Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - KCSE 2021 Past Papers

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. UFAHAMU (Alama 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
  Ulikuwa wakati wa jioni jua limepunguza udhia wake na upepo mwanana ulikuwa ukipita na kuzipapasa ngozi zetu mfano wa pamba. Kama ilivyokuwa desturi yetu hapo kijijini, siku hiyo pia tuliketi nje ya nyumba yetu tukafanya duara kulizunguka birika la kahawa. Kila mmoja alichukua glasi akajimiminia kiasi cha kahawa alichotaka na kurudi kuchukua mahali pake kitini.
  Tulipotia fahamu tulipata mazoea haya yamekita mizizi nasi tukawa hatuna budi kuyakumbatia. Hatukuyakumbatia tu, bali tuliyakumbatia kwa dhati ya moyo. Vikao hivi havikuwa tu hazina kubwa kwetu bali pia vilikuwa vya thamani isiyomithilika. Hapa ndipo tulinoleana bongo kwa kupashana habari. Leo hii tumo katika kuzungumzia nguzo kuu za maendeleo, tena maendeleo ya haja ambayo yataibadilisha sura ya mwananchi na nchi. Nahodha wa kikao cha leo anampa msemaji wa kwanza nafasi naye hakusita kushika usukani.
  "Nionavyo mimi, maendeleo yatawezekana ikiwa elimu itaweza kukidhi haja za watu. Sio nadharia tupu ambayo huwezi kuitumikiza ikaleta matokeo. Lazima nchi imwezeshe kila mtu kupata elimu ya msingi ambayo itamsaidia kufikia habari za kimsingi, iwe ni kupitia kwa magazeti au vitabu. Habari hizo zitamfunua macho, akaona na kuhakiki mambo. Wenzangu, jibu ni elimu! Maendeleo yanategemea elimu," kijana mmoja alisema kwa mhemko.
  Muda wote huo kila mtu alikuwa ametulia. Wapo waliotikisa vichwa kukubaliana naye na wapo waliovitikisa kukataa. Hata hivyo, walikuwepo waliokaa tu kama mawe. Hawakuonyesha ishara yoyote ya kuguswa na maneno yale. Mwendesha mjadala alifanya ishara na mara kijana wa miraba minne aliyekuwa amevaa shati lililompwaya akasimama na kuzungumza kwa sauti nzito. ad "Mtazamo wangirnimi bwana ni tofauti. Ukitazama dontantkotekita nchi iliyoendelea
  imewekeza sana viwandani. Uzalishaji wa viwandani ndio dawa mjarabu. Hebu vuta fikra! Kila tunachotumia kuanzia kalamu, kitabu, nguo, msumari, saruji ... yaani kila kitu chenye nafasi katika maisha yetu kimepitia hatua za uzalishaji viwandani..."
  "Si ndio hayo! Naona unaniunga mkono aisee! Viwanda huendeshwa kwa elimu au ukipenda maarifa. Na maarifa hayo huja kwa mafunzo ambayo ni elimu," alifafanua yule kijana wa kwanza.
  "Nipe muda Sudi! Nipe muda nimalizie hoja yangu. Ninachosema ni kuwa elimu bila utumizi wake kuzalisha huduma na bidhaa muhimu haina nafasi kubwa katika maendeleo ya jamii. Elimu si mwisho wa yote bali mwanzo. Elimu inafaa kuzalisha. Na uzalishaji muhimu zaidi ni wa viwandani. Kwa hivyo, nionavyo mimi msisitizo mkubwa unafaa kuwa katika kutengeneza viwanda na kuvifanya kuzalisha."
  Jama alimaliza mazungumzo yake akatulia na kupiga funda la kahawa. Hapo ndipo mwendesha mjadala alipompa kijana mwingine nafasi naye atoe maoni yake. Kijana huyo mdogo wa kimo na umbo alianza kusafisha koo huku wenzake wakimshangilia. Kwa kawaida kijana huyo alikuwa na mbwembwe nyingi.
  "Bwana Spika," alianza huku wenzake wakishangilia kwa kila namna. Walipotulia aliendelea, "Mimi najua wapo watakaoniita mjinga hapa lakini naamini miundombinu ni muhimu zaidi. Watu hawawezi kuendelea bila mfumo mzuri wa barabara na reli, usambazaji wa kuridhisha wa umeme, viwanja vya kutosha na bora kwa ajili ya vijana kunoa vipawa vyao..."
  Maneno yake yalifunikwa ghafla na kelele za kumshangilia na kumsifu huyu kijana waliyemwita Sumaku. Hii ilikuwa lakabu waliyompa kwa uwezo wake wa kuelewa mambo kwa wepesi na kwa kujua kuwavutia vijana wenzake maana alijua wapi pa kugonga ili gogo litoe mlio. Alipoona bado wanashangilia aliinua mkono wake wa kushoto juu na kusema, "Basi! Basi, wananchi, sina shaka ujumbe umefika." Kisha aliketi na kuwaacha wenzake wakiumwa mbavu kwa vicheko.
  Utulivu ulirejea taratibu. Kabla kila mmoja amakinike, mwendesha mjadala alimpa nafasi mzee mmoja aliyekuwa amevutwa na mazungumzo hayo naye kuchangia. Mzee yule alicheka kidogo, akasafisha koo na kuwapongeza wachangiaji waliomtangulia kisha naye akasema yake.
  "Mambo hayo yote ni kama pacha lakini pekee hayatoshi. Miundomsingi inahitaji watu wa kuitumia, navyo viwanda vinahitaji wafanyakazi. Watu hao wasipokuwepo, vitu hivyo havina maana. Watu hao wanahitaji kuwa na afya bora. Hospitali zinahitaji kuwa katika kiwango cha kutoa huduma za kuridhisha. Zinahitaji wataalamu wasiobabaisha, vyombo vya kisasa vya udodosi na upasuaji, dawa nzuri na mazingira safi kwa ajili ya wagonjwa. Halafu huduma hiyo nzuri iwe inaweza kufikiwa na kila mtu."
  Alitua kidogo. Sasa kila mtu alikuwa ametulia kama ardhi iliyonyeshewa. Kisha akaendelea, "Pamoja na hayo, ipo haja ya huyo mfanyakazi kupata pa kuweka ubavu wake. Akiisha kuichapa kazi anahitaji kurudi nyumbani. Si nyumbani kwa maana ya mahali pa kupangisha bali nyumbani kwa maana ya mahali pake mwenyewe. Hivyo panahitaji kuwepo mpango wa wafanyakazi kununua nyumba kwa bei nafuu. Mtu si kama ndege anayeweza kuishi mtini na akaamka kushika shughuli zake. Mtu huhitaji makao yake. Haya yote yakifanywa kwa pamoja na kwa ufanisi basi tutakuwa tumeanza kujiandaa kupaa kwa mbawa zetu wenyewe."
  Alipomaliza kusema alishika njia na kwenda zake bila kutazama nyuma. Sote tulijikuta tunacheka kwa sauti huku tumetabasamu.
  1. Bainisha mambo matatu ambayo yanaleta utangamano baina ya vijana wa jamii hii. (alama 3)
  2. “Kupata elimu pekee hakutoshi kuleta maendeleo." Thibitisha kwa hoja mbili kutoka kwenye kifungu. (alama 2)
  3. Kwa kutoa hoja nne, onyesha uhusiano uliopo kati ya nguzo mbalimbali za maendeleo kwa mujibu wa kifungu. (alama 4)
  4. Eleza mambo matatu ambayo yanawachangamsha vijana katika kifungu. (alama 3)
  5. Kauli, upepo mwanana ulikuwa ukipita na kuzipapasa ngozi zetu," imetumia tamathali gani ya usemi? (alama 1)
  6. Eleza maana ya, "tulinoleana bongo' kwa mujibu wa taarifa. (alama 1)
  7. Andika kisawe cha hoja kwa kurejelea kifungu. (alama 1)
 2. UFUPISHO (Alama 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
  Binadamu hakuumbwa kuishi katika upweke na kujitenga. Aliumbwa kuwa sehemu ya mfumo wa ushikamano na wenzake. Baadhi ya jamii zinaeleza kwamba Mungu alimuumba mwanamume kwanza na alipoona kwamba anaishi kitwea akamuumbia mwanamke kuwa mshirika wake. Hatua hii ikawa ndio mwanzo wa watu kuishi pamoja kama mke na mume. Yumkini hiki ndicho kiini cha familia. Mshikamano wa familia ni muhimu sana kwa sababu hujenga uhusiano mwema na kushirikiana kimawazo, kikazi na hata zinapozuka haja nyinginezo. Mababu zetu walihitaji sana umoja wa familia. Umoja huo ulifaa mno katika hali mbalimbali. Wakati huo watu walizungukwa na misitu mikubwa ambamo waliishi wanyama wakali kama vile simba, chui na duma. Wanyama hao walikuwa hatari kwa binadamu na hivyo kuwahitaji watu kuungana kuwakabili.
  Enzi hizo za mababu pia zilishuhudia uhasama wa kikoo. Koo mbalimbali zilishindana kunyang'anyana mifugo na kung'ang'ania ardhi ili kujijengea himaya zao. Katika hili pia ushirikiano wa karibu ulihitajika ili kujihami dhidi ya uvamizi wowote ule, kutokuwepo kwa uvamizi kulimaanisha kuwa jamii ilipata utulivu na moyo wa kuendeleza shughuli zao za kila siku ambazo zilikuwa msingi wa maendeleo yao. Watoto nao walipata mazingira salama na tulivu ya kucheza na kukua.
  Ushirikiano huu haupo tu katika familia za wanadamu. Tunawaona wanyama wakiwa katika makundi. Wanatembea, kucheza, kula na kulala katika makundi. Makundi haya ni muhimu sana katika maisha ya wanyama mbalimbali. Ulimwengu wa wanyama una adha tele. Adha hizo huwa kisiki kikubwa katika maisha ya wanyama. Zipo hatari za baadhi ya wanyama kuwindwa na kufanywa kitoweo. Mnyama akiwa peke yake huwa Windo rahisi kwa wawindaji Wakiwa katika kundi husaidiana kushika zamu na kutanabaishuna hatari ibishapo. Kwa kufanya hivyo huokoleana maisha. Nao wanyama wanaowinda huwa na kibarua kigumu kupata windo wakiwa waenda pweke. Hata simba, mfalme wa msitu, huhitaji kufanya shirika na wenzake ili kuliwahi windo kwa urahisi. Wapo wanyama wala nyama ambao hufa kwa kukosa chakula kwa sababu ya kukaa peke yao.
  Hii leo utaona kuwa watu hawashirikiani katika familia tu. Wanashirikiana pia katika mazingira ya shule ambapo wanapokezana maarifa mbalimbali ambayo ni muhimu katika maisha yajayo. Panapokuwa na ushirikiano mzuri kivuno huwa tele kwa mwanafunzi ambaye hujizolea mengi. Hupata elimu ambayo humfungua macho kuona sura tofauti ti hukuza kipawa chake ambacho anakitumia kwa manufaa yake na ya jamii pana, hujifunza udugu ambao ni muhimu katika kuishi na watu wengine baada ya masomo, na mwanafunzi huweza pia kukomaa kimawazo na kuwa kiungo muhimu cha taifa. Hata hivyo, haya hayaji tu na kumtamia mtu eti kwa sababu amefika na kuishi shuleni kipindi chote cha masomo. Hupatikana kwa mwanafunzi kujenga uthabiti wa fikra na mazoea ya daima kulenga kuwa mtu bora kwa wenzake, awe anawajua au hawajui. Kumbuka kuwa hata wanyama hufanya juhudi kubwa katika kujenga ustadi wao kushirikiana kulipata windo au kukwepa wawindaji.
  Taasisi zilizobuniwa kuwa nyenzo za kuendeshea maisha yetu zinajengwa katika misingi hiyo ya familia. Watu huja pamoja na kuunda sheria na kanuni zinazoelekeza utendakazi wao. Bila mpangilio unaohakikisha umoja na ushirikiano miongoni mwa watu, huduma zetu muhimu zingekwama na kutuletea dhiki isiyo mfano. Askari hushirikiana ili kufanikisha kazi yao ya kukomesha uhalifu, walimu hushirikiana kuhakikisha kuwa mwanafunzi amepata elimu ipasayo na ipasavyo, dereva na utingo wake, lazima washirikiane ili kufanikisha safari ya abiria, rais na mawaziri wake hawana budi kushirikiana ili kufanikisha ajenda ya maendeleo.
  Ulimwengu wa sasa unahitaji watu wawezao kushirikiana. Wanaposhirikiana, shughuli iliyo mbele yao huwa nyepesi na matunda yake huwa ya kufana. Tunaona manufaa ya ushirikiano kwa uwazi zaidi viwandani. Wafanyakazi wa viwandani hugawanya majukumu. Kila mmoja huwa na jambo maalumu analofanya katika mfumo mzima wa uzalishaji bidhaa. Na ndio sababu kiwanda huweza kuzalisha bidhaa nyingi bora na kwa wakati mfupi. Mfano huu wa viwanda unatukumbusha kuwa sawa na viungo vya mwili, sisi wanadamu tuna wajibu maalumu wa kutekeleza kwa kushirikiana na wenzetu. Vinginevyo, kila mmoja akifanya jeuri ya kushika njia yake, uzito wa safari utakuwa mkubwa kwake. Ndio maana wakasema kuwa mtu pweke ni uvundo.
  1. Fupisha ujumbe wa aya tatu za kwanza kwa maneno 100. (alama 6)
   Matayarisho.........
   Nakala Safi.........
  2. Eleza kwa maneno 140, masuala ambayo mwandishi ameibua kuanzia aya ya nne hadi ya sita (alama 9)
   Matayarisho.......
   Nakala safi........
 3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
  1. Tofautisha sauti zifuatazo: (alama 2)
   1. /l/na/r
   2. /m/na/b/
  2. Bainisha matumizi ya 'ni' katika sentensi ifuatayo: (alama 1)
   Wasaidieni wale walinisaidia wakati wa shida.
  3. Andika neno moja lenye silabi za muundo ufuatao: (alama 1)
   Konsonanti + Konsonanti, Irabu + Konsonanti, Konsonanti, Irabu
  4. Tunga sentensi kubainisha kiunganishi kitegemezi. (alama 2)
  5. Tumia neno "vile katika sentensi kama:
   1. Kiwakilishi (alama 1)
   2. Kielezi (alama 1)
  6. Kutokana na mzizi '-erevu' unda:
   1. nomino (alama 1)
   2. kivumishi (alama I)
  7. Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani? (alama 2)
   1. teo .................
   2. chanda .................
  8. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo: (alama 3)
   Wale wengine watasafiri ughaibuni kwa ndege.
  9. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya umoja. (alama 1)
   Nguo walizouza madukani mwao ziliwavutia watalii.
  10. Geuza sentensi ifuatayo katika hali yakinishi. (alama 1)
   Makuli hawajakuarifu kwamba mizigo hiyo haikuwa yetu?
  11. Akifisha sentensi ifuatayo. (alama 2)
   lo kadio hamadi ndiye mwandishi wa kisiwa chenye tunu
  12. Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi (alama 2)
   Mama alimwita Juma na kutaka kujua namna alivyofaulu kuuzima moto huo.
  13. Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo. (alama 2)
   Seremala alilainisha mbao. Seremala alikuwa kiwandani. (Unganisha kuwa sentensi moja inayoanza kwa 'Mbao bila kubadilisha maana.)
  14. Andika kinyume cha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia maneno yaliyopigiwa mstari (alama 1)
   Punde tu alipouliza swali hilo Koru aliingia darasani.
  15. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea. (alama 1)
   Jani ambalo lilipukutika lilipeperushwa na upepo.
  16. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari. (alama 2)
   Wakulima hawa wanapanda zao hili daima.
  17. Andika sentensi ifuatayo upya ukianzia kwa yambwa tendewa. (alama 1)
   Andai alimnywesha babu uji kwa kikombe.
  18. Tunga sentensi moja kuonyesha maana mbili za neno somo. (alama 2)
  19. Tunga sentensi kubainisha matumizi yafuatayo ya 'kwa'. (alama 2)
   1. sehemu ya kitu
   2. namna
  20. Tunga sentensi moja kubainisha kishazi huru na kishazi kitegemezi. (alama 2)
  21. Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
   Fundi alimkatia Makaa utepe huo.
  22. Zimwi ilizidi kukimbia
   Shujaa aliongeza mwendo kilifikia
   (Unganisha kuwa sentensi moja kwa kutumia neno 'kadiri") (alama 2)
  23. Tunga sentensi zifuatazo: (alama 2)
   1. agizi
   2. hisishi
 4. ISIMUJAMII (Alama 10)
  1. Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
   "Karibu, karibu! Keti. Naam, jitambulishe kwa jopo hili... Bwana Nuru, ni jambo lipi ambalo linakufanya kuamini kwamba nafasi hii inakuafiki wewe?"
   1. Bainisha sajili ya makala haya. (alama 1)
   2. Eleza sifa nne za sajili hii kwa kurejelea makala haya. (alama 4)
  2. Wewe ni kinara wa chama cha Wanamawasiliano Bora shuleni mwako.
   Umepewa jukumu la kuwatangazia wenzako mashindano ya uogeleaji yakiendelea shuleni mwako. Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia. (alama 5)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. UFAHAMU
  1. Kulifanya mjadala pamoja kuhusu maswala yaliyowasathiri
   1. Kuwa na hali sawa changamoto sawa zilizowazunguka, kama vile haja ya kuboresha matibabu na makazi
   2. Kuwa na maono/ Hali ya kujali maendeleo ya nchi yao iliwaleta pamoja. Msimulizi anazema wapo ili kuzungumzia nguzo kuu za maendeleo
   3. Kuyadhibiti maingiliano/ mazungumzo yao kuwa na utaratibu maalum wa kuendeshea mazungumzo yao. Kuwa na kiongozi/mwendesha mjadala aliyewapa nafasi za kuzungumza katika nafasi maalum kuliwasaidia kukinga dhidhi ya kutoelewana
    Hoja 3 x 1 = 3

    Tanbihi
    Hili ni swali la ufasihi. Mtahini atathmini ya mtahiniwa
  2. Mambo yanayoonyesha kuwa kupata elimu tu hakuwezi kuleta maendeleo
   1. Elimu ya nadhana - hivyo haisaidii
   2. Elimu isipotumiwa kuzalisha haina maana - elimu haina maana ikiwa kuipata kutazamwa kama hatima ya mambo
    Hoja 2 x 1 = 2
  3. Uhusiano kati ya uguzo mbalimbali za maendeleo
   1. Afya na viwanda - watu wanaweza tu kufanya kazi vizuri wakiwa na afya
   2. Viwanda na miondomsingi - bidhaa huweza kufika na kutoka mahali mbalimbali na hata kuzalishwa kwa kuwa na miondomsingi ifaayo
   3. Makao ya watu ni muhimu kwa wafanyakazi ambao huhitaji kupumzika vizuri kufanya kazi
   4. Elimu ni muhimu katika kupata maarifa ya kujenga viwanda na miondomsingi
   5. Elimu inahitaji nyanya nyingine kama vile viwanda ili kupata baadhi ya vifaa kama vile kalamu
   6. Binadamu wenye elimu nahitaji kuwa na afya kuishi mahali panapofaa ili kuweza kuzalisha mali ipasavyo
  4. Mambo matatu yaliyowachangamsha vijana
   1. Mbwembwe za Sumaku wakati wa kusema
   2. Hoja za Sumaku zilizowatetea vijana
   3. Hatua ya mzee kujiondokea bila kuaga
  5. Tashhisi/uhuishaji/ubaishaji - upepo kupewa sifa ya kibinadamu ya kupapasa
   Chuku - haiwezekani katika hali ya kawaida kwa upepo kupapasa
  6. Tulinoleana bongo - tulielimishana/tulitoleana maarifa/ tulierevushana/tulifunzana
  7. hoja - rai, wazo, fikra, shauri

   Tanbihi
   Mwongozo wa kudumu pia uzingatiwe katika utuzaji
 2. UFUPISHO
  1.          
   1. Binadamu aliumbwa kushirikiana na wenzake.
   2. Asili ya familia ni uumbaji alioufanya Mungu ili washidiane
   3. Ushirikiano wa familia ni muhimu tangu enzi za mababu ambapo watu waliungana kupambana na adui na wanyama hatari
   4. Baadhi ya koo zilikuwa na uhasama kwa kushindania mifugo
   5. Kujihami kwa familia kuliwahakikishia watu utulivu
   6. Ushirikiano ni muhimu hata miongoni mwa wanyama ih kujifadhi
  2.      
   1. Ushirikiano leo hit upo katika taasisi mbalimbali
   2. Wanafunzi hufaidi ushirikiano mzuri wakiwepo shuleni
   3. Manufaa ya ushirikiano shuleni huja kwa mwanafunzi kulenga kimaksudi kuwa mtu bora
   4.  Ushirikiano huja kwa mtu kufanya juhudi za kimakusudi.
   5. Taasisi zetu muhimu hutegemea ushirikiano uliojengwa katika misingi ya kifamilia ili kufanikiwa
   6. Katika taasisi watu huja pamoja kuunda kanuni za kuendeshea mambo.
   7. Ulimwengu wa leo unahitaji watu wawezao kushirikiana
   8. Uzalishaji huwa mkubwa watu washirikianapo. 
   9. Mtu ajitengaye na wengine huhangaika kutekeleza majukumu yake.
   10. Ushirkiano humfanya mwanafunzi kuwa wa kutegemewa zaidi.
   11. Ushirikiano huokoa muda
   12. Ushirikiano huboresha uzalishaji.
    Hoja 8 x 1-8
    Alama 1 ya mtiririko (Jumla: alama 9)
 3. MATUMIZI YA LUGHA
  1.      
   1. /l/ - kitambaza
    /r/ - kimadende
   2. /m/ - nazali/king'ong'o/kipua
    /b/ - kipasuo/kiziliwa/
    2 x1 = 2
  2.      
   1. wingi/nafsi ya tatu-wingi/nyinyi
   2. nafsi ya kwanza - umoja/mimi/mtendwa
  3. Mkanda, mlango, mkondo
   mtundu, mpango, mjinga
   1x1=1
  4. Kiunganishi kitegemezi huunganisha vishazi vyenye hadhi tofauti kiskuzi huri na kishazi tegemezi.
   Sentensi ibainishe viunganishi kama vile; ingawa, licha yy, iwapo, kama, ikiwa, para na, minghairi ya Baadhi ya mifano:
   1. Kama angefika mapema angenikuta 
   2. Iwapo unataka ufanisi tia bidi.
   3. Ingawa ana uwezo tunamsaidia
   4. Licha ya cheo chake, hakuisaidia jamii yake
   5. Utaliinua gogo hilo ikiwa utakubali kusaidiana na wenzako.
   6. Alihudhuria hafla hiyo mingairi ya kuonywa na wenzake.
    1 x 2= 2 
  5.    
   1. Kiwakilishi;
    1. Huyu anataka vile
    2. Vile ni vyake.
    3. Mpe vile. 1x1=1
   2. Kielezi :
    1. Mbona unamtazama vile?
    2. Umesikia vile alivyosema?
  6.    
   1. Nomino - werevu - alama 1
   2. Kivumishi - mwerevu alama 1 
  7.      
   1. teo-U-ZI/ZI
   2. chanda - KI-VI/KI- alama 1
  8. wale wengine - kitai nomino
   watasafiri ughaiubuni
   kwa ndege, kitai kihusishi/kirai husishi
  9. Nguo aliyoua dukani mwake ilimvutia mtalii.
   1x1 -1/0
  10. Makuli wamekuatitli kwamba mizigo hiyo ilikuwa yetu? 
  11. Lo! Kadio, Hamadi ndiye mwandishi wa Kisiwa chenye Tunu!
  12. "Jumal Juma! Umefaulu vipi kuuzima moto huu?" Mama akauliza
   au
   "Juma," mama akaita, "umefault vipi kuuzima moto huu/huo?"
  13. Mbao zililainishiwa kiwandani na seremala
   Au
   Mbao zililainishwa na seremala akiwa kiwandani 
  14. Punde tu alipojibu swali hilo Koru alitoka darasani
  15. Jani ambalo hupukutika hupeperushwa na upepo.
   Jani lipukutikalo hupeperushwa na upepo
   Jani linalopukutika linapeperushwa na upepo.
  16. S→KN (N+V) +KT (T+N+V+E)
   au
   S→KN (N+V)+KT(T+KN(N+V)+E
   S→KN + KT
   KN→ N+V
   N→Wakulima
   V→hawa
   KT→T+KN+E
   T→wanapanda
   KN→N+V
   N→zao
   V→hili
   E→daima
  17. Babu aliyeshwa uji na Andai kwa kikombe
  18. Sentensi inaweza kubainisha mbili kati ya maana hizi:
   1. mpango wa mafundisho wa elimu maalum
   2. kipindi cha mafundisho au mazoezi
   3. mtu mwenye jina moja na mwingine/ mwenye jina sawa na lako lazim
   4. mwalimu afundishaye mambo ya kunga unyagoni au kumbini/kungwi
   5. rafiki
  19.      
   1. Sehemu ya kitu: Wanafunzi wawili kwa kumi huchelewa kila siku.
    Au
    Alipata themanini kwa mia katika jaribio hilo.
   2. Namna ya kutenda jambo
    Tindi alimtazama kwa huruma.
    Au
    Ndua anakata kuni kwa upanga
    2x1 = 2
  20. Ukuta uliojengwa kwa mawe    ulidumu.
                   tegemezi                      huru
   Vigozo vya vishazi tegemezi
   Sentensi iwe changamano.
   Iwe na kitenzi kishirikishi
   ki ya masharti
   Matumizi ya po ya masharti 
   Au
   Ukuta ukijengwa kwa mawe  utadumu.
              tegemezi                        huru
   Au
   Maria alitia bidii masomoni  akafaulu
                tegemezi                    huru
   Ingawa alikuwa na mahitaji maalumu  alijitahidi maishani.
                        tegemezi                                    huru
  21. Maana
   1. Fundi alikata utepe akampa Makaa- kwa faida ya Makaa.
   2. Fundi alikata utepe kwa niaba ya Makaa/ badala ya Makaa kuukata utepe
   3. Fundi alimkata Makaa kwa sababu ya utepe
   4. Fundi alikata utepe wa Makao ili kumhasiri ili kumuumiza Makaa
   5. Fundi alimakata Makaa kwa kutumia utepe.
    2x1 = 2
  22. Kadiri zimwi lilivyozidi kukimbia ndivyo shujaa
  23.       
   1. Mifano ya sentensi agizi
    1. Njoo hapa!
    2. Meza tembe mbili mara tatu kwa siku
    3. Tembea hatua tatu kuelekea kushoto kisha upinde kulia.
    4. Unaweza kunipitishia bilauri hiyo?
    5. Tafadhali nipitishie kikombe hicho.
    6. Ukienda sokoni uninunulie kalamu
     1x1 = 1
   2. Mifano ya sentensi hisishi (inayoibua hisia)
    1. Maskini, hakuliona gogo hilo, sasa limemuumiza.
    2. Ni moyo wa nani usiohuzunika kwa tendo kama hilo?
    3. Jamani/Maskini! Anaonckana kuzidiwa na msiba.
    4. Sasa nitafanya nini mimi mnyonge nisiyemjua yeyote?
 4. ISIMUJAMII
  1.    
   1. Mahojiano kati ya mwajiri na mwajiriwa Sajili ya Mahojiano.

    Tanbihi
    (Atakayeandika ni sajili ya mazungumzo. asituzwe.)
    1.      
     1. Kuna istilahi/msamiati maalum wa mahojiano. Kwa mfano, jopo, kujitambulisha kwa jopo, nafasi./msamiati wapokee taule
     2. Lugha dadisi. Ni jambo gani linalokufanya uamini kwamba nafasi hii inakuafiki I wewe?
     3. Kuzungumza moja kwa moja na mhojiwa. Kwa mfano, Bwana Nuru
     4. Lugha ya heshima. Karibu! Karibu keti.
     5. Ni lugha, rasmi. Kwa mfano, 'Bwana Nuru'.
     6. Ni lugha inyozingatia kanuni za kisarufi. Kwa mfano, nafasi hii inakuafiki..."
     7. Kuna matumizi ya sentensi ndefu ndefu hasa kwa upande wa maswali ya mhoji
      K.m. Bwana Nuru ni jambo lipi ambalo ....
     8. Mahojiano kuzingatia utaratibu fulani. Kwa mfano, kukaribishwa, kujitambulisha na kuulizwa maswali
    2. Hii ni sajili ya matangazo ya mchezo wa kuogelea. Sifa za matangazo ya aina hii zijitokeze. Baadhi ya hoja ni:
     1. Kuzungumza moja kwa moja na hadhira
     2. Kutumia msamiati maalum wa uogeleaji. K.m. piga mbizi, free style,
     3. Kuchanganya ndimi. Kwa mfano, mtindo wa 'free style backstroke 
     4. Lugha yenye kupiga chuku. Kwa mfano, "Anampiku samaki katika uogeleaji'.
     5. Lugha ya kusisimua/kuvutia. K.m. Haya , haya mtazamaji. Ndiye huyo duma kwenye kidimbwi, jitazamie mwenyewe, ukimkosa utakonda....
     6. Ni mazungumzo ya kasi kutokana na kasi ya uogeleaji.
     7. Sentensi fupifupi/lugha ya mkato, k.m. Huyoo! Amempita Pendo.
     8. Kutaja waogeleaji kwa majina ya majina ya lakabu au hata majina ya timu km. Papa wa baharini, Pendo, gwiji
     9. Wakati mwingine kuna kuvunja kwa sheria za kisarufi au matumizi ya kibada ya lugha
     10. Kutumia lugha ya kitamathali inayomjengea picha msikilizaji. Kutumia tashbihi isitiara, methali k.m. anapiga mbizi kama samaki ziwani. Huyu ni papa hasa
     11. Lugha yenye porojo k.m. mfuatano wa maneno ambayo huenda yasiwe na maana katika matumizi ya kawaida
      Hoja 5x1 = 5 
     12. Maswali ya badala hutumiwa
     13. Lugha ya vihisishi
     14. Lugha ya kiimbo cha juu

Sifa na mfano alama ½
Tano za mwanzo

 1. Makosa yatolewe kwa mifano
 2. Makosa ya mfano yasiondolewe 

Makosa ya kisarufi

 1. Minyambulike mibaya
 2. Matumizi mabaya ya viakifishi
 3. Kutoakifisha
 4. Matumizi ya herufi ndogo
 5. Matumizi mabaya ya herufi kubwa
 6. Kutumia aina ya neno lisilofaa
 7. Upatanisho usiofaa
 8. Kutoambisha

Makosa ya hijai/tahajia

 1. Kuongeza herufi
 2. Kutenganisha liwe wazi
 3. Kuunganisha maneno 
 4. Kutumia vifupisho
 5. Matumizi mabaya ya ritifaa
 6. Kuendeleza neno vibaya lilichapishwa katika mtihani
 7. Maumbo mabaya ya herufi

Ufupisho

 1.    
  1. Binadamu hakuumbwa kuishi katika upweke
  2. Mungu alimuumba mwanamke na mwanamume washirikiane
  3. Hotua hii ikawa kiini cha familia
  4. Mshikamano wa familia hujenga uhusiano mwema/Mshikamano wa familia in muhimu
  5. Mababu waliitaji umoja ili kujikinga dhidhi ya wanyama
  6. Enzi za mababu zilishuhudia uhasama
  7. Ushirikiano wa karibu uliitajika ili kujihami dhidi ya uvamizi
  8. Utulivu uliwapa watoto mazingira Salama wa kucheza na kukua
  9. Ushirikiana pia upo miongoni mwa wanyama
  10. Ushirikiano huu huwasaidia kujikinga katika hatari
  11. Ardha kawasaidia kupata riziki
 2.      
  1. Watu hawashirikiani katika familia tu bali katika pia shule
  2. Ushirikiano mzuri humfaidi mwanafunzi
  3. Mwanafunzi hukuza kipawa chake anachokitumia 
  4. Maarifa hupatikana kwa mwanafunzi kujenga uthabiti wa fikra - kulenga kwa wenzake 
  5. Taasisi za kuendesha maisha yetu 
  6. Watu huunda sheria zinazoendekeza utendakazi wao
  7. Bila mipangilio huduma zingekwama
  8. Ulimwengu wa sasa unahitaji ushirikiano 
  9. Ushirikiano hufanya shughuli nyepesi
  10. Binadamu ana wajibu maalum kutokeleza kwa kushirikiana na wenzetu
  11. Mtu akijitenga mzigo wa safari utakuwa mzito kwake
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - KCSE 2021 Past Papers.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?