Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - KCSE 2021 Past Papers

Share via Whatsapp

SEHEMU A: TAMTHILIA
P. Kea: Kigogo

 1. Lazima
  1. "Aikose? Asiya ni mwanamke halisi bwana! Amemweka Bi Husda hapa."
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   2. Eleza vipengele viwili vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe.(alama 2)
   3. Fafanua sifa nne za anayeambiwa maneno haya. (alama 4)
  2. "Kuzorota kwa maadili kunachangia kuzorota kwa mahusiano ya kijamii." Thibitisha kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya Kigogo.
   (alama 10)

SEHEMU B: RIWAYA
A. Matei: Chozi la Heri
Jibu swali la 2 au la 3.

 1. Jadili nafasi ya mwanamke katika kuendeleza ukiukaji wa haki za kibinadamu katika riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)
 2.             
  1. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo: (alama 10)
   "Una bahati sana mwenzangu," alisema Kairi siku moja, "wewe hujapitia tuliyopitia. Tulitendwa ya kutendwa. Siku hiyo tulipofurushwa kwetu kama takataka tulitanga na njia bila kujua tuendako mama mbele, sisi nyuma, mama amebeba kitindamimba ambaye baadaye alishindwa kukamilisha safari, roho yake changa ikakatika papo hapo mgongoni mwa mama, amemezwa na njaa na ugonjwa wa udhaifu wa mapafu. Mama alituelekeza kando ya njia, tukaingia kichakani kiasi. Sijui alikotoa kiserema alichokitumia kuchimba kaburi lenye kina cha haja, tukaufukia mwili wa ndugu yetu huku kilio cha uchungu na jitimai kikihanikiza kote".
  2. Jadili nafasi ya wahusika wafuatao katika kuijenga riwaya ya Chozi la Heri:
   1. Cizarina (alama 5)
   2. Tila (alama 5)

SEHEMU C: HADITHI FUPI
A. Chokocho na D. Kayanda (Wah.): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 4 au la 5.

 1. A. Chokocho: Masharti ya kisasa
  "Alipokuwa kiguu na njia akimwinda kama kunguru ... Ajabu lakini, kwa nini misumari ya nyuki inamwuma sasa ila si wakati ule wa tamaa ya ushindi ilipokuwa mbali ..."
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Bainisha toni katika kauli hii. (alama 2)
  3. Fafanua "misumari ya nyuki" kwa kurejelea hadithi: Masharti ya kisasa. (alama 14)
 2.         
  1. “Suala la uozo wa kijamii limejitokeza katika hadithi: Mame Bakari." Thibitisha (alama 10)
  2. Jadili mchango wa wazazi katika maisha ya vijana kwa kurejelea hadithi: Ndoto ya Mashaka. (alama 10)

SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7.

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
  Mtu asiye heshima, aibu ya roho yake
  Mfano wake tazama, kama popo mwendo wake
  Wanaposhindwa wanyama, hudai ndege wenzake
  Na ndege sio wenzake, wanaposhinda wanyama.
  Na siku ya mapatano, ya ndege na wanyama
  Yeye huwa ni miguno, halipati la kusema
  Hana masikilizano, kwa ndege wala wanyama
  Mtu kamaye daima, ni aibu kubwa mno.
  Huwa hatamki neno, kama kinywa kimetuna
  Hapati la mnong'ono, heshima hanayo tena
  Hana heshima ya neno, wala heshima ya jina
  Hapati kuonekana, hampi mtu mkono.
  Hafai kuandamana, mtu huyo umwepuke
  Kama alivyo hiana, juu ya nafsi yake
  Na salama kwako hana, afadhali mtanuke
  Hiana na roho yake, kwako hawi muungwana.
  Mbaya mtu hiana, kuwa naye utajuta
  Dunia ikikubana, na kusongwa na matata
  Atakutupa mchana, mbinguni hakuna nyota;
  Ni mambo yanatukuta, na kisha hutendekana.
  (S. Robert)
  1. Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 4)
  2. Bainisha nafsineni ya shairi hili. (alama 2)
  3. Fafanua umuhimu wa uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili. (alama 6)
  4. Eleza dhima ya aina mbili za urudiaji zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 4)
  5. Bainisha tamathali za usemi katika ubeti wa kwanza na wa pili. (alama 2)
  6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari. (alama 2)
 2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
  Nalilia mazingira yetu haya
  Hakuna kilicho safi
  Vyote ni kombo
  Mrama vimekwenda.
  Tazama mto huu
  Mto utambao katikati mwa jiji kuu
  Jiji la uzungu na usasa
  Lenye warembo na wakwasi
  Wanaolivuka bila fahamu
  Wanaolilima bila kujali
  Wanalifumbia macho ilhali lipo!
  Najua mwakani watakuja usafi kulitia
  Usafi ndugu wa siku moja
  Eti kuupa mji sura!
  Wanaukosha mji, si mto!
  Ni mto ulioona mengi na makubwa kushuhudia
  Lakini kwa kimya ndugu zangu unakwenda
  Labda kwa uchovu na bughudha
  Ningekuwa mimi ningepaaza sauti:
  **Punguzeni bughudha.
  Msinitwike mizigo yenu nload more nere mil
  Maana mimi mnanibebesha mizigo yenu
  Na minyororo ya uchafu kunitia
  Kusudi mpate safika.
  Tangu lini Mto kukoshwa kwa sabuni?
  Hamjui Mto husafisha dhambi?"
  Lakini nionavyo ndugu
  Taswira ya mto huu
  Ni taswira kamilifu ya kizazi chetu!
  Kizazi baina ya kilichopita na kijacho.
  (Limenukuliwa kutoka: Tunu ya Ushairi)
  1. Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 5)
  2. Onyesha mbinu mbili za uhuru wa kishairi katika shairi hili. (alama 2)
  3. Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili. (alama 3)
   1. Tashihisi
   2. Swali la balagha
   3. Kinayake
  4. Onyesha aina mbili za urudiaji zinazojitokeza katika ubeti wa pili. (alama 2)
  5. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
  6. Fafanua aina tatu za taswira kwa kurejelea shairi hili. (alama 3)
  7. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
  8. Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari. (alama 2)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

 1. Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
  Hapo zamani za kale Nungunungu na Fisi walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Walizilea familia zao pamoja. Nungunungu aliwafaa watoto wa Fisi kwa nafaka naye Fisi aliwafaa wa Nungunungu kwa nyama. Wanyama wengi waliuhusudu urafiki wao. Hata hivyo, Sungura hakusita kumtahadharisha Nungunungu mara kwa mara.
  "Ndugu," Sungura alisema, siku moja, “Sijui kilichokuvuta kwa huyu mwenzako, ila nataka ujue kwamba mla mizoga haaminiki, haitakuwa ibra watoto wako wakigeuzwa kitoweo chake."
  Nungunungu aliyatia maneno ya Sungura kwenye mizani, akataka kuyaamini, lakini moyo wake ukamuasa dhidi ya haya. Unajua tena mjukuu wangu kauli za mwenye hila hazisadikiki kwa urahisi. Nungunungu alijisemea moyoni, "Simtarajii ndugu yangu huyu aniendee kinyume. Nimeishi naye kwa miaka mingi, nikimfaa kwa jua naye akinifaa kwa mvua, tukizungumza ya kupwa na kujaa, tukilizana kwa furaha na simanzi. Itatokeaje anisaliti baada ya muda wote huu? Na iwe hiyo tamaa wamsingiziayo lakini kuwafanya kitoweo watoto wangu mimi ambaye hujisabilia kuwalea watoto wake mwenyewe anapomezwa na msitu akitafuta mizoga! Haiwezekani. La! Hasha!"
  Basi mjukuu wangu Nungunungu aliyatia masikio nta; akapuuzilia mbali ushauri wa jirani yake Sungura. Hakuona haja ya kuufuata ushauri huu kwani alijua kwamba ikiwa kweli nloa Fisi alikuwa ndoa, ukweli ungemdondokea viganjani mwake. Mbivu na mbichi ilibainika wakati kiangazi kikubwa kilikumba kijiji walikoishi Nungunungu na Fisi. Ukame ulibisha hodi. Njaa na ukosefu wa maji ukatishia kukipukutisha kizazi kizima cha wanyama.
  Hata hivyo, Nungunungu hakuwa na wasiwasi. Unaweza kusema kwamba yeye alikuwa kondoo mwenye manyoya tele. Maghala yake yalishiba yakatapika nafaka. Hivyo mng'ato wa ukame haukumwathiri.
  Kiangazi kilizidi kung'ata naye Nungunungu akaanza kuona muujiza wa kupungua kwa nafaka ghalani siku baada ya siku. Alipomuuliza Fisi, Fisi alikuja juu. "Nani mwingine ila yule goigoi, Sungura? Mimi kila mara hujituma kuitafuta mizoga, japo mizoga yenyewe imeadimika. Wakati mwingine hulazimika kujiulia mwenyewe."
  Sungura aliposikia hayo alijinyamazia tu. Alijua kwamba za mwizi ni arobaini. Alimwambia Nungunungu, "umdhaniaye ndiye siye." Kisha akaondoka. Jioni hiyo Sungura alitia gundi kwenye lango la ghala la Nungunungu na kujiendea zake kulala.
  Alfajiri mbichi Nungunungu aliamshwa na sauti ya kite. Alipotoka nje alimpata Fisi kaning'inia ghalani hivi, likawa lile la "Mwenye macho haambiwi tazama." Mjukuu wangu, ingekuwa wewe ungemfanyia nini rafiki yako huyu wa dhati?
  Hadithi yangu inaishia hapo. Naomba mbuzi wangu wale majani mabichi na wako wafe kwa kiangazi.
  1.            
   1. Ainisha ngano hii kwa kurejelea kigezo cha wahusika. (alama 2)
   2. Fafanua mbinu sita ambazo mtambaji ametumia kuufanikisha uwasilishaji wa ngano hii. (alama 6)
   3. Eleza shughuli tatu za kiuchumi ambazo zimejitokeza katika utungo huu. (alama 3)
   4. Eleza majukumu manne ya fomyula ya kumalizia katika utungo huu. (alama 4)
  2. Kipera cha ngano kinaendelea kufifia katika jamii yako. Pendekeza mbinu tano ambazo jamii yako inaweza kutumia kukinga dhidi ya hali hii. (alama 5)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. SEHEMU A: TAMTHILIA
  1.      
   1.      
    1. Haya ni maneno ya Boza.
    2. Anamwambia Kombe.
    3. Wako kwenye karakana, sokoni Chapakazi.
    4. Kombe amemwuliza kama mkewe Bozo amepata kandarasi ya kuoka keki ya kusherehekea miaka sitini ya uhuru, ndipo Boza anamjibu hivi.
     Hoja 4 x 1 = (alama 4)

     Tanbihi

     Dondoo limetolewa uk. 7
   2.      
    1. Swali la balagha - Aikose? - kuonyesha kwamba hawezi kukosa. Kujivunia weledi wa mke wake
    2. Unshiraji - Matumizi ya neno "hapa' yanaonyesha mtu anamwelekeza mahali kwenye sehemu ya mwili.
    3. Ulinganuzi anaonyesha mkewe kama anayempiku Husda kwa ulaghai/akili.
     Amemweka Husda hapa kwapani
    4. Taswira
     • hapa - taswira mwendo.
     • halisi - taswira mguso
    5. Nidhae - Mwanamke haliti bwana! (alama 2)
     Hoja 2 x 1
     Kutaja - 1
     Mfano - 1
    6. kwanza mbili
   3. Anayeambiwa ni Kombe
    1. Mwenye utani - Anamtania Boza kwa kumwambia kuwa anagaragara kama kuku anayetaka kutaga (Uk. 1).
    2. Mtambuzi anayatambua masaibu yanayowakumba.
    3. Mdadisi - anataka kujua sababu ya sherehe kuwa mwezi mzima.
    4. Mwenye busara - anakisia kuhusu hali itakavyokuwa iwapo sherehe itakuwa ya mwezi mzima.
    5. Mwenye stihizai-anamwita Sudi Professa wa siasa. Anawaliza Boza na Sudi kwa kejeli, iwapo hawajasikia kuwa kunasherehekewa uhuru uk 6).
    6. Mpatanishi - anawatuliza Boza na Sudi wanapokabiliana
    7. Mwenye bidii - Yeye na wenzake wanachonga vinyango kwa madhumuni ya kuzikimu familia zao.
     Hoja 4 x 1 = alama
     Kutaja- 1
     Mfano-1
  2.      
   1. Uzinifu wa Majoka unapalilia mgogoro kati ya Husda Ashua, Majoka anawakutanisha ofisini, wanapigana.
   2. Tendo la Majoka la kumtaka Ashua mapenzi na kumkejeli kwa kuolewa na mume asiyeweza kuikumu familia yake kunamfanya Ashua amkosee mumewe heshima. Anamwambia Sudi anahitaji matunzo (uk 47). Anamwambia kuwa amechoka kupendwa kimaskini (uk 47). Ashua anamtisha Sudi kwa kudai talaka( uk.47).
   3. Uzinifu wa Majoka unasababisha mgogoro baina yake na Husda.
   4. Ukosefu wa uwajibikaji katika ndoa unazorotesha mahusiano ya kiunyumba kati ya Majoka na Husda. Majoka anamwoa Husda ili kutimiza matakwa ya jamii na anaishia kumdhalilisha. Anasema hampendi, hakumpenda na hatampenda (uk 75). Anaishi na Husda kiwiliwili tu.
   5. Unyakuzi wa mali ya umma (Soko la Chapakazi) unaathiri uhusiano kati ya uongozi na raia. Tunu na Sudi wanaungana na vijana wenzao kuondoa uongozi wa Majoka. 
   6. Mauaji yanayotekelezwa na viongozi yanazorotesha uhusiano kati ya viongozi na wapiganiaji haki pamoja na raia. Tunu anahisi uchungu kwa kuuawa kwa baba yake.
   7. Uongozi kukosa kuwajibikia maslahi ya wanyonge kunakuza mgogoro kati ya viongozi na raja. Sudi analalamikia kukusanywa kwa kodi bila kushughulikia usafi wa soko ambamo wanafanyia kazi.
   8. Ukosefu wa uaminifu wa vijana kwa vijana wenzao unaleta kutoelewana kati yao. Kwa mfano, Ngurumo anatumiwa na Majoka kumpiga na kumuumiza Tunu (uk.63) anamtisha Tunu.
   9. Ukosefu wa uwajibikaji wa Mamapima kuwauzia vijana pombe haramu unazua kutoelewana kati yake na vijana wapigania haki kama vile Tunu. Tunu analalamikia vifo vya vijana kutokana na pombe hii. (uk. 63)
   10. Ukosefu wa mwelekeo thabiti kuhusu maisha unawafanya vijana kutoelewana. Ngurumo na Boza hawaoni ubaya wowote wa kuuzwa kwa pombe haramu ilhali Tunu na Sudi wanapinga hnya. Sudi hapendezwi na tendo la Mtu 1 kumwongezea
    Mtu II dozi ya dawa ya kulevya. (uk. 62)
   11. Ufisadi wa viongozi kunasababisha kutoelewana kati ya wanyonge. Asiya anapewa kandarasi ya kuoka keki kwa sababu ya uhusiano wake na Ngurumo, mumewe Bora anatusiwa kwa kuambiwa kuwa mke wake alioka keki ya uroda (uk63 - 64).
   12. Viongozi wanaelekeza kemikali na taka pale ambapo wanyonge wanafanyia kazi. (uk 2) na kusababisha ugomvi kati ya wanyonge. Boza na Sudi wanazozana (uk2).
   13. Kuwaingiza vijana katika utovu wa mandili na thamani za jamii kunaleta kutoelewana/ migogoro kati ya viongozi na raia. Shule ya Majoka and Majoka Academy imewatelekeza vijana katika matumizi mabaya ya dawa, hali ambayo inasababisha chuki na kutotosheka kwa wapigania haki. Ashua anabishana na Majoka, anasema hawezi kufanya kazi inayowageuza watoto kuwa makabeji.
   14. Jamii kumshinikiza Majoka kuoa ili apate uongozi. Jambo hili linamfanya aishi katika ndoa, asiotaka. Anamsaliti mke wake kwa kuishi naye huku anajua kuwa hampendi. (uk 75).
   15. Ukaragosi wa Kenga, Ngurumo na Boza kunawafanya wasihusiana vyema na vijana wenzao kama vile Tunu na Sudi.
    Hoja 5 x 2 = alama 10
    Kutaja - (ukosefu wa maadili)
    Kueleza -1 (kuzorota kwa mahusiano) 

    Tanbihi
    Sharti mtahiniwa ataje ukosefu wa maadily aonyeshe mahusiano/umusiano unavyoharibika ili atuzwe (alama 2) 

 2. SEHEMU B: RIWAYA
  1. Wanaendeleza mauaji. Mama yake Sauna anamfanya Sauna kuavya mimba. Oa (uk 155)
   • Wanazaa watoto na kuwatupa - Immaculata anaokotwa na Neema kwenye taka. 
   • Huko kwenye taka pia kunapatikana vijusi vilivyotupwa. 
   • Wanajua wenyewe kwa kujiingiza kwenye ulevi - Subira mkewe Kaizari anapatikana amejifia chumbani akiwa na chupa ya kinywaji kikali.
  2. Wanatelekeza haki ya malezi
   • Naomi, mama yake Umulkheri, anawaacha watoto wake kwa kutaka kukimbia umaskini. 
   • Subira, badala ya kutafuta mbinu za kuishi na mama mkwe, anawaacha Mwanaheri na Lime na kuhamia mjini. 
   • Mama yake Pete anaolewa na kumwacha; hajali hata kutaka kujua anavyoendelea shuleni.
  3. Wanachangia katika kuendeleza ndoa za mapema. Mama ya Pete anashirikiana na wajomba wake kumwoza mapema licha ya rai ya bibi yake kwamba wamwache aendelee na masomo (uk 148-149).
  4. Wanaendeleza ulanguzi wa binadamu. Sauna anawateka nyara Dick na Mwaliko, anampeleka Dick kwa Buda. Yeye na Kangara wanawaingiza vijana katika madanguro.
  5. Wanaendeleza ajira ya watoto.
   • Sauna anampeleka Dick kwa buda ambapo anaajiriwa.
   • Kangara ana mtandao ambapo anawapata vijana na kuwasafirisha baadhi ughaibuni kufanya kazi za kujidhalilisha.
   • Pete anamtumia msichana mdogo kumlindia kitoto chake akienda kazini.
  6. Wanaendeleza ubaguzi wa kiukoo. Mamavyan ya Subira anambagua. Anasema Subira ni msichana wa Bamwezi, anamwona kaina asiyoweza kudumu katika ndoa. - Anamkosesha utulivu kwa kumwita mwizi.
  7. Wanachangia kusambaratika kwa afasi ya ndoa. Mavyaa wa Subira anamsimanga Ma Subira hadi Subira anaondoka
  8. Wanasababisha dhiki za kisaikolojia. Mliewe Kiriri anamwachia upweke na kwenda ughaibuni. Naomi anamwachia Lunga upweke hadi Lunga anakufa kwa shinikizo la damu.
  9. Wanahatarisha afya za wengine kwa kuwauzia bidhan duni. Sauna anawauzia watu maji ya mto yaliyoiwa kwenye chupa za mineral water.
  10. Wanawaingiza vijana katika matumizi mabaya ya vileo. Sauna anampeleka Dick kwa Buda ambaye anamtumia kuangua dawa. Dick analazimika kutumia dawa hizo
  11. Wanawanyima raia haki ya kuihudumia jamii yao/ kuhudumiwa na jamii yao. Wanachangia uhamiaji ng'ambo wa nguvumali. Sauna na Kangara wanawapeleka vijana ughaibuni wanapofanya kazi za kujidhalilisha
  12. Anawanyima haki ya kuishi kiuadilifu. Kuwaingiza wanawake wenzao/wasichana kwenye madanguro - Kangara na Sauna.
  13. Wawanyima haki ya kutambuliwa /kujitambua kama binadamu wenye asili. Kutowaambia kuhusu usuli wao - mamake Pete, hamwambii, mama Kipanga as hamwambii kubusu baba yake.
  14. Kuwanyima ushirika na watoto wao Mkewe Kiriri anahamia ng'ambo na watoto ..

   Tanbihi
   Sharti mtahiniwa aonyeshe haki inayokiulowa na loitolea mfano kutoka kwenye kitabu. Aonyeshe mwanamke anayefanikisha ukiukaji hao wa haki za kibinadamu.
 3.      
  1.      
   1. Kuzungumza moja kwa moja na mzungumziwa ili kufupisha masafa-ujumi kati ya mwandishi/Msimulizi na hadhira. "Una bahati mwenzangu...
   2. Tashbihi -- tulifurushwa kwetu kama taka.
   3. Takriti undidi-hujapitia tuliyopitia, tulitendwa ya kutendwa,
    Mama, hapo hapo
   4. Tasbihisi - amemezwa na njaa na ugonjwa wa udhaifu.
   5. Tasfida - alishindwa kukamilisha safari.
   6. Taswira - Tulitanga na njia taswira mwendo) akaingia kichakani ( taswira mwendo),
   7. Chuku - kilio cha uchungu na jitimai kukihanikiza kote/ kumezwa na njaa
   8. Toni ya huzuni.
   9. Nahau – mezwa na njaa.
    - kilio cha uchungu
    kitindamimba
    roho yake changa ikakatikia hapohapo mgongoni
   10. Matumizi ya usemi halisi "Una bahati sana wenzangu."
   11. Tanakuzi - mbele - nyuma.
   12. Matumizi ya sentensi ndefu. 
   13. Mbinu rejeshi-Kairu anaturudisha nyuma kubadithia yaliyotokea

    Tanbihi
    Dondoo limetolewa uk. 91.
    Hoja 5 x 2
    Kutaja- 1
    Mifano-1
  2.      
   1. Cizarina
    1. Kupitia kwake tunatambua umuhimu wa utu. Anasimamia kituo cha Bencfactor kinachowashughulikia watoto waliotelekezwa (uk. 162) kitoto Riziki Immakulata kinnokelewa na kupelekwa katika kituo cha Benefactor.
    2. Anatumiwa kuonyeshazo ukatili wa jamii. Anaeleza kuhusu mazoea ya baadhi ya binadamu kuwatupa watoto wachanga. Anasema kuwa binadamu amezika hadhi na utakatifu wa maisha ya mja katika kaburi la sahau (uk 162)
    3. Kupitia kwake tunatambua mchango wa baadhi ya taasisi zinazotoa huduma kwa madhumuni ya kuboresha maisha ya wanajamii. Anasimamia kituo cha Benefactor (lk 163)
    4. Anaendeleza/anachimuza maudhui ya ukiukaji wa haki za kibinadamu. Anakashifu watu ambao wamezika thamani ya binadamu.
    5. Ni kiwakilishi cha uwajibikaji kuhusu utaratibu wa kisheria na wa kidini unaofuatwa katika kuwapangisha watoto (uk163).
    6. Anaangaza nafasi ya familia katika malezi (ya watoto wao na watoto wa kupanga). anamweleza Neema kuhusu kujitolea kwa familia katika kuwapanga watoto.
    7. Anawaclemisha wanajamii kuhusu suala na utaratibu wa upangaji wa watoto.
    8. Anaendeleza ploti. Kwenyo kituo chake tunahadithiwa kuhusu maisha ya kitoto kilichookolewa na Neema. Kukikubali kitoto kilicholetwa na Neema kunabadilisha mkondo wa maisha ya kitoto hicho
     Hoja 5 x 1
     Kutaja-1
     Mfano-1
   2. Tila
    1. Anadokeza suala la mabadiliko katika jamii na athari zakeyo kwa wanajamii. Kwa mfano, kubadilika kwa mfumo wa uzalishajimali, uongozi kuwakumbatia wanawake katika uongozi). (Rejelea Mazungumzo yake na baba yake(uk 38-44.)
    2. Anadokeza suala la mshikamano wa kifamilia. Palikuwa na uhusiano bora baina yake, nduguye na baba yao, Ridhaa anakumbuka wanawe Tila na Mwangeka walipokuwa wadogo walizoea kumkimbilia kila mara alipotoka kwenye shughuli zake za kikazi (uk 37).
    3. Anaangazia suala la Jinsin. Anahimizatwa katika jamii na katika uongozi. Mungu aina yake na babake kuhusu wake kwa waume kupewa nafasi sawa (uk 39)
    4. Kupitia kwake tunatambua kutownjibika kwa viongozi kutokana na kutotimizwa kwa matarajio ya wenyeji kuhusu ubora wa maisha yao (uk 40).
    5. Anaangazia jinsi umaskini ulivyotamalaki katika jamii. Watu hawamudu mahitaji ya kimsingi: Watoto kufa kwa kukosa lishe bora, asilimia kubwa ya raia ambao hawamudu hata gharama ya matibabu (uk 41).
    6. Anadokeza uwepo wa ukengeushi katika jamii. Walio juu wamekengcuka na hawaoni hawaelewi dhiki zinazowakumba wanyonge katika jamii (uk 43).
    7. Anachangia katika kubainisha hali tata zinazowakumba. Wahafidhina kama vile kuharibika kwa mazingira (kiangazi) na athari zake kwa jamii.
    8. Anaonyesha namna ubaguzi ulivyowaathiri Wahafidhina. Anaonyesha namna rasilimali za mataifa maskini zisivyowafaidi wenyeji bali hufaidi wawekezaji na baadhi ya nchi za kigeni.
    9. Anaendeleza ploti. Ridhaa anayakumbuka mazungumzo kati yake na Tila. Anaaangaza baadhi ya matukio ya awali.
    10. Kupitia kwake, tunaangaziwa unafiki wa baadhi ya wafadhili ambao husingizia kuwa wanasaidia mataifa maskini kujiendeleza ilhali wao ndio hunufaika zaidi (uk 44).
    11. Anadokeza changamoto wanazopitia wafanyakazi kwenye kampuni za kuchimbua madini. Wanadhulumiwa kwa kupewa ujira mdogo (uk 44).
     Hoja 5 x 1 (alama 5)
     Kutaja- 1
     Mfano-1
 4. SEHEMU C: HADITHI FUPI 
  1.        
   1. Msimulizi.
   2. Anamrejelea Dadi.
   3. Matukio yamo mawazoni mwa Msimulizi.
   4. Huu ni ulinganuzi wa hali ya maisha ya Dadi
   5. Baada ya kumchumbia Kidawa ambapo angekuwa na starehe ilhali ni kinyume
    (Dondoo limetolewa uk. 56)
  2. "Toni ya dhihaka/ stihizai
   Hoja 1 x 2
   alama - 2
   Kutaja-1 
  3.      
   1. Dhana kwamba Kidawa anayavunja masharti ya ndoa kwa kumwendea kinyume linamkera Dadi.
   2. Kidawa kumtia Dadi fedheha kwa kusimama na wanaume na kuamkiana na kuzungumza nao (uk 60).
   3. Tabia ya Kidawa ya kupenda fasheni hii na ile na mavazi.
   4. Tabia ya Kidawa ya kujipodoa akiingia ndani akirejea hata nyumbani. Mazoca ya Kidawa ya kujipodoa kila wakati yanamkera Dadi.
   5. Anavyovalia Kidawa. Hajitandi kikamilifu. "... asiyetaka kuziba uso wala kifua chake." (uk 60). Haya yanamtia hisia za kutojiamini Dadi.
   6. Mtazamo wa Dadi- kuonekana na jamii, kuwa amedhibitiwa na mke wake pamoja na hisia kuwa amedhibitiwa na Kidawa kikweli anapofanya kazi za nyumbani. Dadi hana utulivu kutokana na haya.
   7. Utukutu wa Kidawa ambao unamfanya Dadi kuchelea kumwambia shauku aliyo nayo akihofia kuwa Kidawa atamrejesha kwenye "Masharti ya ndoa ya kisasa." (uk 61)
   8. Dadi analisi kuwa "amejitia kitanzi' kwa kutia saini ya kukubali masharti ya kisasa. (uk 61), katika mkataba wa ndoa ya kisasa.
   9. Dadi ni intumwa wa mapenzi kwani licha ya madhila yote anayopitia, anakiri kuwa bado anampenda Kidawa na anahofia kuwa kuvunjika kwa ndoa kutamwathiri mno (uk 62).
   10. Dadi anadhihakiwa/anafanyiwa stihizi na baadhi ya wateja wake kama vile Bi. Zuhura anapomwuliza iwapo ana samaki wa kuuza au anao wa kwenda kumkaangia Bi. Kidawa (uk 62).
   11. Baadhi ya masharti yanamkera na kumhuzunisha Dadi kama vile kupata mtoto mmoja tu. (uk 61). (alama 14)

    Tanbihi 
    1. Misumari ya nyuki ni sitiari ya mambo yasiyopendeza jambo la kuhuzunisha/ jambo linaodhalilisha/ jambo la aibu 
    2. Maana ijitokeze ili mtahiniwa atuzwe alama kamili.
 5.            
  1.      
   1. Ubakaji - Sara alifanyiwa ukatili na janadume moja ambalo lilimbaka alipokuwa anatoka masomoni.
   2. Ubakaji unasababisha ujauzito wa kulazimishwa jambo ambalo Sara anahisi ni kuvunjiwa ujanajike na utu wake na kumharibja maisha.
   3. Ujauzito unachangia uozo mwingine wa kutengwa sio tu na marafiki bali na wazazi pia. Katika ujauzito wake, Sara anafikiri jinsi atakavyotengwa na kila mtu-wa karibu na wa mbali.
   4. Kuna ukandamiziaji wa jinsia ya kike. Sara anahisi kwamba alibakwa kutokana na imani ya jamii kuwa kiumbe mwanamke ni mnyonge. Anasema kuwa hata mama yake Sara anaudhika kuwa wanawake/wasio na nguvu wanazidi kudhulimiwa na wanaowadhulumu wanaachwa kunafasika. Aliyedhulumiwa ndiye anayaendelea kuathirika.
   5. Kuwaachia huru wabakaji/kutowaadhibu wanaowadhalilisha wanawake.
   6. Ulipizaji kisasi - Sana anaishi na chuki linalosababishwa na kubakwa kwake. Anania kulipiza kisasi. Angetaka kumnasa na kumwadhibu yule nduli aitwaye babake mtoto wake.
   7. Mauaji kutokana na watu kupigwa kitum. Badala ya kuchukua hatua za kisheria ya kuachia vyombo vya dola kukabiliana na wahalifu, jamii hii innchukua hatua mikononi mwake na kuwanyeshen washukiwa mvua ya matofali na kuwatia Bakaji linuwa na wahi wenye ghadhabu.
   8. Udaku - Ni jamii innyoshiriki umbea na udaku. Sara anachelea vile majirani wataanza kumsema watakapotambua kuwa ni mjamzito.
    Hoja 5 x 2
    Kutaja - 1
    Mifano - 1

    Tanbihi
    Hoja ijadiliwe kikamilifu na kutolewa mifano ili apate alama 2.
  2.           
   1. Wazazi wanawaclimisha watoto wao - Biti Kidebe alimpeleka skuli Mashaka. Hivyo kumpa mbinu za kujitegemea.
   2. Wazazi wanawalea watoto kwa kuwapa mahitaji ya kimsingi. Biti Kidebe alimlea Mashaka. Wazazi wanawafunza watoto uwajibikaji. Mashaka aliwajibika katika kazi mbalimbali ili kusaidia katika kuikimu familia.
   3. Wazazi wanapaswa kutoa ushajri na uelckezi kwa wana wao. Mastunki na Waridi wanajikuta wakishiriki mapenzi wakiwa wachanga bila ya kufahamu wajibu unaoandamana na tendo hilo na kuishia kulazimika kuoana wakiwa wachanga
   4. Wazazi wanawapa wana wao mbinuishi/ stadi za kukabiliana na maisha. Mashaka anajifunza shughuli za ukulima.
   5. Kufunza matumizi yafaayo ya raslimali ili kujikimu. Biti Kidebe na Mashaka wanalima vishamba vyao na kupata mahitaji ya kila siku.
   6. Kufunza umuhimu wa mahusiano mema ya kijamii umuhimu wa utubora. Biti Kidebe anamchukun nn kumlea Mashaka licha ya kuwa si mwana wake.
   7. Kufunza umuhimu wa kuuwekea msingi mustakabali wa maisha. Biti Kidebe anaweka akiba anayotoa ili kuwasaidia wakati wa upungufu.
   8. Wanawahimiza kudumisha mila na utamaduni. Mzee Rubeya na Shehe wanadumisha mila na utamaduni kwa kuwaoza Mashaka na Waridi wanapoanza kujiingiza katika mapenzi.
   9. Kuwasaidia wana wao wanapokabiliwa na matatizo. Waridi anarejea kwao na watoto wake ili kuauniwa wakati wa shida.
   10. Wanazorotesha hali ya maisha ya watoto wao kwa kuwaoza bila kufikiria mustakabali wao. Mashaka na Waridi wanaishia kukaa katika mazingira duni. Wanaomba nafasi kwa jirani ili watoto wao wapate mahali pa kulala.
   11. Wanawakosesha Wana wao usalama. Watoto wanalazimika kuchezea nje baba yao anaporejea nyumbani.
   12. Wanawadhalilisha watoto wao. Mashaka na Waridi wanaomba nafasi ya watoto mwao kulala huko kwa jirani.
    Hoja 5 x 2 -10
    Kutaja - 1
    Mfano - 1

    Tanbihi

    Hoja ijadiliwe kikamilifu na kutolewa mifano ili apate alama 2.
 6. SEHEMU D: USHAIRI
  1. Ujumbe
   1. Mtu mbaya/asiye na heshima hana msimamo
   2. Asiye na heshima huona aibu kwa kukosa heshima.
   3. Mtu mbaya/mwenye kukosa heshima anafaa kuepukwa.
   4. Mtu mbaya ukiwa na shida atakukimbia peupe ubaki kujuta.
   5. Mtu asiye na heshima hujiaibisha/hujidhalilisha kwa wengine..
   6. Asiye na heshima hawasaidii watu.
   7. Watu wa aina hii ni kawaida kuwapata.
   8. Mtu asiye na heshima ni hatari.
   9. Asiye na heshima habagui analonena( Hana heshima ya neno) alama 4
  2. Nafsiseni - Mshauri
   - Mwelekezi
   - Anayetahadharisha anayeonya
   - Anayetoa nasaha
  3. Uhuru wa kishairi ulivyotumiwa
   1. Miundo ngeu ya kisintaksia/kuboronga sarufi/ kufinyanga lugha - mfano wake tazama - tazama mfano wake kama popo mwendo wake - mwendo wake kama popo. Mshairi amebananga lugha ili kuleta urari wa vina
   2. Udondoshaji wa maneno ili kuleta urari wa mizani (Ubeti 2:1) ya ndege na wanyama, badala ya: ya ndege na ya wanyama.
    Hudai ndege wenzake - hudai ndege ndio wenzake.
   3. Ufupishaji/inkisari ili kuleta urari wa mizani kamaye-kama yeye (Uvel 2:4).
   4. Urefushaji/mazida ili kuleta urari wa mizani / vina hanayo - hana (Ubeti :2); hutendekana - hutendeka (Ubeti 5:3).
    Mifano 3 x 2 = 6
    Kutaja -1
    Umuhimu - 1
  4. urudiaji ulivyotumiwa 
   1. Undiaji (takrii) wa sauti k v. (ke), kuwa alama ya kipumnuo cha shairil kulipa shairi muonjo wa kimuziki.
   2. Urudiaji wa maneno heshima, hiana kutilia mkazo hoja husika/kusisitiza.
   3. Usambamba - miundo inayofanana wa kisintaksia inaturniwa kuleta mvuto katika shairi.
    Hana masikilizano Uheti 2-3
    Hana heshima ya neno Ubeti 3:3
    2 x 2 = 4
    Kutaja-1
    Dhima-1
  5. Tamathali za usemi katika ubeti wa kwanza na wa pili.
   1. Tashbihi - Scama popo mwendo wake (Ubeti 1:2).
   2. Uhaishaji – siku ya ndege na wanyama kupatana (2:1).
    2x1 = 2
    Kutaja½
    Mfano½
  6. Ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari
   Mtu mwenye hiana ni mbaya na ukiwa naye utajilaumu.flitokea kwamba dunia itakutatiza / mtu huyo atakutupa mchana peupe/Haya ni mambo yanayotupata na yanayotendeka.
 7.      
  1.      
   1. Analetea mazingira.
   2. Mito kuchafuliwa na watu wanaofanyia usafl huko.
   3. Hakuna kilicho safi.
   4. Watu hupitia mto uliochafuliwa bila kujali.
   5. Mto kusafishwa siku moja ili kuufanya mji upendeze
   6. Tunahitajika kutetea uhifadhi wa mazingira-Ningekuwa mimi ningepaza sautipunguzeni bughudha.
   7. Linakashifu unafiki watu kuukosha mji mwakani na hali hawajali kuuhifadhi mto. 
   8. Linalalamikia ukosefu wa uwajibikaji watu wanaubebesha mto uchafu ili wenyewe wapate kuwa safi/ wanaelekeza uchafu kwemye mto.
    Hoja 5 x 1 = 5 (alama 5)
  2.       
   1. Miundo ngeu ya kisintaksia/ Kuboronga sarufi/Kubananga lugha - makubwa kushuhudia-kushuhudia makubwa
   2. Inkisari - Safika kusafika
    Hoja 2 x 1 =2 (alama 2)
  3.      
   1. Tashihisi - Mto kuona mengi, mto kushuhudia makubwa, mto kutambaa, mto kuwa kimya, mto kuoshwa.
   2. Swali la balagha-Hamjui mto husafisha dhambi?
    Mto hukoshwa kwa sabuni?
   3. Kinaya
    • Kufumbia jijp macho.
    • Kufanyia usafi mtoni huku wakiuchafua. 
    • Kufanyia usafi mto huku nia yao ikiwa kuufanya mji upendeze. -
    • Kufanya usafi wa mto wa siku moja.
    • Mto kuona mengi hali hausemi chochote. 
    • Mto unaoshwa badala ya wenyewe kutakasa dhambi.
     Hoja 3 x 1 = -3 (alama 3)
  4.        
   1. Urudiaji neno - mto, jiji
   2. Usambamba - Wanaolivuka bila fahamu
    Wanaolima bila kujali
  5. Nafsineni
   1. Mtetezi wa mazingira
   2. Anayelalamikia uchafuzi wa mazingira
   3. Mtetezi wa usafi wa mto
   4. Anayepinga uchafuzi wa mazingira/mto 
   5. Mtu wa kizazi cha sasa.
  6.      
   1. Mwendo - utambao, wanaolivuka, kilichopita
   2. Uoni - wahalifumbia macho.
    - nionavyo
    - ulioona
   3. Hisi - nalilia mazingira
   4. Usikivu – ningepaaza sauti (alama 3)
  7.    
   1. Kulalamika - nalilia mazingira yetu/hakuna kilicho safi.
   2. Dhihaka/kubeza najua mwakani
    Hoja 1 x 2 (alama 2)
  8. Najua kwamba watakuja mwalcani kuusafisha mto kwa siku moja la madhumuni yao ni kuufanya mji upendeze/wala si kuusafisha mto.
   Hoja 4 x 1/2 (8)
 8. SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
  1.          
   1. Hurafa - wahusika wanyama
    Mfano - 1
   2.          
    1. "Dayolojia za wahusika-Sungura anazungumza na Nungunungu.
    2. Uzungumzi nafsia - Nungunungu anajisemea- Simtarajii ndugu yangu huyu aniendee kinyumel.
    3. Swali la balagha - Itatokeaje anisaliti baada ya muda wote huu?
    4. Kuzungumza moja kwa moja na hadhira ili kuibua taathira ifaayo - Basi mjukuu wangu.
    5. Upenyezi wa mambaji - Unajua tena mjukuu wangu kauli za mwenye hila haziaminiki.
    6. Chuku -maghala yalishiba yakatapika nafaka.
    7. Tashihisi – kiangazi kilizidi kung'ata.
    8. Matumizishirikisha hadhira kwa kuuliza maswali- Mjukuu wangu ingekuwa wewe ungemfanyia nini rafiki yako huyu wa dhati?
    9. Matumizi ya lugha sahili
    10. Matumizi ya fomyula ya ufunguzi na ya kuhitimisha/ tamati. 
    11. Taharuki/lugha inayojenga taharuki. 
    12. Muundo sahili wa hadithi. 
   3.          
    1. Ukulima - Nungunungu alikuwa na nafaka/maghala ya nafaka.
    2. Uwindaji - Fisi anamezwa na msitu kutafuta mizoga/anajiulia.
    3. Ufugaji - Mbuzi wangu wale majani mabichi/kumiliki mbuzi.
     3 x 1 = 3
   4. Umuhimu wa fomyula ya mwisho
    1. Kuashiria mwisho wa ngano.
    2. Kuitoa hadhira kwenye ulimwengu wa fantasia hadi ulimwengu halisi.
    3. Kuonyesha niwisho wa mgogoro/suala linaloangaziwa. Fisi anaishikwa.
    4. Ni kitulizo kwa hadhira-imejua hatima ya fisi - ameadhibiwa.
    5. Kusawiri jamii ambamo utungo unapatikana - ni wafugaji.
  2.        
   1. Kuirithisha fani yenyewe ya utambaji kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
   2. Kukifanyia utafiti ili kubainisha sifa za uwasilishaji wazo na kuzihifadhi.
   3. Kuzihifadhi kwenye maandishi.
   4. Kujifunza/shuleni 
   5. Kuzitamba mara kwa mara.
   6. kuzihifadhi kwenye video ili kuhifadhi sifa za uwasilishaji kama vile sauti/kidatu, na miondoko 
   7. Kutafitia vyanzo vya kudidimia kwazo ili kuvidhibiti/ kvitatua.
   8. Kuandaa mashindano ya utambaji wa ngano ili kurithisha utambaji wazo kutoka kizazi hadi kingine/ kuwafanya vijana wavutiwe nazo.
   9. Kufadhili utafiti kuhusu ngano.
   10. Kushirikisha wageni waalikwa katika ujifunzaji wa ngano/ kuzifunza kwa mitindo anuwai ili kuwafanya wanafunzi wavutiwe nazo, na kuziendeleza.
   11. Kuzitumia kufunzia masomo mengine na stadi nyingine kama vile kusikiliza na kuzungumza
   12. Kuandaa vipindi vya redio au runinga na kuwaalika mafanani stadi kutamba ili kuwa vielelezo.
    5x1=5
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - KCSE 2021 Past Papers.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?