- Andika insha mbili. Insha ya kwanza na ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Umetangazwa kuwa mwanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa. Mwalimu Mkuu wa shule ya upili ya Tujitahidi amekualika katika shule hii yake kuwahutubia wanafunzi kuhusu kilichochangia ufanisi wako. Toa hotuba yako.
- Ufisadi umekuwa tatizo sugu katika nchi ya Kenya. Jadili kuhusu madhara yake huku ukipendekeza njia za kuukabili.
- Tunga kisa kitakachodhirisha maana ya methali:
Ukiona vyaelea vimeundwa. - Tunga kisa kitakachomalizika kwa: . . .Hapo ndipo nilipotambua kuwa ukitenda wema umetendea nafsi yako.
MARKING SCHEME
- Huu ni utungo kiuamilifu Vipengele viwili vikuu vya insha ya aina hii viweze kushughulikiwa. Vipengele hivi ni:
- Maudhui
- Muundo
- Muundo wa hotuba. Mtahiniwa azingatie mundo au sura ya hotuba. Vipengele vifuatavyo vya kimsingi vizingatiwe.
- Anwani ya hotuba.
- Anwani itaje kuwa ni hotuba.
- Anwani itaje mada na hotuba.
Maudhui yenyewe hutolewa. Kila hoja hufafanuliwa kwa aya yake. Hoja hupangwa vyema ili mawazo yatiriirike vyema. Mtahiniwa aliyejitosheleza kimaudhui awe na hoja tano au zaidi zilizofafanuliwa vilivyo.
Hatibu anaweza kurejelea aliyoyahutubu kwa muhtasari. Anaweza pia kushukuru hadhira.
Mtahiniwa anaweza kuibuka na hoja zinazohusiana na mada. Baadhi ya hoja hizo ni:
- Kuwa na nidhamu ya hali ya juu.
- Jitihada katika masomo.
- Kuwaheshimu walimu, wazazi na wanafunzi.
- Kufuata ushauri nasaha wa wakubwa.
- Kumcha Mungu.
- Kushughulikia kazi ya ziada na kudurusu vitabu vingi.
- Kutopoteza wakati wowote.
- Kuamka na kuingia darasani mapema.
- Kukamilika kwa mtaala mapema.
- Kuepuka kukwaruzana na mamlaka shuleni.
Tanbihi
Mtahiniwa akikosa sura ya hotuba aadhibiwe kwa kutolewa alama nne za sura 4s.
- Hii ni insha ya kujadili au kufafanua hoja.
Hoja ziweze kuzungumziwa madhara ya ufisadi na vilevile suluhu.
Baadhi ya hoja za madhara ni:- Kutopata huduma muhimu bila hongo.
- Kusambaratika kwa uchumi wa taifa.
- Kutupiliwa mbali kwa mitihani ya kitaifa.
- Watu kufutwa kazi kwa sababu ya ufisadi.
- Kuharibu mazingira.
- Kufungwa jela kwa wahusika.
- Viongozi kupoteza nyadhifa zao.
- Kuleta fedheha kwa familia.
Baada ya hoja za suluhu:
- Kuhamasisha wananchi kuhusu athari za ufisadi.
- Kutia mbaroni wahusika na kuwashtaki.
- Kutaifisha mali iliyonyakuliw kwa njia ya ufisadi.
Tanbihi:
Mtahiniwa aweze kufafanua angaa hoja tano kikamilifu.
- Hii ni insha ya methali
\Kisa kidhidhirishe maana ya methali. Maana ni kwamba ukiona vyombo vya bahari vikielea vimeundwa kisayansi. Tunapoona mambo ya watu yakifanikiwa tukumbuke wameyafanyia kazi. Methali hii inahimiza juhudi na bidii maishani.
Kisa kinaweza kudhihirisha hali zifuatazo:- Mhusika awe amefanikiwa kimaisha kwa sababu ya juhudi zake.
- Anaweza kuwa tajiri kwa sababu ya bidii yake ya kikazi.
- Mtahiniwa aibuke kuwa bora zaidi katika mtihani kwa sababu ya kusoma kwa bidii.
- Kampuni ifanikiwe kwa sababu ya kazi ambzo zimefanywa na wafanyikazi .
Tanbihi:
Kisa kionyeshe upande wa kuundwa na upande wa kuelea. Yaani upande wa bidii na upande kufanikiwa. Kisa kikikosa kuoana na maana ya methali mtahiniwa atakuwa amepotoka. Akiandika kuhusu upande mmoja atakuwa amepungukiwa kimaudhui.
- Hii ni insha ya mdokezo
Maneno kiini ni kutenda mema na kuwa umetendea nafsi yako. Mtahiniwa atunge kisa ambacho kitaoana na mdokezo. Mtahiniwa anaweza kutumia mbinu rejeshi ili kuonyesha wema mhusika aliutenda. Hatimaye aonyeshe vile mhusika huyu aliweza kutendewa wema kama alivyotenda.
Tanbihi:
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 End Term 2 Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students