SHOGAKE DADA ANA NDEVU - Alifa Chokocho - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Bwana Masudi na Bi. Hamida ni mtu na mkewe. Wamejaliwa kupat binti aitwaye Safia. Kabla ya kulala wazazi hawa huzungumz mambo mazito yanayogusa mioyo yao. Walimsifia sana binti yao kwa vile alivyo na mwenendo mzuri. Safia ana tabia inayowafurahisha wazazi wake. Shuleni anafanya vyema kabisa. Wazazi hawa walielewa vyema kabisa kuwa kupata mtoto na kumlea ni mambo mawili tofauti "...kuzaa mwana si pato, pato ni kumvyeleza " (Uk 29)

Walijadili ukweli kwamba wapo wazazi waliojali wa watoto, lakini wakawa balaa. Wakakosa manufaa kwa wazee wao na jamii nzima.

Bi. Hamida anatoa mfano wa mtoto wa Habiba Chechei aitwaye

Mkadi. Mkadi ana vitendo viovu kushinda shetani. Walimlinganisha

Mkadi na Safia na kuona binti yao ni safi hana doa.

Sifa nzuri za Safia zilienea hadi kwa marafiki na watu wote wanaoingia na kutoka kwa Bwana na Bi. Masudi. Kwa nini anasifiwa hivyo?

 • Husaidia wazazi wake.
 • Husaidia kazi zozote habagui.
 • Yeye ni hodari sana shuleni.
 • Kila mtihani huibuka wa kwanza.
 • Humwogopa Mungu na kufuata sheria zake zote.
 • Safia hujiongoza na kufanya hayo yote bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Hayo yote aliyalifanya wazazi wake wakashukuru kupita kiasi.

Safia aliwataka wazazi wake wamruhusu Kimwana shoga yake aje ili wajitayarishe vyema kwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza.

Wazazi wa Safia walikubali wasemavyo wahenga kuwa, . kidole kimoja hakivunji chawa. Analolijua Safia, Kimwana halijui.

analolitambua Kimwana Safia hana habari nalo e " (Uk 31)

Wk 30 Baada ya muda, Kimwana akaanza kuja nyumbani kwa akina Safia na wakawa wanasomea chumbani. Wakaomba kufunga mlango ili wasisumbuliwe na Lulua, ndugu mdogo wa Safia. Wazazi wao wakawaruhusu wafunge mlango kwa ndani. Baada ya muda kupita, Bi. Hamida akawa ana shaka ya kuwa Safia ni mjamzito. Akaanza kuona dalili zote — kutapika na kunyong'onyea na hana uchangamfu. Alipomdadisi, Safia alikasirika na kumlaumu mama yake. Hata hivyo Bi. Hamida alitia shaka, akachanganyikiwa-Safia anasema uongo au ukweli. Alimuuliza mumewe, ambaye alisema kuwa Safia hawezi kuwa mjamzito. Siku moja wakila chamcha, Lulua alitoboa siri kwamba, aliingia chumbani mwa Safia akawakuta wamelala. Na shogake Safia alimwona ana ndevu. Wakati huo huo Bw. Masudi akapata ujumbe kwa simu uliomgutusha — Safia aliyekwenda kliniki kutoa mimba amekufa. Bi. Hamida na Bw. Masudi wakachukue maiti.Anwani

 • Anwani ya hadithi hii inasadifu yale yaliyomo. Safia binti wa Bwana Masudi na Bi. Hamida anajulikana kuwa ana nidhamu ya hall ya juu. Ni mtiifu, anafanya kazi zote za nyumbani na shuleni anaongoza. Wazazi hawa walijua fika kuwa Mungu amewajalia. Kwa imani ya dini, Safia alikuwa mcha Mungu kabisa.
 • Ili kujitayarisha na mtihani wake wa mwisho, Safia aliomba rafiki yake aje kwao wadurusu pamoja. Wazazi wake bila shaka wakamkubalia. Kimwana aliyeaminika kuwa na tabia kama ya Safia akawa anakuja kudurusu. Wakimaliza alirejea kwao. Kuzuia usumbufu wa Lulua ndugu mdogo wa Safia, wazazi wakawaruhusu kujifungia ndani.
 • Safia alianza kuwa mnyonge na kutapika. Mama mtu akaingia shaka. Alipomshirikisha mumewe, hakuafikiana naye wakati walicheza aliwahi kujitoma chumbani akaingia shaka. Alipomshirikisha mumewe, nayc, V,ulua wakati walicheza aliwahi kujitoma chumban akawakuta Safia na shogake wamelala —na shogake ana ndevu Safia alikuwa mjamzito na katika shughuli za kutoa akafariki. Mimba ni ya shogake mwenye ndegu.


Dhamira

 • Mwandishi amedhamiria kuwakumbusha wazazi kuongeza umakini katika malezi ya watoto. Wasiwaamini watoto wao asihmia mia moja.


Maudhui

Changamoto za Malezi

 • Wazazi wanaweza kujitahidi kutoa malezi yanayofaa lakini maamuzi ya kuwa na mwenendo bora ni juu ya mhusika mwenyewe. Mtoto wa Bi. Habiba Chechei aitwaye Mkadl alisemwa kuwa ana tabia chafu sana. Safia alionekana mwenye tabia nzuri. Na alipoamua kuwa mzuri alitekeleza majukumu yote — kusaidia kazi za nyumbani, kuheshimu watu na kutia bidii masomoni. Kwa upande mwingine aliamua kufanya mapenzi kabla ya wakati akijua kuwa sio vyema.
 • Aidha anasema uongo kwa mama yake. Jitihada za Bi Hamida za kutaka ajue ukweli zikagonga mwamba. Safia akaarnua kutoa mimba ingawa alielewa ni kosa. Na alifariki. Akawaachia wazazi na jamii nzima mshangao na masikitiko

 

Unafiki na Uongo

 • Safia alikuwa mnafiki na mwongo. Alijifanya kwamba ana tabia safi kama umande, kumbe alikuwa na tamaa ya ngono Wanakijiji wanamsema vibaya mtoto wa Hamida Chechei na kumfananisha na mbwa. Hawakumsengenya Safia kwa sababu mbele ya macho yao alikuwa na tabia nzuri. Mama anapomuuliza na kumdhihirishia kwamba anamshuku, anapandisha hasira. Baba Safia, Bw. Masudi, alimwamini binti yake mno, hata akakashifu fikra zake. Matokeo yake Safia anafikia hatua ya kudanganya kuwa yule anayesoma naye chumbani ni binti kumbe njemba yenye ndevu.

Tamaa za vijana

 • Safia anajitahidi kwa kila jambo, masomo aliyamudu vyema. Anasifika kwa kazi za nyumbani kama vile kupika, kufua, kupiga pasi na kadhalika. Kanuni au sheria za dini alizizingatia bila wahaka (wasiwasi) wowote. Hata hivyo anawaka tamaa ya kufanya mapenzi. Anaamua kutumia ujanja kwa kutoa ombi ambalo halikuwa na shaka kwa wazazi wake. Na yeye akajichimbia kaburi mwenyewe
 • "Kimwana" anaye anakuwa na tamaa. Alijifutika kwenye buibui na kujifanya kuwa yeye ni kimwana shoga yake Safia. Udanganyifu huo umeleta hali ya mtafaruku kwa wazazi wa Safia. Bi. Hamida anakosa furaha kabisa. Huenda njemba hii hatawahi kujulikana daima kwa kuwa muda wote ilijifutika buibui lililoficha use wake.

Umbea

 • Hamida na wanawake wengine wa mtaani walikuwa wambea. Wamemkashifu na kumuumbua Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei. Wanamwita kwamba yeye ni mbwa koko na uovu wake umezidi wa shetani. Bi. Hamida baada ya mtoto wake Safia kumwendea kinyume hataweza kusema lolote.

Bidii katika Kazi

 • Kutia bidii katika shughuli yoyote zile huleta tija. Awali bidii masomo zilimpatia sifa nzuri Safia kwa sababu alikuwa wa kwanza hadi mwaka wa mwisho. Aidha bidii yake ya kazi za nyumbani, , staha yake na ucha Mungu ulitambuliwa na kila mtu.

Mikasa Maishani

 • Masudi na Bi. Hamida walikuwa na maisha ya utulivu.Wanandoa hawa wawili walikuwa wanaelewana. Upendo na ushirikiano wao hujidhihirisha kwa vile wanavyozungumzia mambo mazito ya nafsi zao. Baada ya kufurahia mwenendo wa binti yao — furaha inakatika ghafla. Wanajikuta katika hali ya kupatwa na janga — janga la kifo cha ghafla cha mwanao na soni mbele ya macho yao.

Tabia na Mienendo ya Vijana

 • Vijana mara nyingi huwa na mihemko ya kupapia mambo kabla ya wakati. Mkadi alikuwa na mwenendo usiofaa.Wanawake wambea akiwemo Bi. Hamida wakamsengenya.Safia naye katafuta njia ya kukidhi tamaa zake kwa njia mwafaka. Wazazi wake mwenyewe wakarahisisha mambo kwa kuwapa ruhusa ya kujifungia ndani. Sio rahisi kutambua mienendo ya vijana. Ni vyema kuviepuka vitendo viovu maana matokeo ya uovu hayafichiki. Bi. Hamida anaanza kutilia shaka unyonge wa Safia na kutapikatapika kwake. Shaka haikuwa uongo bali ukweli mtupu.

Hila na Ujanja

 • Safia alitumia maarifa na ulaghai kuwahadaa wazazi wake. Alijua fika namna atakavyowateka akili bila hata kumtilia shaka. Ujanja wake na hila ukamwezesha kufanya mapenzi ndani ya nyumba ya wazazi wake. Dalili za mimba zilipoanza kudhihirika akasingizia homa ya malaria sugu. Alidanganya kwamba alienda hospitalini. Anapoona mama anam shuku, anatumia ujanja mwingine kuzibia hila zake- Anafanya hila za kuitoa mimba na hatimaye anaonja pepo mwenyewe.

Imani ya dini

 • Dini ni dhana mwafaka ya kumwongoa mtu ili awe mnyofu. Hata hivyo dini inaweza kutumiwa visivyo. Safia alijifanya kwamba ni mshika dini mno — hadi wazazi wake hawakumshuku kwamba anaweza kuwaendea kinyume.
 • Daima alijifunika ushungi hata akiwa humo ndani mwao.Anatumia mwamvuli wa dini kujificha na kufanya uovu mtupu.


Mbinu

Methali

 • Kuzaa mwana si pato, pato ni kumvyeleza (Uk 29)
 • Lisemwapo lipo, kama halipo linakuja (Uk 30)
 • Siri ya kata iulize mtungi (Uk 30)
 • Kidole kimoja hakivunji chawa (uk 31)

Tashbihi

…bintiye aliye safi kama umande s

….hikamoo inayotoka nyuma ya buibui kama kata ya maji mtungini.

Mjadala wa nafsia/ uzungumzi nafsia

 • Bi. Hamida, baada ya kuona hali ya mwanae ya unyonge na kutapika.

Mdokezo

 • Kidugu kidogo cha Safia kilisimulia kisa shogaye kuwa na ndevu kwa kudokeza kidogo kidogo. Juzi... Juzi... Ivyo (Uk 34)

Taharuki

Baba Safia anapoelezwa juu ya kifo cha mwanae alishikwa na mshangao mkubwa. Hatujui vile alivyoathirika. Aidha hatujui vile mama yake Safia alivyochukulia jambo hilo.Wahusika

Safia

 • Huyu ni binti wa Bw. Masudi na Bi. Hamida.
 • Anasifika mno kwa tabia yake nzuri isiyokuwa na doa lolote
 • Katika masomo yake alikuwa anaongoza darasa.
 • Ana kipawa cha uzingativu wa kiwango chajuu.
 • Ni msaidizi mkuu wa mama yake Bi. Hamida.
 • Anamudu kazi zote za nyumbani.
 • Anazifanya bila manung'uniko yoyote.
 • Ni mwenye tamaa: anatamani kufanya mapenzi na akatumia hila kutimiza lengo lake. Alikuwa amejivika ngozi ya kondoo nje, ndani mbwa mwitu.
 • Ni mjanja: anatumia maarifa na hila za kila namna ili kupata fursa ya kufanya mapenzi.
 • Ni mwenye hasira: Bi. Hamida anapomdadisi kuhusu hali yake ya kutapika, anapandisha hasira na kukimblha chumbani mwake.
 • Ni mwongo: anadanganya kuwa ana malaria sugu-

Anadanganya kuwa Kimwana anakuja ili wajadiliane kumbe anayekuja ni mvulana mwenye ndevu na wanafanya rnapcnzi.

 • Ni muuaji: anatoa mimba na kukidhulumu kiumbe kisicbO na hatia. Mambo hayakwenda sawa na yeye akafariki.
 • Ana ubinafsi: anafikiria yeye tu bila kujua madhara ya kiurnbe kilichomo ndani tumboni mwake.
 • Ni mchangarnfu: yeye ana tabia ya uchangamfu ndiornaana ora mama aliyabaini mabadiliko Baraka.

Umuhimu

 • Ujanja na hila zina mwisho wake. Mara nyingi huwa na mwisho mbaya.

Bi. Hamida.

 • Mama yake Safia.
 • Ameolewa na ana watoto wawili, Safia na Lulua.
 • Anawapenda watoto wake na kuwapatia mahitaji yote.
 • Safia anasoma Shule ya msingi na wanampa fursa nzuri ya kujitayarisha ili aingie sekondari.
 • Ana upendo na msikivu kwa mumewe: huwa na masikilizano mema na mumewe Bw. Masudi.
 • Ni mchunguzi: aling'amua hali ya Safia mara tu alipoanza kubadilika na kumdadisi. Ingawa Safia tabia zake ni nzuri sana, alitia shaka na kumweleza mumewe.
 • Anamdadisi Lulua ili kutosheleza mashaka yake kwa Safia.
 • Anajua ukweli kwamba kupata mtoto na kumlea ni mambo mawili tofauti.
 • Mtimiza wajibu: anahakikisha kwamba Safia anapata mandhari mazuri yenye utulivu kwa ajili ya kudurusu.
 • Anampa Safia mwelekeo kuwa akiwa ndani ya nyumba si lazima ajifunike gubigubi.
 • Ni mbea: anamsengenya Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei, kuwa ana tabia mbaya. Anakiri kwamba anashiriki kwenye vikao vya kusengenyana akiwa na wanawake wenzake kila siku (Uk 30)

Umuhimu

Vijana wa kisasa wanatumia hila za kila aina kuwahadaa wazazi. Ni vyema wazazi wawe macho zaidi kufuatilia mienendo ya watoto.

Join our whatsapp group for latest updates

Download SHOGAKE DADA ANA NDEVU - Alifa Chokocho - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest