Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 3 Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

  • Jibu maswa yote.
  1. UFAHAMU (ALAMA 15)

    Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali
    Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni nini hasa? Tunaweza kula demokrasia? Ni dude gani hili lina kichwa au mkia pekee yake? Je demokrasia inazuia njaa? Demokrasia ni himaya ya wasomi tu au vilevile ni haki ya mafalahi? Kwa muda mrefu kumekuwa na kinyang’anyiro kikubwa katika jamii ambacho azma na. matokeo yake yamekuwa ya kutatanisha. Baadhi ya watu wamejitokeza kama mchuzi wa ugali na kuzusha zahama ambazo si za kuyumkinika. Vichwa vya adinasi vikafyekwa kwa miundo na maparange na matumbo yakapasuliwa na kuapakaza utumbo na vijusi kila mahali. Shingo zikapigiwa vigingi na kukomewa ardhini. Demokrasia si mchezo wa lelemama. Ni sharti tujifunge vibwebwe tumwage damu na tufe ili tupate demokrasia ya kweli!” Mmoja wa mibabe wa demokrasia alinguruma kadamnasi ya umati huku ngoma za vita zikirindima.” Hata Marekani na ulaya walimwaga damu. Mamilioni ya watu walipukutishwa na kimbunga cha demokrasia. Chini walilaliana kama Vimatu na tunutu. Hawa manafiki wanafikiri hatuwajui. Katu hatutakubali porojo zao. Wanatupikia majungu kisha wakatoweka. Kuna demokrasia ya Afrika na ile ya Ulaya ‘ mkereketwa wa Uafrika akachanganua.

    Demokrasia ya Afrika basi imefuata mkondo huu wa umwagikaji damu. Kila kukijiri uchaguzi zahama hutawala. Walio madarakani hawataki kubanduka. Hutaruta visababu vya kukwepa wimbi la ushinde. Demokrasia ni mchezo wa mizengwe tu ati. Hali hil imesababisha maafa makubwa, uharibifu mkubwa wa mali, majeraha, ukimbizi wa raia ndani na nje ya mataifa husika, dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake, kuzagaa kwa magonjwa ainati, uhasama wa kikabila. Jambo la kusikitisha ni kwamba raia na viongozi hawaelekei kujifundisha chochote kutokana na hali. Huku mataifa mengi Ulayani na Asia yakikwea daraja moja baada ya nyingine kimaendeleo, Afrika imedumaa tu. Imesalia kuimba ule wimbo wake wa kutokea azali‘ Tutaendelea vipi na tunadhulimiwa na kaka wakubwa”. Siasa ya demokrasia katika bara la Afrika ina tija kubwa hususan kwa wale wachache wanaofanikiwa kudhibiti nyenzo za kutia tonge kinywani. Ulitima wa umma husalia miradi hewa ya tabaka la viongozi ambayo hutumiwa kujinadi zamu nyingine ifikapo tena. Demokrasia ya kweli imo mikononi mwa umma pale utakapojikomboa kimawazo na kwa ujasiri kudai huduma bora, uajibikaji na kuheshimiwa kwa mkataba wa kijamii uliosisiwa na Jean Jacques Rousseau.

    Maswali
    1. Binadamu amechanganyika kwa njia ipi) (Alama 2)
    2. Ni vipi Demokrasia ya kweli inaweza kufikiwa (Alama 2)
    3. Kwa nini inasemekana kuwa ‘Demokrasia ni mchezo wa mizengwe? (Alama 2)
    4. Ni athari gani hutokana na kinyang’anyiro cha Demokrasia? (Alama 4)
    5. “Dhiki za raia zimesalia kuwa mradi-hewa wa wanasiasa” Eleza. (Alama2)
    6. Fafanua maana ya maneno na mafungu yafuatayo jinsi yalivyotumika katika taarifa.    (Alama 3)
      1. Mafahali
      2. Wanatupikia majungu
      3. Ukarabati
  2. UFUPISHO (ALAMA 15)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
    Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.Huenda wakasalia katika hali hii ya kutojua hadi wanapokosa kulipa ujira wa watumishi wao wa nyumbani halafu maskini mwajiriwa huyu anaripoti kwa chifu, kwa kuwa ni hali yake. Chifu ni uzi muhimu katika vazi Ia kijamii. Bila hawa maafisa, jamii kama tunavyoijua ingeporomoka. Wakati mwingine hawaungwi mkono. Mfano mzuri ni kukataliwa kwa katiba kielelezo cha Wako, Novembe 2005, wakati wa kura ya maoni. Kwa sababu jukumu la chifu au kibadala chake halikudhihirishwa wazi wazi katika kielelezo, wengi walikataa stakabadhi hiyo, wakihofia sasa hawataweza kufikia mtawala wao kushughulikia malalamishi yao.

    Nimeishi mtaa wa Nairobi West miaka mingi na kuhudhuria kamati nyingi za lokesheni, chini ya uwenye kiti wa chifu akisaidiwa na naibu na wazee. Mikutano, pia inahudhuriwa na madiwani, inspekta wa askari tawala na wawakilishi wengi na washia dau katika lokesheni. Takribani kila swali linalogusia maslahi ya jamii linajadiliwa na kuchunguzwa na maazimio kupitishwa. Mada muhimu wakati wa mikutano hii ni usalama, taa za barabarani, ulanguzi wa mihadarati hasa karibu na taasisi za elimu, kudumisha usafi wa vyoo vya umma, kudumisha usalama kupitia kwa raia na swala nyeti la vioski.

    Kazi ngumu ya chifu ni kuwazia kila kju. Kwa mfano, mwenye kioski ni sharti apate mkate wa kila siku na sehemu ya biashara yake iliyoko ni muhimu. Ikiwa kioski kitajengwa na kukiuka sheria za baraza la jiji au ikiwa wizi usiofahamika na utumizi wa dawa za kulevya unatokea kufuatia kukua kwa idadi ya vioski katika eneo, shinikizo zinaelekezwa kukuwa kwa wenye vioski. Chifu lazima azingatie shinikizo za umma hatari za kiusalama na hofu za wenye vioski kabla ya kufanya uamuzi ikiwa mijengo hiyo ibomolewe.

    Tatizo jingine ni watoto wa barabarani. Makao ya kuwakimu ni machache kama walivyo wahudumu wa kijamii, suluhu ni nini? Tuwatupe katika ukumbi wa kijamii, ambao watahepa pindi tu, wapatapo fürsa ndogo au wapelekwe huduma kwa vijana wa Taifa, ambapo wachache wanaweza kutunzwa kwa wakati mmoja. Ili kufaulu kwa wengine, sharti wawe katika vituo vya urekebishaji tabia za matumizi ya dawa za kulevya. Tuwakabidhi polisi kwa sababu wanaranda au tujaribu kuungana na vituo vya urekebishaji tabia kuhakikisha hawatarudi barabarani.

    Mazingira ya lokesheni pia huibuka katika ajenda. Hali ya barabara, juhudi za kusafisha mazingira, wizi wa maji na umeme, usafiri wa umma, uchafuzi wa mazingira, hewa na kelele, hii inatokea kupitia malalamishi ya watu wanaoishi karibu na mabaa na uzingativu wa saa ya biashara hujadiliwa kila mara. Chifu ni sharti afahamu sheria na kanuni zinazotawala hali hizo, halafu ajadili na wahusika kabla ya kutoa mwelekeo. Usawa na uwazi katika kugawa fedha za Hazina ya maendeleo ya maeneo Bunge, pia hujadiliwa.

    Katika maswala haya mengine, chifu ndiye aliye nyanjani. Anawajibikia jamii na wakubwa wake na hatarajii shukrani au kutambuliwa kwa kazi njema aliyofanya. Isipokuwa hukashifiwa anapofeli. Watu wengine wana taswira ya Chifu kama mtu kwenye jukwa, kofia yake. na kifimbo kinachompa mamlaka ya kuhutubia baraza, Kajubu tyji zaidi ya hivyo. Kwa mujibu wa kitabu cha mafunzo ya machifu na Naibu wao (Januari 2004), wajibu wa chifu ni kuwakilisha sera na mipango ya serikali kwa wananchi. Chifu ni ajenti wa “mabadiliko” mwenye wajibu Wa kuhamasisha watu katika maendeleo. Anajishughulisha na kujua ni nani maskini katika lokesheni, mkoa, mgonjwa asiyeweza kupata tiba na kupanga jinsi mhasiriwa atakavyopelekwa hospitali kama anavyoweza. Ni sharti ashughulikie ugomvi wa kinyumbani, uhalifu wa watoto, dhuluma za watoto, agawe chakula na mavazi kwa wahitaji na kuhukumu kesi ndogo za wizi na uharibifu. Chifu hutatua kesi za kisheria kwa wasioweza kumudu wakili. Wakati wananchi wanapohisi mbunge wao hafikiliki na hawana imani na polisi, chifu ndiye suluhisho.

    Lakini kuna machifu wachache ambao hawafanyi kazi yao vyema. Kwa ufupi, chifu ni mkusanyiko wa kushngaza; mfalme katika himaya yake, pasta, baba msikivu, wanasaikolojia, mtunga sheria na mdumisha sheria, balozi mchaguzi, mama, mlumbi na askari asiyechelewa. Ingawa halipwi vyema, anafanya kazi bila tarakilishi, na aghalabu hujilipia gharama ya kodi ya afisi yake kutoka mfuko wake. Kwa sababu ni mtumishi wa umma, tunataraji afanye kazi mufti. Hiyo haimaanishi tusishukuru kwa kazi njema aliyofanya. Serikali inaweza kufanya hivi kwa kuimarisha hali yake ya kazi, mazingira yake ya kikazi, na kuhakikisha yana tarakilishi, anapata mafunzo ya uongozi na usimamizi. Wananchi sharti washukuru watu hawa kwa kujitolea sabili.

    Maswali
    1. Fupisha aya nne za kwanza (Maneno 60) (Alama 6, mtiriko,1)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Kwa maneno kati ya 80-90 fupisha aya ya tano hadi mwisho. (Alama 9, mtiririko 1)
      Matayarisho
      Jibu
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1.  
      1. Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi(Alama 1)
      2. Taja sifa mbili bainifu za vokali ‘U’ (Alama 2)
    2. Yakinisha sentensi hii. (Alama 2)
      Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.
    3. Andika upya sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo uliyopewa. (Alama 2)
      Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika bwawa la maji.
      (Anza: Katika bwawa………………………..)
    4. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mbinu ya matawi (Alama 4)
      Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri
    5. Ukizingatia neno lililo katika mabano, andika sentensi hizi katika hali ya kutendeka.
      1. Daraja hili(vuka) tu wakati wa kiangazi (Alama 1)
      2. Kitabu hicho(soma) ijapokuwa sura zingine hazimo. (Alama 1)
    6. Andika katika ukubwa wingi (Alama 2)
      Kitoto kijeuri kikiletwa kitarejeshwa kwao.
    7. Andika katika usemi taarifa. (Alama 2)
      “Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.
    8. Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo pamoja na kivumishi ___ingine(Alama 2)
      1. dau
      2. urembo
    9. Bainisha yambwa tendwa na yambwa tendewa katika sentensi hii. (Alama 2)
      Mbunge wa Mtondo Kaskazini atawajengea wanakijiji josho kisha aghurie mjini.
    10. Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo. (Alama 2)
      1. Nafasi viambata
      2. Visisitizi
    11. Tumia neno dhahiri katika setensi kulingana na maagizo (Alama 3)
      Kama:
      1. Kiambishi
      2. Kivumishi
    12. Tunga sentensi ya neno moja yenye visehemu vifuatavyo vya sarufi. (Alama 3)
      1. Kiambishi kiwakilishi cha kiima
      2. Kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo
      3. Kiambishi kiwakilishi cha kitendewa/mtendewa
      4. Shina la kitenzi
      5. Kiambishi cha kauli ya kutendesha
      6. Kiishio
    13. Bainisha kirai nomino na kirai kivumishi katika sentensi hizi. (Alama 2)
      1. Nguo aliyonunua mzazi ni mpya.
      2. Kondoo mwenye manyoya mengi hupendeza.
    14. Akifisha (Alama 3)
      sikukuu ya madaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana akasema atakuja kuniona pamoja na mkewe siku ya jumapili
    15. Eleza tofauti za kimaana baina ya sentenzi hizi. (Alama 4)
      1. Jambazi kutoka dukani aliiba
      2. Kutoka dukani jambazi aliiba.
      3. Aliiba jambazi kutoka dukani.
      4. Jambazi aliiba kutoka dukani.
    16. Unda nomino mbilimbili kutokana na mizizi ifuatayo. (Alama 2)
      1. -f-
      2. -l-
  4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Eleza maana ya lugha (Alama 1)
    2. Taja sifa nne za lugha (Alama 4)
    3. Eleza sifa za sajili ya maabadani (Alama 5)

FASIHI SIMULIZI

  1. Fafanua Uhusiano uliopo baina ya fasihi simulizi na fasihi andishi. (Alama 10)
  2. Huku ukitoa mifano kem kem, eleza dhima zozote tano za fasihi simulizi.(alama 10)

MARKING SCHEME

UFAHAMU (ALAMA 15)

  1. Ameshindwa kuielewa dhana ya demokrasia. Dhana hii ina fasiri nyingi kutegemea lengo la mtu/kundi la watu/mahali wanapoishi  2x1=Alama 2
  2.  
    1. Pale umma utakapojikomboa kimawazo
    2. Kwa ujasiri kudai huduma bora
    3. Uajibikaji pamoja na kuheshimiwa kwa mkataba wa kijamii    2x1=Alama 2
  3.  
    1. Kinyang’anyiro cha madaraka
    2. Wasio na madaraka watumia kila mbinu kuyapata
    3. Walio madarakani hawataki kubanduka-hutafuta visababu vya kusalia madarakani        2x1=Alama 2
  4.  
    1. Maafa
    2. Uharibifu wa mali
    3. Majeraha
    4. Ukimbizi wa raia nje na ndani ya mataifa husika
    5. Dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake
    6. Uhasama wa kikabila
    7. Kuzagaa kwa aina mbalimbali ya magonjwa           Zozote 4x1=Alama 4
  5.  
    1. Hutumiwa na tabaka la viongozi kujinadi/hasa wakati wa uchaguzi
    2. Wanasiasa hujifanya kuwa wanayajali masilahi ya wanajamiii kumbe huruma zao ni kilio cha mamba 2x1=Alama
  6.  
    1. Mafalahi-wachochole, maskini, raia, penye ukavu
    2. Wanatupikia majungu-wanatufitini au wanatukosanisha
    3. Ukarabati-Urekebishaji, utengenezaji, kubambanya     3x1=Alama 3

MUHTASARI (ALAMA 15)

  1.  
    1. Matajiri wengi mijini hawajui juu ya utawala wa chifu hadi watakapokuwa na kesi mbele ya chifu
    2. chifu ni muhimu na huunganisha jamii
    3. watu wengi huwapuuza
    4. chifu huunda baraza ambazo hujadili maswala muhimu kijijini
    5. kazi ya chifu ni ngumu haswa katika kufanya uamuzi muhimu
      Hoja 5x1=Alama 5
      Utiririko 1x1=Alama1
      aa Jumla=Alama 6
  2.  
    1. Tatizo la chifu ni kutafutia watoto wa barabarani makazi na vituo vya kurekebisha tabia
    2. chifu lazima atunze mazingira ya lokesheni kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa
    3. ahakikishe kuna usawa katika ugawaji wa pesa za maendeleo ya maeneo bunge
    4. kuwasilisha sera na mipango ya serikali kwa wananchi
    5. huongeza miradi ya maendeleo katika lokesheni
    6. hutatua ugomvi na kesi za sheria kwa wasioweza kulipa wakili
    7. machifu wengine hawafa
      1. nyi kazi yao vyema
    8. kutokana na umuhimu wa chifu serikali yafaa kuinua hali yake
      Hoja 8x1=Alama 8
      Mtiririko=Alama 1
      Jumla=Alama 9

MATUMIZI YA LUGHA

  1.  
    1. /s/ na /z/
      ½ x2=Alama 1
    2.  
      • Inapotamkwa ulimi huinuliwa na kuwa juu kinywani
      • Ulimi hurudi nyuma
      • Midomo huwa mviringo na hukaribiana
        Zozote 2x1=Alama 2
  2. Simba anaponguruma/angurumapo wanyama wote hawababaiki 1x2=Alama 2
  3.  
    • Kaika bwawa la maji mmepatikana mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa
    • Katika bwawa la maji amepatikana mbwa aliyeripotiwa kuwa ameibwa
    • Katika bwawa la maji, amepatikana mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa
      Yoyote 1x2=Alama 2
  4.  
    F2SwaET32023Ansd
  5.  
    1. Daraja hili huvukiwa/linavukika tu wakati wa kiangazi Alama 1
    2. Kitabu hicho kinasomeka/chasomeka/husomeka/kilisomeka ijapokuwa sura zingine hazimo
      Alama1
  6.  
    • Majitoto majeuri yakiletwa yatarejeshwa kwao
    • Matoto jeuri yakiletwa yatarejeshwa kwao
      4x ½ =Alama 2
  7. Leo alimwambia Asha kuwa wangewatembelea wazazi wao siku hiyo jioni.    ½ x4=Alama 2
  8.  
    1. Lingine, jingine
    2.  Mwingine     2x1= Alama 2
  9.  
    • Yambwa tendwa-josho
    • Yambwa tendewa-wanakijiji   2x1=Alama 2
  10.  
    1. nafsi viambata
      Atumie moja kati a;a-, ni-, m-, tu-, u-, wa-;
      Kwa mfano ;Alituchezea
    2. Visisitizi.
      Kwa mfano ;yuyu huyu, wawa hawa n.k   2x1=Alama 2
  11.  
    1. Kivumishi
      Jambo dhahiri limesemwa.(tathmini)
    2. Kielelezi
      Ilikuwa dhahiri kuwa alitudanganya (tathmini)   1 ½ x2=Alama 3
  12. Anampigisha
    A-kiima
    Na-wakati
    m-kitendewa
    pig-shina
    ish-kauli ya kutendesha
    a-kiishio cha kitenzi        ½ x6=Alama 3
  13.  
    1. Kirai nomino
      Nguo aliyonunua mzazi       Alama1
    2. Kirai kivumishi
      Mwenye manyoya mengi.    Alama 1
  14. Sikukuu ya Madaraka nilikwenda Eldama-ravine, kumwona Yohana naye akasema atakuja kuniona, pamoja na mkewe Mariamu siku ya Jumapili.     6x ½ =Alama 3
  15.  
    1. Jambazi anayeishi dukani aliiba mahali pengine.
    2. Baada ya kutoka dukani, jambazi aliiba mahali pengine
    3. Kuna mtu aliyemuiba jambazi
    4. Wizi wa kawaida-Jambazi aliiba katika duka      4x1=Alama 4
  16.  
    1. f- -Kufa, mfu, kifo, mfiwa
    2. l- -mlo, chakula, mlaji       4x ½ =Alama 2

ISIMU JAMII

  1. Ni mfumo wa sauti/Ni chombo cha mawasiliano ya binadamu ambacho hutumia ishara na sauti nasibu zilizo na mpangilio maalum.    Alama 1
  2.  
    • Hakuna lugha iliyo bora kushinda zingine-zote ni sawa
    • Kila lugha ina sauti zake zilizo tofauti na zingine
    • Lugha hubadilika kutegemea mazingira aina ya tuko, wakati na watumizi wa lugha hiyo
    • Lugha ina uwezo wa kukua, kwa mfano Kiswahili kimebuni msamiati Tehama(Teknolojia ya habari na mawasiliano) kama vile tarakilishi, rununu n.k
    • Lugha pia hufa kwa msamiati wake kupotea     4x1=Alama 4
  3.  
    • Lugha ya heshima
    • Lugha ya upole
    • Matumizi ya maneno maalum-aleluya, amen
    • Ushawishi
    • Vitisho
    • Kuchanganya ndimi
    • Ukalimani
    • Kurejeleea vitabu vitakatifu
    • Nyimbo za kusifu

FASIHI SIMULIZI

  1. Fafanua Uhusiano / ubia uliopo baina ya fasihi simulizi na fasihi andishi.
    1. Fasihi zote hutumia lugha kwa ubunifu kama nyenzo ili kuwasilisha ujumbe.
    2. Fasihi zote zina vipengele vya fani na maudhui.
    3. Fasihi zote huzaliwa, huwa na hata kubadilika kulingana na wakati.
    4. Dhima kuu ya fasihi zote ni kusawiri maisha. Kioo cha jamii.
    5. Fasihi zote huzaliwa, hukua na huweza kufifia kutegemea mapito ya wakati.
    6. Fasihi zote hushughulikia maswala yanayotokana na migogoro kati ya binadamu.
    7. Tanzu za fasihi andishi zilitokana au ni vimelea /mwendelezo wa fasihi simulizi.
  2. Huku ukitoa mifano kem kem, eleza dhima zozote tano za fasihi simulizi.
    1. Huburudisha, huliwaza na kufurahisha:
      Kwa kawaida, nyingi za tanzu za fasihi za kiswahili huwasilishwa usiku au jioni kama njia ya kujiburudisha baada ya shughuli za mchana. Aidha, nyimbo za kazi huimbwa kuondolea watu uchovu wanapofanya kazi.
    2. Huhifadhi historia na utamaduni ya jamii.
      Fasihi simulizi hupokezwa kwa mdomo kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa njia hii, nyimbo na tanzu zote za fasihi simulizi huhifadhiwa katika jamii kwa kupokelezwa.
    3. Hukuza uwezo wa kufikiria/kudadisi.
      Tanzu kama hadithi, vitendawali, methali na mafumbo humhitaji binadamu kudadisi mazingira yake na kufikiri kwa makini ili kupata jawabu, suluhisho au maana inayokusudiwa
    4. Fasihi simulizi ni nguzo ya utangamano/ kuunganisha watu katika jamii.
      Uwasilishaji wa fasihi simulizi huhitaji uhusika wa watu wawili au zaidi, watu wawe pamoja katika kuimba ama kutega na kutegua vitendawili. Kule kuja pamoja hufanya watu kuhisi kama kundi moja.
    5. Hukuza uzalendo.
      Kwa kushiriki katika miviga ya jando, harusi, ibada, na matambiko, wanajamii hujitambulisha na jamii na kuionea fahari jamii yao.
    6. Hukuza ubunifu
      katika kukuza hadithi, ulumbi na malumbano, wanajamii huimarisha vipawa vya kubuni. Mtambaji bora ni yule anayeweza kuitamba hadithi upya kwa kutumia mtindo mpya.kwa njia hii ubunifu ukakuzwa.
    7. Huwasaidia wanajamii kuelewa historia ya jamii.
      Mighani, visakale, tendi na rara huonyesha historia ya jamii husika, masimulizi ya mashujaa ya jamii hiyo, huelewa katika baadhi ya vipera/tawi vya fasihi simulizi. Basi ni rekodi au kumbukumbu za matukio katika jamii.
    8. Hutambulisha jamii na tamaduni zake.
      Miviga na nyimbo husawiri imani na desturi za jamii husika, upekee huu hudhihirisha tanzu na vipera vya fasihi simulizi yake.
    9. Huongoza jamii / kuelimisha.
      Methali na ngano hutoa mwongozo kuhusu njia za kusuluhisha matatizo na zile za kukabiliana na changamoto mbalimbali maishani.
    10. Hustawisha fasihi andishi.
      Fasihi simulizi ina mchango mkubwa katika kuendeleza fasihi andishi, kwa kuwa waandishi wengi huchota na kutumia vipengele fulani vya fasihi simulizi katika uandishi wao.
      Ni kama kitega uchumi kwa wanajamii hasa walumbi, watambaji, masogora na mayeli/manju.
      Hukuza na kuziendeleza stadi za lugha. Huimarisha uwezo wa kumiliki na kuzimudu stadi za lugha kama vile kupitia vitanza ndimi, tanakali za sauti na nahau.
      5x1=Alama 5

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 3 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest