Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 1 Exams 2023

Share via Whatsapp

Maakizo

 • Jibu maswali yote kwenye nafasi zilizoachwa wazi.

SEHEMU YA  A

Mawasiliano ni neno ambalo asili yake ni wasili.   Wasili lina maana ya kufika kwa mtu, kitu, au jambo fulani baada ya mwendo au safari.  Kwa hivyo kuwasiliana kuna maana watu, kitu au mambo kufikiana kutoka mahali.
 
Katika siku za jadi mawasiliano yalikuwepo lakini ya shida.  Hata hivyo, watu waliwasiliana kwa kutumia moshi, ngomezi au kupiga mbiu.  Mbinu hizi za jadi zilitumiwa baina ya vijiji ili kujulisha wanakijiji jambo la dharura au kuwajulisha jambo lingine lolote.  Mbiu ilitumika kwa jambo la dharura.  Njia za kusafirisha mizigo zilikuwa haba.  Baadhi ya watu walitumia wanyama, kama fahali au farasi kukokotea mizigo yuao.
 
Siku hizi mawasiliano yamepanuka sana.  Mawasiliano ya kisasa yanahusisha simu, mtandao, televisheni na wavuti.  Mawasiliano ya kisasa yamefanya ulimwengu wa kisasa kuwa kijiji kimoja kikubwa.
 
Kwa kuzingatia maudhui haya, vyombo au njia kama redio, simu, waraka, ndege, meli, motokaa na wavuti vimepewa jina la vyombo vya mawasiliano.  Hivyo basi yafaa tutathmini ni vipi vyombo au njia hizi hufanya kazi ya kuwasiliana na huwasilisha nini.  Vyombo hivi vinaweza kuelezwa chini ya vichwa vitatu; usafiri, mazungumzo na picha.  Vyombo mathalan baiskeli, ndege, meli na magari hufanya kazi ya kuwasafirisha watu kutoka janibu moja hadi nyingine.  Watu wanaposafiri huwa wanasafirisha mali yao.  Bidhaa kama kahawa, vyuma na mizigo mingine husafirishwa kwa meli, ndege na magari kupitia majini, hewani au barabarani.
 
Bandari, viwanja vya ndege na barabara zimeimarishwa ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo.  Anayesafirisha bidhaa fulani na wakati huo anatakikana kukusanya nyingine, inamlazimisha asiambatane na bidhaa hizo lakini ahakikishe zimewasili alikozikusudia.  Hivyo basi njia nyingine ya mawasiliano ilivumbuliwa.
 
Njia hii ambayo ni mazungumzo hutumia vifaa kama barua, simu, barua pepe na kipepesi.  Mtumiaji ataandika ujumbe na kuutuma kupitia shirika la posta au mashirika mengine ama mtandao.  Yamkini ilihitajika kuweza kujibizana na kuulizana kati ya watu hao wawili ndipo simu ilipovumbuliwa na kumwezesha mtu kuzungumza na mwingine akiwa mbali sana.  Watu huzungumza na kufahamiana.  Ilipohitaji mtu kukiona kitu anachozungumzia ndipo ilibidi kuunda vifaa vya kuonyesha picha kama vile televisheni.
 
Ilikuwa fahari kubwa sana kwa Wakenya kuwasiliana na nchi ya Ghana wakati wa michuano ya mpira ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika.  Wakenya waliweza kuiona michezo hiyo moja kwa moja ingawa kijiografia Kenya na nchi hiyo zina majira tofauti.
 
Mawasiliano tuliyotaja ni vyombo vya ufundi vilivyoundwa lakini kunayo maswasiliano ya ana kwa ana.  Mwalimu na mwanafunzi darasani huwasiliana kutumia midomo, mikono, macho, kichwa na ishara nyinginezo.  Wanapofanya hivyo huwa wanaelewana.
 
Ndege kama kuku akihisi adui hufanya ishara au mlio fulani wa kutahadharisha viranga wakek katika michezo.  Mwamuzi huwasiliana na wachezaji labda kwa kutumia firimbi au kipenga, kengelel au ishara za mkono.  Kengele pia hutumiwa shuleni ili kuonyesha kukamilika kwa kipindi au kuhitajika mahali pengine.
 
Kwa muhtasari, mawasiliano hutumia chochote ilimradi ujumbe utokao kwa mtu, kitu au mahali fulani ufike panapotarajiwa.
 
MASWALI:   
 1. Taja anwani faafu ya kifungo hiki. (alama 1)
 2. Vyombo vya mawasiliano vimeleta manufaa gani katika maisha ya watu? (2 mks)
 3. Mawasiliano yameelezwa katika vipenge vitatu.  Vitaje. (3 mks)
 4. Andika visawe vya: (2 mks)
  1. Televisheni –
  2. Waraka – 
 5. Nini maana ya: (2 mks)
  1. Ana kwa Ana –
  2. Ulimwengu umekuwa kijiji kimoja kikubwa –

SEHEMU YA B: SARUFI

 1. Taja aina mbili kuu za sauti za Kiswahili. (2 mks)
 2.   Taja vigezo vitatu vinavyotumika kuainisha konsonati. (alama 3)
 3.   Taja aina mbili za konsonanti zenye aina ya vipasuo. (alama 2)
 4.   Andika majukumu tatu ya lugha. (alama 3)
 5. Andika maneno yenya miundo ya silabi ifuatayo. (alama 3)
  1. KI (Konsonanti irabu) –
  2. KKI (Konsonanti, konsonanti, irabu) –
  3. II (irabu) –
 6. Bainisha maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi? (alama 3)
  1. Ngoma –
  2. Ukuta –
  3. Macho-
  4. Ugonjwa –
  5. Mmea –
  6. Maiti –
 7. Andika vinyume vya sentensi zifuatazo:- (alama 2)
  1. Mama anaanika nguo
  2. Baba anaenda sokoni.
 8. Kanusha sentensi zifuatazo. (2 mks)
  1. Mkulima analima shamba.
  2. Mwanafunzi anasoma kitabu.
 9. Onyesha Nomino (N), kitenzi ®, kielezi (E) Kiunganishi (U), na kivumishi (v) katika sentensi hizi (alama 3)
  1. Mtoto anacheza vizuri.
  2. Utacheza au utasoma?
  3. Wanafunzi wawili wanalala.
 10. Toa neno kwa kila moja ya sauti ambatano zifuatazo.
  1. Nyw –
  2. Nd – 
  3. Ngw –
 11. Onyesha silabi inayowekewa shadda kwenye maneno yafuatayo. (alama 4)
  1. Karatasi –
  2. Shairi –
  3. Barabara(njia kuu)
  4. Mto –

SEHEMU YA C: ISIMU JAMII (ALAMA 10)    

 1. Eleza maana ya Isimu jamii. (alama 2)
 2. Taja na ufafanue mambo/dhana nne zinazozingatiwa katika matumizi ya lugha.     (alama 8)

MARKING SCHEME

Mawasiliano ni neno ambalo asili yake ni wasili.   Wasili lina maana ya kufika kwa mtu, kitu, au jambo fulani baada ya mwendo au safari.  Kwa hivyo kuwasiliana kuna maana watu, kitu au mambo kufikiana kutoka mahali.
 
Katika siku za jadi mawasiliano yalikuwepo lakini ya shida.  Hata hivyo, watu waliwasiliana kwa kutumia moshi, ngomezi au kupiga mbiu.  Mbinu hizi za jadi zilitumiwa baina ya vijiji ili kujulisha wanakijiji jambo la dharura au kuwajulisha jambo linguine lolote.  Mbiu ilitumika kwa jambo la dharura.  Njia za kusafirisha mizigo zilikuwa haba.  Baadhi ya watu walitumia wanyama, kama fahali au farasi kukokotea mizigo yuao.
 
Siku hizi mawasiliano yamepanuka sana.  Mawasiliano ya kisasa yanahusisha simu, mtandao, televisheni na wavuti.  Mawasiliano ya kisasa yamefanya ulimwengu wa kisasa kuwa kijiji kimoja kikubwa.
 
Kwa kuzingatia maudhui haya, vyombo au njia kama redio, simu, waraka, ndege, meli, motokaa na wavuti vimepewa jina la vyombo vya mawasiliano.  Hivyo basi yafaa tutathmini ni vipi vyombo au njia hizi hufanya kazi ya kuwasiliana na huwasilisha nini.  Vyombo hivi vinaweza kuelezwa chini ya vichwa vitatu; usafiri, mazungumzo na picha.  Vyombo mathalan baiskeli, ndege, meli na magari hufanya kazi ya kuwasafirisha watu kutoka janibu moja hadi nyingine.  Watu wanaposafiri huwa wanasafirisha mali yao.  Bidhaa kama kahawa, vyuma na mizigo mingine husafirishwa kwa meli, ndege na magari kupitia majini, hewani au barabarani.
 
Bandari, viwanja vya ndege na barabara zimeimarishwa ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo.  Anayesafirisha biodhaa fulani na wakati huo anatakikana kukusanya nyingine, inamlazimisha asiambatane na bidhaa hizo lakini ahakikishe zimewasili alikozikusudia.  Hivyo basi njia nyingine ya mawasiliano ilivumbuliwa.
 
Njia hii ambayo ni mazungumzo hutumia vifaa kama barua, simu, barua pepe na kipepesi.  Mtumiaji ataandika ujumbe na kuutuma kupitia shirika la posta au mashirika mengine ama mtandao.  Yamkini ilihitajika kuweza kujibizana na kuulizana kati ya watu hao wawili ndipo simu ilipovumbuliwa na kumwezesha mtu kuzungumza na mwingine akiwa mbali sana.  Watu huzungumza na kufahamiana.  Ilipohitaji mtu kukiona kitu anachozungumzia ndipo ilibidi kuunda vifaa vya kuonyesha picha kama vile televisheni.
 
Ilikuwa fahari kubwa sana kwa Wakenya kuwasiliana na nchi ya Ghana wakati wa michuano ya mpira ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika.  Wakenya waliweza kuiona michezo hiyo moja kwa moja ingawa kijiografia Kenya na nchi hiyo zina majire tofauti.
 
Mawasiliano tuliyotaja ni vyombo vya ufundi vilivyoundwa lakini kunayo maswasiliano ya ana kwa ana.  Mwalimu na mwanafunzi darasani huwasiliana kutumia midomo, mikono, macho, kichwa na ishara nyinginezo.  Wanapofanya hivyo huwa wanaelewana.
 
Ndege kama kuku akihisi adui hufanya ishara au mlio fulani wa kutahadharisha viranga wakek katika michezo.  Mwamuzi huwasiliana na wachezaji labda kwa kutumia firimbi au kipenga, kengelel au ishara za mkono.  Kengele pia hutumiwa shuleni ili kuonyesha kukamilika kwa kipindi au kuhitajika mahali pengine.
 
Kwa muhtasari, mawasiliano hutumia chochote ilimradi ujumbe utokao kwa mtu, kitu au mahali fulani ufike panapotarajiwa.
MASWALI:
 1. Taja anwani faafu ya kifungo hiki. (alama 1)
  • Mawasiliano
 2. Vyombo vya mawasiliano vimeleta manufaa gani katika maisha ya watu? (2 mks)
  • Kuwasafirisha watu na bidhaa kwa upesi
  • Kuwasilisha ujumbe/taarifa/habari
  • Kuona matukio yakiwepo mbali
  • Kuimarisha uchumi na maendeleo
 3. Mawasiliano yameelezwa katika vipenge vitatu.  Vitaje. (3 mks)
  • Usafiri
  • Mazungumzo
  • Picha
 4. Andika visawe vya: (2 mks)
  1. Televisheni – Runinga
  2. Waraka – Barua
 5. Nini maana ya: (2 mks)
  1. Ana kwa Ana – Hali ya kuwa mnaonana
  2. Ulimwengu umekuwa kijiji kimoja kikubwa – Mawasiliano yamerahisishwa sana ulimwenguni

SEHEMU YA B: SARUFI

 1. Taja aina mbili kuu za sauti za Kiswahili. (2 mks)
  • Irabu
  • Konsonanti
 2. Taja vigezo vitatu vinavyotumika kuainisha konsonati. (alama 3)
  • Mahali zinapotamkiwa
  • Jinsi au namna zinavyotamkwa
  • Mghuna au kutoghuna kwa wauti au mtetemko wa nyuzi za sauti
 3. Taja aina mbili za konsonanti zenye aina ya vipasuo. (alama 2)
  • │p│
  • │k│ 
 4. Andika majukumu tatu ya lugha. (alama 3)
  • Lugha hutumika kwa mawasiliano
  • Ni chombo kinachotusaidia kujieleza na kutoa mawazo yetu
  • Lugha hujenga uhusianao baina ya watu
  • Lugha huimarisha uhusiano kati ya jamii na jamii taifa
  • Lugha ni kitambulisho cha taifa
 5. Andika maneno yenya miundo ya silabi ifuatayo. (alama 3)
  1. KI (Konsonanti irabu) – Kitabu, baba, mama
  2. KKI (Konsonanti, konsonanti, irabu) – Penda unga, panga
  3. II (irabu) – Ua, Oa.
 6. Bainisha maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi? (alama 3)
  1. Ngoma – I -Zi
  2. Ukuta – U-Zi
  3. Macho − li - ya
  4. Ugonjwa – u - ya
  5. Mmea – U - I
  6. Maiti – A – wa
 7. Andika vinyume vya sentensi zifuatazo:- (alama 2)
  1. Mama anaanika nguo
   • Mama anaanua nguo
  2. Baba anaenda sokoni.
   • Baba anatoka sokoni
 8. Kanusha sentensi zifuatazo. (2 mks)
  1. Mkulima analima shamba.
   • Mkulima halimi shamba
  2. Mwanafunzi anasoma kitabu.
   • Mwanafunzi hasomi kitabu
 9. Onyesha Nomino (N), kitenzi ®, kielezi (E) Kiunganishi (U), na kivumishi (v) katika sentensi hizi (alama 3)
  1. Mtoto anacheza vizuri.
      N           T          E
  2. Utacheza au utasoma?
           T       U        T
  3. Wanafunzi wawili wanalala.
           N            V          T
 10. Toa neno kwa kila moja ya sauti ambatano zifuatazo.
  1. Nyw – Kunywa
  2. Nd –  Ndoo, kondoo
  3. Ngw –  jangwa
 11. Onyesha silabi inayowekewa shadda kwenye maneno yafuatayo. (alama 4)
  1. Kara’tasi 
  2. Sha’iri 
  3. Baraba’ra(njia kuu)
  4. ‘Mto 

SEHEMU YA C: ISIMU JAMII (ALAMA 10)

 1. Eleza maana ya Isimu jamii. (alama 2)
  • Ni matumizi ya lugha katika jamii.
 2. Taja na ufafanue mambo/dhana nne zinazozingatiwa katika matumizi ya lugha.   (alama 8)   (Mwanafunzi atoe maelezo)
  • Wahusika
  • Tabaka
  • Jinsia
  • Elimu
  • Umri
  • Wakati
  • Mahali
  • Uhusiano wao
  • Tukio lenyewe
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 1 Exams 2023.

Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest