NDOTO YA MASHAKA - Ali Abdullah Ali - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Hadithi hii inaanza kwa kusimulia uzuri wa ua la waridi na umaarufu wake. Linapendeza na kunukia vizuri. Ni ua lenye haiba. Waridi linasimamia msichana ambaye Mashaka alimpenda mno. Ua lake la waridi lilikwanyuka kwanyu likachukuliwa na upepo. Hivyo ndio

Waridi wake alivyotoweka siku moja.

Mashaka alikuwa na makuzi ya mashaka kama jina lake. Alikuwa na mama mlezi Biti Kidebe, maana wazazi wake wote walifariki

Pindi alipozaliwa. Mashaka amekua katika ukata hadi kifo cha Biti

Kidete. Alikuwa wa kufanya vibarua vya kila aina. Yalikuwa makuzi ya tikiti maji au tango, ya kuponea umande (Uk 57)

Mashaka aliozwa Waridi kwa kufungishwa ndoa ya mkeka. Hii ndoa, hufungwa kwa kushtukiza, pale wazazi wa binti wanapomfuma binti yao yuko kwa mwanaume. Waridi na Mashaka walikuwa wakipiga gumzo humo chumbani mwa Mashaka. Mlango ukapigwa teke na

Mzee Rubeya, akaingia akifuatana na shehe. Wakafungishwa ndoa.

Mzee Rubeya kwa kuwa ni mkwasi, aliona aibu binti yake kuozwa na mtu hohehahe. Yeye na familia yake wakakimbilia Yemeni.

Hali ya Mashaka ya ukata ilizidi. Waliishi chumba kimoja na watu tisa! Yeye mkewe na watoto saba. Mandhari hayo yalikuwa duni.

Walikaa karibu na choo ambacho hufurika mvua inaponyesha.

Mabinti walibanana kwenye kitanda kidogo na wavulana walilowea kwa jirani. Mwenyewe Mashaka ni mlinzi wa ZWS — Zuia Wizi Security.

Maisha yao yalijaa dhiki " Dhiki ilikuwa ndiyo nguo na harufu yetu.

(uk 76)Siku moja alipofika kwake hakumkuta Waridi wala watoto.

Alipofikiri vizuri akaona wimbo aliopenda kumwimbia Waridi ulikuwa na ujumbe wa kumwaga " .Nashundwa kuvumilia mie bora nirudi kwetu " (uk 77) Baada ya hapo Mashaka alibakia akiota ndoto tu. Hali ya ya arnbao ulimsababishia adha kadhaa;

 • Kama sio ukata mke wakc angernheshirnu
 • Asingemtoroka
 • Angekuwa na fcdha kumfrahi%ha yeye na watoto
 • Watoto wangcmpenda yeye Pia
 • Na yeye angejipcnda.

Mashaka aliwaza na kuwazua akatathmini na kutafuta idadi ya

Mashaka Tandale alikoishi na kwingine duniani 'Kuna Tandale ngapi Kenya, kuna Tandale ngapi Uganda kuna akina Mashaka wangapi Afrika nzima (Uk 78)

Anashangaa kwa nini jamii za kimataifa hazitaki kuukemea mfumo huu. Mashaka alijituliza na kujiasa kuwa awe na subira. Hata hivyo hakusaidika.

Katika hali ya kimawazo na kuota baada ya karne moja, Waridi ua lake lilimrudia, akaufurahia uzuri wake na harufu. Kabla ya hapo kulikuwa na maandamano makubwa ya wanyonge. Wasakatonge waliandamana 'Tunataka tufe! Bora tufe! Walibeba mabango na kupiga kelele zilizofika kila mahali. Kelele zao zilipenya kama radi kwa watu wa matabaka ya juu.

Maandamano yalibadilisha kila kitu. Utabaka ukaisha. Maisha polepole yakawa bora. Mashaka akawa na Waridi mkewe. Alifajirika mno. Kwa ghafla kumbe hiyo ilikuwa ndoto, Mashaka akaamka akajikuta yu pale pale katika umaskini wake.Anwani

Anwani ya hadithi hii ni Ndoto ya Mashaka.

maana mhusika mkuu anaitwa Mashaka. Naye alipatwa na alifariki Mashaka alipomaliza chumba cha nane. Mashaka anaozwa binti wa tajiri Mzee Rubeya alipogundua kuwa wanapendana. Ndoa yenyewe ya mashaka. Shehe na Mzee Rubeya waliwafuata Waridi na Mashaka walipokuwa wanapiga gumzo — chumbani na kuwafungisha ndoa. Ndoa hii ilileta aibu kwa familia ya Rubeya na wakahamia Yemeni alikotoka. Mashaka alipata watoto saba. Ufukara ukazidi kipimo. Waliishi katika chumba kimoja kile kibovu. Shida ziliposhamiri mkewe alitoroka na watoto wake. Mara nyingi aliota ndoto ya kuwa Waridi ua lake limerudi, lakini ndoto ikiisha anajikuta yuko pweke kwa mashaka yake. Hivo kisa hiki kinasadifu kuitwa 'Ndoto ya Mashaka 'Maudhui

Mkosi maishani

 • Mashaka alikuwa na mkosi tangu alipozaliwa. Wazazi wote walifariki akiwa mchanga. Alipata mlezi ambaye alikuwa fukara. Mashaka aliishi kwa kufanya vibarua ili kumsaidia
 • Biti Kidebe mlezi wake. Alipomaliza tu chumba cha nane —mama mlezi akafariki. Mashaka anaoa binti mrembo lakini kutokana na ufukara anamkimbia yeye na watoto saba. Licha ya kupigana, mkosi wa ufakara ulimwandama.

Tabaka la chini

Mwandishi anaangazia suala la utabaka. Anadhlhirisha kuwa kuna watu wengi maskini. Ingawaje wanajaribu kupigana nao bado hawajawahi kujinasua. Mwandishi anatoa tathmini pana ya chanzo cha umaskini. Anaonyesha kuwa katika mtaa wake wamo maskini wengi. Na si humo tu, kuna sehemu nyingi nyinginezo. Watu wa tabaka la chini wanakaa sehemu zisizo na mpangalio maalum wa ujenzi. anawaa senemu zisizo na mpango

Chumba cha Mashaka kwa mfano kimepakana na chm cha jirani. Maji ya kuogea yanapita kanbu na chumba cha chao. Watu wanaoishi katika mandhari haya ni wenc

Mvua ikinyesha kundi Zima hili huwa mashakani Vlongozi hutangaza kuwa watu wa bondeni wahame lakini hawapewi mahala mbadala.

Watuwa tabaka la chini au wasakatonge hujitahidi kupigana na kujitoa humo lakini hawajafaulu. Pengine huandamana na kubeba mabango lakini hawafaulu na juhudi huishi patup x

Tabaka la chini hubaguliwa, Mzee Rubeya anahamia na kurudi Yemeni maana hakuweza kustahimili aibu ya binti yake kuolewa na mchochole.

Ukombozi

Wasakatonge wanaona kuwa, hali zao zinakatisha tamaa.

Wanapanga maandamano ili kujikomboa. Waliandamana huku wanapiga kelele "Tunataka tufe! Bora tufe! Walifikia kauli hii kwa sababu walichoka kusubiri. Waandamanaji wanazidisha kelele zao, hadi wakandamizaji waliotia nta maskioni wanalazimika kusikiliza na mambo kubadilika. Utabaka ulififia na hali mpya ikaanza. Hata hivyo kwa kuwa haya yote yalikuwa kwenye ndoto ya Mashaka ni dhahiri kwamba ukombozi halisi haujakita mizizi na kufaidisha wananchi.

Ujenzi wa jamii mpya

Mwandishi anaangazia kwamba kuna umuhimu wa kupunguza pengo la kitabaka ili kuleta usawa. Mazingira mapya yataleta matumaini kwa kina Mashaka. Hata hivyo hiyo itatokea tu wakati sauti za wachochole zitakapoweza kusikika.

Mjenzi mpya utafikiwa ikiwa wachochole watapiga moyo konde na wasilegeze juhudi zao "Katika maandamano yale walikuwa wamefura na kufuriana. Walizidi kuumuka kama vile hamira ya hasira iliyowaenea miilini (Uk 81)

Mjenzi mpya utafikiwa ikiwa Wachochole watapiga moyo konde na wasilegeze juhudi zao "Katika maandamano yale walikuwa wamefura na kufuriana

Walizidi kuumuka kama vile hamira ya hasira iliyowaenea miilini (Uk 81)

Muundo

 • Hadithi hii ina muundo usio sahili. Kuna sehemu zilizogawanywa kwa vinyota. Kila sehemu inabeba maelezo tofauti. Sehemu ya kwanza inaeleza juu ya Waridi binadamu na waridi ua wakati huo huo. Katika msuko wa maelezo hayo ameelezea sifa za waridi ua na Waridi binadamu yaani mkewe. Sehemu hiyo pia inakuwa kama muhtasari wa kisa kizima. Tuligandamana tukawa kitu kimoja mpaka pale dhoruba ilipotutenganisha (Uk 71).

Baada ya kitangulizi hicho msimulizi anaelezea kisa kilichokuwa kimetokea kabla ya sehemu hiyo ya kwanza, iliyotengwa kwa kinyota. Hapa anaeleza usuli wake na mikasa yote iliyomsibu. Sehemu inayofuatia kwa mtiririko mmoja, inaelezea juu ya ndoa yake ya mkeka.

Baada ya nyota (Uk 74) anaelezea maisha ya ndoa yao. Hadi sehemu inayoonyesha maisha ya ndoa. Usimulizi wa mkewe alivyomkimbia na mashaka yaliyompata unafuata.

Sehemu ya mwisho ina kitangulizi au anwani isemayo; 'Siku nyingi tena ' Sehemu hiyo inaonyesha ndoto na mawazo yake aliyokuwa nayo. Akajumuisha mashaka ya wachochole na mikakati yao ya kujikomboa ambayo mwandishi anafikiria kwamba huenda ikachukua miaka na mikaka.Wahusika

Mashaka

Kama lilivyo jina lake alikuwa na maisha ya mashaka. Ni yatima aliyelelewa na Biti Kidebe mwenye roho nzuri lakini mnyonge. Mama mlezi wake alimsomesha hadi darasa la nane. Alipata mkasa wa kumpoteza mlezi wake baada tu ya kumaliza Shule ya msingi.

Alikuwa na bidii: alifanya vibarua vya kila namna kumkimu

Biti Kidebe.

 • Ni maskini: alizaliwakatikaufukaranajuhudazakezakujitoa hazikufua dafu.
 • Ana mapenzi ya dhati: aliwapenda watoto na mke wake, wanapomkimbia anasononeka.
 • Mwota ndoto: mawazo yake na subira kuhusu kujinasua kutoka makucha ya ufukara yanamfanya daima aote ndoto.
 • Anapata faraja sana katika ndoto lakini anapata hangaiko la akili, akiamka na kukuta ni ndoto tu.
 • Ana nyota ya jaha: alibahatika kupendana na binti mkwasi na wakafungishwa ndoa. Hata hivyo familia hiyo haikuwa saidia wakaendelea kusalia katika ulitima.
 • Mwenye majuto: anajutia hali yake ya ufukara na kutamani angeweza kupata suluhisho Ia kudumu.
 • Mwenye tamaa: anatamani kupata fedha ili wanawe wafurahi wampende na yeye ajipende.

Umuhimu

Kwa kupitia kwa mhusika huyu, msimulizi anadhihirisha kuwa ni vigumu kumaliza duru ya uftkara. Mzazi akiwa fukara ni rahisi mtoto awe fukara vivyo hivyo.

Anadhihirisha kuwa mapenzi hayachagui, yanaweza kuota

Ukata una misingi mipana inayotokana na mfrmo wa kimataifa.

Waridi

 • Ni binti wa rnzee mkwasi Rubeya.
 • Ingawa anatoka katika familia ya kitajiri, anampenda yatima maskini Mashaka. Aliolewa na Mashaka wakapata Alitvtpcnda Maghaka na baba yao alipoona hivi ndoa.
 • Mstahmiilivu: alimvumilia Mashaka kwa muda rnrefu watoto saba, Mtantauka: alikata tamaa ya kuwa na maisha ya ahueni hiVY@) akaamua kutMdi kwao, Mtot: antetomka kwa mumcwe na watoto wote saba bila kuwasiliana naye tena.
 • Mbinafsi: anampoka mumewe watoto wote bila kujifikiria kwamba mumcwc angckuwa mpwcke kupita kiasi.
 • Msiri: hakudokezea mtu yeyote kule alikokimbilia.

 

Umuhimu

Ametumiwa na mwandishi kudhihirisha kuwa mapenzi ni kama majani, huota mahali popote pale.

Mzee Rubeya

 • Huyu ni mkwasi mwenye asili ya Yemeni. Alioa mwanamke wa Kimanyema na wakapata watoto. Ni baba yake Waridi.
 • Anamfungisha bintiye ndoa ya mkeka. Hii inatokea baada ya kufahamu kwamba bintiye anamtembelea Mashaka chumbani mwake.
 • Alimchukua Shehe Mwinyimvua Mansuri kakake Waridi naIdi rafiki wa Mansuri. Kitendo cha bintiye kuolewa na mkata kilileta mtafaruku katika familia. Kulichukuliwa kuwa ni fedheha kuu; Mzee Rubeya akaamua kurudi Yemeni.
 • Anathamini usafi wa wasichana katika ndoa ndio maana aliwafungisha ndoa kwa mkikimkiki.

Umuhimu

Ni kielelezo cha watu wa tabaka Ia juu ambao hawataki kuchangamana na tabaka la chini.Mbinu za Lugha

Kuna matumizi ya nyimbo

 • Wimbo wa kwanza ni wimbo wa kuhimiza watu wathamani na kula aina duni ya ndizi ambayo inaweza kufaa ikipata mpishi bora. Wimbo wa pili, umenakiliwa kutoka Redio Tanzania. Huu unatumiwa kuonyesha kuwa Waridi alipomwimbia mumewe Mashaka alikuwa anampa kidokezo kuwa anaondoka kurejea kwa wazazi wake.

Methali

 • Baada ya dhiki faraja (Uk 70)
 • Apewaye ndiye aongezwaye (Uk 75)
 • Kitanda usichokilalia huwajui kunguni wake (Uk 75)
 • Jungu kuu halikosi ukoko (Uk 72)
 • Siri ya mtungi iulize kata (Uk 75)
 • Ngoja ngoja huumiza matumbo (Uk 79)
 • Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha (Uk 79)
 • Kila chenye mwanzo kina mwisho (Uk 81)
 • Pangu pakavu (Uk 78)
 • Liwalo liwe (Uk 81)
 • lwe iwavyo (Uk 71 )

Tanakali za sauti

 • Kokoko iikoo (Uk 82
 • Kwa kwaa (Kwan. Uk 82)
 • Puu ngwaaa (Uk 73)
 • Pwaa (Uk 75)

Si ya sasa, si ya baadae (Uk 81)

Kinaya

Mzee Rubeya tajiri mtajika wa ukoo wa Mwinyi anamuo bintiye kwa kijana hohehahe.

Takriri

Miguuhiyo mie nitaingianayo kaburini! Eemiguu migt gani hii (Uk 72)

Jazanda

Kibuyu hakifichi mbegu (Uk 72). Mashaka anarejelea vi ambavyo siri hazifichiki.

Taswira

 • Kuna taswira oni — wanyonge wakiwa wamebeba maband yaliyoandikwa kwa wino uliokoleza (Uk 81)
 • Kifafa cha uzazi kilimpiga dafrau akaanguka chini — Pich ya mama Mashaka ya kufa ghafla.

 Tashhisi

 • Rangi ya urujuani ilichungulia katika nyufa (Uk 82)
 • Kitanda changu cha mayowe kikapiga ukelele (Uk 82)

Tashbihi

 • zimepotea bilashi kama moshi (Uk 81)
 • kufuriana kama unga uliomwagiwa hamira (Uk 81). .Rubaa ya watu wane ikajitoma chumbani kama askari wa Fanya Fujo Uone (Uk 73)

Sitiari

Dhiki ndiyo nguo na haruiil yetu.

Balagha

Hadi lini lakini hadi lini subira hiyo (Uk 79) Matshaka akifikiria ukata wake unavyochukua muda mreli*. Je kuna

Tandale ngapi Tanzania (Mashaka akiwaza juu ya idadi ya maskini ) Kuna akina Mashaka wangapi (Uk, 78). Balagha zingine ziko Uk wa 72, 75, 76, 78, 80

Ndoto

Baada ya Waridi kumkimbia Mashaka aliota ndoto, kwarnba wanyonge waliandamana wakadai haki zao kwa nguvu, Walisubiri lakini hawakufaulu. Wakaanza tena harakati zao. Wakati huu wakawa wana hasira zaidi na wakazidisha kelele. Pia wakabeba mabango yenye ujumbe mkali zaidi.

Mabadiliko yakaanza, na wanyonge wakapata maisha bora.

Mashaka naye alikuwa miongoni mwao walioishi katika mazingira mazuri... Nilijiona nimezaliwa upya katika kizazi kipya (Uk 82)

Join our whatsapp group for latest updates

Download NDOTO YA MASHAKA - Ali Abdullah Ali - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest