KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 MASENO MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Jibu maswali yote.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa Kiswahili.
 1. UFAHAMU (Alama 15)
  Soma makala yafuatayo kwa makini kasha ujibu maswali yanayofuatia.

  Katika afisi yake moja alimfuma mpiga taipu akimwambia karani mwingine, “…..kamnyoa yule yatima shilingi zake elfu mbili maskini……..” Lakini maongezi yalikatika kwa kutokeza Salma, na Salma hakutaka kuambiwa nani ‘kinyozi’.
  “Yupo?” aliuliza.
  “Ke – keshaoondoka, bibi,” alibabaika mpiga taipu,
  “Kuelekea afisi ya kati.”
  Salma naye alielekea afisi ya kati. Huko pia mlango wa ofisi yake aliukuta umefungwa, na watu kadha wakimsubiri nje.

  “Ameitwa na mheshimiwa waziri, tafadhali kaa umsubiri bibi, “Mwandishi alimwambia Salma, na Salma akapweteka juu ya kiti pamoja na wengine kumsubiri Karim.
  “Je, umesikia mambo hayo?” Sauti ilinong’ona karibu na Salma, miongini mwa watu waliokuwa wakisubiri na kumfanya Salma atege sikio. “Usifanye mzaha, mjomba wangu kofutwa shilingi mia nane ndipo alipopewa waraka wa nyumba yake. Mzee mmoja jirani yangu kasumbuliwa we-e-e, hata na kutahamaki kupanguswa haki yake yote. Na wangapi! Na wangapi! Basi na weye jihadhari.
  “Yatakwisha hayo! Hoja umoja wetu,” mtu mmoja alieleza.
  “A – a – a ! Na hawa wanaodhulumiwa haki zao hufanyaje?” sauti nyingine iliuliza.
  “Wanalo?” ilijibiwa. “Labda humjui mtu huyu weye. Mkuu wa polisi nduguye kwa baba na mama, Mwenyekiti wa sheria baba yake mdogo, Jaji Mkuu mtani wake – haya tena, pangupakavu atapita wapi….?”

  “Hakuna pa kupita,” Salma alijibu rohoni mwake, yeye akiwa ndiye mwenye kumjua kuliko wote. Hali kadhalika, Salma alijua kuwa pengine Karim hatarejea siku ile, na hata angerejea kauli yake isingerudi nyuma. Akiwaacha wale watu wakijadili juu ya haja iliyopo ya mabadiliko kwa nchi nzima iliyojaa dhuluma, Salma aliona afadhali aende tena kwa mama yake akamjaribu, ingawa tama haikuwapo.
  Alipoingia Mbiju na gari lake jekundu, alimkuta mamake na birika mkononi akitilia maji bustani yake ya maua, kavaa kanzu nyepesi, ya kukokota, rangi ya bahari. Alionesha mtu mzima tena, ingawa umalidadi ulimpa nuru.
  “Karibu,” alisema huku akizungusha birika katika shina la mwasumini. “Leo pia hukumleta Karim.”
  “Kashunghulika na makazi yake,: Salma alisema, mkono wake mmoja mfukoni na mwingine kashika mkoba wake uliokuwa ukining’inia chini ya ukwapa.

  “Haijambo wewe unanikumbuka kuliko Samir huko Ulaya. Hupita miezi sita hajaniletea barua, na anapoleta huwa kashikwa na haja. Hiyo huko ndani ya baraua yake, nimeipata jana, anataka shilingi elfu kumi. Ikiwa barua zenyewe za kutaka mapesa tu amhonge huyo kafiri wake wa kizungu, afadhali asiniletee,” Bibi Adila alisema huku akikung’uta birika tupu chini ya shina la mwaridi. Laiti angelizitaka yeye mwenyewe ningempelekea japo nusu yake, lakini haja hizo zimeanza tangu kupambana na huyo kafiri wa Kizungu; anazitaka amhonge Mzungu wake, na sisi atufanye mahayawani kama yeye sipekeleki hata senti moja.

  Salma ambaye hapo kabla hakuwa na tamaa ya kupata mradi wake, sasa alivunjika moyo kabisa kabisa kwa maneno ya mama yake. Samir, mwana mpenzi kuliko wote, atanyimiwa alichotaka, seuze yeye Salma ambaye miezi miwili iliyopita alipewa shilingi elfu tatu.
  (Unukuzi kutoka Nyota ya Rehema, S. A. Mohamed)
  1. Kwa kurejelea muktadha wa ofisini, fafanua aina sita za mabadiliko yaliyohitajika nchini kwa mujibu wa masimulizi haya. (Alama 6)
  2. Thibitisha kwamba Salma hakuwa mgeni katika ofisi ya kwanza aliyozuru. (Alama 3)
  3. ‘Haijambo wewe unanikumbuka kuliko Samir’. Fafanua jinsi kauli hii haikuwa na ukweli kwa kumrejelea Salma. (Alama 2)
  4. Taja mambo mawili yaliyomkatisha tamaa Salma kuhusu ufanisi wa ombi aliloendea kwa mama yake. (Alama 2)
  5. Kwa kuzingatia maana katika kifungu, andika vinyume vya matumizi ya lugha yafuatayo: (Alama 2)
   1. Kutahamaki
   2. Pangupakavu
 1. UFUPISHO (ALAMA 15)

  Mikopo ni njia mojawapo inayotumiwa na watu wengi kwa lengo la kujiendeleza na kujikuza kiuchumi na kwa hivyo kukopa ni jambo lisilokwepeka. Mikopo inakubalika katika mataifa yote ya ulimwenguni na kwa sababu hiyo, mathalani serikali nyingi hurasimisha ardhi za wananchi kwa ajili ya kutumika katika kukopa kutoka kwenye taasisi rasmi. Kutokana na uzoefu, na labda urahisi wa namna fulani, watu wengi hupendelea mikopo isiyo rasmi inayopatikana kwenye mikoba na vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa.

  Ikumbukwe kwamba haiwezekani kupata mkopo wa pesa kutoka kwenye taasisi rasmi bila kulipa deni. Ili kuonyesha uaminifu wake na uhakika wa kurejesha fedha za wenyewe, mkopaji hulazimika kuweka rehani nyumba, hatimiliki ya ardhi, mshahara wake kama yuko kwenye ajira rasmi au mali yake nyingine yeyote kama gari. Hii huwa ndiyo dhamana ya mkopo wake. Dhamana hii husimama kama mbadala wa mkopo ili kulipa deni taraa mkopaji atashindwa kurudhisha fedha alizokopa.

  Watu wanaokopa mikopo wanaweza kukumbwa na hatari mbalimbali kutokana na kulemewa na kulipa madeni yao. Kushindwa kusimamia biashara au miradi wanayoanzisha kwa mikopo hiyo ni miongoni mwa hatari hizo. Wanaoshindwa kudhibiti biashara au miradi yao hukosa kupata fedha za kulipia madeni yao kwa sababu ya kuhasirika. Aidha baadhi ya wakopaji huwekeza kwenye miradi isiyozalisha faida na kwa hivyo mtaji wao unamomonyoka na hata kumalizika kabisa na kwa hivyo wanapata hasara mara mbili, ya kupoteza mtaji ambao ni mkopo na kukosa fedha za kulipa mkopo wao. Kuna baadhi ya watu wanaoomba mikopo na kwenda kuitumia katika anasa na starehe na kuishia kufilisika. Hawa ni wakopaji ambao hukopa bila mpango. Ole wao wanaoomba kwa njia hii!

  Kadhalika hatari nyingine ya kukosa kulipa madeni ni kwamba mali iliyowekwa rehani inaishia kwa mauzo ya kupigwa mnada. Aghalabu, hii hufanywa na benki za kibiashara. Hii inapotokea, wanaoathirika moja kwa moja ni wakopaji, familia zao, wafanyakazi na jamii inayomtegea mkopaji.

  Kuna haja ya kutafuta namna ya kuwanusuru wakopaji kutokana na adha hii. Wakopaji wanafaa kushirikishwa katika namna bora za kutumia fedha za mkopo kwa ajili ya uwekezaji endelevu. Vilevile, wanafaa kuelimishwa kuhusu mbinu za kulipa madeni ili waepuke kufilisika. Kwa mfano, wanaweza kushauriwa waanze kulipa mikopo mara tu biashara yao inapoanza kushika japo kidogo kidogo il muradi bandu bandu huisha gogo.

  Baadhi ya wakopaji hushindwa kulipa madeni kwa sababu ya kukopa mikopo mikubwa sana kuliko uweze wao wa kulipa. Hawa ndio wanaostahili kutathminiwa kwa kina kabla ya mikopo yao kuidhinishwa kama nhia mojawapo ya kuwaepusha kujiingiza katika jinamizi la kushindwa kulipa madeni. Waama, baadhi ya mashirika ya kifedha hutoa mikopo kwa awamu kama namna ya kuwadhibiti wakopaji wasibadhiri fedha za mkopo. Imethibitshwa kwamba mbinu hii imewafaa baadhi ya wakopaji.

  Kijumla basi, hamna shaka kwamba mikopo ni namna ya kujiendeleza kiuchumi na ni sharti watu wakumbatie uwajibikaji mbele ya mikopo ili kujiepusha kujiingiza katika lindi la ufukura.
  1. Tumia maneno 50 kuandika mawazo yanayodokezwa katika aya mbili za kwanza. (Alama 5)      
  2. Kwa kurejelea aya za tatu hadi sita eleza hatari zinazowakumba wakopaji na suluhisho kwa hatari zenyewe.              (Alama 8)
   Maneno 75 – 85                                                    
 1. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Ainisha vokali zifuatazo ukizingatia mwinuko wa ulimi (Alama 1)
   1. /o/
   2. /a/
  2. Andika maneno mawili ya Kiswahili sanifu yenye silabi tatu za vokali. (Alama 1)
  3. Ni nini kinyume cha:
   1. Wazalendo wengi walisifiwa na kiongozi wa nchi? (Alama 1)
   2. Kile cha kwanza hakikuuzwa na mnadi. (Alama 1)
  4. Tumia kauli ya kutendeka katika sentensi zifuatazo;-
   1. Raia aliyezusha uvumi alishikwa. (Alama 1)
   2. Wanamuziki watapata sifa kwa kuimba nyimbo za kutukuza maadili. (Alama 2)
  5. Mbali na kutumika katika ngeli, kiambishi ‘i’ kina matumiza mengine onyesha matumizi mengine matatu ya kiambishi hiki. (Alama 3)
  6. Tunga sentensi yenye mpangilio wa maneno ufuatao: (Alama 2)
   Nomino katika ngeli u – zi wingi, kivumishi cha nafasi katika orodha, wakati ujao hali timilifu na kielezi cha mahali.
  7. Onyesha kwa kutumia sentensi mbili jinsi neno ‘shuleni’ linaweza kuwa nomino na kielezi.(Alama 2)
  8. Andika mzizi wa neno lililopigiwa msitari katika sentensi ifuatayo.
   Kamba zilizotumiwa zilikuwa ndefu.   (Alama 1)
  9. Tofautisha maana mbili zilizo katika sentensi :- (Alama 2)
   Mariam alibeba mkoba wake hadi nyumbani.
  10. Tunga sentensi moja ukitumia ‘kati ya’ kuleta dhana za kielezi na kihusishi. (Alama 2)
  11. Akifisha :
   rosa mistika ni riwaya iliyoandikwa na euphrase kezilahabi mmesikia mwalimu ndolo akawaambia wanafunzi.
  12. Tumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mistari katika kuandika upya sentensi hii.  (Alama 3)
   Wachezaji waliozua rabsha uwanjani walitiwa nguvuni na walinda usalama.
  13. Andika maneno mawili yaliyo na viambishi tamati vyenye dhima zifuatazo: kauli tendeka, kiishio na urejeshi unaoonyesha uzoefu.      (Alama 3)
  14. Eleza ukitoa jozi mojamoja ya mfano, miundo miwili ya nomino zilizo katika ngeli ya
   U – U.                 (Alama 3)
  15. Badilisha iwe katika udogo. (Alama 1)
   Ndizi mbivu zimewekwa ndani ya kikapu kikuukuu.
  16. Andika sentensi mbili kudhihirisha miundo miwili ya virai vumishi. (Alama 2)
  17. Jaza pengo ukitumia maneno yaliyo katika parandesi katika hali inayofaa.
   1. Mwanafunzi mwenye __________________________________________ (buni)
   2. Huwafanya ____________________________________ (elimu) wake kufurahi. (Alama 2)
   3. Andola aliachiliwa kwa sababu ya ________________________(Kosa) wa _____________________
    (Shuhudia) wa kutosha.           (Alama 2)
 1. Isimujamii (Alama 10)
  Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.

  Baada ya mjadala mrefu kuhusu mswada huu, na kwa kuzingatia sheria za bunge hili tukufu, kifungu cha 4, kipengele cha 6, ibara ya 3 ningependa kutangaza kupitishwa kwa mswada huu na sasa utawasilishwa kwa rais kusubiri sahihi yake. Kupitishwa kwa mswada huu kwa kauli moja ni tukio la kihistoria kwa bunge hili.
  1. Sifa mbalimbali za sajili ya bunge zinadhihirija katika kifungu hiki. Andika sifa zozote tano.                      (Alama 5)
  2. Rejelea sifa zingine tano za lugha zinazoambatana na muktdha huu. (Alama 5)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 2 - KCSE 2019 MASENO MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest