SHIBE INATUMALIZA - Salma Omar Hamad - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Ni kisa kinachohusisha Mzee Mambo ambaye ni waziri kivuli wa wizara zote. Yeye mwenyewe anakiri kwamba hana kazi yoyote.

Hivyo yeye ameamua kutumia fursa hiyo ili kujishibisha, "...Mimi nipo kuongeza idadi ya walaji karamuni " (Uk 37)

Jambo linalodhihirika wazi ni kwamba katika taifa Ia Mzee

Mambo, hakuna uwajibikaji. Fedha za umma hutumiwa kiholela.

Kinachotazamwa zaidi ni kuenda kazini na si kufanya kazi (Uk 37)

Mzee Mambo hupakua mshahara yaani hujitwalia yeye mwenyewe.

Yeye hapewi mshahara.

Baada ya kujipakulia mshahara, sasa kuna kusherehekea — kuna shangwe, hoihoi na nderemo. Mzee Mambo anapokuwa na sherehe kuna wimbo unaopigwa daima. Wimbo wenyewe una fumbo ndani yake:

" ...Mola ndiye atowae

akampa mahuluki

mali,

Humpa amtakae

huyo ndo humbariki.

Na kila amnyimae

kupata hatodiriki

Mpewa

hapokonyeki, aliyepewa kapewa

Hata ukifanya chuki, bure unajisumbua UK 37)

Wimbo huu unaonekana kukejeli wale wasio na vyeo. Wimbo huu unaonesha Mzee Mambo kashiba shibe kweli. Hii ni sherehe ya kusherehekea mtoto wake wa kwanza kuingia Shule ya chekechea

(nasari skuli).Yule wa mwisho ameota vijino viwili kutokana na

matukio hayo kuna sherehe kubwa.

Sherehe hiyo inarushwa moja meia kwenye televisheni ya Taifa. Aidha, inasambazwa kwenye mitandao Mingine yote ya mawasiliano.

Licha ya kupata uhondo wa kupakua mshahara, Mzee Mambo anaendelea kupewa tilt-sa ya kuhujumu mali ya taifa.

Katika sherehe ya Mzee Mambo, magari ya serikali yalipewa m: qukumu mengi; kuleta maji, mapambo, ikibidi kupeleka watoto

Wakati huu watu wanakula vyakula mbalimbali ingawa hakuna kupika. Kuna vyakula vya kubwakia, kutafuna n k. Aidha kuna vinywaji tele tele — vikali, vitamu n k. Vyakula vinavyoliwa hapo haxikutayarishwa. Basi kuna hatari kwamba vyakula hivyo sio

bora. Hata hivyo watu hawachunguzi.

Wakati wa mchana Sasa na Mbura walipata fursa ya kula vyakula.

hakula ambavyo wamevipata. Ingawaje wana haki ya kula vyakula hivyo vilikuwa vimenyakuliwa na watu wengine. Hivyo wanaviita yetu vyao!" yaani ni "vyetu lakini ni vyao " (Uk 40)

Wakati muafaka walioungoja Sasa na Mbura unafika na wao wakajiunga kwenye foleni na kula kupita kiasi. Wakati huu wote mitambo inaendelea kurusha matangazo. Baada ya wao kushiba wanaanza ushindani usio wa msingi. Wanalinganishana aina mbalimbali za mchele — kati ya mchele wa Mbeya na Basmati.

Kutokana na shibe kubwa sasa anakumbuka shairi ambalo hnabainisha kwamba wale walalao wataamka baada ya kupata matatizo mbalimbali. Wakati huu wote matukio yanarushwa hewani.

Kuna Wimbo wa kejeli ambao waporaji wa mali ya umma. Hawajali hata wakilaumiwa. Yeye anaomba kuishi kwa amani na watu.

Wimbo huu unadhihirisha kuwa wanyakuzi wa mali ya umma hawajali. Wananyakua mabilioni kwa kutumia mbinu na hila za kila namna. Misingi na mipangilio yenye kunufaisha taifa hutupiliwa

Wanafungua maduka ya dawa zilizonyakuliwa kutoka kwenye bohari za serikali.

Wanapata huduma zote muhimu bure ilhali wenye kipato kidogo mno huzipata kwa malipo. Huduma ambazo wanyakuzi huzipata bure ni pamoja na; maji, umeme na matibabu.

Shibe waliyokuwa nayo Sasa na Mbura ziliwapa usingizi mzito.

Wakagundua kwamba kula kunatumaliza (Uk 44)



Anwani

  • Anwani ya hadithi hii ni "Shibe Inatumaliza". Anwani hii imebeba maudhui yaliyomo barabara. Dhuluma, ufujaji wa mali za umma na ukandamizaji wa wanyonge ni matokeo ya shibe waliyonayo viongozi walioko madarakani. Mapuuza yote ya shida za wanyonge ni matokeo ya shibe ya watawala.

 



Dhamira

  • Mwandishi amedhamiria kubainisha namna viongozi serikali wanavyolewa madaraka na kufanya wanavyotaka. Mzee Mambo ni waziri asiye na wizara lakini anakwapUa mshahara mnono na anatumia mali za serikali kwa namna anavyotaka yeye.


Maudhui

Unyakuzi wa mali ya umma

  • Kuna unyakuzi unaofanywa na viongozi mbalimbali. Kwa mfano Mzee Mambo ana cheo ambacho hakina wadhifa wowote serikalini. Hata hivyo yeye anajichukulia ujira au rnshahara wa kiwango cha juu mno. Katika kuendesha shughuli zake zote za kibinafsi anatumia mali za serikali —magari, madereva, mafuta n k.
  • Fedha na mali za serikali zinatumiwa na wakubwa kwa shughuli duni zisizo na maana. Mzee Mambo anafanya sherehe kubwa mno kwa sababu kifungua mimba ameingia 'nasari skuli' na kitinda mimba ameota meno. Vyakula vingi vyote vilivyoandaliwa ni mali ya umma.

Ubadhirifu

  • Mali ya umma inatumiwa ovyo ovyo na hakuna anayejali. Magari ya serikali hubeba mapambo, maji na kadhalika.
  • Huingia na kutoka kumshughulikia mtu mmoja. Vyakula vinavyoliwa na vinywaji ni vingi mno.

Mapuuza

  • Makosa yote yanayotendwa na wakuu ya kuharibu mali yanapuuziwa — 'sijali lawama'. Hata watu waumie kwa kiasi gani wao hawajali. Viongozi wengine badala ya kuchukua hatua zifaazo dhidi ya wanyakuzi — wanangojea wakati muafaka ili nao wanyakue. Pindi wapatapo nafasi hutumia mwendo wa kasi kujinyakulia na kulimbikiza "NaSisi twende tusogee kule " jungu lile linateremshwa.(Uk39)
  • Vyombo vya habari vimemuangazia unyakuzi wa Mzee Mambo na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
  • Viongozi wananyakua mabilioni ya fedha lakini hawachukuliwi hatua yoyote. Haya ni mapuuza.

Ukandamizaji wa Wanyonge

Katika taifa la Mzee Mambo, wachochole hukandamizwa kwa njia nyingi.

  • Wao wana dhiki na ufukara.
  • Hulazimika kulipia huduma zote muhimu.
  • Wakubwa wanadai kuwa wanakula kwa niaba ya wanyonge.


Wahusika

Mzee Mambo

  • Ni waziri kivuli wa wizara zote. Aidha ni mkuu asiye na kazi maalum. Hivyo vyeo vyake viwili humtatiza yeye mwenyewe kwa kuwa hajui kazi yake hasa nini.
  • Licha ya kutokuwa na majukumu yoyote, Mzee Mambo anapata mshahara mkubwa sana wa bure (hakuufanyia kazi)Hufurahia hali yake hiyo ya kupiga ubwete.
  • Ni mbinafsi: hutumia vyombo vya umma kwa matumizi ya kibinafsi.
  • Ni mbadhirifu: tukio dogo la kifungua mimbakuanza 'nasari skuli' linamfanya aandae sherehe kubwa mno. Kulikuwa na;
  • Magari ya serikali hutumiwa ovyo ovyo — kubeba mapambo, kupeleka watoto kuogeshwa.
  • Mitambo ya runinga za serikali inarusha na kuonyesha sherehe hii moja kwa moja (Huu ni ubadhirifu maana sherehe hii haina umuhimu wa kuonyeshwa na kituo cha Televisheni ya Taifa.

Umuhimu

  • Mzee Mambo ni kielelezo Cha watu wanaopiga ubwete na kufuja mali ya umma kwa kulipwa mishahara.
  • Ni kielelezo cha watu wa tabaka la juu ambao hawana uzalendo hata kidogo — kuifilisi serikali na hajali.
  • Ni kielelezo cha viongozi wanaofuja mali ya vizazi vijavyo na kuwaacha bila chochote.

Sasa na Mbura

  • Hawa ni mawaziri wa wizara moja. Ni Wizara ya mipango na mipangilio.
  • Wanafanya kazi ngumu zaidi na wizara hii ndio muhimu zaidi
  • Wanafanya kazi ngumu zaidi na wizara hii ndio muhimu zaidi kuliko zote.
  • Wao hujituma ili kuhudumia taifa lao. Wanatengwa mbali na hawatambuliwi na taifa.
  • Ni walafi: wanapopata fursa ya kupata mali, wanaitumia
  • Wana mapuuza: ingawa wanafahamu uzembe uliopo na unyakuaji wa mali ya umma, hawachukui hatua mwafaka.

Umuhimu

  • Wametumiwa na mwandishi kudhihirisha jinsi wananchi wenyewe wanavyochangia katika kuzorotesha nchi — kwa kuachilia unyakuzi uendelee. Walioko madarakani wanakaa tayari kunyakua mara tu wapatapo fursa ya kufanya hivyo.


Mbinu za Lugha

Jazanda

  • Majina ya wahusika "Sasa na Mbura" yametumika kijazanda.Kusasambura ni kutoa nguo zote. Wahusika hawa wametumiwa kuonyesha vile ambavyo viongozi wanavyovua taifa Iao mali yote iliyokusanywa na vizazi vilivyopita. Aidha, wananyakua rasilimali hata za vizazi vijavyo. Mali za serikali kama dawa zinatolewa katika bohari na wanyakuzi wanafungua maduka ya dawa.

Aina mbili za mchele

  • Mchele wa basmati — unasimamia bidhaa duni zinazolundikwa katika nchi changa na mataifa mengine. Mawaziri wanaohusika hawaja chukua hatua yoyote.
  • Mchele wa Mbeya: Vitu asilia vya nchini ni bora na vina manufaa zaidi.

Nyimbo

  • Kuna nyimbo tatu zilizoangaziwa katika hadithi hii. Nyimbc hizi ni za dhihaka na kejeli.Wimbo wa kwanza unachezwa mara kwa mara MzeeMambo anapokuwa ana sherehe. Wimbo huu ni wa kufumba watu macho kuhusu chanzo cha mali ya Mzee Mambo inayotumika kiholela. Ujumbe wa nyimbo ni kwamba Mola ndiye anayempatia mja mali Yule anayemtaka. Na mtu akishapewa mali yake hawezi akanyang'anywa.
  • Ubeti wa shairi unasikika baada ya Sasa na Mbura kula na kuwa katika usingizi wa mang'amumang'amu " Ujumbe wa ubeti huu ni kwamba watu wakishalemewa na dhuluma za wakubwa itabidi waanze kudai haki zao "
  • Wimbo wa tatu nao umejaa kejeli vilevile. Unabainisha wazi —'majuju'- watu wa hadhi ya Mzee Mambo kwamba hawajali lawama zinazotolewa na watu kuhusu vitendo vyao. Wanahiari watu wote wakae salama bila kulaumiana, na watu wakijitenga na kutojihusisha nao ni kuwadhulumtl
Join our whatsapp group for latest updates

Download SHIBE INATUMALIZA - Salma Omar Hamad - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest