MAPENZI YA KIFAURONGO - Kena Wasike - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Kifaurongo ni mmea ambao majani yake hujikunyata yanapoguswa.

Dennis ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu ch Kivukoni. Ndani ya nafsi yake anasononeka kwa ufukara uliomwandama yeye na familia yak-e. Umaskini unamsumbua maana hali yake na ya watoto wa matajiri ilikuwa zimeachana wazi kabisa kama mbingu na ardhi.

Kulikuwa na tofauti katika mavazi, chakula, simu na vifaa vingine kisasa.

Hali ya umaskini inamfanya asielewe yale ambayo mhadhiri

Dkt Mabonga alikuwa akiwafundisha. Licha ya tatizo lake la umaskini, Dennis amekabiliwa na ugumu wa somo hili. Dkt Mabonga aliwakatisha tamaa wanafunzi wake kutokana na shutma zake kwamba wao hawafikirii na kutafakari mambo kwa kina kama wanafunzi wapevu wa Chuo kikuu. Alipoulizwa maswali aliwakashifu kwamba hawastahili kuwa humo kwenye darasa Ia chuoni.

Kwa Dennis hili liliongeza uzani zaidi wa tatizo lake. Dennis hakuweza kuchangamana na wanachuo wakwasi. Kulikuwa na matabaka — wenye jadi kubeli wanapitajuu na wachochole wanapita chini (Uk 17). Wanafunzi wakwasi walipoona masomo yanatatiza walikuwa na fursa ya kurejea makwao na kuendeleza miradi ya wazazi wao. Kwa Dennis hili lisingewezekana. Wazazi wake walikuwa wanategemea vibarua vya kulima mashamba ya watu Wengine. Yeye ndoto yake ilikuwa kumaliza masomo na kupata kazi ili aweze kuumaliza ukata wake na wazazi wake.

Umaskini wake ulimfanya asiwazie hata kuwa na rafiki wa kike.

Penina msichana wa tabaka Ia juu anamtembelea Dennis na kutaka Wawe marafiki. Dennis analipinga jambo hilo kutokana na tofauti zao za kitabaka; lakini Penina anang'ang'ania kuwa tofauti zao kiuchumi haziwezi kuwa kikwazo. Penina alitaka mwanaume ambaye ni mwaminifu. Anasisitiza, "Nataka tupige vita fikra kwanlba kijana wa kitajiri hawezi kutangamana na mwenziwe (Uk 21)

Mapenzi ya Penina aliyetoka katika familia ya wakwasi na Dennis tkara yalidumu kwa miaka miwili. Baada ya kumaliza Chuo walnshi mtaa wa watu wastani kimapato. Pamoja najitihada zoteza kutatilta kazi. Dennis hakufanikiwa. Barua zake nyingi alizotuma hazikumletea tumaini lolote.

Fursa moja aliyopata katika shirika Ia uchapishaji magazeti aliipoteza baada ya kushindwa kujibu swali la kwanza katika mahojiano.

Mapenzi ya kifaungo ya Penina yanajitokeza wazi. Anamfukuza Dennis na kumwonya kwamba nyumba yake aione paa. Alielezea majuto yake ya kusuhubiana naye na kumkanya kwamba asije akaelezea watu wengine kwamba waliwahi kupendana.

Dennis alifungasha nguo zake na kuondoka akiwa haamini. Kumbe mapenzi ya Penina yalikuwa ya kifaurongo.Anwani

Anwani ya hadithi hii ni "Mapenzi ya Kifaurongo.Kifaurongo ni mmea ambao unajikunja Pindi tu unapuguswa na hujikunjua baada ya muda mfupi. Katika hadithi hii mhusika Penina anampenda Dennis kwa kuwa alikuwa mwaminifu. Walimaliza masomo yao lakini baada ya miaka miwili, kutokana na ukosefu wa kazi mapenzi yake yalididimia na kunyauka kabisa. Hakutaka kuhusishwa tena na Dennis. Alimfukuza kama mbwa. Ahadi zake za mapenn zikawa kama za ule mmea. Dennis alihitaji kazi na alikuwa na ari ya kufaulu usaili lakini; anaulizwa swali moja tu na ananywea na kushindwa kujibu na hivyo anarudi nyumam bila tumaini lolote.

huduma ni sawa na mmea wa kifaurongo. Anaonesha Kuwa penzi la Penina na Dennis linanyauka baada ya Dennis kukosa kazi ambayo ingcmpatia kipato cha kumhudumia mkewe.Maudhui

Ndoto za maisha.

 • Wazazi wa Dennis walifanya juu chini ili waepukane na ukata lakini uliendelea kuwaandama. Walimsomesha Dennis wakitegemea kwamba baadaye angewasaidia lakini Dennis hakufanikiwa kupata kazi. Dennis alikuwa na ndoto zake. Alitaka kufaulu vizuri-hii ndoto ilitimia. Alitarajia kupata kazi baada ya kuhitimu ndoto hii haikutimia, licha ya yeye kuandika tawasifu yake na kuituma sehcmu nyingi.
 • Aidha, Dennis alikuwa na matarajio ya kumwoa mchumba wake Penina. Hilo halikutokea, na isitoshe waliachana kwa njia mbaya-Penina alimfukuza atoke kwake.
 • Dennis alikuwa na ndoto ya kuwa mtangazaji wa redio. Alifanya mazoezi mengi na kujipatia ujuzi ambao watu wengi waliafiki kwamba atakuwa mtangazaji bora mno. Hata hivyo ndoto yake hiyo haikutimia.

Matabaka

 • Dennis anatoka katika familia maskini. Wazazi wake walikuwa wachochole, hawakuwa na mali Waliiitahidi sana kutoka katika ufukwe huo haikuwezekana walimiliki majumba mengi na wengine walikuwa misururu ya mabasi na matatu ya abiria. Shakila alikuv wa tabaka la juu — mama yake alikuwa mkurugenzi tnku wa shirika la uchapishaji. Wanachuo waliotoka tabaka laju walikuwa na maisha mazuri, libasi (nguo) zao ni bora, wan; simu nzuri, tarakilishi na vitu vingine. Dennis mavazi yak, valikuwa duni, kula kwa shida na kadhalika.
 • Kulikuwa na watu walioendesha magari ya kifahari makubwa na mazuri. Wazazi wa Dennis ni wa tabaka la chini. Walifahamu kuweka majembe begani na kulima vibarua tu.

 

Umuhimu wa kazi.

 • Kila binadamu lazima afanye kazi. Kazi humzatiti binadamu. Elimu hutumiwa kama kidato cha kujipatia kazi. Kazi ndiyo msingi wa maisha. Maisha hayawezi kusonga mbele kama hufanyi kazi yoyote. Kitendo cha Dennis kukosa kazi, kinamfanya aonekane kama mzigo asiye na faida yoyote kwa Penina. Penina anaamua kuachana naye na kumfukuza kabisa atoke kwake

Mapenzi

 • Wanafunzi wa Chuo cha Kivukoni wanaonekana wengi wao kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Wale wa tabaka muia huonekana wakiongozana mvulana na msichana kufanya starehe za hapa na pale.
 • Aidha, Penina mtoto kutoka katika tabaka la wenye nacho, anasalitiwa na mpenzi wake ambaye naye ni wa tabaka la juu. Katika kutafuta suluhisho Ia mapenzi ya dhati Penina anaamua kupelcka mapenzi yake kwa Dennis ambaye anatoka katika tabaka la chini. Mapenzi yao yananoga kama kinu na mchi wakati wakiwa chasm. Penzi linakuja kuwa Ia kifaurongo pale wanapomaliza chuo na Dennis kukosa kazi


Wahusika

Dennis

 • Kutokana na ukata wa wazazi wake, Dennis anaishi maisha ya kimaskini chuoni.
 • Anakuwa mpweke chuoni. Umaskini wake ulimfanya asijiamini na aghalabu alikuwa mwenye huzuni. Anaisitikia hali yake duni, akawa msononevu.
 • Anabahatika kupendwa na Penina, msichana mrembo kutoka familia ya kitajiri. Mvuto wa Penina unamfanya Dennis abadili msimamo wake wa awali-akasalitika na kukubali kuwa na mahusiano naye.
 • Ukosefu wa ajira unamfanya afukuzwe na Penina-akajikuta mpweke tena asiye na makao. Kauli ya Dennis ya hapo awali ikatimia; "Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa" (Uk 20)
 • Ni mvumilivu: anavumilia hali yao ya umasikini na ukosefu wa vifaa vya kisasa alipokuwa chuoni.
 • Ana bidii: anajitahidi sana katika masomo hadi akafaulu vyema. Alisomea kijijini kwenye shule za kawaida lakini akafaulu na kuingia chuo kikuu.
 • Alitafuta kazi kwa bidii, alituma tawasifu yake mahali pengi.
 • Ana tamaa: alitamani awe na rafikimpenzi kama wanachuo wengine. Kuwa na gari la kifahari-"Sikomi kuyamezea mate hayo". Alitamani hali njema ya siha mavazi bora ya watu wakwasi. Alitamani wazazi wake wangekuwa matajiri
  Kutokana na ukata wa wazazi wake, Dennis anaishi maisha ya kimaskini chuoni. Anakuwa mpweke chuoni. Umaskini wake ulimfanya asijiamini na aghalabu alikuwa mwenye huzuni. Anaisitikia hali yake duni, akawa msononevu. Anabahatika kupendwa na Penina, msichana mrembo kutoka familia ya kitajiri. Mvuto wa Penina unamfanya Dennis abadili msimamo wake wa awali-akasalitika na kukubali kuwa na mahusiano naye. Ukosefu wa ajira unamfanya afukuzwe na Penina-akajikuta mpweke tena asiye na makao. Kauli ya Dennis ya hapo awali ikatimia; "Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa" (Uk 20)
 • Ni mvumilivu: anavumilia hali yao ya umasikini na ukosefu wa vifaa vya kisasa alipokuwa chuoni. Ana bidii: anajitahidi sana katika masomo hadi akafaulu vyema. Alisomea kijijini kwenye shule za kawaida lakini akafaulu na kuingia chuo kikuu. Alitafuta kazi kwa bidii, alituma tawasifu yake mahali pengi. Ana tamaa: alitamani awe na rafikimpenzi kama wanachuo wengine. Kuwa na gari la kifahari-"Sikomi kuyamezea mate hayo". Alitamani hali njema ya siha mavazi bora ya watu wakwasi. Alitamani wazazi wake wangekuwa matajiri
 • Mwenye hasira: anamkashifu Dennis kwa kasbfa no kukosa kazi,

 

Umuhimu Wake

Ametumiwa kuangazia ugumu wa kupata apra hata ya kupata shahada. Aidha. Dennis ametumika kudhihirisha kuwa si Rihisi kijana wa kiume mchochole kupendwa na msichana wa tabaka la juu na mahusiano yao kudumu.

Penina

 • Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Kivukoni.
 • Msichana kutoka kwenye familia yenye utajiri mwingi.
 • Baba yake Bw. Kitime ni Katibu wa kudumu katika Wizara ya Fedha.
 • Penina anapata masurufu mengi ya kutosha, shilingi elfu tano kila juma.
 • Ni mshawishi: alimshawishi Dennis kuwa pesa na mapenn ni vitu tofauti. Dennis alikubaliana naye.
 • Ana tamaa ya mapenzi: ingawa alipewa pesa za kutosha alikuwa na majonzi kwa ajili ya kukosa mpenzi.
 • Ni jasiri: alimpasulia Dennis ukweli kuwa amempenda na anataka wawe wapenzi badala ya kusubiri afuatwe yeye.
 • Hana uvumilivu sana: aliweza kukaa na Dennis kwa miaka miwili tu akamtupa nje ya nyumba yake.
 • Ni mwenye msimamo: alikata kauli ya kupendana na mwanaume asiye na pesa. Alitoa uamuzi kwamba hataolewa mpaka Dennis apate kazi kubwa. Alipokosa ajira anamfukuza na kumtukana.
 • Hana subira: aliweza kumvumilia Dennis kwa kipindi Cha miaka miwili tu-
 • Mwenye hasira: anamkashia Dennis kwa kashfa kali kutokana na kukosa kazi.
 • Mdadisi: aliweza kujua jina Ia Dennis hadi chumba chake katika Mastura Hall. Alijua kuwa Dennis hana fedha na kumweleza bayana.

Umuhimu

Anadhihirisha kuwa sio rahisi msichana wa tabaka Ia juu kuolewa na mvulana mchochole.

Dkt Mabonga

 • Mhadhiri wa Chuo kikuu.
 • Anaifahamu mada yake ya fasihi vyema.
 • Anakatisha wanafunzi tamaa kwa majibu yake ya mkato na makavu.
 • Mkweli: hasiti kusema yale yaliyomo moyoni hata kama yataleta maudhi.
 • Ingawaje ni msomi anashindwa kuwafafanulia wanafunzi wake dhana ngumu zinazowatatiza.

Umuhimu

 • Ametumiwa kudhihirisha ugumu wa masomo ya Chuo kikuu na namna walimu wanavyohitaji wanafunzi watafute maarifa wao wenyewe.

Shakila

 • Mwanachuo na mwanamji wa Kivukoni.
 • Msichana am baye hakupata shida za kutafuta kazi.
 • Ana mlahaka mwema: anamkumbuka na kumsalimia vizuri Dennis wakati Dennis ameenda kuomba kazi.
 • Ni mwenye maiivuno
 • Ni mwenye majivuno: alijigamba chuoni kwamba yake ni mkurugenzi wa shirika moja la kuchapisha
 • Ni mfariji: anampa moyo Dennis kwamba Mungu apate kazi ile.

Umuhimu

 • Kudhihirisha matabaka yaliyo katika jamii.

Bwana na Bi. Kitime

 • Hawa ni wazazi wa Penina.
 • Bwana Kitime ni Katibu wa kudumu wa Wizara ya Fedha.
 • Ni wakwasi, wako katika daraja la juu.
 • Wanamtumia binti yao fedha za kutosha kila wiki.
 • Wanampa binti yao malezi ya hali yajuu kwani wanajiweza.
 • Wanawapatia Penina na Dennis masurufu yote wakielewa fika kuwa hawana kazi.
 • Ni washauri: walimtahadharisha Penina kuhusu kuolewa na mchochole asiye na kazi. Hata hivyo walimwachia Penina uhuru wa kujiamulia.


Mbinu za Lugha

Taharuki

 • Kuna taharuki, wakati mlango wa Dennis unapogongwa: Mja huyo ni nani, Penina alijuaje kuwa huyu kijana anaitwaDennis.
 • Wakati kisa kinapomalizikia pia kuna taharuki: Je Dennis alienda wapi? Alipata mastakimu vipi bila fedha? Penina aliendelea kuishi katika nyumba ile.

Balagha

 • Wavulana wangapi wamejikuta wakining'inia bila kupenda kwao'? (Uk 18)
 • Kwani swali langu liko vipi? Kwa nini wanafunzi anacheka? Maswali haya yanamhusu Dennis. Kwa nini ninalia sasa (Uk 13)
 • Fukara aliyefukarika mpaka mwisho aseme mm mbele ya wanaojigamba na kujishaua?(Uk 16) ...
 • Nitawalipaje wazazi wangu wema walionitendea (Uk 25)

Tashbihi

 • Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi (Uk 25)
 • Nimetoka ofisini kama mgonjwa mahututi.
 • Nimeweweseka kama ubua (Uk 25)
 • Mapenzi ni matamu kama uki (Uk 16) Yametengana kama ardhi na mbingu (Uk 17)
 • Njaa inanitafuna kama mbwa anavyouguguna mfupa (Uk 17)
 • Kutetemeka kama aliyenyeshewa na mvua kubwa kumwibua bingwa ni kama kupata maziwa kutoka kwa kuku (Uk 13)

Methali

 • Mzoea sahani vya kigae haviwezi (Uk 20)
 • Ujapokosa la mama hata la mbwa huanwa (Uk 17)
 • Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura (Uk. I 5)
 • Mtu huvuna alichopanda (Uk 20)
 • Mzungu wa kula haufunzwi mwana (uk 15 )
 • Mgomba changaraweni haupandwi ukamea (Uk 27)

 

 

Misemo

 • Hazipunguzi hazizidishi (uk 21)

Utabiri

 • Dennis alitabiri vile ambavyo Penina alimpenda wakati huo" akasema kesho anaweza kuwa chanzo cha kero na usumbufu. Huba litakuwa limekufa na kufukiwa kaburini.
 • Hili lilitokea baada ya kukaa kwa miaka miwili na mchumbake Penina.

Litifai

Kuna maneno yaliyodondolewa katika riwaya ya utengano "Na nyumba hii uone " (Uk 27)

Kuchanganya ndimi

 • Your competence is doubtful, (uk 25)
 • Tarmacking (uk 26)

Mjadala wa nafsi

 • Dennis anapofukuzwa anajizungumzia sijui kama mimi ndiye kupe au mlazadamu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download MAPENZI YA KIFAURONGO - Kena Wasike - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest