Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

  1. UFAHAMU (alama 10)
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

    Changamoto kubwa inayowakabili watu wengi katika mataifa yanayoendelea ni suala la chakula. Suala hili linaweza kuangaliwa katika sawia mbili tofauti. Kuna tatizo linalofungamana na uhaba wa chakula chenyewe. Uhaba huu unaweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa zaraa kama nyenzo kuu ya uzalishaji wa chakula.

    Zaraa katika mataifa mengi hususan yanayoendelea, hutegemea mvua. Kupatikana kwa mvua huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ulimwnguni. Matendo na amali za watu kama ukataji wa miti na uchafuzi wa mazingira huwa na athari hasi kwenye tabianchi hiyo. Mabadiliko ya tabianchi huweza kuvyaza ukame kutokana na ngambi ya mvua.

    Kibinimethali kutokea wakati mafuriko yanapotokea na labda kuyasomba mazao mashambani na kusababisha baa la njaa. Hali hizi mbili husababisha matatizo makubwa ya chakula na kuathiri pakubwa suala zima la usalama wa chakula. Ili kuzuia uwezokano wa kuwepo kwa shida hii, pana haja ya kuwepo kwa mikakati na sera za kuhakikisha kuna usalama wa chakula. Kwa mfano, pana haja ya kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua. Kwa upande mwingine, sharti zichukuliwe hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari za gharika.

    Changamoto nyingine inahusiana na usalama wa chakula chenyewe. Chakula kilichosibikwa na vijasumu au kwa njia nyingine ile huweza kumdhuru anayehusika. Msibiko wa chakula unatokana na vyanzo tofauti. Mathalan uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo, kutozingatia mbeko za usafi, uandaaji wa chakula na kukiweka katika hali ya uvuguvugu kabla ya kukipakua – hali inayochochea ukuaji wa viini na ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.

    Ili kuepuka uwezekano wa kuathirika, pana haja ya kuzingatia usafi wa chakula na uandalizi unaofaa. Fauka ya hayo, vyombo vya uandalizi viwe safi, kanuni za usafi zifuatwe, upikaji na uandaaji uwe kamilifu. Hali hii isipozingatiwa, siha za raia wenyewe zitaathirika pakubwa.

    Maswali.
    1. Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea. (alama 2)
    2. Taja hatua MOJA inayoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo la chakula. (alama 1)
    3. Eleza jinsi TATU tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama? (alama 3)
    4. Kwa nini ni rahisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu? (alama 1)
    5. Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa? (alama 3)
  2. SARUFI: ALAMA 20
    1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au sighuna. (ala 2)
      /s/,/z/
    2. Eleza maana ya shadda. (ala 2)
    3. Tafautisha kati ya irabu na Konsonanti (al2)
    4. Orodhesha sauti mbili za nazali. (al1)
    5. Tafautisha kati ya (al 2)
      \e\ na \i\
    6. Tia shadda kwenye maneno yafuatayo ili kuleta maana iliyo katika mabano .(al4)
      Ala (kifaa)
      Ala (mshangao)
      Barabara (njia kuu)
      Barabara (sawasawa)
    7. Toa mifano miwili ya aina za kamusi. (ala 2)
    8. Taja vipashio vya lugha. (ala 2)
    9. Andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo; (ala 3)
      KKI
      II 
      KI

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. UFAHAMU
    1. Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea.-
      • Uhaba wa chakula, ukosefu wa chakula au upungufu wa chakula unaoweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa kilimo kama njia ya uzalishaji wa chakula.
      • Usalama wa chakula chenyewe kwani chakula kilichosibikwa na vijasumu huweza kumdhuru anayehusika.

    2. Taja hatua mbili zinazoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo la chakula.
      • kuwepo kwa mikakati ya kuhakikisha kuna usalama wa chakula kwa kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua na kuchukuliwa hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari za gharika.
      • Kuwepo kwa sare za kuhakikisha kuna usalama wa chakula.

    3. Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama?
      • Uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo
      • Kutozingatia mbeko za usafi.
      • Kukiandaa chakula na kukiacha katika hali vuguvugu kabla ya kukipakua.
      • Ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.

    4. Kwa nini inahalisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu?
      • Chakula kipakuliwe baada ya kuandaa tu ili kuzuia hali inayochochea ukuaji wa viini na kwa njia hiyo kuhakikisha kuwa chakula hakitakuwa na viini.

    5. Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa?
      • Haja ya kuzingatia usafi wa chakula.
      • Uandalizi unofaa.

  2. SARUFI: ALAMA 20
    1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au sighuna. (al2)
      • /s/ - si ghuna
      • /z/ - ghuna

    2. Eleza maana ya shadda. (ala 2)
      • Shadda ni mkazo unaowekwa katika neno ili kuleta maana iliyokusudiwa.

    3. Tafautisha kati ya irabu na Konsonanti(al2)
      • Irabu hutamkwa kwa ulaini ilhali konsonanti hutamkwa kwa hewa kuzuiliwa.

    4. Orodhesha sauti mbili za nazali.(al1)
      • M,n,ng,ny

    5. Tafautisha kati ya (al 2)
      • \e\ na \i\

    6. Tia shadda kwenye maneno yafuatayo ili kuleta maana iliyo katika mabano.(al 4)
      • ‘Ala
      • A’la!
      • Bara’bara – (njia kuu)
      • Ba’rabara – (sawasawa)

    7. Toa mifano miwili ya aina za kamusi. (ala 2)
      • Kamusi ya methali
      • Kamusi ya semi

    8. Taja vipashio vya lugha. (ala 2)
      • Sauti /m/
              ↓
        Silabi ma
              ↓
        Neno mama
               ↓
        Sentensi mama anapika

    9. Andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo;
      • II – oa, au
      • KKI –mti ,mtu
      • KI - la, pa, wa, na, 

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest