Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Mid Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp

UFAHAMU (al 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuatia.

Nchi yetu imeraukia mawio ya machafuzi ya kisiasa baada ya shughuli za uchaguzi zilizogonga mwamba mkuu. Hili lilijiri baada ya Tume ya Uchaguzi kukosa kuendeleza uchaguzi kwa njia iliyostahiki. Jambo hili lilizaa msukosuko wa kisiasa usiomithilishwa katika historia ya taifa letu.
Hivi sasa Wakenya wanaishi kwenye kambi za watu wasio na makazi. Hiki ni kinaya kikuu kwani matukio haya yamezuka baada ya zaidi ya miongo minne ya uhuru. Vilio vya Wakenya vimeshamiri na kupaaza sauti vikilalamikia kukosa makazi, lishe na hata ndoa kusambaratika. Ndoa zimevunjika baada ya ‘wenyeji’ kuwatimua ‘wageni’ na damu kumwagika.

Misukosuko ya kisiasa kama hii imekumba mataifa mengi ya Afrika miaka nenda rudi na kuchangia bara kudumaa na kuvia kiuchumi.Kenya imekuwa miongoni mwa mataifa yanayowapa faraja wakimbizi kutoka nchi jirani zinazokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, zikiwemo Somalia na Sudan. Kinaya ni kwamba Wakenya wamekuwa wakimbizi katika nchi yao wenyewe.Vita katika Somalia vimesababishwa na koo mbali mbali zinazopigania uongozi hali ambayo imekwamisha shughuli zote za kiuchumi.Hali ya sasa ya Kenya imechochewa na msururu wa sababu.

Ukabila na tamaa ya uongozi zilionekana wazi katika miundo ya vyama vikuu vya kisiasa na katika kampeni zao. Wakenya walipiga kura kwa misingi ya kikabila kila upande ukitazamia mtu wao kushinda uchaguzi huo. Kwa upande mwingine, viongozi hao kutokana na tamaa ya uongozi walikuwa wameamua kushinda uchaguzi huo kwa vyovyote vile. Leo tunavuna matunda ya siasa za ukabila na tamaa ya mamlaka.Maelfu ya Wakenya ni wakimbizi nchini na katika nchi jirani ya Uganda. Wakenya hao wanahitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi. Serikali na Shirika la Msalaba Mwekundu zimefanya juhudi kuwasaidia wahasiriwa Lakini, kuna tetesi kwamba ubaguzi umejipenyeza katika ugawaji wa msaada huo.Waliopewa jukumu la kugawa msaada huo ni sharti waelewe kuwa waathiriwa ni Wakenya wenzao na hawafai kubaguliwa kwa misingi ya makabila yao. Matukio kama haya hayastahili kutukia asilani katika taifa hili.

Twahitaji zao aali la viongozi wasiojitwika ubabe bali wawe watumishi wa wananchi. Wanastahili kutupilia mbali tamaa za kujilimbikizia mali na kung’ang’ania uongozi. Pia katiba inafaa irekebishwe. Wakenya wanastahili kuelimishwa kuhusu udugu na utaifa. Fauka ya haya, masuala yanayohusiana na umiliki wa ardhi yanafaa kutadarukiwa kwa dhati.

Maswali ya Ufahamu

  1. Toa anwani mwafaka kwa makala haya. (al 2)
  2. Taja madhara mawili ya ukabila. (al 2)
  3. Shughuli za ugawaji wa misaada zimekumbwa na changamoto gani? (al 4)
  4. Eleza tofauti ya chanzo cha vita nchini Somalia na Kenya. (al 2)
  5. Mwandishi anatoa mapendekezo yepi kwa kutatua tatizo hili la ukabila. (al 4)
  6. Eleza kinaya cha maisha ya wakenya kwa sasa. (al 2)
  7. Taja matatizo mawili ya shirika la msalaba mwekundu. (al 2)
  8. Eleza maana ya maneno hayo yaliyotumika katika kifungu cha ufahamu. (al 2)
    1. Mawio
    2. Tadarukiwa

MATUMIZI YA LUGHA

  1. Eleza maana ya: (al.2)
    1. Kiimbo
    2. Shadda
  2. Andika maneno mawili yenye muundo ufuatao. (al.2)
    Irabu + irabu + irabu
    Irabu + kinsonanti + irabu
  3. Fafanua matumizi matatu ya kistari kifupi. (al. 3)
  4. Bainisha maneno katika sentensi zifuatazo. (al. 4)
    1. Mtoto wa Amina ni mtundu sana
    2. mbuzi na kondoo wamepelekwa malishoni.
  5. Eleza maana ya mofimu. (al. 2)
  6. Andika kinyume cha sentensi zifuatazo. (al.2)
    1. Kizito amefunika mkoba taratibu.
    2. Wameshurutishwa kuzibua mtaro.
  7. Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? (al. 2)
    1. Huzuni
    2. mate
  8. Eleza maana ya: (al.2)
    1. Kiunganishi
    2. Kihusishi
  9. Kamilisha tanakali za sauti zifuatazo . (al. 3)
    1. Maliza –
    2. Anguka –
    3. Lewa –
  10. Taja aina tatu za vitenzi. (al. 3)

ISIMU JAMII

UFAHAMU  (al 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuatia.

MASWALI YA UFAHAMU

  1. Toa anwani mwafaka kwa makala haya.
    • Siasa
    • Misukosuko ya kisiasa
    • Uchaguzi     (al.2)
  2. Taja madhara manne ya ukabila. (al 4)
    • Wakenya kukosa makazi
    • Kukosa lishe bora
    • Ndoa kusabaratika
    • Kumwagika kwa damu
    • Uchumi kusorota
  3. Shughuli za ugawaji wa misaada zimekumbwa na changamoto gani? (al 2)
    • Ubaguzi kwa misingi ya kikabila katika ugawaji wa misaada.
  4. Eleza tofauti ya chanzo cha vita nchini Somalia na Kenya. (al.2)
    • Vita katika Somalia vinasababishwa na koo zinazopigania uongozi ilhali Kenya vinasababishwa na ukabila na tamaa  ya uongozi.
  5. Mwandishi anatoa mapendekezo yepi kwa kutatua tatizo hili la ukabila. (al 4)
    • Viongozi wawe watumishi wa wananchi
    • Wasijilibikizie mali na kung’ang’ania uongozi
    • Katiba irekebishwe
    • Wakenyua waelimishwe kuhusu udugu
    • Washughulikie masuala ya umiliki wa mashamba.
  6. Eleza kinaya cha maisha ya wakenya kwa sasa. (al 2)
    • Wakenya kuwa wakimbizi katika nchi ilhali awali waliwahifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani.
  7. Taja matatizo mawili ya shirika la msalaba mwekundu. (al 2)
    • Ubaguzi umejipenyeza katika ugawaji wa msaada.
  8. Eleza maana ya maneno hayo yaliyotumika katika kifungu cha ufahamu. (al 2)
    1. Mawio - Mwazo wa machafuzi/misukosuko
    2. Tadarukiwa - Shughulikiwa

MATUMIZI YA LUGHA

  1. Eleza maana ya: (al.2)
    1. Kiimbo - Kupanda na kushuka kwa sauti.
    2. Shadda – Ni mkazo
  2. Andika maneno mawili yenye muundo ufuatao.    (al.2)
    Irabu + irabu + irabu - Aua
    Irabu + kinsonanti + irabu - Aoa
  3. Fafanua matumizi matatu ya kistari kifupi. (al. 3)
    • katika tarehe
    • Kuonyesha neno linaendelea
    • Kutenga silabi
    • Kuonyesha vipindi (1920-1930)
    • Kuunganisha  maneno (Isimu – jamii)
  4. Bainisha maneno katika sentensi zifuatazo. (al. 4)
    1. Mtoto wa Amina ni mtundu sana
      N  H  t V  E
    2. mbuzi na kondoo wamepelekwa malishoni.
      N  U  N  T  E
  5. Eleza maana ya mofimu. (al.2)
    • Nikipashio kidogo zaidi katika lugha chenye maana kisanifi                                                                                                                     
  6. Andika kinyume cha sentensi zifuatazo. (al.2)
    1. Kizito amefunika Nkoba taratibu.
      • Amefunua
    2. Wameshanitisha kuzibua mtaro.
      • Kuziba
  7. Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? (al. 2)
    1. Huzuni
      • I – ZI  - Huzuni
    2. mate
      • Ya -  Mate
  8. Eleza maana ya: (al.2)
    1. Kiunganishi – Fungu la maneno linalounganisha maneno virai, vishashi au sentensi.
    2. Kihusishi – Neno linaloonyesha uhusiano baina ya neno moja na jingine.
  9. Kamilisha tanakali za sauti zifuatazo . (al. 3)
    1. Maliza – Fyuu
    2. Anguka – tifu
    3. Lewa –  chopi
  10. Taja aina tatu za vitenzi. (al. 3)
    • Kitenzi halisi
    • Kitenzi kikuu
    • Kitenzi kisaidizi
    • Kitenzi kishirikishi
    • Vitenzi sambamba.

ISIMU JAMII

Taja sifa tano za mazungumzo ya kituo cha polisi. (al.5)

  1. Lugha yenye ukali kw. Polisi.
  2. Lugha ya kudhadisi/maswali ni majibu.
  3. Kuchanganya ndimi.
  4. Lugha isiyozingatia kanuni za kisarufi.
  5. Lugha ya unyenyekevu kwa mshukiwa.
  6. Lugha ya kuamrisha.
  7. Lugha inayoeleweka kwa urahisi
  8. Lugha ya misimu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Mid Term 2 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest