Kujibu Maswali na Majibu ya Insha na Muktadha wa dondo - Mwongozo wa Chozi la Heri

Share via Whatsapp


Aina ya maswali

Apa mna maswali ya aina mbili.

 • Maswali ya insha
 • Maswali ya Muktadha wa dondo.

Maswali ya Insha

Haya ni maswali ambayo hutoa kauli inayohitaji kujibiwa kwa kirefu na kwa kina. Swali linaweza kuwa la jumla yaani linalohusu Riwaya nzima. Pia, swali laweza kulenga sehemu ya kazi husika katika nyanja na maudhui, wahusika na hulka zao, mafunzo na fani. Maswali haya huhitaji zaidi uwezo wa kukumbuka wa mtu, kupanga hoja na kuelezea msimamo au maoni yake kuhusiana nayo. Mtahiniwa anahitajika kutoa hoja na kuziteteta kwa mifano dhabiti. Mtahiniwa asitumie vistari vistari, afafanue hoja kikamilifu akiandamisha mifano mingi kutoka kwa Riwaya

Maswali ya muktadha wa dondoo.

Maswali haya hujitokeza kwa namna ya maneno yaliyodondolewa kutoka kwenye kazi ya Fasihi. Dondoo hunukuliwa kisha maswali yanayohusiana na dondoo hilo huulizwa. Dondoo laweza kuwa maneno ya mhusika mmoja ambaye hatatajwa au maelezo katika kazi. Maswali huenda yakarejelea matukio yaliyotokea kabla au baada ya dondoo. Katika kulijibu swali la muktadha wa dondoo, mtahiniwa huhitajika kuangazia mambo yafuatayo;

 1. Kumtaja msemaji wa maneno haya
 2. Kumtaja msemewa(anayerejelewa)
 3. Kueleza mahali yalikofanyika mazungumzo haya.
 4. Kueleza kiinisababu ya mazungumzo haya kutokea.
 1. " Lakini itakuwaje historical injustice, nawe Ridhaa, hapo ulipo sicho kitovu chako?"
  1. Eleza muktadha wa dondoo
   Hayo ni maneno ya Ridhaa yaliyokuwa yakimpikia baada ya kumjibu Tila mawazoni. Hii ni baada ya Ridhaa kukubali maneno ya Tila ya hapo awali. Inadhihirika kuwa amekubali kuwa yeye ni mgeni, si mwenyeji.
  2. Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye dondoo hili (alama 4)
   Swali balagha- ...hapo ulipo sicho kitovu chako?
   Kuchanganya ndimi- historical injustice.
  3. Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya (alama 6)
   Msemaji wa Maneno haya ni Ridhaa.
   Umuhimu wake. Ridhaa ametumiwa na mwandishi kutuonyesha na ukabila. Ridhaa ni kielelezo cha watu wasiobagua watu wengine hakujali wanakijiji wenzake ni wa ukoo gani bali yeye alitekeleza miradi ya maendeleo ili kuwafaidi wote. Ridhaa ametumiwa kuuonyesha udhalimu wa watavoa kwa hadithia namna majumba yake yalivobomolewa
  4. Ni mambo gani yaliyowokumba wale ambao kitovu ( Alamo 6)
   Jibu walichomewo nyumba zao kwa mfano Ridhaa alichomewa jumba lake la kifahari. Watu wao waliuwawa kwa mfanofamilia ya Ridhaa ilichomwa na Bwana Kedi jirani yao. Walikimbia na kutorokea msituni. Watoto wao walibakwa kwa mfano mabinti zake Kaizari walibakwa na vijana wenzao. Walitoroka kuacha makwao wakawa maskwota au wakimbizi wa ndani kwa ndani.

 2. Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya ya Chozi Heri tetea kauli hii kwa kutolea hoja kumi zisizopinglka ( alama 20)

  Katika jamii hii kuna biashara haramu kama ile ya uuzaji wa dawa za kulevya. Dick alipotekwa nyara alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wa miaka kumi. Kuna ukabila. Suala hili la ukabila ilijitokeza kikamilifu wakati kulizuka vita vya baada ya kutawazwa. Majironi waliwageuko wenzao ambao walikuwa wametoka katika kabila au ukoo tofauti na wao. Kuna mauaji. Watu wengi waliwapoteza wapendwa wao kutokano na migogoro iiyozuka baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya. Katika jamii hii kuna matumizi ya pombe haramu vijana wa vyuo vikuu wanabugia pombe hii ya sumu inayowafanya wengine kuiaga dunia. Kuna ukeketaji wa watoto wa kike. Wasichana wa Shule ya msingi wanapashwa tohara. Wasichana wengine wanayapoteza maisha yao huku wengine wakiponea chupuchupu na kuwwa hospitalini kwa mfano Tuama anayeitetea mila hii iiyopitwa na wakati aliponea kidogo kuiaga dunia. Ndoa za mapema. Wasichana wachanga wanalazimishwa wolewe na vizee na kuacha masomo yao. Kuna wizi uporaji wa mali ya wengine. Wakati vita vya baada ya kutawazwa kuzuka, vatu walionekano kupora maduka ya Kihindi, Kiarabu na hata ya Waafrika wenzao. Katika jamii hii wanawake huavya mimba. Sauna alipachikwa mimba na babake mlezi. Mamake mzazi alimsaidia kuavya kisha akamwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa babake. Kuna baadhi ya wazazi wanaohusiana kimapenzi na watoto wao. Sauna alipachikwa mimba na babake mlezi. Mamake mzazi alimsaidia kuavya kisha akamwonya dhidi ya kumwambja yeyote kuhusu unyama wa babake. Wanawake wengine katika jamii hii wanawaacha waume zao na familia zao na kwenda kuyaishi maisha yao kwingineko. Mamake Umulkheri aliwaacha na kwenda kuishi mjini. Rejelea mhusika Naomi. (Mwanafunzi aongeze hoja nyingine) .

 3. Fafanua namna mwandishi alivyotumia mbinu ya kisengere nyuma katika riwaya (alama 20)

  Mwandishi huyu amefaulu sana kutumia mbinu hii. Kisengere nyuma imetumika katika mazingira yafuatayo. Ridhaa anakumbuka vijikaratasi vikienezwa vikiwatahadharisha kuwa mna gharika baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya. Kisa cha namna Mzee Kedi(jirani yao) alivyomsaidia Ridhaa kupata shamba lake na kuwa ameyadhamini masomo ya wapwaze wawili kimetolewa kwa urejeshi. Mijadala baina ya Ridhaa na Tila imetolewa kwa njia ya urejeshi. Kisa cha yule mwana wa mlowezi maarufu aliyemiliki mashamba ya Theluji Nyeusi katika Eneo la Kisiwa bora kimetolewa kwa urejeshi. Kisa cha yule kiongozi wa Kiimla wa kike aliyekuwa akisimuliwa katika visakale cha majirani zao no narnna aivyowatumikisha wanaume kimetolewa kwa urejeshi. Kaizari anasimuia yaliyojiri baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya aliyekuwa mwanamke kwa njia ya kurejelea. Moyo wa Kaizari uipoanza kumsuta, alikumbuka kisa cha wafuasi wa Musa ambao baada ya kukosa chakula jangwani walimshtumu kwa kuwatoa kule Misri. Ridhaa anapokuwa ameketi kwenye chumba cha mapokezi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Rubia, alikumbuka namna walivyorudi nyumbani baada ya kuishi katika Msitu wa Mamba kwa miezi sita. Anakumbuka pia alivyokuwa akihisi. Ridhaa anamkumbuka Tila bintiye aivyokuwa anapenda masuala yanayohusiana na sheria, haki na siasa. Mwangeka alipolitazama tabasamu la babake, alihisi kuwa sasa amezingirwa na uzio imara. Akawa anakumbuka wimbo ambao mamake alizoea kumwimbia kila mara babake alipokuwa ameenda katika safari za kikazi. Kisa cha namna Ami zake Kangata walivyokuwa wamekataa mwana wao aolewe na mtu wa ukoo mwingine kimetolewa kwa urejeshi. Kisa namna Lunga aivyostaafishwa kwa kuwa na msimamo imara kuhusiaria na sakata ya mahindi kimetolewa kwa urejeshi. (mwanafunzi azidishie hoja hizi) zozote 10x2=20  

 4. Fafanua ufaafu wa anwani Chozi la Heri (alama 20)

  Mwandishi anatueeza kuwa Ridhaa alipokwendo shuleni siku iyo kwanza alitengwa na wenzake kwani hawakutaka ashiriki michezo yao. Kijana mmoja mchokozi alimwito 'mfuata mvua' aliyekuja kuwashinda katika mitihani yote. Ridhaa alifululiza nyumbani na kujitupa mchangani na kulia kwa kite na shake. Mamake alimliwaza na kumhakikishia kumwona mwalimu keshoye. Tangu siku hii, huu ukawa ndio mwanzo wa maisha ya heri kwa Ridhaa kwani baada ya mwalimu Kuzungumza na wanafunzi umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano, Ridhaa alipea kwenye anga ya elimu hadi kufikia kilelecha cha elimu na kuhitimu kama daktari. Ridhaa alipotoka kwenye Msitu wa Mamba alijiona nafuu kwani wapwa zake- Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu. Dadake Subira alitibiwa akapona. Mwamu wake Kaizari amepona donda lililosababishwa na kuwatazama mabinti zake wakitendewa ukaini(kubakwa) na vijana wenzao. Ridhaa anajua kuwa Kaizari ni afadhali kwa sababu hakuna aliyemtenga na mmoja kati ya jamaa zake. Ridhaa anapomfikiria Kaizari anajiambia heri nusu shari kuliko shari kamili. Ridhaa aliposikia sauti ya kike ikitangaza, tangazo lile lilimrudisha katika mandhari yake ya sasa. Aijaribu kuangaza macho yake aone anakoenda lakini macho yaijao uzito wa machozi ambayo alikuwa ameyaacha yamchome na kutiririka yatakavyo. Wakati Ridhaa alimkazia macho Mwangeka-waka Mwangeka alikuwa akijiuliza iwapo babake amekuwa mwehu kwa kukosa kushirikiana na majirani kuchimba kaburi kuyazika majivu, matone mazito ya machozi yalitunga machoni mwake Mwangeka. Akayaacha yamdondoke na kumcharaza yatakavyo. Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa machozi haya uliulainisha moyo wake, ukampa amani kidogo. Moyo wake ukajaa utulivu sasa kwa kujua kuwa wino wa Mungu haufutiki. Wakatl Ridhaa_ alikuwa- akusimulia Mwangeka msiba iliyomwandama tangu siku alipoondoka kwenda kuweka amani Mashariki ya Kati Ridhaa alisita akajipagusa kijasho kilichokuwa kimetunga kipajini mwake kisha akatoa kitambaa mfukoni na kuyafuta machozi yaliyokuwa yameanza kumpofusha. Uk 48 Mwangeka alipokuwa ameketi mkabala na kidimbwi cha kuogelea mawazo yoke yalikuwa kule mbali alikoanzia. Akawa anakumbuka changamoto za ukauji wake. Akawakumbuka wanuna wake. Alipomkumbuka Annatila(Tila) mwili ulimzizima kidogo akatabasamu kisha tone moto la chozi likamdondoka. Katika Msitu wa Simba kulikuwa na maelfu watu waliogura makwao. Kati ya familia zilizoguria humu ni familia ya Bwana Kangata. Kwa Kangata na mkewe Ndarine, hapa palikuwa afadhall kwani hawakuwa na pa kwenda kwa kuwa hata kule walikokuwa wakiishi awali hakukuwa kwao. Uk 57 Wakati Dick walikutana kisadfa na Umu katika uwanja wa ndege, walikumbatiana kwa furaha. Machozi yaliwadondoka wote wawili na wakawa wanalia kimyakimya. Walijua fika kuwa jaala ilikuwa imewakutanisha na kwamba hawatawahi kutengana tena. Maisha sasa yalianza kuwa ya heri kwao. Baado ya miaka kumi ya kuuza dawa za kulevya, Dick alifaulu hatimaye kujinasua kutoka kwa kucha za mwajiri wake. Alianza biashara yake mwenyewe ya kuuza vifaa vya umeme. Sasa akaanza kujitegemea kwa kuwa amejiajiri. Alikuwa ameufungua ukurasa mpya katika maisha yake. Maisha yake sasa ni ya heri. Wakati Neema na Mwangemi walikabidhiwa mtoto wao wa kupanga na Mtawa Annastacia, Mwaliko alimkumbatia Neema na kumwita mama na kumwahidi kuwa ataenda naye. Neema alidondokwa na chozi la furaha na kumkumbatia Mwaliko kwa mapenzi ya mama mzazi. Hili lilikuwa ni chozi la heri kwa Neema. (mwanafunzi aongezee hoja) zozote IC)x2=20

 5. Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za kiafrika. Tetea kauli hii ukirejelea chozi la heri (aiama 20)

  Ukabila ni matendo au fikira za mtu za kuthamini kabila lake mwenyewe tu na kuwabagua wa makabila mengine. Ukabila umejitokeza kama ifuatavyo katika Chozi la Heri. Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao. Mwanaheri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya Mamwezi lakini babake alikuwa wa jamiii tofauti. Kila mara Subira aliitwa 'muki' au huyo wa kuja. Kwa miaka mingi aliweza kuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda. Mwishowe alihiari kujiondokea na kwenda mjini alikojinywea kinywaji kikali, akafaia alitengwa katika michezo yao. Kijana mmoja alimwita 'mfuata myua' jambo lililomuumiza sana Ridhaa. Mzee Kedi alimtendea udhalimu Ridhaa na kuiteketeza aila yoke licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini. Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na Kedi. Ami zake Kangata walimsuta mno kwa kumwoza mwanawao kwa mtu wa jamii tofauti na yao. Walishangaa ni vipi mwana wao ataozwa kwa mtu wa ukoo ambao huvaa nguo ndani nje. Waliamini kuwa ukoo huo huzaa majoka ambao hata kiporo cha juzi hayawezi kukupa. Ndoa ya Selume iisambaratika baada ya Vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya. Alibaki mwenye kilio baada ya wambea kumfikishia ujumbe kuwa mume wake amekwisha kuoa msichana wa kikwao. Tulia alimsaidia Kaizari kufunganya na kumsindikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi Mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake. Akamjuvya kuwa uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja.

 6. Auntie Sauna alishikwa na polisi "
  1. Liweke dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
   Maneno haya yalisemwa na Mwaliko. Alikuwa akiwaambia Umulkheri na Dick. Tendo hili lilitukia katika mkahawa wa Majaliwa walipokutana kisadfa. Hii ni baada ya Mwaliko kumpeleka babake mlezi maeneo yale kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake.
  2. Fafanua sifa tatu za msemaji (alama 6) 
   Msemaji ni mwaliko. Ana sifa zifuatazo:
   1. Mwenye maadii mema- Mwaiko alipoleewa na Mwangemi na Neema aliinukia kuwa ghulamu mwenye nidhamu ya hali yajuu akiwaheshimu wazazi na majirani na kuwatii wazazi.
   2. Mwenye shukrani- Mwaliko aliamua kumnunulia babake chakula cha mchana siku yake ya kuzaliwa kwenye hoteli ya Majaliwa
   3. Mwenye bidii- alifanya bidii masomoni hadi kufikia Chuo kikuu Alijisajili kwa shahada ya uzamili katika taaluma ya mawasiliano na kuhitimu. Mwaliko anafanya kazi yake kwa bidii ya mchwa. Zozote 3x2= 6
  3. Tamathali (alama2) Kuchanganya ndimi- Auntie
  4. Ni kwa nini Auntie Sauna alishikwa na polisi? Elezea kikamilifu (alama 8)
   Baada ya Umu kupiga ripoti kwenye kituo cha polisi kuwa nduguze wanuna wamepotea, Polisi walifanya uchunguzi wao na kujua kuwa walitekwa nyara. Aliyetekeleza kitendo hiki ni kijakazi Sauna. Sauna alikuwa akimfanyia biashara Bi. Kangora. Polisi walipojua mahali alikokuwa akijificha Bi. Kangara, walishika njia hadi nyumbani kwake ambako waliwatia mbaroni Bii Kangara na Sauna. Walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la ukiukaji wa haki za watoto hivyo basi wakafungwa miaka saba gerezani na kazi ngumu.

 7. Fafanua namna mbinu ya sadfa ilivyotumiwa atika Riwaya (alama 20)

  Sadfa ni matukio mawili ambayo hayakupangwa kutukia wakati mmoja. Sadfa imejitokeza katika mazingira yafuatayo. Kukutana kwa Umu na Dick kwenye uwanja wa ndege kulifanyika kisadfa - lakini cheti choke cha usafiri kikawa kimechelewa. Safari ikawa leo na ndipo Umu na Dick wakakutana. Ni sadfa kuwa wakati Umu anampa Dick ushauri wakiwa katika safari, ndipo Dick alikuwa ameamua kuyabadilisha maisha yake. Ni sadfa kuwa Mwangeka ndiye mlezi wa Umu na Dick naye binamu yake Mwangemi ndiye mlezi wa Mwaliko lkumbukwe kuwa Umu, Dick na Mwaliko ni ndugu. Ni sadfa kuwa hoteli aliyoichagua Mwaliko kumpeleka babake ili amnunulie chakula cha mchana ndiko akina Umu walikuwa na wazazi wake. Kukutana kwa Mwaliko na ndugu zake wawili ilikuwa ni sadfa. Hakujua kuwa wangekutana kwenye Hotel ya Majaliwa. Ni sadfa kuwa siku yake Umu ya kuzaliwa ilikuwa ndiyo siku ya kuzaliwa kwa Mwangemi. Ni sadfa kuwa siku aliyoitwa Ridhaa kwenda kumhudumia mgonjwa ndiyo siku Gila yake iliangamizwa na kumponyoka. (Mwanafunzi aongezee hoja)

 8. Jadili maudhui ya kifo kama yanavyoangaziwa katika Riwaya (alama 20)

  Kifo/mauti ni hali ya kutokwa na uhai. maneno marehemu mamake kuwa mwanamume hufumbika hlsia na kuwa machozi ya mwanamume hayapaswi kuonekana hata mbele ya majabali ya maisha. Terry na wanawe walikumbana na janga hili la kifo baada ya kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba yao. Kangata na Ndarine waliiaga dunia- mwandishi anatujuvya kuwa kwa sasa, miaka mitano imepita na Kangata na Ndarine wameipa dunia kisogo. Kiriri alikumbwa na mauti- mwandishi ametueleza kuwa Kiriri aliiaga dunia muda mfupi kutokana na kihoro cha kufilisikavna ukiwa aliokuwa ameachiwa na mkewe Annette na wanawe. Subira alikumbana na mauti baada ya Subira kuondoka nyumbani alienda mjini Kisuka na baada ya miezi kadha mumewe alimpata kwenye chumba chake akiwa amejifia, Nduguye Mwangeka alikumbana na mauti. Mwangeka anapomkumbuka Tila anatabasamu kisha tone moto la chozi linamdondoka. Kumbukumbu ya Annatila inavuta taswira ya mnuna wake mkembe aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka sita wakati ile Mwangeka akiwa na umri wa miaka kumi na miwili tonna ile ilipowafika. Baada ya Lunga kuachwa na mkewe aliiaga dunia mwandishi dhuho wa mwaka alifariki na kuwaacha watoto wake na mikononi mwa wao. Vijana waliofyatuliwa risasi waliiaga dunia tumeelezwa walimiminiwa risasi vifuani mwao na wote wakaiaga dunia kifo cha kishujaa kwani walijitolea mhanga kupigania uhuru tatu. Kaizari alitokwa na machozi na kuwahurumia Vijana hawa waliokufa kifo walichoweza kukiepuka. Lily Nyamvula na mwanawe Becky waliiaga dunia- Mwangeka ameketi mkabala mwa kidimbwi cha kuogelea nje ya jumba lake la kifahari ambalo yeye aliliona kama makavazi ya kumtonesho donda lililosababishwo na kifo cha mke wake Lily Nyamvula, Mgonjwa mmoja aliyejifia ni kijana anayesomea shahada ya uzamili, aiikuwa mwathiriwa wa pombe haramu. Wasichana waliokeketwa waliaga dunia. Mgonjwa kwa jina Tuama alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake waliokuwa wamepashwa tohara kama yeye. Tunaeezwa kuwa miezi mitatu baadaye ami yake Mwangeka aliyeitwa Makaa alichomeka asibakie chochote alipokuwa akiwaokoa watu ambao walikuwa wakipora mafuta kutoka kwenye lori lililokuwa lime bingiria. Mwanafunzi aongezee hoja. Zozote 10*2 = 20

 9. Jadili maudhui ya 'asasi ya ndoa' kama yalivyoangaziwa riwayani (alamo 20)

  Ndoa ni maafikiano rasmi baina ya mwanamume na mwanamke ili waweze kuishi pamoja kama mke na mume. Ridhaa alikuwa na mke kwa jina Terry. Walibarikiwa kuwa na watoto wafuatao: Mwangeka, Tila na marehemu Dede. Ndoa hii haikudumu kwani janga la moto iiliisambaratisha aila hii na ndipo Terry, Tila, Lily na Becky wakaiaga dunia. Ridhaa akabaki mjane. Mwangeka alikuta na Lily Nyamvula katika chuo kikuu na kumwoa. Walibarikiwa na mtoto mmoja kwa jina Becky. Ndoa hii haikudumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto. Baada ya ndoa ya mwanzo kusambaratika, Mwangeka alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa. Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema. Hawakufaulu kupata mwana wao kindakindaki japo walipanga mwana wao kwa jina Mwaliko. Kangata alikuwa na mke wake kwa jina Ndarine. Walibarikiwa na wana wafuatao. Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri. Lucia Kiriri -Kangata – alikuwa ameolewa katika ukoo wa Waombwe ambao awali walikuwa maadui sugu wa ukoo wa Mwongezo mzima lakini kutokana na Msimamo imara wa Kangata halikusimama. Watu wa ukoo wa kina Kangata walishangaapikwo nini mwana wao akaozwa kwa watu ambao huvaa nguo nje na pia huzaa majoka ya mdimu ambayo ni machovo kupindukia. Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira. Walibarikiwa na mabinti wawili, Lime na Mwanaheri. Lunga alikuwa na mke kwa jina Naomi. Walikuwa wa watatu, Umu, Dick na Mwaliko. Ndoa hii haikudumu Naomi alimwacha Lunga na kwenda mjini alikokuwa shangingi kwelikweli. Pete na Fungo- tunaelezwa kuwa Pete alipoingia darasa la saba alipashwa tohara nao wajombake wakapokea posa na baadaye' mahari kutoka kwa buda mmoja kwa jina Fungo aliyemuoa kama bibi wa nne. Ndoa hii haikudumu kwani Pete alihiari kumwacha baba huyu. Mwanafunzi aongezee hoja. Zozote

 10. Jadili maudhui ya nafasl ya mwanamke katika jamii (alama 20)

  Mwanamke amesawiriwa kwa namna mbalimbali: Mwanamke ni Msomi-Tila alikuwa akimudu masuala ya sheria. Hakuna aliyethubutu kuuchangia mijadala kwani katika masuala ya sheria Tila alikuwa ameyamudu kweli kweli. Selume- Ridhaa alimfariji na kumwomba asilie kwani mwana wake yu hai tena ana kisomo na amehitimu kama mkunga, anaweza kujitegemea. Umulkheri pia alisoma na kuhitimu vizuri. Mwanomke ni Mjinga- Tuama alikuwa amejipata katika hali mbaya kwa kukubai kupashwa tohara. Alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake. Tuama anaitetea mila hii ya upashaji tohara kwa wanawake eti haijapitwa na wakati kwani bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Huu ni ujinga na upumbavu. Mwanamke ni mwenye bidii- tunaelezwa kuwa Umulkheri alikuwa nyuma yake Dick akiwa amepiga foleni. Anasafiri ng'ambo kwa shahada yake ya uhandisi katika masuala ya kilimo. Umu, baada ya kuchukuliwa na Mwangeka na Apondi alifanya bidii masomoni na kufuzu vyema katika mitihani yake. Mwanamke ni mwenye tamaa ya mali- Naomi hakuwekwa na mazingira haya mapya(Mlima wa Simba). Asubuhi moja ' alimtumia Lunga ujumbe na kumtaarifu kuwa ameondoka; akatambe na ulimwengu na huenda akaambulia cha kumsaidia Lunga kuikimu familia. Akawaacha Lunga na wanawe. Mwanamke ni mwenye huruma- Apondi na Neema walijitwika jukumu la kuwalea wana ambao si wao kwa upendo na imani. Mwanamke ni katili muuaji- Mamake Sauna aimsaidia Sauna kuavya mimba aliyokuwa amepachikwa na babake mlezi. Neema naye alikuwa ameavya mimba nyingi akiwa kwenye Chuo kikuu. Mwanamke ni mwenye majuto- Neema aikuwa mwenye kujuta kwa kupoteza nafasi ya kupanga mtoto. Mwanamke ni mwenye kujiheshimu- Zohai amewahi kupigana na majitu yaiiyokuwo yakitako kuuhujumu utu wake kwa kumnyanyasa kijinsia. Mwanamke ni mcheshi- Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza bali alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini. (Mwanafunzi aongezee hoja. Zozote 10*2=20)

 11. Fafanua maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii (alama 20)

  Wana(jinsia zote) Ni wasomi- vijana kama Tila, Umu na Mwaliko walikuwa wenye bidii masomoni. Walanguzi wa dawa za kulevya — Dick alikuwa akilangua za kulevya kwa muda wa miaka kumi. Wenye Umu na Dick walikuwa na bidii katika masomo yao. Wajinga - vijana wengine wa kike walikubali kukeketwa. Wengine waliiaga dunia na wengine kulazwa zahanatini. Waraibu wa dawa za kulevya- Dick anasema kuwa alikuwa akitumia dowa hizi ili kujirahisishia kazi yoke ya kulangua. Wapenda fujo vijana ndio waliotumiwa na wanasiasa kuute-1F keleza uovu wa mauaji na kuyaharibu mali ya wenzao. Katili- kuna vijana waliowabaka mabinti zake Kaizari na kumuumiza mke wake.  Wasio na huruma- vijana wengine walikuwa wakiwaua wenzao bila huruma. Wasio na msimamo dhabiti- vijana wengine wakipotoshwa na wanasiasa bila kuwaza na kuwazua. (Mwanafunzi aongeze hoja Zozote 10 X 2 = 20)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kujibu Maswali na Majibu ya Insha na Muktadha wa dondo - Mwongozo wa Chozi la Heri.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest