Tuesday, 08 February 2022 06:24

Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 4 End of Term 3 Exams SET 2 2022

Share via Whatsapp

SEHEMU YA KWANZA

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA (alama 5)
Ninaitwa Bi/Bw                  .na ningependa tuzungumzie kuhusu bendera yetu.

 1. Rangi za bendera ya Kenya ni ngapi? (alama 1) (Mwanafunzi ajibu)
 2. Rangi za bendera ya Kenya ni zipi? (alama 2) (Mwanafunzi ajibu)
 3. Sema kila rangi inaashiria nini. (alama 2) (Mwanafunzi ajibu)

II. KUSOMA KWA SAUTI.
Soma kifungu kifuatacho kwa sauti mwalimu akisikiliza. (alama 10)
Kemoi anaishi katika kijiji cha Tia Adabu. Yeye na dada yake Chebet wanapendana sana. Ni kawaida kwa Kemoi kuamka kabla ya Chebet. Anapoamka huchukua kiberiti na kuwasha taa ya kibatari. Kemoi anajua kukoka moto akitumia makumbi ya nazi. Yeye hujikaza kupika kahawa na kaimati ya kiamshakinywa. Baada ya kuoga, Kemoi huvaa suruali ya zambarau na sweta ya buluu.
(Alama 20) (alama 3)

III. SARUFI. 

 1. Andika sentensi hizi kwa wingi
  1. Jasho lilimtiririka.
  2. Jua limechomoza.
  3. Giza limeingia.
 2. Tunga sentensi ukitumia maneno haya.(alama 3)
  1. omba radhi
  2. toa shukrani
  3. piga hodi
 3. Tumia "li" au "ya" kujaza pengo(alama 4).
  1. Godoro                  menyeshewa.
  2. Madirisha                   lifunguliwa.
  3. Soko                  lijengwa upya.
  4. Madawati yote                  mepanguswa
 4. Andika sentensi hizi kwa umoja. (alama 3)
  1. Milango imefunguliwa.
  2. Mizizi imeinuka juu.
  3. Miche ilikauka.
 5. Kamilisha methali hizi. (alama 3)
  1. Teke la kuku                   
  2. Mtoto akibebwa hutazama                  
  3. Mtoto umleavyo                  
 6. Andika maneno ya upole badala ya maneno yafuatayo. (alama 4)
  1. Wanahara -                   
  2. Amezaa -                   
  3. Ana mimba -                   
  4. Matako -                   

IV. KUSOMA UFAHAMU. (alama 5)
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Yohana aliamka akiwa na furaha. Mjomba wake clikuwa amewapangia ziara. Ilikuwa ziara ya kutembelea mbuga ya wanyama ya Mc asai Mara. Bwana Upendo, mjomba wake, alikuwa amekodi gari la kuwapeleka ziara hiyo.
Yohana alipingia mjomba alipiga gari moto na safari ikaanza. Yohana na binamu zake Bidii na Rehema waliona vitu vingi safarini. Waliona magari, watu, mashamba na pia waliona bonde kubwa. Bwana Upendo aliwaambia linaitwa Bonde la Ufa. Waliona Mlima Longonot ndani ya bonde lile. Baada ya kusafiri kwa muda walifika Maasai Mara. Walilipa pesa na kuingia ndani ya mbuga wakielekezwa na mlinzi.

 1. Kwa nini Yohana aliamka akiwa na furaha? (alama 1)
 2. Yohana aliandamana na akina nani safarini? (alama 1)
 3. Taja baadhi ya vitu walivyoviona Yohana na binamu zake wakiwa safarini. (alama 2)
 4. Yohana na binamu zake waliona bonde gani? (alama 1)
 5. Walipofika Maasai Mara walifanya nini ili kuruhusiwa kuingia mbugani? (alama 1)

INSHA
Kuandika (Alama 10)

Andika insha kuhusu:
MWALIMU WANGUMARKING SCHEME

 1. Kusikiliza na kuzungumza 
  1. nne
  2. nyeupe, nyekundu,nyeusi, kijani
  3. kijani - mimea 
   nyekundu - damu iliyomwagika wakati wa kupata uhuru 
   nyeusi - rangi ya wakenya
   nyeupe - amani ya nchi yetu.
 2. Kusoma kwa sauti
 3. Sarufi
  1.      
   1. jasho liliwatiririka.
   2. jua limechomoza.
   3. giza limeingia.
  2. Sahihisha sentensi iliyotungwa sahihi kisarufi.
  3.      
   1. li
   2. ya
   3. li
   4. ya
  4.      
   1. Mlango umefunguliwa.
   2. Mzizi umeinuka jua.
   3. Mche ulikauka.
  5.      
   1. halimuumizi mwanawe.
   2. kisogo cha nina.
   3. ndivyo akuavyo.
  6.      
   1. wanaendesha
   2. amejifungua c) 22
   3. ni mja mzito
   4. makalio
 4. Ufahamu
  1. mjomba wake alikuwa amewapangia ziara.
  2. mjomba na binamu zake Bidii na Rehema.
  3. magari, watu,mashamba, wanyama, bonde kubwa, mlima Longonot.
  4. Bonde la ufa
  5. walilipa pesa
 5. Kuandika
  • Mpangilio wa sentensi katika aya.
  • uakifishaji wa sentensi.
  • hati
  • ubunifu
  • maendelezo
  • msamiati na mambo mengine muhimu. 

Download Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 4 End of Term 3 Exams SET 2 2022.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.