MASWALI
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. (alama 10)
Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule
Tungo zenye kusifika, zenye na nasaha tele
Naomba la uhakika, jawabu enyi wavyele
Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto !
Tangu dahari miaka, mikono ina upole
‘Meungana pasi shaka, ni miwili vile vile
Mmoja ukisumbuka, mwingine hujaa ndwele
Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto !
Wa kuume ukicheka, wa kushoto nao vile
Ulipofanya dhihaka, kwamba unao upele
Wa kushoto hutanzuka, kuukuna kwa vidole
Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto !
Kimako leo amaka, kushoto haoni mbele
Kumbe kuume kushika, kudhibiti mtale
Misuli ‘metutumuka, hajali hana simile
Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto !
Tamati ninaondoka, nawachia wakale
Uamuzi wa haraka, ufanyike msilale
Umenijaa wahaka, mwanzo wa ngoma ni lele
Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto !
Maswali- Shairi hili ni la aina gani? (Alama 1)
- Eleza vina vya shairi hili. (Alama 2)
-
- Mizani ni nini ? (Alama 1)
- Shairi hili lina mizani ngapi katika ubeti wa nne mshororo wa tatu ? (Alama 1)
- Taja na ueleze maana ya kibwagizo cha shairi hili. (Alama 2)
- Taja jambo ambalo hufanywa na mikono yote miwili kwa pamoja. (Alama 1)
- Toa maana ya maneno haya kama yaliyotumiwa katika shairi. (Alama 2)
- Dahari
- Kuume
- MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 20)
- Taja konsonanti ,mbili za ufizi. (Alama 2)
- Taja irabu mbili za nyuma. (Alama 2)
- Toa mifano mitatu ya ala tuli za kutamkia. (Alama 3)
- Ni nini maana ya kiyeyusho/nusu – irabu ? (Alama 1)
- Andika maneno mawili kwa kila mojawapo ya sauti hizi mwambatano. (Alama 2)
- Nj
- Sw
-
- Eleza maana ya silabi. (Alama 1)
- Onyesha silabi za neno parapanda. (Alama 2)
- Taja aina moja ya kamusi. (Alama 1)
- Mtu anayehudumu maktabani huitwaje ? (Alama 1)
- Tambua aina za maneno katika sentensi hii. (Alama 2)
Mtoto mtukutu ameadhibiwa vibaya. - Nomino hizi ziko katika ngeli gani ? (Alama 1)
- Mkoba
- Ngao
- Kamilisha methali hizi. (Alama 1)
- Kikulacho ……
- Jambo usilolijua …
- Onyesha matumizi mawili ya nukta pacha/koloni. (Alama 1)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- Tarbia
- Kina cha kati/ndani – ka, kina cha mwisho/nje – le
-
- Sauti yenye mdundo katika shairi.
- Mizani kumi na sita
-
- Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto !
- Tangu lini mkono wa kulia ukaukata wa kushoto ?
- Kucheka, kusumbuka
-
- Zamani, kale
- Kulia
- MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 20)
- /d/,/t/,/n/,/l/,/r/,z/,/s/
- /o/,/u/
- kaakaa laini, kaakaa ngumu, ufizi, meno, koo, pua
- Konsonanti inayotamkwa bila ya hewa kufungiwa/ kuzuiliwa/ kubanwa
-
- Njema, njumu, njama, njuga, njenje, njiiti, njozi (mtahini ahakiki jibu)
- Swali, swara, sweta, Kiswahili, swila (mtahini ahakiki jibu)
-
- Tamko linalotolewa kwa mpigo katika neno/ mpigo mmoja wa sauti katika neno.
- Pa-ra-pa-nda
-
- Kamusi ya kiswahili sanifu
- kamusi ya semi na nahau
- kamusi ya methali
- kamusi ya vitendawili
- kamusi ya sayansi (mtahini ahakiki jibu)
- Mkutubi
- Mtoto mtukutu ameadhibiwa vibaya.
N V T E -
- U – I
- I – ZI
-
- Ki nguoni mwako
- Ni kama usiku wa kiza
-
- Hutumika kabla ya kutoa orodha
- Kuandika tarehe
- Kuandika saa
- Kuonyesha masomo ya Biblia
- Kutoa mada ya barua rasmi
- Katika mazungumzo ya moja kwa moja/ mchezo wa kuigiza ( Baada ya jina la msemaji)
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 2 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students