KISWAHILI KARATASI YA 2 Marking Scheme - 2019 KCSE Prediction Majibu Set 1

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU
    1. Taja kichwa mwafaka cha makal haya
      • Chanzo na madhara ya ufisadi (1×2 = 2)
    2. Eleza kiini cha zimwi linalozungmziwa katika makala haya
      • Ubepari - watu kumiliki kila kitu
      • Wafanyakazi kutolipwa vizuri hivyo kutafuta njia mbadala ya kutosheleza mahitaji yao
      • Serikali kutovalia njuga swala hili
      • Watu kuongozwa na tamaa (4×1 = 4)
    3. Thibitisha kwamba ufisadi ni 'kidonda ndugu'
      • Kulemaza utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi
      • Usalama kudorora kwa sababu polisi wanashirikiana na wahalifu
      • Wanachi wengine kutoajiriwa kwa kutoa hongo
      • Kukosa wawekezaji hivyo uchumi kuathirika (4×1 = 4)
    4. Eleza namna uchumi umelemazwa kwakuwepo ufisadi
      • Serikali kukosa ushuru
      • Wawekezaji kutofika/kukwepa nchi (2×1 = 2)
    5. Toa maana ya 
      1. Utashi - tamaa/hiari ya kutendo/hamu ya kutaka/shauku
      2. Kadhongo - hongo/mlungula
      3. Kutovalia njuga - kupuuza/kutofuatilia jambo kwa makini (3×1 = 3)
  2. UFUPISHO
    1.  
      • Watoto wa maskini hushinda njaa shuleni
      • Walimu wao hwana ari ya kufunza kutokana na mazingira mabovu ya kufanya kazi
      • Watoto hawa huvaa matambara yenye viraka
      • Tatizo hili limetokana na utandawazi na mfumo wa soko huru unaoruhusu shule za kibinafsi kuendeshwa kibiashara
      • Shule za kibinafsi zina mazingira na vifaa vya kutosha
      • Asilimia kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na shule za upili hutoka shule za kibinafsi ambazo huendeshwa kibiashara
      • Juhudi za wizara ya elemiu hazijafua dafu/matajiri wajanaj husajili watoto wao katika shule za mashambani
      • Shule za kibinafsi huwa na idadi ndogo ya wanafunzi/makundi madogo madogo ya wanafunzi
      • Nafasi zote katika shule za upili za kitaifa na vyuo huchukuliwa na watoto wa matajiri. 
      • Nafasi ya mtoto maskini inazidi kudidimia (7×1 = 7)
    2.  
      • Mikakati ya kimakusudi inahitajika kabla ya balaa kuzuka
      • Ujenzi wa shule vielelezo unahitajika katika kila wilaya/gatuzi
      • Shule za umma ziwe na mpango wa lishe bora
      • Utu unahitahika katika uteuzi wa wanafunzi katika ngazi mbalimbali
      • Shule za umma zinahitaji walimu na madarasa ya kutosha
      • Kuanzishwa kwa mpango lazima wa elimu bila malipo katika shule za msingi
      • Sera kuhusu shule za chekechea lazima izinduliwe kitaifa
      • Shule za malezi ziwe za viwango sawa ili kila mtoto awe na msingi bora wa elimu/maandalizi sawa
      • Mitaala yetu ilenge kuzalisha binadamu ambaye atajinufaisha yeye kibinafsi na taifa kwa jumla (6×1 = 6)
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Nyumba yake haina milango mikubwa wala mapambo mengi (2×1 = 2)
    2.  
      • Mtoto wa mrejelewa ndiye mnunuzi wa ng'ombe/badala/niaba yake
      • Alinunua ng'ombe na ndama
      • Alinunuliwa n'ombe na mtoto wa mrejelewa (mtoto wa mtu)
      • Alinunuliwa ng'ombe kwa gharama ya ng'ombe na mtoto wake
      • Yeye na mtoto wake walinunuliwa ng'ombe
    3. S → KN + KT
      KN → N + S
      N → Wanafunzi
      S → Wasiofuata maagizo
      KT → T + KN
      T → Watapata
      KN → N+ S
      N → alama 
      S → ambazo zitawaudhi
    4.  
      1. Ni maneno ya kuliwaza; pole
      2. Mtu anayekabiliwa na tatizo au kasoro fulani na hana nia ya kujinasua kwayo au mtu anapewa uwezo/talanta asiyohitaji
    5.  
      1. Kirai ni fungu la maneno ambalo hudokeza maana lakini maana hiyo si kamili au fungu la maneno lisilo na uhusiano wa kiima na kiarifu
        Au 
        Fungu la amaneno ambalo haunishwa kwa kuzingatia neno lake kuu. K.m. Kivumishi ndilo neno kuu katika kirai kivumishi
      2. Wale wasichan watundu - kirai nomino
        chini ya - kirai kihusishi
    6.  
      • Sentensi amrishi/agizi/sharuti
      • Sentensi za rai/ombi
      • Senetensi za sharuti/masharti
      • Sentensi hisishi (atoe mfano wa sentensi - aina ½ mfano ½)
    7.   
      1. "Mtakaporudi nyumbani ogeni(muoge), mle halafu muanze kusoma punde tu badala ya kupoteza wakati wenu kwa kutazama vipindi vya runinga." Mwalimu aliwaambia wanafunzi wake. "Tena wanaofanya maonyesho kwenye runinga tayarai wamefuzu vyuoni na wameajiriwa kazi." (1/3 ×12 = 4)
      2. Mwalimu aliwaambia wanafunzi wake, "Mtakaporudi nyumbani, mwoge, mle halafu muanze kusoma punde tu badala ya kupoteza wakati wenu kwa kutazama runinga. Tena wanofanya maonyesho kwenye runinga tayari wamefuzu vyuoni na kuuajiriwa kazi" (1/3 ×12 = 4)
    8. Tulipokiona kilikuwa kikisoma kitabu (½ × 4 = 2)
    9. Kiambishi -KI
      • Kunuesha udogo kwa mfano;- kijitu
      • Ngeli ya KI-VI (KI-umoja VI - wingi)
      • Kiambishi cha mfananisho kwa mfano: Anakula kifisi
      • Kuonyesha kitendwa kwa mfano: Alikitoa
      • Ukanushi kwa mfano: hakuendeki
      • Vitendo viwili wakati mmoja kwa mfano : Alikuwa akipika, yeye akiosha nguo (½ × 2= 1)
    10. Kiambishi - KU- 
      • Kitenzi nomino/ngeli kucheza
      • Upatanisho wa kisarufi - kulitufurahisha
      • KU - mahali kusikodhihirika - huku
      • Ukanusho wa wakti uliopita - hakufurahi (½ × 4= 2)
    11. Kishazi tegemezi ni kishazi ambacho hakiwezi kutoa maana iliyokusudiwa kikiwa peke yake. Hutegemea vishazi vingine ili kuleta maana. Kwa mfano, Kazi ilipofanywa, alifurahi
    12. Mgeni anatuandalia chakula sasa hivi (2× 1 = 2)
    13. Mshazari/mkwaju
      • Katika uandishi wa kumbukumbu - kumb 2/7/17
      • Kuonyesha visawe - aila/familia
      • Kaudnika tarehe - 28/02/1992
      • Kuonyesha au/ama - kisu/kijiko (2× 1 = 2)
    14.  
      1. Mofimu ni kipashio kidogo zaidi cha lugha chenye uamilifu wa kisarufi (1× 1 = 1)
      2. A-li-kimbi-li-a
        li-wakati uliopita
        li- kauli ya kutendea
    15.  
      1. Shadda ni mkazo unaotiliwa kwenye silabi ya neno ili kuleta maana fulani au nguvu inayotumika katika utamkaji was silabi
      2. Kata'kata - kuwa vipande vipande
      3. 'Katakata - kabisa kabisa (nahau)
    16. Vitate
      1. Vuka - toka upande mmoja hadi upande wa pili; kiuka
      2. fuka - toa moshi; uji mwepesi unaopewa mwanamke aliyejifungua.
        kwa mfano , Alivuka mto ili kuelekea ng'ambo alipoona nyumba yake inafuka moshi (2× 1 = 2)
    17. Shirika
      Kwa mfano, wafanyikazi wa shirika(N) hili hufanya kazi kwa ushirika (E) ili wafanikiwe (2× 1 = 2)
    18. nomino dhahania
      -cha: uchaji
    19. /ch/ - kipasuo-kikwamizo/kizuio-kwamizo
      -hafifu/sighuna
      -kaakaa gumu (2× ½ = 1)
  4. ISIMU JAMII
    1. Kiswahili ni kibantu
      • Kiswahili kina irabu tano kama zilivyo lugha zingine za kibantu
      • Muundo wa msamiati wa Kiswahili huchukua mtindo wa: Konsonanti Irabu (KI)
      • Mpangilio wake wa nomino hukitokeza katika lugha nyingine za kibantu
      • Wageni waliita upwa wa Afrika Mashariki sahili - wingi wake siwahili
      • Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa wasafiri wa kale kama Ibn Batuta wamnukuliwa kutaja majiana ya Kiswahili kama 'Mkono wa tembo', kisukari, majina haya hata sasa yanatumika
      • Kutokana na maoni ya fasihi simulizi, asili ya Kiswahili ni Kiongozi. Mashairi ya Hamziya yaliyoandikwa katika karne ya 18 yaliandikwa kwa kingozi
      • Jamii nyingi za waafrika zina koo zao. Halikadhalika Waswahili wana jamii zao ambazo huunda jamii kubwa ya Waswahili. Kwa mfano, wabarawa, Wasiu, Wangazija na Wajomvi (4× 1 = 1)
    2. Istilahi katika Isimu Jamii
      1. Uwili lugha na ujozi lugha
        Uwili lugha ni uwezo wa kujua na kutumia lugha mbili
        Ujozi lugha - Uwezo wa kujua na kutumia lugha mbili sawia. Umilisi wa lugha mbili katika viwango sawa
      2. Lafudhi na Lahaja
        Lafudhi ni upekee wa matumizi ya lugha ya mtu binafsi
        Lahaja ni vijilugha mbali mbali vya lugha moja
      3. Sajili na msimbo
        Sajili ni matumizi ya lusha katika mazingira/miktadha maalum
        Msimbo ni utaratibu wa kutoa mawasiliano (2× 3 = 6)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 2 Marking Scheme - 2019 KCSE Prediction Majibu Set 1.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest