Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 Term 3 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya LAZIMA.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia
  • Kila insha isipungue maneno mia nne (400)
  • Kila Insha ina (alama 20)
  1. Hali ya usalama katika kijiji cha Kazikeni imezorota sana.Wewe kama Waziri wa Usalama umekutana na chifu wa eneo hili ili kumhoji kuhusu chanzo cha tatizo hili na jinsi ya kusuluhisha.Andika mahojiano yenu.
  2. Mitandao ya kijamii ina faida na hasara. Jadili
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
    Ngozi ivute ingali maji.
  4. Tunga kisa kitakachomalizika kwa maneno yafuatayo:
    …….Hapo ndipo nilipogundua kuwa umoja na mshikamano katika familia ni nguzo muhimu katika utatuzi wa shida katika jamii.

MARKING SCHEME

  1. Hii ni insha ya mahojiano .Vipengele muhimu vya insha ya aina hii viweze kujitokeza. Yafuatayo yazingatiwe:
    1. Muundo
      Sura ya mahojiano idhihirike.
      1. Kichwa au anwani
        Kichwa kionyeshe wahusika na mada inayoshugulikiwa
      2. Utangulizi
        Haya ni maelezo mafupi kwenye mabano ambayo hufafanua mazingira ambapo mahojiano yanaendelea. Huweza pia kutaja majina ya wahusika.
      3. Mwili
        Sehemu hii hujumuisha ujumbe au maudhui yanayoshughulikiwa.
        Huchukua mtindo wa  kitamthilia.
        Majina ya mhoji na mhojiwa huandikwa  kushoto mwa pambizo yakifuatwa na koloni kisha kauli zao.
        Maelezo ya ziada huandikwa kwenye mabano.
      4. Hitimisho
        Huhitimishwa na mhoji kwa kutoa shukrani kwa mhojiwa.
    2. Maudhui
      Baadhi ya hoja ni :
      1. Uhasama wa makabila tofautitofauti unakosesha amani.
      2. Ukosefu wa ajira unafanya watu wengine kuwa wahalifu.
      3. Tamaa ya kutajirika inawafanya wengine kuibiana.
      4. Tofauti za kitabaka.
      5. Ufisadi. Wenye pesa huhongana na kufanya vitendo viovu.
      6. Idara ya mahakama kutotoa adhabu kali kwa wahalifu.
      7. Vijana kujiunga na makundi haramu.
        Suluhisho
        1. Watu kuelimishwa  kuhusu uzuri wa kuishi kwa amani.
        2. Kupanuliwa kwa nafasi za ajira.
        3. Watu kuhimizwa kutosheka na kile Mungu amewajalia.
        4. Adhabu kali kutolewa kwa wahalifu.
          Tanbihi 
          • Mtahiniwa awe na hoja tano au zaidi ili aweze kujitosheleza kimaudhui.
          • Mtahiniwa akikosa muundo wa mahojiano aadhibiwe kwa kutolewa alama nne za sura (4s)
  2. Hii ni insha ya mjadala. Makala yaonyeshe faida na hasara za mitandao ya kijamii.
    1. Faida za mitandao ya kijamii :
      1. Kuboresha mahusiano
      2. Kuboresha mawasiliano.
      3. Hutumika katika kutafuta kazi.
      4. Hutumika kupunguza misongo ya mawazo.
      5. Huburudisha.
    2. Hasara za mitandao.
      1. Kutumia muda mwingi mtandaoni na kuwafanya watu kuwa wazembe.
      2. Wafanyikazi huiba muda wa wajiri wao.
      3. Kuathiri watu kimaadili.
      4. Kupenyezwa kwa utamaduni wa nje.
      5. Kueneza umbeya.
      6. Wizi wa mawazo na fedha.
        Mtahiniwa awe na hoja tano na zaidi ili kujitosheleza kimaudhui.
  3. Hii ni insha ya methali  
    • Kisa kidhihirishe maana ya methali.
    • Maana ya methali hii ni kuwa jambo linaloenda tenge linafaa kurekebishwa kabla halijaharibika kabisa. Mtu anafaa kufanya jambo mapema, baadaye haitawezekana.
  4. Hii ni insha ya mdokezo. Mtahiniwa anafaa atunge kisa kinachooana na mdokezo aliopewa.
    • Msimulizi anaweza kutumia mbinu rejeshi na kusimulia kisa kuhusu jinsi mhusika alisaidiwa na familia yao.
    • Mtahiniwa akikosa kuandika mdokezo atakuwa amepungukiwa kimtindo.
    • Mtahiniwa akitunga kisa kisichooana na mdokezo atakuwa amepotoka kimaudhui.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 Term 3 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest