Chozi la Heri Dondoo Questions and Answers - Chozi la Heri Maswali na Majibu ya Dondoo

Share via Whatsapp

Chozi la Heri Dondoo Questions and Answers

Maswali haya hujitokeza kwa namna ya maneno yaliyodondolewa kutoka kwenye kazi ya Fasihi. Dondoo hunukuliwa kisha maswali yanayohusiana na dondoo hilo huulizwa. Dondoo laweza kuwa maneno ya mhusika mmoja ambaye hatatajwa au maelezo katika kazi. Maswali huenda yakarejelea matukio yaliyotokea kabla au baada ya dondoo. Katika kulijibu swali la muktadha wa dondoo, mtahiniwa huhitajika kuangazia mambo yafuatayo;

 1. Kumtaja msemaji wa maneno haya
 2. Kumtaja msemewa(anayerejelewa)
 3. Kueleza mahali yalikofanyika mazungumzo haya.
 4. Kueleza kiinisababu ya mazungumzo haya kutokea.

Swali la dondoo 1

“Kuukata mkono niliostahili kuubusu yalinifika ya kunifika”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (Alama 4)
 2. Eleza namna msemaji alivyoukata mkono aliostahili kuuibusu. (alama 6)
 3. Eleza tamathali ya usemi unaojitokeza katika dondoo hili. (alama.2)
 4. Fafanua sifa nne za msemaji wa kauli hii (alama 8)

Majibu ya dondoo 1

 1. Kuukata mkono uk (70-71)
 2. Anapokuwa mkurugenzi katika shirika la uzalishaji nafaka, Lunga anapinga kuagizwa kwa nafaka ambayo yalihofiwa kuharibika na hayangefaa kwa matumizi ya binadamu.
 3. Jazanda-kuukata mkono aliostahili kuubusu-kuwapinga wakubwa wake.
 4.  
  • Mwenye Msimamo Dhabiti: anakataa kushawishika na wakubwa wake kukubali uuzaji wa mahindi yaliyohofiwa kuharibika
  • Mwenye bidii: asifika kwa uhodari wake wa ukulima. Amepandikwa jina mkulima namba wani Uk 70
  • Mwajibikaji: anawajibika kutetea umma dhidhi ya kuuziwa mahindi yaliyokuwa yameharibika na mabayo ni sumu kwa Binadamu
  • Mwenye tamaa: anapooana zao la mahindi katika msitu wa mamba, anaghairi nia ya kuhamisha babake asishiriki uharibivu wa mstitu na kuanza ukulima katika msitu wenyewe.
  • Jasiri:anaamua kutetea umma japo anafahamu fika kuwa ni sawia na kuukata mkono aliostahili kuubusu na kuwa angefutwa kazi wakati wowote
  • Mpenda haki: anatoa mhanga kutetea maslahi ya wanyonge jambo linalosababisha afutwe kazi.
  • Mwenye busara:anatoa ushauri kuwa raia wanastahili kufunzwa jinsi ya kutuia ardhi kwa njia endelevu (uk.71)
  • Mwanaharakati wa mazingira: aawali anapofika katika msitu wa mamba,anataka kuhamisha babake kwani anaona ni Edeni pa wanyamapori na si vizuri kuuharibu

Swali la dondoo 2

“Hili lilimtia …………. uchungu, akajiona kama aliyedhalilishwa na mwanamke.”

 1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake (alama 4)
 2. Taja suala linalodokezwa katika dondoo hili (alama 1)
 3. Kwa kutumia hoja kumi na tano, eleza namna suala ulilolitaja hapo juu 1 (b) linalijitokeza. (ala. 15)

Majibu ya dondoo 2

 1.  
  • maelezo ya mwandishi
  • Anamrejelea Bwana Kimbaumbau
  • Ni baada ya Sauna kukataa kushiriki mapenzi naye
  • Wote wawili walikuwa Kazini
 2. Ubabedume/ Taasubi ya kiume
 3.  
  • Jamaa za Kangata kupinga elimu ya mabinti zake
  • Kimbaumbau kumdhulumu Naomi anapokataa kujihusisha kimapenzi naye.
  • Mwimo Msubili kutotaka kukutana na mwanamke asubuhi kwa madai kuwa ni Mkosi.
  • Lime na Mwanaheri kunajisiwa na vijana wahuni.
  • Bwana Maya anamdhulumu mamake Sauna kwa mapigo na matusi aulizapo swali lolote lile.
  • Kuuzwa kwa Pete kwa Fungo ili wazazi wake wapate pesa za kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.
  • Pete anabakwa na mlevi anapolewa chakari
  • Mamake Zohari kuridhia kila asemalo mumewe na kushidwa kumtetea anapopata himila.
  • Mamake Mwangeke aliwahi kumwonya kulia kama msichana. Hii ni ishara kuwa jamii yamwona mwanamke kama mnyonge.
  • Mwanzi anakataa kukubali matokeo ya uchaguzi madhali anashindwa na mwanamke, Mwekevu.
  • Wahafidhina kuamini kwamba mtoto wa kiume ndiye pekee anayestahili kuwa mrithi wa mali ya babake. 
  • Ushindi wa Mwekevu unaonekana kama kutoheshimiwa kwa mwanaume.
  • Mwekevu kusingiziwa wizi wa kura anapomshida Mwanzi.
  • Kutishwa, kutusiwa na hata kutengwa kwa Mwekevu anapojitosa katika siasa zilizoaminiwa kuwa ni za wanaume
  • Fungo anamharibia Pete maisha anapomwoa kisha kumfukuza anapojifungua mtoto.
  • Mwanamke kuonekana kama mnyonge anayestahili kulia akabiliwapo na vizingiti au changamoto maishani. Mwanaume hafai kulia

Swali la dondoo 3

“ Kwa kweli ni hali ngumu hii”

 1. Weka dondoo katika muktadha wake. (alama 4)
 2. Ni hali gani yamsemewa inayorejelewa kwenye dondoo. (alama 16)

Majibu ya dondoo 3

 1.  
  • Mzungumzaji ni Ridhaa
  • Anayezungumziwa  ni Kaizari
  • Ni katika kambi/mabanda- Kwenye Msitu  wa Mamba
  • Ni baada ya Kaizari kumsimulia Ridhaa magumu aliyoyapitia kutoka  kwake nyumbani hadi kujipata kweye hali nyingine ngumu katika kambi.
 2.  
  • Mke wa Kaizari, Subira ananyakwa kofi kubwa
  • Anarejelewa kama kidume kijoga-kudharauliwa
  • Mke wake anakatwa kwa sime na kuzirai kwa uchungu
  • Bintize –Lime na Mwanaheri- wanafanyiwa unyama na mabarobaro
  • Jirani yake Tulia anamfukuza anapojaribu kuwapa mke wake  na watoto huduma za kwanza
  • Wanawe wanazirai ubavuni mwake
  • Anaabiri gari bila kujua waendako na jamaa zake
  • Walitazama mabasi yakichomwa kwenye safari iliyokuwa ndefu 
  • Gari linaisha petroli- wanajitoma msituni
  • Wanakula mate usiku wa kwanza kutokana na ugeni/ukosefu wa chakula
  • Kuna hali mbaya ya baridi na umande wa asubuhi
  • Wanakosa maji safi ya kunywa kwenye msitu
  • Kunywa maji ya Mto wa Mamba kunawasababishia homa ya tumbo.
  • Vijumba vichache havikutosha kuhimili idadi ya wakimbizi
  • Huduma za kijamii zinaadimika –ukosefu wa misala na misala ya kupeperushwa 
  • Sandarusi za kutumiwa kama misala  zilitafutwa mbali kwenye milima ya taka.
  • Roho za watoto zilibwakurwa na magarimoshi kwenye reli walipoenda haja kule
  • Kuna hali ya njaa na vilio vya watoto wenye njaa

Swali la dondoo 4

“Watu husema kuwa binadamu hawawi sawa ila kifoni…”

 1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alalama 4)
 2. Tambua mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
 3. Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya. (alama 6)
 4. Thibitisha kuwa hakuna usawa baina ya wanadamu. (alama 8)

Majibu ya dondoo 4

 1. Haya ni maneno ya Kaizri. Anamwambia Ridhaa. Wapo katika Msitu wa Mamba. Ni baada ya kufurushwa kutoka Mlima wa Simba baada ya vita vya baada ya uchaguzi kuzuka. Anarejelea usawa kiasi uliokuwa ukionekana kuwepi pale kambini. (4×1= 4)
 2. Kinaya- watu hawawi sawa ila kifoni(1×2= 2)
 3.  
  • Sifa za Kaizari.
   • Ni mwenye busara. Anaelewa kuwa hakuna usawa wakati wa kifo kati ya maskini na matajiri ikizingatiwa wanavyokufa na wanavyozikwa (uk 14- 15).
   • Ni maskini. Matone mazito ya mvua yalianguka kwenye ngozi ya wanawe, Lime na Mwanaheri. Hana uwezo wa kuwasaidia. Hata tambara hana (uk 15- 16).
   • Ni mcha Mungu. Anamshukuru Mungu kuwa wangali hai licha ya hali ngumu (uk 16).
   • Mwenye huruma. Aliwahurumia vijana waliouwawa kwa risasi na polisi wa Penda Usugu Ujute (uk 24).
   • Mzalendo. Aliihurumia nchi yake ambayo ilielekea kushindwa kuwashawishi watu wake kuelewa umuhimu wa usalama (uk 24- 24).
   • Mwenye mapenzi ya dhati. Alijaribu sana kuwaokoa wanawe waliokuwa wakibakwa ila akashindwa (uk 25).
   • Mwenye tahadhari. Siku za kwanza kambini hakuweza kutumia vyoo vya kupeperushwa (uk 29).
   • Mshawishi. Aliwasihi wakimbizi wenzake kuchimba misala (long drop) (uk 29). (3×1= 3)
           Kila sifa ifafanuliwe. Sifa zisianze kwa vinyume kama: hana utu, si mwenye tahadhari n.k.
  • Umuhimu wa Kaizari
   • Anawakilisha watu wenye busara katika jamii.
   • Ametumiwa kuonyesha matatizo wanayokumbana nayo wakimbizi.
   • Anawakilisha athari zinazotokana na vita vya kikabila.
   • Ametumiwa kuwajenga wahusika wengine kama Ridhaa.
 4.  
  • Sheria za kikoloni zilimpa mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao na umilikaji wa ardhi na Waafrika sehemu hizi kupigwa marufuku (uk 7).
  • Hata katika kifo hamna usawa. Kuna wanaokufa wakipepewa na wauguzi katika zahanati za kijijini. Wengine hulala maumivu yao yakiwa yamefishwa ganzi kwenye hospitali za kifahari (uk 14).
  • Pia kuna tofauti katika mitindo ya mazishi ya matajiri na maskini. Matajiri huvishwa mavazi ya kifahari tofauti na maskini (uk 15).
  • Mwalimu aliwaambia kina Tila kuwa utawala huteuliwa maksudi kuendeleza mfumo uliopo wa kiuchumi kwa maslahi ya watawala na tabaka ambalo linazimiliki nyenzo za uzalishaji mali (uk 39).
  • Bwana Kangata na jamii yake walilowea kwa shamaba la mwajiri wao ambaye alikuwa akiishi jijini (uk 64).
  • Kimondo alimweleza Lunga kuwa kuishi kwao wanyonge kuliamuliwa na matajiri (uk 69).
  • Waafrika wafanyakazi maskini walinyimwa matibabu kwa kukosa Medical Scheme kama alivyoeleza daktari mwafrika (uk 70).
  • Baada ya wakimbizi kuishi katika Msitu wa Mamba kwa kipindi fulani, jamii ilianza kutwaa uchangamano wa mtu kutambua kuwa yeye alitokana na ukoo mtukufu na jirani yake alikopolewa na ukoo wa mlalaheri (uk 75).
  • Katika wimbo wake, Shamsi anaeleza kuhusu matajiri wanaomchungulia na kumcheka wakiwa kwenye roshani zao wakipunga pepo baada ya kujaza matumbo yao (uk 130).
  • Ridhaa alihamia mtaa wa Afueni. Mtaa wa watu wenye kima cha juu kiuchumi. Daraja kubwa limeutenga mtaa huu na mtaa wa Kazikeni, mtaa wa watu wenye maisha ya kubahatisha (uk 137- 138).

Swali la dondoo 5

“Alikumbuka jinsi rafiki yake……..alivyofishwa kwa njia hii. Akili yake ilimtambia kisa chenyewe kana kwamba inataka kumwonya (uk.120)

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. Al.4
 2. Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. Al.4
 3. Tathmini nafasi ya anayelengwa na kauli hii katika kuijenga riwaya hii. Al.12

Majibu ya dondoo 5

 1.  
  • Haya ni maneno ya msimulizi
  • Yanamhusu Dick akikumbuka rafiki yake lemi ambaye aliuawa na umati
  • Anakumbuka kisa hiki anapoitshwa kuwa angetupwa nje na mwajiri wake, Buda, kisha asingiziwe wizi na kuchomwa moto.
  • Hofu hii ndiyo iliyomchochea kuingilia ulanguzi wa dawa za kulevya.
 2.  
  • Tashihisi - Akili ya Dick ilimtambia kisa chenyewe kama kwamba inataka kumuonya.
  • Chuku - Akili ilimtambia kisa
 3. Umuhimu wa Dick
  • Ametumiwa kuonyesha nafasi ya familia katika malezi.Kuondoka kwa mama yake kunaisambaratisha familia yake;Dick na mwalike wanaibwa na sauna.
  • Ametumiwa kukashifu ufisadi. Anasema kwamba maafisa wa usalama wanaingia kwa Buda kwa tabasamu na kutoka kwa vicheko.
  • Anaendeleza swala la matumizi mabaya ya dawa. Anatumia dawa na kuzilangua.
  • Anachimu za maudhui ya mabadiliko. Anaamua kuacha ulanguzi wa dawa, kujielimisha na kuanzisha biashara ya kuuza vifaa vya simu.
  • Anaonyesha nafasi ya vijana katika kuboresha maisha ya jamii zao. Anawaajiri vijana wenzake. Ni kielelezo cha vijana wanaotambua makosa yao na kujirekebisha.
  • Ametumiwa kujenga tabia za wahusika.
  • utu wa mwangeka. Anamchukua kama mwanawe na kumwelekeza.
  • Ukakamavu wa Umu – umu anamwambia Dick kuwa yeye, umu, atawalea yeye Dick pamoja na mwaliko kwa viganja vyake japo umu ni mchanga wakati huo.
  • anaendeleza ploti kukutana kwake na umu kunabadilisha mkondo wa hadithi. Anaelekezwa na umu kwa mwangeka ambaye anamsaidia kuyatengeneza maisha yake zaidi.

Swali la dondoo 6

“Msamehe ….., hakuna mja aliyekamilika.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.   (alama 4)
 2. Eleza umuhimu mnenewa katika dondoo hili.   (alama 4)
 3. Kwa kurejelea wahusika mbalimbali riwayani, thibitisha kuwa hakuna mja aliyekamilika.     (alama 12)

Majibu ya dondoo 6

 1.  
  • Ni maneno ya mamake Sauna
  • Anamzungumzia Sauna
  • Ni katika kumbukizai za Sauna
  • Ni baada ya Sauna kutendewa unyama na babake mlezi             
  • Sauna anabakwa na kuambulia ujauzito, hali inayobainisha mkondo wa maisha ya Sauna.
 2. Mnenewa ni Sauna
  • Dhuluma kwa watoto katika ndoa/ familia. Anabakwa na babake mlezi.
  • Kikulacho ki nguoni mwako. Anawaiba wanawe Lunga ilhali aliaminiwa kuwatunza.
  • Anaendeleza maudhui ya usaliti. Anatumia furs aya uaminifu wa watoto kuwaiba na kuenda kuwauza.
  • Ukatili wa mamake. Mamake anamshurutisha kuavya mimba na kujificha tukio hilo kuwa siri.
 3.  
  • Sauna
   • Ulanguzi wa watoto
   • Biashara haramu , kuwauzia watu maji machafu
  • Mamake Sauna
   • kumshurutisha mwanawe Sauna kuavya mimba.
   • Kuficha maovu ya mumewe
   • Anatoroka mumewe (Bwana Kero) baada ya kufutwa kazi
  • Bwana Kero
   • mlevi kupindukia hali inayomsababishia kufutwa kazi.
  • Bwana Maya
   • kumpiga makonde mkewe kila wakati,
   • Kumtisha na kumtusi mkewe
   • Kumbaka mwanawe – Sauna
  • Lunga
   • Tamaa ya kuwa mkulima. Kuharibu misitu
   • Kujigamba kuwa alitoka katika ukooo wa Kiriri
  • Naomi
   • Anamtoroka mumewe na kumwacha katika upweke.
   • Alipenda kufanya nongwa na kulalamikia maisha duni baada ya kutolewa Msitu wa Mamba.
  • Sally
   • Anakataa usuhuba wa Billy
   • Dharau, anaita jumba la Billy kiota. Hawezi kuishi kwenye kiota.
  • Bwana Kalima
   • Laghai, anamfuta kazi Lunga kwa kisingizio cha kustaafisha wafanyikazi ili kupunguza gharama.
  • Annette
   • Katili/ saliti ; anamwacha Kiriri katika ukiwa baada yao kufilisika
   • Alipenda kumsimanga mumewe kwa kuwaita watumishi wake ; vimada.
  • Mzee Kedi
   • Katili,saliti ; anamchomea Ridhaa nyumba yake na kuingamiza ailayake.
  • Zohali
   • Tamaa na ulimbukeni wa ujana unamsababishia ujauzito.
  • Fumba
   • Anamringa Rehema mwanafunzi wake.
   • Anamtelekeza Chandachema kwa kumwachia bibiye malezi.
  • Bwana Tenge
   • Mzinifu/asherati ; aliwaleta wanawake kwa nyumba wakati Bi.Kimai alikuwa shamba.
  • Tindi
   • Kaidi ; anakosa kufuata ushauri wa mamake wa kurejelea nyumbani mapema – kabla ya saa kumi na moja magharibi.
  • Mzee Buda
   • Mlanguzi wa mihadarati
   • Vitisho ; kumtishia Dick kusingiziwa wizi ili auawe.
  • Shamsi
   • Mlevi kupindukia
   • Kuwapigia watu kelele usiku
  • Subira
   • Kutamauka ; anashindwa kuvumilia nongwa na masimango ya mavyaa wake.
   • Anatoroka na kuwaacha wanawe na mumewe – Kaizari
  • Kipanga
   • Mraibu wa dawa za kulevya
   • Ananusurika kifo kutokana na kangaara iliyowaua watu sabini.

Swali la dondoo 7

“Kumbe hata mja akafanikiwa vipi kielimu na kitaaluma, maisha yake huwa ombwe bila mwana, awe wa kuzaa au wa kulea?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili    (alama 4)
 2. Taja tamathali moja iliotumika katika dondoo (alama 1)
 3. Onyesha ukweli wa kauli hii ukirejelea wahusika wowote watano riwayani (alama 5)
 4. Fafanua umuhimu wa elimu katika jamii ukirejelea riwaya nzima. (alama 10)

Majibu ya dondoo 7

 1.  
  • Msemaji ni Mwangeka
  • Anajisemea kimoyomoyo ( uzungumzi nafsi)
  • Yeye na Neema wako katika afisi ya Annastacia katika kituo cha watoto cha Benefactor
  • Wamekwenda kumchukua mwanao wa kupanga (Mwaliko) baada ya kukosa kufanikiwa kuwa wan a mwana wa kuzaliwa. Wanamlea kwa tunu na kumsomesha hadi chuo kikuu.
 2. Istiara- maisha huwa ombwe
 3.  
  • Selume – amehitimu kuwa mkunga na kuajiriwa kama muuguzi katika hospitali kuu ya Tumaini na hatimaye katika kituo cha Afya cha Mwanzo Mpya.
   Maisha yake yanaonekana kuwa ombwe baada ya kutengana na mumewe ambaye anachukua binti yao Hajui kama atakutana na mwanawe Sara baada ya mumewe kuoa msichna wa kikwao
  • Ridhaa- amehitimu katika taaluma ya udaktari na kufanikiwa maishani. Ni mkurugenzi, mfanyi biashara mkubwa na anamiliki hospitali ya Mwanzo Mpya
   Maisha yake yanaonekana kuwa ombwe anapopoteza mwanawe Dede na Tila baada ya jumba lake kuchomwa na mzee Kedi. Anapomkumbuka Tila anatokwa na machozi yanayolovya kifua chake.
  • Mwangeka- amehitimu katika taaluma ya uhandisi, anajiunga na vikosi vya usalama na kupanda ngazi hadi juu.
   Maisha yake yanakuwa ombwe anapompoteza bintiye Becky katika mkasa wa moto, anabaki katika upweke mkuu. Anajuta kutofuata ushauri wa mkewe Lily. (uk62)
   Apondi anapoamua kumlea Umu, Mwangeka anamwona Umu kama Baraka kutoka kwa Mungu, fidia ya mwanawe aliyekufa. (uk 118)
  • Neema na Mwangemi- Neema amehitimu katika taaluma ya uhasibu na ameajiriwa katika Hazina ya Kitaifa kama hasibu mwandamizi na Mwangemi ana shahada ya uzamili katika uuguzi. Miaka mitano katika ndoa bila mtoto inawahuzunisha, wanachekwa kuwa Neema hawezi kulea mimba.
   Maisha yao yanakuwa ombwe wanapompoteza mwanao Bahati kutokana na ugonjwa wa sickle-cell.
   Hatimaye wanaamua kupanga mtoto, wanajaliwa kupata Mwaliko (uk 159-167)
  • Naomi- anamwacha Lunga na kwenda kutafuta riziki baada ya Lunga kupoteza kazi na mali yake.
   Hatimaye anajuta kuwatelekeza wanawe, anawatafuta kote na anapata habari kuwa Dick na Mwaliko waliibwa na Sauna anahuzunika.
 4. Umuhimu wa elimu        (alama 10)
  • Chombo cha kueneza amani na upendo (uk 11)
   Mamake Ridhaa anamtuliza Ridhaa baada ya kusimangwa na wanafunzi wenzake shuleni na kumshauri kuwa ni vyema kujifunza kuishi na wenzake bila kujali tofauti za ukoo na nasaba.
  • Nyenzo ya kumfikisha binadamu kwenye kilele cha ufanisi (uk 11)
   Mwangeka, Ridhaa, Mwangemi, Lunga n.k wanafanikiwa maishani kutokana na elimu.
  • Chanzo cha umilisi na stadi za kujitegemea (uk 21)
   Kijana mmoja wakati wa vurumai baada ya uchaguzi analalamikia uongozi duni unaohimiza elimu duni isiowasaidia vijana. Anasema elimu inafaa kuwafunza ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kujitegemea.
  • Nyenzo ya kuzindua jamii. (uk 38-39)
   Shuleni Tila wanafunzwa kuhusu mabadiliko, uwajibikaji wa mtu usipimwe kutokana na jinsia. Mwekevu anachaguliwa kama kiongozi baada ya jamii kuzinduliwa.
  • Nyenzo ya kutoa maarifa ya kuendeleza jamii. (uk 67-68)
   Lunga anatumia elimu katika kilimo kuwaelimisha raia kuhusu mbinu bora za kilimo
  • Nyenzo ya kuleta mabadiliko. (uk 97)
   Mwanaheri anajiunga na shule ya Tangamano kwa lengo la kuandama elimu ili aweze kuleta mabadiliko katika jamii.
  • Nyenzo ya kuwaokoa vijana kutokana uovu. Uk88
   Hazina anaokolewa kutokana na kinamasi cha uvutaju gundi na matumizi ya mihadarati anapopelekwa shuleni katika mradi wa serikali.
  • NJia ya kukabiliana na changamoto za maisha (uk 88)
   Hazina anapata kazi katika hoteli , wengi wao (watoto wa mtaani)ni maseremala, waashi na mafundi wa juakali baada ya kuelimishwa.
  • Nyenzo ya kuondoa mwemeo wa mawazo/huzuni (uk92)
   Wasichana katika shule ya Tangamano wanatumia fursa hiyo kusimulia juu ya maisha yao na kuliwazana. Walimu pia wanawaliza wanafunzi wao na kuwapa matumaini..mf Mtawa Pacha anamliwaza Zohali.
  • Chanzo cha kuboresha miundo msingi katika jamii
   Ridhaa anajenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya.
   Serikali inajenga makao ya watoto pamoja na shule ili kufadhili elimu.
  • Kigezo cha kupima uwajibikaji
   Neema anakiokota kitoto barabarani kwani alielewa haki za watoto.
   Mwangeka anamshauri Dick kuacha ulanguzi wa dawa za kulevya na pia anakubali uamuzi wa Apondi kumlea Umu.
   Mwekevu anaikwamua jamii kwa miradi ya maji kinyume na wagombea wenza

Swali la dondoo 8

“Una bahati kupata mfadhili, mimi mzazi wangu wa pekee ni mama ambaye ni muuza samaki na baada ya ule mzozo… biashara imepigwa na mawimbi makali.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo    (alama 4)
 2. Jadili jinsi mwandishi alivyoshughulikia maudhui ya ufadhili. (alama 6)
 3. Ukirejelea hadithi zozote tano riwayani, onyesha jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya hadithi ndani ya hadithi kujenga maudhui.(alama 10)

Majibu ya dondoo 8

 1.  
  • Msemaji ni Kairu
  • Anamwambia Umu
  • Bwenini, shule ya Tangamano pamoja na wanafunzi wengine; Zohali, Chandachema na Mwanaheri.
  • Baada ya Umu kusimulia hadithi yake na jinsi alivyopata ufadhili katika makao.
 2.  
  • Shirika la Makai Bora lilijitolea kuwajengea wakimbizi nyumba bora.
  • Misikiti na makanisa yalikusanya magunia ya vyakula kuwalisha wakimbizi. (CWA, Woman’s Guild, Mothers Union)
  • Serikali inajenga makao ya watoto wa mtaani na kufadhili elimu yao. Mf Hazina (uk 88)
  • Serikali inazindua hazina ya kufadhili masomo ya watoto (Idara ya Watoto). Mf Umu (uk 89)
  • Kituo cha Wakfu wa Mama Paulina kinawafadhili watoto wa mtaani kama Zohali.
  • Familia ya Bw. Tenge inamfadhili Chandachema kwa kukubali kuishi naye anapopata nafasi katika shule ya Msingi ya Kilimo (uk105)
  • Shirika la kidini la Hakikisho la Haki na Utulivu lilimpeleka Chandachema katika makao ya Jeshi la Wajane (uk 107)
  • Ridhaa anawasomesha wapwaze Mzee Kedi .
 3.   
  • Hadithi ya Billy na Sally (uk 80)
   -mapenzi na ndoa       -usaliti             -utabaka
  • Hadithi ya Lemi na Tindi (uk 121)
   -Anasa -ukatili/ mauaji
  • Hadithi ya Pete (uk 146)
   -Ndoa (migogoro)       -malezi duni    -utamaduni ( tohara,ndoa za lazima) -taasubi ya kime          -ajira duni       -ukatili/uavyaji mimba
  • Chandachema (uk 102)
   -elimu              -tanzia/mauti   -ukiukaji wa haki za watoto( malezi duni, ajira) -umaskini         -ukware
  • Hadithi ya Zohali (uk 98)
   -utabaka          -elimu              -malezi duni/kutowajibika/ ukiukaji wa haki za watoto -majuto                        -changamoto za vijana( mimba za mapema)
  • Hadithi ya Mwanaheri (uk 93)
   -elimu              -ndoa na changamoto zake -ukabila           -majuto            -mauti
  • Kairu (uk 91)
   -tanzia             -utamaduni                              -ukimbizi -umaskini         -malezi duni

Swali la Dondoo 9

‘…familia yake bado inamiliki mashamba ya michai na mibuni pamoja na mashirika mengi…’

 1. Weka dondoo hili katika muktadha wake.      (alama 4)
 2. Kwa kurejelea mifano minane, eleza umuhimu wa msemaji katika kujenga riwaya hii. (alama 8)
 3. Jadili kwa hoja nane suala la ukoloni mambo leo lilivyoshugulikiwa katika riwaya. (alama 8)

Majibu ya dondoo 9

 1.  
  • Maneno ya Chandachema
  • Akiwaambia Umu, Zohali na Mwanaheri.
  • Wakiwa katika bweni la wasichana ya Shule ya Tangamano.
  • Alikuwa akiwaeleza usuli wa uwepo wake katika shule hiyo. 1X4 = 4

  • Mmoja kati ya wasimulizi wa hadithi ya Chozi la heri ndiye anayesimulia kuhusu maisha ya wahusika kama vile Fumba na Tenge.
  • Kupitia kwake, mwandishi anasisitiza umuhimu wa familia katika malezi.
  • Baba anamtelekezea kwa nyanyake baada ya kifo cha nyanya, anaishi katika familia ya jirani yao Satua, na hatimaye kwa Tenge. Hawa wote wana mchango katika malezi yake.
  • Mwandishi amemtumia kukashifu ukiukaji wa haki za kibinadamu. Baba yake anamtunga mwanafunzi wake mimba na baadaye kumtelekeza mtoto -Chandachema.
  • Chandachema anaendeleza ajira ya watoto. Anafanya kazi katika shamba la chai kwa malipo kidogo.
  • Anachimuza umuhimu wa mashirika ya kidini katika kutetea haki za kibinadamu. Makao ya Jeshi la wajane Wakristo yanawahifadhi watoto waliotupwa na wazazi pamoja na wale wazazi wahitaji.
  • Ni kielekezo cha vijana wasiokata tamaa. Anawaambia akina Umu kuwa atajitahidi masomoni ili ahitimu kuwa mwanasheria au afisa wa maslahi ya kijamii na kuweza kutetea haki za kibinadamu.
  • Anaendeleza maudhui ya elimu na kuonyesha jinsi elimu inachangia kuleta mustakabali mwema wa msomi siku za usoni. Chandachema angependa kuwa Mwanasheria au Afisa wa maslahi ya Kijamii na kuweza kutetea haki za binadamu
  • Kupitia kwake, dhiki zinazowapata wafanyikazi wa kima cha chini zinaangaziwa.
  • Anafunza mbinu-ishi ya uvumilivu. Anavumilia maisha ya taabu baadaya kifo cha nyanyake hadi anapopata ufadhili na kujiunga na shule yaTangamano.
  • Anajenga tabia za wahusika. Kupitia kwake, tunaona utu wa Waridi anayemsomesha, ukatili na ukosefu wa uwajibikaji wa Fumba ambaye anamuacha Chandachema kulelewa na nyanya yake, Fumba mwenyewe akihamia ng’ambo na familia nyingine.
  • Uzinifu wa Bwana Tenge kunakusababisha dhiki ya kisaikolojia kwa wanawe na Chandachema
 2. Jadili kwa hoja nane suala la ukoloni mamboleo lilivyoshugulikiwa katika riwaya. (alama 8)
  • Watoto wa walowezi wa kikoloni kumiliki mashamba yaliyomilikiwa na familia zao-shamba la Tengenea,wazungu wanamiliki mashamba ya michai na mibuni pamoja na mashirika ya utengenezaji wa mazao ya mimea nchini.
  • Baadhi wa Wahafidhina wanamiliki mashamba huku Waafrika wengine wakiwa maskwota au wafanyikazi-Kangata anafanya kazi na kuishi katika shamba la Kiriri.Watoto wa Kangata hata wanajitambulisha kwa jina la Kangata.
  • Wahafidhina inaendeleza umilikinafsi wa ardhi ulioanzishwa na mzungu.
  • Wageni kuamua kitakachokuzwa Wahafidhina.
  • Unyonyaji-wenyeji kukuza zao na kuwapa wageni kuwasagia huku wakiwauzia kwa bei ghali.
  • Mifumo kandamizi ya utawala- uongozi unatuma vyombo vya dola kudhibiti upinzani
  • Utegemezi. Wanahafidhina wanawategemea washiria wa kimaendeleo wakati mikasa inapotokea. Kudhibitiwa na malengo ya kimataifa- Tila anamwambia Ridhaa kwamba wangependa kufikia Malengo ya Kimilenia. Haya ni matakwa ya kimataifa ambayo nchi hujifunga kutimiza.
  • Kampuni za kigeni kuchimbua madini katika sehemu za mashambani na fedha kuwaendea hao hao wageni. Raia wanaoajiriwa kuchimbua madini kulipwa mshahara duni.Tila analalamikia haya.
  • Hoja zozote 8

Swali la dondoo 10

 1. ``Kumbe hata wewe shemeji..............upo?’’
  ``ndio tu hapa na wengi’’
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.    alama 4
  2. 'Wengi ‘ wanaorejelewa katika dondoo hili walikumbwa na matatizo yapi?   alama 8
 2. ``Kule kulazimika kupapasa kwenye giza kutafuta............’’
     Mrejelewa katika kauli hii anayafichua maovu yapi katika jamii?   alama 8

Majibu ya dondoo 10

 1.  
  1.  
   • Kauli ya kwanza ni ya Ridhaa. Anamwambia Kaizari.
   • Kauli ya pili ni jibu la Kaisari kwa Ridhaa.
   • Walikuwa kambi ya wakimbizi.
   • Ridhaa alikuwa amemwona shemeji yake Kaizari alipotoka kutafuta mizizi mwithi kutokana na uhaba wa chakula kambini.
  2.  Matatizo yanayowakumba wakimbizi.
   • Msongamano kambini- Kairu anasema kuwa uongozi mpya haukusuruhisha matatizo yao bali uliwapa ardhi zaidi wajenge vibanda na kupunguza msongamano kambini     (uk a2)
   • Kukata tamaa- Baada ya kusubiri kwa muda mrefu kurudishwa nyumbani, wakimbizi hukata tama. Kairu anasema kuwa hawaoni kama pana nyumbani pema zaidi kuliko kule kambin ( uk 92)
   • Umaskini – Mamake Kairu hana uwezo wa kulipa karo kwa wakati. Anategemea biashara ya kuuza samaki ambayo imeathiriwa sana baada ya mzozo kuhusu umiliki wa ziwa kuu ( uk 93)
   • Wakimbizi wanaorejea kwao wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa tena.( uk 94) Mzee kaisari aliishi kwa hofu ya kushambuliwa tena hata baada ya kuhakikishiwa na wenyeji kuwa hilo halitawahi kutokea tena (94uk)
   • Mazingira machafu. Ukosefu wa maji safi ukosefu wa vyoo.
   • Njaa kula matunda mwitu.
   • Magonjwa, homa ya matumbo, kipindupindu
   • Safari ndefu
   • Dhiki za kisaikolojia wanaishi katika sehemu walizosongamana wakiwa na watoto wake na wazazi pamoja. (hoja 8x1=8)
 2.  
  • Ukosefu wa glavu za kuwahudumia wanawake wanaojifungua
  • Ukosefu wa umeme na hivyo wauguzi hufanya kazi gizani.
  • Usimamizi wa hospitali kutolipia bili za sitima.
  • Wagojwa kufa kwa kukosa huduma za kimsingi.
  • Ukosefu wa dawa na zilizopo kuuziwa wasimamizi wa hospital wenye maduka.
  • Uongo mwingi kama wa performance contract, kuimarisha kampeni dhidi ya polio na kuwachanja watoto wate chini ya umri wa miaka mitano kujenga vituo zaidi vya kutolea huduma za ushairi kwa waathiriwa wa UKIMWI na saratani.
  • Chanjo ya polio huuziwa maskini
  • Wenye uwezo kiuchumi hunyekua dawa za ukimwi na saratani zilizotengewa raia wasiojiweza.  (hoja 8x1=8)

Swali la Dondoo 11

“…liandikwalo ndilo liwalo? since when has man ever changed his destiny?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
 2. Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (al 6)
 3. Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, liandikwalo ndilo liwalo”, inavyojitokeza katika Chozi la Heri. (al 10)

Majibu ya Dondoo 11

“….liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
  • Maneno ya Terry
  • Akimwambia Ridhaa
  • Nyumbani kwao
  • Baada ya kugundua kuwa anaamini ushirikina
  • Ni mawazo ya Ridhaa akikumbuka maneno aliyoambiwa na mkewe Terry
  • Kwa sababu ya kuamini kuwa milio ya bundi na kerenge’nde huashiria jambo Fulani lingefanyijka.
  • Yuko kando ya vifusi vya nyumba yake iliyochomwa
  • Baada ya familia yake kuchomewa ndani.
 2. Bainisha mbinu tatu za kumtindo zinazojitokesa katika dondoo hili. (al 6)
  • Methali –liandikwalo ndilo liwalo
  • Kuhamisha ndimi/msimbo-kauli ya kutumia sentensi nzima kwa lugha nyingine.
  • Since when has man ever changed his destiny?
   Tanbihi: mbinu hii si kuchanganya ndimi. Atakayeandika hivi asituzwe.
  • Swali la balagha – “liandikwalo ndilo liwalo?
   Since whaen has man ever changed his destiny?”
   3x2
 3. Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, “liandikwalo ndilo liwalo”, inavyojitokeza katika Chozi la Heri. (al 10)
  • Neema na Mwangemi wanajitahidi kupata mtoto lakini hawafanikiwi na wanaishia kumpanga Mwaliko.
  • Wafuasi wa Mwanzi wanajaribu kushinda wa mwekevu lakini wanashindwa.
  • Kaizari anajitahidi kuzuia wahuni wasiwabake binti zake lakini wanamzidi nguvu na kuwabaka.
  • Lunga anajitahidi kumrithia na kumpendekeza mkewe Naomi lakini hatimaye anamtoroka na kumwachia Watoto
  • Kiriri anampinga Annette asiende ughaibuni lakini anampuuza na kuhamia huko.
  • Kiriri anawasihi wanawe warudi nyumbani lakini waliendelea kuishi ughaibuni hata baada ya kukamilisha masomo yao.
  • nyanyake Pete anajizatiti kupinga ndoa ya Pete lakini hatimaye Pete anaozwa.
  • Kipanga anataka kuambiwa babake halisi baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana lakini mamake hakumwambia.
  • hata baada ya mabwanyenye kutoa hongo ili nyumba zao zisibomolewe katika mtaa wa Tononokeni, zilibomolewa.
  • Dick anakataa kutumiwa na Buda kulangua dawa za kulevya lakini anamtishia na baadaye kuuza dawa za kulevya.
  • Naomi alimtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini lakini anaishia kuteseka Zaidi na baadaye kufa
  • Amize Lucia wanajizatiti kupinga ndoa ya Lucia lakini baadaye Lucia anaolewe.
  • Wanaume wanatishia kumtusi Mwekevu anapojitosa siasani ili kumvunja moyo lakini anavumilia mpaka anachaguliwa kuwa kiongozi wa Wahafidhani.
  • Pete anakunywa dawa ya kuua panya ili afe lakini anapelekwa kituo cha afy cha Mwanzo Mpya na kuendelea kuishi.
  • Pete anajaribu kuavya mimba ya mtoto wake wa pili na wa tatu lakini anaishi kuwazaa watoto hawa.
   (zozote 10x1=10)

Swali la Dondoo 12

"Maisha yangu yalijaa shubiri tangu utotoni."

 1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
 2. Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
 3. Jadili jinsi mwandishi amesawiri suala la ukatili. (alama 12)

Majibu ya Dondoo 12

 1.    
  • Maneno ya Chandachema
  • Kwa Zohali, Umu, Kairu na  Mwanaheri
  • Bwenini shuleni Tangamano
  • Walikuwa wakihadithia maisha yao ili kumliwaza Umu asione kuwa ni yeye tu amepitia magumu.
 2.    
  • chuku- maisha kujaa shubiri tangu utotoni
  • jazanda- shubiri-mahangaiko/ shida/tabu/ matatizo
 3.    
  • Kuchoma. Kedi kuchoma familia ya Ridhaa./ Raia kuchoma Lemi. 
  • Kunyakua wa ardhi ya wengine.
  • Wakoloni kuchukua ile ardhi ya Waafrika iliyokuwa na rutuba.
  • Kulazimishwa kazi. Wakoloni kutumia vijana.
  • Kulawitiwa. Vijana walilalitiwa na hakuna aliyewatetea.
  • Vitisho. Mwekevu kutukanwa na kutishwa na wanaume anapowania uongozi.
  • Mauaji. Polisi kuua wakimbizi/
  • Kukatwa. Subira
  • Kubakwa. Lime na Mwanaheri. / Maya kubaka Sauna.
  • Kutishia afya. Viongozi kumwaga taka mtaa wa Sombera.
  • Kuuzia raia mahindi yaliyoharibika.
  • Kuteka nyara. Sauna
  • Kudhalilisha watoto. Wazazi wa Zohali.
  • Kupachika mwanafunzi mimba. Fumba kwa Rehema.
  • Tohara kwa wasichana. Tuama kuunga mkono.
  • Kuozwa mapema. Pete kuozwa na mamake na wajomba kwa Fungo.
  • Kuavyawa. Pete/ Sauna waliavya mimba na kunyimana nafasi ya kuishi.  
   Zozote 12

Swali la Dondoo 13

“Kumbe hata mja akafanikiwa vipi kielimu na kitaaluma, maisha yake huwa ombwe bila mwana, awe wa kuzaa au wa kulea?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
 2. Taja tamathali moja iliotumika katika dondoo (alama 1)
 3. Onyesha ukweli wa kauli hii ukirejelea wahusika wowote watano riwayani (alama 5)
 4. Fafanua umuhimu wa elimu katika jamii ukirejelea riwaya nzima. (alama 10)

Majibu ya Dondoo 13

 1. Muktadha wa dondoo (alama 4)
  • Msemaji ni Mwangeka
  • Anajisemea kimoyomoyo ( uzungumzi nafsi)
  • Yeye na Neema wako katika afisi ya Annastacia katika kituo cha watoto cha Benefactor
  • Wamekwenda kumchukua mwanao wa kupanga (Mwaliko) baada ya kukosa kufanikiwa kuwa wan a mwana wa kuzaliwa. Wanamlea kwa tunu na kumsomesha hadi chuo kikuu.
 2. Tamathali moja (alama 1)
  • Istiara- maisha huwa ombwe
 3. Ukweli wa kauli (alama 5)
  1. Selume – amehitimu kuwa mkunga na kuajiriwa kama muuguzi katika hospitali kuu ya Tumaini na hatimaye katika kituo cha Afya cha Mwanzo Mpya.
   Maisha yake yanaonekana kuwa ombwe baada ya kutengana na mumewe ambaye anachukua binti yao Hajui kama atakutana na mwanawe Sara baada ya mumewe kuoa msichna wa kikwao
  2. Ridhaa- amehitimu katika taaluma ya udaktari na kufanikiwa maishani. Ni mkurugenzi, mfanyi biashara mkubwa na anamiliki hospitali ya Mwanzo Mpya
   Maisha yake yanaonekana kuwa ombwe anapopoteza mwanawe Dede na Tila baada ya jumba lake kuchomwa na mzee Kedi. Anapomkumbuka Tila anatokwa na machozi yanayolovya kifua chake.
  3. Mwangeka- amehitimu katika taaluma ya uhandisi, anajiunga na vikosi vya usalama na kupanda ngazi hadi juu.
   Maisha yake yanakuwa ombwe anapompoteza bintiye Becky katika mkasa wa moto, anabaki katika upweke mkuu. Anajuta kutofuata ushauri wa mkewe Lily. (uk62)
   Apondi anapoamua kumlea Umu, Mwangeka anamwona Umu kama Baraka kutoka kwa Mungu, fidia ya mwanawe aliyekufa. (uk 118)
  4.  Neema na Mwangemi- Neema amehitimu katika taaluma ya uhasibu na ameajiriwa katika Hazina ya Kitaifa kama hasibu mwandamizi na Mwangemi ana shahada ya uzamili katika uuguzi. Miaka mitano katika ndoa bila mtoto inawahuzunisha, wanachekwa kuwa Neema hawezi kulea mimba.
   Maisha yao yanakuwa ombwe wanapompoteza mwanao Bahati kutokana na ugonjwa wa sickle-cell.
   Hatimaye wanaamua kupanga mtoto, wanajaliwa kupata Mwaliko (uk 159-167)
  5. Naomi- anamwacha Lunga na kwenda kutafuta riziki baada ya Lunga kupoteza kazi na mali yake.
   Hatimaye anajuta kuwatelekeza wanawe, anawatafuta kote na anapata habari kuwa Dick na Mwaliko waliibwa na Sauna anahuzunika.
 4. Umuhimu wa elimu (alama 10)
  1. Chombo cha kueneza amani na upendo (uk 11)
   Mamake Ridhaa anamtuliza Ridhaa baada ya kusimangwa na wanafunzi wenzake shuleni na kumshauri kuwa ni vyema kujifunza kuishi na wenzake bila kujali tofauti za ukoo na nasaba.
  2. Nyenzo ya kumfikisha binadamu kwenye kilele cha ufanisi (uk 11)
   Mwangeka, Ridhaa, Mwangemi, Lunga n.k wanafanikiwa maishani kutokana na elimu.
  3. Chanzo cha umilisi na stadi za kujitegemea (uk 21)
   Kijana mmoja wakati wa vurumai baada ya uchaguzi analalamikia uongozi duni unaohimiza elimu duni isiowasaidia vijana. Anasema elimu inafaa kuwafunza ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kujitegemea.
  4. Nyenzo ya kuzindua jamii. (uk 38-39)
   Shuleni Tila wanafunzwa kuhusu mabadiliko, uwajibikaji wa mtu usipimwe kutokana na jinsia. Mwekevu anachaguliwa kama kiongozi baada ya jamii kuzinduliwa.
  5. Nyenzo ya kutoa maarifa ya kuendeleza jamii. (uk 67-68)
   Lunga anatumia elimu katika kilimo kuwaelimisha raia kuhusu mbinu bora za kilimo
  6. Nyenzo ya kuleta mabadiliko. (uk 97)
   Mwanaheri anajiunga na shule ya Tangamano kwa lengo la kuandama elimu ili aweze kuleta mabadiliko katika jamii.
  7. Nyenzo ya kuwaokoa vijana kutokana uovu. Uk88
   Hazina anaokolewa kutokana na kinamasi cha uvutaju gundi na matumizi ya mihadarati anapopelekwa shuleni katika mradi wa serikali.
  8. NJia ya kukabiliana na changamoto za maisha (uk 88)
   Hazina anapata kazi katika hoteli , wengi wao (watoto wa mtaani)ni maseremala, waashi na mafundi wa juakali baada ya kuelimishwa.
  9. Nyenzo ya kuondoa mwemeo wa mawazo/huzuni (uk92)
   Wasichana katika shule ya Tangamano wanatumia fursa hiyo kusimulia juu ya maisha yao na kuliwazana. Walimu pia wanawaliza wanafunzi wao na kuwapa matumaini..mf Mtawa Pacha anamliwaza Zohali.
  10. Chanzo cha kuboresha miundo msingi katika jamii
   Ridhaa anajenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya.
   Serikali inajenga makao ya watoto pamoja na shule ili kufadhili elimu.
  11. Kigezo cha kupima uwajibikaji
   Neema anakiokota kitoto barabarani kwani alielewa haki za watoto.
   Mwangeka anamshauri Dick kuacha ulanguzi wa dawa za kulevya na pia anakubali uamuzi wa Apondi kumlea Umu.
   Mwekevu anaikwamua jamii kwa miradi ya maji kinyume na wagombea wenza

Swali la Dondoo 14

Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba, mmoja baada ya mwingine.
 1. Bainisha muktadha wa dondoo hili.                                      (alama 4)
 2. Eleza sifa tatu za anayerejelewa.                                                 (alama 3)
 3. Eleza tamathali ya usemi katika dondoo.                            (alama 2)
 4. Fafanua masaibu yaliyomkumba mrejelewa           (alama 3)

Majibu ya Dondoo 14

 1. Bainisha muktadha wa dondoo hili.                                      (alama 4)
  • Ni maneno ya mwandishi/msimulizi.
  • Anamrejelea Lunga Kiriri Kangata
  • Ni baada ya kutolewa katika Msitu wa Mamba.
  • Moyo wa Lunga ulikuwa umekataa kuyakubali mazingira mapya katika Mlima wa Simba.
 2. Eleza sifa tatu za anayerejelewa.                                                 (alama 3)
  • Msomi – alikuwa anasomea kilimo ambapo baadaye aliajiriwa kama Afisa wa Kilimo nyanjani.
  • Mhifadhi mazingira/mwajibikaji – aliasisi Chama  cha Watunza Mazingira wasio na Mipaka akiwa shuleni. Anawahutubia kuhusu uhifadhi wa mazingira.
  • Mwenye bidii – baada ya kustaafishwa anafanya kazi ya ukulima kwa bidii hadi anaitwa jina la msimbo ‘ mkulima namba wani’.
  • Mwenye msimamo thabiti – licha ya rai za wakubwa anapinga tendo la kuwapa raia mahindi yaliyoharibika.
  • Mtetezi wa haki – anahiari kupoteza riziki ili kuyaokoa maisha ya wanyonge wasio na hatia.
  • Mwenye tamaa- anapoona uzuri wa zao la mahindi katika shamba la babake, anapatwa na uchu unaolemaza uadilifu wake.
  • Mwenye mapenzi ya dhati – anajisabilia kwa hali na mali kumridhia na kumpendeza mkewe.
 3. Eleza tamathali ya usemi katika dondoo.                            (alama 2)
  • Tashbihi – alijiona kama mfa maji
   Kutaja 1 kueleza 1
 4. Fafanua masaibu yaliyomkumba mrejelewa           (alama 3)
  • Kuachishwa kazi kwa kupinga uagizaji wa mahindi mabaya.
  • Kufukuzwa katika Msitu wa Mamba hivyo kupoteza mali yake yote.
  • Anakosa pesa za kuwapeleka wanawe hata katika shule za watu wa kima wastani kwa sababu alilipwa fidia isiyotosha.
  • Anawapoteza ndugu na marafiki zake.
  • Kuachwa na mkewe Naomi.
  • Kufurushwa kutoka kwa Kiriri wakati wa wa zahama baada ya kutawazwa.       

Swali la Dondoo 15

“Maisha yangu yalianza kwenda tenge nilipojiunga na kidato cha pili. Unajua hali ya mtafaruku wa kihisia inayowapata vijana…”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Bainisha kipengele kimoja cha kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
 3. Fafanua umuhimu wa nafsineni katika kuijenga riwaya hii. (alama 4)
 4. Kando na nafsineni. Eleza jinsi maisha yalivyowaendea tenge vijana wengine katika riwaya hii. (alama 10)

Majibu ya Dondoo 15

 1. Msemaji – zahali
  Msemewa/wasemewa- umu, kairu, mwanaheri, chandachema.
  Mahali – kwenye bweni katika shule ya Tangamano.
  Sababu – Ni baada ya zohali kusimuliwa utambaji wa marafiki zake kuhusu hali yao ya maisha ambao ulimchochea na kwatolea wenzake duku duku lake. 3x1=4
 2. Nahau – kwenda tenge. 1x2=2
 3.      
  • Anajenga tabia za wahusika wengine. Mfano babake ni katili.
  • Anajenga ploti. Usimulizi wake unatupa chanzo cha kuondoka nyumbani, kwenda mtaani na hatimaye katika wakfu wa mama Paulina.
  • Kupitia kwake tunaona changamoto zinazowakumba vijana. Anaambulia ujauzito katika umri mdogo na kusitisha masomo yake.
  • Anaonyesha dhiki za familia za mitaani. Yeye na wenzake wanalala kwenye barabara.
  • Anajenga maudhui ya malezi baada ya kupata ujauzito wazazi wake wanamtekeleza na anaamua kuondoka hadi mtawa wa pacha.

Swali la Dondoo 16

 1. … haya imekuandama tangu usiku ukimtongoza fulani; siku za kuchora ramani ya Afrika kwa vyanda vya miguu hadi sasa? Ama ni hizo mvi unaficha ? Nasikia ile mid-life crisis ikawashika wazee ndiyo hivyo;
  1. Weka dondoo hili kwenye muktadha wake. (alama 4)
  2. Tambua mbinu zozote tatu za kimtindo kwenye dondoo hili.(alama 4)
  3. Jadili sifa zozote sita za msemewa katika dondoo hili.(alama 6)
 2. Sauna amechangia vipi katika kuendeleza ploti katika Riwaya ya Chozi la Heri.(Alama 6)

Majibu ya Dondoo 16

 1.  
  1. Weka dondoo hili kwenye muktadha wake. (alama  4)
   • Msemaji  ni Terry mawazoni mwa Ridhaa.
   • Msemewa ni Ridhaa 
   • Ridhaa yuko kwenye mawazo uwanjani wa ndege wa Rubaa
   • Anakumbuka maisha yake mkewe na aila yake huku akimngoja Mwangeka awasili anayetoka ng’ambo.
  2. Tambua mbinu zozote tatu za kimtindo kwenye dondoo hili.(alama 4)
   • Taswira mwono-kuchora Ramani ya Afrika
   • Maswali balagha-Hadi sasa?
   • Kuchanganya ndimi-mid-life crisis
   • Mbinu rejeshi-Ridhaa kukumbuka yaliotokea kitambo.
  3. Jadili sifa zozote sita  za msemewa katika dondoo hili.(alama 6)
   • Ni mwenye bidii-alisoma hadi akahitimu kuwa daktari
   • Ni mkarimu-aliwafadhili kimasomo wapwa wa Mzee Mkedi
   • Ni mwajibikaji –alitafuta njia mbadala ya kuchimba misala badala ya kutumia sandarusi
   • Ni mbaraza-alikuwa na uhusiano mzuri na Bibi yake Terry na wanawe
   • Ni mlezi mwema-aliwasomesha watoto wake hadi Mwangeka akahitimu chuo kikuu
   • Mshauri mzuri-anamshauri Mwangeka aoe tena baada ya kumwomboleza bibi yake kwa muda.
    Swali funge-za kwanza 6*1=6
    Kadiria jibu la mwanafunzi
 2. Sauna amechangia vipi katika kuendeleza ploti katika Riwaya ya Chozi la Heri.(Alama 6)
  • Anapata mimba baada ya kubakwa na babake wa kambo Maya
  • Mamake anamkanya kutompaka babake wa mashuzi
  • Amalazimisha kuavya mimba
  • Baadaye Sauna anaamua kutoroka kutoka kwao
  • Anajiingiza kwa biashara haramu na bibi  Kangara ya ulanguzi wa watoto
  • Anapata kazi kwa akina Mwaliko na baada ya mama yao Naomi na baba yao Lunga Kiriri kuaga awamwiba Mwaliko na Dick na kuwaingiza katika biashara haramu
  • Baadaye Sauna na bi Kangara wananaswa na mkono mrefu wa serikali na kutiwa mbaroni

Swali la Dondoo 17

“Sandarusi zenyewe mtu anazitafuta kwenye mlima taka zinazotolewa huko waishio waheshimiwa kuja kutuua huku”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Taja kwa kufafanua mbinu –ishi wakimbizi walizozizua kukumbana na chanagamoto zao.. (alama.12)
 3. Onyesha umuhimu wa msemaji katika kuzua sifa za wahusika wengine. (alama 4)

Majibu ya Dondoo 17

“Sandarusi zenyewe mtu anazitafuta kwenye mlima taka zinazotolewa huko waishio waheshimiwa kuja kutuua huku”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  Masimulizi ya kaizari akimwelekeza Ridhaa wakiwa katika msitu wa Mamba akielezea jinsi maisha yalivyokuwa hapa.
 2. Taja kwa kufafanua mbinu –ishi wakimbizi walizozizua kukumbana na chanagamoto zao..
  1. Watoto wake kupata ushauri nasaha kukabiliana na udhalimu wa kubakwa.
  2. Kuchimba vyoo kukabaliana na tatizo la ukosefu wa misala
  3. Kukubali kupanga foleni ili kupata mgao wa chakula ulioletwa na mashirika tofauti tofauti.
  4. Kula miziz na matunda mwitu ili kuzima njaa ilipowazidi.
  5. Kujijengea vibanda ili kupata pahali pa kujisitiri.
  6. Wazazi kutafuta muda wa kuhusiana kimapenzi mchana wakati watoto wao walitoka kucheza.
  7. Kutobaguana kicheo au kitabaka katika kambi hii.
   hoja 6 x 2 = (alama.12)
 3. Onyesha umuhimu wa msemaji katika kuzua sifa za wahusika wengine. (alama 4)
  Kizani anauza sifa za
  1. Ridhaa – Mshauri mzuri anapowashauri wenzake kambini kuchimba misala
   Anakubali mabadiliko yaliompata kambini na kuamua kuendelea na maisha.
  2. Selume – Ana kihoro – anaposimulia chanzo chake cha kubagwaliwa na aila ya mumewe kwa msingi eti alimpigia kura Mwekevu.
   - Pia ana heshima – anapotambulisha ujio wake kwa kina Kaizani kabla akaribie kibanda chao.


Swali la Dondoo 18

“Nyamaza wewe! Nyinnyi ndio mnaoturudisha nyuma miaka yote hii!”

 1. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
 2. Kwa kurejelea hoja saba, eleza jinsi msemaji alivyorudishwa nyuma (alama 7)
 3. Eleza umuhimu wa msemaji katika riwaya (alama 6)
 4. Eleza toni ya dondoo hili (alama2)
 5. Toa sifa moja ya msemaji katika dondoo hili. (alama1)

Majibu ya Dondoo 18

 1.  
  1. Msemaji- Kijana mwenye fulana iliyoandikwa ’Hitman’ mgongoni
  2. Msemewa- Mmoja wa wasafiri/kiongozi aliyekuwa ndani ya gari/Mbwenyenye ndani ya gari
  3. Mahali- Barabarani
  4. Kiini- Hasira kutokana na uhaba wa kazi hata baada ya kuhitimu
   4x1
   TANBIHI: Hakuna mhusika anayeitwa Hitman
 2.                                    
  1. Vishahada vya vyuo haviwasaidii kupata ajira k.m mate yawakauka vinywani wakifunga bahasha za kutafuta kazi.
  2. Wanafunzwa kukariri nadharia bila kuwazia umilisi, stadi,kufungiwa njuga za kujitegemea
  3. Mtu anapata digrii tatu na kula lami kwa miaka kumi
  4. Kukosa mtaji wa kuanzisha biashara – ujasiriamali
  5. Unyakuzi wa ardhi
  6. Tume za kuchunguza kashfa za unyakuzi wa ardhi hazitoi ripoti baada ya uchunguzi-ripoti zinakuwa Rafiki wa rafu makavazini.
  7. Unafiki wa viongozi wanaojifanya kuwahurumia vijana- kumbe ni machozi ya mamba
  8. Kuhongwa kwa vijana wakati wa kura- kuhadaiwa kwa vihela vya kushikilia uhai
  9. Njama za kifisadi -kudanganywa kwa ajuza wazee kutia alama ya makasi kwenye kura kuonyesha hamtaki kiongozi na hivyo kumpigia kura pasi na kujua
  10. Uwezo wa kuzalisha mali haupo nchini
  11. Ukabila- k.m katika hazina ya vijana
  12. Unasaba-k.m katika hazina ya vijana  7x1
   Za kwanza saba
 3.                            
  1. Mwenye hasira k.m ‘”nyamaza wewe!”
   Lazima atoe mfano, la sivyo apewe nusu alama
   1x1
 4. Uchungu/huzuni/masikitiko/majonzi   2x1
 5. Kupitia kwake tunapata kujua kuhusu:
  1. Hadaa za viongozi kuhusu ajira
  2. Udanganyifu wa viongozi wakati wa kupiga kura
  3. Upungufu/ sera mbovu ya elimu chuoni
  4. Ufisadi katika miradi ya kusaidia vijana-ukabila na unasaba
  5. Ukosefu wa kazi
   Anaendeleza maudhui yafuatayo:
  6. Elimu
  7. Kutamauka
  8. Ukatili (mauaji)
  9. Unyakuzi wa ardhi
  10. Uharibifu wa mali (kuchoma magari)

Swali la Dondoo 19

“Lakini itakuwaje historical injustice, nawe Ridhaa hapo ulipo sicho kitovu chako?”

 1. Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4) 
 2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (Alama 4)
 3. Eleza umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya. (Alama 4)
 4. Ni mambo gani yaliyowakumba walioishi penye kitovu kisicho chao? (Alama 8)

Majibu ya Dondoo 19

 “Lakini itakuwaje historical injustice, nawe Ridhaa hapo ulipo sicho kitovu chako?”

 1. Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
  • Haya ni mawazo ya Ridhaa. Ridhaa yupo katika lililokuwa jumba lake ambalo lilikuwa sasa limeteketezwa na Mzee Kedi na kuangamiza familia yake. Ridhaa anakumbuka mijadala mipana aliyokuwa na bintiye Annatila (Tila). Ridhaa anahuzunika jinsi Waafrika walivyofanyishwa kazi ngumu, wakiwamo watoto wadogo wasiokomaa. Anamuuliza Tila mawazoni kama hali hii ndiyo historical injustice, ila anajikumbusha kuwa naye hakuwa mzaliwa asilia wa eneo lile. (Hoja 4×1= 4)
 2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (Alama 4)
  • Uzungumzi nafsia- Ridhaa anakumbuka mjadala wake na Tila.
  • Kisengere nyuma/mbinu rejeshi- Ridhaa anakumbuka mjadala wake na Tila.
  • Balagha- hapo ulipo sicho kitovu chako?
  • Kuchanganya ndimi- lakini itakuwaje historical injustice.         (zozote 2×2= 4 - kutaja 1, kueleza 1)
 3. Eleza umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya. (Alama 4)
  Umuhimu wa Ridhaa
  • Anawakilisha watu walio na uwezo wa kukumbuka mambo muhimu yanayotokea maishani mwao.
  • Anaonyesha watu ambao wanaendelea kuwa na imani katika ushirikina na uhalisia wake katika jamii ya kisasa.
  • Anawakilisha watu walio na bidii katika shughuli za kuiauni jamii zao.
  • Anawakilisha watu wazalendo wanaoitetea jamii zao.
  • Ni kiwakilishi cha waathiriwa wa siasa za kikabila na athari zake kwa jamii.
  • Anaonyesha watu wenye moyo na imani walio tayari kuwasaidia watu na watoto wa wazazi wengine.
   (zozote 4×1= 4- lazima mtahiniwa ataje kuwa msemaji ni Ridhaa ndiposa apate alama za umuhimu)
 4. Ni mambo gani yaliyowakumba walioishi penye kitovu kisicho chao? (Alama 8) 
  • Walibaguliwa na wenzao- Ridhaa alibaguliwa shuleni.
  • Walifurushwa makwao- Ridhaa, Kaizari
  • Walivamiwa na kupigwa- Kaizari, mkewe na wanao.
  • Walilazimika kuwa wakimbizi.
  • Chakula kilikuwa adimu.
  • Kulikuwa na changamoto ya maji safi ya kunywa.
  • Kama wakimbizi, wengi walipata homa ya matumbo.
  • Wengine kuyapoteza maisha yao.
  • Wakimbizi walizidi kuongezeka nayo hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu.
  • Idadi kubwa ya wakimbizi ilifanya kuwe na vyoo vya kupeperushwa.
  • Tishio la maenezi ya kipindupindu.
   (zozote 8×1= 8- mtahiniwa aeleze hoja zake kwa mifano ili atuzwe alama 1)

Swali la Dondoo 20

“Sijui kama kijana umesoma ile nadharia ya “deconstruction”. Ni muhimu pia ujue kwamba , ikiwa unataka kujiokoa au kuzoea hali mbaya inayokukabili, ni muhimu kujiingiza katika hali yenyewe, ukaikabili vilivyo ili uache kuiogopa , au iache kukuathiri vibaya.’’

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili ( alama 4)
 2. Tambua mbinu ya lugha iliyotumika kwenye dondoo. ( alama 1)
 3. Eleza sifa nne za msemewa wa dondoo hili. ( alama 4)
 4. Kwa kutolea mifano mwafaka riwayani, jadili nadharia ya ‘Deconstruction’ (alama 11)

Majibu ya Dondoo 20

 1.      
  1. msemaji ni Ridhaa
  2. msemewa ni mwangeka
  3. pale nyumbani mwa Ridhaa/gofu/ganjo/kiunzi
  4. mwangeka alipomtazama baba / Ridhaa kana kwamba anataka kuhakikishiwa jambo/ ridhaa anapokataa kuyaondoa majivuya familia yake iliyoteketea. 
 2. kuchangaya ndimi – deconstruction 
 3. sifa za mwangeka 
  • mwenye utu
  • mshauri bora
  • mlezi mwema
  • amewajibika
  • mwenye upendo
  • mdadisi
  • mwenye majuto
  • mwenye bidii
  • mwenye mawazo mapevu
  • mwenye msimamo imara
  • mzalendo
  • kumbukizi
  • mbunifu
  • mkakamavu/jasiri
  • mvumilivu
  • karimu
  • mtiifu
  • mwenye mzaha/mcheshi/
  • msomi
  • mnyenyekevu 
 4.        
  • ridhaa anakataa kushirikiana na majirani kuyachimba “mass grave” na kuyazika majivu ya familia yake.
  • Mwangeka anamshawishi Ridhaa akibomoe bkiunzi kile cha chumba lakini babake anakataa na kushikilia ndilo kaburi la ukumbusho wa familia yake. 
  • Ridhaa siku za mwanzoni pale kambini hakuweza kuitumia misala ya sandarusi lakini baadaye ilimbidi kujizoazoa na kuyatumia. 
  • Kaizari walipokuwa msituni na aila yake iliwabidi bkukata miti na kuvijenga vijijumba vilivyoezekwa kwa nyasi na kukandikwa udongo baada ya kufukuzwa makwao. 
  • Wakimbizi wakiwemo Ridhaa na Kaizari walipata changamoto ya maji safi ya kunywa lakini kiu ilipobisha hodi iliwabidi wanywe maji yale. 
  • Selume alipokosa glavu na vifaa vingine hopitalini ilimbidi kuvinunua ili awazalishe wajawazito.
  • Umu alipowakosa ndugu zake ilimbidiaanze kuwatafuta na kuelekea hadi kituo cha polisi.
  • Umu ilimbidi aelekeee mjini karaha kuanza maisha mapya /kutafuta usaidizi baada ya kuachwa peke yake.
  • Chandachema alikuwa analala kwingi ikiwemo kwenye michai iliyo na baridi ili aendele na masomo yake. Alifanya hivyo hadi akafuzu katika mtihani.
  • Waziri mstaafu pale kambini alilazimika kuishi maisha ya ukimbizi hata akasaidia katika ugawaji wa chakula. 
  • Dick alipoiingizwa katika biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya alilazimika kufanya kuzisafirisha hadi ughaibu baada ya kutishwa na Buda.
  • Zohali alipoona kuwa pale nyumbani hatakikani baada ya kupata mimba anatorokea mjini anakoanza maisha ya kuzururazurura mtaani.
  • Pete alilazimika kufanya kazi mbalimbali jijini baada ya fungona baadaye nyangumi kumfukuza. Alifanya kazi duni ili kuwakimu wanawe. 
  • Sauna anapobakwa na babake mlezi anaondoka kwao na kuungana na Bi kangara anapohusishwa na biashara ya ulanguzi wa watoto.
  • Mwangemi na Neema wanapokosa mtoto, inawabidi kumchukua mwaliko kama mtoto wao wa kupanga. 
  • Bi. Mwekevu alipojitosa siasani akijua kwamba jamii ina  taasubi dhidi ya wanawake.
  • Lunga anapokataa wananchi kuuziwa mahindi yaliyoharibika na shirika la Maghala na Nafaka akijua ataingia matatani.
  • Ridhaa anapobomolewa na kuchomewa majumba yake, anaendelea na ujenzi hadi anapojenga nyumba mpya ktika mtaa wa Afueni. 
  • Licha ya Mwangeka kumptoteza mkewe Lily na Mwanawe Becky anaamua kumuoa Apondi na kuanza maisha upya.
  • Naomi anaamua kumwacha mumewe na wanawe anaposhindwa kuyavumilia maisha mapya na kuamua kuenda kupambana na ulimwengu , huenda atasaidia familia yake .
  • Viongozi wanaposhindwa kuwajengea wakazi wa mtaa wa somber misala, inawabidi kutumia sandarusi kama misala.
  • Tuama anapashwa tohara baada ya shinikizo kutoka kwa wasichana wenzake na hamwambii babake mzee maarifa. 

Swali la Dondoo 21

Usalama ni mojawapo ya mahitaji ya kibinadamu, kwa hakika, tunaweza kusema kuwa usalama ni mojawapo ya mahitaji ya kimsingi. Bila usalama binadamu hawezi hata kushiriki shughuli………”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala.4)
 2. Eleza umuhimu wa mzungumzaji katika kujenga ploti (ala.8)
 3. Mzungumzaji anazungumzia swala la usalama. Jadili matokeo ya ukosefu wa usalama ukirejelea matukio katika riwaya ya Chozi la Heri. (ala.8)

Majibu ya Dondoo 21

 1.  
  • Kimuundo ni shairi. Unaweza pia kuchukuliwa kama utendi (shairi la ushujaa) kwa sababu unazungumzia sifa za shujaa na vita alivyopigana.
   • Kimaudhui ni sifo/wimbo wa sifa- unamsifu shujaa
 2.  
  1. Matukio ya ajabu kama vile.
   • Kusema na miungu alipozaliwa.
   • anayesema ana nguvu za kipekee japo ni kilema.
   • Anayesema kazaliwa akishika mkuki
  2. Matumizi ya chuku kama vile:
   • maadui elfu kufa anaposhika silaha.
   • Kufagia vijiji vinane kwa pigo moja la kiganja chake.
  3. Utungo unahusu shujaa wa vita- amegpigana vita vingi visivyohesabika
  4. Anayesemwa amezungukwa na migogoro – mahasidi waliochukua mashamba na wasaliti.
  5. Utungo umechanganya historia na mambo ya kidini – anazungumza na miungu anapozaliwa – haya ni mambo ya kiimani.
 3.  
  1. kejeli/stihizai – anaitwa jana la ajabu.
  2. chuku:
   • Kijiji kizima kuja kuona mtoto
   • Maadui elfu kufa kwa anayesemwa kushika silaha
   • Mwili kuwa na nguvu za majagina mia moja
  3. ritifaa – anazungumza na mahasidi ambao hawapo kana kwamba wapo.
  4. tashbihi:
   • Maadui wamwonapo hutetemeka kama jani
   • Kuwayeyusha kama barafu
  5. sitiari:
   • umekuwa nahodha
   • Akili yako sumaku
  6. usambamba:
   • Likalovya change kidari
   • Likanavya chako kipaji
  7.  taswira:
   • Mama alivyolia na kujilovya machozi na kumlovya mwanawe
   • Alivyopigana na utawala wake au jamii yake. Kijiji kizima kinavyomiminika kwake nyumbani.
 4.        
  1. Waume huoa wake wengi – Anasema, Uke wenza ukamhimiza kuchukua buruji kueneza habari.
  2. vilema walitupwa kichakani – Ilosema kwa moja kauli utokomezwe chakani utupwe.
  3.  Ni wafugaji – Kutupoka mifugo.
 5. Anayeimba ni mama. Anasema nilipokuopoa.
 6. tofauti kati ya mighani na visasili;
  • Mighani husimulia kuhusu mashujaa, ilhali visasili husimulia asili ya vitu.
  • Mighani husimulia historia ya jamii, ilhli visasili husimulia mianzo ya vitu au mambo ulimwenguni.
  • Katika mighani, wahusika ni mijagina, ilhali katika visasili wahusika ni vitu tofauti kama vile miungu, wanyama na binadamu.
  • Mighani hueleza sifa za majagina , ilhali visasili hueleza mianzo ya desturi.

Swali la Dondoo 22

“Nimeonja shubiri ya kuwa mtegemezi kihali na mali: lakini katika hayo yote, nimejifunza mengi.

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al. 4)
 2. Jadili nafasi ya vijana katika kuiendeleza na kuiumba jamii kwa mujibu wa riwaya Chozi la Heri. (al. 16)

Majibu ya Dondoo 22

 1.                        
  1. Haya ni maneno ya ridhaa
  2. Anamwamia Mwangeka
  3. Wamo katika ganjo la nyumba iliyochomwa
  4. Anamweleza dhiki ambazo amepitia tangu ghasia za baada ya kutawazwa kiongozi mpya.
   4 x 1 =4
 2. Mchango wa vijana katika ujenzi wa jamii mpya.
  Kujenga jamii mpya ni kurekeisha maovu yaliyokuwa yakitendeka katika jamii kwa kutenda mema/ kuyanyoosha yaliyoenda kombo. Baadhi ya hoja ni:
  1. Tila anataka jamii ambayo wananchi wanapata haki mahakamani. Anataka kusoma na kuwa jaji wa mahakama ya juu ili atatue kesi ambazo hazijasikizwa kwa miongo kadhaa, hivyo kuwapa mahabusu ambao wamekaa kwenye rumande muda mrefu haki yao – uk 45
  2. Tila anawahimiza wanajamii kumchagua kiongozi wa jinsia yoyote, awe mwanamke au mwanamume almradi alete maendeleo katika taifa. Hivi ndivyo anavyowaambia baba yake Ridhaa – uk 40
  3. Lucia – Kiriri anawatahadharisha wanajamii dhidi ya ukabila kwa kukubali kuolowa katika ukoo wa Waombwe amabo una uadui na ukoo wake wa Anyamvua – uk 66 – 67
  4. Umu anafunza umuhimu wa kuwasaidia wasiojiweza/maskini katika jamii. Anampa ombaombamjini karaha shilingi mia mbili licha ya mamake mzazi kukataa kuwasaidia. Apondi na Mwangeka pia wanahimiza jamii kuwasaidia wasiojiweza katika jamii. Wanawasaidia maskini waliomiminika kiamboni mwao kutoka sehemu mbalimbali za eneogatuzi lao. – uk 86
  5. Umu anawafunza vijana umuhimu wa kutumia pesa vizuri/ kutofuja pesa. Anatumia pesa alizodunduiza kutokana na masrufu aliyokuwa akipewa babake kumsaidia ombaomba mmoja mjini karaha – uk 86
  6. Rachael Apondi anaonya askari dhidi ya kutatua mizozo kwa makeke na bunduki. Anawaambia kwamba hilo ni jambo ambalo limepitwa na wakati – uk – 113
  7. Dick anawaonya vijana dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya kwa kuiacha biashara hiyo haramu na kufungua biashara halali ya kuuza vifaa vya simu/umeme – uk 123 – 124
  8. Daktari anahimiza jamii kuthamini haki za watoto kwa kukataa kumsaidia Pete kuavya mimba baada ya kumeza tembe – uk 151
  9. Dick pia anaifunza jamii umuhimu wa kuthamini elimu. Licha ya kukatiziwa masomo na Buda, anapojinasua kutoka mikononi mwake anarudi shuleni na kujiendeleza kimasomo – uk 124
  10. Kipanga anahimiza msamaha na maridhiano katika jamii. Licha ya kuwachukia na kuwatoroka wazazi wake baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana, anawasamehe wote hatimaye baada ya kunusurika kifo cha kangara. – uk 143
  11. Kipanga anaionya jamii dhidi ya unywaji wa pombe haramu kwa kubadilika na kuacha kuinywa baada ya kuwaua watu sabini. – uk 143
  12. Neema anahimiza jamii kuthamini haki za watoto kwa kumwokota motto aliyetupwa kwenye biwi la taka na kumpeleka kwenye kituo cha mayatima cha Benefactor – uk 161
  13. Dick anataka jamii ambayo vijana wanajitengemea kimaisha. Anafungua duka lka kuuza vifaa vya simu na kuwaajiri vijana wengine ili wapate riziki ya kujikimu. Uk 124/174
  14. Dick anahimiza wanajamii kusameheana- licha ya mama yao Naomi kuwatoroka walipohitaji malezi yake, anawahimiza nduguze Umu na Mwaliko kumsamehe akidai kwamba hakuna binadamau hata mmoja aliyekamilika. Uk 193
  15. Hazina anaionya jamii dhidi ya tabia ya utegemezi/kuombaomba – amekuwa akiombaomba jijini karaha lakini anakubali kuelimishwa na serikali na kusomea upishi na huduma za hotelini, hivyo kumwezesha kujikimu kimaisha baada ya kuajiriwa katika hoteli mojawapo jijini – uk 85/88
  16. Chandachema anaifunza jamii umuhimu wa bidii – licha ya kuwa motto mdogo, alijikakamua na kuchuma majanichai kwenye shirika la Tengenea asubuhi kabla ya kuenda shuleni na jioni baada ya kutoka shuleni ili kupata hela za kununua madaftari na sare za shule – uk 106
  17. Neema anaionyesha jamii umuhimu wa kuwatunza mayatima – anamchukua mpwawe Cynthia na kumlea baada ya wazazi wake wote kufariki dunia – uk 169
  18. Mwangeka na Mandu wanaonyesha jamii umuhimu wa kudumisha amani kwa kuenda katika mataifa ya nje kudumisha amani. Mwangeka alikuwa katika taifa la Mashariki ya kati – uk 5/115
  19. Mwangeka na Apondi wanaifunza jamii umuhimu wa kupanga uzazi – wanapanga kuwa na watoto wawili ili kuepuka kero la vinywa vingi vya kulisha. Uk 116
  20. Watu walikuwa na imani potofu kuwa uanajeshi ulitengewa tu watu wa viwango vya chini vya elimu lakini mwangeka anabadilisha imani hii kwa kujiunga na uanajeshi licha ya kuwa na shahada ya uhadisi kutoka chuo kikuu.

Swali la Dondoo 23

‘Nakumbuka asubuhi ya pili baada ya mtafaruku kuanza. Nilikuwa sebuleni na mwanangu tukitazama runinga.’’

 1. Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
 2. Eleza nafasi ya msemaji katika kuwakuza wahusika wengine riwayani. (alama 5)
 3. Tambua mbinu kuu ya kimtindo iliyotumika katika dondoo hili. (alama 1)
 4. Eleza jinsi mbinu uiliyotaja hapo juu (c) ilivyotumika kukuza maudhui riwayani.(alama 10)

Majibu ya Dondoo 23

“Nakumbuka asubuhi ya pili baada ya mtafaruku kuanza. Nilikuwa sebuleni na wanangu tukitazama runinga. (uk.20)

 1.      
  1. Msemaji ni Kaizari
  2. Msemewa ni Ridhaa
  3. Walikuwa katika kambi la wakimbizi.
  4. Kaizari alimsimulia Ridhaa kadhia zilizotokea baada ya uchaguzi (4 x 1= 4)
 2. Msemaji ni Kaizari
  1. Ametumika kuonyesha jinsi ukimbizi ulivyovunja hadhi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha. Anaonekana aking’ang’ania chakula na wakimbizi wengine.
  2. Anawasilisha matatizo yanayowakumba Lime na Mwanaheri kambini. Wao wanapigwa na matone ya mvua kwa kukosa makazi.
  3. Anaonyesha mabadiliko ya kiwajihi yaliyomkumba Subira baada ya kuvamiwa. uk. 16
  4. Ametumiwa kubainisha malalamishi ya Tetci kuhusu ubaguzi unaoendelezwa dhidi ya wanaume.
  5. Ametumiwa kubainisha bidii za Mwekevu. Mwekevu alijitosa kwenye uga wa siasa na kuomba kura kama walivyofanya wanaume.
  6. Ametumiwa kuonyesha ukatili wa kijana aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitman’. Analirushia bomu la petrol gari lililokuwa likipinduka kana kwamba alikuwa akinyunyizia viwavi dawa.
  7. Anaonesha utu wa mhusika Tulia. Tulia alienda kwa nyumba ya Kaizari ili kuwaokoa wakati wa uvamizi.
  8. Ametumia kuonyesha umaskini uliomkumba Makiwa na wenzake katika Mtaa wa Sombera.
  9. Ametumiwa kusawiri tabia ya ufisadi ya Bwana Kute. Bwana Kute anatumia ujanja ili kupata mafungu zaidi ya vyakula vya msaada . zozote 5 x 1 =5
 3.      
  1. Tambua mtindo uliotumika katika dondoo hili. (alama1)
   Mbinu rejeshi: Msimulizi anasimulia matukio yaliyotukia awali. (1×1=1)
  2. Eleza jinsi mbinu uliyotaja katika (c) (i) ilivyotumika kukuza maudhui riwayani. (alamal0)
 4. Kupitia mbinu rejeshi maudhui yafuatayo yanakuzwa:
  1. Ushirikina — Ridhaa anakumbuka matukio kama vile: kupepesa kwa jicho lake Ia kulia kwa muda wa wiki mbili mtawalia, kuanguka kwake bila kuona kilichomkwaa na jeshi la kunguru lililotua katika paa la maktaba yake. Aidha, anakumbuka milio ya kereng’ende na bundi usiku. Matukio hayo yote ni ishara ya mambo mabaya ambayo yangetokea.
  2. Ubabedume — Ridhaa anakumbuka maneno ya marehemu mama yake kuwa unyonge haukutunukiwa majimbi bali makoo (Uk. 3).
  3. Usaliti — Kedi, ambaye alikuwa jirani ya Ridhaa, anamsaliti Ridhaa kwa kuteketeza jumba lake pamoja na jamaa zake.
  4. Uharibifu wa mali — jumba la Ridhaa linateketezwa. Aidha, mahindi katika shamba la Ridhaa yanateketezwa.
  5. Mauaji/ukatili — Terry, Lily Nyamvula, Annatila na Becky wanauawa baada ya nyumba yao kuchomwa moto.
  6. Vita — Mwangeka alikuwa ameenda kudumisha amani katika Mashariki ya Kati.
  7. Ukoloni mamboleo — Hata baada ya uhuru, mmiliki wa mashamba ya Theluji Nyeusi ni mlowezi maarufu. Aidha, Myunani anayamiliki maekari na maekari ya mashamba katika eneo la Kisiwa Bora ambapo wenyeji wamegeuzwa kuwa maskwota.
  8. Utegemezi — Kwa mujibu wa Tila, wenyeji hawana mashamba wanategemea wageni kwa vyakula na ajira.
  9. Udhalimu — sheria za kikoloni zilimpa Mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi. Hali hii iliwalazimu Waafrika kama Msubili kuwa maskwota au vibarua katika mashamba ya wakoloni.
  10. Utumwa — vijulanga vilinyakuliwa kutoka kwenye susu zao, hata vifua havijapanuka; na kupelekwa katika maeneo mbalimbali kufanya kazi.
  11. Upangaji uzazi — Mwimo Msubili alikuwa na watoto wa kiume ishirini. Hivyo, ardhi iligawanywa hadi haingewatosha tena. Aidha, Msubili anakabiliwa na changamoto ya kuwalisha wanawe wengi.
  12. Mgogoro katika familia — Wingi wa vinywa vya kulishwa katika familia ya Msubili ulizua mgogoro, uhasama na uhitaji mkubwa.
  13. Ubaguzi — Ridhaa anatengwa na wanafunzi wenzake kwa kuwa walimwona kama Mfuata Mvua.Hawakumchukulia kuwa, alikuwa mmoja wao.
  14. Elimu — Mamake Ridhaa anatilia mkazo umuhimu wa elimu. Anadai kuwa, elimu inapaswa kuwa chombo cha kueneza amani na upendo.
  15. Uhasama wa kisiasa unasababisha kuvunjika kwa ujirani — Kedi ndiye aliyemtafutia Ridhaa shamba alilolijenga. Aidha, Ridhaa alidhamini masomo ya wapwa wake wawili. Hata hivyo, Kedi anashiriki katika mauaji ya jamaa za Ridhaa.
  16. Vitisho — vikaratasi vilisambazwa kuwatahadharisha akina Ridhaa kuwa, kuna gharika baada ya kutawazwa kwa Musumbi (kiongozi) mpya.
  17. Unyakuzi wa ardhi — baadhi ya mabwanyenye wanajenga majumba mahali ambapo pametengwa kwa ajili ya upanuzi wa barabara. Mengine yalijengwa chini ya vigingi vya nyaya za stima.
  18. Ufisadi — kuna mabwanyenye ambao wanaonekana wakitoa milungula hadharani.
  19. Ndoa- kwamba si wanawake pekee watesekao katika ndoa. Kuna wanaume ambao wanateseka kutokana na mapigo na dhuluma za kisaikolojia kutoka kwa wake zao (uk.17).
  20. Mabadiliko — wimbi la mabadiliko liliwakumba Wahifidhina kisiasa ambapo mwanamke anachaguliwa kama kiongozi kinyume na ilivyokuwa hapo awali.
  21. Umuhimu wa vyombo vya dola — vyombo vya dola vilitumwa ili kudumisha usalama katika vijiji na mitaa.
  22. Wizi — wengine waliingia katika maduka ya Kihindi, Kiarabu na hata ya Kiafrika na kupora walichoweza kubeba.

Swali la Dondoo 24

‘‘Mama mtu alikuwa ameamua kwamba hapa hapamweki tena. Alikuwa amehudumu katika afisi za umma kama mhazili mwandamizi kwa miaka mingi mpaka kazi hii akaiona inamfanya kusinya, hana hamu tena.’’

 1. Eleza umuhimu wa mrejelewa katika kukuza riwaya ya Chozi la Heri. (alama 4)
 2. Huku ukitoa mifano jadili changamoto zinazokumba asasi ya ndoa kwa mujibu wa riwaya ya Chozi la Heri. (alama 8)
 3. Jadili umuhimu wa mandhari katika kuijenga riwaya ya Chozi la Heri kwa kurejelea:
  1. Shule ya Tangamano. (alama 4)
  2. Hoteli ya Majaliwa. (alama 4)

Majibu ya Dondoo 24

 1. Umuhimu wa mrejelewa; (Annete-mkewe kiriri) (lazima amtaje)
  1. Kielelezo cha malezi mabaya-aliwanyima watoto wake ushirika na babake
  2. Anaonyesha ubinafsi-anahamia ughaibuni na kumwacha mumewe anayeaga dunia kutokana na kihoro
  3. Anaonyesha usaliti anapomwacha mumewe,
  4. Kuonyesha mgogoro katika ndoa
  5. Anyaonyesha ukengeushi anapovutiwa na inchi ya ughaibuni na kuiona bora kuliko nchi yao
  6. Anaonyesha uhusiano uliopo baina ya wazazi na wanao
  7. Anaonyesha madhara ya kuvunjika kwa ndoa
  8. Anachimuza sifa/tabia za Kiriri
   (Zozote 4 x 1 = 4)
 2. Changamoto zinazokumba asasi ya ndoa
  1. Vifo - Terry, Lilly
  2. Ukosefu wa watoto — Mwangemi na Neema
  3. Ukabila/ ukoo — Lucia, Subira, Selume
  4. Wazazi kukataa wanao kuolewa — Rehema
  5. Ukosefu wa uaminifu — Bw. Tenge
  6. Chuki Pete kuonewa na wake wenza
  7. Vita katika ndoa — mamake Sauna anadhulumiwa na Maya
  8. Migogoro katika ndoa — babake Pete anamkataa Pombe! ulevi — babake mzazi Sauna - Umaskini - Naomi kumwacha Lunga
  9. Upweke — Lunga
  10. Uhasama katika ndoa — Mzee Mwimo
  11. Wazee kuoa wasichana wadogo — mzee Fungo anamuoa Pete
  12. Tofauti za kisiasa — Selume na mumewe
  13. Malezi ya watoto — Annete anaenda ughaibuni na watoto
  14. Ndoa za kujaribisha — Nyangumi na Pete
  15. Kudanganywa — Pete anadanganywa na mwanamme
  16. Wanandoa kutoacha nasaba zao baada ya kuolewa — Naomi Maonevu/ kutengwa -Subira
  17. Usaliti — Billy na Sally (zozote 8×1=8)
 3. umuhimu wa mandhari
  1. shule ya Tangamano
   • Kuonyesha masaibu yanayoikumba familia ya ummu
   • Matatizo wanayokumbana nayo wakimbizi — Kairu
   • Kuonyesha umaskini — familia ya Kairu
   • Ubaguzi wa kiukoo — mamake mwanaheri
   • Matatizo ya vijana wa kike katika umri mdogo — Zohali , Rehema
   • Jukumu la familia kusambaratisha watoto — Chandachema
   • Uwajibikaji wa vijana — Chandachema
   • Nafasi ya dini
   • Ukosefu wa uaminifu katika ndoa uasherati — Bw.Tenge
   • Ukatili wa Bw. Tenge (zozote 4×1=4)
  2. Hoteli ya majaliwa
   • Kukutanisha watoto wa Lunga.
   • Kuonyesha malezi mema — mwangeka na mwangemi
   • Uhafidhina wa babu
   • Taasubi ya kiume ya babu
   • Msamaha — Naomi / watoto wake

Swali la Dondoo 25

“ Umu hawa ni marafiki wangu wa chanda na pete. Ni watu wakarimu na wenye imani’

 1. Eleza muktadha wa dondo hili. (alama 3)
 2. Taja mbinu ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 1)
 3. Fafanua umuhimu wa Umu. (alama 6)
 4. Huku ukirejelea riwaya nzima chambua maudhui ya ukarimu. (alama 10)

Majibu ya Dondoo 25

 1. mnenaji :mawazo ya Umu ya maneno ya mwalimu Dhahabu
  Mahali: shuleni Tangamano
  Sababu: Mwangeka na Apondi walikuwa wamekuja kumpanga Umu. (Alama 1X3)
 2. msemo- chanda na pete
 3. Umuhimu wa Umu
  1. Ni kielelezo cha vijana wasiokufa moyo maishani hata wanapokumbwa na shida tele
  2. Anaendeleza maudhui ya uwajibikaji anapowalea wadogo wake sophie na Ridhaa wazazi wake wanaposafiri
  3. Ananendelelza maudhui yautu anapompa ndugu yake chakula chake
  4. Anajenga sifa za Mwangeka na apondi kama wakarimu
  5. Anajenga sifa za sophie kama mwenye hasira anapokuwa dawa yake ya hasira zake za kivolkani
 4. Ni tendo la kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali bila masharti
  • Ridhaa anatumia uwezo wake kuwavutia wanakijiji maji ya mabomba ili yawapunguizie makali ya ukosefu wa maji uk 11
  • Shirika la makazi bora linajitolea kuwajengea wakimbizi wa msitu wa mamba makazi ma kuwapa vyakula na maji uk 11
  • Ridhaa aliwasaidia watu mbalimbali kutokana na matatizo mengi waliyokuwa wakiyashuhudia uk 35
  • Mashirika yasiyo ya kiserikali yanawatuma wawakilishi wao ili kuwapa ushauri na nasaha waathiriwa wa makabiliano yaliyowaishia kulowea msitumi uk 36
  • Julida anamkaribisha umu kwa furaha na kumhakikishia kwamba atakuwa salama hadi wakati atakapokabidhiwa kwa idara ya watoto uk 189
  • Marafiki wapya wa umu shuleni wanamhimiza kwa ukarimu avumilie maisha ya shule mpya, kwani siku moja atayazoea uk 91
  • Mtawa pacha anawonyesha zohali ukarimu kwa kumuokoa kutoka njia ya uharibifu uk 99
  • Mwalimu mkuu Bi Tamasha wa shule ya msingi wa kilimo anasikiliza kwa makini na ukarimu mkuu masaibu ya chandachema na hatimaye kumsaidia uk 105
  • Chandachema anaokolewa na shirika la hakikisho la haki na utulivu uk 107
  • Mwangeka na apondi wanakuwa wakarimu kwa watu wenye mahitaji mbalimbali uk 116
  • Apondi na mwangeka wanakubali kumchukua umu kama mtoto wao wakiwa radhi kumtunza uk 117
  • Neema na mwangemi wanakuwa wakarimu wanapokubali kumchukua mwaliko kama mtoto wao wa kupanga.

Swali la Dondoo 26

“Alikuwa wapi siku kiduka changu ambacho mimi na aila yangu tumekitegemea kwa miaka kumi kilipoporwa na kugeuzwa majivu?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Tathmini umuhimu nne wa msemaji katika kuijenga riwaya hii. (alama 4)
 3. Jadili umuhimu wa mandhari katika kujenga riwaya ya Chozi la Heri kwa kurejelea Msitu wa Mamba. (alama 12)

Majibu ya Dondoo 26

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.    (alama 4)
  • Msemaji ni Kaumu, Msemewa ni Askari, Mandhari ni Msitu wa Mamba. Hii ni baada ya askari huyo kuwasihi wakimbizi kuwa watulivu wanapogawiwa chakula na makanisa na masikiti.
 2. Tathmini umuhimu nne wa msemaji katika kuijenga riwaya hii.    (alama 4)
  • Maudhui ya uwajibikaji:Askari kutoajibika wakati kiduka chake kiliporwa.
  • Uporaji wa mali ya umma,Kiduka chake kiliporwa na kugeuzwa majivu.
  • Mapuuza,Askari kuwatazama kama wehu walipokuwa wakililia usaidizi.
  • Ukimbizi;mzee Kaumu ni mmoja wa wakimbizi
  • Utegemezi/umaskini;wanategemea chakula cha msaada unaotolewa.
  • Umuhimu wa Amani nchini;sasa hivi ndio anaona thamani ya utulivu nchini.
  • Mabadiliko
  • Kupitia kwake, athari za vita miongoni mwa Wahafidhina inabainika.
  • Anatumiwa kujenga sifa za Wahafidhina kama Mhusika aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitman’ za uhuni.
  • Ametumiwa kuonyesha nafasi za asasi za utawala katika kutekeleza majukumu yao.
 3. Jadili umuhimu wa mandhari katika kujenga riwaya ya Chozi la Heri kwa kurejelea Msitu wa Mamba.  (alama 12)
  • Kuonyesha dhiki za kisaikolojia inayopata wakimbizi.mfano Kaizari na aila yake.
  • Kuonyesha suala la ubakaji. Mfano Mwanaheri na Lime
  • Kuonyesha shida ya njaa na kupigania chakula. Kuna milolongo mirefu ya chakula.Ridhaa anatafuna mzizi mwitu
  • Kuonyesha mabadiliko,Mwekevu kupewa nafasi ya kuongoza.
  • Kuonyesha suala la ukimbizi;Misafara ya wahafidhina waliohama bila kujua waendako.
  • Kuonyesha vita baada ya uchaguzi;mizoga ya watu,magofu ya majumba nk.
  • Kuonyesha suala la ulawiti wa wanaume na hakuna anayewatetea.
  • Kuonyesha uporaji wa mali ya umma.mfano magari kuchomwa,maduka ya wahindi kuporwa.
  • Kuonyesha unafiki;katika upigaji kura kwa wasiojua kusoma.
  • kuopnyesha ahadi hewa walizopea vijana
  • kuonyesha utabaka,msitu wa mamba ulikuwa na usawa wa watu.Daktari Ridhaa,Kaizari,Selume
  • Kuonyesha usaliti na ubinafsi wa viongozi;viongozi wenyewe baada ya kupiga kura walikalia majumbani mwao.
  • Kuonyesha tanzia.mamia za roho zisizo na hatia zilisalimu amri chini ya pambaja za risasi.
  • Kuonyesha suala la ufisadi;viongozi mfano kugawia kila mtu shilingi mia mia.
  • Kuonyesha ukoloni mamboleo;
  • Kuonyesha athari ya ukabila.Tulia kuwasihi Kaizari watoke kama bado wanataka kuishi.
  • Kuonyesha mchango wa mashirika mbalimbali. 

Swali la Dondoo 27

“…poa sana sistee,wewe ni mnoma.siku moja nitakuhelp hata mimi…”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Eleza sifa mbili za mnenaji zinazojitokeza kwenye kauli hii. (alama 4)
 3. Taja na ufafanue maudhui yoyote mawili yanayotokana na matini haya. (alama 4)
 4. Je, ahadi aliyoitoa mnenaji ilikuja kutimia? Eleza kwa kina. (alama 8)

Majibu ya Dondoo 27

 1.    
  1. Maneno ya Hazina.
  2. Akimwambia umulkheri.
  3. Walikuwa barabarani wakati Hazina alikuwa ombaomba.
  4. Anamshukuru Umulkheri kwa sababu amemfaa kwa uhitaji wake anapompa shilingi mia mbili.
   (1x4)
 2. Mnenaji ni Hazina.
  1. Mwenye shukrani-alimshukuru Umulheri kwa kumuauni wakati huo kwa vile sio wengi hufanya hivyo.
  2. Mwenye matumaini-anatumaini kuwa hali yake ingeimarika.Anatumaini kuwa siku moja angekutana naye na pia akapata fursa ya kumsaidia.
   (2x2)=4
 3.  
  1. Umaskini-Hazina ni ombaomba aliye barabarani kwa sababu ya ulitima uliomzingira.
  2. Ukarimu-Umulkheri alimsaidia Hazina ambaye anaahidi kumsaidia siku moja pia.
   (2x2 = 4)
 4.  
  1. Hali yake Hazina inaimarika wakati anapochukuliwa na serikali na kupelekwa shuleni.Amejifunza upishi na anafanya kazi kwenye hoteli.
  2. Umulheri anapofika mjini anakutana na Haina ambaye anamfaa,anampa chakula
  3. Hazina anamwongoza Umulkheri na kumpeleka kwenye makao na kumjulisha kwa Bi.Julida msimamizi wa makao hayo.
  4. Kupitia juhudi za Julida Umulkheri alijiunga na shule ya upili ya Tangamano na kuendelea na masomo yake tena.

Swali la Dondoo 28

“Nitapigana kwa jino na ukucha kuulinda utu wangu.”
 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
 2. Eleza umuhimu wa msemaji wa dondoo hili. 
 3. Kwa kutolea mifano riwayani, thibitisha namna binadamu alivyopungukiwa na utu. (alama 12)

Majibu ya Dondoo 28

“Nitapigana kwa jino na ukucha kuulinda utu wangu.”
 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
  • Msemaji ni Umulkheri
  • Anajizungumzia
  • Akiwa nyumbai kwao
  • Ni baada ya kijakazi Sauna kwaiba ndugu zake, naye kwa kuchelea kutendewa kitendo kama hicho anaamua kuchukua hatua  ya kutetea nafsi yake kwa kutoroka nyumabni kwao. 
 2.  Eleza umuhimu wa msemaji wa dondoo hili.
  Msemaji ni Umulkheri
  Anawakilisha:
  • Vijana jasiri katika jamii – anapiga ripoti kwa polisi kuhusu kupotea kwa ndugu zake.
  • Vijana wenye bidii na kujitolea – anasoma hadi kufuzu na kuwa injinia
  • Vijana wanaowajibikia majukumu wanayotwikwa – anapania kuwatunza ndugu zake baada ya kifo cha baba yao na kutoweka kwa mama mzazi.
  • Kuthibitisha methali kuwa, “Hakuna refu lisilokuwa na ncha”Umulkheri anateseka maishani lakini mwishowe anakuja kufaulu baada ya kusoma na kufuzu kuwa injinia.
  • Ametumiwa kuonyesha wazi uhayawani wa Sauna – kuwaiba ndugu zake.
 3. Kwa kutolea mifano riwayani, thibitisha namna binadamu alivyopungukiwa na utu. (alama 12)
  • Ukatili – Majirani wanachoma nyumba ya Ridhaa na kusababisha kuangamia kwa aila yake katika mkasa wa moto.
  • Wivu – wanafunzi wanamwonea gere anapowapiku masomoni kwa kumwita mfuata mvua na mwizi wa kalamu zao.
  • Tamaa – Lunga analima maekari wa mashamba bila kujali uharibifu wa mazingira.
  • Chuki – Subira anachukiwa na wakwe zake kwa kuwa Kaizari alioa kutoka ukoo mwingine.
  • Mapendeleo – Mzee Msubili anawachukua wake wawili na kuwahamishia Msitu wa Heri.
  • Mapuuza – Mabwenyenye wanapuuza notisi waliopewa ya kubomoa mijengo yao.
  • Ufisadi – mabwenyenye wengine walionekana wakito milungula hadharani.
  • Uporaji – raia kuingia kwa maduka ya wafanyabiashara na kupora walichoweza kubeba.
  • Uchoyo – Naomi anakataa kuwasaidia watoto ombaomba. Anaposisitiziwa na Umu kuwasaidia anamtupia Umu shilingi ishirini.
  • Usaliti – Billy anasalitiwa na Sally hata baada ya kujenga jumba la kifahari kwa kukaa usuhuba wake.
  • Usingiziaji – Lunga anafutwa kazi kwa kisingizio kuwa shirika limeamua kupunguza idadi ya wafanyakazi katika ngazi ya juu.
  • Unafiki – watu kukosa kuwasaidia watoto ombaomba waliokuwa karibu na kanisa huku wakienda kanisani kunakohubiriwa usawa na usaidizi kwa wengine.  (zozote 12 x 1 = 12)

Swali la Dondoo 29

“Haiwezekani! Hili haliwekazi! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                          (alama 4)
 2. Eleza kwa kifupi yaliyowapata wahafidhina baada ya usemi huu. (alama.4)
 3. Riwaya ya chozi la heri inaonyesha maovu yanayotamalaki katika jamii.Thibitisha. (alama 12)

Majibu ya Dondoo 29

Haiwezekani! Hili haliwekazi! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                          (alama 4)
  • Maneno ya Tetei, Mwanaharakati
  • Anawaambia wananchi/wapiga kula.
  • Baada ya mwekevu kutawazwa/ Kiogozi mwanamuke
  • Watu walishukuwa silaha kupigania uhuru wao.
 2. Eleza kwa kifupi yaliyowapata wahafidhina baada ya usemi huu. (alama.4)
  • Watu walishukuwa silaha kupigania uhuru wao.
  • Mlio ya buduki ilisikika.
  • Vilio vilijaa hewani.
  • Vyombo vya dola vilitumwa kudumisha amani.
  • Msafara ya watu ilionekana ikimaha kwao.
  • Mazao yalichomwa mashambani
  • Majumba yalichomwa
  • Watu waliuliwa.
 3. Riwaya ya chozi la heri inaonyesha maovu yanayotamalaki katika jamii.Thibitisha. (alama 12)
  • Nyumba ya Ridhaa inateketezwa
  • Luga anafutwa kazi bila sababu.
  • Mwanaheri kunajisiwa
  • Fumba kuringa mwanafunzi wake mamba
  • Familia ya ridha kuteketezwa majirani.
  • Pete kuozwa
  • Subira kubaguliwa Kwa sababu za kiukoo.
  • Naomi kuwatelekeza wanawe.
  • Uharibifu wa mazingira – serikali inakata miji.
  • Chandachema chema anadhumiwa kimapenzi na mwalimu wake fumba.
  • Shamba lao shamusi linanyakuliwa.
  • Pete anakeketwa.
  • Ndoa za mapema/pete
  • Uuzaji wa pombe haramu
  • Ulaguzi wa madawa ya kulevya
  • Ulaguzi wa watoto.
   TANBIHI Kadiliria jawabu la mwanafunzi zozote kumi na mbili. (12x1)

Swali la Dondoo 30

“…haifai kucheza na uwezo wa vijana, waoni kama nanga. Huwezi kuzamisha nakuiongea merikebu.”
 1. Eleza muktadha wa dondoo hili
 2. Bainisha tamathali mbili za usemi zilizo tumika katika dondoo (4x1=4)
 3. Kwa kurejelea riwaya hii, onyesha jinsi vijana wamezamisha merikebu yawa hafidhinai.

Majibu ya Dondoo 30

“…haifai kucheza na uwezo wa vijana, waoni kama nanga. Huwezi kuzamisha nakuiongea merikebu.”
 1. Eleza muktadha wa dondoo hili
  • Ni maneno yake mwangeka 
  • Anamwambia Ridhaa
  • Wamo katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Rubia.
  • Ni baada ya kuyakumbuka maneno ya Tila kuwa haifai kucheza na uwezo wa vijana katika jamii 
 2. Bainisha tamathali mbili za usemi zilizo tumika katika dondoo (4x1=4)
  • Tashibihi – wao ni kama nanga. 
  • Jazanda –merikebu inasimamia taifa la wahafidhina.
  • Taswira – Picha ya merikebu inayozamishwa.
 3. Kwa kurejelea riwaya hii, onyesha jinsi vijana wamezamisha merikebu yawa hafidhinai.
  • Genge la wavulana watano linawabaka lime na mwanaheri kwa kukisia kwamba wazazi wao hawakumpagia kwa mwanzi.
  • Wanazorotesha usalama kwa kumvamia Subira na kumkata kwa sime kwa kumdhania kuwa hakumpigia kura Mwanzi.
  • Vijana wanawavamia abiria barabarani wakiongozwa na kijana aliyekuwa amevaa shati lenye maandishi “Hitman” na kuwachomea ndani ya magari.
  • Wanayachoma magari barabarani.
  • Sauna awaiba watoto wake Lunga-Dick na Mwaliko na kuwatenga na dada yao Umu.
  • Pete anameza vidonge ili kuavya kitoto chake cha pili ila hakufanikiwa.
  • Zohali anajiingiza katika mapenzi na kupata mimba akiwa kidato cha pili.
  • Wanawe Kiriri wanakataa kurundi nyumbani.  Kutoka ughaibuni walikoenda kusoma.
  • Vijana wanamdhalilisha Mwekevu baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi.
  • Kipanga anaachia masomo kidato cha pili na kuanza kunywa kangara –ananusurika kifo.
  • Wanafunzi shukeni –anakomesea Ridhaa, wanaendeleza ukabila dhidi ya wanafunzi walowezi.
  • Vijana wanapokea hongo kutoka kwa wanasiasa kama papa iti wawachague, hivyo kuimarisha uongozi mbaya.
  • Vijana wasichana wanajifungua watoto na kuwatupa kwenye majaa ya taka kama Yule aliyeokolewa na Neema.
  • Wanavunja sheria kwa kuandamana huku wamebeba picha za Mwanzi na kumhimiza atawale ingawa alikuwa ameshindwa n.k (6x2=12)

Download Chozi la Heri Dondoo Questions and Answers - Chozi la Heri Maswali na Majibu ya Dondoo.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest