Maswali na Majibu ya Insha katika Riwaya ya Chozi la Heri PDF

Share via Whatsapp

Chozi Insha Questions and Answers

Maswali ya Insha

Haya ni maswali ambayo hutoa kauli inayohitaji kujibiwa kwa kirefu na kwa kina. Swali linaweza kuwa la jumla yaani linalohusu Riwaya nzima. Pia, swali laweza kulenga sehemu ya kazi husika katika nyanja na maudhui, wahusika na hulka zao, mafunzo na fani. Maswali haya huhitaji zaidi uwezo wa kukumbuka wa mtu, kupanga hoja na kuelezea msimamo au maoni yake kuhusiana nayo. Mtahiniwa anahitajika kutoa hoja na kuziteteta kwa mifano dhabiti. Mtahiniwa asitumie vistari vistari, afafanue hoja kikamilifu akiandamisha mifano mingi kutoka kwa Riwaya.

Swali la Insha 1

Haki za watoto hazitiliwi maanani katika jamii nyingi za kiafrika. Eleza ukweli wa kauli hii kwa kurejelea Riwaya ya chozi la heri (Alama 20)

Haki ya watoto kusoma inakiukwa. Ami za Lucia na Akelo wanapinga elimu yao na kudai kuwa kuwaelimisha wasichana ni kufisidi raslimali.

Watoto wanahusishwa katika ajira. Akiwa mdogo,Sauna anaajiriwa kwenye machimbo ya mawe,kuuza maji na hata pombe baani. Vilevile Chandachema anahusishwa katika ajira ya uchunaji wa majani chai akiwa mtoto wa darasa la tano kwenye shirika la chai la Tengenea.

Kuna wizi wa watoto. Sauna anawaibia Dickson na mwaliko na kuwapeleka kwa Bi. Kangara ambaye ni Mlangunzi hodari wa watoto.

Watoto wanauawa na magari moshi kwenye mtaa wa madongoporomoa wa Sombera wanapoenda haja kwenye reli

Watoto wanahusishwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya. Dickson anatumiwa na mzee Buda kusafirisha dawa za kulevya ughaibuni.

Baadhi ya watoto wasichana wanaolewa na vikongwe kwa lazima. Fungo anamwoa Pete kwa lazima akiwa darasa la saba kama mkewe wanne.

Kunajisiwa/kubakwa – Sauna anabakwa na babake wa kambo Bwana maya na Kutungwa mimba. Pia lime na Mwanaheri wananajisiwa na vijana wahuni.

Watoto wanapotoshwa na watu wazima. Bi. Kagara anampotosha Sauna kwa kuhadaa ajihusishe na biashara haramu ya ulanguzi wa watoto. Anapotoshwa,Sauna anahusika katika wizi wa watoto na kuwalangua

Baadhi ya watoto wanapozaliwa wanatupwa. Naomi anamwokoa mtoto aliyetupwa jalalani na kumpeleka kwenye kituo cha polisi. Matawa Cizarina anasema kwamba kuna mtoto aliyetupwa langoni mwa kituo cha watoto cha Benefactor akiwa amefungwa kijiblanketi kikuukuu.

Naomi anawahini wanawe malezi anapomtoroka mumewe. Anamtoroka Lunga baada yake kufutwa kazi na kuwa maskini jambo hili linawafanya Umu, Dickson na Mwaliko kulelewa na baba yao pekee

Sauna anapotoshwa na Bi. Kangara anapohusishwa na wizi na ulanguzi wa watoto. Bi.Kangara anamhadaa Sauna na kumwingiza katika biashara hii haramu.

Watoto wanapokea vitisho kutoka kwa watu wazima wanaopania kuwatumia vibaya. Mzee Buda anamtisha Dickson anapojaribu kukataa kujihusisha katika biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya. Anamwambia kwamba anamtupa nje na kumsingizia wizi. Jambo hili lingemfanya Dickson kuvamiwa na kuuawa na raia kama alivyofanywa Lemi.

Watoto wanatumiwa kama vyombo vya mapenzi. Bi.Kangara anawaiba wasichana na kuwauza kwenye mandanguro (shambiro) ili watumiwe kama vyombo vya mapenzi na wanaume katili. Fumba anajihusisha na mwanafunzi wake kimapenzi na kumringa.

Kuna ubaguzi wa watoto. Wazazi wa Pete wanamwoza kwa lazima kwa mzee Fungo kama mke wanne. Wanafanya hivi ili wapewe mahari itakaayotumiwa kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.

Watoto walio mijini ya mama zao wanaavywa. Mamake Sauna anamsaidia kuavya kitoto chake. Anafanya hivi kwa kumwogopa Bwana Maya aliyemnajisi Sauna. Umulikheri kuachiwa ulezi wa Dickson na baada ya Mama yao Naomi kutoroka na baba yao kuaga.

Tuama kukumbwa na maswala ya ukeketaji wa watoto wa kike

Dick kulazimishwa kushiriki ulanguzi wa dawa za kulevya na Buda

Mwanawe Selume Sara anatengwa na mamake mzazi baada ya mumewe kumwacha Selume na kumwoa msichana wa kikwao. Anachukuliwa na babake. (Uk35)

Kairu anaeleza jinsi walipofukuzwa kwao na jinsi si kitindamimba wao anapoaga dunia kutokana na njaa.uk 91

Mwanaheri na Lime wanafanyiwa unyama-wanabakwa na vijana mbele ya baba yao. Na baadaye wanakosa penzi la Mama yao Subira anapowatoroka baada ya kupitia machungu ya kubaguliwa .Uk 97

Zohali kuhusishwa katika mapenzi mapema na kupachikwa mimba. Zohali Anadhulumiwa kimapenzi uk 98

Chandachema kutelekezwa na babake Fumba na kuachwa alelewe na Bi. Kizee ambaye anaaga akiwa darasa la kwanza. Pia hajui aliko mama yake.

Rehema, Mamake Chandachema anadhulumiwa kimapenzi kwa kuringwa mimba na Fumba mwalimu wake akiwa kidato cha tatu. Uk 103

Chandachema anaizimika kufanya kazi katika shrika la chai la Tengenea ili kujikimu akiwa darasa la pili maadamu apate nafasi ya kusoma Uk.105

Chandachema   na wanawe Tenge wanalazimika kushuhudia bwana Tenge akigeuza chumba chao Danguro japo ni watoto wachanga…na kusababishiwa dhiki ya kisaikolojia. Uk 106

Swali la insha 2

Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri  ( al. 20)

Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao.

Mwanaheri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya mamwezi lakini babake alikuwa wa jamii tofauti. Kila mara subira aliitwa ‘muki’ au huyo wa kuja.

Kijana mmoja alimwita Ridhaa mfuata mvua jambo lilimuumiza sana Ridhaa.

Mzee kendi alimtendea udhalimu Ridhaa na kuiteketeza aila yake licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini. Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na mzee kendi.

Ndoa ya Selume ilisabaratika baada ya vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya kuoa msichana wa kikwao.

Tulia alimsaidia kaizari kufunganya na kumsidikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi Mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake

Uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja.

Subira aliweza kuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda, Mwishowe alihiari kujiondokea na kwenda mjini alikojinywea kinywaji kikali. (zozote 10 x 2)

Swali la insha 3

Jadili nafasi ya sehemu zifuatazo katika riwaya ya Chozi la Hari:

 1. Hotuba (alama 10)
 2. Uozo katika jamii (alama 10)

Hotuba

Hotuba ni maelezo maalumu yanayotolewa na mtu mmoja mbele ya watu. Pia huitwa hutuba. Mwandishi wa riwaya hii ametumia hutuba kwa ustadi mkuu kupitisha ujumbe mbalimbali.

Hotuba hizi ni:

Hotuba ya Racheal Apondi kwa maafisa waliohudhuria warsha kuhusu jukumu la vikosi vya askari katika kudumisha usalama, amani na maridhiano nchini (uk 112- 113). Katika hotuba hii, Racheal Apondi anasisitiza kuwa: Suala la usalama haliwezi tena kupuuzwa. Usalama umekuwa mojawapo ya mahitaji ya kibinadamu. Anasema kuwa bila usalama, binadamu hawezi hata kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali, hivyo hata mahitaji yake mengine ya kimsingi kama vile chakula, malazi na makazi hayawezi kukidhiwa. Kila binadamu ana jukumu la kudumisha amani na usalama. Wafanyakazi wa umma, hasa polisi na wanajeshi wana jukumu kubwa zaidi la kudumisha usalama na amani. Kila mmoja wetu anastahili kuhakikisha kuwa ameepuka vitendo vya kihalifu. Ni vyema mtu kuwaangaza wahalifu wakati wote. Vikosi vya polisi na wanajeshi vimefunzwa maarifa ya kukabiliana na kadhia za jinai na upelelezi. (4×1= 4)

Hotuba ya Lunga Kiriri- Kangata kwa walimu na wanafunzi gwarideni (uk 68-69). Hotuba hii ilisisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Anasisitiza kuwa: Suala la uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu. Misitu ilikuwa imevamiwa na viongozi wenye mate ya fisi. Baadhi ya vinara wa taasisi mbalimbali za umma wamewaacha wanyama kama mayatima kwa kuwapoka makazi yao. Maelfu ya maekari ya misitu yamefyekwa na kujengwa viwanda. Badala ya mibambakofi na miti mingine inayosafisha hewa, michai imetwaa nafasi yake. Wanaohusika na matendo haya wanapoulizwa hudai kuwa michai si adui ya mazingira! Wengine wanasema kuwa misitu haina budi kukatwa ili kupanda mimea inayotoa chakula, kwani jamii lazima ijitosheleze kwa chakula. La kuhuzunisha ni kwamba hawa hawa wanaosema hivyo ndio wanaokita majengo ya kifahari katika sehemu ambazo zinastahili kutengewa upanzi wa chakula! Wengine wamediriki kunyakua hata madhabahu kwenye Mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli kubwa za kitalii. Wazee wetu hata hawana mahali pa kuchomea kafara! Tunakata miti bila kupanda mingine. Hata mabustani ya maua tunashindwa kuyastawisha. Tukiendelea kuharibu mazingira sehemu yetu itazidi kuwa jangwa. (2×1= 2)

Hotuba ya Umu katika hoteli ya Majaliwasiku yake ya kuzaliwa. Umu anawashuku Mwangeka na Apondi kwa kuwa wazazi wake wema. Anawashukuru kwa kumsomesha. Anawashukuru kwa kumsaidia Dick kujiendeleza kimasomo. Mwangeka na Apondi wanamshukuru Umu kwa kuwapa furaha. Apondi anamshukuru kwa kumlea mdogo wao kwa maadili bora. (2×1= 2)

Hotuba ya Dick katika hoteli ya Majaliwa siku ya kuzaliwa kwa Umu. Dick anamshukuru Umu kwa msaada wake na ahadi ya kumlea. Anamkumbusha siku walipokutana katika uwanja wa ndege na ilivyokuwa muhimu kwake. Anamshukuru Umu kwa kumwelekeza kwa wazazi wao wale. Anawashukuru Apondi, Mwangeka na wanawe kwa ushauri wanaompa. (2×1= 2)

Mtahiniwa ataje hotuba kisha aeleze masuala muhimu yanayoibuliwa na kila moja.

Uozo katika jamii (alama 10)

Uozo ni hali ya kuzorota na kutozingatiwa tena kwa maadili mema katika jamii. Ni hali ambapo milazote na desturi njema huvurugwa na wanajamii wanaofanya mambo yaliyo kinyume nahali halisi ya maisha. Mwandishi amejadili suala hili kwa undani kama ifuatavyo;

Jamii inaendeleza ubakaji. Genge la mabarobaro watano lilifululiza hadi walipokuwa maskini Lime na Mwanaheri na kuwabaka mbele ya baba yao (uk 25).

Kuna ulanguzi wa dawa za kulevya. Dick alipotoroshwa na Sauna alipelekwa kwa tajiri mmoja aliyemwingiza katika kusafirisha dawa za kulevya kutoka nchi moja hadi nyingine (uk 119- 120).

Wanajamii wanaendeleza uporaji na wizi wa mali. Vijana wanawavamia watu, kuwaua na kupora katika maduka ya kihindi, kiarabu na ya waafrika wenzao.

Jamii inaendeleza ufuska/ ukahaba. Sauna aliiba watoto na kuwapeleka kwa mama mmoja aliyewatumia kwa biashara ya nipe nikupe (uk 84).

Biashara haramu inaendelezwa. Bi. Kangara alifanya biashara ya kuwauza watoto na vijana- Safari yake ilipata mkondo mwingine baada ya polisi kupata fununu kuhusu njama ambazo yeye na Bi. Kangara walikuwa wakiendesha. Mabibi hawa walikuwa na mtandao ambao kazi yake ilikuwa kuwauza watoto na vijana (uk 84).

Kuna tatizo la mimba za mapema. Vijana wana mazoea ya kukumbatia mtafaruku wa kuhisia unaowapata na mara hujipata wameambulia ujauzito kama alivyofanya Zohali (uk 98).

Baadhi ya wanajamii wanaendeleza uavyaji mimba. Sauna alijaribu awezavyo kuavya mimba na mwishowe, baada ya kushindwa, anaamua kujiua.

Kukiuka maadili ya kikazi. Fumba (mwalimu) anakiuka maadili ya kazi na kujihusisha kwa mapenzi na mwanafunzi wake, Rehema, na hatimaye kumpachika ujauzito (uk 102).

Wazazi wanawabaka wana wao. Babake Sauna anafanya mapenzi na mwanawe kila apatapo nafasi, na mwishowe, Sauna anapata mimba.

Starehe na anasa kwa vijana. Vijana wa vyuo vikuu wameshindwa kutofautisha usiku na mchana. Tindi anasahau kumrejesha Lemi nyumbani kutokana na muziki (uk 121).

Wazazi wanakwepa malezi na kuwatupa wanao wakiwa wachanga. Neema anampeleka mtoto aliyemwokota kwa polisi (uk 162).

Vijana kuwaiga wazee. Mwangemi na Mwangeka walikuwa na tabia mbovu ya kumuiga babu yao (uk 186). (10×1= 10)

Mtahiniwa afafanue kwa mifano kutoka katika riwaya.

Swali la insha 4

 1. Fafanua namna mbinu ya majazi ilivyotumiwa katika riwaya. 10
 2. Jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.  Al.10

Fafanua namna mbinu ya majazi ilivyotumiwa katika riwaya. 10

Ridhaa – Kukubali ama kutosheka. Mhusika Ridhaa anakubali na kutosheka na makuruhu aliyofanyiwa ya kuteketezewa mali na familia yake.

Bwana Tenge – Tenge ina maana ya fujo. Bwana Tenge anamfanyia mkewe fujo na vitimbi anamwendea kinyume mke wake, Bi. Kimai. Bwana Tenge anashiriki mapenzi na wanawake wengine.

Mzee Kedi – Neno kedi lina maana ya mambo yasiyopendeza, mambo ya hila pia ni kiburi.   Mzee Kedi anamfanyia ridhaa hila kwa kuhusika katika kuiangamiza familia yake.

Bwana Mkubwa – Mkubwa ni neno lenye maana ya cheo au hadhi kubwa. Bwana mkubwa ana cheo kikubwa serikalini.

Tetei – ina maana ya kutetea. Bi. Tetei ni mwanaharakati anayetetea haki za wanaume.

Mwalimu Dhahabu ni madini yenye thamani. Mwalimu dhahabu ni mwalimu anayekuwa wa msaada kwa Umulkheri

Hazina – Hazina ina maana mali iliyohifadhiwa. Mhusika Hazina anakuja kuwa kama hazina kwa Umukheri kwani anamfaa Umu jinsi alivyomfaa kwa kimpa noti ya shilingi mia mbili.

Zohali – Neno hili lina maana ya ajizi. Mhusika Zohali anapachikwa mimba akiwa kidato cha pili ni dalili ya uzembe na kutomakinika masomoni.

Chandachema – Chandachema ni jina lililoundwa kutokana na Chanda kidole) chema ambacho huvikwa pete. Mhusika huyu ingawa anapitia changmoto tele maishani anaishia kupewa ufadhili wa masomo(kuvishwa pete) na shirika la kidini.

Bwana Mabavu – Mabavu ni nguvu. Bwana Mabavu anatumia nguvu kumpoka babake Shamsi ardhi yake.

Mzee Maarifa- anatumia maarifa na hekima kuanzisha kituo cha kupigania hakiza kibinadamu.

Neema ni mkewe Mwangemi. Neema ina maana ya Baraka. Mhusika huyu anakuwa Baraka kwa mume   na pia kwa mwaliko.

Bwana Kimbaumbau ni mtu kigeugeu. Bwana Kimbaumbau anamsaliti Naomi kwa kutaka kufanya mapenzi naye.

Jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

vijana ni wasomi mf. Umu, tila.

Ni walanguzi wa dawa za kulevya mf. Dick.

Vijana wengine wa kike wakubali kukeketwa na wengine wanaaga dunia na kulazwa hospitalini mf. Tauma.

Vijana ni wapenda fujo.

Vijana hutumiwa na wanasiasa kutekeleza uovu na mauaji.

Ni dhihirisho kama wasio na huruma. K.m kuua wenzao bila huruma.

Wasio na msimamo dhabiti. Wanapotoshwa na wanasiasa bila kuwazia madhara waliosababisha.

Vijana ni wenye bidii katika kazi zao mf. Dick.

(Tanbihi: kadilia hoja za wanafunzi.) 10 x 1 = 10

Swali la insha 5

Jadili jinsi mwandishi wa riwaya hii alivyofaulu kutumia mbinu ya kinaya na sadfa. (alama 20)

Kinaya

 • Kinaya ni maelezo ya mambo kinyume na yalivyo.
 • Mwangeka anashiriki udumishaji wa amani Katika Mahariki ya kati huku familia yake ikiangamia nyumbani kutokana na ukosefu wa amani.
 • Mzee Kedi anaua familia ya Ridhaa ilhali ni yeye aliyethamini masomo ya wapwaze.
 • Ni kinaya wenye maduka kufunga milango wakati jumba la Ridhaa lilipochomeka badala ya kuyaacha wazi watu wotorokee .
 • Ni Kinaya Lunga Kirir kuachishwa kazi baada ya kutetea wanyonge wasiuziwe mahindi yaliyokuwa na sumu.
 • Ni kinaya Sauna kujifanya mzuri ilhali anawaiba watoto
 • Ni kinaya Neema kupeleka mtoto kwa makazi ya watoto na mwishowe kwenda kupanga mtoto huko
 • Ni kinaya Naomi kutoroka mmewe nawanawe ilhali hapo baadaye anajilaumu
 • Ni kinaya nchi ambayo ¡na miaka hamsini kuonekana kama mtoto wa mika hamsini
 • Ni kinaya kuwa wafrika wanakuwa wafanyikazi katika mashamba yao chini ya wakoloni
 • Ni kinaya watu walioishi na Ridhaa kwa amani wanawageukia na kuchoma nyumba yake pamoja na familia yake
 • Ni kinaya vijana kumbaka lime na Mwanaheri mbele ya wazazi wao
 • Ni kinaya mamakwe kufukuza subira kwa kuwa hawakuwa wa jamii moja
 • Ni kinaya mzee Maya kumbaka mwanawe Sauna
 • Ni kinaya wazazi wa Zohali ambao ni wasomi kumtesa Zohali kwa ajili ya ujauzito
 • Ni kinaya Tuama kusifu utamad uni wa tohara za kike iIhali ndio sababu ya kuwa hospitalini
 • Ni kinaya watu wan chi ya Wahafidhina kumkataa kiongozi wa kike na ndiye anayewafanyia kazi
 • Ni kinaya kwa pete kutaka kujia kwa kuwa na watoto watatu akiwa umri wa chini ya mia ishirini na moja   Hoja zozote 10 X1=10

Sadfa

 • Sadfa ni kuwaleta wahusika kadhaa pamoja bila kukusudiwa.
 • Selume kufikiria kustaafu katika hospitali ya uma wakati Ridhaa alikuwa anamalizia ujenzi wa hospitali ya Mwanzo Mpya
 • Umu kukutana ana Hazina alipokuwa akimtafuta.
 • Safari ya Umu kuchelewa inamfanya akutane na Dick katika uwanja wa ndege.
 • Mwangeka kukutana na Apondi katika karakana ni sadfa.
 • Ni sadfa Umu, Dick na Mwaliko kukutana katika Hoteli ya Majaaliwa.
 • Inasadifiana kuwa wakati Selume anapotaka kiacha kazi katika hospitali ya umma ndio Ridhaa anama liza kujenga hospitali ya mwanzo mpya
 • Siku ya kuzaliwa kwa Umu inasadifiana nay a Mwangemi
 • Inasadifiana wakati Neema akienda ofisini ana kiona kitoto kilichokuwa kimetupwa
 • Umu na Dick wanakitana kisadfa katika uwanja wa ndege
 • Ni sadfa Mwaliko kupangwa na binamuye mwangeka aliyempanga nduguye
 • Inasadifu kuwa Dick alipokuwa akiwaza juu ya nduguye Umu alikuwa nyuma yake
 • Kukutana kwa wana wa Lunga katika hoteli ya Majaliwa ni sadfa
 • Ni sadfa kuwa Umu anapowaza sana juu ya maisha yake wenzake wana matatizo kumliko Hoja zozote 10 X1=10

Swali la insha 6

Tathmini umuhimu wa mbinu zifuatazo katika kuijenga riwaya ya Chozi la Heri

 1. Nyimbo   (alama 10)
 2. Barua   (alama 10)

Nyimbo

Wimbo wa Shamsi unaonyesha ukengeushi,

Licha ya elimu aliyo nayo, Shamsi ameshindwa kukabiliana na changamoto za maisha. Anaingilia matumizi mabaya ya pombe.

Unabainisha ukosefu wa uwajibikaji, badala ya kutafuta mbinu ya kukabiliana na hali duni ya maisha, analalamika kwamba wenye nguvu hawakumpa kazi walizoziahidi.

Unakashifu unyakuzi wa ardhi za wanyonge. Shamba la kina Shamsi linachukuliwa na Bwana Mabavu.

Unachimuza ufisadi – Bwana Mabavu anawaonyesha hati miliki bandia na kuwafukuza shambani mwao

Unaendeleza maudhui ya ukoloni mamboleo – Mabavu anamiliki shamba la Baba ya Shamsi na kuwageuza kuwa maskwota.

Unaangazia ukiukaji wa haki za binadamu – Shamsi na wenzake wanafutwa kazi kwa kuwazia kugoma.

Inaonyesha umaskini wa familia ya Shamsi – Babake Shamsi anakufa kwa kula mizizi mwitu wenye vijaasumu

Unakashifu unyonyaji wa wafanyikazi – Shamsi na wenzake wanalipwa mishahara duni.

Unasawiri tatizo la matumizi mabaya ya vileo- Shamsi anaingilia ulevi baada ya kufutwa.

Wimbo wa Shamsi unaoghaniwa na Ridhaa

Wimbo wa majigambo unaosawiri tabia ya Shamsi – anajivunia na kusema kuwa anaogopwa kwa kutoka katika jadi tukufu.

Unamfanyia tashtiti Shamsi kwa kujisifu kwa kuzua mikakati ya kukabiliana na hali ya uhitaji na hali mwenyewe ni mlevi.

Unaonyesha uovu wa jamii – wauza pombe wanatia vijaasumu ili iwe tayari haraka bila kuwazia madhara ya watumia wayo. Zozote 10 X 1 = 10

Barua

Barua ya Lunga

Barua ya kustaafishwa kwa Lunga inaonyesha dhuluma kwa wafanyikazi. Lunga anafutwa kwa kutetea wanyonge dhidi ya kuuziwa mahindi hatari kwa afya.

Inaonyesha uadilifu wa Lunga anavyosema Afisa Mkuu Mtendaji

Inakashifu ukatili wa waajiri – Lunga anafutwa bila hali yake kuwaziwa

Inaonyesha mbinu-hasi za uongozi – Viongozi wanawaangamiza wanaowapinga njama zao za kiufisadi.

Kuonyesha uongo/ unafiki wa waajiri- kusingizia kuwa shirika linapunguza wafanyikazi kutokana na changamoto za kifedha kutokana na gharama ya uzalishaji mali ilhali Lunga anafutwa kwa kukashifu kutaka kuuza mahindi yaliyoharibika. (hoja 5)

Barua ya Subira

Inaonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa Subira – anaondoka bila kuwazia hali ya baadaye ya watoto wake.

Inadokeza maudhui ya malezi – Subira anamuusia Mwanaheri amtunze mnuna wake na pia wamtii baba yao.

Inakashifu ubaguzi – Subira analalamikia kubaguliwa na mavyaa Inaonyesha uwajibikaji wa mzazi kwa watoto wake japo Subira anaondoka anawaachia wanawe ujumbe kwamba ameondoka na kuwashauri

Anakashifu ukiukaji wa haki za kibinadamu – anasimangwa na kuitwa mwizi.

Inajenga tabia ya wahusika – imesawiri udhaifu wa nia wa Kaizari. Hamtetei mkewe dhidi ya dhuluma ya mavyaa. Inakuza ukatili wa mavyaa kwa kumwita muuki na mwizi.  (hoja 5)

Swali la insha 7

Matatizo mengi yanayowakumba wahusika wengi katika riwaya hii ni mwiba wa kujidunga. Jadili (al.20)

Wahusika katika riwaya ya Chozi la Heri wanakumbwa na matatizo mbalimbali. matatizo hayo ni ya kiuchumi na kijamii.

Vyanzo vya matatizo yenyewe ni tofauti tofauti, kuna yale yanasababishwa na wahusika wenyewe ilhali mengine yanaletwa na watu wengine.

Tunaweza kusema kuwa matatizo mengine ni mwiba wa kujidunga huku mengine yakiwa ya kudungwa na wengine.

 • Jumba moja la Ridhaa linabomolewa kwa kuwa alilijenga katika ardhi iliyotengewa ujenzi wa barabara katika mtaa wa zari. Hakuchunguza uhalali.
 • Terry mkewe Ridhaa anapuuza maonyo na maneno ya mumewe kuhusu mkasa ambao ungetokea hivyo anateketea.
 • Ami wamwangeka anaagamia katika mkasa wa moto alipoenda kuwasaidia watu waliokuwa wanateketea.
 • Walioteketea katika moto wa lori walijiigiza matatani wenyewe kwani walikuwa wameonywa kulikuwa na hatari.
 • Uhasama, migogoro na ukosefu wa mahitaji muhimu unaoikumba familia ya Mwimo Msubili hii ni kwa sababu ya yeye kuwaoa wake wengi.
 • Kufutwa kazi kwa Lunga Kangata Kiriri baada ya kukataa kukubali mahindi ya jano kuuziwa wananchi ni mwiba wa kujidunga.
 • Mauti yanayowakumba vijana waliokuwa wakiandamana baada ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi mpya.
 • Tendo la Subira kuondoka nyumbani na kumwacha mumewe
 • Pete anapokubali kuolewa na Nyangumi bila kufanya uchunguzi wa kina.
 • Tukio la Zohari kupata mimba na kutumbukia katika mateso mengi.
 • Tendi la Mwangeka na Mwangemi kufanyia babu yao mzaha, kwa kuwa usiku mmoja aliamua kuwalipua viboko.
 • Mwangeka anakubaliana na Tila kuigiza maombolezi ya Dedan Kimathi ambayo yanamfanya babake kumwadhibu kwa kutowajibika.
 • Kukamatwa kwa Sauna na mwajiri wake Bi. Kangara kwa kujihusisha na Biashara ya ulanguzi wa watoto.
 • Tuama anaathirika vibaya baada ya kupaswa tohara na kulazwa hospitalini ni tendo alilolitenda kinyume na mapenzi ya baba yake.
 • Walevi wenza wa Shamsi ambao wanapoteza uwezo wa kuona au uhai wao kwa kubugia vileo.
 • Mumwewe Selume anamfukuza mkewe kwa kuwa si wa kabila lake baadaye anamlea mtoto peke yake.
 • Mandu anapouawa katika vita akiwa ughaibuni ni mwiba kwani huenda hangepoteza maisha kama hangeenda huko mapema.
 • Fujo zinazosababishwa na uhafidhina baada ya uchaguzi ambapo wanapoteza uhai na mali.
 • Wakimbizi waliohamia katika mimea na baadaye kufukuzwa ulikuwa mwiba kwani si halali kulima msituni.
 • Naomi kumwacha mumewe Lunga Kiriri na watoto na baadaye kuwatafuta baadhi ya kifo cha bwanake ulikuwa mwiba wa kujindunga. Zozote (20 x 1) = 20)

Swali la insha 8

Jadili maudhui ya 'asasi ya ndoa' kama yalivyoangaziwa riwayani (alama 20)

Ndoa ni maafikiano rasmi baina ya mwanamume na mwanamke ili waweze kuishi pamoja kama mke na mume.

Ridhaa alikuwa na mke kwa jina Terry. Walibarikiwa kuwa na watoto wafuatao: Mwangeka, Tila na marehemu Dede. Ndoa hii haikudumu kwani janga la moto iiliisambaratisha aila hii na ndipo Terry, Tila, Lily na Becky wakaiaga dunia. Ridhaa akabaki mjane.

Mwangeka alikutana Lily Nyamvula katika chuo kikuu na kumwoa. Walibarikiwa na mtoto mmoja kwa jina Becky. Ndoa hii haikudumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto.

Baada ya ndoa ya mwanzo kusambaratika, Mwangeka alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa.

Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema. Hawakufaulu kupata mwana wao kindakindaki japo walipanga mwana wao kwa jina Mwaliko.

Kangata alikuwa na mke wake kwa jina Ndarine. Walibarikiwa na wana wafuatao. Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri.

Lucia Kiriri - Kangata - alikuwa ameolewa Kangata walishangaa mwana wao akaozwa kwa watu ambao huvaa nguo nje na pia huzaa majoka.

Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira. Waliborika no mabinti wawili, Lime na Mwanaheri.

Lunga alikuwa na mke kwa jina Naomi. Walikuwa wa watatu, Umu, Dick no Mwaliko. Ndoa hii haikudumu

mahari kutoka kwa buda mmoja kwa jina Fungo aliyemuoa kama bibi wa nne. Ndoa hii haikudumu kwani Pete alihiarikumwacha baba huyu.

Mwanafunzi aongezee hoja. Zozote

Swali la insha 9

Kwa kutumia hoja kumi kumi eleza jinsi maudhui ya utu na uozo wa kijamii yalivyoshughulikiwa katika Chozi la Heri (alama 20)

Maudhui ya utu katika chozi la heri

 • Dkt.Ridhaa anaonekana kujawa na utu kwa kudhamini masomo ya wapwa wawili wa mzee Kedi.
 • Ridaa alijenga kituo cha afya cha mwanzo mpya ili kunusuru maisha ya binadamu waliokuwa wakiangamia kwa kukosa huduma bora za afya
 • Mwangeka na Apondi walikubali kumchukua umu na kuwa motto wao wa kupanga.
 • Kiriri aliyekuwa mwajiri wa kangata alionyesha utu kwa kumwacha kangata afaidi ardfhi yake kiasi cha kuchukuliwa kuwa wanatoka mbari moja na kangata
 • Neema anaonyesha kujawa na utu kwa kitendo cha kumwokota mtoto Immaculata aliyekuwa ametupwa jaalani akampekeka pamoja na mwanapolisi wakampeleka katika kituo cha watoto cha Benefacto.
 • Mtawa Gizarina wa kituo cha kituo cha benefactor alikuwa na utu kwa kuwa alijitoa kuwapokea watoto mbali mbali waliohitaji msaada wa malezi.
 • Mtawa pacha aliyemhudumia zohali, baada ya kupata mimba na kuteswa na wazazi
  wake, alimtafutia shule ili aendelee na masomo aliyokuwa ameachishwa mashirika ya kidini yalitoa misaada kwa waadhiriwa wa majanga mbali mbali katika jamii. Wakristo nawaisilamu waliungana pamoja kutoa msaada katika kambi waliotimuliwa kutoka kwao.
 • Shirika la jeshi la wajana wa Kristo lilidhihirisha utu lilipoamua kujenga makao ya watoto yatima.
 • Watoto waliotupwa na wazazi wao na wenye wazazi wahitaji. Chanda chema alipata msaada kupitia kwa shirika hili.
 • Shirika la kidini la lakikisho la itaki na utulivu linadhihirisha utu kwa kuwasaidia watoto kupata elimu bora. Chanda chema anasaidika kuendelea na masomo yake kupitia shirika hili.
 • Tulia alimsaidia Kaizari kufunganya na kumsindikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka kutoka kwake.
 • Katika hospitali aliyofanya kazi Selume,kuna mgonjwa aliyepelekwa na wasamaria wema katika hospitali baada ya kuumizwa katika mgogoro wa kupigiana ardhi katika eneo la Tamuchungu.

Maudhui ya uozo wa maadili katika jamii ya chozi la heri.

 • Ubakaji. Lime na mwanaheri walibakwa na mabarobaro watano mbele ya macho ya wazazi wao.
 • Ulanguzi wa dawa za kulevya. Dick anaifanya kazi ya kusafirisha dawa za kulevya kutoka nchi moja hadi nyingine.
 • Uporaji na wizi-vurugu za baada ya uchaguzi alipochacha vijana walivunja maduka ya waarabu, wahindi na hata waafrika wenzao.
 • Mauaji-kendi anaichoma nyumba ya Ridhaa ambapo aila ya Righaa inachomeka.
 • Unyakuzi wa ardhi watu wamejinyakulia maelfu kwa maelfu ya ekari wakajenga Viwanda na maduka ya kibiashara kuwaacha wenyeji bila hata makazi.
 • Uendelezaji wa biashara haramu-Bi.kanagara walishirikiana na sauna Katika kutekeleza biashara ya kuwauza watoto
 • Kuavya mimba-Baada ya sauna kubakwa na baba yake wa kambo(bwana maya) mamake Sauna anamshurutisha kuavya mimba hiyo.
 • Kutupwa kwa watoto wachanga. Neema anamwokota mtoto katika jaala na kumpeleka katika Makazi ya watoto ya benefactor.
 • Mapenzi ya baba na bintiye (Sauna).
 • Ukabila-huu unajitokeza baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya mwanamke ambapo majirani waliwagueuka wenzao waliokuwa wametoka kwa kabila tofauti
 • Matumizi ya pombe haramu - Vijana wanasomea shahada za uzamili wanajihusisha na unywaji wa pombe haramu na kufariki.
 • Ukeketaji wa watoto wa kike - Tauma anaelezea kuwa asingepashwa tohara asingeolewa.
 • Ndoa za mapema-Pete anaozwa kwa mzee fungo kama mke wake wane
 • Ufisadi katika mtaa wa tononokeni kuna watu waliojenga majumba yao katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara
 • Uuzaji wa mahindi yaliyoharibika-Lunga alipigwa kalamu baada ya kugundua mahindi yaliyokuwa yametoka ughaibuni yalikuwa hatari kwa usalama ,hata wa panya.
 • Kuajiriwa kwa watoto wadogo ambao hata vifua havijapanuka watoto walinyakuliwa na kupelekwa sehemu mbali mbali nchini kufanya kazi.
 • Kutupwa kwa taka karibu na nyumba za watu-katika mtaa wa mabanda wa somber Anakoishi Bw.makiwa taka linamwagwa katikati mwa msongamano wa kibanda Kutoka kwa waishipo waheshimiwa. "Nimekuja kuwakombao...."

Swali la insha 10

Jadili ufaafu wa anwani Chozi la Heri.

Mwandishi anatueleza kuwa Ridhaa alipoenda shuleni siku ya kwanza alitengwa na wenzake kwani hawakutaka ashiriki michezo yao. Kijana mmoja mchokozi alimwita 'mfuata mvua' Ridhaa alikuja kuwashinda katika mitihani yote. Ridhaa alifululiza nyumbani na kujitupa mchangani na kulia kwa kite na shake.

Mamake alimliwaza na kumhakikishia kumwona mwalimu keshoye. Tangu siku hii, huu ukawa ndio mwanzo wa maisha ya heri kwa Ridhaa kwani baada ya mwalimu kuzungumza na wanafunzi umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano, Ridhaa alipaa kwenye anga ya elimu hadi kufikia kilele cha elimu na kuhitimu kama daktari.

Ridhaa alipotoka kwenye Msitu wa Mamba alijiona nafuu kwani wapwa zake Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu. Dadake Subira alitibiwa akapona. Mwamu wake Kaizari amepona donda lililosababishwa na kuwatazama mabinti zake wakitendewa ukaini(kubakwa) na vijana wenzao. Ridhaa anajua kuwa Kaizari ni afadhali kwa sababu hakuna aliyemtenga na mmoja kati ya jamaa zake. Ridhaa anapomfikiria Kaizari anajiambia heri nusu shari kuliko shari kamili.

Ridhaa aliposikia sauti ya kike ikitangaza, tangazo lile lilimrudisha katika mandhari yake ya sasa. Alijaribu kuangaza macho yake aone anakoenda lakini macho yalijaa uzito wa machozi ambayo alikuwa ameyaacha yamchome na kutiririka yatakavyo.

Wakati Ridhaa alimkazia macho Mwangeka-waka Mwangeka alikuwa akijiuliza iwapo babake amekuwa mwehu kwa kukosa kushirikiana na majirani kuchimba kaburi kuyazika majivumatone mazito ya machozi yalitunga machoni mwake Mwangeka. Akayaacha yamdondoke na kumcharaza yatakavyo. Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa machozi haya uliulainisha moyo wake, ukampa amani kidogo. Moyo wake ukajaa utulivu sasa kwa kujua kuwa wino wa Mungu haufutiki.
Wakati Ridhaa_ alikuwa akimsimulia Mwangeka msiba uliyomwandama tangu siku alipoondoka kwenda kuweka amani Mashariki ya Kati Ridhaa alisita akajipagusa kijasho kilichoku- wa kimetunga kipajini mwake kisha akatoa kitambaa mfukoni na kuyafuta machozi yaliyokuwa yameanza kumpofusha. Uk 48 Mwangeka alipokuwa ameketi mkabala na kidimbwi cha kuogelea mawazo yake yalikuwa kule mbali alikoanzia.

Akawa anakumbuka changamoto za ukuaji wake. Akawakumbuka wana wake. Alipomkumbuka Annatila(Tila) mwili ulimzizima kidogo akatabasamu kisha tone moto la chozi likamdondoka. Katika Msitu wa Simba kulikuwa na maelfu watu waliogura makwao. Kati ya familia zilizoguria humu ni familia ya Bwana Kangata. Kwa Kangata na mkewe Ndarine, hapa palikuwa afadhali kwani hawakuwa na pa kwenda kwa kuwa hata kule walikokuwa wakiishi awali hakukuwa kwao. Uk 57

Wakati Dick walikutana kisadfa na Umu katika uwanja wa ndege, walikumbatiana kwa furaha. Machozi yaliwadondoka wote wawili na wakawa wanalia kimyakimya. Walijua fika kuwa jaala ilikuwa imewakutanisha na kwamba hawatawahi kutengana tena. Maisha sasa yalianza kuwa ya heri kwao. Baada ya miaka kumi ya kuuza dawa za kulevya, Dick alifaulu hatimaye kujinasua kutoka kwa kucha za mwajiri wake. Alianza biashara yake mwenyewe ya kuuza vifaa vya umeme 189 :111 P Sasa akaanza kujitegemea kwa kuwa amejiajiri. Alikuwa ameu fungua ukurasa mpya katika maisha yake. Maisha yake sasa ni ya heri.

Wakati Neema na Mwangemi walikabidhiwa mtoto wao wa kupanga na Mtawa Annastacia, Mwaliko alimkumbatia Neema na kumwita mama na kumwahidi kuwa ataenda naye. Neema alidondokwa na chozi la furaha na kumkumbatia Mwaliko kwa
mapenzi ya mama mzazi. Hili lilikuwa ni chozi la heri kwa Neema. (mwanafunzi aongezee hoja)

(Hoja zozote 20 x 1 = 20)

Swali la Insha 11

Maovu yametamalaki katika riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha (al 20)

 • katika jamii hii kuna biashara haramu kama ile ya uuzaji wa dawa za kulevya. Dick alipotekwa nyara alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wamiaka kumi
 • kuna ukabila, suala la ukabila linajitokeza wakati kulizuka vita vya baada ya kutawazwa kwa mwekevu
 • usaliti mzee kedi anamgeukia Ridhaa na aila yake
 • malezi mabaya-mamake sauna kuficha tendo la babake sauna kumpachika mimba
 • uuzaji wa Watoto-mtandao wa walanguzi wa bi kangara
 • kutupa mtoto baada ya kujifungua -Riziki immaculate
 • wizi na uporaji wa mali yaw engine- wakati vita vya baada ya kutawazwa kuzuka , watu walionekana kupora maduka ya kihindi,kiarabu n ahata waafrika wenzao
 • wanawake kuavya mimba katika jamii hii- sauna anaavya mimba ya babake
 • ndoa za mapema- wasichana kuozwa kwa vikongwe kama pete
 • matumizi ya pombe haramu – vijana wa vyuo vikuu wanabugia na kufariki
 • kutowajibika kwa wasimamizi wa hospitali -ukosefu wa dawa
 • visingizio- Lemi anasingiziwa
 • Dhuluma kwa wafanyikazi kv Naomi na mwajiri wake
 • kuna mauaji- watu wengi walipoteza wapendwa katika ghasia za baada ya uchaguzi
 • ubakaji- lime na mwanaheri wanabakwa
 • Wanawake wanawacha waume na aila zao- umulkheri wanaachwa
 • wazazi wanahusiana kimapenzi na wana wao mfano ni Sauna
 • wazazi wa zohali wanamwachia kazi zote hii ni ajira kwa watoto
  (Zozote 20x1=10)

Swali la Insha 12

Mwandishi amejadili kwa kina maudhui ya mapuuza. Thibitisha . (alama 20)

 • Viongozi kuharibu misitu. Msitu wa Mamba. Kukata miti ya makaa na mbao.
 • Mwalimu kupachika mwanafunzi mimba. Fumba kwa Rehema 
 • Kutupa mtoto kwenye taka. Aliyeokotwa na Neema.
 • Kuacha familia. Annete. Naomi. Subira
 • Kutorudi nchini. Wanawe Kiriri wanakatalia ughaibuni badala ya kurudi kumsaidia biashara na kujenga nchi 
 • Kutogharamia malezi. Fumba kuachia Chandachema nyanyake.
 • Kumwaga taka. Mtaa wa Sombera
 • Wanasiasa kupuuza vijana baada ya kuwafanyia kampeni.
 • Kutahiri wasichana. Tuama. Wasichana wanakufa
 • Kupuuza umuhimu wa masomo. Zohali kufanya mapenzi akiwa shuleni na kupachikwa mimba.
 • Mamake Umu kukataa kusaidia ombaomba
 • Kuuzia raia mahindi yaliyoharibika.
 • Raia kupokea hongo. Wanapuuza jukumu lao la kuboresha uongozi. Papa anatoa hongo na basi kuendeleza uongozi mbaya.
 • Tindi kupuuza ushauri wa mama kutorudi nyumbani baada ya saa kumi na moja magharibi na anarudi siku inayofuata. Kifo cha Lemi. 
 • Terry kupuuza Ridhaa kuhusu milio ya bundi kuwa mbiu ya mgambo na kuishia kuchomwa na Kedi.
 • Kupuuza kuelekeza mtoto. Wazazi wa Zohali waliodhalilisha badala ya kumwelekeza alipopata mimba na akatoroka nyumbani.
 • Polisi kurusu magari makuukuu barabarani kwani yanamilikiwa na miamba isiyogusika
 • Viongozi kutoimarisha viwango vya
 • Sauna/ Umu. Kutenganisha na nduguze.
 • Fumba/ Rehema. Mimba na kumkatiza masomo
 • Fumba/ Chandachema. Kutokea
 • Satua/ Chandachema. Kuteta vitu vidogo kuisha na alijua hana walezi.
 • Tenge/Kimai. Kuwa na uhusiano nje ya ndoa
 • Maya/ Sauna. Kumbaka
 • Kimbaumbau/ Naomi. Kumtaka mapenzi kumsingizia, kumtusi na kumfuta kazi.
 • Wazazi wa Zohali/ Zohali
 • mlevi/ Pete. Kumbaka
 • Pete/ kitoto chake cha pili
 • Mama Pete/Pete. Kumwachia nyanya ulezi bila kutuma mahitaji
 • Mama na wajomba wa Pete/ Pete. Kumkatizia masomo ili wamwoze kwa Fungo aliye na wake watatu tayari.

Swali la Insha 13

Wananchi katika riwaya hii wanasaidiana na kuinuana katika maisha. Jadili kweli wa kauli hii kwa kutoa mifano ishirini, (al. 20)

 1. Ridhaa anawalipia wapwazo Kodi kavo.
 2. Anawajengea maskini hospitali
 3. Wakimbizi kwenye msitu wa mamba wanawapa chakula wale ambao hawakuwa nacho. (nafaka)
 4. Mothers union, Ewa, Guild Ansaa - wanawa pelekea wakimbizi chakula
 5. Anampanga umu - Anamsaidia Dick alipotaka kunzisha biashara
 6. Anampa babake hifadhi baada ya kurudi kutoka mashariki ya kati
 7. Umu - angempa nduguye chakula alipokuwa mdogo
 8. Lunga - anawatetea wananchi ili wasiuziwe mahindi haramu
 9. Tenge - anampa makao Chanda Chema
 10. Dhahabu - anamsaidia umu kupata udhamini wazazi
 11. Bi Tamasha anamsaidia Chanda chema kupangwa na familia ya Tenge
 12. Mwangemi na neema - Kumpanga mwaliko na kumpa malezi mazu
 13. Raia wanaojaribu kumwokoa Lemi na kumtopeleka hospitali
 14. Dick - anawaajiri vijana wenzake
 15. Hazina - Kumsaidia umu kupata makao Kumnunulia cjhakula
 16. Pacha - Kuwasaidia watoto mayatima. Kupata makao, malezi chakula mapenzi na elimu. Ikuwahifadhi waliotoroka kwao
 17. Kaizani - wakiwa ukimbizini aliwasaidia wakimbizi na wazo la long drops hivyo kupunguza magonjwa
 18. Aliyekuwa wazi - anasaidia kupanga water hivyo kuepusha sintofahamu
 19. Selume + Meko - Licha ya kuwapa wagonjwa matibabu wanawapa ushani pia. Wengi wamefaidi.
 20. Mzee Maarifa- anafanya juhudi za kukomesha tohara/mila na tamaduni zilizopitwa na wakati
 21. Tetei - Anawatetea. Anawatetea watoto wa kiume dhidi ya unyanyasaji
 22. Neema - anakiokota kiokota kitoto riziki Immaculata na kukisaidia kupata makao
 23. Kairo, chandachema, zohali na Lemi wanampa mawaidha umu na kumsaidia kuutua mzigo mzito wa mawazo
 24. Mkewe kuwa alimpa Jairo zawadi

Swali la Insha 14

Tambua mandhari yoyote manne na umuhimu wake katika Riwaya ya chozi la Heri. (alama 20)

 1. Nyumbani kwa Ridhaa 
  • Kuzua maudhui ya vifo- aila yake innangamizwa
  • Maudhui ya utani-alivyotaniana na mkewe Terry
  • Ushirikina- Ishara zilizoonyesha maafa-mlio wa bundi
  • Ukabila-Mzee Kedi kuangamiza kwa sababu ni’ mfuata mvua’
  • Kuzua tabia ya wahusika –Mzee Kedi –mkabila
 2. Msitu wa Mamba
  • Kuendeleza ploti-Kaizari anasimulia yaliowakuta baada ya kutawazwa kwa Mwekevu
  • Kudhihirisha matatizo yanayowakumba wakimbizi wa ndani kwa ndani kama njaa, maradhi, makaazi duni, ukosefu wa vyoo, vifo vya watoto
  • Kudhihirisha usawa miongoni mwa watu ambao awali walikuwa na nyadhifa mbalimbali ; maskini kama Makiwa na  matajiri kama Ridhaa na Kaizari
  • Kusawiri jinsi ukabila huasambaratisha ndoa- Selume
  • Kuonyesha juhudi zinazofanywa  kukabiliana na matatizo;
   Vyoo-ujenzi wa long-drop
   Njaa- vyakula vya msaada kutoka kwa mashirika
  • Kudhihirisha matatizo yanayotokana na vururgu baada ya uchaguzi jinsi yalivyosimuliwa na Kaiari
  • Kituo cha Mwanzo mpya
  • Kuonyesha changamoto zina zokumba hospitali za umma-Selume  anashangaa mama alivyoweza kustahimili matatizo kama vile ukosefu wa glavu hospitalini
  • Kuangazia suala la ufisadi-dawa zilizotegemewa hospitali zinauzwa na wasimamizi wa hospitali –Ruzuku kutolewa kwa wasiostahili
  • Kuendeleza ploti-Kupitia sadfa –kituo kinakamilika wakati Selume anajiuzulu anapata kazi katika kituo hiki na mkondo wa maisha yake kubadilika.
  • Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa wasimamizi wa taasisi za umma-Hospitali haijalipia umeme
  • Kuonyesha migogoro inayosababishwa na tama ya rasilimali-Mgonjwa analemazwa  katika mapigano ya kung’ang’ania ardhi
 3. Mandhari ya shule ya  Upili  ya Tangamano
  • Kuendeleza ploti wakati wasichana hawa wanavyohadithiana matatizo waliokumbana katika maisha yao
  • Ufaafu wa anwani kila msichana anapata heri katika shule hii kama Zohali
  • Madhui ya ukarimu-Mtawa Pacha alivyomsaidia Zohali na Kitoto chake
  • Umu naye kupitia kwa shule hii ana matumaini ya kusoma hali kuwa wakili wa kutetea haki za watoto
  • Kuibua tabia za wahusika wengine-Mamake Zohali alishindwa kumsaidia Zohali alipopata ujauzito mpaka akatoroka kwa sababu ya kazi nyingi.
  • Shuleni na masimulizi yao yanaibua toni ya matumaini- kwamba kuna maisha zaidi ya matatizo walioyapitia awali
 4. Mandhari katika uwanja wa ndege
  • Chozi la heri –kwamba hata ingawa familia yake ililiangamia katika moto-Mwanawe Mwangeka yu hai kwa sababu alikuwa ughaibuni
  • Mbinu rejeshi-Ridhaa analivyokumbuka siku ya kuhawailishwa kutoka Msitu wa Mamba hakuwa na matumaini ya maisha bora kwani hakuwa na mwenzi wala mtoto wa kuendea.
  • Ukabila –kupitia kwa Ridhaa selume hakujua ataenda wapi kwani mumewe alikuwa ameoa msichana wa kikwao.
  • Sifa ya Ridhaa –mfariji-alimkumbusha Selume kuwa angalau mtoto wake Srah alikuwa hai na salama kwa babake ilhali yeye familia yake ilikuwa imeangamia
  • Alipata mafunzo ya umuhimu wa kutangamana na watu wakiwa wakimbizi-thamani ya binadamu.
  • Ni katika Msitu wa Mamba  Ridhaa alipata ushauri nasaha na kuweza kukabiliana na  tatizo lake la shinikizo la damu  lililotokana na mshutuko wa kupoteza jamaa yake na mali yake kwa dafrao moja.

Swali la Insha 15

Fafanua nafasi ya vijana katika jamii kwa mujibu wa Riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)

 • Nafasi ya vijana imeshughulikiwa pia katika kazi hii. Kuna maswala mbalimbali yanayoendelezwa au kuwakumba vijana. Mifano kutoka riwayani:
 • Elimu inayotolewa kwa vijana haiwawezeshi kuwa katika nafasi ya kuzalisha mali katika maisha yao. Hata wale waliosoma hadi vyuo vikuu na kupata shahada za ukapera, uzamili na uzamifu hawajapata nafasi ya kujipatia kazi; ila wao huwa katika nafasi ya kukariri nadharia walizofunzwa bila kujitegemea maishani mwao. Hii ina maana kwamba stadi zinazotolewa katika vyuo vikuu haziwapi wanafunzi nafasi ya kushiriki kikamilifu katika uzalishaji wa mali na raslimali.
 • Swala lingine kuwahusu vijana ni kuwa hawako katika nafasi ya kujiajiri kutokana na ukweli kwamba hawana mataji wa kuanzisha biashara ambazo zinaweza kuzalisha nafasi za kazi kwao na kwa jamii kwa jumla. Hali hii inayafanya maisha ya vijana kuwa magumu ziaidi.
 • Viongozi wanawahimiza vijana kurudi mashambani katika maeneo gatuzi yao, ili wakazalishe mali huko. Tatizo ni kwamba baadhi ya vijana hawana mashamba ya kuzalisha mali kutokana na mashamba haya kuuziwa watu wengine na aila zao. Hii ndiyo sababu inayowafanya vijana kushindwa watarudi mashambani wanakohimizwa warudi wakafanye nini!
 • Vijana wana jukumu la kuelemishana kuhusu nafasi ya kila mmoja wao katika kuuboresha uongozi uliopo sasa kwa kuzalisha nafasi za kazi. Vijana hawa wanapasa kutumia vipawa vyao kwa njia endelevu, ili kusaidia katika kuzalisha nafasi za kazi badala ya kungojea serikali iwatafutie kazi. Hii ina maana kwamba, vijana hawapasi kungoja wafanyiwe kila kitu na serikali.
 • Vijana wana jukumu la kutambua kwamba wanatumiwa na viongozi kwa minajili ya kutimizwa matakwa yao ya kisiasa. Mwangeka anawashukuru vijana kwa kutambua kwamba wanatumiwa na viongozi wenye tama kuzua vita na mauaji yasiyokuwa na sababu maaalum.
 • Vijana wanakumbwa na hali ya mtafaruku wa kihisia kutokana na umri wao mdogo unaoufanya damu yao kuchemka. Baadhi yao huingilia swala la mapenzi kwa pupa na kuishia kuambulia ujauzito. Umri wa ujana wa Zohali unamfanya kuingilia maswala ya mapenzi ambapo hatimaye anaambulia ujauzito usiotarajiwa.
 • Viajana ni watu wanotafuta njia za kuyamaliza alu kuyapunguza matatizo yanayowakumba kwa nljia moja au nyingine. Chaurembo anafanya kazi katika shamba la majanichai kama njia ya kumpunguzia mzigo mfadhili wake kwa jina Bwana Tenga. Kidogo anachopata kutokana na kazi hii anakitumia kununulia sare za shule na adaftari.
 • Vijana ni watu wanaofuata utamaduni wa jamii zao. Tuama na wasichana wengine wanashiriki katika itikadi za tohara za jamii yao. Wanaamini kwamba msichana hawezi akaolewa kama hajapshwa tohara. Hata hivyo, wengi wao wanaaga dunia kutokana na tohara hii.
 • Vijana hukumbwa na mabadiliko mengi wanapoendelea na kukua. Baadhi ya mabadiliko hayo huwa ni ya kimwili na kimaumbile. Sare za awali za Pete zinapoanza kukata mwili kutokana na iukuaji wake ananunuliwa nyingine na mamake. Hii ina maana kwamba ukuaji wa maumbile ya msichana huyu umeanza kufanya kazi.
 • Vijana wana uhuru wa kujichaguliwa wake aul waume watakaowaoa. Nyanyake Pete anataka mjukuu huyu wake ajichagulie mume wa kumuoa baada ya kutimiza maazimio yake ya elimu. Hata hivyo, wajomba wake na mamake wanamshurutisha kuolewa na Fungo ambaye ni mzee mwenye wake kadhaa, jambo ambalo hapendezwi nalo. Hatimaye anatoroka kutoka kwa mumewe mzee huyu.
 • Vijana wanalaghaiwa kwa urahisi na watu wenye pashau ya kujitajirisha kwa kuahidiwa kazi nzuri kule ughaibuni ambazo kwa hakika hazipo. Vijana wanauzwa ng’ambo kupitia mtandao mpana wa Bi. Kangara bila ufahamu wao watakumbana na kazi duni kuliko za nchi yao. Baadhi yao wanateswa na waajiri wao. Inakuwa ni bora kama wangeishi nchini mwao kuliko kwenda huko ng’ambo ambako wanakumbana na maisha magumu zaidi kuliko yale yaliyoko nchine mwao.

Swali la Insha 16

Tathmini umuhimu wa usimulizi wa Pete katika kuijenga Riwaya Chozi la Heri.    ( alama 20)

 • Kuonyesjha shida zinazokumba ndoa k.m Pete na babake
 • Kukashifu uavyaji mimba km. Pete kumeza vidonge
 • Kuchimuza maudhui ya umaskini km. Pete hana sodo
 • Kuendeleza maudhui ya utamaushi km. anaamua kunywa sumu ya panya afe
 • Kuonyesha maudhui ya mapuuza km. nyanyake pete anawarai wajomba kutomwoza Pete kwa Fungo lakini wanampuuza.
 • Kujenga maudhui ya utu km. anamlea pete baada ya kukanwa na babake mzazi
 • Kuendeleza maudhui ya elimu. Pete alikuwa darasa la saba akiozwa kwa fungo
 • Kukashifu ndoa za lazima km. 
 • Kudokeza athari za tohara ya wasicjhana km. 
 • Kuendeleza maudhui ya uwajibikaji km. nynyake anapinga tendo la kumwoza pete
 • Kubainisha changamoto zinzokumba ndoa ya mitara
 • Kukashifu ubaguzi wa kijinsiia km. pete anakatizwa masomo ili nduguze wasome
 • Kuchimuza maudhui ya utegemezikm Pete anategemea wanaume kukilisha kitoto
 • Kuendeleza maudhui ya usaliti
 • Kuomnyesha madhara ya ulevi – mlevi mmoja anambaka pete
 • Kuendeleza maudhui ya mabadiliko – pete anataka kubadilisha ,ustakabali na kuamua kutoishi
 • Kukashifu ukiukaji wa hakli za wafanyakazi
 • Kuonyesha ukiukaji wa haki za watoto
 • Anajenga sifa za wahusika 
 • Ukatili wa mamake pete unabainika anapomwoza pete akiwa darasa la saba
 • Kuendeleza ploti ya Riwaya. 


Swali la Insha 17

Fafanua jinsi riwaya ya chozi la Heri ililenga kuiadilisha jamii. (ala. 20)

 • Kupitia kangara na Sauma, tunafunzwa kuwa uovu wa ulanguzi wa watu humfanya mtu afungwe jela.
 • Tunaadilishwa kuwa watu hawafai kutumia misala ua kupeperushwa. Wakimbizi wa msitu wa mamba wanakabiliwa na kipindupindu na homa ya matumbo; wengi wanakufa
 • Tunausiwa kuwa wanawake kama Naomi ambao hawapendi ndoa zao hujutia maamuzi yao baadaye.
 • Kupitia kwa aila ya Kaizari, tunausiwa kuhusu umuhimu wa kufunza mazingira.
 • Kpitia kwa wahusika kama lunga, tunafinzwa umuhimu wa watumishi wa umma kutumikia wananchi kwa uadilifu.
 • Kupitia kwa Pete, tunausi kuhusu shida wanazopitia wasichana wadogo wanaoozwa kwa mibaba; tunausiwa kuuepuka.
 • Kupta kwa Tuama, tunausiwa umuhimu wa kupigana na desturi ya zamani ya kukeketa wasichana.
 • Kupitia kwa Dickson, tunausiwa kuwa mui huwa mwema, kwamba vijana wanaweza kubadilisha tabia zao mbaya ya kulangua dawa za kulevya.
 • Kupitia kwa Dickson, tunaadilishwa kuwa vijana wanaweza kutatua tatizo la uhaba wa ajira kwa kujiajiri.
 • Kupitia Lemi, tunausiwa umuhimu wa kutochukua sharia mikononi mwetu; kwa upigaji kitutu wa watu unaweza kuua watu ambao hawana hatia.
 • Kupitia kwa Ridhaa tunausiwa umuhimu wa kupenda kazi na kujitolea kuwa msaada kwa ndugu zetu- anasanbaza naji ya mabomba kijijini.
 • Kupitia kwa Mwekevu, wanawake wanausiwa kuwa vijana hawafai kupigana na walinda usalama, ni kupiga ngumi ukuta!
 • Tunaadilishwa kuwa walimu hawafai kuwa na uhusiani wa kimapenzi na wanafunzi wao. Fumba anamringa Rehema na kuzaa Chandachema ambaye anatelekezwa.
 • Tunaadilishwa kwa mashariki kama CWA, Ansar Mwangaza na Shirika la Makazi Bora tunausiwa kuhusu nafasi ya mashirika ya kijamii katika maendeleo ya nchi.
 • Tunaadilishwa kuwa raia wanafaa wapende nchi zao. Annette na songoa wanahamia ughaibuni na kumsononesha Kiriri.
 • Tunafunzwa umuhimu wa kutambua makosa yetu na kupenda kazi. Naomi anatambua makosa yake na kujifunza umuhimu wa kufanya kazi kwa kujiajiri.
 • Tunausiwa kuzika tofauti zetu na kupanga maisha yetu upya. Ridhaa anakubali majaaliwa yake na kujenga nyingine katika mtaa wa afueni.

Swali la Insha 18

Riwaya ya Chozi la Heri ni ya Utamaushi jadili kauli hii (alama 20)

utamaushi ; ni ile hali ya kukata tamaa kwa jambo Fulani maishani. Wahusika mbalimbali waliweza kukata tamaa kwa njia moja aua nyingine;

 • Pete anakata tamaa maishani baada ya kupata watotto watatu akiwa chini ya miaka shirini na moja jambo linalomfanya kutaka kujiua
 • Ridhaa mkewe na familia yake ilipoangamia kwa moto alikata tamaa ya mapenzi katika maisha yake
 • Zohali licha ya kuzaliwa katika familia ya tabaka la juu anakata tamaa katika maisha na kuingia mtaani kutumia gundi na wenzake
 • Mwangemi na Neema wanakata tamaa ya kupata mtoto na kuamua kupanga Mwaliko
 • Shamsi anakata tamaa ya kupata kazi na kudhamini pombe licha ya kuwa wa kwanza kuingia chuo kikuu kutoka eneo lao’
 • Naomi anakata tamaa kuishi na Lunga na kuamua kwenda kutafuta kazi mjini
 • Naomi anakata tamaa kuishi mjini na kurudi msitu wa samba ila anakuta Lunga aliaga na watoto wakaondoka
 • Umu anakata tamaa ya kupata nduguye hasa baada ya kugundua kuwa hapati usaidizi katika kituo cha polisi
 • Mwanaheri anakata tamaa baada ya kifo cha mamake Subira
 • Subira anakata tamaa ya kuishi kwa Kaizari kutokana na chuki ya mamamkwe kwa kiini kuwa hawakuwa wametoka katika jamii moja
 • Lunga anakata tamaa ya maisha baada ya kuachishwa kazi, kunyakuliwa kwa mazao yake na kuachwa na mkewe jambo linalosababisha kufa kwake
 • Chandachema anakata tamaa baada ya nyanya yake kufariki na kunyanyaswa na jirani yake satua.

Swali la Insha 19

 1. “Nina wazazi wawili, ila hawa ni wazazi tu, hawajadiriki kuwa walezi wangu, wala jina ‘mlezi’ haliwaafiki.”
  Onyesha jinsi kauli iliyopigwa mstari inavyowaafiki baadhi ya wazazi katika Jumuiya ya Wahafidhina ukirejelea riwaya Chozi la Heri. (alama 12)
 2. “Tumeendelea kuwakweza akina dada huku tukididimiza nguzo ya jamii yetu.”
  Kwa hoja nane, onyesha jinsi ambavyo nguzo ya jamii inadidimizwa kwa mujibu wa riwaya Chozi la Heri. (alama 8)
 1. Nina wazazi wawili, ila hawa ni wazazi tu, hawajadiriki kuwa walezi wangu, wala jina ‘mlezi’ haliwaafiki.”
  Onyesha jinsi kauli iliyopigwa mstari inavyowaafiki baadhi ya wazazi katika Jumuiya ya Wahafidhina ukirejelea riwaya Chozi la Heri. (alama 12) 
  • Naomi anawahini wanawe malezi kwa kumtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini.Umu,Dick na Mwaliko wanaishia kulelewa na kijakazi sauna.
  • Baba Kairu anamtelekeza Kairu kwa kumwacha kulelewa katika maisha ya umaskini kwa sababu mamake hakujiweza kiuchumi.
  • Wazazi wa Zohali wanamdhalilisha na kumsimanga Zohali baada ya kupachikwa mimba na kufukuzwa shuleni badala ya kumsaidia kukabili hali yake mpya.
  • Fumba anamtelekeza mwanawe Chandachema kwa nyanyake bila kumpa pesa za matunzo yake.
  • Baba Kipanga anamkana Kipanga kuwa mwanawe wa kuzaa,hali inayomsababisha kutoroka nyumbani na kuanza kunywa kangara.
  • Baba Pete anamkataa Pete kuwa mwanawe akidai kwamaba hawafanani.Pete anaishia kulelewa na nyanyake katika hali ya kimaskini.
  • Mama Pete anamtelekeza Pete kwa nyanyaake bila kumnunulia mahitaji kama sodo.Inabidi Pete kutumia tambara la blanketi.
  • Subira anawakosesha Lime na Mwanaheri malezi kwa kumtoroka Kaizari kutokana na dhuluma za mavyaa ake.
  • Baadhi ya wanawake kutupa watoto kwenye biwi la takataka.
  • Maya anambaka Sauna na kumringa mimba.
  • Mama Sauna anamomonyoa maadili ya Sauna kwa kumsaidia kuavyaa mimba.
  • Mama mwangemi na mama Mwangeka kuwanyima Mwangemi na Mwangeka chakula baada ya kuiga babu yao.
  • Fungo anamfurusha Pete na mwanawe bila kuwazia hatima ya mtoto huyo.
  • Ami za Lucia wanaendeleza ubaguzi wa kijinsia kwa kupinga masomo ya Lucia na Akello kwa kuwa ni wasichana.
  • Satua anamdhulumu Chandachema kwa kuwa anajua hana walezi.
  • Tenge anafanya ukahaba machoni pa wanawe hivyo kuwaachia dhiki za kisaikolojia.
   (Mtahiniwa aonyeshe jinsi wazazi wanavyokosa kuwajibika katika kuwalea wanao hivyo kuwaasababishia kutaabika.)
 2.  “Tumeendelea kuwakweza akina dada huku tukididimiza nguzo ya jamii yetu.”
  Kwa hoja nane, onyesha jinsi ambavyo nguzo ya jamii inadidimizwa kwa mujibu wa riwaya Chozi la Heri. (alama 8)
  • Buda anashiriki katika ulanguzi wa mihadarati kwa kutumia watu kama Dick na kuwahonga polisi.
  • Mhusika aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitman’ anatamauka baada ya kusaliotiwa na viongozi na kusiriki uhuni pamja na mauaji.
  • Ridhaa anabaguliwa na wanafunzi wenzake wanapomwita mwizi wa kalamu na mfuata mvua.
  • Shamsi anageuka na kuambulia ulev ili kukumbana na utamaushi uliomkumba.
  • Lunga anageukia ukataji miti ili kukumbana na kupoteza kwake ajira.
  • Mwanaharakati Teteti anaendelea propaganda dhidi yake dhidi ya wanawake na kuonyesha jinsi wanawake walivyowakandamiza wanaume katika enzi za kiistiimari.
  • Hazina anasawiriwa kama ombaomba anayeshiriki katika uvutaji gundi kabla ya serikali kumwokoa na kumsomesha.
  • Dick anatumiwa na Mzee Buda kulangua mihadarati.
  • Kipanga, baada ya kutengwa na wazaziwe, anazamia unywaji pombe haramu.
  • Bwana Maya anamnajisi mwanawe Sauna.
  • Bwana Mwanzi anakataa kukubali kushindwa licha ya Bi. Mwekevu kushindwa waziwazi.
  • Makaa anachomeka anapojaribu kuwasaidia waliokuwa wakichomeka baada ya kujaribu kuchota mafuta kwenye lori.
  • Wanawe Kaizari wananajisiwa mbele yake, jambo linalomwacha akiuguza majeraha ya moyo.
  • Tenge anashiriki ufuska kila mara Bi. Kimai anapoondoka.
  • Mze Kedi anashiriki katika kuteketeza familia ya Ridhaa, anachoma jamaa za Ridhaa hadi wanageuka majivu.
  • Mabavu ananyakua shamba la kina Shamsi na kuwatumikisha kwenye shamba lao.
  • Kimbaumbau anatisha kumdhulumu Naomi kimapenzi na hata kumtesa baada ya kumwajiri, jambo linalomfanya kuacha kazi.
  • Babu Mwimo Msubili ana mtazamo hasi kuhusu wanawake na kuchukulia kuwa kukutana nao asubuhi ni balaa.
  • Wajombaze Pete wanashiriki katika kumwoza licha ya pingamizi kutoka kwa nyanyake.
  • Babake Kairu anambagua na kumtenga Kairu kwa vile ni motto aliyezaliwa nje ya ndoa.
  • Babake zohali anamtumikisha na kumfanyisha kazi nyingi baada ya kuambulia ujauzito.
  • Bwana fumba anajihusisha katika uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wake Rehema na hata kumpa mimba.
  • Ami zake Luca wanapinga ndoa kati ya ukoo wa anyamvua na Waombwe licha ya kutohusika katika kumlea na kumsomesha.


Swali la Insha 20

Ukirejelea riwaya nzima ya Chozi la heri:

 1.  Fafanua umuhimu wa elimu katika jamii. (alama 10)
 2.  Jadili jinsi mwamndishi alivyoshughulikia maudhui ya ufadhili. (alama 10)
 1. Umuhimu wa Elimu (al.10)
  1. Chombo cha kueneza amani na upendo
   mamake Ridhaa anamtuliza baada ya kusimangwa na wanafunzi wenzake shuleni na kumshauri kuwa ni vyema kujifunza kuishi na wenzake bila kujali tofauti za ukoo na nasaba.
  2. Nyenzo ya kumfikisha binadamu kwenye kilele cha ufanisi
   Mwangeka, Ridhaa,Mwangemi,Lunga wanafanikiwa maishani kutokana na elimu.
  3. Nyenzo ya kuzindua jamii.
   Shuleni Tila wanafunzwa kuhusu mabadiliko,uwajibikakji wa mtu usipimwe kutokana na jinsia.
   Mwekevu anachaguliwa kama kiongozi baada ya jamii kuzinduliwa.
  4. Nyenzo ya kutoa maarifa ya kuendeleza jamii
   Lunga anatumia elimu katika kilimo kuwaelimisha raia kuhusu mbinu bora za kilimo.
  5. Nyenzo ya kuleta mabadiliko
   Mwanaheri anajiunga na shule ya Tangamano kw lengo la kuandama elimu ili aweze kuleta mabadiliko katika jamii.
  6. Nyenzo ya kuwaokoa vijana kutokana na uovu.
   Hazina anaokolewa kutokana na kinamasi cha uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati anapopelekwa shuleni katika mradi wa serikali.
  7. Njia ya kukabiliana na changamoto za maisha
   Hazina anapata kazi katika hoteli,wengiwao(watoto wa mtaani) ni maseremala,waashi na mafundi wa juakali baada ya kuelimishwa.
  8. Nyenzo ya kuondoa mwemeo wa mawazo/huzuni
   Wasichana katika shule ya Tangamano wanatumia fursa hiyo kusimulia juu ya maisha yao na kuliwazana.
   Walimu pia wanawaliwaza wanafunzi wao na kuwapa matumaini.mf Mtawa Pacha anamliwaza Zohali.
  9. Chanzo cha kuboresha miundomsingi katika jamii
   Ridhaa anajenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya.
   Serikali inajenga makao ya watoto pmoja na shule ili kufadhili elimu.
  10. Kigezo cha kupima uwajibikaji
   Neema anakiokota kitoto barabaranui kwani alielewa haki za watoto.
   Mwangeka anamshauri Dick kuacha ulanguzi wa dawa za kulevya na pia ankubali uamuzi wa Apondi kumlea Umu.
   Mwekevu anaikwamua jamii kwa miradi ya maji kinyume na wagombea wenza.

   Zozote 10x1
 2.  
  1. Shirika la Makao bora lilijitolea kuwajengea wakimbizi nyumba bora.
  2. Misikiti na makanisa yalikusanya magunia ya vyakula kuwalisha wakimbizi.
  3. Serikali inajenga makao ya watotowa mtani n kufadhili elimu yao.
  4. Serikali inazindua hazina ya kufadhili masomo ya watoto(idara ya watoto)
  5. Kituo cha wakfu wa Mama Paulina kinawafadhili watoto wa mataani kama Zohali.
  6. Familia ya Bw Tenge inamfadhili Chandachema kwa kukubali kuishi naye anapopata nafasi katika shule ya msingi ya kilimo
  7. Shirika la kidini la Hakikisho la haki na utulivu lilimpeleka Chandachema katika makao ya jeshi la wajane
  8. Ridhaa anawasomesha wapwaze Mzee Kedi.

Swali la Insha 21

 1. ”Siasa mbaya maisha mabaya.”Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri. (al.10).
  • Kuleta mauaji – Mamia ya roho zisizo na hatia zilisalimu amri chini ya pambaja za visasi.
  • Uharibifu wa mali  - Vita vilipozuka baada ya bi.Mwekevu kuchaguliwa, nyumba nyingi na mali ziliteketezwa.
  • Wizi wa mali – Maduka ya wafanyabiashara yaliporwa walipotoroka vita vilivyozuka baada ya Bi. Mwekevu kuchaguliwa.
  • Kusababisha wakimbizi wa ndani. Mamia ya watu walilazimika kutoroka kwao na kupiga kambi kwenye msitu wa mamba.
  • Uharibifu wa mazingira – mizoga ya watu na wanyama, magufu ya majumba yaliyotekelezwa kwa moto na viunzi vya mumea iliyonyong’onyezwa na moto ilijikita kila mahali.
  • Ubakaji – mwanaheri na lime walibakwa na mabarobaro watu, kwa sababu babake alikuwa akimwunga mkono Bi. Mwekevu.
  • Vitisho – Bi.Mwekevu alipokea vitisho kutoka kwa wanaume kuna sababu ya kujitosa kwesa siana kama wanaume.
  • Matusi – Bi. Mwekevu alipokea matusi kutoka kwa wanaume waliopinga azima yake ya kutoania uongozi.
  • Kutengwa – Bi. Mwekevu alitengwa na jamii ya wanawake kwa kujitosa kwenye ulingo wa kisiasa uliotengewa wanaume.
  • Hofu – Familia ya kaizari na wanafidhina wengine walipokuwa wakitoroka kwao walishuhudia mabasi yakichomwa, mifyatuko ya risasi na tanzia nyingine zilizowatia shaka na shauku.
  • Kutenganisha ndoa. Subira walitengana na kaizari walitenganishwa.
  • Ukabila – Jirani wa Ridhaa alikataa kuzungumzwa naye baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
  • Utegemezi – ilibidi wageni kutoka mataifa ya nje kuja kudumisha Amani.
  • Ukosefu wa ajira. Watu walikosa kazi baada ya machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi.
 2. Fafanua athari za umaskini katika jamii ukirejelea Riwaya ya Chozi la Heri.
  • Ndoa za mapema – pete aliozwa mapema akiwa darasa la saba ili kugharamia karo ya nduguye wa kiume.
  • Ajira ya watoto – chandachema alilazimika kufanya kazi ili kugharama mahitaji yake.
  • Kuleta taasubi ya kiume – pete anaozwa ili nduguye wa kiume.
  • Utengano wa ndoa – Naomi alimwacha Lunga baada ya Lunga kufutwa kazi.
  • Kutekeleza watoto – Naomi alitekeleza wanawe kutokana na umaskini wa babake.
  • Kufanya kazi duni – Pete alilazimika kuuza pombe ili kukidhi mahitaji ya wanawe
  • Uozo – Pete alijaribu kuavya mimba kwa sababu hangeweza kuwalisha watoto wengi.
  • Kukosa mtaji wa kuanzisha biashara – Mamake Kairu alikosa pesa za kuanzisha biashara nyingine baada ya biashara ya samaki kukumbwa na mzozo.
  • Ulanguzi wa dawa za kulevya – Dick alishiriki biashara ya kulangua dawa za kulevya ili kutosheleza mahitaji yake
  • Wizi – Wanafidhina kadhaa wanangamana wakijaribu kufyonza mafuta kutoka kwa lori lililoanguka.
  • Vifo – Makaa aliaga dunia alipokuwa akijaribu kuwaokoa maskini wakichota mafuta.

Swali la Insha 22

Eleza jinsi maudhui ya ufisadi yalivyoshughulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri.
 • Nyumba za maskini zinapobomolewa Tononokeni, mabwanyenye wanaanza kutoa milungulu ili nyumba zao zisibomolewa.
 • Viongozi wanapowapoka raia ardhi zao, raia walalamikapo hupozwa roho kwa kuambiwa kuwa kumeundwa tume za kuchunguza kashfa hizo.
 • Wakati wa uchaguzi, wanasiasa wanawahonga raia ili wawachague.  Papa aliwahonga kwa pesa na unga.
 • Hazina ya Jitegemee inalenga kuwafaidi vijana wa taifa la Wahafidhina lakini ukabila na unasaba unapoliandama hawanufaiki.
 • Nyumba zinazolengwa kupewa maskini katika mtaa duni wa Sombera zinachukuliwa na viongozi baada ya ujenzi kukamilika.
 • Familia ya Bwana kute inajigawa na kuwa familia tatu ili wapate msaada mwingi kuliko wakimbizi wengine.
 • Serikali inabomoa majengo ya raia katika mtaa wa Tononokeni na Zari bila kuwafidia. 
 •  Raia wanaiba mafuta ya lori ili wawauzie madereva wa wakubwa au walinda usalama ili wayauze kwingine.
 • Madereva wa wakubwa wanafyonza mafuta kwa mirija na kuwauzia wenye magari ya kibinafsi.
 • Askari wananunua mafuta ambayo yameibiwa na kuyauza kwingine.
 • Matapei wanawauzia wananchi wenzao ardhi ya makaburi bila kujali
 • Raia matapeli wanauza ardhi zao mara mbili kwa watu wawili tofauti na kutoa hati miliki mbili halali na bandia
 • Viongozi wananyakua ardhi iliyotengewa upanzi wa chakula na kujenga nyumba zao mf. Madhabahu kwenye mlima wa Nasibu yalinyakuliwa ili kujenga hoteli za kitalii.
 • Vigogo wanauza mahindi yanayotolewa na mataifa ya nje kama msaada.
 • Vigogo wanawalazimisha wataalamu wa maswala ya lishe kuidhinisha uuzaji wa mahindi yaliyoharibika.
 • Viongozi wanapasua mbao na kuchoma makaa katika msitu wa mamba baada ya msitu huo kupigwa marufuku.
 • Viongozi wanahamisha wakimbizi kutoka msitu wa Mamba na kuanza kuvuna mahindi yaliyopandwa na wakimbizi badala ya kuwaruhusu kuyavuna kabla ya kuwaondoa.
 • Baada ya Fumba kumpachika mimba mwanafunzi wake, aliachishwa kazi kwa muda kisha akahamishwa kwingine hivyo kumsababishia Rehema kutopata haki yake.
 • Baadhi ya walinda usalama wanashirikiana na wahalifu ili wagawane mali iliyoibiwa.
 • Magari ya vigogo hayaondolewi barabarani na askari licha ya kuwa mabovu.
 • Buda anawahonga askari wanapoenda nyumbani kwake kumtia mbaroni.(biashara ya ulanguzi wa mihadarati)      (Zozote 20x1=10)

Swali la Insha 23

Madhila anuwai yanayowazonga wahusika wengi katika riwaya ya Chozi La Heri yanafungamanishwa na hiari ya maamuzi yao. Jadili (al.20) 
 
Wahusika katika riwaya ya Chozi la Heri wanakumbwa na matatizo mbalimbali. matatizo hayo ni ya kiuchumi na kijamii. Vyanzo vya matatizo yenyewe ni tofauti tofauti, kuna yale yanasababishwa na wahusika wenyewe ilhali mengine yanaletwa na watu wengine. Tunaweza kusema kuwa matatizo mengine yanatokana na uamuzi mbaya wanaaoufanya wahusika wenyewe.
 • Jumba moja la Ridhaa linabomolewa kwa kuwa alilijenga katika ardhi iliyotengewa ujenzi wa barabara katika mtaa wa zari. Hakuchunguza uhalali. 
 • Terry mkewe Ridhaa anapuuza maonyo na maneno ya mumewe kuhusu mkasa ambao ungetokea hivyo anateketea. 
 • Ami wa Mwamwangeka anaagamia katika mkasa wa moto alipoenda kuwasaidia watu waliokuwa wanateketea. 
 • Walioteketea katika moto wa lori walijiigiza matatani wenyewe kwani walikuwa wameonywa kulikuwa na hatari.
 • Uhasama, migogoro na ukosefu wa mahitaji muhimu unaoikumba familia ya Mwimo Msubili hii ni kwa sababu ya yeye kuwaoa wake wengi. 
 • Kufutwa kazi kwa Lunga Kangata Kiriri baada ya kukataa kukubali mahindi ya jano kuuziwa wananchi ni tokeo la uamuzi na msimamo wake.. 
 • Mauti yanayowakumba vijana waliokuwa wakiandamana baada ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi mpya.
 • Tendo la Subira kuondoka nyumbani na kumwacha mumewe linaisambaratisha familia yake na hatimaye kuletea maangamizi mwenyewe.
  Pete anapokubali kuolewa na Nyangumi bila kufanya uchunguzi wa kina ni uamuzi uanokuja kumvnja moyo baadaye baada ya mke halisi wa Nyangumi kurudi. 
 • Tukio la Zohari kupata mimba na kutumbukia katika mateso mengi linasababishwa na uamuzi wake wa kushiriki katika mapenzi akiwa shuleni kidato cha pili.
 • Tendo la Mwangeka na Mwangemi kufanyia babu yao mzaha, kwa kuwa usiku mmoja aliamua kuwalipua viboko. 
 • Mwangeka anakubaliana na Tila kuigiza maombolezi ya Dedan Kimathi ambayo yanamfanya babake kumwadhibu kwa kutowajibika.
 • Kukamatwa kwa Sauna na mwajiri wake Bi. Kangara kwa kujihusisha na Biashara ya ulanguzi wa watoto.
 • Tuama anaathirika vibaya baada ya kupaswa tohara na kulazwa hospitalini ni tendo alilolitenda kinyume na mapenzi ya baba yake.
 • Walevi wenza wa Shamsi ambao wanapoteza uwezo wa kuona au uhai wao kwa kubugia vileo. 
 • Mumwewe Selume anamfukuza mkewe kwa kuwa si wa kabila lake baadaye anamlea mtoto Sara peke yake.
 • Mandu anapouawa katika vita akiwa ughaibuni ni hiari yake kwani huenda hangepoteza maisha kama hangeenda huko mapema. 
 • Fujo zinazosababishwa na wahafidhina baada ya uchaguzi ambapo wanapoteza uhai na mali. 
 • Wakimbizi waliohamia katika msitu na kupanda mimea na baadaye kufukuzwa ilikuwa ni hiari yao kwani si halali kulima msituni.
 • Naomi kumwacha mumewe Lunga Kiriri na watoto na baadaye kuwatafuta baadhi ya kifo cha bwanake Zozote (20 x 1) = 20)

Swali la Insha 24

 Baada ya dhiki faraja. Onyesha vile ukweli wa methali hii unavyodhihirika kwenye riwaya 

 • Ridhaa anapata uchungu baada ya mali yake kuteketezwa, na kuwa mkimbizi. Anarejea hali ya kawaida baadaye anapojenga kituo cha afya cha mwanzo mpya.
 • Ndugu Kaizari anapitia adha mbalimbali na kuishia katika kambi ya wakimbizi. Baadaye anaajiriwa na Ridhaa katika kituo cha afya kama Afiza wa matibabu.
 • Salome anafurushwa kwa mumewe kwa sababu ya ukabila na kuwa mkimbizi. Mwishowe anajiunga na kitui cha afya cha mwanzo mpya kama muuguzi.
 • Zohali anaringwa akiwa kidato cha pili na kusimangwa na wazazi wake. Baadaye anajifungua salama na kurejea shuleni.
 • Mwangeka anasononeka kwa kumpoteza mkewe Lily na mwanaye Becky. Baadaye anamwoa Apondi na kuishi kwa raha.
 • Apondi anaishi kwa woga wa kuhusiana na mwanamume wingine kwa miaka sita lakini baadaye anakutana na mwangeka na kufunga nikaha.
 • Pete anakataliwa na babake, kuozwa kwa lazima, kujaribu kuavya na kujitia kitanzi. Baadaye anawaza jinsi ya kuboresha maisha yake bila kujjidhalilisha.
 • Maisha ya Umu yamejaa mateso-kuachwa na mama, kufa kwa babake na kutoroshwa kwa ndugu zake, Dick na Mwaliko. Baadaye anaishi kwa raha nyumbani mwa Mwangeka, kusoma na muhitimu kama mtaalamu wa Zaraa.
 • Dick anaingizwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya. Hatimaye anaanza biashara yake mwenyewe –kuuza vifaa vya umeme.
 • Mwaliko anaibwa na sauna na kuishia mikononi kwa Bi. Kangara. Baadaye anaokolewa na polisi na kupelekwa kwa kituo cha watoto ambako anapangwa na Mwangemi.
 • Mwangemi na Neema wanaishi bila mtoto baada ya kifo cha Bahati. Hata hivyo wanafaulu kumpanga mtoto mvulana,Mwaliko. 
 • Chandachema anaishia kuchuna majani katika shirika la chai la Tengenea baada ya kumpoteza nyanyake. Baadaye anaokolewa na kupelekwa katika makao ya watoto mayatima anakoendeleza masomo. n.k (10x2=20)

Swali la Insha 25

Mwanamke ametwezwa katika kiwango sawa na namna alivyotukuzwa. Thibitisha ukweli wa madai haya kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri.  (alama 20)
 • Kiumbe katili – Sauna anawaiba watoto aliokuwa ameachiwa kuwatunza
 • Msaliti – Naomi anaisaliti aila yake (Mumewe na wanawe) kwa kuwatoroka na kuwaacha.
 • Mtu mwenye dharau – Sally analidharau jumba alilojengewa na Billy kwa kuliita kiota.
 • Watu wanaopenda kulalamika – Naomi heshi kufanya nongwa na kulalamika kuhusu nyumba waliyoishi baada ya kufurushwa kutoka msitu wa mamba.
 • Mtu bahili/ mchoyo – Naomi anakataa kumsaidia kijana ombaomba na kusema kuwa wanatumwa na watu wao matajiri.
 • Amesawiriwa kama mtu aliyejaa wivu/ gere – mavyaa wa Subira anamwonea gere Subira na kumwona kama mtu aliyekuja kumbwakura mwanawe.
 • Watu wenye kukata tamaa/ majuto – Subira anashindwa kuvumilia madhila, masimango kutoka kwa mavyaa na kuamua kutoroka kuwaacha wanawe.
 • Binadamu aliyesheheni ubinafsi – Subira anajali nafsi yake tu kwa kusema kuwa alikuwa amechoka kuvumilia. Hivyo basi, kutoroka na kuwaacha wanawe na mumewe.
 • Watu waliojaa manung’uniko – Satua alinung’unika kuhusu kila kitu nyumbani: kuisha kwa sabuni, kubanana kwa jeshi la watoto kwenye chumba cha malazi n.k.
 • Watu waliojaa woga – mamake Zohali hakufanya chochote kumtetea Zohali katika ujauzito wake. Aliridhia yote yaliyosemwa na mumewe.

Kutukuzwa kwa mwanamke

 •  Mhisani/ msaidizi – Dhahabu anamtafutia Umu malezi/ wahisani wanaomtunza.
 • Wapenda amani – Rachael Apondi anatoa hutuba ya kuwatangamanisha watu na kuwahimiza kuishi kwa amani.
 • Ni mtambuzi – Dhahabu anatambua kwa urahisi matatizo ya Umu na hata mawazo yanayomtoa darasani.
 • Watu wenye bidii – mamake Kairu anajibidiisha kumlea kwa mkono mmoja kuhakikisha kuwa mwanawe amesoma.
 • Karimu – Julida anamkaribisha Umu katika makao ya watoto.
 • Washauri bora – Subira anawashauri wanawe na kuwahimiza kumtii baba yao na kuzingatia masomo
 • Ni wasomi – Mamake Zohali alikuwa mwalimu mkuu wa shule maarufu ya kitaifa
 • Wanaojali watoto mayatima – makao ya watoto mayatima ya Jeshi la Wajane Wakristo lilianzishwa na wanawake wajane kwa lengo la kuwapa hifadhi watoto mayatima.
 • Wacha Mungu – Nyamvula alikuwa ‘born again’ na alipinga kazi ya mumewe kuwa askari kwa kuwa alihuzisha kazi hiyo na umwagikaji wa damu.
 • Watu wavumilivu – Bi Kimai anavumilia madhila na visanga vya mumewe, Tenge ili aweze kudumisha ndoa yake.

Swali la Insha 26

Eleza jinsi maudhui ya ufisadi yalivyoshughulikiwa katika riwaya ya Chozi la Heri.

 • Nyumba za maskini zinapobomolewa Tononokeni, mabwanyenye wanaanza kutoa milungula ili nyumba zao zisibomolewe.
 • Viongozi wanapowapoka raia ardhi zao, raia walalamikapo hupozwa roho kwa kuambiwa kuwa kumeundwa tume za kuchunguza kashfa hizo.
 • Wakati wa uchaguzi, wanasiasa wanawahonga raia ili wawachague, Papa aliwahonga kwa pesa na unga.
 • Hazina ya Jitegemee inalenga kuwafaidi vijana wa taifa la Wahafidhina lakini ukabila na unasaba unapoliandama hawanufaiki.
 • Nyumba zinazolengwa kupewa maskini katika mtaa duni wa Sombera zinachukuliwa na viongozi baada ya ujenzi kukamilika.
 • Familia ya Bwana Kute inajigawa na kuwa familia tatu ili wapate msaada mwingi kuliko wakimbizi wengine.
 • Serikali inabomoa majengo ya raia katika mtaa wa Tononokeni na Zari bila kuwafidia.
 • Raia wanaiba mafuta ya lori ili wawauzie madereva wa wakubwa au walinda usalama ili wayauze kwingine.
 • Madereva wa wakubwa wanafyonza mafuta kwa mirija na kuwauzia wenye magari ya kibinafsi
 • Askari wananunua mafuta ambayo yameibiwa na kuyauza kwingine
 • Matapeli wanawauzia wananchi wenzao ardhi ya makaburi bila kujali
 • Raia matapeli wanauza ardhi zao mara mbili kwa watu wawili tofauti na kutoa hati miliki mbili-halali na bandia
 • Viongozi wananyakua ardhi iliyotengewa upanzi wa chakula na kujenga nyumba zao mf. Madhabahu kwenye mlima wa Nasibu yalinyakuliwa ili kujenga hoteli za kitalii.
 • Vigogo wanauza mahindi yanayotolewa na mataifa ya nje kama msaada.
 • Vigogo wanawalazimisha wataalamu wa maswala ya lishe kuidhinisha uuzaji wa mahindi yaliyoharibika.
 • Viongozi wanapasua mbao na kuchoma makaa katika msitu wa mamba baada ya msitu huo kupigwa marufuku.
 • Viongozi wanahamisha wakimbizi kutoka msitu wa Mamba na kuanza kuvuna mahindi yaliyopandwa na wakimbizibadala ya kuwaruhusu kuyavuna kabla ya kuwaondoa.
 • Baada ya Fumba kumpachika mimba mwanafunzi wake, aliachishwa kazi kwa muda kisha akahamishwa kwinginehivyo kumsababishia Rehema kutopata haki yake.
 • Baadhi ya walinda usalama wanashirikiana na wahalifuili wagawane mali iliyoibiwa.
 • Magari ya vigogo hayaondolewi barabarani na askari licha ya kuwa mabovu.
 • Buda anawahonga askari wanapoenda nyumbani kwake kumtia mbaroni (biashara ya ulanguzi wa mihadarati)              

Swali la Insha 27

Athari ya vita katika nchi ya Wafidhina ni kioo cha bara la Jadili 

 • watu kuuawa, kuacha makwao na kukimbilia maisha yao huku wakipoteza mali kwani waliokimbia makwao kila walichokiacha kiliteketezwa
  kupora maduka ya Kihindi, kiarabu na hata Waafrika wenzao
 • Misafara ya wakimbizi ikawa kwenye barabara na vichochoro vya Wahafidhina
 • Mizoga ya watu na wanyama
 • magofu ya majumba yaliyoteketezwa kwa moto
 • uharibifu wa mali na
 • Nyimbo za uchochezi mpinzani wa Mwekevu anambiwa tawala wahafidhina , mwanzi wetu tawala.
 • Kuchomwa kwa magari kana kwamba ni mabiwi ya taka
 • Vilio kwa waliokuwa wakiteketezwa
 • Kubakwa kwa mabinti wa Kaizari yaani Lemi na Mwanaheri
 • Askari wa fanya fujo uone kuwafyatulia risasi vijana walioamua kufa
 • Magonjwa ya homa ya matumbo
 • Njaa na ukosefu wa maji safi
 • Kukimbilia chakula kwa watu wazima jinsi wafanyavyo watoto

Swali la Insha 28

Jadhili dhana ya chozi katika riwaya ya Chozi la Heri

 • Umu alilia sana alipowakumbuka nduguye Dick na Umu anahuzunika kwa kukosa kwao nyumbani
 • Watoto wa Lunga Dick, umu na mwaliko walilia machozi ya heri walipopatana katika hoteli ya majaliwa
 • Ridhaa analia machozi ya furaha baada ya mwanawe mwangeka kufunga ndoa na Apondi Reachel
 • Vilio vya kite vilitanda baada ya makundi mawili kukutana, yaani lililomuunga mkono mwekevu na la mpinzani wake
 • Ridhaa analia baada ya familia yake na jumba lake la kifahari kuteketezwa
 • Neema analia machozi ya furaha mwaliko anapokubali kuwa motto wao wa kupanga
 • Neema analia kwa uchungu wakati alipokumbuka kisa cha Riziki Immaculate kitoto alichookota na akaogopa kukichukua na
 • Mwangeka analia kilio cha uchungu babake alipomweleza sababu ya kutozika mabaki ya familia yake
 • Umulkheri na Dick wanapokutana kisadfa katika uwanja wa ndege wanatoa machozi ya
 • Selume analia inapomlazimu kuondoka na kuacha motto na nyumba yake kwa sababu ya ukabila
 • Subira alipokatwa kwa sime alilia kwa kite kabla ya kufa kwake
 • Subira anakilovya kifua chake machozi sababu ya mamamkwe anayemshutumu na kuacha mwanawe na mumewe
 • Mwangemi walipomtania babu Msubili pamoja na Mwangeka walichapwa wakatoa machozi ya uchungu
 • Kaizari alitoa machozi ya uchungu alipoona vijana wakipigwa risasi kwa kukataa kuondoka barabarani
 • Ridhaa analia kwa kubaguliwa shuleni
 • Abiria waliochomewa katika gari la kuabiri na vijana waasi walilia kwa uchungu
 • Mwanaheri anadondokwa na machozi anapowasimlia wenzake kifo cha mamake katika shule ya tangamano
 • Ridhaa alilia machozi ya uchungu alipomwelezea Mwangeka mkasa wa kupoteza mali yake
 • Viongozi wanatoa machozi kikinaya kuonyesha njisi ambavyo wanawahurumia maskini
 • Ridhaa akiwa katika magofu anakumbuka kilio cha Mwangeka akiwa mtoto
 • Kumbukizi za maongezi kati ya Terry na Ridhaa zinamfanya atokwe na machozi
 • Mwangeka na Annatila wanalia walipokuwa wakiigiza kifo cha mdogo wao Kim
 • Wenyeji walilia katika mazishi ya Kim wakilizunguka jeneza
 • Umulkheri analia alipoenda kuhusu kupotea kwa nduguze katika kituo cha polisi
 • Umu alipokutana na Hazina alilia machozi ya mseto wa furaha na huzuni
 • Kairu na mamake wanalia kwa matatizo waliyopata na kujifia kwa kitoto chao walichozika porini

Swali la Insha 29

Akikosa la mama hata la mbwa huamwa kwa kurejelea methali hii, eleza umuhimu wa mashirika ya misaada

 • Mashirika ya kidini yanaungana pamoja kuwasaidia waathiriwa kwa kuwapa chakula katika kambi mbalimbali
 • Kituo cha Benefactor kimeokoa maisha ya watoto wengi;
 • Mwaliko
 • Mtoto aliyeokolewa na Neema na watoto wengine
 • Shirika la jeshi la wajane la Wakristu linasaidia maisha ya mayatima kama vile Chandachema, Umu na Mwanaheri uk95
 • Shuleni tangamano iliwasaidia wanafunzi kama vile mwalimu Dhahabu anamwambia Umu arudi darasani anapoona amekumbwa na mawazo
 • Mamake kairu ni maskini kwamba kulipa karo ni jambo linalomtatiza ila anaongea na mwalimu mkuu kumruhusu mtoto wake asome akilipa kidogo kidogo
 • Mwalimu Dhahabu anajishughulisha kuwatafutia mayatima wazazi wa kuwapanga
 • Shirika la Hakikisho la Haki na Utulivu linajishughulisha katika kusaidia watoto kupata elimu kama ville chandachema
 • Kituo cha wakfu cha mama Paulina kinamsaidia Zohali aliyepelekwa alipokaribia kujifungua

Swali la Insha 30

Athari za matumizi ya mihadarati

 • Zohali anajiunga na kundi la vijana na kuvuta gundi inayomfanya kusahau matatizo anayopitia bila kujua mathara yake
 • Pete anahamia kwa kazi ya kuuza pombe inayosababisha kupata watoto ambao anashindwa kuwalea na kutaka kujiua
 • Dick anaingizwa na Sauna katika ulanguzi wa dawa za kulevya zinazohatarisha maisha ya muuzaji anaweza kamatwa na polisi na kufungwa
 • Dick anashurutishwa kumeza dawa za kulevya na kasha akifika ughaibuni asitapike kutokana na uangalizi mkali katika viwanja vya ndege
 • Dawa za kulevya zinasababisha vifo kijana msomi anakufa katika hospitali ya mwanzo mpya kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya
 • Shamsi anawapigia kelele majirani wake katika mji wa Ahueni kutokana na ulevi wake
 • Aidha ulevi unamfanya aishi katika mtaa wa makabwela wa Kazikeni
 • Kapanga ananusurika kifo kwa matumizi ya kangara inayosababisha vifo vya watu sabini uk143

Swali la Insha 31

Hakuna msiba usiokuwa na mwingine. Kwa hoja ishirini thibitisha ukweli wa methali hii kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)

 1. Ridhaa mbali na kupoteza familia yake, nyumba yake inateketezwa kwa moto.
 2. Mkewe Kaizari anakatwa kwa sime na binti zake kubakwa. Wakati wa usafiri lori linaisha petroli.
 3. Wahafidhina kwa kutaka uongozi mpya ni ishara walitaka mabadiliko lakini mabadiliko yanakuja kwa maafa na ghasia.
 4. Dick anatekwa nyara baada ya baba yao kuaga na kuuzwa kwa Buda. Anahofia maisha yake na mwisho kukubali kulangua dawa za kulevya.
 5. Wafanyabiashara wanawafungia wateja ndani ya maduka yao kwa kuhofia kuibiwa. Hawa wanakufa kwa mkasa wa moto.
 6. Subira aliyekatwa kwa sime anawatekeleza wanawe kutokana na ugomvi baina yake na mama mkwe.
 7. Serikali ilikosa kuwajibikia mahitaji ya vijana kama vile kuwapa kazi. Kuna vijana wanaokaukiwa mate ya kufunga bahasha za kuomba kazi. Viongozi hurejea kila baada ya miaka mitano kuwapa ahadi hizi za ujanja.
 8. Katika kambi za wakimbizi, vitoto vinakufa vilipoenda haja kwenye reli, njaa na magonjwa. Uk.29
 9. Chandachema anatelekezwa na wazazi wake na kupata malezi duni kutoka kwa bibi(nyanya) yake.
 10. Pete baada ya kukanwa kuwa hafanani babake alienda kulelewa na bibi mzaa mama. Huku anapatwa na matatizo ya hedhi na kukosa mapenzi na ushauri. Anadhani ana bahati kumpata Nyangumi lakini mkewe halisi anaporudi anafukuzwa.
  Vita vilipochacha, viongozi walikituma kikosi cha askari cha Penda Usugu Ujute. Kikosi hiki kinatumia risasi na vitoza machozi kuwakabili waandamanaji.
 11. Kitoto chao Kairu kinakufa kutokana na njaa na ugonjwa wakati walipofukuzwa kwao.
 12. Lunga anaachwa na mkewe baada ya kufutwa kazi.
 13. Umu baada ya kubaki yatima, kijakazi Sauna anawateka nyara ndugu zake.
 14. Vita vinatokea kutokana na uchaguzi. Watu wanahamia Msitu wa Mamba kama wakimbizi. Huku wanakumbana na matatizo kama uhaba wa vyumba na chakula.
  Wakimbizi wanafanya Msitu wa Mamba kuwa makao yao. Wanafanya ukulima na kujenga lakini mwishoni wanaondolewa kwenye msitu huu. Hakuna aliyejua mahindi ya akina Lunga yalikwenda wapi. Uk.77
 15. Wakoloni wananyakua mashamba ya Waafrika na kuwafanya wenyeji hazina ya vibarua.
 16. Tila anaonyesha kuna uongozi mbaya umaskini, ufisadi, ukosefu wa gharama za matibabu ya kimsingi na ukosefu wa lishe bora.
 17. Kazi nyingi za serikali kupeanwa zabuni kwa kapuni za kigeni ambao wanajilimbikizia mali ya wahafidhina.
 18. Subira anakata tamaa ya kuishi kwa Kaizari kutokana na chuki ya mamamkwe kwa kiini kuwa hawakuwa wametoka katika jamii moja
 19. Lunga anakata tamaa ya maisha baada ya kuachishwa kazi, kunyakuliwa kwa mazao yake na kuachwa na mkewe jambo linalosababisha kufa kwake
 20. Chandachema anakata tamaa baada ya nyanya yake kufariki na kunyanyaswa na jirani yake Satua
 21. Pete anakata tamaa maishani baada ya kupata watoto watatu akiwa chini ya miaka ishirini na moja jambo linalomfanya kutaka kujiua kwanza 20x1
  (hoja ziangazie pande zote mbili za methali)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Maswali na Majibu ya Insha katika Riwaya ya Chozi la Heri PDF.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest