Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 3 Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo:

  • Jibu maswali yote.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili

UFAHAMU (ALAMA 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuata

Leo hii suala la kuwaonyesha watoto mapenzi ni suala la ziada. Kuna mambo mengine mengi maishani mwetu ambayo tunayachukulia kuwa muhimu zaidi. Ni vizuri tuwaokoe watoto wetu, tusije tukawalilia baadaye. Kuna vitendo vya ukatili ambavyo watoto hutendewa.

Hivi majuzi tumekuwa na visa vya vilenge kung’olewa mimbani viumbe hawa walipokatiziwa uhai, maiti zao zilitupwa kama takataka. Hiyo ni miili ambayo ilipatikana je, ni maelfu mangapi ya miili mingine kama hiyo inayotupwa? Hii tu ilikuwa tone ndogo tu la bahari ya dhambi ambazo zote tunaogelea ndani.

Mambo kama haya ni mazao ya mimea yetu ambayo tulipanda sisi ambao hatuchelewi kujiita watu walio huru, walio na maendeleo na wa kisasa. Tumekuwa watu wa kupuuza mambo ya kimapokeo ya kuzingatia utu na kuficha aibu aghalabu tumejitia usasa kwa kutazama filamu na video chafu, kusikiliza muziki wenye maneno machafu. Tunapoona watoto wetu wakitembea nusu uchi, hatushughuliki hata kidogo kuwakanya.

Kama ni kosa, sisi sote tumehusika kwa njia moja au nyingine kwa njia tofauti. Ni vizuri tuelewe kuwa sisi ni wakuuzaji na walizi wa ndugu zetu kwa kila njia.

Tutawaokoa watoto kwa kukataa mambo yote yanayowanyanyasa. Lazima tuwaonyeshe watoto mapenzi, mapenzi si chakula, mavazi na makazi tu. Mapenzi si kuwaachia vijana uhuru watende watendavyo. Mapenzi sio kuwanunulia watoto vitu vya bei ghali au kuacha kuwakemea wanapokosa mwelekeo.

Mapenzi kwa watoto ni kuwaheshimu na kuwatendea kama binadamu yeyote. Lazima mzazi akumbuke kwamba mtoto hujifunza kutoka kwake. Mtoto atakutendea isitoshe jinsi unavyomtendea. Isitoshe jinsi unavyomtendea mtoto wako ndivyo atakavyowatendea watoto wake na wale wote ambao atapata kuhusiana nao kwa njia moja au nyingine.

Tuwaokoe watoto wetu katika viwango vyote vya ukuaji. Kusiwe na mwanya baina ya mzazi na mtoto. Watoto wawe kutuambia yote yanayowahangaisha mioyoni mwao, na hali hii itawapa wazazi fursa ya kuwasaidia. Mtoto anapokosa, tuwe tayari kumwonyesha kosa lake na kumwadhibu kwa mapenzi.

Mtoto wa mwenzetu akipotoka pia tuwe tayari kumkosoa na kuwaarifu wazazi wake. Tuwache ubinafsi wetu kumbuka kuwa mwana wa mwenzio ni wako. Ni jambo la busara kuhakikisha kuwa kama wazazi, tuzingatie haki zote za watoto.

Maswali

  1. Kwa nini suala la kuwaonyesha watoto mapenzi limekuwa la ziada. ( alama 2 )
  2. Ni mambo gani ambayo yanaweza kutufanya tuwalilie watoto wetu baadaye? ( alama 2 )
  3. Toa sababu zinazowafanya watu kuavya mimba. ( alama 2 )
  4. Ni mambo yapi ambayo yanachangia kupotoka kwa jamii ? ( alama 4 )
  5. Mwandishi ametumia tamathali za usemi. Zitaje huku ukitoa mifano kwa kila mojawapo. ( alama 3
  6. Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari. ( alama 2 )
    1. Vilenge
    2. Mwanya

MATUMIZI YA LUGHA ( ALAMA 40)

  1. Taja makundi mawili ya sauti za Kiswahili. (alama 1)
  2. Sauti hizi hutamkiwa wapi? (alama 2)
    1. /d/ ........................................................................................................................................
    2. /k/ ........................................................................................................................................
  3.  
    1. Ni nini maana ya sauti mwambatano? ( alama 2)
    2. Andika mfano wa neno lenye sauti mwambatano. (alama 1)
  4. Pigia mstari silabi zinazotiliwa shadda katika maneno yafuatayo. (Alama 2)
    1. Runinga
    2. Mto
  5. Andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo. (alama 2)
    1. KKKI
    2. KKI
  6. Bainisha maneno katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
    Aka! Mwalimu mrefu sana anaandika vizuri.
  7. Ainisha viambishi katika neno lifuatalo. (alama 2)
    Waliowachezea
  8. Onyesha matumizi mawili ya mkwaju katika sentensi. (alama 2)
  9. Eleza miundo mitatu ya nomino katika ngeli ya A-WA (alama 3)
  10. Andika sentensi hii kwa wingi. (alama 2)
    Msimamo unaofaa ni wa uadilifu.
  11. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii. (alama 2)
    Nilimchinjia mama yangu kuku.
  12. Bainisha aina za nomino zilitumika katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
    Zabibu alipata malezi mazuri kutoka kwa wazazi wake.
  13. Tunga sentensi yenye kitenzi kisaidizi na kitenzi kuu. (alama 2)
  14. Andika katika hali ya udogo (alama 2)
    Kiti cha mzee huyu kimevunjika
  15. Ainisha viunganishi katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
    1. Duma hukimbia kuliko mwanadamu.
    2. Una chaguo, soma ama uende nyumbani.
  16. Andika kinyume cha sentensi hii (alama 2)
    Nyanya aliingia chumbani na akazima taa.
  17. Yakinisha senensi ifuatayo. (alama 2)
    Hatutahitimisha masomo mwaka huu
  18. Tumia kihisishi hadi kudhihirisha. (alama 2)
    1. Wakati
    2. Mahali
  19. Kamilisha methali; (alama 1)
    Makuukuu ya tai.........................................................................................................................

ISIMU JAMII ALAMA 10

  1. Eleza sifa tatu za sajili ya hospitali. ( alama 6)
  2. Taja sifa mbili za lugha ya kitaifa. (alama 2)
  3. Taja majukumu mawili ya lugha rasmi. (alama 2)

FASIHI SIMULIZI ALAMA 15

  1. Sanaa ni nini? (alama 1)
  2. Eleza tofauti sita kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi. (alama 6)
  3. Fafanua dhima tano za fasihi simulizi katika jamii yako (alama 5)
  4. Taja aina tatu za wahusika katika kazi za fasihi simulizi. ( alama 3)

MARKING SCHEME

UFAHAMU

MASWALI NA MAJIBU

  1. Kwa nini suala la kuwaonyesha watoto mapenzi limekuwa la ziada ?
    • Kuna mambo mengine ya muhimu ambayo hushughulikiwa katika maisha yao. (1x2=2)
  2. Ni mambo gani ambayo yanaweza kutufanya tuwalilie watoto wetu baadaye?
    • Watoto wetu wanaweza kupotoka kisha sisi wazazi tujute. (1x2=2)
  3. Toa sababu zinazowafanya watu kuavya mimba .
    • Msichana ambaye hajaolewa
    • Wasichana wanapopata mimba wakiwa shuleni
    • Wanawake wanaonajisiwa
    • Msichana anapokataliwa na mpenziwe
    • Mama anapougua na maisha yake kuwa hatarini (Zozote 2 x 1 = 2)
  4. Ni mambo yapi ambayo yanachangia kupotoka kwa jamii?
    • Wazazi kuwa na shughuli nyingi
    • Kutowapenda watoto wao
    • Kutowatendea kama binadamu na kutowaheshimu watoto
    • Mzazi kutokuwa kielelezo chema kwa watoto
    • Kukiwa na mwanya baina ya mzazi na mtoto
    • Kukiwa na ubinafsi wa kutomkosoa mtoto wa mwenzetu anapokosa na kuarifu.     (Zozote 4x 1 =4)
  5. Mwandishi ametumia tamathali za usemi. Zitaje huku ukitoa mifano kwa kila mojawapo.
    • Tashbihi – Maiti zilitupwa kama takataka
    • Maswali ya balagha – Je, ni maelfu mangapi ya miili mingine kama hiyo inayotupwa ?
    • Jazanda – Mambo kama haya ni mazao ya mimea yetu ambayo tulipanga sisi    (3x1=3)
  6. Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari.
    1. Vilenge – Vijusi / watoto wasiofikia umri wa kuzaliwa (1 x 1 = 1)
    2. Mwanya – Pengo / nafasi (1 x 1 = 1)

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1.  
    1. konsonanti
    2. irabu (2 x1 =2)
  2.  
    1. /d/ ufizini
    2. /k/ kaakaa laini (2 x 1 =2)
  3. sauti za konsonanti mbili au tatu zinazotamkwa kwa pamoja (1x2=2)
  4.  
    1. runinga
    2. mto (2x1=2)
  5. KKK        mf         ku-nywa
    KKI         mf          li-nda (2x1=2)
  6. Aka!Mwalimu mrefu sana anaandika vizuri
    I N V E T E (6 x ½= 3)
  7. waliowa-viambishi awali
    ea- viambishi tamati (2x1=2)
  8. Mkwaju
    1. Kuandika tarehe mf Alizaliwa tarehe 5/6/1998.
    2. kuonyesha kumbukumbu mf KUMB 1/2009
    3. kuonyesha visawe mf Nenda katika shule/skuli.
    4. Kuonyesha au Wanawake/wanaume wataajiriwa.
      mwanafunzi atunge sentensi (2x2=2)
  9. M-WA Mtu-watu
    KI-VI kipofu-vipofu
    Ø-Ø samaki-samaki
    Ø-MA daktari-madaktari
    M-MI mtume-mitume (3x1=3)
  10. Misimamo inayofaa ni ya uadilifu (1x2=2/0)
  11.  
    1. nilimchinja kuku kwa niaba ya mama
    2. Nilichinja kuku ili mama ale
    3. Nilichinja kuku ili mama aone (zozote 2x1=2)
  12.  
    1. Zabibu; nomino ya pekee
    2. malezi; nomino ya dhahania
    3. wazazi; nomino ya kawaida (3x1=3)
  13. Mwanafunzi alikuwa akicheza uwanjani.
                           Ts              T                             (2x1=2)
  14. Jikiti la jizee hili limevunjika (1x2=2)
  15.  
    1. kuliko; U cha kulinganisha
    2. ama; U cha uteuzi (2x1=2)
  16. Nyanya aliondoka chumbani na akawasha taa (2x1=2)
  17. Tutahitimisha masomo mwaka huu. (2x1=2)
  18. wakati; Alimsubiri hadi jioni
    mahali;Fagia hadi hapa (2x1=2)
  19. Makuukuu ya tai si mapya ya kengewa (1x1=1)

ISIMUJAMII (ALAMA 10)

  1. Sajili ya hospitalini
    1. Hutumia lugha ya taifa au rasmi
    2. Msamiati maalum wa hospitalini kv majina ya dawa
    3. Maswali na majibu baina ya mgonjwa na mhudumu
    4. Kuchanganya ndimi/msimbo
    5. Lugha nyepesi isipokuwa katika hali mahsusi
    6. Lugha ya huruma kwa wagonjwa
    7. Lugha ya masimulizi na maelezo kutoka kwa mgonjwa
    8. Lugha ya utohozi kv dawa na vifaa
    9. Lugha isiyo na tasfida kv kuhara
      mwanafunzi aeleze (6x1=6)
  2. sifa za lugha ya taifa
    1. Huweza kuteuliwa kutoka kwa lugha mojawapo ya kabila fulani.
    2. Inazungumzwa na watu wengi nchini
    3. Ina uwezo wa kuondoa hisia za kikabila na kufanya watu kuhisi kuwataifa moja.
    4. Ina uwezo wa kukidhi mahitaji ya kimawasiliano.     (zozote 2x1=2)
  3. Majukumu ya lugha rasmi
    1. Kuendesha shughuli za ofisi za serikali
    2. Kufundishia shuleni na vyuoni
    3. Kutumiwa katika hati zote za serikali    (2x1=2)

FASIHI SIMULIZI (ALAMA 15)

  1. Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha hisia na fikra za binadamu. (alama 1x1=1)
  2.  
    1. Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
    2. Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi.
    3. Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi.
    4. Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.
    5. Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi.
    6. Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira.
    7. Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira.
    8. Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum.
    9. Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi, maigambo.
    10. Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya.
    11. Fasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamu
    12. Fasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalum.
    13. Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi simulizi sio lazima iwasiliane na mwandishi.
      za kwanza 6x1=6
  3. dhima ya fasihi katika jamii
    1. Kuburudisha/kustarehesha/kufurahisha/ kuchangamsha/kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili – ujumbe huwasilishwa kwa njia ya kuvutia na kuleta ucheshi
    2. Kuadilisha /kufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na kukataa sifa hasi za wahusika.
    3. Kukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo.
    4. Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi wa fasihi andishi.
    5. Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k.hizi hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
    6. Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k.
    7. Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ - Mtu hawezi kumwoa dadake.
    8. Kuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k.
    9. Kukuza lugha k.v. ulumbi na misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha sanifu.
    10. Kukuza ubunifu k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k.
    11. Kukuza uzalendo kwa kufanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa au watu waliotendea jamii makuu.
    12. Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k.
      (za kwanza 5x1=5)
  4. aina za wahusika
    1. wanyama
    2. binadamu
    3. mazimwi
    4. vitu(viumbe visivyo uhai)
    5. fanani
    6. hadhira
      (zozote 3x1=3)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 3 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest