KISWAHILI KARATASI YA 2 - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

 

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali uliyopewa

    Kila mmoja wetu anafahamu jukumu muhimu linalotekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali almaarufu kama NGOs katika shughuli ya kuleta maendeleo muhimu humu nchini.
    Ni dhahiri kuwa maendeleo mengi ambayo tunajivunia kama jamii - hasa katika sehemu za mashinani - yametekelezwa na mashirika haya ambayo hufadhiliwa na serikali na mashirika ya kigeni. Sio tu miradi ya kupambana na ugonjwa hatari wa Ukimwi, maji ya kunywa, kilimo, ufadhili wa kimasomo n.k, bali hata inayohusu uhifadhi wa mazingira.
    Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kuwa ingawa mashirika haya yanajivunia kutekeleza mengi, maendeleo ni machache mno ikilinganishwa na kiasi cha pesa ambacho kimetolewa na wafadhili. Madai yaliyotolewa na wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu nchini majuma kadhaa yaliyopita kuwa walaghai wa kitaalamu wameingia sekta hii kuwapora wafadhili pesa zao yana ukweli fulani.
    Kuna mbinu kadhaa ambazo zinatumiwa na mashirika laghai kuwapora wafadhili pesa zao. Mbinu ya kwanza ni kupitia uandishi wa mapendekezo ya miradi isiyokuwepo. Mengi ya mapendekezo hayo huandikwa kwa lugha ya mvuto kuwashawishi wafadhili watoe fedha zao. Kuna uwezekano umewahi kukutana na wasomi waliobobea katika taaluma ya kuandika mapendekezo ya miradi kwa malipo. Hao ndio wajuao mambo ya kujumuishwa kwenye mapendekezo ya miradi ili kuwateka wafadhili. Kile wafanyacho ni kuandika mapendekezo na baadaye hupewa sehemu yao ya pesa hizo punde zinapotolewa.
    Njia ya pili sio wizi wa wazi kwani huhusisha matumizi ya pesa kwa njia ambazo hazikukusudiwa. Badala ya kutumia pesa za wafadhili kutekeleza miradi ya maendeleo iliyopendekezwa, baadhi ya wasimamizi wa mashirika haya huweka pesa mifukoni mwao.
    Viongozi wa mashirika mengine hutumia ufadhili huo kuzuru mataifa ya kigeni kwa kisingizio cha kuhudhuria makongamano ya maendeleo. Baadhi yao huwa hawaendi mbali; wao huandaa makongamano ya kukata na shoka kila mwezi katika hoteli kubwa kubwa nchini. Kinaya kilioje kuwa pesa zilizotafutwa kusaidia wajane katika vijiji vya mashambani zinatekeleza miradi bandia mijini? Inasemekana miradi ya baadhi ya mashirika hutekelezwa kimaandishi tu na maafisa wanaosimamia mashirika haya bila kuwahusisha waliolengwa.
    Isitoshe, baadhi ya mashirika haya hutumia nyingi ya pesa zake kwa masulala ya utawala na usimamizi badala ya miradi ya maendeleo

    Maswali
    1. Taja jukumu muhimu linalotekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali.  (alama 2)
    2. Ni miradi ipi ambayo imetekelezwa na mashirika haya?    (alama 5)
    3. Ni kwa nini maendeleo ambayo yametekelezwa na mashirika haya ni machache?   (alama 2)
    4. Ni mbinu zipi zinazotumiwa na mashirika laghai kuwapora wafadhili pesa zao?  (alama 4)
    5. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kifunguni. (alama 2)
      1. walaghai
      2. kuwapora
  1. MUHTASARI (ALAMA 15)

    Mfumo wa elimu wa 8.4.4 ulipoanzishwa nchini mnamo 1983, lengo kuu lilikuwa ni kuwapa wanafunzi maarifa ya kielimu hasa ya kiutendakazi ili kuwawezesha kijitegemea baada ya kumaliza masomo. Hata hivyo, wakosoaji wa mfumo huu wanasema kwamba yaliyomo kwenye mtaala ni mengi mno na kwamba mtaala wenyewe ni mzigo mzito kwa wanafunzi kando na kuegemea mno mitihani.
    Hata baada ya kupunguzwa kwa idadi ya masomo ya kutahiniwa kwenye mfumo huu, mambo yalikuwa changamano zaidi wakati serikali ya NARC ilipoingia mamlakani na kuanzisha mfumo wa elimu ya msingi bila malipo mnamo 2003. Hatua hiyo ilisababisha idadi ya wanafunzi waliojiunga na shule za msingi kuongezeka maradufu-kutoka wanafunzi milioni 5 hadi wanafunzi milioni 8 mnamo 2009.
    Licha ya kwamba mfumo wa elimu ya msingi bila malipo umesifiwa hapa na pale, wadadisi wa mambo hata hivyo wanatilia shaka masuala fulani kuuhusu. Mojawapo ya masuala haya ni viwango vya ubora wa elimu wanayopata watoto wetu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya Uwezo Kenya mnamo Oktoba mwaka 2009, ilibainika kwamba mwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi wanne katika kiwango cha shule ya msingi hufika katika darasa la tano bila ya kuwa na uwezo wa kujibu maswali ya masomo ya mwanafunzi wa darasa la pili.
    Pamoja na hayo, uchunguzi huo ulibainisha kwamba takriban asilimia nne ya wanafunzi chini ya mfumo wa elimu ya msingi bila malipo husoma na kukamilisha masomo ya darasa la nane bila kupata maarifa ya kimsingi ya kusoma na kuandika au hata ujuzi wa kufanya hisabati za kimsingi
    Hatua ambazo zimekwisha kuchukuliwa na serikali mpaka sasa-hasa ujenzi wa madarasa na amara ya kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya wanafunzi katika mfumo wetu wa elimu-hazijafanikiwa sana.
    Aidha, ingawa serikali imeamua kuwaajiri walimu kwa mpango wa kandarasi, ili kukidhi nakisi ya takriban walimu 60,000 katika shule za msingi na upili, hatua hizo bado hazijatatua lolote!
    Hali hii imesababisha uwiano kati ya mwalimu na wanafunzi kuwa 1:80 katika baadhi ya sehemu nchini na kufanya walimu kushindwa kutoa huduma bora kwa kila mwanafunzi. Katika hali ya kawaida, mwalimu mmoja anapaswa kuwafundisha wanafunzi kati ya 35 hadi 40. Hii inamaanisha kwamba mwalimu mmoja hushughulika idadi maradufu ya kiwango kilichoidhinishwa kote ulimwenguni. Katika mazingira kama haya, inakuwa vigumu mno kwa mwalimu kufundisha na kuwaridhisha wanafunzi-hasa wale ambao si wepesi wa kushika mambo.
    Kuhusiana na vifaa vya kufundishia, bado kuna mushkili hasa ikichukuliwa kwamba kashfa iliyowakumba Waziri wa Elimu, Prof. Sam Ongeri, na aliyekuwa katibu katika wizara hiyo, Prof. Karega Mutahi, haikusuluhishwa. Kwenye kashfa hiyo, fedha zilizonuiwa kununua vifaa kama vile vitabu au kugharimia mpango wa elimu bila malipo zilitoweka kwa njia ya ajabu sana.
    Hivi sasa, serikali imekaa tutwe huku watoto wetu wakiumia shuleni kana kwamba hakuna lolote lililotendeka. Shule nyingi hasa za msingi zina maktaba zilizojaa vitabu vya kiada. Hali hii bila shaka haiwachochei wanafunzi kuwa na msukumo wa kusoma kwa lengo la kujua mambo, husoma ili kupita mitihani tu. Utamaduni wa kusoma nchini unatiliwa shaka sana na hatujui ni lini utakapoimarika.
    Watoto wanapaswa kukuzwa katika mazingira ya mfumo wa elimu unaothamini kusoma kwa minajili ya kupata maarifa na kupanua mtazamo wao, kinyume na sasa ambapo wanafunzi wanaotia fora katika mitihani hawajui chochote nje ya mitihani hiyo.
    Tangu 2001, wadau katika sekta ya uandaaji na uchapishaji wa vitabu nchini Kenya, Uganda na Tanzania chini ya mwavuli wa Mradi wa Ustawishaji wa Vitabu Afrika ya Mashariki wamekuwa wakifanya juhudi za kimakusudi za kukuza na kupalilia utamaduni wa kusoma.
    Nina wasiwasi kwamba kutokana na mlipuko wa ‘teknohama’ kote ulimwenguni, huenda watoto wetu wakaweka vitabu pembezoni na kushabikia mtandao wa intaneti na runinga badala ya kuchangamkia vitabu, majarida, magazeti na maandishi mengine kwenye karatasi.

    Maswali
    1. Eleza kasoro za mfumo wa 8.4.4 kulingana na kifungu. (Maneno 25)    (alama 4)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Mfumo huu wa elimu ya msingi bila malipo unatiliwa shaka kwa sababu ya mambo kadhaa. Fafanua.   (Maneno 75) (Alama 11, 2 za mtiririko)
      Matayarisho
      Jibu
  1. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Ukirejelea mkondo wa hewa kutoka mapafuni, eleza sifa za kimatamshi za ving’ong’o.(alama 2)
    2. Kwa kuzingatia sehemu zilizopigiwa mstari, toa dhana inayojitokeza katika sentensi hii. (alama 2)
      Alisugua meno, akaoga akala kisha akaondoka.
    3. Tumia neno vile kama       (alama 3)
      1. Kivumishi
      2. Kiwakilishi
      3. Kielezi
    4. Yakinisha sentensi hii.  (alama 1)
      Kanisani simo wapatikanapo wezi.
    5.  
      1. Andika sentensi hii katika kinyume.  (alama 1)
        Mvua iliponyesha baba alienda kondeni.
      2.  Andika hali ya ukubwa wingi.  (alama 2)
        Nyoka yule alimuuma mtoto mkono.
    6. Tunga sentensi moja kudhihirisha kihusishi cha ‘na’ ya mtenda. (alama 2)
    7. Onyesha dhana mbili zinazojitokeza baada ya kitenzi kunyambuliwa katika kauli ya kutendeka.    (alama 2
    8. Eleza matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mstari.   (alama 2)
      Amkeni mwende dukani!
    9. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.   (alama 2)
      Kasisi alitushauri, “Yafaa tamaduni ambazo hazitufai ziachwe”.
    10. Tumia kitenzi ‘alikuwa’ katika sentensi kama
      1. Kitenzi kisaidizi.   (alama 1)
      2. Kitenzi kishirikishi kikamilifu.   (alama 1)
    11. Tofautisha sentensi hizi.   (alama 2)
      1. Ningalimwona jana ningalifurahi
      2. Ningemuona jana ningefurahi
    12. Kwa kuzingatia sehemu iliyopigwa mstari, toa maana inayojitokeza.
      1. Wao huenda msikitini kila ijumaa   (alama 1)
      2. Watoto wacheza   (alama 1)
    13. Tambua chagizo katika sentensi hii.(alama 1)
      Yeye huchapwa na mkewe mara kwa mara.
    14. Weka shadda katika maneno haya.  (alama 1)
      1. Mtoto                                                                                                                                   
      2.  Mto                                                                                                                                      
    15.  Huku ukitoa mfano eleza maana ya
      1. Silabi wazi  (alama 1)
      2. Silabi funge   (alama 1)
    16. Nyambua vitenzi hivi katika kauli ya kufanyiza.
      1. Jua       (alama 1)
      2. Kana    (alama 1)
    17. Onyesha viambishi katika sentensi hii.     (alama 3)
      Nitamtafutisha
    18. Tunga sentensi moja kuonyesha maana ya maneno haya
      1. Figo         (alama 1)
      2. Pigo         (alama 1)
    19. Pambanua sentensi hii ukitumia kielelezo matawi.
      Japo alifanya kazi zote hakulipwa.    (alama 3)
    20.  Tunga sentensi ukitumia ‘O’ rejeshi ya tamati.   (alama 1)
  1. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Eleza mitazamo miwili kuhusu chimbuko la lugha ya kiswahili nchini Kenya.    (alama 2)
    2. Eleza mambo manne yaliyochangia kuenea kwa lugha ya kiswahili zama za ukoloni.    (alama 8)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 2 - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest