Kiswahili Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali yote.


MASWALI

  1. SEHEMU YA A-TAMTHILIA:KIGOGO (Pauline Kea)
    “Oooh bebi,miaka yaenda mbio sana,nayo sura yako inachujuka…”
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake.(alama 4)
    2. Mhusika anayehusishwa na wimbo huu ana msimamo gani wa kimapinduzi?(alama 8)
    3. Eleza sifa zozote nane za mhusika huyu.(alama 8)
  2. SEHEMU YA B-DIWANI YA TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI ZINGINE (Wah. Dumu Kayanda Na Alifa Chokocho)
    Shibe Inatumaliza:Salma Omar
    1. Jazanda ni mbinu mojawapo ya mbinu za lugha zilizotumiwa kwa ukamilifu.ukirejelea hadithi shibe inatumaliza fafanua mifano kumi.(alama 10)
    2. “…lakini kula kunatumaliza vipi?
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
      2. Eleza jinsi kula kunavyo tumaliza kwa mujibu wa hadithi.(alama 6) 
  3. SEHEMU YA C- RIWAYA YA CHOZI LA HERI (Assumpta K. Matei)
    “…Maisha yangu yalijaa shubiri tangu utotoni.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
    2. Kwa kutolea mfano,bainisha tamathali ya usemi inayojitokezakatika kauli hii.(ala2)
    3. Jadili athari za vita katika jumuia ya chozi la heri.(alama 14)


MWONGOZO

  1. ”oooh bebi,miaka yaenda mbio sana,nayo sura yako inachujuka…
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake.(alama 4)
      • Ni wimbo wa daudi kabaka anaouimba ngurumo.
      • Anamwimbia tunu
      • Wako mangweni pahali pa ulevi
      • Alikuwa anamdhihaki tunu na wanaharakati wengine kuwatembelea ili kuwahamasisha kuhusu udhalimu wa majoka na kuwa ni vyema waupinge.
    2. Mhusika anayehusishwa na wimbo huu ana msimamo gani wa kimapinduzi?(alama 8)
      1. Ana msimamo dhabiti.Tunu anasimama kidete bila uoga kupambana na udhalimu wa utawala wa Majoka.
      2. Ni mfano bora wa watu wa jamii:kuwajibika na kuchukua jukumu la kuikomboa jamii inayokandamizwa.
      3. Anafanikiwa kushawishi wananchi wasihudhurie sherehe za uhuru na badala yake wakusanyike katika eneo la soko la Chapakazi ili wadai uhuru wa kweli.
      4. Mateso ya kupigwa na kudhulumiwa na utawala havikatizi ari yake katika kuleta mapinduzi.
      5. Baadaye kutokana na jitihada zake pamoja na wanaharakati wengine,uongozi wa Majoka unaondolewa na soko linafunguliwa tena.
      6. Anakataa kuozwa kwa lazima
      7. Ni mwanamke jasiri kwani hamuogopi Majoka.
      8. Ni mwanaharakati wa kimapinduzi.
    3. Eleza sifa zozote nane za mhusika huyu.(alama 8)
      • jasiri na mkakamavu
      • mwenye busara
      • mwenye msimamo dhabiti
      • Ni mzalendo mwenye mapenzi ya dhati kwa nchi yake.
      • Mshawishi
      • Mwajibikaji
      • Msomi
      • Mwenye utu/mkarimu
      • King’anga’nizi-aling’ang’ania kudai haki mpaka akaangusha utawala wa Majoka.
      • Mtetezi
        (mwanafunzi lazima aweze kufafanua sifa zozote )
  2.                
    1. Mifano kumi ya jazanda katika “shibe inatumaliza”. (alama 10)
      • "sasa” na “mbura”-kusasambura(kumaliza kila kitu ,kupora mali yote.)
      • sherehe-mipango isiyo na maana ya kufilisi mali ya umma.
      • mchele wa Mbeya-bidhaa za humu nchini za zenye manufaa makubwa/rasilmali za kiasili.
      • mchele wa basmati-bidhaa duni za kigeni.
      • kupakua vyakula-kupora mali ya umma.
      • kupika-kuzalisha mali
      • magonjwa-matatizo yanayokumba nchi
      • shibe-tamaa inayosababisha ufisadi.
      • kula-kufisidi nchi
      • Sherehe-unyakuzi wa mali za umma
      • wapishi-wafanyakazi/wanaozalisha mali.
      • vyakula-rasilmali za nchi
    2. “…lakini kula kunatumaliza vipi?
      • Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
        Haya ni maneno ya sasa akimwambia mbura katika sherehe baada ya kula .wanazumzia ile hali ya matumbo yao kushiba ilhali wengine wanadhikika tu.
      • Eleza jinsi kula kunavyo tumaliza kwa mujibu wa hadithi.(alama 6) 
      • Magonjwa-sukari,presha,saratani,obesity,madonda ya tumbo.
      • Vifo-kuuana kwa mabomu,risasi,kunyongana,kuuana kifikra.
      • Kunyang’anyana vinavyoonekana na visivyoonekana-haki,utu,heshima,uhuru.
      •  Kutochunguza vyakula
      • Kutochunguza utendakazi wa wafanyikazi.
      • Kutowajibikia kazi zao
      • kuwalipa watu hawafanyi kazi mishahara.
      • Kukosekana kwa dawa
      • Kuchangia kuzorotesha uchumi.
      • Mali ya umma kunyakuliwa.
  3. SEHEMU YA C. RIWAYA YA CHOZI LA HERI.
    “maisha yangu yalijaa shubiri tangu utotoni.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
      • Haya ni maneno ya chandachema.anawaambia kairu,umu,zohali na mwanaheri.wako katika shule ya tangamano.
      • Chandachema anawasimulia wenzao dhiki alizopitia maishani mwake baada ya kuzaliwa.
    2. Kwa kutolea mfano,bainisha tamathali ya usemi inayojitokeza katika kauli hii.(alama 2)
      • Msemo/nahau-kujaa shubiri
      • Jazanda-kujaa shubiri:maisha yake yalikuwa na matatizo mengi.
    3. Jadili athari za vita katika jumuia ya chozi la heri.(alama 14)
      1. Vifo:vitabaina ya pande za mwekevu na yule mpinzani wake wa kisiasa vilisababisha mauaji.
      2. Uharibifu wa mali.aila ya Ridhaa kuangamizwa katika moto:nyumba na mali kuteketezwa.
      3. Ukosefu wa makazi bora.kaizari na wenzake wamekosa makazi bora kule msitu wa mamba walikotorokea.vibanda vinasongomana.
      4. Huzuni –ridhaa alihuzunika sana baada ya aila yake na mali zake kuteketezwa kwa moto.
      5. Hasara kwa wafanyabiashara.wahalifu waliingia katika maduka ya kibiashara za kihindi,kiarabu na kiafrika na kupora mali ya wenyewe.
      6. Kutiwa nguvuni:waporaji waliopora maduka wakati wa vita walitiwa nguvuni na kukabiliana na mkono wa kisheria hapo baadaye.
      7. Watu kutoroka Makwao:wahafidhina walihama makwao wakati wa vita bila kujua walikokuwa wakielekea.
      8. Utegemezi:kukosekana kwa chakula katika kambi yam situ wa mamba kulifanya watu kutegemea msaada wa chakula kutoka kwa wahisani k.v shirika la msalaba mwekundu.
      9. Majeruhi. Kuna mwanamme aliyevamiwa na kuumizwa kwenye mgogoro wa kupigania ardhi katika eneo la tamuchungu.Alilazwa katika kituo cha mwanzo mpya.
      10. Kukatizwa masomo.mfano lime na mwanaheri
      11. Kusababisha uyatima-vita katika kambi yam situ wa mamba vinasababisha walinda usalama kuua wazazi na kuwaacha watoto peke yao.
      12. Kubakwa-baada ya fujo kuzuka lime na mwanaheri wanabakwa na wahuni.
      13. Magonjwa-ridhaa aliugua shinikizo la damu kutokana na mshtuko wa kupoteza jamaa yake.
      14. Kusambaratishwa kwa jamaa.mfano selume
      15. Athari za kisaikolojia

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 4 Mid Term 2 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest