Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp

MASWALI

UFAHAMU (ALAMA 10)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

KAWI

Kuenezwa kwa huduma za nguvu za umeme ni kigezo muhimu cha kupimia kiwango cha maendeleo katika maeneo mengi nchini. Hali hii imetokana na wingi wa shughuli zinazoambatisha aina hii ya kawi. Shughuli hizi ni pamoja na zile za kibinafsi nyumbani, viwandani na kwenye asasi mbalimbali. Aidha, nguvu za umeme zinazidi kuhitajika kila uchao hasa katika sekta ya Tehama. Kukosekana kwa huduma hii muhimu hata kwa muda mfupi huwa na athari kubwa. 

Njia kuu ya uzalishaji wa nguvu za umeme ni ile ya kutumia mitambo inayoendeshwa kwa maji. Katika miaka ya hivi majuzi uzalishaji wa ainia hii umekumbwa na uhaba wa maji kwenye mabwawa. Baadhi ya vituo vya kuzalishia umeme vimelazimika kufungwa. Ukosefu wa mvua ya kutosha umetokana na mabadiliko ya hali ya anga. Kukosekana kwa uhifadhi wa misitu na vyanzo vya chemichemi na mito ndiko kulikochangia pakubwa katika kupungua kwa maji kwenye mito na hatimaye kwenye mabwawa.

Kutokana na hali ilivyo sasa, ni dhahiri kuwa lazima vyanzo vya kawi mbadala vitafutwe. Kawi mbadala itahitajika ili kudumisha na kuimarisha kiwango cha maendeleo kitakikanacho.

Kawi mbadala inayopendekezwa itafitiwe ni ile itokanayo na jua. Sehemu nyingi za nchi huwa na mihula mirefu ya jua. Jua ni chanzo muhimu cha kawi. Vioo na betri maalumu huweza kuvuna kawi hii isiyoisha kutoka kwa jua. Inaweza kutoa huduma za nguvu za umeme kwa matumizi mbalimbali. Sehemu ambazo zimependekezewa aina hii ya kawi ni zile zilizo mbali na mtandao wa nguvu za umeme za kawaida. Manufaa makubwa ya kawi ya jua ni kuwa mtumizi hahitaji kulipa bili yoyote. Hata hivyo, uwekezaji wa awali unaweza kuwa na gharama kubwa hasa kwa mtu binafsi.

Kawi mbadala nyingine ni ile inayotokana na mvuke. Uzalishaji wa kawi hii umeegemezwa kwenye matumizi ya mitambo inayoendeshwa kwa mvuke. Nchini kuna vyanzo vingi vya mvuke hasa katika eneo la bonde la ufa. Nguvu za umeme zizalishwazo huunganishwa kwenye mtandao wa kitaifa. Kampuni inayotegemewa kuzalisha na kuimarisha kawi nchini humu ni Kengen.

Chanzo kingine cha kawi mbadala ni upepo. Matumizi ya upepo yamekuweko kwa karne nyingi katika mataifa ya Bara Uropa. Ajabu ni kwamba humu nchini hayajastawishwa ipasavyo. Nchi hii ina maeneo mengi ambayo yameinuka na tambarare ambako upepo huvuma kwa nguvu nyakati nyingi za mwaka. Tangu zamani upepo umekuwa ukitumiwa kuzungushia mapanka makubwa yaliyoendesha mitambo mbalimbali. Baadhi ya mitambo hiyo ni vinu vya kusagia nafaka. Mitambo ya kupasua mbao au kutoa maji visimani. Utafiti uliofanywa umeonyesha kuwa mapanka yaya haya yaendeshwayo kwa upepo yanaweza kuendesha mitambo ya kuzalisha nguvu za umeme.

Njia zingine zitakazovumbuliwa zikiimarishwa nchi yetu itaacha kuwa tegemezi kwa mvua isiyotabirika. Hali hii itachangia katika uimarishaji na udumishaji wa kasi ya maendeleo. 

Maswali

  1. Taja sehemu tatu ambako kawi ya umeme hutumiwa. (ala 3)
  2. Eleza changamoto inayoikumba nchi inayotegemea maji kama chanzo ha kawi. (ala 1)
  3. Mbali na maji, taja vyanzo vingine vya kawi. (ala 3)
  4. Kwa mujibu wa taarifa, andika matumizi matatu ya kawi ya upepo. (ala 3) 

SARUFI (ALAMA 30)

  1. Tofautisha kati ya irabu na konsonanti. (ala 2)
  2. Taja sifa bainifu za irabu zifuatazo.      (ala 2)
    • /o/
    • /e/
  3. Tofautisha kati ya sauti ghuna na sauti sighuna. (ala 2)
  4. Taja vipashio vya lugha. (ala 2)
  5. Andika kwa wingi (ala 1)
    Mtoto mvulana angali anacheza kandanda.
  6. Andika neno lenye mpangilio ufuatao wa silabi. ( ala 2)
    • KKKI
    • KKI
  7. Bainisha aina za maneno katika sentensi ifuatayo. (ala 2)
    Mwanafunzi mrefu anavuka barabara.
  8. Tofautisha kati ya ala tuli na ala songezi na utolee mifano. (ala 2)
  9. Ainisha viambishi viliyotumika maneno haya ( ala 3
    Alikimbia
  10. Taja aina tatu za maktaba. (ala 3)
  11.                        
    1. Taja matumizi matatu koma/ kipumuo. (ala 3)
    2. Toa mifano ya kila matumizi ya koma/kipumuo uliyoitaja  ( ala 3)
  12. Taja matumizi/dhima mbili za lugha .( ala 2)
  13. Weka shadda katika neno hili (ala 1)
    Runinga 

FASIHI SIMULIZI   (ALAMA 10)

  1.                      
    1. Taja aina mbili kuu za fasihi ( ala 2)
    2. Taja tanzu nne za fasihi simulizi ( ala 4)
    3. Taja umuhimu wa fasihi simulizi (ala 4)

MAAKIZO.

UFAHAMU (ALAMA 10)
Maswali

  1. Taja sehemu tatu ambako kawi ya umeme hutumiwa. (ala 3)
    1. Nyumbani
    2. Viwandani
    3. Asasi mbalimbali.
  2. Eleza changamoto inayoikumba nchi inayotegemea maji kama chanzo cha kawi (ala )
    • Mvua isiyotabirika.
  3. Mbali na maji, taja vyanzo vingine vya kawi. (ala 3)
    • Jua
    • Mvuke
    • Upepo
  4. Kwa mujibu wa taarifa, andika matumizi matatu ya kawi ya upepo. (ala 3)
    • Kuendeshea mitambo ya;
    • Kusaga nafaka
    • Kupasulia mbao
    • Kutolea maji visimani.

SARUFI (ALAMA 15)

  1. Tofautisha kati ya irabu na konsonanti. (ala 2)
    • Irabu ni sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini bila ya hewa kuzuiliwa.
  2. Taja sifa bainifu za irabu zifuatazo. (ala 2)
    1. /o/ - Ni irabu ya nyuma chini. ( ½ al)
      • Inapotamkwa midomo huviringwa ( ½ al)
    2. /e/ - Ni irabu ya mbele chini ( ½ )
      • Inapotamkwa midomo hutandazika ( ½ )
  3. Tofautisha kati ya sauti ghuna na sauti sighuna. (ala 2)
    • Sauti ghuna ni sauti ambazo zinapotamkwa husababisha mrindimo wa nyuzi za sauti.
    • Sauti sighuna zinapotamkwa hazisababishi mrindimo wa nyuzi za sauti.
  4. Taja vipashio vya lugha. (ala 4)
    • Sauti → Silabi → Neno → Sentensi 
  5. Andika kwa wingi (ala 1)
    • Mtoto mvulana angali anacheza kandanda.
    • Watoto wavulana wangali wanacheza kandanda.
  6. Andika neno lenye mpangilio ufuatao wa silabi.
    1. KKKI  mf. Mchele, mbwa.
    2. KKI mf. Mti, mtoto. (ala 2) 
  7. Bainisha aina za maneno katika sentensi ifuatayo. (ala 2)
    • Mwanafunzi mrefu anavuka barabara.
          N           V          T            N
  8. Tofautisha kati ya ala tuli na ala songezi na utolee mifano. (ala 2)
    • Ala tuli hazisogeisogei wakati wa kutamka sauti mf. Kaakaa gumu, kaakaa laini
    • Ala sogezi husogeasogea wakati wa kutamka sauti mf. Ulimi, mdomo,
  9. Ainisha viambishi vilyotumika katika neno hili ( ala 3)
    Nilikimbia
    • Ni (nafsi), li (wakati) kimbi( mzizi) a ( kiishio )
  10. Taja aina tatu za maktaba. (ala 3)
    • Shule, darasa, nyumbani ,kitaifa, maktaba maalum
  11.                
    1. Taja matumizi matatu koma/ kipumuo. (ala 3)
      • Kuorodhesha vitu zaidi ya mbili
      • Kutoa maelezo zaidi
      • Katika tarakimu gugawa elfu
      • Kuandika tarehe
      • Kuonyesha pumziko fupi katika sentensi
      • Kuandika anwani
    2. Toa mifano ya kila matumizi ya koma/kipumuo uliyoitaja  ( ala 3)
      Mwalimu atathmini mifano
  12. Taja matumizi/dhima mbili za lugha .( ala 2)
    • Hutumika katika mawasiliano
    • Hutumika kujieleza kimawazo
    • Hujenga uhusiano baina ya watu
    • Lugha huimarisha uhusiano Kati ya jamii na jamii na taifa na taifa
    • Lugha ni kitambulishi cha taifa
  13. Eka shadda katika neno hili (ala 1)
    • Ru'ninga - mwanafunzi aeke shadda kwenye silabi ni

Fasihi simulizi

  1.                          
    1. Taja aina mbili kuu za fasihi ( ala 2)
      • Fasihi andishi
      • Fasihi simulizi
    2. Taja tanzu nne za fasihi simulizi ( ala 4)
      • Hadithi, maigizo, ushairi ,semi
    3. Taja umuhimu wa fasihi simulizi (ala 4)
      • Kuelimisha
      • Kuburudisha
      • Kuelekeza
      • Kuonya na kushauri
      • Kukuza uwezo wa kufikiria

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 2 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest