MAME BAKARI - Mohammed Khelef Ghassany - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Kitoto Cha Sara ambacho kilizaliwa kilifanya baba mtu aanze kumheshimu mwanae. Sara alipata mimba iliyotokana na kubakwa.

Baba yake akazidi kumpa bintiye heshima kama njia ya kumpa moyo na faraja iliyotokana na kisa hicho.

Kisa kinaanza kwa kuzingatia mashaka ya Sara msichana wa Shule ambaye alibakwa na lianaume fulani. Machozi yalimkurupuka yakamwagika njia mbilimbili. Alikuwa na majuto makuu ambayo yaliandamana na mishale iliyomchoma mwilini mwake. Kila alipokumbuka kisa hicho kilitonesha kidonda kwa upya ndani mwake.

Sara alibakwa Jumatano moja usiku alikuwa ametoka kwenye masomo ya ziada. Kisa hicho Cha kinyama kilinata akilini mwake, akawa anakumbuka kila kitu. Janadume lenye harufu kali ya kutuzi lilimvamia na kumbaka ghafla. Alijaribu kujipapatua lakini akazidiwa nguvu. Likambamiza ardhini na kumkandamiza. Sara alipoteza fahamu kwa nusu saa. Alipozindukana alifahamu wazi kuwa ameshapoteza uanawali wake.

Tukio hilo la kinyama, lilimsababishia Sara majonzi si haba.

Alijaribu kutatua shida yake. Akawaza na kuwazua. Hakumweleza baba yake maana alihofia hangesadiki tukio hilo na badala yake angemfukuza.

Sara alihofia vile ambavyo angeai bika, kutengwa najamii, ku fukuzwa

Shule na watu kusengenywa. Alifikiria jinsi ya kujiauni kwa aidha kujiua au kutoa mimba. Mambo hayo yote mawili hakuyaafiki.

Hawezi kujiua maana yeye hakuwa mkosaji, aliyekosa ni lile jitu.

Yeye Sara hakudhulumu, bali ni mdhulumiwa. Wazo la kutoa mimba

Pia hakuliafiki. Kwa sadfa siku mbili kabla ya kubakwa alikuwa amesoma shairi la 'Usiniuwe' Ia Abdullatif Abdalla, lihusulo utoaji

Wa mimba. Kitoto kichanga kilisema na mama yake tumboni. Sara

wazazi wa Sara mashaka yake kutokana na mapenzi yao wakaanza kumpa msaada. Baba mtu akaanza kumwita Sara mama. Wakagharamia matibabu yake yote. Wakampa faraja kuu wakati Sara alipopigwa na mshangao wa kuwakuta hospitalini " Hapajaharibika jambo mama'ngu " Mapenzi ya dhati kwa mtu aliyepatwa na janga kubwa kama hili ni tiba mjarabu.



Maudhui

Siri

  • Mtu anapopatwa na shida nzito huhitaji kuiweka siri hadi wakati mwafaka. Sarina alitunza Siri ya Sara kwamba ni mja mzito. Aidha walipomweleza Beluwa naye aliahidi kuiweka Siri. Daktari Beluwa aliweka siri lakini akawa ametafuta dawa bora zaidi —ya kuwaeleza wazazi wao.
  • Wazazi nao waliiweka siri hadi wakati mwafaka ulipotimia na hapakuwa na haja ya kuficha kitu chochote "hakuna haja ya siri hakuna haja ya hofu " Hili lilileta faraja kubwa kwa Sara hatimaye akajifungua salama salimini.

Uhalifu

  • Yule nduli ambaye ndiye baba mtoto wa Sara, alitenda tendo la kinyama kwa msichana. Msichana mnyonge na dhaifu, alijaribu kupigana nalo likamshinda nguvu. Hata hivyo uhalifu haulipi chochote. Alimdhulumu Sara na kutoroka akamwacha amezirai nusu uchi. Unyama huo unafikia mwisho wakati alipojaribu kubaka msichana mwingine.Aliadhibiwa vikali akautoa uhai wake. Wakati wa kipigo alitamani ahurumiwe lakini watu walimuua kabla polisi hawajafika.
  • Uhalifu una malipo yake. Watu walimwadhibu vikali hasa baada ya Sara kumwasa "ulidhani uhalifu wako ungedumu milele

Maudhui mengine

  • Kifo
  • Mabadiliko
  • Malezi
  • Elimu n k


Mbinu za Lugha

Taswira

  • Kuna taswira ya chemchemi ya majonzi ya Sara ilipomwaga mito Inaonyesha huzuni na majonzi makuu aliyokuwa nayo.
  • Kitumbo chake kilichokwishaanza kufura. Hii ni inaonyesha mabadiliko ambayo yalijilazimishia kwa Sara baada ya kubakwa.
  • Kuna taswira chafu ya janadume lililombamiza ardhini —kuonyesha ukatili wa tendo hilo.
  • Kuna taswira hisi — ya mkandamizo na mdidimizo hadi akapoteza fahamu.

Kuna aina nyinginezo nyingi za taswira katika hadithi hii.

Mjadala wa nafsi/ uzungumzi nafsia

  • Baada ya janga la kubakwa kumfikia Sara alikuwa na mjadala mrefu wa nafsi. Sara alijizungumzia mwenywe;

- Ili kutafuta ufumbuzi alipohakiki chanzo cha yeye kufikiwa na janga hilo.

- Athari za tukio hilo n k

mbinu inayoonyesna dhana mbili tofouti zinazopingana

Dhana moja na kinyume chake. Kwa mfano: yeye ni mkosewa si mkosa. Ni mdeni si mdaiwa. Ni mdhulumiwa si dhalimu (Uk 50)

Mbinu rejeshi / kisegere nyuma

  • Sara anarejelea Jumatano moja saa tatu na nusu akitoka stadi za ziada wakati alipobakwa. Aidha, anakumbuka daima sura mbaya ya nduli aliyembaka na yale yote aliyopitia.
  • Sara anakumbuka shairi la 'Usiniuwe' alilosoma shuleni na yeye akawa mtetezi sana
  • Sara na Sarina wanakumbushana vile ambavyo waliapa kusaidiana wawili Pindi wapatapo shida " Ahadi ya kale ni ile ile Sara"

Sadfa

  • Ilikuwa sadfa kwa Sara kuwa mtetezi wa shairi la usiniuwe na siku mbili baadaye anabakwa. Na yeye akawa katika njia panda ya kutoa mimba au la "Sitakuua mwanangu kamwe"
  • Wakati Sara alipobakwa ilisadifu kuwa uzazi wake ulikuwa sawa akashika mimba. Hii ni sadfa.

Balagha

  • Haya ni maswali yasiyohitaji majibu. Ni kauli za kuleta uzindushi. Udhaifu na unyonge si ndio maana ya uanauke? Si kwa sababu ya umbile langu ndio mwili wangu ukatumiwa kukidhi utashi wao (Uk 48)
  • Kwa nini hakutoa taarifa siku ile "Ati umebakwa? Nani akubake wewe?" (Uk 48)
  • Sara anajiasa mwenyewe aache kulia kwa kujiuliza "Matone mangapi ya machozi amekwishajirovya?" (Uk 50)

Mawazo mk gizana.

suluhisho mwafaka.

k 50)

kila wazo likatangaza suluhisho mwafaka (uk 50)

mangapi ya machozi amekwtsna

Mawazo mkururo yakipangizana kila wazo likatang suluhisho mwafaka (Uk 50)

Tashbihi

  • “….Wengi mno " na kumtenga kama mgonjwa wa ukoma (Uk

Jazanda

Mzigo kupata wachukuzi — tatizo likapata ufumbuzi.

Sitiari

Mwanamke ndiye shetani (Uk 48-50)

Taharuki

Kuna taharuki mwanzo wa kisa hiki. Msomaji haelewi nini Sara ana majonzi mpaka asome kisa zaidi "Je, lile ndul bakaji lilifumaniwa vipi na kulifululiza hadi karibu na Sara "



Wahusika

Sara

Msichana wa Shule ambaye alibakwa akiwa ametoka kwenye stadi za jioni. Msichana mwaminifu ambaye amejitunza vema. Kitendo hicho kinamsononesha mno, hasa ilipoto kwamba jibakaji hilo lilimpachika mimba.

Sara anapata uchungu usioneneka na akawa anajisaka ni kwa nini machungu ya namna hiyo yalimfika. Je, ni kutokana na jinsi yake au unyonge. Alijaribu kubaini chanzo cha masaibu yake hayo yote. Baada cha kilio na uchungu mwingi anatoa

Hayazoleki . Anamweleza mwendani wake Sarina naye akauchukua mzigo ule kama wake. Hatimaye akafanikiwa kujiepusha na mzigo huo akajifungua salama.

Sifa zake

  • Ni mwenye kupenda masomo: fikra kuwa angefukuzwa
  • Shule zilimtia moto na uchungu.
  • Ni msichana aliyejitunza: alilia sana kwa kuupoteza usafi wake wa kisichana.
  • Ni mwoga: aliogopa ukali wa baba yake baada ya kutendwa unyama na hakusema
  • Ana mapenzi ya dhati: yeye na Sarina wanapendana sana.
  • Ana busara: anaamua kuwa kujiua sio suluhisho mwafaka maana yeye siye aliyekosa.
  • Ana utu: hakutaka kuavya mimba kwa hivyo akakihifadhi kitoto.
  • Ni mwelewa wa jamii yake: alijua vile watu walivyo wanapenda kudodosa mambo ya wengine.

Umuhimu

Ametumiwa na mwandishi kudhihirisha uovu wa ubakaji na athari zake mbaya. Sara ni kielelezo cha vijana ambao hutumia busara zao katika kupambana na majanga ya maisha.

Sarina

  • Huyu ni mwendani wa Sara. Anapojulishwa mkasa wa Sara, anatia shaka kidogo halafu anampa kila aina za msaada.
  • Ni mwaminifu: alitimiza ahadi yao wawili ya kusaidiana.
  • Ni mwaminifu: alitimiza ahadi yao wawili ya kusal
  • Ni mcheshi: anamwonya Sara awe mwangalifu asibakwe tena.
  • Mkarimu: alikuwa tayari kumpeleka Sara hadi kwao shambani akajifungulie huko.
  • Mwenye hila na maarifa: anapanga mpango kuwa Sara avae jilbabu nyumbani na shuleni ili kuficha mimba.

Umuhimu Wake

Ni kielelezo cha marafiki wema ambao hukirimu wandani wao wakiwa katika shida.

Bakari

  • Huyu ni baba yake Sara.
  • Anaonyesha kuwa ni mtu mkali sana maana binti yake anashindwa na kumweleza tukio la kubakwa shuleni.
  • Baadae anabadilika na kuwa mpole akampatia matunzo mtoto wake.
  • Ni mcha Mungu: anafanya sherehe ya Maulidi baada ya mame Bakari kuzaliwa.
  • Ana mlahaka mwema na majirani: anawakaribisha watu wote wakiwemo majirani.
  • Ni mfariji: anamfariji mwanawe na kumpoza wakati alipoangua kilio katika chumba cha daktari.
  • Mwenye mapenzi ya dhati: baada ya kugundua kuwa Sara ana himila alimheshimu na kumwita mama.
  • Ni msiri: ingawaje walifahamishwa hali ya Sara mapema na mkewe, waliiweka siri na hawakuonyesha kama walifahamu chochote — hadi siku rasmi iliyopangwa.

Umuhimu

kutoa msaada kwa wanaodhulumiwa. Aidha, ni kielelezo

Cha wazazi ambao wako tayari kubadilisha msimamo mkali wa ulezi na kutoa msaada unapohitajika.

Janadume bakaji

  • Ni jitu lisilo na utu linalovizia wasichana usiku na kuwabaka.
  • Ni katili: anambamiza Sara ardhini hadi akazimia na kumwacha hivyo.
  • Lenye tamaa na uchu: baada ya kumbaka Sara aliendelea na tabia hiyo mbaya hadi akafumaniwa na kupigwa vibaya hadi akafa.

Umuhimu Wake

jadili

Join our whatsapp group for latest updates

Download MAME BAKARI - Mohammed Khelef Ghassany - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest