KISWAHILI PAPER 2 - KAPSABET BOYS 2019 TRIAL MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp
Download PDF for future reference Join our whatsapp group for latest updates
 1. UFAHAMU (ALAMA 15)
  Soma kifungukifuatachokishaujibumaswaliyanavyofuata
  Wakati wananchi katika kila pembe ya dunia waliadhimisha siku ya wapendanao maarufu kama “Valentine Day,” kwa mitindo mbalimbali, hali hiyo ilikuwa tofauti kwa baadhi ya wanaume nchini Kenya, baadaya kulalamika kuhusu kunyanyaswa na wake zao.
  Kulingana na mwenyekiti wa chama cha kutetea haki za wanaume nchini, idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka mno.Alisema juzi kuwa utafiti wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za kumpa mwanamke uwezo zimeathiri maadili na kusababisha kuwadharau wanaume. Mwanaharakati huyo alidai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali yakuwa wanawake wengi sasa wanakipato kikubwa kuliko waumezao.Mwisho ni wa mwezi polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri, baada ya kumshambulia mumewe na kumjeruhi kwa panga.Mwanamme huyo badoa napata matibabu hospitalini.Yeye alirudi nyumbani kama amevaa miwani ndipo akakatwa katwa usoni na uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.
  Inadaiwa kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake zao mwakajana na kwamba utafiti washirika la kuwatetea wanaume umeonyesha kuwa kesi nyingi za wanaume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika kati mwanchi.
  Hata hivyo, baadhi ya wanaume katika eneo hilo wameunga mkono hatua ya wanawake kuwashambulia waumezao. Wanasema kuwa wanapigwa kwa sababu wamekosa kuwajibika kwa familia zao.Wanadai kuwa wanaume wengi hawajulikani nyumbani kwao. Wake zao wanawajua makasisi ambao huja kuwaombea kuhusu matatizo ya nyumbani huku mabwana zao wakizama katika ulevi.Wanawake na waume wa Nyeri wametaka serikali kukomeshe uuzaji na unywaji wa pombe haramu ambayo imechangia sana katika ugomvi wa nyumbani.

  Maswali
  1. Yape makala haya anwani inayofaa (alama 1)
  2. Eleza sababu zawanaume kupigwa na wanawake katika ndoa (alama 4)
  3. Mwandishi anamaanisha nini anaposema kuwa wanaume wengine hawajulikani nyumbani kwao?                                                                                                 (alama 2)
  4. Fafanua majukumu ya makasisi katika jamii kwa mujibu wa kifungu hiki (alama 2)
  5. Ni mabadiliko yepi yametokea katika asasi ya ndoa kwa mujibu wa kifungu? (alama 3)
  6. Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumika kifunguni (alama 3)
   1. Mwana harakati
   2. Amevaa miwani
   3. Waliadhimisha
 1. UFUPISHO (ALAMA 15)
       Ujambazi wa kimataifa ni tatizo linalowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana.Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupamba na na janga hili.Hata hivyo, fanaka haijapatikana, wala haielekei kuwa itapatika na leo au karne baadaye.
        Yamkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhanaya ”Ujambazi” tena “wakimataifa”. Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pilini kibusi. Kuna wale wafu binafsi na hasa viongozi wa nchi kubwa kubwa na serikali zao zilizojiaminisha kuwa ujambazi ni balaakweli, tenabelua, lakini huo ni wahuko, wala hauwezi kuwagusa licha ya kuwashtua wao.
        Kulingana na maoni ya wataka buri hao, ujambazi ni wa watu washenzi wasiostarabika, wapatika nao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi wa pekee wanao uona unafaa kukabiliwa ni dhidi ya mbubujiko wa dawa za kulevya iliosababishwa na vinyangarika kutoka nchi hizo maaluni za “ulimwengu wa tatu”. Kulingana na wastaarabu wanchi zilizoendelea,vinyangarika hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa ustaarabu ulimwengu na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma.Baadayakusagwasagwa, ulimwenguni mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa ardhini itakamilika.
        Imani ya watu hawa yakuwa ujambazi, hata hivyo upo, hauwezi kuwashtua wala kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu.Ilikuwa kamili na timamu hadi hapo mwezi Septemba terehe kumi na moja, mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilizoelekea katika majumba mawili ya fahari,yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na kuyatwa ngilia mbali.Mstuko na kimako! Kimako kwa kuwa kabla ya siku hiyo, wamarekani hangeweza kudhani kwamba ingewezeka taifa lolote au mtu yeyote kuthubutu kuishambulia nchi yao, taifa wasifa lililo jihami barabara dhidiya aina yoyote ile ya uchokozi kutoka pembe yoyote ya dunia.
        Hakuna ulimwengu mzima, aliye amini kuwa marekani ingeweza kushambuliwa. Kwa ajili hiyo, mshtuko ulitingisha ardhi yote na huzuni kutanda kote, kama kwamba sayari nzima imeshambuliwa, wala sio marekani pekee.
        Mintarafu hiyo,marekani ilipo lipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani ilishangilia na kusheherekea. Kwa bahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara-pachaya New York naileya Pentagon, utiwa uwezo wa Marekani ilizorota. Kuna wengi waliodhani huoni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi ya Wakristo na kwa muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa.

  Maswali.
  1. Bila kubadilisha maana, fupisha ayaza kwanza.(maneno 65-70) (alama6)
  2. uKizingatia aya tatu za mwisho, fafanua fikira za watu na mambo yote yaliyotendeka baada ya Septemba 11,2001.( maneno65-70) ( alama 7)
 1. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
  1. Eleza sifa mbili bainifu za sauti /a/ (alama 2)
  2.  
   1. Mofimu ni nini? (alama 2)
   2. Ainisha mofimu katika kitenzi; (alama 2)
    Alimwona
  3. Andika kitenzi chenye muundo ufuatao ; (alama 2)
   Kiambishi ngeli, wakati uliopita, mzizi, kauli tendwa na kiishio.
  4. Barabara nyingi zimesakafiwa.
   (Tumia wakati ujao hali ya mazoea)
  5. Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi (alama 4)
   Cherotich aliwahakikishia wazazi wake kwamba angetia bidii katika masomo yake iliapite mtihani wake
  6. Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia rejeshi-amba (alama 2)
   1. Mshukiwa alipelekwa mahakamani
   2. Mshukiwa alichukuliwa hatua
  7. Changanua sentensi ifuatayo kwa mtindo wa jedwali (alama 4)
   Mto uliofurika mwaka jana uliwaua mamba wengi
  8. Tambua shamirisho, chagizo na kihusishi katika sentensi (alama 3)
   Mgonjwa alitibiwa na daktari jana jioni.
  9. Taja ngeli za nomino zifuatazo (alama 2)
   1. Sandarusi
   2. Saa
  10. Yakinisha sentensi ifuatayo (alama 2)
   Mamlaka makubwa ya Raisha ya kwa zijuhudi za upinzani
  11. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi kifuatacho (alama 2)
   La
  12. Tunga sentensi kudhihirisha maana za vitate vifuatavyo (alama2)
   Bure
   Pure
  13. Andika katika hali ya ukubwa wingi (alama 2)
   Msichana mrembo ameolewa na mwanamume hodari.
  14. Kamilisha tanakali za sauti zifuatazo             (alama 2)
   Maji yalijaa
   Barabara imenyooka
  15. Eleza maana ya mzizi wa kitenzi (alama 1)
 2. ISUMU JAMII (ALAMA 10)
  1. Lugha rasmi ni nini? (alama 2)
  2. Eleza sababu zozote tatu ambazo huenda zikamfanya mzungumzaji afanye makosa ya kisarufi na kimatamshi (alama 3)

MARKING SCHEME

 1. UFAHAMU
  1. Ndoa/kunyanyaswa kwa wanaume ( 1 x1=alama 1)
   1. Kutowajibika kwao
   2. Wengine hawajulikani nyumbanikwao.
   3. Wamezama katika ulevi
   4. Wanawake kuwa na kipato kikubwa kuliko waume zao ( 4 x 1=alama 4)
  2. Hawafiki nyumbani kwa jamaa zao ( 1 x 2=alama 2)
  3. Kuwaombea kuhusu matatizo ya kinyumbani ( 1x2=alama 2)
   1. Wanaume kutowajibika
   2. Wanawake kupewa uwezo
   3. Wanawake kuwadharau na kuwapiga waumezao                                         ( 3x1=alama3)
  4.  
   1. Anayepigania haki za wengine
   2. Kulewa
   3. Walisherehekea                                                                                             ( 3x1=alama3)
 2. UFUPISHO
  1.  
   1. Fanaka haijapatikana wala haielekei kupatikana
   2. Tatizo kubwa ni kuhusu jelezi la dhana ya ujambazi wa kimataifa.
   3. Vinyang’arika sharti viangamizwe ili ulimwengu mstaarabu uzidi kutotonoka
    (zozote 6x1=alama 6)
  2.  
   1. Marekani ili lipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu huko Afghanistan.
   2. Tafsiri ya shambulizi la minara pacha ya New York na Pentagon ulizorota.
   3. Wengi walidhani kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa vita dhidi ya Wakristo
   4. (zozote 6x1=alama6)
    a=6,
    b=6
    ut=3                
 1.  
  1.  
   1. Ni irabu
   2. Ni irabu ya kati ya ulimi
   3. Hutamkwa mdomo ukiwa umetandazwa.                              (za kwanza 2x1=alama 2)
  2.  
   1. Mofimu ni sehemu ndogo ya new yenye maana ya kisarufi na isiyoweza kuvunjwavunjwa zaidi.
   2. Alimwona
   3. Mofimu ya nafsi/ngeli
    li-Mofimu ya wakati
    mw-Mofimu ya kitendewa
    a- Mofimu ya kiishio                                                                                             (4x½=alama 2
  3. Mfano :Ilipandwa
  4.  
   1. Sentensi ya swali – Ulimwona mwalimu saa ngapi?
   2. Sentensi ya mshangao – Hoyee! Timu yetu imeshinda.
   3. Sentensi ya taarifa – Nilimwona Simba msituni jana.
   4. Sentensi ya ombi – Naomba/tafadhali nisaidie na nauli
   5. Sentensi ya amri – Toka nje haraka!
  5.  
   1. Kijitabu kiki hiki kilirushwa na kiranja ( 1x2=alama2)
   2. Barabara nyingi zitakuwa zimesakafiwa/zitakuwa zikisakafiwa (1x2=alama2)
  6. Cheroiti chali wahakikishia wazazi wake, “Nitatia bidii katika masomo yangu ili nipite mtihani wangu.” (8x½=alama 4)
  7. Mshukiwa ambaye alipelekwa mahakamani alichukuliwa hatua.                   (1x2=alama2)
  8. S

   KN

   KT

   N

   S

   T

   N

   V

   Mto

   Uliokauka mwakajana

   uliwaua

   mamba

   wengi

   Shamirisho – Mgonjwa(8x½=alama4)
   Chagizo – janajioni
   Kihusishi–na                                                                                                        (3x1=alama3)
   1. I-ZI
   2. I-ZI (2x1=alama2)
  9. Mamlaka makubwa ya Rais yana kwaza / hukwanza juhudi za upinzani. (1x2=alama2)
  10.  
   1. Kula
   2. Mlo
   3. Chakula
   4. Mlaji (2x1=alama2)
  11.  
   1. Bure
    Kitu kinacho patika nebila jasho/bwerere
    Ovyo
    Kitu kisicho na thamani (1x1=alama1)
   2. Pure – Chakula cha mchanganyikowapunjezamahindinamaharagwe. (1x1=alama1)
    Tan: Kadiriamatumizimwafaka
  12. Masichana marembo yaliolewana majana umme hodari.                                     (4x½=alama2)
  13.  
   1. Pomoni
   2.  Twaa (2x1=alama2)
  14. Mzizi wa kitenzi ni sehemu inayobeba maana kuu na ambayo haiwezi kubadilishwa.                                                                                                                                            (1x1=alama1)
 1.  
  1. Lugha rasmi ni lugha ambayo hutumika katika shughuli za kiofisi.
   Kutofahamu ngeli za Kiswahili
   Kuwa na upungufu katika baadhi ya viungo vya kutamkia
   Kuzungumza kwa haraka
   Kuwa na athari ya lugha ya kwanza/lafudhi
   Kimaksudi hasa wakati wa uigizaji (za kwanza 3x1=alama3)
  2. Ni lugha yenye msamiati teule K.V spika, mswada, mbunge.
   Ni lugha ya majibizano kwani huhusisha maswali na majibu
   Ni lugha ya kimaelezo hasa mbunge anapochangia hoja.
   Ni lugha inayotumia viziada lugha na ishara za mikono.
   Lugha huwa rasmi
   Lugha yenye ucheshi
   Lugha yenye heshima na adabu             (zozote 5x1=alama5)

Download KISWAHILI PAPER 2 - KAPSABET BOYS 2019 TRIAL MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-


Read 2313 times Last modified on Monday, 30 March 2020 11:47

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Print PDF for future reference