Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA

 • Jibu maswali manne pekee
 • Swali la kwanza ni la lazima
 • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki ; yaani : riwaya, Tamthlia, hadithi fupi na ushairi.
 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

       SEHEMU YA A: LAZIMA:FASIHI SIMULIZI

 1. Soma kisa kifutacho kasha ujibu maswali
  Hapo zamani za kale paliishi mtoto katika kisima kimoja. Siku moja, mtoto aliokota kijiwe karibu na soko kuu. Kijiwe kilikuwa kikimeremeta kwa rangi mbalimbali na kuzingirwa na pete ya dhahabu.

  Mtoto huyo na wenzake walianza kurushiana kijiwe hicho. Baada ya muda kikaanza kuongezeka umbo na kuonekana kama kiwiwili cha binadamu. Kikaanza kuwakimbiza wale watoto wawili. Kutokana na ukelele wao, watu walikuja kutazama ni nini kilikuwa cha mno. Walipofika walikutana ana kwa ana na dubwana hilo. Lilizidi kuongeza kwa umbo na likawameza wote pamoja na mifugo wao. Wachache waliojaribu kukimbia liliwashika kwa mikono yake mirefu na mipana. Kwa bahati njema kulikuwa na mama mmoja aliyeyaona hayo yote. Alikuwa mbali kiasi na hapo. Aliteremka kutoka kilele cha mlima na kuwapata wakulima makondeni na sawia akawajuza kuhusu kilichomwogofya sana. Wote wakaacha shughuli zao na wakatwaa silaha zao wakaelekea soko kuu.

  Dude sasa lilikuwa limejilaza baada ya shibe. Wakulima wale waliwachagua watu sita ambao walijulikana kwa ushujaa wao. Pamoja walilinyemelea lile nyangarika na kulikata mara moja. Lilitoa mkoromo mkuu kabla halijakata kamba. Punde, wanakijiji kwa uangalifu mkubwa walitoboa tumbo lake wakitarajia kupata maiti za wapenzi wao. Wote walijawa na furaha kuu walipoona wapenzi wao wakichomoza kutoka tumboni, mmoja baada ya mwingine hadi akatoka yule wa mwisho. Mbuzi, kondoo na ng’ombe wote walitoka mmoja mmoja.

  Siku hiyo kuliandaliwa sherehe kuu ya kumshukuru muumba kwa wema wake. Watoto wakashauriwa wasithubutu kuchezea vitu wasivyojua. Hadithi yangu inaishia hapo.
  1. Bainisha kipera cha utungo huu. (alama. 1)
  2. Fafanua sababu nne za kuthibitisha jibu lako. (alama 4)
  3. Eleza manufaa manne ambayo jamii itapata kwa kurithisha kipera hiki kwa jamii. (alama 4)
  4. Bainisha shughuli mbili za kiuchumi zinazoendelezwa na jamii inayosawiliwa na utungo huu (alama 2)
  5. Bainisha mbinu za kimtindo ambazo msimulizi ametumia kufanikisha ujumbe wake. (alama 4)
  6. Kipera hiki kimeanza kudidimia kutoka kwa jamii yako. Eleza hatua tano ambazo utashauri jamii yako ichukue ili kudumisha kuwepo wake katika jamii. (alama. 5)

   SEHEMU YA B: USHAIRI
 2. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
  Wasiwasi n’ondokeya, ondoka enenda zako,
  Ondoka andama ndiya, n’ondosheya uso wako,
  Ondoka!wanisikiya? ziwate jeuri zako,
  Jishughulishe na yako, yangu wayatakiani?

  Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
  Haisatahimiliki, uwovu umekithiri,
  Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri
  Siitaki yako shari, enda zako wasiwasi

  Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
  Viumbe na zao nyoyo, vitwa kuwagotanisha,
  Hiino ndiyo kaziyo, yenye kukufurahisha,
  Ni kazi isokuchosha, mno umeizoweya.

  Tukaapo wanambia, hayawi niyatakayo,
  Kwamba tamaa ngatiya, nasumbuwa wangu moyo,
  Kwamba hata ningojeya, hayo niyangojeyayo,
  Ng’o siyapati hayo, ni bure najisumbuwa.

  Mara waja na bahari,mambo yalivyo nyumbani,
  Ati mambo si mazuri, mambo yote tafashani,
  Wanitaka nifikiri,usemayo ni ya yakini,
  Nisononeke moyoni, upate kufurahika.

  Au mara unijiya, na kingine kisahani,
  Kukhusu zao afiya,hao waliyo nyumbani,
  Huwa hwishi kunambiya, hali zao taabani,
  Zingawa; watakiyani? Ni zako au ni zao?

  Na mara huja nambiya, nitakapotoka humu,
  Ya kwamba yaningojeya, nde maisha agumu,
  Ulilonikusudiya, ni kunitiya wazimu?
  Kama ndiyo yako hamu, basi ushatahayari

  Huo urafiki wako, wa kuja niungulisha,
  Kunipa masikitiko, na mateso yasokwisha,
  Kutoka leo ni mwiko, sitautaka maisha,
  Kamwe hutanikondesha, tokomeya mwanakwenda.                (Abdilatif Abdala, 1971)
  Maswali
  1. Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 3)
  2. Taja na ueleze umuhimu wa aina ya urudiaji katika shairi hili. (alama 2)
  3. Bainisha aina zifutazo za idhini za kishairi katika shairi hili (alama 4)
   Inksari
   Lahaja
   Mazda
   Kubananga sarufi
  4. Eleza namna sheria za kiarudhi zimetumiwa kuboresha ubeti wa kwanza wa shairi hili (alama. 4)
  5. Bainisha nafsinenewa wa shairi hili. (alama 2)
  6. Eleza toni katika shairi hili. (alama 1)
  7. Andika ubeti wa mwisho katika lugha nathari. (alama 4)

   SEHEMU YA C: NGUU ZA JADI: JIBU SWALI LA 3 AU 4
 3. Bainisha nguu mbalimbali zilizotinga maendeleo ya nchi ya Matuo kulingana na riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 20)
 4. ‘‘Mrima, dunia yote inajua aliyemsaliti Yesu Kristo. Unajua mtu huyo aliishia wapi?
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
  2. Tambua mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Fafanua namna wahusika walivyowaendea kinyume wenzao katika riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 12)

   SEHEMU YA D: BEMBEA YA MAISHA: JIBU SWALI LA 5 AU 6
 5. ‘‘Japo nilipungukiwa na mengi niliyotamani, nilitaka nyinyi muote mbawa mpae juu na kuitazama dunia kutoka kule juu kwa niaba yangu. Stahamala yangu haikuniletea hasara...’’
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
  2. Bainisha toni inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
  3. Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili (alama 8)
  4. Onyesha namna stahamala ya msemaji ilimletea manufaa (alama 6)
 6. ‘‘....Mara ile ya kuzuka, ulikuwa kimbaumbau mwiko wa pilau. Upepo kidogo tu ungekuyumbisha kama jani kavu wakati wa kipupwe.’’
  1. Tambua mbinu nne za kimtindo katika dondoo hili (alama 4 )
  2. Onyesha namna wahusika mbalimbali walivyoyumbishwa na hali tofauti katika tamthilia (alama 10)
  3. Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kukuza : (alama 6)
   1. ploti
   2. wahusika wengine

    SEHEMU YA E: MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE: JIBU SWALI LA 7 AU 8
 7. Fafanua namna ukiukaji wa haki umeendelezwa katika hadithi zifuatazo (alama 20)
  1. Fadhila za Punda
  2. Sabina
  3. Kifo cha Suluhu
  4. Nipe Nafasi
   Pupa: F.M. Kagwa
 8.  
  1. “Pupa imenitumbukiza kwenye kisima nilichochimba, sasa naingia mwenyewe …”
   1. Bainisha mbinu za kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
   2. Huku ukitolea mifano mwafaka, onyesha ukweli wa kauli hii. (alama 8)
    Kila Mchezea Wembe: Pauline Kea Kyovi
  2. “Dunia hii nayo kubwa, anasa zake nyingi huwezi kuzimaliza”
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   2. Fafanua toni katika dondoo hili. (alama 2)
   3. Jadili namna ambavyo anasa imejitokeza katika hadithi hii. (alama 4)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. SWALI 
  1. Ngano za mazimwi (1x1=1)
  2.  
   • Kuna mhusika zimwi
   • zimwi linawakilisha sifa hasi za binadamu km ukatili
   • imejaa uharibifu; kula watu na mifugo
   • matumizi mengi ya fantasia; watu na mifugo kumezwa na kutoka wangali hai
   • Kipengele cha safari hujitokeza k.v. mwanamke mmoja -kwenda kutafuta suluhisho.
   • Ushindi kujitokeza;zimwi kushindwa/ kuuawa
   • zimwi huwa na sifa zinazokiuka mipaka ya binadamu k.m. mikono mirefu na mipana  (za kwanza 4x1=4)
  3. Manufaa manne ambayo jamii itapata kwa kurithisha kipera hiki kwa jamii.
   Umuhimu
   • Jamii itajifunza Kukashifu tabia ya uovu, ulafi, na ukatili.
   • Jamiiitaburudika kutokana na masimulizi
   • Kutia moyo waliodhulumiwa kuwa waliowanyanyasa wataadhibiwa siku moja.
   • Huwafunza watoto kuwa watiifu na kuzingatia makanyo wanayopewa ili waepuke madhara.  (za kwanza 4 x 1=4))
  4.  
   • ukulima; wakulima walikuwa makondeni
   • ufugaji; zimwi lilimeza mifugo (2 x 1=2)
  5.  
   • nahau; ana kwa ana, halijakata Kamba
   • chuku; zimwi kumeza watu na mifugo kadhaa
   • kinaya; watu na mifugo kutoka tumboni mwa zimwi wakiwa hai
   • uhaishaji; kijiwa kuanza kuwakimbiza Watoto
   • taswira oni; walipoona wapenzi wao..
   • taswira mwendo; .wakichomoza kutoka tumboni..   (4x1=4)
  6.  
   • Kuendelea kufundisha kipera hiki shuleni
   • Kuihifadhi ili vizazi vijavyo viweze kuifahamu mfano kwa kurekodi
   • Kuifanya utafiti wa kina
   • Kuionyesha kwenye vyombo vya habari kama runinga.
   • Kusisitiza uendelezwaji wake katika mashindano ya shule
   • kuitia katika maandishi   (5x1=. 5)
 2. SWALI
  1.  
   • Ondoka ujishughulishe na mambo yako
   • Urafiki usio na manufaa si mzuri
   • Rafiki ana uvivu na kukosanisha watu
   • Rafiki anavunja watu moyo
   • Rafiki muongo    (3x1=3)
  2. urudiaji wa neno; ondoka; kusisitiza ujumbe (1x2=2)
  3.  
   • inkisari; n’ondokeya-niondokee, yasokwisha- yasiyokwisha
   • lahaja; ndiya- njia, ziwate-ziwache n.k
   • mazda; enenda-enda
   • kubananga sarufi; viumbe na zao nyoyo-viumbe na nyoyo zao    (4x1=4)
  4.  
   • Umepangwa katika mishororo (minne)
   • mishororo imegawika katika vipande (viwili)
   • vina vya kati (ya) na vya mwisho (ko)
   • urari wa mizani( 8 kila kipande, 16 kila mshororo)   (4x1=4)
  5. Mtu aliyechoshwa na rafikiye; kutoka leo ni mwiko, sitautaka maisha (1x2=2)
  6. malalamiko; wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri (1x1=1)
  7. Huo urafiki wako ambao utanidhuru na kunipa matatizo daima nimeukatiza leo na sitakubali unipe taabu kwa hivyo enda zako. (4x1=4)
 3. SWALI 
  Nguu mbalimbali :
  1. Mila zilizowanyima wanawake uhuru wa kujichagulia wachumba.
  2. Mila zilimzuia mwanamume kutunzwa na mkewe.
  3. Mifumo ya uongozi mbaya inayosababisha ufisadi;
  4. Mila ziliwanyimawanawake nafasi ya kusema mbele ya umati;
  5. Chuki za kikabila kati ya waketwa na wakule
  6. Utabaka ulishamiri katika nchi ya Matuo
  7. Wanaume kujiingiza katika matumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya
  8. Mifumo wa ubabedume /taasubi ya kiume inayodhalilisha wanawake na watoto wa kike.
  9. Mila zinazomnyima mtoto wa kiume nafasi ya kujiendeleza.
  10. Umaskini uliokithiri
  11. Mwanamake kutotafuta mumewe akienda kujistarehesha.
  12. Waketwa kunyimwa nafasi za uongozi;
  13. Mwanamke hakuruhusiwa kumwuliza mumewe alikotoka.
  14. Mwanamke alitarajiwa kumtegemea mumewe kwa kila hali.
  15. Watoto wa kitajiri kuwa wavivu na kutofanya kazi
  16. Mwanamke hakupata nafasi ya kujiendeleza kielimu
  17. Vijana walitumbukia kwenye ukware kutokana na ulevi;
  18. Mtoto hakutarajiwa kuping maovu ya baba yake;
  19. Desturi ya kuhodhi mali na kujilimbikizia pesa
  20. Desturi ya mali kumilikiwa na wachache
  21. Wingi wa maisha ya raha na starehe ni desturi ya wanamatuo.
  22. Wanaume wana desturi ya kukosa adabu wanapowanyemelea wake za watu.
  23. Desturi ya ukiukaji wa haki za Watoto;
  24. Ukosefu wa uaminifu katika ndoa.
  25. Viongozi kuunda hila/njama za kisiasa;   (za kwanza 20x1=20)
 4. SWALI 
  ‘‘Mrima, dunia yote inajua aliyemsaliti Yesu Kristo. Unajua mtu huyo aliishia wapi?
  1. uk 114 Maneno ya Sagura kwa Mrima nyumbani kwa Mrima. Alikuwa akimkejeli Mrima kwa kupokea bahasha yenye pesa za kumhonga ili kumsaidia Sagilu na Mtemi Lesulia kwenye kampeni zao. (4x1 =4)
  2.  
   • Tarihi / tadmini ; aliyemsaliti Yesu Kristo
   • balagha; unajua mtuhuyo aliishia wapi?
   • Utohozi; Yesu Kristo-Jesus Christ   (2x2=4)
  3. wahusika walivyowaendea kinyume wenzao
   1. Chifu Mshabaha anaisaliti jamii ya Waketwa kwa kushiriki katika njama ya kuwaondoa kutoka katika makao yao (uk. 55).
   2. Chifu anamsaliti Mangwasha anapompa Mrima bahasha ya pesa kama hongo ya kuendesha kampeni za Mtemi Lesulia (uk. 110), kinyume na matakwa ya jamii yake.
   3. Chifu Mshabaha pale anapomsaliti Mangwasha kwa kumleta msichana mwingine kazini kwake ili kumfuta yeye kazi (uk. 135).
   4. Nanzia anamsaliti Mtemi Lesulia kwa kushiriki mapenzi nje ya ndoa na Sagilu na mhindi
   5. Sagilu anamsaliti mwanawe Mashauri kwa kuhusika kimapenzi na Cheiya, mpenziwe Mashauri.
   6. Sagilu anasaliti mila na utamaduni, anajihusisha kimapenzi na wasichana wadogo, anajihusisha na mpenzi wa mwanawe.
   7. Mashauri anamsaliti babake kwa kumwambia Ngoswe kuwa hana baba tena anamwondoa katika fikrana uhai wake.
   8. Mtemi anaisaliti nchi pamoja na wananchi wa Matuo kwa kuzorotesha uchumi kupitia kwa sera mbovu za uongozi na ufisadi uliokithiri.
   9. Mtemi anaisaliti jamii ya Waketwa kwa kuibagua katika ajira, biashara, hata katika makazi yao.
   10. Licha ya mwanasheria Mafamba kuifanyia serikali yake kazi na kumfichia uovu wake katika kesi za ufisadi, anamnyang'anya cheti cha uanasheria na kumtowesha kutoka mjini Taria.
   11. Pia anamnyang'anya hakimu cheti chake cha uanasheria na kumfuta kazi licha ya kwamba alikuwa akitekeleza majukumu yake kulingana na sheria.
   12. Sagilu anaisaliti jamii ya Waketwa walioishi Matango kwa kushiriki katika kuchoma makazi yao licha ya kwamba yeye mwenyewe alitaka achaguliwe kuwa mbunge wao.
   13. Sagilu anamsaliti Mrima kwa kumhonga pesa ili ashiriki katika anasa huku akimlenga mkewe kimapenzi.
   14. Sagilu anamsaliti Mangwasha kwa kumtembelea na kujifanya anayajali maslahi yake ilhali ndiye anayemfadhili Mrima kushiriki ulevi na anasa hadi kufutwa kazi.
   15. Sagilu anamsaliti mwanawe Mashauri kwa kumnyang'anya mchumba wake Cheiya bila kujali heshima yake.    Kadiria (za kwanza 12x1=12)
 5. SWALI
  1. uk 67 Msemaji ni Sara. Msemewa ni Neema wakiwa nyumbani mwa sara. Sara anamweleza namna alivyovumilia mateso ili binti zake wapate kufanikiwa maishani kama Watoto wa kiume tu. (4x1=4)
  2.  
   • matumaini; Sara alivumilia akitumai wanawe kufanikiwa (kuota mbawa)
   • kukata tamaa/kutamauka…..nilipungukiwa na mengi niliyotamani (1x2=2)
  3. mandhari haya ni nyumbani mwa Sara na Yona.
   • yameendeleza maudhui ya ndoa
   • yameangazia sifa za Sara kuwa mstahimilivu, mshauri mwema, mlezi mwema
   • yameendeleza maudhui ya utamaduni
   • yameendeleza suala la nafasi ya mwanamke katika jamii
   • Suala la malezi
   • Yameendeleza suala la ubabedume
   • Majuto yameendelezwa humo
   • Suala la mawaidha kwa Watoto limejitokeza
   • Suala la uvumilivu limeangaziwa hapa   (zozote 8x 1=8)
  4. stahamala ilivyomfaa:
   • Hatimaye alipata Watoto
   • Bintize walisoma
   • Ndoa yake ilidumu
   • Bintiye aligharamia matibabu yake
   • Bintiye alimwajiria wafanyakazi
   • Bintiye na mume wake (Bunju) walimjengea nyumba
   • Bintiye alimsaidia kugharamia elimu ya wanuna wake
   • Bintiye alimnunulia gesi ya kupika ili asiathirike na moshi.  (zozote 6x1=6)
 6. SWALI
  1.  
   • tashbihi; ...kama jani kavu..
   • jazanda/sitiari; kimbaumbau mwiko wa pilau; mkondefu
   • chuku; upepo kidogo tu ungekuyumbisha
   • mbinu rejeshi; mara ile ya kuzuka, ulikuwa.... (4x1=4)
  2.  
   1. Asna; ukosefu wa kazi
   2. Bunju; mkopo wa benki
   3. Bunju; kazi nyingi afisini na wafanyakazi wachache
   4. Bunju; Gharama ya ugonjwa wa mamake Neema
   5. Sara; ugonjwa wa moyo
   6. Sara; mapigo ya mumewe
   7. Sara; hali ngumu ya kiuchumi akiwalea wanawe
   8. Sara na Yona, kukosa watoto kwa muda mrefu, kusengenywa na wanakijiji
   9. Yona; ulevi unaomharibia kazi
   10. Neema; matibabu ya mamake (zozote 10 x 1=10)
  3. Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kukuza :
   1. ploti;
    • Mazungumzo yake na Yona kuhusu upishi alasiri
    • Mazungumzo na Dina alipokuja kumsaidia upishi jioni ile
    • Ziara ya kwenda mjini kupata matibabu
    • Kukaa na Asna mjini (3 x 1=3)
   2. wahusika wengine
    • Dina; mhisani
    • Yona; mwenye taasubi ya kiume, dhalimu
    • Asna ni mwenye usasa/ amekengeuka
    • Neema ; mwajibikaji (3 x 1=3)
 7. SWALI
  FADHILA ZA PUNDA
  1. Luka nampiga lilia teke tumboni anapokosa kuipokea simu yake akashindwa kujinyoosha kwa siku mbili kwa maumivu.
  2. Luka nampiga Lilia kwa kisingizio kuwa chakula hakikukolea chumvi.
  3. Luka anamlazimisha Lilia kuacha kazi na kumtawisha nyumbani.
  4. Habari zinapomfikia Luka kuwa Lilia alifika katika kituo cha polisi, Luka alimpiga hadi akazirai.
  5. Luka anaandamana na wanawake wengine lakini mkewe anaomuuliza anapokea kipigo kikali.
  6. Luka anamnyima Lilia uhuru wa kutoka nje ya lango na hata kuhusiana na marafiki zake.
  7. Luka anakosa kurudi nyumbani kwa siku mbili licha ya kujua kuwa Lilia ni mjamzito na kumpiga katika hali hiyo hadi akatungua mimba.
  8. Luka anamtusi na kumfokea Liliakwa kukataa kuandamana naye kwenye mikutano ya kisiasa kutokana na uja uzito wake wa miezi minne.
  9. Luka anahamia kasri la gavana na kumwacha Lilia kijijini akidai kuwa anafaa kuwa karinbu na raia.
  10. Luka anapiga marufuku Lilia kuenda ofisini mwake na hata kumpiga alipoenda huko bila taarifa.
  11. Luka anampiga Lilia kipigo cha mbwa hadi kuzirai na kuondoka nyumbani akimwacha ajifilie
                   SABINA
   1. Mimba za mapema – Nyaboke -kidato cha pili
   2. Kukataliwa baada ya kupachikwa mimba – Nyaboke
   3. Kukatiza masomo/ elimu -Nyaboke
   4. Kutengwa – Sabina
   5. Elimu yam toto wa kike kupuuzwa – Sabina
   6. Kupigwa – Sabina
   7. Kutumikishwa – Sabina
   8. Kusimangwa – kukejeliwa – anaitwa kiokotwe – Sabina
   9. Kuhusishwa katika biashara
   10. Kukosa natibabu – Nyaboke – anapelekwa kwa mganga maarufu kijijini
   11. Kukosa mavazi mazuri – Sabina kuvaa sare iliyoshiba viraka vya kila rangi
   12. Kukosa malezi ya baba na mama – wazazi wawili
   13. Kufanya vibarua ili kupata mahitaji ya kila siku – Nyaboke (ajira ya Watoto)
            KIFO CHA SULUHU
    1. Mauaji – Bwana Suluhu – mamake Abigael
    2. Kunyanganywa mali – Bwana Suluhu kumnyanganya Mamake Abigael
    3. Kutelekeza malezi ya Watoto – Bwana Suluhu anamwachia mkewe , Bi Suluhu malezi
    4. Kupachikwa mimba na kuachwa bila tumaini/msaada
    5. Kutumia njia za hila ili kuhitimu masomo kabla ya muda wa kuhitimu masomo kuwadia
    6. Kushiriki ukahaba – kuwanyonya wanaume
    7. Kutia dawa kwenye vinywaji
    8. Kumwibia mtu pesa – Abigael na Natasha wanapanga njama dhidi ya Bwana Suluhu
    9. Kufuja pesa za wananchi
    10. Uchafuzi wa mazingira – ukataji wa miti
     NIPE NAFASI
     1. Kukosa vyakula
     2. Kutelekeza majukumu – msimulizi anasema baba yao Moshi hakuwa akimtumia mama yake pesa za matumizi mwaka mzima.
     3. Kupuuza malalamishi – wazazi wa Moshi wanadinda kusikiliza malalamishi ya mama Kazili
     4. Mamake Kazili kukosa kupewa pesa ambazo mumewe Moshi anatetemeka
     5. Kukosa mavza mazuri yanayositiri baridi. Msimulizi amasmea …tulikuwa tumevaa marumaru
     6. Kifo
     7. Kunyimwa nafai ya kujiteteta   (4x5=20)
 8.  
  1. “Pupa imenitumbukiza kwenye kisima nilichochimba, sasa naingia mwenyewe…”
   1. Mbinu za kimtindo
    1. Jazanda -kisima nilichochimba sasa naingia mwenyewe (mahali penye matatizo)
    2. Mdokezo …kisima nilichochimba, sasa naingia mwenyewe
    3. Taswira – taswira oni, taswira ya mwendo
    4. Tashihisi- pupa kuwa na uwezo wa kutumbukiza        (2x1=2)
   2.  
    1. Kusafirishwa asikojua – Mkwakuona
    2. Kuvalishw anguo zinazoomyesha mwili wake bila hiari
    3. Kung’ang’aniwa na wanaume danguroni – chenga -ways
    4. Kuingizwa kwenye chumba amnacho anasubiriwa na mwanamume mkota-dume
    5. Kufungiwa mlango kutoka nje na mwanamapokezi
    6. Kuuzwa kwa mtu mwenye umri mkubwa kuliko babake mzazi siku yake ya kwanza katika jengo la Chenga- Ways
    7. Kugeuzwa kifaa cha kutumiw aovyo
    8. Anatokwa na machozi yasiyokauka
    9. Anakatiziwa masomo
    10. Kutawishwa katika jengo la Chenga Ways – haruhusiwi kutoka nje
    11. Kulindwa anapoenda msalani (8x1=8)
  2. Kila Mchezea Wembe: Pauline Kea Kyovi
   1. “Dunia hii nayo kubwa, anasa zake nyingi huwezi kuzimaliza”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Fafanua toni katika dondoo hili. (alama 2)
    3. Jadili namna ambavyo anasa imejitokeza katika hadithi hii. (alama 4)
     Muktadha
     • Ni kauli ya Emmi
     • Anamwambia Tembo
     • Bwana Tembo anayakumbuka akiwa Hospitali ya Uhai ni Neema
     • Ni baada ya Bwana Tembo kujutia matendo yake ya uraibu wa pombe ambayo yanamsababishia madhara ya kiafya. (4x1=4)
    4. Toni
     • Toni ya kushauri – Emmi alikuwa anamshauri mumewe, Bwana Tembo kuacha tabia zake za kupapia anasa za dunia (1x2=2)
    5. Anasa
     • Kuwa mraibu wa ulevi/pombe
     • Kusakata rhumba- Bwana Tembo na wenzake (walevi)
     • Kucheza rhumba na wanawake wengine ambao hakuwa anawajua
     • Kulala kwa mwanamke asiyemjua
     • Kuendeleza ukahaba – Angelica
     • Kufuja pesa (4x1=4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest