TUMBO LISILOSHIBA - Said A. Mohamed - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Mukhtasari

Hadithi inaanza kwa taharuki kuhusu uvumi uliogeuka mnong'ono ukaeneza wasiwasi-hofu. Wasiwasi ulikuwa vibanda vitabomolewa vote. Watu wakubwa walitaka kuchukua makao ya watu ili kuendeleza ujenzi wao. Kwa Mzee Mago ndiko kituo cha kuzungumzia juu ya haki zao. Yeye huwakusanya wenzake iii wajadili juu ya haki zao za kuishi pale wanapochagua. Wanahojiana mambo juu ya:

 • Kustahili kuishi kwa amani na furaha popote nchini mwao.
 • Namna ya kuruka vikwazo vya sheria vilivyowekwa ili watu wadogo wasiweze kupoteza mali zao.
 • Kushawishiana watafute wanasheria waaminifu iii kutatua (mazonge ya sheria). Wanadai kuwa wanasheria waaminifu wameadimika — hakuna haki siku hizi.
 • Kunasihiana na kuamshana juu ya kukubali maendeleo yanayopiga kasi nchini mwao.
 • Maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu — mdogo kwa mkubwa, wa kike kwa wa kiume.

Mtu hawezi kukimbia ukweli, upya na usasa hutazamiwa kuleta mafanikio kwa watu wote. Mzee Mago huwaonya wauchunguze huo upya na usasa waujue jmst uhvyokaa — utaleta faida au hasara. Umaskini sio ujinga. Watu maskini wangeshauriwa wangeweza kuonyesha watakavyochangia maendeleo ya nchi yao. Watu wadogo hukasirika kwani wao hufanywa kuwa kama takataka. Hasira yao ndiyo inayowapa motisha wa kusema na kujitetea. Wakubwa walidai kuwa jiji limejaa na halina nafasi tena, suluhisho ni kubomoa baadhi ya mitaa. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, majumba ya Mall, maduka n k. Kwa hiyo, suluhisho la uhaba wa nafasi jijini ni kubomoa sehemu zingine. Mzee Mago aliwaleta wenzake pamoja kupigania haki za hapo Madongoporomoka — pasibomolewe.

Baadhi ya wanyonge hawa wanataka wapewe visenti vyao vichache vaondoke. Wengine wanadai, hakuna kuondoka. Wanataka vvabaki pale pale na kupigania haki zao. Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawataweza, kwani wanaogopa umma wa Madongoporomoka. Bi. Suruta aliwatahadharisha kuwa wakubwa hawaogopi kitu chochote.

Wakati mjadala ukiendelea, chakula cha pale mgahawani kilikuwa tayari na kikaanza kunukia na kuwatamanisha wale waliobarizi hapo. Mara likatokea jitu kubwa na kukaa mle ndani. Jitu hilo liliamuru liletewe chakula Chote cha wateja wa Mzee Mugo. Jitu hilo lilifagia aina zote za vyakula: wali wa nazi, mchuzi, nyama ya kuchoma, kachumbari n k.

Baada ya kula vyakula vyote vya mgahawani hapo lililipa hela yote kisha likaahidi kuwa kesho tena lingekuja na liandaliwe chakula mara mbili ya kile kilicholiwa. Likawaacha kwa kitendawili kuwa, kesho kama wakiamka salama kama watafungua milango ya nyumba zao zilizosimama juu ya ardhi adhimu.

Alfajiri iliyofuata, polisi wakiwa na mirau na bunduki walikuwa wanalinda askari wa baraza la mji wakiviporomosha vibanda vyote.
Kulikuwa na mahangaiko ya wanyonge wasiwasi na hatan Mbio... Hawajui waokoe mali zao duni au nafsi zao kelele' kwenzi vilio, malalamiko, vumbi (Uk 10).

Kumbe kile kitendawili cha jitu kilimaanisha kuwa ardhi Yao ingetwaliwa yote. Hata hivyo, wanyone wanashikilia msimamo wao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katikia ardhi yao. Baada ya wiki tatu za vurugu hilo; vibanda mshenzi Vya MadongoporomOka viliota, tena vingi kuliko vya awali.Anwani

Hadithi hii imepewa kichwa ambacho kinasadifu Yale yaliyomo. Wananchi wa Madongoporomoka walisikia uvumi kwamba kulikuwa na mpango wa kubomoa makao yao ili kutoa nafasi ya upanuzi wa jiji. Walijadiliana mara kwa mara wakiwa katika mkahawa mshenzi wa kiongozi wao Mzee Mago. Walijadili nini? Walitaka wapate suluhisho ili kujiauni na janga hilo, hawakuwa na makao mengine.

Wakiwa katika mgahawa huo wanaagiza vyakula mbalimbali. Linatokea jitu moja kubwa likatoa agizo kwamba lipewe vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja wengine. Lilitishia kwamba wapende wasipende angejitwalia vyakula hivyo.

Jitu lilikula aina zote za vyakula na kunywa chupa kadhaa za soda. Mwishowe lililipa na kuahidi kwamba lingehitaji chakula mara mbili zaidi kesho yake. Siku iliyofuata, lile jitu litifika kuja 'kula ardhi' ya Madongoporomoka. Lile tumbo halishibi si chakula tu, bali rasilimali za raia kama ardhi.

Tumbo lisiloshiba husimamia wenye mamlaka ambao hawatosheki — wanamiliki mali nyingi lakini bado wanahitaji kumiliki kite kidogo walicho nacho wanyonge. Usasa na maendeleo yameleta ahueni kwa wananchi wachochole au yamezidisha unyanyasaji?Dhamira

Mwandishi amedhamiria kuonesha namna tabaka la juu linavyokandamiza haki za wanyonge. Tabaka hili linajilimbikizia mali na kutwaa rasilimali za wanyonge bila kushiba.Maudhui

Ukatili na Dhuluma

Wakazi wa Madongoporomoka wanadhulumiwa ardhi yao. Tabaka la mabwanyenye wanawatoa katika ardhi you no kuwavunjia vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia yao na kuwavunjia vibanda vyao pasipo hata fidia. Unyanyasaji huu unafanyika kwa kuwa wakazi Madongoporomoka hawana mtetezi. Haki imenunuliwa wenye nacho. Hata hawajaoneshwa mahali mbadala watakwenda.

 

 

Matabaka

Hadithi hii inasawiri kuwapo kwa matabaka katika jamii. Kuna tabaka la mabwanyeye na tabaka la wanyonge. Tabaka la mabwanyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge. Katika hadithi hii jitu kubwa linaonekam likisimamia shughuli ya ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporomoka. Tabaka hilo la mabwanyeye linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza Ia mji na askari polisi katika kuwakandamiza wanyonge.

Ukosefu wa Haki

Katika jamii iliyojaa dhuluma hakuna haki. Watu wa Madongoporomoka wanaporwa haki yao ya kumiliki ardhi. Ardhi inatwaliwa na wenye nacho. Hata wanaposhauriana kutafuta wanasheria waaminifu bado wanashindwa kuwapata. Wanasheria wamezibwa midomo kwa fedha za mabwanyenye. Haki za watu zinasiginwa bila uteten wowote.

Umoja na mshikamano

Hata hivyo nguvu ya mnyonge ni Urnoja. Wakazi waMadongoporomoka wanaapa kuwa fujo hazitasaidia lolote. 1 yao kwa sababu ya fujo. Baada ya wiki tatu za fujo hiyo wanaungana na kurejeshaWahusika

Mzee Mago

 • Mpenda haki na mtetezi wa haki: yeye hakupuuza ule uvumi bali alijaribu kuutafutia suluhisho
 • Ni mwenye bidii: shughuli ya kupigania na kuzuia mipango ya watu wakubwa sio rahisi. Ilibidi mzee Mago ajinyime, awatafute wenzake wazungumze na kulijadili jambo hili ambalo lilikuwa nyeti sana kwao.
 • Ni mshawishi: aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho.
 • Ni mzindushi: aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo. Aliwazindua kwamba maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu — wa kike kwa wa kiume, wadogo kwa wakubwa n k. Aidha, aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayowanufaisha.

Kabwe

 • Anapenda ushirikiano. Alishirikianana wanyongewenzake katika kutafuta ufumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.
 • Anaamini kuwa sheria inaweza kuwa suluhisho la matatizo yao.
 • Ni mpenda amani na haki. Alitaka watafute suluhisho linalofaa kwa watu wa Madongoporomoka.

Bi. Suruta

 • Ni hodari katika kutoa hoja kwenye mashauriano. Anawapiku wanaume wote.

Bi. Fambo

 • Mwanamke mojawapo wa wanyonge.
 • Ni mwelewa masuala ya unyanyasaji.
 • Anaeleza bayana kwamba wakubwa hawajali wanyonge wakihamishwa kwenye ardhi watakwenda wapi.

Jitu la miraba minne

 • Hili lilikuwa ndovu — mtu kwa ukubwa wake.
 • Ni mkubwa wa kimo: yeye alikuwa pandikizi la jitu Alipoingia katika mgahawa mshenzi wateja wote waligutuka
 • Ni tajiri: mavazi yake ya suti na tai yalidhihirisha kuwa ni tajiri. Aidha yeye aliendeshwa na dereva wake maalum "chauffeur" katika gari Ia Audi Q 7.
 • Ni mlafi: alikula vyakula vyote vya wateja waliokuwePO katika mgahawa wa Mzee Mago na kurudia mara tano kabl ya kushiba. Aidha alikunywa soda nyingi sana. vyakula vyote na hata hakusaza chochote.


Tanbihi; Ikumbukwe kwamba vyakula hivyo vilikuwa vimeagizva na wateja mbali mbali. Wote wamwachie vyakula vyao walivyokuwa wameagwa - wapende wasipende. Anahusika katika uvamizi na unyakuzi wa ardhi ya Madongoporomoka.

Ni ishara ya wakubwa wa mji na sehemu nyingine ambao hawatosheki na mali nyingi walizo nazo. Daima hujinyakulia mali za wanyonge ili kuzidi kujinufaisha. Maendeleo ni mazuri lakini wakati mwingine yanazusha mtafaruku katika jamii.

Askari wa baraza la mji

 • Hawa walibomoa vibanda vya wananchi wa Madongoporomoka.
 • Ni watiifu wa amri za wakubwa-hawakujali vilio na malalamiko ya wanyonge.

Kikosi cha polisi:

 • Kinalinda askari wa baraza wakati wa kubomoa vibanda madongoporopoka.


Mbinu za Lugha

Taharuki.

 • Hadithi inapoanza kuna taharuki. Huo ni uvumi gani? Unazushwa na nani kwa sababu gani? Anaposema haukuwa wa kupasuka bomu au kulipuka mzinga anaendelea kuitilia uzito taharuki hiyo.
 • Taharuki nyingine ni ile ya jitu liloingia mkahawa mshenzi lilitokea wapi? Kwa nini liliamua kuutembelea siku hiyo. Je ziara yake ni kula tu chakula au kufanya uchunguzi?
 • Je jitu lenye tumbo kubwa lina uhusiano gani na kubomolewa kwa vibanda? Je ni kitu gani kilifanya vibanda vingi kushamiri baada ya kubomolewa?

Taswira

 • Kuna taswira nyingi katika kisa hiki. Kuna taswira ya jitti la miraba mine kutokana na maelezo ya lile jitu lilivaa suti nyeusi na shati jeupe. Wakati mabuldoza yalipokuwa yakiangusha vibanda na kuwatimua watu. Ni taswira inayoangazia jinsi haki za wanyonge zinavyofifishwa. Aidha jeshi la polisi hushadidia jambo hilo hilo la unyanyasaji wa w anyonge.

Balagha

 • Haya ni maswali yasiyohitaji majibu, yanayomzindua mhusika.
 • Mifano: yote hayo lakini yafae nini mbele ya nia ya kuhakikisha nafasi za biashara na malengo ya starehe ya wakubwa (Uk 10)
 • Chupa mbili za Coca Cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo (Uk 8)

Mdokezo

 • Maelezo machache ambayo hayakamiliki, yakitumiwa kuashiria jambo fulani. Lile jitu la miraba minne lilidokeza kwamba kungekuwa na tukio fulani. Kesho kama sote tutaamka salama. Kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimama juu ya ardhi hii adhimu.

Tashbihi

 • Bweu lilipasuka kama mzinga (Uk 9)
 • Kiti kilionekana kama cha Shule ya chekechea (uk 7)
 • Kauli yajitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama aliyechapwa bakora.

Kuchanganya ndimi

 • Chauffeur (Uk ll)
 • AudiQ7 (Uk10)
 • Coca Cola
 • Departmental stores, casinos (Uk 4)

Methali

 • Kuna matumizi ya methali kama kimya kingi kina mshindo (Uk 3)

Takriri

 • "Hawawezi, hawawezi kabisa hawawezi" (uk 5)

Mbinu rejeshi

 • Uvumi kuhusu kubomolewa kwa vibanda ulianza halafu ukatoweka. Baadaye uvumi huo unarejelewa tena katika kibanda cha Mzee Mago.

Chuku

 • Ukubwa wa tumbo la mtu mwenye miraba mine limetiliwa chuku (uk 9)Kwa nini mwandishi amefanya hivi? Jim lilivyolamba sahani zote — halikubakisha hata ishara a chembe moja ya chakula chochote alichokula (Uk 9)

Taashira

 • Msitari wa fedha ulipasuka kutoka mbinguni hii ni ishara za matumaini, mwangaza au nuru huashiria jambo jema.Hali ya mstari huo kumulika mpaka ndani ya mioyo ya watu na wakati huo huo uso wa lile jitu lisiloshiba kuonekana. Hii ishara ina maana kuwa ndani ya nafsi za wanyonge wakiongozwa na Mzee Mago wanajua kuwa taabu zao zinatokana na wale wakubwa wasioshiba — wakiwakiJishwa najitu ndani ya Audi Q 7.
Join our whatsapp group for latest updates

Download TUMBO LISILOSHIBA - Said A. Mohamed - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest