KISWAHILI PAPER 2 - 2019 KCSE STAREHE MOCK EXAMS (QUESTIONS AND ANSWERS)

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU-ALAMA 15
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
    Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au kuathirika zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. Watu wengi ambao hujitolea kuokoa majeruhi baada ajali kama za barabarani, maporomoko ya ardhi au nyumba huwa hawang’amui hata chembe jinsi ya kukabiliana na uokoaji. Hatima ya juhudi zao ambazo hulenga kutenda mema ni kuathirika zaidi kwa majeruhi.

    Hali ya uokoaji inaweza kurekebishwa kwa kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma. Elimu hii yahitajika na kila mkenya kwani mikasa ya ajali za barabarani na nyinginezo inaendelea kutokea kila siku.

    Ajali zinapotikea si ajabu kuona makundi ya waokoaji wakibeba majeruhi hobelahobela bila kuzingatia madhara wanayoweza kuwaongezea kutokana na ubebaji wao. Kutojua namna ya kumbeba majeruhi kunaweza kumbatanisha na hata kumsababisha kifo.

    Kuna mambo mbalimbali ambayo makundi ya waokoaji yanatakiwa kuzingatia wakati yanatoa huduma ya kuokoa. Kwanza ni muhimu kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza ikatokea na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi. Makundi ya waokoaji yameweza kufanya hivi kwa kuliingilia eneo la ajali mbumbumbu kama mzungu wa reli.

    Hatua ya pili ni kutafuta idadi ya majeruhi. Pana uwezekano wa majeruhi kutupwa mbali na eneo la ajali. Vivyo hivyo, kuna majeruhi ambao huweweseka baada ya ajali na kuanza kutembea wasijue wanakoelekea. Wengi wao huanguka karibu na eneo la ajali au wakaenda mbali.

    Hatua ya tatu ni kuchunguza kama majeruhi amezimia, moyo unapiga na jinsi anavyopumua. Ili kuhakiksha kuwa majeruhi anapumua, mwokoaji atazame kama kifua kinapanda na kushuka. Halikadhalika, mwokoaji anaweza kuskiliza au kugusa kifua na kuona kama kuna ishara za kupumua. Iwapo majeruhi anapumua, muokoaji amweke katka hali ambayo itaimarisha kupumua kwake. Anaweza akamlaza chali au kumgeuza kwa pamoja na kichwa chake ili kufungua mkondo wa hewa. Pia mwokaji ahakikishe hamna chochote kinywani kinachoweza kumsakama. Ikiwa hapumui, mwokoaji anaweza kujaribu kumfanya apumue kwa kupuliza hewa mdomoni mwake.

    Fauka ya hayo, upulizaji wa hewa utahakikisha kuwa damu inazunguka mwilini vizuri. Hatua nyingine ni kuchunguza vile amejeruhiwa. Chunguza kama majeraha ni vidonda tu au kuna kuvunjika kwa mfupa na kubainisha ni mfupa upi. Haya yatamwezesha mwokoaji kujua jinsi ya kumbeba majeruhi. Pakiwa na kuvunjika kwa mfupa, ni muhimu kutotumia kiungo kilichovunjika anapobebwa.

    Pia kuchunguza vile majeruhi amejeruhiwa, humwezesha mwokoaji kujua huduma ya dharura atayoitumia. Majeruhi akiwa anavuja damu sana, ni muhimu kuzuia uvujaji huu. Iwapo ni kidonda kidogo, kinahitaji kufungwa ili kuzuia uambukizaji. Mwokoaji anaweza kutumia kifaa chochote kilicho karibu kutolea huduma hizi. Kwa mfano, anaweza kupasua nguo ya majeruhi ili apate kitambaa cha kusaidia kuzuia kuvuja kwa damu au kufunga kidonda.

    Hatua inayofuata ni kusafirisha majeruhi toka eneo la ajali hadi hospitalini. Mwokoaji anaweza kuwatumia watu wengine kutafuta msaada. Wanaweza kupiga simu kwa kutumia nambari za simu za dharura kama zile za polisi, wazimamoto au makundi ya wataalamu wa shughuli za uokoaji. Nambari hii ya simu ni 999 popote na huwa na haina malipo. Wanaopiga simu ni vyema kutoa maelezo ya mahali ambapo ajali imetokea, ama ya ajali na hudumaza dharura zinazohitajika.

    Ikiwa makundi ya wataalamu wa uokoaji hayakupatikana, ni jukumu la mwokoaji kuhakikisha majeruhi wamehamishwa na kupelekwa hospitalini. Majeruhi wakiwa wengi ni bora kuanza na wale waliozimia au wenye matatizo ya kupumua kisha kuwaendea wanaovuja damu sana. Baadaye mwokoaji awasaidie waliovunjika mifupa huku akimaliza na wenye majeraha yasiyohatarisha maisha. Ni muhimu kuwabeba majeruhi kwa kutumia machela. Hii hupunguza kuathirika zaidi kwa majeruhi. Iwapo hamna machela karibu, mwokoaji anaweza kuunda moja kwa kutumia vipande viwili vya mbao, blanketi, shuka au makoti.Ujuzi wa huduma ya kwanza ni mojawapoya mambo muhimu ambayo kila mtu anapaswa kuwa nayo.

    Maswali
    1. Kipe kifungu hiki anwani mwafaka.                                                                                    (alama1)
    2. Eleza hatua inayofaa kuchukuliwa ili kuboresha hali ya uokoaji wa majeruhi.                   (alama2)
    3. Waokoaji wengi hutahadharisha maisha ya majeruhi. Thibitisha.                                     (alama 2)
    4. Eleza mambo yanayofaa kutiliwa manani wakati wa kuwaokoa majerihi.                         (alama 6)
    5. Onyesha njia mbili ambazo mwokoaji anafaa kutumia ili kubainisha kuwa majeruhi hajafa. (alama 2)     
    6. Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kwa mujibu wa kifungu                                               (alama 2)
      1. Mbumbumbu kama mzungu wa reli
      2. Hawang’amui hata chembe
  1. MUHTASARI- ALAMA15

    Soma makala yafuatayo halafu ujibu maswali yanayofuata.
    Suala mojawapo linaloshughulisha jamii ya ulimwengu ni kiwango cha ubaguzi unaotokea katika mazingira ya kazini. Tafiti ambazo zimefanywa zinabainisha kuwepo kwa ubaguzi wa kila nui katika mazingira ya kazi. Misingi ya ubaguzi huo ni tofauti kuanzia hisia za dharau , taswira mbaya na dumifu kuwahusu wanajamii na kuwepo kwa mashirika ambayo yamekuwa sugu kiasi cha kutozibwia sera mpya au kuchukua hatua ambazo zinaweza kuukomesha ubaguzi.

    Utafiti uliofanywa na shirika la leba ulimwenguni (ILO) umebainisha mambo kadha kuhusianana na suala la ubaguzi. Kwanza kuwa ubaguzi ungali unapatikana katika mazingira ya kazini. Kuwepo kwa uhamaji ulimwenguni, watu kutoka sehemu moja hadi nyingine pamoja na kupanuka kwa mipaka ya kitaifa pamoja na kuongezeka kwa matatizo ya kiuchumi na uhaba wa nafasi za ajira ni vichocheo vikubwa vya ubaguzi. Matukio haya yanaishia kuziamsha hisia za kuwachukia wageni miongoni mwa wanajamii fulani. Chuki za rangi pamoja na hisia zenye misingi ya kidini zinaelekea kuimarika zaidi katika mazingira haya. Ugunduzi mwingine ni kuwa harakati za kupambana na ubaguzi hazielekei kuonyesha usawazisho maalum. Ubaguzi wa kijinsia ungali unaendelea. Upo mpaka mkubwa baina ya makundi mbalimbali na wanajamii wanaobaguliwa; baadhi wanafanikiwa kupanda mpaka juu ilhali wenzao wanakwamia pale pale chini.

    Kuwepo kwa ubaguzi kumeishia kuwafanya watu wengine kuishia kuselelea kwenye ngazi za chini za kiuchumi- wakifanya kazi za kitopasi na kulipwa mishahara tumba isiyoweza kuwafaidi. Kundi hili la watu hunyimwa istihaki muhimu za kazini, hifadhi ya kajamii, mafunzo ya kujiendeleza, ardhi na hata mikopo. Kwa njia hii ile ilhamu yao ya utendakazi inaathirika vibaya sana. Wanawake, wanapolinganishwa na wanaume, wanaishia kufanya kazi za kitopasi au amali ambazo zinaishia kupuuzwa katika jamii, mchango wao kiuchumi hauzingatiwi.

    Ukosefu wa harakati za kupambana na ubaguzi unamaanisha kuwa mkufu wa umaskini unaendelea kuwaongoza wanajamii. Ubaguzi unazua utando fulani wa umaskini, kazi ya lazima, ajira ya watoto na kutengwa kijamii. Basi ikiwa jamii yoyote ile inadhamiria kuindoa hali hii, haina budi kupambana na ubaguzi huu. Kila mwanajamii atafaidika kwa kuondolewa au kufutwa kwa ubaguzi katika mazingira ya kazini. Wafanyakazi ambao hawabaguliwi watafanya kazi kwa kujitolea kwa njia hii kuchangia uzalishaji katika jamii yao.

    Maswali
    1. Fupisha aya za kwanza mbili. (alama 9, 1 ya mtiririko) (maneno 100)
    2. Ubaguzi katika mazingira ya kazini una athari hasi. Thibitisha. (alama 6, 1 ya mtiririko) (maneno 45)
  1. MATUMIZI YA LUGHA- ALAMA 40
    1. Taja mifano miwili miwili ya konsonanti ambazo:
      1. Hutamkwa kama irabu   (alama1)
      2. Zinapotamkwa husababisha mrindimo wa nyuzi za sauti                                      (alama 1)
    2. Tambua viambishi ngeli vya nomino zifuatazo    (alama 1)
      1. Kikaragosi
      2. Nyuzi
    3. Andika sentensi ifuatayo kwa wingi
      Bwana Kizito ameenda Kisiwani kununua riwaya iitwayo Msimu wa Vipepeo.            (alama 2)
    4. Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiunganishi mwafaka
      Utakula limau? Utakula tikitimaji? (alama 2)
    5. Badilisha vivumishi katika sentensi zifuatazo kuwa viwakilishi vilivyoonyeshwa mabanoni.
      1. Mtoto mzuri ameniazima kalamu yake. (viradidi vya mbali kidogo)               (alama 1)
      2. Mti mrefu utaliangukia jumba kubwa. (vya pekee vinavyoleta dhana ya ziada) (alama 1)                        
    6. Kanusha sentensi ifuatayo
      Mtoto alipomwona mama alifurahi na kumkumbatia.        (alama 2)
    7. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao         (alama 2)
      Shamirisho kitondo, kitenzi, shamirisho kipozi, kivumishi cha umilikaji, kihusishi, kiima
    8. Tunga sentensi ili kudhihirisha matumizi yafuatayo ya neno “li”                                       (alama 3)
      1. Njeo
      2. Kitenzi
      3. Ngeli
    9. Andika neno lenye muundo ufuatao                                                                                    (alama 3)
      Kiambishi kikanushi cha nafsi ya tatu umoja, kiambishi kikanushi cha hali timilifu, kiambishi kiwakilishi cha yambwa, mzizi wa sauti moja, kiambishi cha hali ya kutendesha na kiambishi cha hali ya kutenda.
    10. Tunga sentensi yenye kirai kielezi cha mamna kikariri na kielezi cha namna halisi.       (alama 1)
    11. Andika sentensi ifuatayo upya ukitumia vinyume vya vitenzi vilivyopigiwa mstari.        (alama 2)
      Watu walimdharau kiongozi wao hadi akaanza kubabaika.
    12. Tunga sentensi ifuatayo upya kwa kutumia nomino ya jamii badala ya maneno yaliyopigiwa mstari.
      Mchezaji alivishwa mtungo mrefu wa maua shingoni baada ya ushindi wake.                (alama 1)
    13. Tunga sentensi ukitumia kisawe cha neno “ kiroho”
    14. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali ya kuendelea
      Abdan anasafisha nguo zake vizuri sana.                     (alama 2)
    15. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale
      Watu wote walioalikwa mkutanoni wanajiandaa kusafiri.
    16. Andika kwa msemo wa taarifa
      “Tetei! Njoo hapa nikutume sokoni,” baba alisema.                                                          (alama 2)
    17. Tenganisha silabi katika neno lifuatalo kisha uonyeshe miundo ya silabi hizo.                (alama 2)
      Mbuni
    18. Andika neno moja lenye sauti mwambatano za:                                                               (alama 2)
      1. ufizi
      2. midomo
    19. Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia kiambishi –ku- kuonyesha:                                 (alama 2)
      1. Wakati
      2. Nafsi
  1. ISIMUJAMII-ALAMA 10
    1. Eleza maana ya lugha ya taifa        (alama 2)
    2. Fafanua sababu nne zilizosababisha Kiswahili kuteuliwa kuwa lugha ya taifa nchini Kenya.      (alama 4)
    3. Eleza majukumu manne ya Kiswahili nchini Kenya.                                                   (alama 4)


MARKING SCHEME

  1. Ufahamu
    1. Uokoaji wa majeruhi
    2. Kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma
    3. Kubeba majeruhi hobelahobela bila kuzingatia madhara wanayoweza kupata kutokana na ubebaji huo
    4.  
      • Kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza kutokana na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi
      • Kutafuta idadi ya majeruhi
      • Kuchunguza kama majeruhi amezimia
      • Kupulizia majeruhi hewa ili kuhakikisha kuwa damu inazunguka mwilini vizuri
      • Kuchunguza vile majeruhi amejeruhiwa ili kujua huduma ya dharura atakayopewa
      • Kusafirisha majeruhi toka eneo la ajali hadi hospitalini
      • Mwokoaji kuhakikisha kuwa majeruhi wamehamishwa na kupelekwa hospitalini
    5.  
      • Kutazama kama kifua kinapanda na kushuka
      • Kusikiliza / kugusa kifua ili kubaini kuwa kuna ishara za kupumua
    6.  
      • mjinga
      • hawaelewi kabisa

        adhabu
      • Ondoa alama 3 za makosa ya hijai yanapotokeakwa mara ya kwanza, yaani, ½ alama hadi kufikia makosa sita.
      • Ondoa alama ½ kwa kila kosa la sarufi kufikia ½ ya alama alizopata katika kila kisehemu.
  1. muhtasari
    1. Suala mojawapo linaloshughulikiwa na ulimwengu ni ubaguzi unaotokea kazini
      • Tafiti zimebaini kuwepo kwa ubaguzi wa kila nui kazini
      • Misingi ya ubaguzi huu ni tofauti/mbalimbali
      • Utafiti wa shirika la leba ulimwenguni umebainisha mambo kadha kuhusu ubaguzi
      • Ubaguzi ungali unapatikana kazini
      • Ubaguzi huu unachochewa na mambo mbalimbali
      • Vichocheo hivi huamsha hisia za kuwachukia wageni
      • Chuki za rangi na za kidini zinaelekea kuimarika
      • Harakati za kupambana na ubaguzi hazileti usawazisho
      • Ubaguzi wa kijinsia ungalipo
      • Upo mpaka mkubwa baina ya makundi mbalimbali ya wanajamii
        (zozote 8×1=8)
    2. Kuwafanya watu wengine kuselelea kwenye ngazi za chini za kiuchumi
      • Watu kunyimwa istihaki muhimu kazini
      • Wanawake kufanya kazi za kitopasi zinazoishia kupuuzwa katika jamii
      • Mkufu wa umaskini unaendelea kuwazonga watu
      • Utando fulani wa umaskini
        (zozote 5×1=5)
        a-8
        b-5
        ut-2

        adhabu
      • Ondoa alama 3 za makosa ya hijai yanapotokea kwa mara ya kwanza, yaani nusu alama hadi kifikia makosa 6.
      • Ondoa ½ alama kwa kila kosa la kisarufi kufikia nusu ya alama alizopata kutoka kila sehemu.
      • Mtahini akiorodhesha majibu badala ya kutumia aya asituzwe alama za utiririko
      • Mtahini aspoandika nakala chafu asisahihishiwe nakala safi
  1. Matumizi ya lugha
    1.  
      1. /y/ na /w/
      2. sauti zote ghuna
    2.  
      1. A-WA
      2. U-ZI
    3. Kina Bwana Kizito wameenda Kisiwani kununua riwaya iitwayoMsimu wa Vipepeo.
    4. Utakula limau au tikitimaji?
    5.  
      1. Huyo huyo amenizima hiyo hiyo.
      2. Mwingine ameliangukia jingine.
    6. Mtoto alipomwona mama hakufurahi wala kumkumbatia.
    7. Mtoto alitengenezewa kijigari chake na baba.
    8.  
      1. alisoma
      2. Embe li mtini
      3. Limeoza
    9. hajamlisha/ hajamfisha
    10. Waliingia darasani polepole mno/ hobelahobela sana
    11. Watu walimheshimu kiongozi wao hadi akaanza kutulia.
    12. Koja la maua
    13. Simanzi/ ukiwa/ majonzi/ jitimai
    14. Abdan alikuwa akisafisha nguo zake vizuri sana.
    15. S→KN + KT
      KN→N+V+S
      N→Watu
      V→wote
      S→walioalikwa mkutanini
      KT→T+T
      T→wanajiandaa
      T→kusafiri
    16. Baba alimwita Tetei na kumwambia aende alikokuwa ili amutume sokoni.
    17. Mbu-KKI, ni-KI
    18.  
      1. funzwa /ndama
      2. pweza/mwana/mboni
    19.  
      1. hakusoma
      2. alikusamehe
  1. Isimujamii
    1. Ligha iliyoteuliwa kama kitambulisho cha utamaduni na ustaraabu wa taifa fulani.2×1=2
    2.  
      • Kinazungumzwa na watu wengi nchini
      • Kinabeba amali, utamaduni na historia ya watu wengi nchini
      • Kina uwezo wa kutoa hisia za kikabila na kuwafanya watu kuhisi kuwa taifa moja
      • Kina uwezo wa kukidhi mahitaji ya kimawasiliano.
        4×1=4
    3.  
      • Ni kiwakilishi cha amali, utamaduni na historia ya watu
      • Ni chombo cha mawasiliano, maingiliano na maelewano baina ya watu
      • Ni nyenzo ya kuwaunganisha watu wenye asili mbalimbali na kujihisi kuwa taifa moja
      • Ni chombo cha kuushirikisha umma katika shughuli zote za taifa
      • Ni ala inayolipa taifa la Kenya na wananchi wake hadhi na haiba
      • Kinawaunganisha wananchi
        Zozote 4×1=4

        adhabu
      • Ondoa alama 3 za makosa ya hijai yanapotokeakwa mara ya kwanza, yaani, ½ alama hadi kufikia makosa sita.
      • Ondoa alama ½ kwa kila kosa la sarufi kufikia ½ ya alama alizopata katika kila kisehemu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 2 - 2019 KCSE STAREHE MOCK EXAMS (QUESTIONS AND ANSWERS).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest