Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • JIBU MASWALI YOTE.

MASWALI

  1. INSHA (ALAMA 20)
    Insha yako isipungue maneno 350.
    Andika insha inayoafiki methali “Fadhila za punda ni mateke”
  2. UFAHAMU
    SOMA UFAHAMU UFATAO KISHA UJIBU MASWALI (Alama 15)

    Beata alikuwa msichana mrembo lakini alikuwa haambiliki, hasemezeki . Fauka ya hayo, alikuwa na tama isiyo na kifani.
    Alipokuwa katika shule ya msingi, walimu na wazazi walimfunza umuhimu wa kuwa na maadili. Isitoshe, alifunzwa masomo vyema lakini akili yake ilikuwa butu. Akawa haingizi chochote cha maana ila uchafu wa fikira. Nyumbani nako hakuzingatia maonyo. Alikuwa hatulii.
    Wakati fulani wa krismasi, Beata alipomaliza tu shule ya msingi, alikutana na mwanamume mmoja mliliwa na wasichana wengi;mtajika kwa mali na jina lake ni Mshikaji . Beata akadanganywa akadanganyika. Akatorokea kwa huyu Mshikaji ambaye alikuwa ameshawataliki wake wawili tayari. Akawa mke mlezi. Ikabidi awalee watoto waliobaki na baba yao baada yamanazao kutanzuka. Beata mwanzoni aliona raha, ingwa alikereka kuitwa mama kabla hata ya kumkopoa mwana wake mwenyewe. Aliwabeza waliokuwepo awali na akajiona kuwa yeye ndiye mchukuzi bora. Akadharau kuwa pakacha likivuja, nafuu huwa ni kwa yule mchukuzi. Aliwaona wenzake kama maua yaliyonyauka na lake ndilo kwanza linaonana na jua.
    Muda si muda, akajikuta ana wana watatu kwa kipindi kifupi. Mumewe naye hakutulia na mambo ya nje. Akaimarisha nyendo zake za kiguu na njia, akipochoka, akiingia garini na kuikata mitaa. Beata aende wapi? Alifungika nyumbani ndi ndi Akamlea mwana huyu na Yule; wake na wale wa kambo. Vijisenenesenene vikazidi. Lakini akajaribu kuvumilia akidhani atazila mbivu, wapi! Alipoligema ilibidi alinywe. Siku zikaja na kupita. Beata akajuta kwa kutosikiliza wakuu na kumkimbilia mtu ambaye hata hakuwa anmuelewa vizuri. Pesa na raha alizokuwa amezikimbilia akawa anazisikia kama hadithi ndotoni. Kwao nako kukawa hakurudiki. Beata akawa majamzito tena kama kawaida akawa anaenda kliniki za wajawazito. Alipopimwa ikabainika kuwa ana ukiwi. Mtoto alipozaliwa akafariki. Yule mumewe akaanza kumnyanyasa.
    Baada ya miaka mitatu, bwana Mshikaji, aliyekuwa akijitapa kwa unene na mali, akaanza kupotelewa na kiriba chake cha tumbo. Homa za hapa na pale zikaanza kumyemelea. Vipelevipele vikamsambaa mwilini. Hata akamsingizia Beata kuwa ni yeye aliyeuleta huo ukimwi Ilikuwa ni wazi kuwa msambazaji alikuwa ni yeye bwana. Waliokuwa pembe za chaki waliujua ukweli ulipokuwa . Baadhi ya vidosho wake walishaanza kupukutika kama majani yafanyavyo wakati wa mapukutiko. Isitoshe, wengine walikuwa hoi vitandani wakiwa hawajui waingiao wala watokao. Ugonjwa wa kamata ulishawakamata. Mwisho akawa ni wa kulazwa na kutoka hospitali hizi na zile. Pesa zikawaishia, wakawa waya. Beata akawa hana budi kuviuguza vidonda ndugu vyake na vya mumewe. Hatimaye, mumewe akabwagwa chini na ukimwi na akafafo!
    Si ndugu si marafiki, hawakumuelewa Beata. Waliamuona kama pweza aliyejipalia makaa makubwa ya moto makali. Ada za shule zikawa ni shida. Huruma ikwaingia watu. Watu wakasema. “Lisilobudi hutendwa.” Wakaubeba mzigo kwa hiari yao. Wakawafanyia watoto harambee ya ada na peza za matibabu. Mwishowe Beata naye aliaga dunia akiwa bado mbichi kwa umri. Hata miaka ishirini alikuwa bado hajafikisha. Watoto ikabidi walelewe na wahisani.
    Hapo walimwengu wakaja kutambua ukweli kwamba, uzuri si hoja hoja ni tabia. Isitoshe mtu akikimbiliwa na kila mtu, ukimwi hatauepuka. Mtu akiupata, hufa. Anadidimiza watu wengi pamoja na familia yake. Jamii ilifunzwa pia kuwa unene si hoja. Hata watu vibonge huweza kuleta ukimwi. Basi, jamii hiyo ikaazimia kuwa wao hawatakuwa watumwa wa tabia iletayo ukimwi. Walitambua kuwa ukimwi unarudisha nyuma maendeleo na kuipakaza jamii mizigo isiyo tarajiwa. Nasi tutahadhari kabla ya hatari
    1. Andika kichwa kifaacho kisa hiki (ala.1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    2. Ni jambo gani lililomkera Beata baada ya kuolewa na Mshikaji? (ala.1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    3. Toa sababu moja iliyomfanya Beata kuwadharau wenzake waliomtangulia kwa mshikaji? (ala.1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    4. Ni kwa nini Beata alianza kujuta? (ala2)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    5. Toa sababu moja kuonysha kuwa Mshikaji ndiye aliyeusambza ukimwi (ala.1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    6. Kulingana na kifungu hiki taja hasara zinazoletwa na ukimwi. (ala.3)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    7. Kwa nini walimu na wazazi hawangelaumiwa kwa yale yaliyompata Beata? (ala.1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    8. Andika maana ya: (ala.5)
      1. butu
        …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
      2. Kope zikawa si zake
        …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
      3. Akiwa bado mbichi
        …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
      4. Kuzanzuka
        …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
      5. Vijisenensenene.
        …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………

MATUMIZI YA LUGHA

  1. Taja aina mbili kuu za sauti.katika kiswahili (ala.2)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  2. Taja:
    1. Irabu za mbele. (ala.2)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    2. Irabu ya kati (ala.1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    3. Irabu za nyuma (ala. 1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  3. Kiungo ambacho hutetemaka na kutoa sauti huitwaje. (ala.1)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  4. Viungo ambavyo hutumika katika utamkaji wa sauti huitwa je? (ala1)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  5. Taja aina mbili za konsonanti. (ala.2)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  6. Andika konsonanti tatu mabazo ni vipasuo. (ala.3)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  7. Toa mifano miwili ya sauti za nazali/ving’ong’o. (ala.2)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  8. Suati mwambatano nini? (ala.1)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  9. Taja vipashio vine vya lugha. (ala.4)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..
  10. Tenganisha neno lifuatalo katika viambiu vyake mbalimbali. (ala.3)
    …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  11. Eleza maana ya:
    1. Kiimbo (ala1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    2. Shada (ala.1)
      …………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  12. Andika sentensi zifuatazo kwa wingi. (ala 4)
    1. Ukuta mbao ulianguka ni huu
      ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
    2. Mwanagenzi yule amepita mtihani vizuri
      ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………
  13. Sentensi zifuatazo ziko katika nyakati / hali gani? (ala.2)
    1. Otieno hula samaki kila siku
      ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    2. Yeye anaandika tu kitabu
      ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  14. Tambulisha manene mbalimbali katika sentensi zifuatazo. (ala 4)
    1. Mwanafunzi mvumilivu alisoma vizuri.
      ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    2. Yule ameongea manene mengi
      ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  15. Taja
  16. Kanusha sentensi ifuatayo. (ala2)
    1. Nyumba hiyo ifafunfuliwa
      ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  17. Eleza matumizi ya ‘Koloni’
    Kisha utungie sentensi. (ala.1)
    ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

FASIHI SIMULIZI (alama 15)

  1. Fasihi simulizi ni nini? (ala.2)
    ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  2. Taja na ueleze majukumu matano ya fasihi simulizi (ala 8)
    ……………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
  3. Eleza tofauti tano kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi (ala 10)
     FASIHI SIMULIZI   FASIHI ANDISHI
       
  4. Taja tanza nne kuu za fasihi simulizi. (ala.4)
    ……………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

MARKING SCHEME

INSHA

  1. Hii ni insha ya methali
    -maana yake
    Mtu akitendewa mema naye anakosa kuonyesha shukrani .
    1. mtahiniwa atoe kisa kinacholenga maana hii
    2. si lazima mtahiniwa aeleze maana na matumizi ya methali
    3. mtahiniwa ni sharti aisome insha yote kuzingatia vipengee muhimu vipengee hivi ni ?
      1. maudhui
      2. msamiati
      3. mtindo
      4. sarufi
    4. ngazi mbalimbali za kiwango kwa muhtasari
      KIWANGO NGAZI ALAMA
      A                 A+     19-20
                         A       18
                         A-      16-17
      B                B+      14-15
                        B        13
                        B        11-12
      C                C+      09-10
                        C        08
                        C-       06-07
      D                D+     04-05
                        D        03
                        D-       01-02

UFAHAMU

  1.                
    1. Asiyesikia na mkuu huvunjika guu
    2. umekuwa pweza kujipalia makaa?
      Sahihisha kichwa kingine chochote kinachoafiki kifungu hiki [alama 1]
  2. Kuitwa mama kabla ya kumkopoa mwana wake mwenyewe [alama 1]
  3. -Alijiona kuwa yeye ndiye mcukuzi bora
    - Aliwaona wenzake kama maua yaliyonyauka na lake ndilo kwanza linaonana na jua
    [alama 1]
  4. -kwa kutosikiliza wakuu na kumkimbilia mtu ambaye hata hakuwa anamuelewa vizuri
    - pesa na raha alizokimbilia akawa anazisikia kama hadithi ndotoni [alama 2]
  5. - mumewe hakutulia mambo ya nje , alikuwa kiguu na njia
    -Alikuwa na wanawake wengi nje ya ndoa–kukonda
  6. -homa hapa na pale
    -vipelevipele mwilini [alama 3]
  7. –walikuwa walimfunza umuhimu wa kuwa na maadili [alama 1]
  8.              
    1. isiyo na makali
    2. kuona aibu, soni, fedheha, haya
    3. -akiwa bado mdogo
      -Bado hajakomaa
    4. kuondoka mahali kwa haraka
    5. vijinenoneno

MATUMIZI YA LUGHA

  1.          
    1. konsonauti
    2. irabu
  2.                
    1. e,i
    2. a
    3. o,u
  3. nyuzi za sauti
  4. ala za sauti/ala za kutamkia
  5. –konsonauti ghuna [GH]
    -konsonauti sighuna [H]
  6. b,p,t,d,j,k,g
  7. m,n,ng, ny
  8. Ni sauti ambazo huundwa kwa kuweka pamoja konsonauti mbili au zaidi , kila herufi huweza kutambulika
    Mfano ny, nd,ng,mw,kw,n.k [alama 1]
  9. sauti___ silabi ___neno ____sentensi [alama 4]
  10. a____nafsi
    li------wakati
    ye ---- -kirejeshi
    m-------kitendwa
    pig------mzizi wa kitenzi
    a--------kiishio
  11.              
    1. ni mawimbi ya sauti jinsi sauti inavyopanda na kushuka mtu anapoongea
    2. ni mkazo unaowekwa kwenye silabi Fulani ya neno ili neno hilo liweze kutokeza maana yake halisi
  12.                
    1. kuta ambazo zilianguka ni hizi
    2. wanagenzi wale wamepita mtihani vizuri
  13.        
    1. mazoea
    2. uliopo
  14.        
    1. N, V,T, E
    2. W,T,N,V
  15. Nyumba hiyo haitafunguliwa
  16. kutanguliza orodha ya maneno
    kutanguliza maneno Fulani
    kutanguliza usemi halisi
    kutenganisha mada kuu na mada ndo go
    mwanafunzi atungie sentensi moja kuonyesha matumizi

FASIHI SIMULIZI

  1. Ni fasihi inayowasilishwa kwa njia ya mdomo [alama 2]
  2.              
    1. kuburundisha
    2. kuelemisha
    3. kuelekeza
    4. kuonya wa kushaur
    5. kututazamisha mazingira yetu
    6. kuukuza uwezo wa kufikiria
    7. kuendeleza utamaduni
      Mwanafunzi aeleza hoja kikamilifu maki moja kutaja maki moja moja kueleza [alama10]
  3.             
 FASIHI SIMULIZI  FASIHI ANDISHI
 Huwasilishwa    kwa njia   ya  mdomo [1]   Huwasilishwa  kwa njia  ya  maandishi
 Huhifadhiwa akilini  Huhifadhiwa kwenye  maandishi 
 Huweza kubadilishwa  hapo hapo wakati  wa kusimulia   Maandishi  yaliyoandika  ni  vigumu   kubadilishwa
 Ni mali  ya jamii nzima   Ni  mali  ya  mwandishi 
 Muundo   wake  ni rahisi  kufuatika   Muundo  wake  ni mgumu  kufuatika 
Hutegemea ubingwa  wa  msimulizi Hutegemea  usanii wa  mwandishi

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 2 Exams 2023.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest