MAAGIZO
- Andika jina lako na nambari ya usajili kwenye nafasi ulizoachiwa hapo juu.
- Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako.
- Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha
- Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”
- Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo.
Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele.

MWONGOZO
- TAWASIFU
Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako.
SURA- Atumie nafsi ya kwanza
- Atumie aya kuwasilisha hoja zake
- Maisha ya kuzaliwa, kukua na elimu ichukue nafasi ndogo katika tawasifu
- Mtahiniwa ashughulikie ufaafu wake.
BAADHI YA MAUDHUI - Yeye mwenyewe kwa mtoto wa kurandaranda
- Aokolewa na ajiunga na elimu
- Kuwa kiongozi wa shirika la kusaidia watoto shleni – aelezee shughuli walizohusika nazo
- Shahada yake ni kuhusu nini?
- Baada ya kuhitimu ameshughulikia mradi ipi?
- Je kuna masuala aliyochangia kimaadhishi
- Je amehusika na makao mangapi ya watoto wanaorandaranda
Tashbihi - Akitumia mtindo wa hotuba kama vile salamu hana sura – 4mm ( sura)
- Lazima atumie nafsi ya kwanza
- Akikosa – 4 mm (sura)
- Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha
SURA- Hili ni swali elekezi kila hoja itajwe, ifafanuliwe na ikamilike
- Ikiwa hoja haijakamilika isituzwe
- Lazima mtahiniwa awe na hoja zaidi ya saba kuhitimisha maudhui
- Lazima atumie hoja mufti
BAADHI YA HOJA - Hufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu
- Hufanikisha biashara
- Hufanikisha elimu
- Hukuza utangamano
- Kuboresha mahusiano
- Kuboresha usalama
- Huburudisha – husaidia watu kukabiliana na matatizo k.v msongo wa mawazo n.k
- Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”
- kisa kinafaa kioana na methali
- Mwanafunzi azingatie methali husika
- maana ya hiyo iwe anayekutangulia si lazima akamilishe mkondo anaweza kukosa kufika
- mtahiniwa atunge kisa kimoja
- aonyeshe sehemu zote mbili za methali
- dhana ya kutangulia ionekane vizuri
- dhana ya kutofika ijitokeze hata kama ni aya chache au sentensi moja
- Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo
Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele.
Jibu- Mtahiniwa ajikite katika kisa ambacho kinaelezea mambo magumu ambayo yamezunguka maishani hadi kufikia upeo wa ufanisi
- Mtahiniwa pia aeleze namna ambavyo amefanikiwa maishani baada ya masaibu mengi
- Kisah kisimuliwe katika nafsi ya kwanza
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kassu Joint Mock Examination 2021.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates