Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp
MAAGIZO
 1. Jibu maswali manne pekee.
 2. Swali la kwanza ni la lazima.
 3. Maswali hayo mengine matatu yachanguliwe kutoka sehemu tatu zilizobaki :
  Tamthilia, riwaya na ushairi.
 4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja. 

                                                                       SEHEMU A : FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1. Eleza tofauti sita baina ya fasihi Andishi na fasihi simulizi.      (alama 6)
  2. Taja aina sita tofauti za hadithi. (alama 6)
  3. Jadili sifa mbili za vitanza ndimi kwa kurejelea sauti. (alama 2)
  4. Tambua istilahi zinazotokana na maelezo.
   1. Msimulizi wa fasihi simulizi anaitwaje kwa jumla ? (alama 1)
   2. Shujaa katika mighani pia anaweza kuitwa nani ? (alama 1)
   3. Sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi fulani maalum huitwaje. (alama 1)
   4. Mavazi au vifaa vinavyotumiwa na wasanii kuakisi hali ya mambo wakati wa kuwasilisha fasihi huitwaje.       (alama 1)
   5. Mtambaji wa hadithi hutumia ujuzi gani anapoibadilisha hadithi yake moja kwa moja mbele ya hadhira bila kuathiri usimulizi wake? (alama 1)
   6. Wanaosimuliwa ili kuonyesha kazi ya fasihi simulizi hupewa jina hili. (alama 1)

                                                                     SEHEMU B: KIGOGO (Pauline Kea)

 1. Fafanua njia zozote kumi alizozitumia Majoka kuendeleza uongozi wake. (alama 20)
                                                               au
 2. Eleza nafasi ya mwanamke inavyojitokeza katika tamthilia ya kigogo. (alama 20)

                                                              SEHEMU C: CHOZI LA HERI (Assumpta K Matei)

 1.  “...liandikwalo ndilo liwalo. » Since when has man ever changed his destiny?”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Tambua mbinu tatu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.          (alama 6)
  3. Kwa kurejelea wahusika wowote watano thibitisha ukweli wa kauli hii.           (alama 5)
  4.  
   1. Eleza sifa tatu za msemewa.           (alama 3)
   2. Taja ishara mbili zilizodhihirisha kuwa yaliyoandikwa yangekuja kuwa. (alama 2)
                                                         au
 2.  
  1. Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao.            (alama 12)
   1. Ridhaa
   2. Kiriri
   3. Kaizari
   4. Neema
  2. Fafanua matatizo yaliyowakumba wahafidhina katika msitu wa mamba. (alama 8)

                                                              SEHEMU D: USHAIRI

 1. Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha uyajibu maswali yatakayofuatia.

  1. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: ulinamba:
           Moyo ………………… uushindilie,
                                        Usitamani watu!
           Lakini n’lipotazama
                                        Vyangu vinatamaniwa
           Na tena kumbe ‘tamani’ – pumzi za mlimwengu!
  2. Mama – ewe mama !
   Nakumbuka, 
   Nakumbuka kama leo : uliponamba :
             Moyo …………………..uukinaishe,
                                      Usichukuwe vya watu !
             Lakini n’lipotazama,
                                      Vyangu mimi vyaibiwa
             Na tena vyang’wapuriwa
             Na kumbe unyang’anyi – ndio uhai wa leo!
  3. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: uliponamba:
            Mwana …………………..na uwe msamehevu
                                     Kwa wanaokukosea!
   Lakini nilipotazama,
                                     Nilizidi kukosewa
   Na tena ninaonewa
   Na kumbe usamehevu – bado haujazaliwa!
  4. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: uliponamba :
           Mwana ….............. mwana nenda ukicheka,
                                    Siinunie dunia!
   Lakini nilipotazama
                                    Ni mimi n’nanuniwa
   Na kisha nabaguliwa,
   Na kumbe kicheko – sisi hatujaumbwa!
  5. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: uliponamba:
          Mwana …………….. himili, mwana himili,
                                   Himili vile mbivu
   Lakini nilipotazama,
                                   Kila siku nala mbovu
   Na kumbe uvumilivu – ni mzigo wa balaa !
   Mama mama nimeshamaiza;
   Nimetambua ya kwamba
                  Tamani imezaliwa; itaishi nasi
                  Moyo unoelemewa, haukinashuki
                                   Kwani inanajisiwa!
   Dunia si samehevu; na hajapata hiyo kuwa :
   Mama, na kwamba:
                                   Kuna wanolia, katika wanaocheka
   Basi – siwezi, katu siwezi – wasia kushika!

