Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 3 Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
  • Kisha chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400
  • Kila insha ina alama 20
  • Karatasi hii ina kurasa 2. Matahiniwa ni lazima aangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo
  1. SWALI LA LAZIMA.
    Visa vya dhuluma dhidi ya mtoto wa kike vimeongezeka sana nchini.Andika taarifa ya hali hii nchini.
  2. Uhifadhi wa mazingira una manufaa mengi kwa binadamu .Thibitisha.
  3. Kutangulia si kufika.
  4. Malizia kwa………tulifukumana huku nyuso zetu zikiwa na tabasamu la matumaini.

 

 

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1.  
    • Hii ni taaarifa
    • Ipewe kichwa/anwani inayotaja mada
    • Utangulizi unaoafikiana na mada utolewe.
    • Taarifa iandikwe kwa kuripoti.
    • Mawazo yawasilishwe kwa aya mbalimbali na kwa kuzingatia kanuni za uandishi k.v. mtiririko,msamiati,sarufi.
      HOJA
    • Ukeketaji wa mtoto wa kike/kupasha tohara.
    • Ubakaji.
    • Ndoa za lazima.
    • Ndoa za mapema.
    • Ajira –vijakazi.
    • Kunyimwa elimu.
  2. Manufaa ya uhifadhi mazingira
    • Kuwepo kwa miti - Ivutayo mvua.
                                  - Ipayo chakula ,dawa.n.k.
                                  - Hutupa mbao za ujenzi.
    • Tabaka la Ozoni likihifadhiwa tutakingwa dhidi ya miale ya jua isababishayo kansa ya ngozi.n.k.
    • Binadamu atakuwa na afya nzuri kutokana na hewa safi yenye oksjeni.
    • Uhifadhi wa misitu utazuia maporomoko ya ardhi yasababishayo vifo na uharibifu mkubwa.
    • Misitu pia itasaidia kuzuia gharika iletayo maafa.
    • Wanyama na mimea itakua bila matatizo yatokanayo na kemikali hatari na takataka nyingine.
    • Mito na maziwa na maji safi.
  3. Hili ni swali la methali
    • Mtahiniwa si lazima aeleze maana ya methali .
    • Mtahiniwa aanze na kisa moja kwa moja .
    • Dhana ya kutangulia ieleweke vizuri katika kisa chake.
    • Aonyeshe sehemu hizo mbili.
      1. Kutangulia kwa maana ya mafanikio maishani –utajiri, elimu na nyanja zingine za maisha.
      2. Si kufika
        Utajiri kuishi na wengine kuibuka matajiri au kupitwa na wengine katika uwanja wa maisha.
        1. Mwanafunzi achukue msimamo yaani kuunga mkono methali kwani kila methali ni ukweli usiopingika.
        2. Mwanafunze aepuke msamiati wa paukwa pakawa ambacho ni kipengele cha fasihi simulizi.
  4. Hii ni insha ya mdokezo
    Mwanafunzi atunge kisa ambapo yeye na wenzake wanahudhuria mkutano /kikao cha kutatua shida fulani inayowakamba mfano ukosefu wa usalama,ukosefu wa ajira,n.k. ambapo swala lao linashughulikiwa au ahadi kutolewa na wahusika wanaosikiliza kilio chao.

    Nafsi tajwa izingatiwe haswa nafsi ya kwanza wingi(sisi)(tu-)
    Atakayemalizia kwa maneno mengine tofauti na yaliyo kwenye swali,atakuwa amejitungia swali lake na hivyo amepotoka.Atuzwe bakshishi. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 3 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest