu na nchi yetu ni wa mpito au ni wa kudumu?

    Maswali
    1. Taja kigezo cha kuzungumzia mahusiano.        (al. 1)
    2. Eleza imani ya watu kuhusu mahusiano ya watu.    (al. 1)
    3. Fafanua athari ya teknolojia kwenye mahusiano ya watu. (al. 2)
    4. Eleza sababu nne kuu za kuharibika kwa mahusiano katika maisha ya leo.  (al. 4)
    5. Taja sifa kuu za mahusiano ya muda mfupi.    (al. 2)
    6. Je, kifungu hiki kina ujumbe gani mkuu?    (al. 2)
    7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika kifungu.    (al. 3)
      1. inasigana
      2. yameghoshi
      3. vighairi
  2. UFUPISHO (Alama 15)
    Soma kifungu kisha ujibu maswali


    Jamii ya leo inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni ya maarifa.  Inawezekekana kusema kuwa uchumi wa jamii za leo na zijazo utategemea maarifa zaidi kuliko utakavyotegemea wenzo wowote mwingine.  Utambuzi wa uwezo mkubwa wa maarifa katika maisha ya binadamu ndio msingi wa watu kusema ‘maarifa ni nguvu’

    Maarifa huelezwa kwa tamathali hii kutokana na uwezo wa: kuyadhibiti kuyaendesha, kuyatawala na kuyaongoza maisha ya binadamu popote pale walipo.  Mtu ambaye ameyakosa maarifa fulani huwa ameikosa nguvu hiyo muhimu na maisha yake huathirika pakubwa.  Kwa msingi huu, maarifa yanaweza kuangaliwa kama utajiri mkubwa ambao binadamu anaweza kuutumia kwa faida yake au kwa faida ya wanajamii wenzake.  Ukweli huu ndio unaoelezwa na methali ya Kiswahili: ‘Elimu ni mali.’ Elimu ni chimbuko la maarifa muhimu maishani. 

    Msingi wa utajiri na maendeleo ya binadamu popote alipo basi ni maarifa. Je, maarifa kwa upande wake yana sifa gani?  Maarifa yenyewe hayana upinzani.  Maarifa uliyo nayo huweza kuwa na watu wengine pasiwe na upinzani baina yenu kwa kuwa kila mmoja ana maarifa sawa.   Kila mmoja ana uhuru wa kuyatumia maarifa hayo kama chanzo cha kuyazalisha maarifa mengine.  Utumiaji wa maarifa yenyewe hauyamalizi maarifa hayo.  Maarifa hayawezi kugusika ingawa mtu anaweza kuyanyumbua maarifa yenyewe kwa kuyatumia kwa namna tofauti.

    Maarifa huingiliana na maarifa mengine.  Maarifa aliyo nayo mtu mmoja huweza kuhusishwa na maarifa aliyo nayo mtu mwingine ili kuvyaza au kuzuka na maarifa tofauti.  Maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa namna ambavyo mtu hawezi kufanya bidhaa nyingine ile.  Kwa mfano, ni muhali mtu kulalamika kuwa hawezi kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa sababu ana mzigo mzito wa maarifa kichwani.

    Sifa nyingine muhimu ya maarifa ni kuwa yanaweza kuwasilishwa kwa njia za ishara au mitindo mingine ya kidhahania.  Ikiwa unataka kukihamisha chombo fulani kutoka sehemu moja hadi nyingine, lazima uwazie ukubwa wake, uzito wake na labda hata umbali wa panapohusika.  Maarifa huweza kubadilishwa au kugeuzwa na kuwa ishara ambazo huyafanya kuwasilishwa kwa njia nyepesi kuliko kwa mfano ikiwa mtu atayawasilisha katika muundo wa kwa mfano, kitabu.

    Maarifa yana sifa ya uhusianaji.  Kipengele fulani cha maarifa huwa na maana kinapowekwa sambamba au kugotanishwa na kipengele kingine cha maarifa.  Huo huwa muktadha mzuri wa kueleweka au kuwa na maana.  Kwa mfano, neno ‘mwerevu’ huweza kuwa na maana kwa kuwekwa katika muktadha wa ‘mjinga’, mjanja’, mjanga’, ‘hodari’ na kadhalika.

    Maarifa huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo sana.  Suala hili linaeleweka kwa njia nyepesi tunapoangalia maarifa katika muktadha wa teknolojia.  Data zinazowahusu mamilioni ya watu, ambazo zingehitaji maelfu ya maktaba na lukuki ya vitabu, huweza kuhifadhiwa kwenye kifaa kidogo kinachoweza kutiwa mfukoni.

    Maarifa hayawezi kudhibitiwa au kuzuiliwa mahali fulani yasisambae. Maarifa huenea haraka sana.  Maarifa ni kitu kinachoepuka pingu za watu wanaopenda kuwadhibiti binadamu wenzao.  Hata pale ambapo mfumo wa kijamii au wa kisiasa unafanya juu chini kuwadhibiti raia au watu wenyewe, ni muhali kuyadhibiti maarifa yenyewe. Inawezekana kuzidhibiti njia fulani za ueneaji wa maarifa lakini maarifa hayo yatapata upenyu wa kusambaa. Ni kweli kuwa maarifa ni nguvu inayozishinda nguvu zote.
    1. Fupisha aya ya pili na ya tatu kwa maneno 55-60. (al. 6)
      Matayarisho
      Nakala safi
    2. Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane kwa maneno 100 - 110.    (alama 8, 1 mtiririko)
      Matayarisho
      Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
    1. Andika maneno yenye miundo ifuatayo. (al. 2)
      1. Kizuiwa ghuna cha midomo, kiyeyusho cha midomoni, irabu ya kati chini, kilainisho ambacho wakati wa kutamka hewa hutambaa kinywani na irabu ya kati nyuma.
      2. Nazali ya ufizi, kipasuo ghuna cha kaakaa laini, irabu ya nyuma juu, kimadende cha ufizini na irabu ya mbele juu.
    2.  
      1. Eleza maana ya sauti mwambatano. (al. 1)
      2. Andika mfano mmoja wa sauti mwambatano inayotamkiwa ufizini. (al. 1)
    3. Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika wakati uliopita, hali isiyodhihirika. (al. 1)
      Mkurugenzi anawaamuru wafanyikazi katika kampuni yake.
    4. Andika neno lenye mofimu zifuatazo. (al. 3)
      Nafsi ya tatu wingi, njeo, kielezi cha namna kinachojengwa kwa silabi moja, yambwa, kauli tenda.  (al. 3)
    5. Tunga sentensi moja yenye mpangilio ufuatao wa maneno: (al. 2)
      Nomino ya kitenzi jina, kivumishi cha kuashiria cha wastani, kivumishi cha pekee chenye dhana ya bila kusaza,na kitenzi halisi.
    6. Andika ukubwa wa sentensi ifuatayo katika hali ya ukanusho. (al. 1)
      Mbwa wenye ukali walimfukuza mtoto.
    7. Tunga sentensi ya masharti inayoonyesha kuwa kitendo kilifanikiwa kutokana na kufanikiwa kwa kitendo kingine. (al. 1)
    8. Andika katika wingi. (al. 1)
      Ukwato uo huo ulimsaidia kutambua kondoo wake.
    9. Andika sentensi hii upya ukianza na yambiwa. (al.1)
      Mbunge wa Mtondo aliwajengea watu wake hospitali sita mwaka uliopita.
    10. Andika sentensi zenye vipashio vifuatavyo. (al. 3)
      1. Yambwa tendwa ambayo ni kirai nomino
      2. Kishazi tegemezi ambacho ni chagizo ya wakati
      3. Kirai kihusishi ambacho ni kielezi cha mahali.
    11. Andika kinyume cha sentensi ifuatayo ukizingatia maneno yaliyopigigwa mstari. (al. 1)
      Mvua ilinyesha wageni walipofika.
    12. Eleza matumizi ya kiambishi na neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo. (al. 2)
      Mtahiniwa alijisuta baada ya kupata alama tano kwa ishirini.
    13. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi. (al. 3)
      Yalijaa yakamwagika.
    14. Onyesha miundo yoyote miwili ya ngeli ya KI-VI. (al. 2)
    15. Andika katika usemi halisi. (al. 3)
      Mkufunzi alishangaa na kutaka kujua kama Awiti ndiye aliyekuwa amemwibia mwenzake siku iliyotangulia.
    16. Andika sentensi yenye muundo ufuatao. (al. 2)
               __
      KN – (S) + KT [(Ts + Ts + T + RE(E+E)]
    17. Nyambua vitenzi hivi katika kauli ambayo hutoa dhana ya kinyume bila kubainisha mtendaji. (al. 2)
      1. fuma
      2. shona
    18. Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha Kibantu na kihusishi cha mtenda. (al. 2)
    19. Ainisha sentensi ifuatayo kiuamilifu. (al. 1)
      Jibu maswali yote katika sentensi hii.
    20. Andika sentensi ifuatayo upya ukibadilisha maneno yaliyopigiwa mstari kuwa nomino. (al. 3)
      Mchoraji alichora picha hiyo vizuri akawafurahisha watalii.
    21. Mama ni kwa nina na akali ni kwa …………….. na dua ni kwa …………………. (al. 2)
  4. ISIMUJAMII (ALAMA 10)
    Wewe ni wakili katika kesi ya jinai inayoendelea katika Mahakama ya Haki na Uwajibikaji. Hata hivyo, umegundua kuwa hadhira haijamakinika kukusikiliza.  Fafanua sifa za lugha utakayotumia ili hadhira imakinike.    (alama 10)

MARKING SCHEME

  1. UFAHAMU
    1. Kukichuza/kupima/kukadiria/kuchunguza kipindi cha mahusiano.    (Alama 1x1=1
    2. Ni wa kudumu/ni wa muda mrefu/hautavunjika/ ni wa milele.    (Alama 1x1=1)
    3.  
      1. Huwezesha watu walio mbali kuwasiliana.
      2. Ni nyenzo ya kudumisha uhusiano.      (Alama 2x1=2)
    4.  
      1. Talaka
      2. Maisha ya mjini ambayo yanabadilikabadilika.
      3. Mfumo wa maisha ya kibepari/ubinafsi mwingi.
      4. Uhamaji
      5. Ufutwajikazi
      6. Ubadilishaji kazi
      7. Hali zisizotegemewa
      8. Mifumo ya kimataifa
      9. Mifumo ya kisiasa    (zozote 4 x 1 = Alama 4)
    5. Hujiri katika muktadha wa huduma fulani/Ni uhusiano wa chembe chembe/Ni uhusiano ulio tovuka na hisia za utu.
    6. Aina tofauti za mahusiano/mahusiano katika jamii/Tuhakiki/tuchunguze,mahusiano ya jamii.  (Alama 1x2=2)
    7.  
      1. Inasigana – inatofautiana/inapingana/inakinzana/inahitilafiana    (Alama 1x1=1)
      2. yameghoshi –  yamejaa/yamesheheni/yamebeba/yametawaliwana/yameseta/yamerundika/yazindisha/yameongeza (Alama 1x1=1)
      3. Vighairi – kinyume/tofauti      (Alama 1x1=1)

        Mwongozo wa kuadhibu makosa
        Mwongozo wa usahihishaji wa karatasi hii uzingatiwe
  2. UFUPISHO
    1. Fupisha aya ya pili naya tatu kwa maneno 55-60. (alama 6)
      1. Maarifa huyadhabiti, huyaendesha, huyatawala na kuyaongoza maisha ya binadamu.
      2. Anayekosa maarifa huathirika pakubwa.
      3. Maarifa ni utajiri mkubwa ambao binadamu hutumia kwa faida yake na wanajamii wenzake.
      4. Elimu ni mali chimbuka cha maarifa muhimu maishani.
      5. Maarifa hayana upinzani.
      6. Kila mtu ana uhuru wa kutumia maarifa kuzalisi maarifa mengine/kujanyambua maarifa yenyewe kwa namna tofauti
      7. Utumiaji wa maarifa hauyamalizi maarifa.
      8. Maarifa hayawezi kugusika.      (zozote 6 x 1 = Alama 6)
    2. Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane kwa maneno 100-110. (alama 8, 1 ya utiririko)
      1. Maarifa huingiliana na maarifa mengine. 
      2. Maarifa hutolewa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
      3. Yanaweza kuwasilishwa kwa njia za ishiara au vitendo vingine ya kidhahanio.
      4. Yanaweza kubadilishwa/kugeuzwa.
      5. Yana sifa ya uhusianaji.
      6. Maarifa yanaweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo sana. 
      7. Maarifa hayawezi kudhibitiwa /kuzuiliwa yasizambae/maarifa huenea haraka sana.
      8. Huepuka pingu za watu kuepuka wenzao.Maarifa ni nguve inayozishinda nguvu zote.   (zozote 8 x 1 = Alama 8)

        Kutuza
        Hoja 6, alama 6, utiririko - alama ½
        Hoja 8, alama 8, utiririko - alama ½
        JUMLA = 15
        Kuadhibu
        S – hadi makosa 6 (6x½=3)
        H – hadi makosa 6 (6x½=3)
        Ziada – maneno 10 – ondoa alama 1
  3.  
    1.  
      1. bwalo Alama 1/0
      2. nguri Alama 1/0
    2.  
      1. Sauti mwmbatano ni konsonanti mbili au zaidi ambazo huwekwa pamoja na hutamkwa kama sauti moja.   Alama 1/0
      2.  
        • /nd/ - ndizi
        • /nz/ - upanzi
        • /sw/ - mswaki
        • /ndw/ - ndwele
        • /nzw/ - tunzwa
    3. Mkurugenzi alikuwa awaamuru wafanyikazi katika kampuni yake. Alama 1/0
    4. walivyompenda/wanavyompenda/walivyonipenda
      (tathmini majibu ya wanafunzi)
    5. Kucheka huko kwote kunafurahisha. Alama 4x½=2
    6. Majibwa yenye ukali hayakulifukuza toto/jitoto/ Alama 1/0
    7. Nisingeenda nisingempata. /Nisingeenda nisingelimpata./Nisingelienda nisingelimpata. Alama 1/0
    8. Kwato zizo hizo ziliwasaidia kuwatambua kondoo wao. Alama 1/0
    9. Watu wake walijengewa hospitali sita na mbunge wa Mtondo. Alama 1/0
    10.  
      1. Mama alipiga mtoto wake. Alama 1/0
      2. Mvua ilinyesha walipofika. Alama 1/0
      3. Wanafunzi walisiamama juu ya meza. Alama 1/0
    11. Mvua ilipusa wageni walipoondoka. Alama 2x½=1
    12. ji – kirejeshi cha hali ya kujitendea
      kwa – sehemu ya kitu kizima. Alama 1x2=2
    13.  
      SwaSukF42023PrMP2
    14.  
      • KI-VI, Mfano, kiti – viti
      • Ch-Vy, Mfano, chombo-vyombo
      • Ki - ɵ, mfano, kimo
      •  ɵ - Vi, mfano, vita        Alama 1x2=2
    15. “Lo! Awiti, wewe ndiwe ulikuwa umemwibia mwenzako jana?” Mkufunzi aliuliza.
      au
      “Lo! Awiti ndiye alikuwa amemwibia mwenzake jana?” Mkufunzi aliuliza.   Alama 6x½ = 3
    16. Aliyekuwa kanisani alikuwa angali anatembea vizuri sana. Alama 1x3=3
    17.  
      1. fumuka Alama 1x1=1
      2. shonoka Alama 1x1=1
    18. Walimu na wanafunzi walipokelewa na waziri. Alama 1x2=2
    19. Sentensi agizi/sentensi ya maagizo Alama 1x1=1
    20. Uchoraji mzuri wa picha hiyo wa mchoraji ulisababisha/uliwapa/uliwaletea furaha (kwa) watalii.
      Kuchora kuzuri kwa mchoraji wa picha hiyo ulisababisha/uliwapa/uliwaletea furaha watalii. Alama 1x2=2
    21. Ndogo/chache/haba/kalili
      ombi/sala Alama 1x2=2
  4. ISIMUJAMII
    Sifa za sajili ya mahakamani/kortini
    1. Matumizi ya msamiati maalum mfano kesi, mshukiwa, hakimu, mshtakiwa.
    2. Kurejelea kwa vitabu kama katiba na sheria za nchi mfano sheria kifungu nambari 3 sehemu 4…
    3. Lugha ya kudadisi au maswali na majibu ili kuweza kubaini ukweli kabla ya uamuzi kufanywa.
    4. Sentensi ndefu ndefu ili kutoa maelezo ya kina kuhusu uamuzi wa kesi husika.
    5. Matumizi ya lugha rasmi mfano Kiswahili au kiingereza.
    6. Utohozi wa misamiati mfano jaji - judge, korti - court.
    7. Matumizi ya msamiati uliokopwa mfano amicua curiae.
    8. Lugha nyepesi na rahisi kueleweka na watu wa viwango vyote vya elimu.
    9. Matumzi ya lugha sanifu ili kuepuka kupotosha ujumbe au maelezo yanayotolewa.
    10. Kuhamisha na kuchanganya ndimi kwa mfano “Mshtakiwa unaweza kujitetea sasa. Tell the court what happened on that day.”
    11. Lugha ya unyenyekeve na heshima hasa kutoka kwa mshatakiwa mfano “mheshimiwa jaji, naomba mahakama inihurumie kwa kunipunguzia kifungo…”
    12. Kuzungumza moja kwa moja na mshukiwa – wewe mshukiwa.
    13. Urudiaji au uradidi ili kuweka wazo wazi/kusisitiza.
    14. Msamiati wa kawaida kupewa maana maalum, kwa mfano, learned friend kummanisha mwanasheria.
    15. Kauli fupifupi hasa wakati wa kuhoji.
    16. Lugha ya kushawishi ili kutetea upande wako.
    17. Matumizi ya lugha chakavu/kikale.
    18. Kutumia lugha ya mapokezano.
    19. Lugha ya kutaja tareje na wakati wa tukio.
    20. Matumizi ya ishara/viziada lugha ili kusisitiza na kufafanuaa ujumbe.  zozote 10x1=10

      Kutaja: ½ alama
      Mfano/maelezo: ½ alama
      Mfano bila maelezo: 0
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?