                                                                                  MASWALI

 1. Toa kichwa mwafaka cha shairi hili. (alama 2)
 2. Zungumzia uhusika katika shairi hili huku ukionyesha maoni ya kila mhusika. (alama 4)
 3. Kwa kusoma shairi hili, sauti gani inayosikika dhahiri na sauti gani iliyojificha?   (alama 2)
 4. Zungumzia dhima/ kazi ya ubeti wa mwisho wa shairi hili hasa ukigusia maana na falsafa ya mshairi. (alama 2)
 5. Ni mbinu gani kuu ya lugha inayotawala katika shairi hili. (alama 2)
 6. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
 7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili; (alama 4)
  1. Uushindilie
  2. Uukinaishe
  3. Msamehevu
  4. Siinunie
                                       au
 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  1. Pupa litakupa ndwele, tamaa si kitu chema,
   Kutaka huku na kule, huwa hapana salama,
   Ni kweli tama mbele, mauti yako kwa nyuma,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola,

  2. Ukinai kwa kadiri, alichokupa Karima,
   Kwani kwakoni hatari, mambo usipoyapima,
   Ikiwa ni wa shubiri, asali hupati pima,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola
  3. Halifai lako pupa, kupapia darahima,
   Kwani mengi atatupa, na kupoteza heshima,
   Mungu akitaka kupa, tamaa si lazima,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola
  4. Fuata wako mwenendo, watokea hizo zama,
   Usishike lako pendo, moyo unavyokutumia,
   Kwa kuandama magendo, siku moja waja kwama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

  5. Ukiitaka sahali, upate vyema kuchuma,
   Utosheke kwa kalili, sitake dunia nzima,
   Shika moja si wawili, kisha la pili andama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

  6. Ilokweli nakwambia, sahibu ninayosema,
   Sikia tena sikia, fuata yangu kalima,
   Tamaa ya kupapia, mwisho vitakusakama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

  7. Hapana nilipofika, ndipo pangu  kaditama,
   Na sasa inavyotaka, sote ni kufanya hima,
   Tamaa kuiyepuka, isitufike lawama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

MASWALI

 1. Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
 2. Andika methali zozote tatu zimedokezwa katika shairi hili. (alama 3)
 3.  
  1. Eleza kwa tafsili uzingativu wa arudhi katika ubeti wa tatu kwa upande wa mizani na vina. (alama3)
  2. Uhuru wa kishairi unamruhusu mshairi kutumia lugha pasipo kujali sarufi. Ukizingatia msamiati na sarufi fafanua kauli hii kutokana na ubeti wa nne na wa tano. (alama 4)
 4. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
 5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi hili. (alama 4)
  1. Ndwele
  2. Ukinai
  3. Darahima
  4. Kalili

MWONGOZO

 1. FASIHI SIMULIZI
  1. Eleza tofauti sita baina ya fasihi Andishi na fasihi simulizi. (alama 6)

    Fasihi Andishi  Fasihi simulizi
    Huwasilishwa kwa mwandishi  Huwaslilishwa kwa mdomo
    Huhifadhiwa maandishini Huhifadhiwa akilini 
    Ni mali ya mtu binafsi  Ni mali ya jamii 
    Inahadhira tuli  Inahadhira tendishai
    Ni ya majuzi  Ni kongwe zaidi 
    Hugharimu pesa  Haigharimu chochote
  2. Taja aina sita tofauti za hadithi. (alama 6)
   • Hurafa                            
   • hekaya
   • Visaili
   • Visakale
   • Hadithi za usuli
   • Hadithi za mazimiwi
   • Mighani
   • Hadithi za mtanziko
   • Soga
   • Kumbukumbu
   • Hadithi za kichimbakazi
   • Tarihi
   • Hadithi za kimafumbo
  3. Jadili sifa mbili za vitanza ndimi kwa kurejelea sauti. (alama 2)
   • Vitanza ndimi huhusisisha maneno yenye sauti zinazokaribiana kimatamsho.
   • Huhisisha suati zinazotatiza kutamka.
   • Huwa ni mchezo wa sauti ili kuimarisha matamshi.
  4. Tambua istilahi zinazotokana na maelezo.
   1. Msimulizi wa fasihi simulizi anaitwaje kwa jumla ? (alama 1)
    • Mtambaji/Fanani
   2. Shujaa katika mighani pia anaweza kuitwa nani ? (alama 1)
    • Jagina/Nguli
   3. Sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi fulani maalum huitwaje. (alama 1)

    • Miviga
   4. Mavazi au vifaa vinavyotumiwa na wasanii kuakisi hali ya mambo wakati wa kuwasilisha fasihi huitwaje. (alama 1)

    • Maleba
   5. Mtambaji wa hadithi hutumia ujuzi gani anapoibadilisha hadithi yake moja kwa moja mbele ya hadhira bila kuathiri usimulizi wake? (alama 1)

    • Ufaraguzi
   6. Wanaosimuliwa ili kuonyesha kazi ya fasihi simulizi hupewa jina hili. (alama 1)

    • Hadhira

KIGOGO (Pauline Kea)

 1. Fafanua njia zozote kumi alizozitumia Majoka kuendeleza uongozi wake. (alama 20)
  1. Kuwaua wapinzani k.m Jabali.
  2. Kuwajeruhi wapinzani k.m Turu alivunjwa mguu
  3. Kutumia akari kuwafurusha waandamanaji
  4. Kuwaua waandamanaji k.m vijana watano wafanyakazi wa Majoka na Majoka company.
  5. Kufunga vyombo vya habari k.m Mzalendo.
  6. Kupiga marufuku vyama vya upinzani k.m Mwege cha Jabali
  7. Wizi wa kura k.m Majoka alisema iwapo Tunu angepata kura nyingi, Majoka angetawala
  8. Kutumia propaganda k.m kuenez ahabari za uongo kuhusu wapinzani
  9. Kutoa ahadi za uongo kuangamiza upinzani k.m Sudi anaahidiwa ziara ughaibuni pamoja na familia iwapo atachonga kinago cha ngao.
  10. Kutumia ukabila/tenga utawale - kutisghia makabila yasiyomuunga mkono Majoka k.m Akina Kombe wanaonywa wahame.
  11. Kutumia mapendeleo k.m Asiya(mamapima) anaruhusiwa kuunda pombe haramu na kupewa kandarasi kukoka keki ya uhuru kwa sababu anamuunga mkono Majoka.
 2. Eleza nafasi ya mwanamke inavyojitokeza katika tamthilia ya kigogo. (alama 20)
  1. Mwanamke ni chombo ch akukidhia mahitaji ya mwanaume k.m Majoka anamrai Ashua kumtimizia haja za kimapenzi.
  2. Mwanamke ni msaidizi wa mume k.m Ashua anuza chai na mahamri ili kumsaidia Sudi kupata riziki.
  3. Mwanamke ni mshiriki wa ufisadi k.m Asiya anapata kandarasi ya kuoka keki kwa sababu Ngurumo rafikiyo anajuana na Husda mkewe Majoka.
  4. Mwanamke anachukuliwa kama kiumbe duni katika jamii k.m Majoka anasema 'mwanamke ni mwamanmke tu' wakati wa mgogoro wa Husda na Ashua.
  5. Mwanamke ni msomi k.m Tunu amesoma hadi akapata uzanifu  katika uanasheria , Ashua amesomea ualimu.
  6. Mwanamke ni mwenye wivu k.m Husda anamgombeza Ashua kwa sababu anadhani kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mumewe Majoka.
  7. Mwanamke ni mwenye jicho la nje k.m Husada anaonekana kujipendekeza kwa Chopi. Pia asiya ni mpenziwe Ngurumo.
  8. Mwanamke ni mtiifu k.m Siti anatii anapoambiwa na Tunu awapeleke watoto wa Sudi kwa mamake Hashima wapewe chakula.
  9. Mwanamke ni mzinduzi k.m Tunu anaamsha ari ya wanasagamoyo kupigania haki zao.
  10. Mwanake ni mwanaharakati wa kupigania haki k.m Tunu anawaongoza Wanasagamoyo kuuondolea mbali uongozi dhalimu wa Majoka.
  11. Mwankamke ni mwenye kipawa cha kuongoza k.m Tunu anachukua hatamu za uongozi kutoka kwa Majoka anayeng'atuliwa.

CHOZI LA HERI

 1. “...liandikwalo ndilo liwalo. » Since when has man ever changed his destiny?”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 

   • Haya ni amaneno ya mwanishi akionyesha mawazo ya Ridhaa, akikumbuka maneno ya mkewe Terry akimkejeli Ridhaa kwa kuamini ya kishirikina
  2. Tambua mbinu tatu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 6)
   1. Methali - liandikwalo ndilo liwalo
   2. Kuchangaya/kuhamisha ndimi - Since when has man ever changed his destiny?
   3. Swali la balagha - Since when has man ever changed his destiny?
  3. Kwa kurejelea wahusika wowote watano thibitisha ukweli wa kauli hii. (alama 5)

   1. Lunga - alipoteza kazi yake ya afisa wa kilimo na pia shamba lake na mkewe
   2. Umidkheri beck na mwaliko walimpoteza baba na mma ayo.
   3. Mwegemi na Neema wakikosa watoto wao wa kuzaa.
   4. Kaizari alishuhudia bintiza mnwanaheri na Lime wakikabwa.
   5. Bi. Kangara na Sauna waliweza kutiwa mbaroni kwa kuhusika na ulanguzi wa watoto.
  4.  
   1. Eleza sifa tatu za msemewa. (alama 3)
    • Msemewa ni ridhaa
    • Mwenye utu - Aliwaajiri Kaizri na Selume katika kituo chake cha afya.
    • Mvumilivu - Alivumilia matatizo mengi k.m kuchomewa jumba na familia yake.
    • Msomi - alisomea taaluma ya kuhusudiwa ya utabibu
   2. Taja ishara mbili zilizodhihirisha kuwa yaliyoandikwa yangekuja kuwa. (alama 2)
    • Kupepesa kwa jicho lake la kulia kwa wiki mbili mtawalia
    • Anguko ambalo Ridhaa sebuleni mwake
    • Mavune yaliyomwandama mwili wake na kunyongonyeza kwa muda bila sababu maalum.
    • Jeshi la kunguru liliotua juu ya paa la maktaba ya Ridhaa ya nyumbani adhuhuri ya juzi ile.
    • Mlio wa kereng'ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya mkasa.
 2.  
  1. Eleza sifa na umuhimu wa wahusika wafuatao. (alama 12)
   1. Ridhaa
    Sifa
    • Msomi - alisoma hata akawa tabibu
    • Mvumilivu - alistahimili shida nyingi.
    • Mwenye utu - aliwapa watu maji na huduma za afya.
     Umuhimu
    • Ni kielezo cha watu wenye utu katika jamii
    • Anawakilisha watu wenye moyo imara wasiokata tamaa hata baada ya kuzongwa na matatizo mengi
   2. Kiriri
    Sifa
    • Mvumilivu - alistahimikli hali ya kuachwa na mkewe na wanawe
    • Karimu - anampat Kang'ata (babake Lunga) shamba alime na aishi humo.
     Umuhimu
    • Ni kielelezo cha watu wanaojali maslahi ya watu wenye uhitaji/maksini
   3. Kaizari
    Sifa
    • Mstahimilivu - anavumilia kushuhudia binitize wakibakwa.
    • Mwenye mapuuza - Alipuuza hali ya mkewe Subira kukandamizwa na aila yake.
    • Mwenye bidii - alitia juhudu katika kazi aliyopewa na Ridhaa katika kituo cha afya.
     Umuhimu
    • Ni mfano wa watu wenye mapuuza amabao hawana dharura ya kutatua shida kabla haijapita mipaka.
   4. Neema
    Sifa
    • Mvumilivu - alikaaa kwa muda mrefu bila mwana
    • Mwenye mapuuza - alipuuza kumlea mwana aliyemwokota
    • Mlezi mwema - alimlea Mwaliko vyema japo hakumzaa.
     Umuhimu
    • Ni kielelezo cha cha watu wenye nia njema kwa wengine na wanaojali maslahi yao.

  2. Fafanua matatizo yaliyowakumba wahafidhina katika msitu wa mamba. (alama 8)
   1. Ukosefu wa maji safi ya kunywa
   2. Msongamano wa watu kambini
   3. Kuzuka kwa magojwa hatari kama kipindupindu, homa ya matumbo n.k
   4. Ukosefu wa chakula 
   5. Ukosefu wa huduma za afya
   6. Ukosefu wa shule za watoto kusomea
   7. Ukosefu wa vyuo
   8. Ukosefu wa kazi na pesa
   9. Usumbufu wa kiakili wa waathiriwa
 3. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  1. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: ulinamba:
           Moyo ………………… uushindilie,
                                        Usitamani watu!
           Lakini n’lipotazama
                                        Vyangu vinatamaniwa
           Na tena kumbe ‘tamani’ – pumzi za mlimwengu!
  2. Mama – ewe mama !
   Nakumbuka, 
   Nakumbuka kama leo : uliponamba :
             Moyo …………………..uukinaishe,
                                      Usichukuwe vya watu !
             Lakini n’lipotazama,
                                      Vyangu mimi vyaibiwa
             Na tena vyang’wapuriwa
             Na kumbe unyang’anyi – ndio uhai wa leo!
  3. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: uliponamba:
            Mwana …………………..na uwe msamehevu
                                     Kwa wanaokukosea!
   Lakini nilipotazama,
                                     Nilizidi kukosewa
   Na tena ninaonewa
   Na kumbe usamehevu – bado haujazaliwa!
  4. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: uliponamba :
           Mwana ….............. mwana nenda ukicheka,
                                    Siinunie dunia!
   Lakini nilipotazama
                                    Ni mimi n’nanuniwa
   Na kisha nabaguliwa,
   Na kumbe kicheko – sisi hatujaumbwa!
  5. Mama – ewe mama!
   Nakumbuka,
   Nakumbuka kama leo: uliponamba:
          Mwana …………….. himili, mwana himili,
                                   Himili vile mbivu
   Lakini nilipotazama,
                                   Kila siku nala mbovu
   Na kumbe uvumilivu – ni mzigo wa balaa !
   Mama mama nimeshamaiza;
   Nimetambua ya kwamba
                  Tamani imezaliwa; itaishi nasi
                  Moyo unoelemewa, haukinashuki
                                   Kwani inanajisiwa!
   Dunia si samehevu; na hajapata hiyo kuwa :
   Mama, na kwamba:
                                   Kuna wanolia, katika wanaocheka
   Basi – siwezi, katu siwezi – wasia kushika!

                                                         MASWALI
   1. Toa kichwa mwafaka cha shairi hili. (alama 2)
    • Wasia/mawaidha/ushauri
   2. Zungumzia uhusika katika shairi hili huku ukionyesha maoni ya kila mhusika. (alama 4)
    1. Mama
     • Mama alimwambia mwana kufanya haya - asitamani vya watu/ aukanishe moyo wake/awe msamehevu/awe mvumilivu na atakula mbivu.
    2. Mwana alimjibu
     • Tamani ni pumzi ya ulimwengu
     • Uvumilivu ni mzigo wa balaa
     • Unyanganifu ndio uhalifu wa ulimwengu
     • Duni si samehevu
     • Usamehevu bado haujazaliwa
     • Kicheko bado sisi hatujaambiwa
     • Mwana alikataa kushika wasia 
   3. Kwa kusoma shairi hili, sauti gani inayosikika dhahiri na sauti gani iliyojificha? (alama 2)
    • Sauti ya mwana yasikika na ya mama imefichika.
   4. Zungumzia dhima/ kazi ya ubeti wa mwisho wa shairi hili hasa ukigusia maana na falsafa ya mshairi. (alama 2)
    • Mshairi ameshatambua na kufahamu kwamba tamaa imetawala na itadumu nasi/moyo unapolemewa na tamaa haijizuii kutenda maovu kwa sababu umeathirika/ Hakuna msamaha duniani na usamehevu haupatikani duniani miongoni mwa watu.
   5. Mbinu gani kuu ya lugha inayotawala katika shairi hili. (alama 2)
    • takriri
   6. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
    • Ewe mama ninakumbuka ulioniambia kama ni leo. Umeniambia mtoto unafaa kua msamehevu kwa wale waliokukosea. Nilipoangalia nilizidi kukosewa na kuonewa. Kweli usamehevu haupo.
   7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili; (alama 4)
    1. Uushindilie 
     • Uzuie/ukanye
    2. Uukinaishe
     • Ujitosheleze/utosheke
    3. Msamehevu
     • Unayeweza kuachia wanaokukosea
    4. Siinunie
     • Usiichukie
 4. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  1. Pupa litakupa ndwele, tamaa si kitu chema,
   Kutaka huku na kule, huwa hapana salama,
   Ni kweli tama mbele, mauti yako kwa nyuma,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola,

  2. Ukinai kwa kadiri, alichokupa Karima,
   Kwani kwakoni hatari, mambo usipoyapima,
   Ikiwa ni wa shubiri, asali hupati pima,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola
  3. Halifai lako pupa, kupapia darahima,

   Kwani mengi atatupa, na kupoteza heshima,
   Mungu akitaka kupa, tamaa si lazima,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola
  4. Fuata wako mwenendo, watokea hizo zama,
   Usishike lako pendo, moyo unavyokutumia,
   Kwa kuandama magendo, siku moja waja kwama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

  5. Ukiitaka sahali, upate vyema kuchuma,
   Utosheke kwa kalili, sitake dunia nzima,
   Shika moja si wawili, kisha la pili andama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

  6. Ilokweli nakwambia, sahibu ninayosema,
   Sikia tena sikia, fuata yangu kalima,
   Tamaa ya kupapia, mwisho vitakusakama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

  7. Hapana nilipofika, ndipo pangu  kaditama,
   Na sasa inavyotaka, sote ni kufanya hima,
   Tamaa kuiyepuka, isitufike lawama,
   Tosheka na chako kima, ulichopewa na Mola

                  MASWALI
   1. Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)
    • Tuepukane na tamm na tutosheke na kile tulicho nacho 
   2. Andika methali zozote tatu zimedokezwa katika shairi hili. (alama 3)
    • Tamaa mbele mauti nyuma
    • Njia mbili zilimshinda fisi
    • Mfauta mawili moja humponyoka watatu
    1.  Eleza kwa tafsili uzingativu wa arudhi katika ubeti kila mshororo wa tatu kwa upande wa mizani na vina. (alama3)
     • Mizani 8 - 8 = 16 
      pa – ma
      pa – ma
      pa – ma
      pa – la
    2. Uhuru wa kishairi unamruhusu mshairi kutumia lugha pasipo kujali sarufi. Ukizingatia msamiati na sarufi fafanua kauli hii kutokana na ubeti wa nne na wa tano. (alama 4)
     • Kubananga sarufi - fuata wako mwendo, badala ya ku fuata mwenendo wako.
     • Inkisari (kufupisha) - siatake badala ya usitake
     • Mazida (kurefusha) ukiitaka badala ya ukitaka
   3. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
    • Endelea na tabia zako tabia zako tangu zamani na wala usifwate kile moyo wako unachotamani. Ukiendelea kufanya magendo, siku moja utajuta/utaumia/utapoteza/utafariki. Tosheka na kiasi hicho uilichopewa na Mungu.
   4. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi hili. (alama 4)
    1. Ndwele
     • Maradhi/ugonjwa/magonjwa
    2. Ukinai
     • Utosheke/uridhike
    3. Darahima
     • Fedha/pesa/faranga/darahimu/ngwenje/njenje/ganji
    4. Kalili
     • Kidogo/kichache 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2023.

Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest