Kenya Certificate Of Secondary Education(KCSE 2013) Kiswahili Karatasi ya Tatu with Marking Scheme

Share via Whatsapp

SEHEMU A : FASIHI SIMULIZI

 1. Lazima
  1. Huku ukitoa mfano, eleza maana ya vitanza ndimi. (alama 2)
  2. Fafanua majukumu sita ya vitanza ndimi katika jamii. (alama 6) 
  3. Eleza mbinu sita unazoweza kutumia katika kukusanya na kuhifadhi habari kuhusu vitanza ndimi. (alama 12)

SEHEMU B: RIWAYA
Said A. Mohamed: Utengano
Jibu swali la 2 au la 3.

 1. Walifanya kazi, walimenyeka,
  Njaa , ndiyo ilikuwa misumeno
  Lakini walilala na njaa ...
  Iliyokeketa matumbo yao, ...”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Kwa kurejelea riwaya, onyesha jinsi wanyonge walivyomenyeka. (alama 12)
 2. Jadili uhusiano uliopo kati ya wahusika na maudhui kwa kurejelea wahusika wafuatao:
  1. Shoka (alama 10)
  2. Kazija (alama 10)

SEHEMU C: TAMTHILIA
T. Arege: Mstahiki Meya
Jibu swali la 4 au la 5.

 1. Jadili mchango wa Wanacheneo katika kuivunja jamii yao. (alama 20)
 2. “Ndiyo hivyo bwana. Elimu yetu hapa ni ya kawaida mno. Haina kubwa la kumfaa mtoto mwenye mzazi anayeona mbali.”
  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Bainisha tamathali ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili ukirejelea msemaji wa kauli hii(alama 2)
  3. uliyotaja katika (b) hapo juu. (alama 14)

SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7.

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
  Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,
  Kiwa ni riziki yangu, mapokeo, kuoa na kuona,
  Nashukuru kwa ugumba, wenye ndimi, wanipagazao nao,
  Haupandiki mgomba, wana nyemi, fisadi wa hadhi zao,
  Ni lipi lenye kukera, kwa Muumbi, marufuku kwenye misa,
  Ugumba na ukapera, sio dhambi, wala haujawa kosa,
  Bora tungeni vitabu, magazeti, mutangaze kwa rediyo,
  Na zaidi muhutubu, kwa umati, muwambe ambayo siyo,
  Hidhuru yote ni bure, sio kitu, kudhiki asodhikika,
  Kwa shangwe na njerejere kila mtu, mdomo utafumuka,
  (Mwalaa M. Nyanje)
  1. Eleza jambo ambalo mzungumzaji (nafsineni) katika shairi hili anasingiziwa. (alama 2)
  2. Eleza umuhimu wa viishio vya beti za shairi hili. (alama 2)
  3. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
  4. Eleza muundo wa shairi hili. (alama 5)
  5. Bainisha matumizi mawili ya tasfida katika shairi hili. (alama 2)
 2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
  1 Huno wakati mufti, vijana nawausia,
  Msije juta laiti, mkamba sikuwambia,
  Si hayati si mamati, vijana hino dunia,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  2 Japo aula kushufu, na machoni vyavutia,
  Dunia wana dhaifu, yaugua nisikia,
  Vijana nawasarifu, falau mkisikia,
  Ukiona vyang’aria, tahadhari vitakula.
  3 Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria,
  Msije andama baa, makaa kujipalia,
  Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  4 Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia,
  Wajimwaie uturi, na mapoda kumichia,
  Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  5 Wawapi leo madume, anasa walopapia?
  Wamepita ja umeme, leo yao sitoria,
  Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  6 Nambie faida gani, nambie ipi fidia?
  Upatayo hatimani, waja wakikufukia,
  Ila kufa kama nyani, kasoro yako mkia,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  7 Kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia,
  Ujifanye kama kwamba, u jiwe huna hisia,
  Wakwambe watalokwamba, kwa lolote vumilia,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  8 Vyatiririka tiriri, vina vyanikubalia,
  Alo bora mshairi, pa tamu humalizia,
  Nahitimisha shairi, dua ninawapigia,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  9. Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia,
  Wakingie wanarika, na anasa za dunia,
  Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia,
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  (Mwalaa M. Nyanje)
  1. Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 4)
   kiarudhi katika shairi hili. (alama 8)
   (alama 2)
  2. Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili. (alama 3)
  3. Bainisha toni ya shairi hili. (alama 3)

SEHEMU E: HADITHI FUPI
K Walibora na S. A. Mohamed: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine
sisi tulifuata mitindo.”

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Onyesha jinsi Wanatekede wanavyofuata mitindo na kuacha chungu kinatokota bila
 3. Fafanua kwa kutoa mifano, mbinu nne alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya
 4. Nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili inasema na pande mbili. Zieleze pande hizo.
  Kikaza” (Robert Oduori)
 1. ‘Wakaacha chungu kinatokota - bila kuivisha chakula’. Kwa hakika walijibu, “Ndio mtindo, na kuivisha chakula. (alama 16)


MARKING SCHEME

FASIHI SIMULIZI

 1.    
  1. Maana ya Vitanza Ndimi
   Vitanza ndimi ni virai/vishazi au sentensi zenye sauti zinazokaribiana au zinazofanana kimatamshi na ambazo hutatiza mtu kuzitamka. Aghalabu huundwa kwa vitate, vitawe, au hata kurudia maneno yale yale katika sentensi. Kwa mfano:
   1. Wali huliwa na mwana wa liwali. Asiyekuwa mwana wa liwali hali wali.
   2. Wali huliwa na wanawali, wasio wanawali hawali wali.
   3. Shirika la reli la Rwanda lililiathiri lile la reli la Kenya.
   4. Mzee aliyevaa koti lililofika gotini alianguka akaumia goti kisha koti lake lenye kufika magotini likachanika. (alama 2)
  2. Majukumu ya Vitanza ndimi
   1. Kumzoesha mtoto/mtu kuzitamka sauti au maneno vizuri.
   2. Ni nyenzo ya burudani. Vikao vya mashindano ya utamkaji hutumiwa kuwachangamsha wanajamii.
   3. Msingi wa kumsaidia mtoto kujua lugha kwa undani. Huundwa kwa vitate au vitawe, hivyo mtu hujifunza vipengele hivi vya lugha.
   4. Husaidia kuimarisha uwezo wa kimawasiliano wa anayehusika. Utamkaji wa vitanza ndimi kwa kasi humzoesha mzungumzaji kuweza kuwasilisha hoja bila kusitasita.
   5. Huendeleza utamaduni. Jinsi wanajamii wanavyoshirikishwa katika utamkaji ndivyo wanavyorithishwa utamaduni wao au desturi yenyewe ya kushiriki katika utamkaji.
   6. Hujenga stadi ya ukakamavu. Kadiri mtu anavyoshiriki katika utamkaji ndivyo anavyoimarisha ujasiri wake wa kuzungumza hadharani.
   7. Huibua ucheshi na kudumisha uhusiano mwema. Utani unaoibuliwa katika mashindano ya utamkaji ni msingi wa kujenga uhusiano.
   8. Hukuza ubunifu. Wanajamii huweza kubuni vitanza ndimi hapohapo, wakavitamka.
   9. Ni kitambulisho cha jamii. Kila jamii ina vitanza ndimi vyake vinavyohusu mazingira yake.
   10. Hukuza utangamano katika jamii. Vikao vya mashindano ya utamkaji huwaleta wanajamii pamoja hivyo kujihisi kuwa kundi moja.
   11. Kuonya/kushauri - baadhi hufumbata maonyo/ushauri. Kwa mfano, Mzaha mzaha huzaa usaha. (6 x 1 = 6)
    Kutaja ½ Mfano ½
  3.    
   1. Utazamaji wa kushiriki au kutoshiriki. Mtu anaweza kushiriki katika kikao cha utamkaji wa vitanza ndimi, hivyo kujua vinavyoendelezwa katika jamiihusi ka.
   2. Video. Mtu anaweza kupiga picha za video watu wakitamka/wakishindana katika. utamkaji wa vitanza ndimi ili kuja kuchanganua baadaye.
   3. Matumizi ya hojaji. Mtu anaweza kuandaa maswali katika hojaji ili kudadisi kwa mfano, kama vipo katika jamii fulani, wanaohusika katika vikao vya utamkaji na uundaji wake.
   4. Kurekodi kimaandishi (kuandika) ili kuvirithisha au hata kuvichanganua baadaye.
   5. Majadiliano ya vikundi lengwa, Mtafiti anaweza kuteua vikundi, kwa mfano, vijana, ili kuchunguza namna wanavyoviunda na kuvitamka, na athari ya vitanza ndimi hivi kwao.
   6. Mahojiano Mtafiti anaweza kuandaa mahojiano rasmi na kundi / sampuli lengwa ili kuchunguza kwa mfano, majukumu ya vitanza ndimi katika jamii husika
   7. Matumizi ya vinasa sauti na sidii ili kunasa utamkaji wenyewe na kuchanganua sifa zake.
   8. Kutumia kumbukumbu ya mtafiti mwenyewe. Utafiti ambaye in mmoja wapo wa wanajamii katika eneo analofanyia utafiti anaweza kurithisha yale anayokumbuka baada ya kuyashuhudia.
   9. Kusoma majarida na vitabu (maktabani) vyenye habari kuhusu vitanza ndimi. (6 x 2 = 12)

    Tanbihi

    Hoja zifafanuliwe ili kupata alama kamili.
    Utengano: Said A. Mohamed
 2.    
  1.    
   1. Ni shairi analolikumbuka (Inspekta) Fadhili katika diwani yake: Kilio cha
    Wanyonge.
    Au:
    Ni maneno ya Fadhili Katika diwani yake : Kilio cha Wanyonge.
   2. Yumo nyumbani (sebuleni)mwa Maksuudi.
   3. Alikuwa ameitwa na Maksuudi.
   4. Ameyaona mabadiliko (fanicha) katika sebule ya Maksuudi ndipo akakumbuka haya.
    (4 x 1 = 4)

    Tanbihi

    Dondoo limetolewa uk. 71 - 72
  2.    
   1. Kinaya - Wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii lakini wanalala njaa.
   2. Sitiari - Njaa kufananishwa moja kwa moja na msumeno.
   3. Taswira - Picha ya watu wakimenyeka/wakiteseka.
    Picha ya msumemo ukikeketa matumbo.
   4. Jazanda - Msumeno ni jazanda ya njaa inayowaumiza raia. (2 x 2 = 4)
  3.      
   1. Wakulima wanalima lakini mapato hawayapati Rejelea maneno ya
    Shoka (Uk. 113).
   2. Wanyonge kuandamwa na magonjwa (uk. 72).
   3. Wakulima wanapunjwa; wageni k.v Marekani ndio wanaodhibiti bei za mazao.
   4. Maimuna, Dora na wenzake danguroni kwa Mama Jeni - wanashiriki ukahaba lakini mapato yanamwendea Mama Jeni.
   5. Maimuna anatumiwa na Biti Sururu kama kivutio cha walevi. Biti Sururu anamtazama na kusema kimoyomoyo atawafaa (UK.95). Anawaambia walevi amepata kisura. Kazi kwa Biti Sururu inamfanya Maimuna kudhoofika kiafya.
   6. Wazazi k.v Mama Dora anamtelekeza kwa kumuuza kwa Mama Jeni.
    Dora anakuwa kahaba.
   7. Dhuluma katika ndoa - Tamima kutawishwa, kupigwa - Mwanasururuna kutalikiwa na Maksuudi.
   8. Dhuluma katika malezi - Maimuna kutawishwa, Maksuudi kukinyima kitoto chake na Tamima malezi ya mama na kusababisha kifo.
   9. Wanawake kubaguliwa katika elimu. Maimuna anasomeshewa nyumbani ilhali Mussa amesoma hadi chuo kikuu.
   10. Maimuna kutumiwa kama chombo cha kuzalisha pesa pale Rumbalola - mapato yanamwendea mwingine.
   11. Maksuudi kumpokonya Mwanasururu mali na kumfanya kuishia kuwa mwendawazimu.
   12. Wizi/unyakuzi wa mali ya umma. Maksuudi kunyakua shamba la Via - kina Haji wanaishia kuwa maskini wanaomtegemea.
   13. Maksuudi kuwatesa wanyonge, anauza sahihi yake; anamtaka mke wa Mzee Japu kulipa shillingi 200 kwa sahihi yake tu (Uk. 78).
   14. Mwanasururu anamtaka Kabi kutenda yasiyofaa na baadaye kusababisha kukatwa kwa mguu wake.
   15. Biti Kocho na Farashuu wanamtorosha Maimuna na kumwingiza kwenye mtandao wa ufasiki / ukahaba.
   16. Farashuu anamuumbua Maimuna mbele ya mchumba wake - Kabi. Anamwita mhuni na mchafu (uk.168)
   17. Raia wametekelezwa kwenye ujinga na umaskini. Maazimio ya baada-uhuru. kutofikiwa (uk. 72).
   18. Kazija anashirikiana kimapenzi na Mussa ambaye ana umri mbichi, kwa nia ya kumtenganisha Mussa na babake. Anaishia kumfanya kupigwa na baba yake.
    Anawatenganisha.
   19. Farashuu - kumenyeka kazini, mwanawe Mwanasururu kudhulumiwa, mazingira duni, n.k.
   20. Maksuudi - baada ya kifungo, kupoteza asilimia kubwa ya mali yake, kupoteza hadhi, kuumbuliwa na Maimuna pale Rumbalola, ukiwa unaomwandama baada ya kusambaratika kwa familia yake, kipigo na ugonjwa, Tamima kukataa kumsamehe, nk.
    (12 x 1 = 12)

    Tanbihi

    1. Mnyonge anaweza kufasiriwa kwa namna zufuatazo:
     1. Maskini
     2. Asiye na mamlaka kisiasa
     3. Anayehitaji msaada
     4. Mwenye umri mdogo kuliko mwingine
     5. Aliye katika hali fulani, kama vile ugonjwa
     6. Mwana kwa mzazi
     7. Wafanyakazi
    2. Kumenyeka kunaweza kumaanisha:
     1. kuteseka
     2. kudhulumiwa/kunyimwa haki
     3. kuaibika
     4. kutofikia maazimio
     5. kutengwa na familia
 3. Utangulizi
  Wahusika na maudhui huchangiana kujenga kazi ya sanaa. Wahusika huteuliwa kuendeleza maudhui. Matendo yao ni msingi wa maudhui. Nayo maudhui hujumuisha matukio au hali zinazowaathiri wahusika. Tabia za wahusika huathiriwa na hali au matukio yanayowazunguka.
  1. Shoka
   1. Anaendeleza maudhui ya ukoloni. Anapinga hali ya wafanyakazi kuzalisha mali bila kufaidika.
   2. Anaonyesha ukosefu wa uwajibikaji katika ndoa. Anamwachia Selume mzigo wa malezi.
   3. Anaendeleza uozo wa kijamii (usherati) kwa kuhusiana na Maimuna kimapenzi.
   4. Anaendeleza ukandamizaji wa wanawake. Anamwambia Selume hatamwacha talaka, anamwachia ulimwengu umtimbe.
   5. Anaonyesha matumizi mabaya ya vileo. Pesa zake zinaishia vilabuni.
   6. Anaendeleza maudhui ya ubinafsi. Anakula nje na kuja kugawana kidogo kilichoko na wanawe.
   7. Anaonyesha changamoto zinazohusishwa na ndoa. Ingawa anamtesa Selume, Selume bado anaishi naye kutokana na mapenzi ya Selume kwake.
   8. Ni ishara ya ubabedume Anatarajia mkewe amheshimu licha ya kwamba hamshughulikii. Selume analalamikia utumwa wa wanawake.
   9. Anaonyesha ajizi ya wanawake / ukosefu wa wanawake kung’amua hadhi yao.
    Selume anadai kuteseka lakini mumewe akikosa kurudi anakwenda kumtafuta.
   10. Anachimuza / Ni ishara ya shida zinazowakabili wafanyakazi. Wachukuzi na wakulima wanafanya kazi za sulubu na hali mazao yanawaendea wageni.
   11. Ndiye anayesababisha na kukuza ugomvi kati ya Maimuna na Kijakazi, hivyo kuonyesha jinsi wanawake wanavyong’ang’ania kuwategemea wanaume. (5 x 2 = 10)
  2. Kazija
   1. Ni kielelezo cha ukandamizaji wa jamii ya mwanamke. Anasema mamlaka, elimu na pesa zote ni kwa mwanamume.
   2. Anaendeleza upujufu wa kimaadili kwa kushirikiana na Mussa na babake kimapenzi.
   3. Anaonyesha wanawake kama vyombo vya kusambaratisha asasi ya familia.
    Anamtenganisha Maksuudi na Mussa. Anamteka maksundi kuzuru kwake hata kumwacha mkewe akiwa mja mzito.
   4. Anaendeleza dhamira ya kisasi. Anamkutanisha Mussa na babake ili kumlipizia kisasi Farashuu.
   5. Ndiye anayewafichulia raia unafiki wa Maksuudi hivyo kuendeleza maudhui ya mapinduzi.
   6. Anachangia katika mwamko wa kijamii. Anawafanya raia kutomchagua Maksuudi na Zanga.
   7. Anaendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi. Anahusiana na Maksuudi na Mussa ili afaidike kwa fedha zao.
   8. Anaendeleza maudhui ya unafiki. Anamwita Maksuudi Bwana ili aendelee kufaidika kwake.
   9. Ni kielelezo cha ujasiri. Kule kumkabili Maksuudi katika uwanja wa uhuru kunaonyesha ukakamavu wake.
   10. Kutatizwa kwake katika ploti kunaakisi kutojengeka (kutokamilika) kwa dhamira ya ukombozi wa mwanamke. Mwandishi anambainisha tu mara mbili katika hadithi na baadaye kumfifilisha.
   11. Anafichua (anaonyesha) mfumo wa ubabedume. Anamchukia mwanamume kwa kuwekwa mbele. Anachukia kujipamba ili kumfurahisha mwanamume.
   12. Anaonyesha usaliti wa viongozi k.v Zanga ambaye hatimizi ahadi alizowapa waliomchagua. (5 x 2 = 10)

    Tanbihi

    Si lazima mtahiniwa atangulize kwa kuonyesha uhusiano kati ya maudhui na wahusika. La muhimu ni kujadili maudhui, hali au dhamira zinazoendelezwa na wahusika aliopewa.
    Mstahiki Meya: T. Arege
 4.    
  1. Badala ya Wanacheneo kutafuta suluhisho kwa matatizo yao wanadai kwamba nchi ni maskini. Waridi anamwambia Siki kwamba nchi ni maskini ombaomba, ndivyo wanavyoambiwa na vyombo vya habari, wasomi na wanasiasa.
  2. Badala ya Meya kushughulikia matatizo ya Wanacheneo, anasema Cheneo ni kisiwa cha kupigiwa mfano. Anajifananisha na majirani dhaifu kiuchumi na kukosa kuiendeleza Cheneo zaidi.
  3. Meya anaupujua uongozi wa Cheneo kwa kuwaacha washauri wapotoshi kuuingilia.
   Anamhusisha Bili katika maamuzi muhimu kama vile utoaji wa kandarasi na hali Bili si mtaalamu katika masuala haya.
  4. Meya anaifilisi Cheneo kwa kuidhinisha malipo yasiyofaa kama vile nyongeza ya mshahara wa madiwani, na malipo kwa Bili kwa kutoa ushauri ambao kwa kweli unahusu wizi wa fimbo ya Meya.
  5. Viongozi wa kidini kama vile Mhubiri wanachangia katika kudhoofika kwa uongozi wa kisiasa kwa kutomshauri Meya vyema. Anamwombea Meya ili naye (Mhubiri) afaidike kwa sadaka anayoidhinisha Meya.
  6. Viongozi wanaufisidi uchumi kwa kutotekeleza malengo ya kimaendeleo. Meya anasema yeye anazingatia maazimio ya kimilenia ambayo kwa kweli hayashughulikii; watoto bado wanakufa kwa magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe.
  7. Viongozi wanawaachia wageni kuingilia masuala ya kiuchumi. Maamuzi muhimu kama vile kugawana kwa gharama ya matibabu yanatolewa na wageni na kuwafanya raia wateseke.
  8. Meya anaifanya jamii ya Cheneo kuwa tegemezi kwa misaada. Anahofia kwamba hali ya usafi ikizorota wafadhili hawatakuja.
  9. Viongozi wanaufifilisha uchumi kwa ubadhirifu wao. Meya anatumia pesa za ufadhili kununulia mvinyo kutoka ng’ambo badala ya kuanzishia miradi.
  10. Meya anapunguza kodi ya mapato ya Baraza kwa kuidhinisha kutolipa kodi kwa madiwani. Kupuuza malalamishi ya wafanyakazi kunasababisha kutokusanywa kwa pesa, hivyo kuliteteresha pato la Baraza.
  11. Wafanyakazi kama vile Waridi wanajiuzulu wanapoona hali ni mbaya badala ya kukabiliana nayo.
  12. Viongozi wanashindwa kuwahakikishia raia usalama wa chakula. Mama anamlisha mwanawe wali na maharagwe yaliyolala na kusababisha kifo. Anasema wanakula chakula cha mbwa.
  13. Wanataaluma wanajiepusha na siasa, hivyo kutochangia kuiboresha siasa (mfano Siki).
  14. Kumpa Meya mamlaka makubwa kunachangia kupalilia udikteta badala ya demokrasia.
  15. Kutoshughulikia afya ya kijamii kunasababisha magonjwa kama vile utapiamlo yanayotokana na ukosefu wa lishe.Waridi anashangaa vipi mama anawaletea mtoto mwenye ugonjwa wa utapiamlo; kwake hili ni jambo dogo.
  16. Badala ya raia kuimarisha viwango vya elimu na huduma za afya, wanawapeleka jamaa zao ng’ambo kwa huduma hizi. Meya analalamikia elimu duni, anampeleka mwanawe kusomea ng’ambo. Anampeleka mkewe kuzalia ng’ambo. Kwa njia hii anaujenga uchumi wa nchi husika na kuuibia ule wa Cheneo.
  17. Meya analiibia baraza na kuufisidi uchumi wake kupitia kwa kandarasi. Pia anaidhinisha wizi wa fimbo ya Meya/ardhi.
  18. Askari wanazorotesha amani na usalama wa raia. Wanawahangaisha raia kwa bunduki na vitoa machozi.
  19. Viongozi wanasababisha kuzorota kwa hali ya usafi Cheneo kwa kutoshughulikia malalamishi ya wafanyakazi. Hili linailetea Cheneo aibu na kuiumbua machoni mwa jamii ya kimataifa. Wageni wanaahirisha ziara yao. Mji umejaa uvundo unaohisika hata nyumbani mwa Meya.
  20. Watu wanawachagua viongozi licha ya kujua kuwa viongozi hao wamekosa uwajibikaji, hivyo kuzizorotesha siasa za nchi/kuuzorotesha uongozi wa kisiasa.
  21. Meya anauangamiza uongozi wake mwenyewe kwa kupuuza ushauri wa Diwani wa III na Siki.
  22. Mapuuza ya Meya yanapalilia ukosefu wa utulivu kupitia kwa migomo ya wafanyakazi.
  23. Meya analifilisha Baraza kwa kulipagaza deni. Bili anamshawishi amwambie mwanakandarasi alishtaki Baraza alipwe fidia, naye Meya apate fungu lake.
  24. Meya na madiwani wanazorotesha uongozi kwa kutumia mbinu hasi za utawala kama vile propaganda, badala ya kuyashughulikia matatizo.
 5.    
  1. Haya ni maneno ya Meya.
   1. Anamwambia Bili.
   2. Wamo afisini mwa Meya.
   3. Meya anaelezea sababu za kuwapeleka wanawe ng’ambo kusomea huko. (4 x 1 = 4)

    Tanbihi

    Dondoo limetolewa uk.25. Nakala nyingine zinaweza kutofautiana ki-ukurasa.
  2. Kinaya, Meya anaikosoa elimu ambayo anastahili kuiboresha. (alama 2)
   au
   Kejeli/dhihaka/ stihizai. Meya kuidunisha elimu. Meya anajidhalilisha kwa kudunisha elimu ambayo anastahili kuiboresha mwenyewe. (alama 2)
   1. Kinaya
   2. Kauli ya Meya inadokeza kuwa yeye ni mzazi mwenye busara (kuona mbali) na hali anahiari kutumia pesa nyingi kuwasomeshea wanawe ng’ambo badala ya kuboresha elimu humu.;
   3. Meya anawadanganya raia kwamba dawa zimeagizwa ilhali sivyo, hatutarajii haya kutoka kwa kiongozi.
   4. Meya anadai Cheneo ni kisiwani cha hazina na hali watu wanakufa (yule mtoto) kwa kukosa huduma za afya.
   5. Badala ya Meya na madiwani kuendeleza mpango wa kimaendeleo wa mji, Meya anadai kwamba wanathamini malengo ya kimilenia na hali kwa kweli hata haya hayashughulikiwi.
   6. Meya anamruhusu Bili kuiba fimbo ya Meya ambayo kwa kweli ndiyo kitambulisho cha umeya.
   7. Meya anampeleka mkewe kujifungulia ng’ambo badala ya kuimarisha huduma za kiafya Cheneo.
   8. Meya anataka mwanawe apate uraia ng’ambo na hali yeye ni kiongozi anayetarajiwa kupalilia uzalendo.
   9. Meya anabadhiri mali ya umma kupitia ‘entertainment vote’, huku akidai kuwa ni matunda ya jasho lake. Haya hayatarajiwi kwa kiongozi.
   10. Meya anaidhinisha kuongeza mishahara ya madiwani ilhali Baraza lina nakisi ya fedha.
   11. Meya kulalamikia udogo wa mayai na hali watu hawana chakula.
   12. Meya analipagaza baraza deni badala ya kulisaidia kutumia fedha vyema.
   13. Meya analalamikia kupunjwa kwa kuletewa viyai vidogo na hali yeye anawapa wafanyakazi mishahara duni.
   14. Watu wanamchagua Meya wakitarajia kuimarika kwa hali zao za maisha.
    Meya anaishia kuwatelekeza katika njaa na magonjwa .
   15. Meya anaidhinisha pendekezo la Diwani II la kuundwa kwa kamati za kuhudumu na hali anafahamu kwamba baraza halimudu gharama hii.
   16. Ni kinaya kutarajia mama muuza ndizi kulipa kodi na hali Meya anawaruhusu walionacho kama vile madiwani na kutolipa.
   17. Meya, badala ya kudhibiti matumizi mabaya ya mali ya umma, anajigawia vipande vinane vya ardhi na kumgawia Bili pia.
   18. Ni kinaya kwa Meya kutomshughulisha Diwani III katika maamuzi yanayohusu matumizi ya fedha na hali ndiye mtaalamu katika masuala haya.
   19. Ni kinaya kwa Meya kumruhusu Diwani I ambaye anastahili kulihakikishia Baraza usalama kufanikisha wizi wa fimbo ya Meya.
   20. Meya anaidhinisha Baraza kutoa sadaka ya shilingi laki moja kila mwezi na hali anajua lina nakisi ya fedha.
   21. Badala ya Meya kushughulikia matatizo ya raia, anaeneza propaganda kupitia Diwani I kuhusu kujitolea kwa Baraza kutetea demokrasia.
    (7 x 2= 14)

    Au

    Mtahiniwa anaweza kuibua hoja zifuatazo kuhusiana na kejeli.
    Kejeli
    1. Anwani ya tamthilia inafumbata kejeli kwa kumwita Meya mstahiki na hali hata anaidhinisha wizi wa fimbo yake.
    2. Meya anajidhalilisha kwa kulalamikia mambo madogomadogo kama vile mayai.
    3. Uongozi wa Meya unadhihakiwa kwa kushindwa hata kuiendesha zahanati. Zahanati haina hata dawa za kimsingi.
    4. Meya anaikejeli elimu ya humu nchini kwa kusema ni duni mno; kwa njia hii anajidhalilisha pia kwani yeye anastahili kuchangia kuiboresha .
    5. Meya anajidhalilisha mwenyewe kwa kumwachia Bili kuliendesha Baraza na hali Bili si mtaalamu katika masuala ya uongozi.
    6. Meya anaudunisha uongozi wake kwa kuidhinisha nyongeza ya mishahara ya madiwani huku akifahamu kwamba hazina ya Baraza haimudu kugharamia nyongeza hii.
    7. Mwandishi anamkejeli Meya kwa kumfanya kushindwa kung’amua udanganyifu wa Bili.
    8. Mwandishi anamkejeli Meya kwa kumfanya kutumia pesa za msaada kuagizia mvinyo kutoka ng’ambo na kuishia kurudisha pesa hizo hizo huko ng’ambo.
    9. Meya anadai kwamba kungekuwa na Phd ya uongozi angekuwa nayo na hali anaendeleza mbinu hasi za uongozi kama vile propaganda.
    10. Meya anasawiriwa kama mwenye mawazo finyu, anayeshindwa kuona umuhimu wa mpango wa kimaendeleo wa Cheneo.
    11. Meya anadhihaki uongozi wake kwa kuidhinisha malipo kwa kazi ambayo haijatekelezwa. Anaidhinisha kulipwa kwa Bili.
    12. Meya anajidhalilisha kwa kulipagaza Baraza deni. Anakubali mshawasha wa Bili kwamba amwambie mwanakandarasi alishtaki Baraza n.k.
    13. Meya amajidhalilisha kwa kudai kuwa ni mzazi mwenye kuona mbali na hali hata anashidwa kung’amua umuhimu wa usafi. Pia anahadaiwa na Bili kwa urahisi. (7 x 2= 14)

     Tanbihi

     1. Hoja zinazohusu kinaya zinaweza pia kujadiliwa kama kejeli au stihizai, mradi mtahiniwa amezifafanua zikaeleweka kuwa ni Kejeli.
     2. Mifano yote, ihusiane na Meya hata kama inawarejelea wahusika wengine.
     3. Baadhi ya watahiniwa, ambao si makini, huenda wakachukulia kuwa tamathali ya usemi iliyotumiwa ni nahau au msemo (anayeona mbali). Hawa washughulikiwe kulingana na jinsi wanvyojieleza na kutoa mifano. Hata hivyo, mifano ya semi wanayotoa lazima, ihusiane moja kwa moja na Meya.

      Ushairi
 6.    
  1. Mzungumzaji (nafsineni) asingiziwa ugumba hasa kwa kutoshiriki mapenzi nje ya ndoa. (1 x 2 = 2 )
  2. Mambo ambayo anapinga ni:
   1. Kuiga rika; hususa kushiriki ulevi pamoja na kufukuza wasichana
   2. Mzungumzaji kupakwa tope (kuaibishwa) kwa kuwa yeye ni gumba
   3. Wamsemao kudai kuwa anatamani kuwa kama wao
   4. Eti kuwa ugumba na ukapera ni kosa
   5. Kuharibu maisha kwa ujana
   6. Kusingiziwa atapenda (atatamani) hali za wamsemao
   7. Watu kueneza uvumi kuwa yeye ni gumba (5 x 1 = 5 )
  3. Umuhimu wa viishio
   1. Viishio hivi ni vifupi na hivyo vinatoa ujumbe kwa namna iliyo madhubuti
   2. Viishio hivi vinaunga ujumbe wa kila ubeti/vinasisitiza ujumbe; wa shairi
   3. Viishio vinachimuza/kuonyesha/kubainisha dhamira au mwelekeo wa mshairi kuhusu hali ya vijana kujiingiza katika mahusiano yasiyofaa.
    (1 x 2 = 2)
  4. Mtindo ufuatao unaweza kukubalika:
   Ni jambo gani ambalo linamkasirisha Mungu ambalo halikubaliki kanisani?
   Je, ni mtu kuwa kahaba na mwenye vioja ama mtu aliyezaliwa akiwa tasa? Kuwa gumba au kapera si kosa na wala haliwezi kuwa kosa. Kwa kweli mimi sina makosa. (4 x 1= 4)
  5.    
   1. Kila ubeti una mistari minne.
   2. Mistari mitatu ya kwanza ina viapande vitatu ilhali wa nne una kipande kimoja.
   3. Vina katika kila kipande vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
   4. Kiishio kimefupishwa.
   5. Kila mstari una mizani 20 isipokuwa kiishio chenye mizani 8.
   6. Shairi lina beti 5. (4 x 1 = 4)
  6.    
   1. Mbio za wasichana - uasherati/uzinzi/uzinifu
   2. Haupandiki mgomba - hana uwezo wa kujamiiana. (2 x 1 = 2)
 7.    
  1.    
   1. Shairi hili ni wasia kwa vijana; unaowaonya dhidi ya kushiriki mapenzi.
   2. Linashauri kuwa wanaovutia machoni wanaugua na hivyo wanaweza kuwaambukiza maradhi yasiyotibika.
   3. Zinaa hii haichagui wala kupendelea yeyote. Hata wenye nguvu au warembo wamesalimu amri (ubeti 4).
   4. Vijana wajikaze kuhakiksiha kuwa hawaingii kwenye mtego wa kushiriki mapenzi.
   5. Wapo watakaowasema wenye kujitunza lakini hilo lisiwafanye kutetereka. (4 x 1= 4)
  2.    
   1. Tabdila - Kubadili miendelezo ya maneno pasi na kubadili idadi ya mizani. Neno ‘nisikia’ lingekuwa ‘nisikie’.
    Limetumiwa hivi ili kukidhi mahitaji ya vina.
   2. Inkisari - kufupisha maneno. Inkisari imetumiwa kuleta ulinganifu wa mizani.
    Maneno yaliyofupishwa nikama vile:
    1. ‘Sikuwambia’ badala ya ‘Sikuwaambia’
    2. ‘Jepusheni’ badala ya ‘Jiepusheni”
    3. ‘ngawa’ badala ya ‘ingawa’
    4. ‘waone’ badala ya ‘uwaone’
    5. ‘mkamba’ badala ya ‘mkaamba’
    6. ‘ngia’ badala ya ‘ingia’
    7. ‘walopapia’ badala ya ‘waliopapia’
    8. ‘watalokwamba’ badala ya ‘watakalokwamba’
   3. Miundo ngeu ya kisintaksia / kuboronga sarufi. Mpangilio wa maneno katika tungo haufuati utaratibu wa kisarufi wa lugha ya Kiswahili. Baadhi ya matumizi ya mbinu hii ni:
    1. ‘yaugua nisikia’ badala ya ‘nisikie yaugua’
    2. ‘si mlango nyumba nzuri’ badala ya ‘nyumba nzuri si mlango’
    3. ‘makaa kujipalia’ badala ya ‘kujipalia makaa’
     ‘madhara kukadiria’ badala ya ‘kukadiria madhara’
     ‘mapoda kumichia’ badala ya ‘kumichia mapoda’
   4. Mazida - ‘vyang’aria’ badala ya ‘vyang’ara’
   5. Utohozi - Sitoria - history
    Mazida na utohozi zimetumiwa kuleta urari wa vina
    Mbinu (4 x 2 = 8)
    Kutaja - alama 1
    Kufafanua, au mfano - alama 1
  3. Pande mbili ambazo mshairi anasema nazo ni:
   1. Vijana (ubeti 1 - 8)
   2. Mungu (ubeti 9) (2 x 1 = 2)
  4. Umuhimu wa maswali ya balagha.
   1. Maswali ya balagha ambayo yanalenga msomaji wa kazi ya fasihi hunuiwa kumfanya kulitafakari jambo hivyo kujifunza kwalo.
   2. Humfanya msonaji kulidadisi jambo linaloibuliwa. Katika ubeti wa sita msomaji atavuta fikra kuhusu ‘faida’ ya kuingia kwenye anasa ya kumuua.
    Kwa kulidadisi hili ataona kuwa hamna faida na hivyo kujirudi.
   3. Hutumiwa kusuta watu au kukashifu jambo. Ubeti wa 5 unawakashifu waliopapia anasa na kuwatahadharisha wasomaji kwa kuonyesha kuwa hatima ya anasa ni kifo.
   4. Hutumiwa kusisitiza wazo au kumfanya msomaji kushawishika na mtazamo wa msanii. Kwa mfano, katika ubeti wa 6, mshairi anamshawishi msomaji kwamba hakuna faida ya kuingilia anasa.
   5. Hutumiwa kuzindua. Ubeti wa 5 unamzindua msomayi kuona kuwa hata wenye nguvu huangamizwa na zinaa (3 x 1 = 3)
  5. Toni ya huzuni/ kusikitika
   1. Anasikitikia madhara yatakayowapata wanaoingilia, zinaa kwa kauli kama vile ‘wawapi leo madume, anasa walopapia’?(ubeti 5)
    Au
   2. Toni ya kunasihi au kushawishi. Anawasihi vijana kuepuka zinaa. Kwa mfano anawaambia, “kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia”. (ubeti 7)
   3. Kukejeli/kudharau/stihizai/bezo.
   4. Uchungu - anaonea uchungu tabia ya vyana.
    Kutaja - alama 1
    Kueleza na kutoa mfano - alama 2 (1 x 3 = 3)
 8.    
  1.      
   1. Mandhari ni nyumbani mwa Mzee Babu.
   2. Wanatekede wamekusanyika kwa Mzee Babu kujadili kuhusu mabadiliko ya hali ya anga.
   3. Bi Cherehani na Bwana Pima ambao ndio washona kikaza wamo kikaoni.
   4. Bwana Machupa amemwomba mzee Babu kuwafafanulia kitendawili cha hali hii ya anga
   5. Mzee Babu anawaambia wanakijiji wawaulize washona kikaza. (Cherehani na Pima)
   6. Wanapoulizwa hawatoi jibu la kuridhisha, wanasema ndio mtindo na walifuata mtindo. (4 x 1= 4)

    Tanbihi

    Dondoo limetolewa uk. 42
  2. Maneno kiini katika swali hili ni wanavyofuata mitindo na kuacha chungu kinatokota bila kuivisha
   Watahiniwa wanaweza kulifasiri swali kwa namna zifuatazo:
   1. Watu/viongozi kutoshughulikia hali inayowakabili
   2. Viongozi kufuata mitindo ya uongozi ya viongozi watangulizi badala ya kuiboresha
   3. Watu kufumbia macho makosa ya viongozi
   4. Viongozi kusaliti nafasi yao kwa kuendeleza uovu na uharibifu badala ya kuukosoa, nk.
   5. Viongozi na raia kuendeleza vitendo na hali hasi kama vile tamaa na ubinafsi
   6. Raia kuwawekea vikwazo viongozi na kungojea waporomoke.

    Hoja zifuatazo zinaweza kujitokeza.
    1. Kobe anachangiwa manyoya na ndege kupaa angani lakini wanapofika anakula wanavyopewa bila kuwagawia waliomkweza ila waliobahatika kupata makombo.
    2. Mtajika anahujumu demokrasia kwa kupata kura kwa njia ya udanganyifu.
    3. Mtajika hafanyi lolote kutatua shida za wanakijiji. Tunaambiwa mambo yakiwa mabaya hasemi lolote kwani ameshapata aliyotaka.
    4. Viongozi wanawasaliti washona kikaza (wapiga kura) kwa kuwadharau, kuwapuuza na kutowathamini licha ya kwamba ndio waliowachagua.
    5. Wanakijiji (raia) wanajua Mtajika amevunja masharti ya kikaza (uongozi) lakini hawamkosoi, wananyamaza, wanayafungia macho makosa ya viongozi.
    6. Mtajika anamruhusu mkewe kukishika kikaza (kuingilia uongozi) kinyume na kaida za jamii.
    7. Bi Mtajika anavunja kanuni za uhusiano mwema hata katika sherehe. Hata anatamka kuwa hakuna kiongozi mwingine kushinda yeye.
    8. Viongozi wanayaharibu mazingira badala ya kuyahifadhi. Tunaambiwa jibu la kitendawili cha mawingu bila maji limo katika kikaza.
    9. Machupa ambaye ni msemaji wa wanakijiji si wa kutegemewa. Anafaidika kwa Mtajika. Tunaambiwa kwamba yeye huenda na (huunga) upande unaomfaidi.
     Tunaambiwa alijua namna ya kuishi.
    10. Viongozi wamewatelekeza raia kwenye njaa na magonjwa (uk 47).
    11. Mtajika amewaaibisha wanakijiji kwa kutokilinda kikaza (uongozi).
     Bi Chirenga anasema kikaza kimepasuka.
    12. Mtajika na wenzake wanaipora mali ya umma; wanaifukarisha jamii kwa ubinafsi wao. Tunaambiwa kama ni nguruwe walijua kuchagua (uk 47).
    13. Raia kutokuwa na uwajibikaji wa pamoja japo wote ni washiriki katika ushonaji wa kikaza (uteuzi wa viongozi). Wanawatarajia Bi Cherehani na Bwana Pima
     kuelezea kitendawili cha kutonyesha kwa mvua (uk 42).
    14. Raia kutowajibikia vitendo vyao. Wanashiriki katika ushonaji wa kikaza (uteuzi wa viongozi) bila kuwazia uzito wa tendo hili. Wanachagua viongozi ambao wanawaathiri wenyewe (uk 43- 44).
    15. Viongozi wanakwezwa uongozini na raia kisha wanawatelekeza pindi tu wanapofika kileleni (istiara ya kobe - na ndege (uk. 44).
     Vikaragosi wanashirikiana na viongozi kuwadhulumu wanyonge. Kobe na vibarakala wake wananyakua kila kitu na kuwaachia wachache waliobahatika masalio (uk.44).
    16. Raia wanashiriki katika uharibifu wa mazingira na kusababisha kutotegemewa kwa hali ya anga. Mvua, ama inanyesha nyingi kupindukia, au hainyeshi kabisa (uk. 40). Machupa anawaambia wanakijiji kuwa jibu la kitendawili cha wawingu bila maji ni kikaza na raia ndio wenye kupima na kushona kikaza (uk. 46).
    17. Viongozi kuendeleza uongo na udanganyifu. Mtajika angeubadilisha ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli (uk 44).
    18. Badala ya viongozi kushughulikia uhalisia wa mambo, wanaishi katika ulimwengu wa ndoto. Hata nchi inapokumbwa na changamoto, Bwana Mtajika anaota tu badala ya kukabiliana na changamoto zenyewe (uk. 44). Hata raia wanapoutaka ushauri wake, hasemi lolote; ashapata aliyopangia kupata (uk 44).
    19. Raia wanaogopa, hivyo wanayafumbia kinywa matendo hasi ya viongozi.
     Tunaambiwa ni wachache wanaoweza kusema ukweli, hasa unaohusu viongozi (uk. 45). Bwana Mtajika anavunja kaida za kikaza (Kaida za uongozi) na hawamkosoi.
    20. Unafiki wa baadhi ya raia unaifanya Tekede kudorora kimaendeleo. Tunaambiwa kuwa Machupa hula kuwili. Anasikiliza wasemayo wanakijiji kumpelekea Mtajika na hapohapo anawaonyesha wanakijiji kuwa tatizo limo kwenye uongozi. Yeye anajitoa lawamani badala ya kushirikiana na raia kutatua tatizo la uharibifu wa mazingira (uk. 46).
    21. Viongozi wanawatelekeza raia waliowachagua katika njaa, umaskini na ugonjwa. (uk. 47).
    22. Bwana Mtajika anashindwa kuulinda uongozi: anashindwa kulidhibiti taifa.
     Cherehani anasema kwamba kikaza kimepasuka.
    23. Wizi wa mali ya umma unawafanya wafuasi wengine wa Mtajika kutotaka kuonekana hadharani isipokuwa Machupa ambaye anajua namna ya kuishi
    24. Hivyo viongozi hawadiriki kutatua matatizo ya raia.
    25. Raia wanawawekea viongozi vikwazo vinavyosababisha kuanguka kwao.
     Cherehani anapunguza kiwango cha kikaza maksudi; kikaza kinapasuka.
     (uk 48)

Download Kenya Certificate Of Secondary Education(KCSE 2013) Kiswahili Karatasi ya Tatu with Marking Scheme.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest