Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Lainaku 1 Joint PreMock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Riwaya, Tamthilia, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  • Watahiniwa lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

                                                                             SEHEMU A: USHAIRI

  1. LAZIMA
    T. Arege: Wimbo wa Kichaa
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.

    Bustani za jadi
    Maua ya kuchezea vipepeo
    Na pua kufurahisha
    Sasa ni mabaki ya kumbukumbu
    Za yaliyojiri hapa
    Na kukiacha Kijiji kinywa wazi.

    Hapa walimpiga mwereka
    Dada yangu; mdogo wangu
    Shuleni akitoka
    Na mkoba wa kilo nzito za vitabu
    Chini akakandamiziwa
    Wakachana mbuga na wake ubikira!

    Pale kando ya mto
    Walimvizia na kumburura shangazi
    Binamu zangu wadogo wakiona
    Marinda wakamchania
    Kabla ya kumtia kidonda shangazi
    Naye ami kumchania kovu moyoni!

    Ni hapa kando ya barabara kuu
    Ambapo nyanyangu walimshika mkono
    Uchochoroni wakamburuta
    Na kumfanya kujutia
    Bahati mbaya ya kuishi kwingi
    Akaganda uchochoroni
    Hadi alipoletwa nyumbani kesho yake
    Na wachungaji wa muchungani.

    Si hapa walipomshurutisha mama
    Chini wakamkanyagia
    Kama kuku wa kuchinja
    Baada ya yake sidiria kuikata?
    Si hapa sebuleni mwetu?
    Si hapa sokoni
    Nilipopata vazi la stara
    La wangu mke mpendwa
    Lilikatwa yake mihimili?

    Yule kichaa wa mwetu sokoni.
    Akawa kichwani amelivaa
    Na kuimba wimbo wa maombolezi
    Huku wanakijiji wakimpuuza
    Na watoto kumcheka?

    Ni hapa ambapo usiku ulipoingia
    Hawakusita kuhakikisha kuwa
    Yule kichaa amewazalia mtoto
    Na kujitia kundini kushangaa
    Kilichomtuma atake kujifungua!

    Maswali
    1. Tambulisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
    2. Eleza dhamira ya mshairi. (alama 2)
    3. Fafanua mbinu za kimtindo zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 5)
    4. Eleza aina za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 4)
    5. Bainisha toni ya mshairi. (alama 2)
    6. Onyesha matumizi ya mishata katika shairi hili. (alama 1)
    7. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 4)

                                                                        SEHEMU B: RIWAYA
                                                                        A.MATEI: Chozi la Heri
                                                                          Jibu Swali La 2 au 3
  2. ‘‘Tokeni ! Tokeni kama bado mnataka kuishi!”
    1. Jadili umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kuendeleza ploti ya riwaya hii. (alama 4)
    2. Jadili umuhimu wa mandhari haya katika kuendeleza riwaya ya Chozi La Heri . (alama 6)
    3. Riwaya ya Chozi la Heri imekumbwa na migogoro mingi. Jadili migogoro hii na visababishi vyake. (alama 10)
  3. ‘‘Machozi ya mwanaume hayapaswi kuonekana hata mbele ya majabali ya maisha”
    1. Eleza majabali ya maisha yaliyomkumba msemewa katika dondoo hili kwa kurejelea riwaya nzima. (alama 10)
    2. Kwa kurejelea hoja kumi kutoka kwenye riwaya, jadili namna haki za watoto zinavyokiukwa. (alama 10)

                                                                         SEHEMU C: TAMTHILIA
                                                                     T.M. Arege: Bembea ya Maisha
                                                                              Jibu swali la 4 au la 5
  4.  
    1. Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho (alama 10)
      ‘‘Mwanangu usitake sana kuhoji alacho kuku. Utachafukwa roho umchukie kuku bure. Wala usitake kujua nyuki ameitengenezea nini asali. Hutaila. Maadamu yameshakuja,yapokee. Mtoto akinyea kiganja hakikatwi wala hatuulizi kwa nini. Ni maumbile.
      Maumbile hayo,sawa na vidole, hayafanani. Sawa na watoto wachezeao bembea, tumeicheza na tungali tunaicheza sehemu yetu kwa zamu. Haidhuru iwe ya kamba au chuma. Muhimu ni kwamba tumeshirikiana kusukumana kwenye bembea ya maisha. Upo wakati inakuwa raha tele na upo wakati inakatika na kutubwaga. Hiyo ndiyo raha hasa ya maisha. Ni sawa na chombo kinachomenyana na mawimbi katika bahari. Hutufanya kuwa macho katika safari…”
    2. Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia usukaji wa tamthilia. (alama 10)
  5. ‘‘Walishasema baada ya dhiki ni faraja, Faraja ni zao la dhiki. Leo hii kikapu cha mama kimejaa ndago.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Eleza vipengele viwili vya kimtindo kwenye dondoo. (alama 4)
    3. Eleza maudhui mawili yanayodokezwa kwenye dondoo. (alama 2)
    4. Eleza sifa za msemaji. (alama 5)
    5. Kwa kutolea mifano mwafaka eleza dhiki alizopitia mama ambaye sasa kikapu chake kimejaa ndago. (alama 5)

                                                                     SEHEMU D: HADITHI FUPI
                        D.W Lutomia na P. Muthama (Wah): Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine
                                                                      Jibu Swali la 6 au La 7
  6. R.Wangari: Fadhila za punda
    Anwani ‘Fadhila za Punda’ inaafiki hadithi hii” Thibitisha. (alama 20)

  7. W.N Ogeche: Sabina
    1. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo; (alama 6)
      ‘Athari ya mawazo yake ilijiandika dhahiri shahiri usoni mwake. Alianza kwa kuachia tabasamu pana mithili ya msafiri aliyefika salama. Baada ya dakika chache machozi yalianza kumtoka njia mbilimbili huku kajishika tama. Alifikiria kuhusu mtihani uliodhamiriwa kuanza siku ya Jumanne. Mtihani ambao ungemwezesha kupata ufadhili katika shule ya upili ya bweni ikiwa angepita vyema. Hili ndilo wazo lililozua tabasamu. Lakini, angefeli je?Hatima yake ingekuwa ipi? Maswali haya yalimliza yakamwacha akisinasina kama mgonjwa wa mafua. Akiwa katika hali hii, aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu, ‘‘mizizi ya elimu ni michungu ila matunda yake ni matamu. Ikiwa mnataka kuyaonja matunda ya elimu, lazima mtie bidii kwani mtaka cha mvunguni sharti ainame.”
    2. Bainisha mbinu mbili zinazoweza kutumiwa kutambua sifa za mhusika Sabina kwa kurejelea hadithi Sabina. (alama 2)
    3. Taja na ueleze aina mbili za taswira zinazojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 2)
    4. Kwa kutolea mifano mwafaka eleza matatizo yanayomkumba mwanamke katika hadithi Sabina. (alama 10)

                                                                    SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
  8.  
    1. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
      Kila kukicha mashaka
      Ni kero hili si huba
             Mimi pendo la viraka, heri demu la mkoba
             Mimi mno nataka, kuishi nawe muhiba
             Pendo viraka viraka
             Litanishinda kuziba
      Kamwe sitoshughulika
      Nawaje wenye kuziba
             Viumbe wanosifika, kwa fedha, chuma na shaba
             Walostarabika, si mimi wa tobatoba
             Pendo viraka viraka
             Litanishinda kuziba
      Naapa sitojitweka
      Limenichosha si haba
            Nasomba vyangu viraka, nitie kwenye mkoba
            Sikuye ya kuzinduka, mjinga hawi ni juba
            Pendo viraka viraka
            Litanishinda kuziba
      1. Huu ni wimbo wa mapenzi. Thibitisha. (alama 2)
      2. Eleza sifa mbili za nafsi nenewa katika wimbo huu. (alama 2)
      3. Fafanua mbinu tatu ambazo nafsineni ametumia kufanikisha uwasilishaji wake. (alama3)
      4. Eleza faida nne za kurithisha wimbo huu kwa vizazi vijavyo. (alama 4)
    2. Unanuia kufanya utafiti kuhusu utungo wa maigizo :-
      1. Eleza hatua tatu utakazofuata katika utafiti wa utungo huu. (alama 3)
      2. Unanuia kutumia hojaji kutafitia utungo huu. Eleza umuhimu na udhaifu wa kutumia njia hii. (alama 6)

                                                       MWONGOZO WA USAHIHISHAJI (FASIHI)

  1.  
    1. Mwanaume ambaye jamaa zake ni wahasiriwa wa ubakaji . (alama 1x2)
    2. Kuonyesha namna watu mbalimbali wanavyoathiriwa na matendo ya ubakaji.   (alama 1x2)
    3.  
      1. Maswali balagha - Baada ya yake sidilia kuikata?
      2. Nidaa- kilichomtuma atake kujifungua! (siyahi)
      3. Taswira - ya ubakaji
      4. Kinaya - wabakaji kujitia kundini na kushangaa kilichomtuma atake kujifungua!
        Tasfida - wakachana mbuga na wake ubikira
      5. Tabaini - si hapa walipomshurutisha mama. Si hapa sebuleni mwetu. Si hapa sokoni mwetu
      6. Takriri - si hapa
      7. Tashbihi - Kama kuku wa kuchinja
      8. Kuboronga sarufi- shuleni alitoka na wangu mke mpendwa
      9. Chuku-mkoba wa kilo nzito za vitabu        (Zozote 5x1)
    4.  
      1. Taswira mnuso - maua ya kufurahisha pua
      2. Taswira mguso - Walipiga miereka,kumburura shangazi, walimshika mkono
      3. Taswira oni/mwono- binamu zangu wakiona
      4. Taswira mwendo – wakachana mbuga na wake ubikira
      5. Taswira hisi - Baada ya yake sidira kuikata?
                                  - si hapa sebuleni mwetu?       (Zozote 4x1)
    5.  
      1. Toni ya uchungu - kwa jamaa ya nafsi neni kubakwa.
      2. Toni ya masikitiko - kubakwa kwa kichaa. (1x2)
    6.  
      1. Za yaliyojiri hapa
      2. Na pua kufurahisha
      3. Na kumfanya kujutia
      4. Si hapa sokoni        (1x1)
    7.  
      1. Beti saba
      2. Mishororo inatofautiana kwa kila ubeti
      3. Mizani inatofautiana kwa kila mshororo
      4. Lina kipande kimoja kwa mshororo        (Zozote 4x1)

                                                      SEHEMU B: RIWAYA- CHOZI LA HERI
  2.  
    1. Msemaji ni Tulia
      Umuhimu wa Tulia
      1. Kuendeleza maudhui ya uwajibikaji-anasaidia familia ya Kaizari kuepuka madhara zaidi ya ghasia za uchaguzi.
      2. Anachimuza maudhui ya utu- anajuza familia ya Kaizari hatari iliyopo.
      3. Kielelezo cha watu wanaojitolea kutunza mali ya watu walio kwenye changamoto
      4. Kielelezo cha jirani mwema.
      5. Anachimuza sifa za wahusika wengine kwa mfano majirani waliovamia familia ya Kaizari.
      6. Anachimuza maudhui ya ukabila na athari zake.   (Zozote 4x1)
    2. Muhimu wa mandhari haya
      1. Kuendeleza maudhui- vita baada ya uchaguzi
      2. Kuendeleza dhamira/ lengo- kutahadharisha athari za vita
      3. Kuchimuza wahusika mbalimbali—familia ya Kaizari
      4. Kuchimuza sifa zao.
      5. Kuendeleza ploti ya riwaya yenyewe.
      6. Kuonyesha migogoro katika jamii.
      7. Kuchimuza njia mbalimbali za kusuluhisha migogoro hii.
      8. Kuchimuza mahali na wakati wa tukio fulani. (Zozote 3x2)
    3. Migogoro na visababishi vyake.
      1. Mgogoro wa kisiasa - kutawazwa kwa Mwekevu kama mshindi.
      2. Mgogoro wa kijinsia - ubabedume wa wafuasi wa Mwekevu.
      3. Mgogoro wa kifamilia - idadi kubwa ya watoto wa Mwimo hivyo kulazimu ahamishe baadhi yao.
      4. Mgogoro wa kijamii - sera za mkoloni zilizomfanya Mwafrika kuwa skwota.
      5. Mgogoro wa kinafsi - Ridhaa familia yake inapoteketezwa.
      6. Mgogoro wa ndoa - Mzee Fungo anapomuoa Pete na kumchukua kama mali bali si mke.
      7. Mgogoro wa kikabila- Selume anatengana na mumewe.
      8. Mgogoro wa ardhi - Wakazi wa Tamuchungu wanapigania ardhi.
      9. Mgogoro wa kimaadili- Lunga anafutwa kazi kwa kukataa uuzaji wa mahindi yenye vijasumu.
      10. Mgogoro wa shinikizo la rika -Tuama kujipeleka kukeketwa
      11. Migogoro ya kikazi - Shamsi anafutwa kazi.
      12. Mgogoro wa kiuchumi - Makaa anaaga dunia akijaribu kusaidia wahasiriwa wa uchotaji mafuta.
      13. Mgogoro wa kimazingira - Msitu wa Mamba kuvamiwa na mazingira kuharibiwa (Zozote 10x1=10)
        Tan: Kadiria jibu la mwanafunzi
  3.  
    1. Majabali yaliyomkumba msemewa(Ridhaa)
      1. Familia yake kuteketezwa.
      2. Nyumba yake inateketezwa.
      3. Mwanawe Dede kufa akiwa na umri wa miaka sita tu.
      4. Shinikizo la damu baada ya kupitia madhira mengi.
      5. Alimpoteza ndugu yake Makaa.
      6. Jumba lake la kupangisha kuteketea kutokana na hitilafu ya umeme.
      7. Kutengwa shuleni na wanafunzi.
      8. Kubomolewa kwa majumba yake yaliyodaiwa kujengwa kwa sehemu ya upanuzi wa barabara
      9. Kufurushwa hadi Msitu wa Mamba.
      10. Familia yao kuzozana kutokana na ardhi ndogo.
      11. Kuhamishwa pamoja na mamake hadi Msitu wa Heri.
      12. Kumpoteza dadake Subira kwa vileo.        (alama 10x1=10)
    2. Ukiukaji wa haki za watoto
      1. Haki za watoto kupata elimu-Ami zao Lucia na Akello.
      2. Watoto wanahusishwa katika ajira- Dick.
      3. Wizi wa watoto- Dickson na Mwaliko.
      4. Watoto wanauwawa- wanauwawa na magari moshi madongoporomoka.
      5. Watoto kuhusishwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya –Dickson.
      6. Watoto wasichana kulazimishwa kuolewa- Fungo kumuoa Pete.
      7. Wananajisiwa- Sauna anabakwa na babake wa Kambo.
      8. Watoto wanapotoshwa na watu wazima-Bi. Kangara anapotosha Sauna.
      9. Watoto wanatupwa wanapozaliwa- Riziki aliokotwa na Naomi.
      10. Kuhini Watoto malezi- Naomi anahini wanawe malezi.
      11. Vitisho kwa Watoto- Mzee Buda kumtisha Dick.
      12. Kuwatumia kama vifaa vya mapenzi- Bi. Kangara anawaiba wasichana.
      13. Ubaguzi wa Watoto- wazazi wa Pete kumuoza kwa Fungo.
      14. Ukeketaji- Tuama.
      15. Dhuluma za kisaikolojia- Chandachema na wanawe Tenge kulazimika kushuhudia wana Tenge akigeuza kwake danguro.
        (Za kwanza 10x1=10)
        Tamthilia: Bembea
  4.  
    1. Mtindo
      1. Usemi halisi “mwanangu….
      2. Msemo- Kuchafukwa roho
      3. Jazanda- kuku, nyuki, Kamba, chuma, bembea
      4. Sentensi fupifupi-Hutaila.
      5. Mdokezo wa methali- yameshakuja, yapokee
      6. Taswira- mtoto akinyea kiganja.
      7. Takriri- Maumbile, maumbile.
      8. Usambamba- sawa na vidole hayafanani, sawa na watoto
      9. Kinaya- raha unapobwagwa na bembea.
      10. Tashihisi- chombo kumenyana na mawimbi.
      11. Mdokezo- safari…   (zozote 5x2=10)
    2. Umuhimu wa mandhari haya
      1. kuchimuza maudhui
      2. kuchimuza dhamira
      3. kujenga ploti
      4. kuchimuza wahusika.
      5. kuchimuza sifa zao (wahusika)
      6. kuchimuza mahali na wakati wa tukio
      7. kuchimuza njia ya kusuluhisha mgogoro ule      (zozote 5x2=10)
        Tan: maelezo ya mandhari lazima yakite mizizi katika dondoo pekee wala si kitabu kizima
  5.  
    1. Msemaji ni Dina kwa Kiwa nyumbani kwa Dina. Dina anataka kumuonyesha kuwa Sara alikuwa amepitia shida nyingi.
    2. Vipengele vya kimitindo
      1. Methali-baada ya dhiki ni faraja
      2. Jazanda- leo kikapu cha mama kimejaa ndago (2x2)
    3. Maudhui mawili
      1. Mabadiliko - kitambo Sara na familia yake walipitia dhiki na sasa hivi wana faraja.
      2. Uvumilivu - Sara ni mtu ambaye alivumilia dhiki nyingi na baadaye zikampa faraja.    (Zozote 2x1)
    4. sifa-Dina
      1. Mwenye huruma
      2. Ujirani mwema
      3. Mwenye roho safi
      4. Mwenye mapenzi ya dhati
      5. Mcha Mungu
      6. Mfariji
      7. Mwenye utani (Atoe maelezo 5x1=5)
    5. Mama (Sara)
      1. Kukosa watoto na kusemwa na wanajamii
      2. Kukosa mtoto wa kiume na kusemwa na majirani
      3. Mumewe (Yona) kuingilia ulevi na kumdhulumu.
      4. Anaachiwa jukumu la malezi
      5. Anapata maradhi ya moyo kutokana na mateso ya mumewe.        (Zozote 5x1)
  6. Fadhila za punda - Ufaafu wa anwani
    1. Luka anauza kanisa lililomlea baada ya kuneemeka.
    2. Luka anampuuza Lilia licha ya kuwa alimsaidia kukubalika na babake (mhubiri).
    3. Lilia anapigania penzi lake Luka kwa babake anayelipinga baadaye Luka anamtesa.
    4. Licha ya Lilia kumuunga mkono Luka katika siasa Luka anampuuza na kumtusi.
    5. Lilia anampenda Luka; Luka hamjali anapopoteza mimba yake.
    6. Lilia anamuunga mkono Luka kupata kiti cha ugavana anapokipata anamtenga akaishi shamba.
    7. Lilia anaamua kuacha kazi kwenye benki kumuunga mkono Luka malipo ni dharau.
    8. Lilia kuacha kazi kwenye benki ili kudhibiti pesa za kanisa malipo Luka analiuza.
    9. Lilia kuonyesha Luka mapenzi- malipo ni kipigo kwa mambo madogo madogo kama chakula kukosa chumvi.
    10. Lilia anaridhia matakwa yote ya Luka katika ndoa malipo Luka anachukua vimada kotekote.
    11. Babake Lilia kumtendea Luka mengi malipo Luka anamuoa mtoto wake na kuanza kumtesa.
    12. Wananchi wanamuunga Luka kupigania kiti cha gavana anapokipata anawasaliti.
    13. Kimada wake Luka kumzuzua lakini Luka anapopata ajali anamtoroka
    14. Lilia licha ya kumpenda Luka anapoenda kumuona ofisini anamfokea, kumfukuza na baadaye kumpiga.
    15. Licha ya Lilia kuwa na Imani na mkuu wa kituo cha polisi,mkuu huyu anampuuza na hata kumsaliti kwa mumewe anapomjuza kuhusu tukio la Lilia kwenda pale.       (zozote 10x2=20)
      Tan: Kadiria jibu la mwanafunzi-Jibu lionyeshe pande zote mbili;fadhila na mashuzi.
  7.  
    1. Mbinu za kimtindo
      1. Taswira – athari kujiandika
      2. Msemo- kajishika tama
      3. Tashbihi- mithili ya msafiri
      4. Balagha- angefeli je?
      5. Uzungumzi nafsi- Sabina anajizungumzia
      6. Mbinu rejeshi- aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu
      7. Jazanda- mizizi ya elimu
      8. Methali- mtaka cha mvunguni sharti ainame
      9. Tashihisi- maswali yakamwacha…
      10. Takriri- mtihani, mtihani (Zozote 6x1)
    2.  
      1. Ayasemayo mhusika
      2. Matendo ya mhusika
      3. Wayasemayo wahusika wengine
      4. Maelezo ya mwandishi kuhusu mhusika mwenyewe
      5. Uhusiano wake na wahusika wengine (Za kwanza 2x1)
    3. Aina za taswira kwenye kifungu
      1. Oni- usoni mwake
      2. Mwendo- msafiri aliyefika salama
      3. Hisi- kujishika tama
      4. Usikivu- alifikiria
      5. Onji- mizizi ya elimu ni michungu (Za kwanza2x1)
    4. Matatizo yanayomkumba mwanamke
      1. Mimba za mapema - Nyaboke
      2. Kukatiza masomo - Nyaboke
      3. Kufanyishwa kazi nying i- Sabina
      4. Kukataliwa na wanaowadunga mimba - Nyaboke kukataliwa na janadume lililompachika mimba
      5. Kujukumizwa ulezi wa mapema - Nyaboke
      6. Kukatisha wazazi tamaa
      7. Kukosa malezi ya baba mzazi - Sabina
      8. Kufanya kazi za sulubu ili mtoto apate mahitaji ya kimsingi
      9. Kifo cha mzazi - Sabina
      10. Kifo cha walezi - babu na nyanyake Sabina
      11. Kutelekezwa na wanakijiji – Wanakijiji kuapa kukaa mbali naye baada ya kushuku familia hiyo imelaaniwa.
      12. Kutengwa – Sabina anatengwa na watoto wa mjomba wake (Ombati)
      13. Dhiki za kisaikolojia - Sabina anapoitwa na mwalimu mkuu
      14. Kushukiwa - mwalimu mkuu anamshuku Sabina anapinga adhabu ya kuchelewa kufika shuleni.
      15. Kuchapwa/kuteswa - Sabina anapigwa na shangazi yake.(Yunuke)
      16. Matusi - Sabina anatusiwa kiokote na Yunuke
      17. Kunyimwa vifaa vya kimsingi vya matumizi- Yunuke anamzimia Sabina kibatari alipokuwa akisoma, rinda la Sabina ni kuukuu.(Zozote 10x1=10)
  8.  
    1.  
      1.  
        • Ni kero hili si huba
        • Mimi pendo la viraka (1x1)
      2.  
        • Mwenye tamaa - kupenda fedha/pesa
        • Mwenye ubinafsi - kujali pesa kuliko mapenzi
        • Msaliti - kupenda pesa badala ya kufuata penzi.
        • Mwenye mapuuza-anapuuza penzi
        • Mgomvi - Kamwe sitoshughulika.     (za mwanzo 2x1)
      3.  
        • Jazanda/sitiari - mimi pendo la viraka
        • Takriri - pendo viraka viraka
        • Inkisari - wanasifika, walostarabika
        • Kuboronga sarufi - Nasomba vyangu viraka ingawa mno nataka
        • Mishata - Pendo viraka viraka
        • Usambamba - Mimi pendo la viraka
                               - Mimi mno nataka (Za kwanza 3x1)
      4.  
        • Hutumiwa kuburudisha jamii
        • Hutumiwa kutakasa hisia
        • Hutumiwa kusifu/kukashifu tabia za mapenzi katika jamii
        • Hutumiwa kukuza ubunifu wa jamii ili kuibua hisia k.v Huzuni, huruma n.k
        • Ni nyenzo ya kupitisha maarifa au elimu ya jamii. (Za kwanza 4x1)
          Tan; Kadiria hoja za mwanafunzi
    2.  
      1.  
        • Kufanya maandalizi-ili kujua walengwa, muda wa utafiti, gharama na mbinu za utafiti.
        • Kukusanya data kwa kupitia kwa hojaji, mahojiano, kushiriki ama kutazama.
        • Kurekodi data kupitia kwa maandishi, kunasa sauti ya mhojiwa.
        • Kuchunguza data upya/ maelezo yaliyotolewa na kuyanakili jinsi yalivyo ili kuchanganua baadaye.
        • Kuchanganua data na kutafsiri kwa matokeo ya uchunguzi kuhusu maigizo.     ( 3x1)
      2. Umuhimu wa hojaji
        • Ni njia ya gharama ya chini zaidi.
        • Inafikia idadi kubwa kwa kipindi kifupi.
        • Inatumika kama mwongozo wa njia zingine.
        • Humpa mhojiwa muda wa kuwazia maswali.
        • Hazina athari kwa mtafitiwa / wahojiwa.
        • Inaweza kubadilishwa kulingana na elimu ya wahojiwa.     (Zozote 3 x1)

          Udhaifu wa hojaji
        • Maswali tata hupata fasiri mbali mbali.
        • Watu kukataa kujaza hojaji kikamilifu.
        • Watu kukataa kujaza hojaji ikiwa ndefu.
        • Ni vigumu kuchanganua data.
        • Wahojiwa kudanganya.
        • Wahojiwa kuchelewa kurejesha hojaji.
        • Wahojiwa wasiojua kusoma hawawezi kuzijaza.
        • Baadhi ya sifa kama vile toni hupotea.             (Zozote 3x1)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Lainaku 1 Joint PreMock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?