Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Jibu maswali mawili
 • Swali la kwanza ni la lazima
 1. Wewe ni katibu wa kamati iliyoteuliwa na afisa mkuu wa elimu katika jimbo lako kushughulikia visa vya uchomaji na uharibifuwa mali ya shule. Andika kumbukumbuku za mkutano wa kamati hiyo. (Alama 20)
 2. Mtoto wa kiume ametelekezwa sana katika jamii. Eleza. (Alama 20)
 3. Baada ya dhiki faraja. (Alama 20)
 4. Andika insha itakayoanza kwa: (Alama 20)
  “Naikumbuka siku hiyo vizuri sana, sijawahi kufedheheka jinsi ile maishani mwangu………………………………………………


MARKING SCHEME

 1.  
  1. Hii ni insha ya kiuamilifu.
  2. Sura ya kumbukumbu ijitokeze ifuatavyo
   • Kichwa
   • Waliohudhuria
   • Waliotumaudhuru
   • Waliokosa
   • Wageni
    AJENDA
    1. Kufunguliwa kwa mkutano.
    2. Kumbukumbu za mkutano uliopita.
    3. Yatokanayo na kumbukumbu hizo.
    4. Vyanzo vya uchomaji na uharibifu wa mali ya shule
    5. Njia za kuzuia
    6. Shughuli nyinginezo
    7. Kufungwa kwa mkutano.
  3. Mwanafunzi anayekosa sura ya kumbukumbu aondolewe alama 4 za sura baada ya utuzaji.
  4. Maudhui yasipungue 6. Mwanafunzi aliye na chini ya Maudhui sita asipate zaidi ya nusu alama yaani 10.
  5. Baadhi ya hoja:

   Vyanzo
   1. Uongozi mbaya
   2. Matokeo duni katika mtihani wa kitaifa
   3. Dhuluma kwa wanafunzi wengine
   4. Chakula kibaya
   5. Ukosefu wa mawasiliano bora miongoni mwa walimu na wanafunzi
   6. Vikundi vibaya
   7. Dawa za kulevya
   8. Shinikizo kutoka nje

    Suluhisho
    1. Ushaurinasaha
    2. Mawasiliano bora 
    3. Kusikiza vilio vya wanafunzi
    4. Kuwachukulia hatua wanaopatikana na makosa.
 2. Utelekezaji wa mtoto wa kiume
  Jinsi ametelekezwa (Kuunga mkono)
  • Kukosa wa elekezi
  • Kukosa mashirika ya utafiti ku wahusu
  • Kunyimwa nafasi ya masomo
  • Kutwikwa majukumu wakiwa wachanga
  • Kutopewa ufadhili wakielimu
  • Kutopigiwa debe kama wasichana
  • Kwenda chuo kwa alama za juu
  • Kutoulizwa na wazazi aendako wala atokako
  • Kuachwa kujifanyia maamuzi
 3. Mwanfunzi atambue hii ni methali kisha aandike kisa kitakachooana na methali hii. Kisa ni kimoja.
  Maana
  Dhiki – shida au taabu
  Faraja – raha au utulivu
  Maana – Baada ya kupata shida au taabu, inayofuata ni raha au utulivu
  Inatupa mayo pale mtu apatapo shida, asife moyo bali awe mvumilivu na apambane na zile shida.
  Tanbihi: Methali ina pande mbili
  Kisa cha mwanfunzi kionyeshe dhiki na pia faraja.
 4.  
  1. Hii ni insha ya mdokezo.
  2. Mtahiniwa atunge kisa kinachooana na mdokezo.
  3. Lazima mtahiniwa aandike maneno yote katika mdokezo – afuate maagizo
  4. Lazima mtahiniwa ajihusishe na kisa chenyewe na kudhihirisha kabisa kufedheheka kwake na kiini.

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest