Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lainaku II Joint Mock Examination 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 1. Lazima
  Kama mhariri wa gazeti la Angaza, andika tahariri ukitoa maoni yako kuhusu changamoto zinazotokana na mfumo mpya wa elimu ya umilisi.
 2. Fafanua madhara ya mitandao ya kijamii na utandawazi kwa jamii.
 3. Buni kisa chenye kudhihirisha maana ya methali hii:
  Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
 4. Andika insha itakayochukua mwisho huu.
  … nilipotua nchini mwetu, nilishusha pumzi, nikashukuru Maulana kwa kuponea chupuchupu katika uvamizi huo.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Swali la lazima
  Ni insha ya tahariri
  Muundo wa tahariri uzingatiwe
  • Jina la gazeti
  • Siku na tarehe ya tahariri kutokea gazetini
  • Jina la mhariri
  • Mada
  • Mwili wa tahariri unaobeba maudhui
  • Hitimisho
   Baadhi ya hoja
  • Mtaala huu ni ghali mno na unaegemea sana katika matumizi ya vifaa halisi vya kufunzia
  • Walimu wengi wangali wanatatizika jinsi ya kuendeleza mafunzo haya kwa wanafunzi
  • Wanafunzi wanahitajika kutumia asilimia kubwa ya muda uliotengewa kila somo wakijifunza kwa vitendo wakiwa pamoja, hivyo muda mwingi hupotezwa.
  • Hakuna muda wa kutosha wa kutathmini kazi ya kila mwanafunzi
  • Masomo kama vile muziki, uchoraji yanaibua changamoto kwa walimu kwa sababu hawajazoea kuyafunza.
  • Mbinu zinazopendekezewa walimu za kufunza ni geni na walimu hawana uzoefu wa kutosha.
  • Baadhi ya wazazi hawajasoma. Hawana uwezo wa kuwasaidia wanao.
  • Wazazi wanaona kuwa wanasumbuliwa wanapoagizwa kugharimia vifaa vya kufundishia kila mara.
  • Kazi nyingi ya kufanikisha mfumo huu imeachiwa wazazi.
  • Shule za mijini zisizo na maeneo makubwa ya ardhi kukabiliwa na tatizo la kufunza somo la kilimo/ zaraa.
  • Masomo mengi zaidi – takriban 13 kwa mwanafunzi wa gredi ya nne. Mzigo mkubwa sana kwa watoto hawa.
  • Ni vigumu kukadiria viwango vya kufuzu kutoka darasa moja hadi lingine.
  • Ulipoanzishwa raia hawakutayarishwa/ kufahamishwa ipasavyo kupitia vikao vya umma
  • Uchache au uhaba wa vitabu katika masomo mbalimbali.
  • Idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa moja.
  • Uhaba wa madarasa yenye mazingira na vifaa vinavyostahili kufunzia mtaala huu.
  • Mfumo huu unaweza kuwa chanzo cha ubaguzi kati ya walionavyo na wasionavyo.
   Tanbihi: Kadiria hoja nyingine sahihi
 2. Madhara ya mitandao
  • Hupalilia uzembe miongoni mwa wanajamii.
  • Makundi ya matapeli na walaghai hutumia kuendeleza uhalifu wao.
  • Inaishia kuwapotosha watu kimaadili
  • Huwa na filamu zinazohimiza watu kuwa wazinifu
  • Baadhi ya matangazo mitandaoni huchangia katika kupotoka kimaadili kwa wanajamii, mihadarati na vileo
  • Ununuzi wa nyenzo za mtandao na utumizi wake unagharimu pesa nyingi.
  • Huchochea wanajamii kuiga mila na tamaduni za kigeni na hivyo kupunjua utamaduni wetu wa kiasili kv ,mavazi na mienendo
  • Kuna wanajamii wanaoitumia mitandao kueneza hisia za chuki na propaganda.
  • Mitandao hii imechangia katika kuvunjika kwa ndoa, uchumba na familia
  • Vifaa hivi huweza kusababisha magonjwa kv ya macho na saratani
  • Wanajamii huishia kuganda kwenye mitandao hii na hivyo kupoteza muda muhimu wa kufanya kazi.
  • Tanbihi:
   1. uza hoja nyingine mwafaka
   2. Mtahiniwa arejelee madhara/ maovu pekee.
 3. Ni insha ya methali. Mtahiniwa aandike insha yenye kudhihirisha maana na matumizi ya methali husika.
  • Maana ya methali: Usidharau mtu au kitu kilichokufaa awali kwani huenda ukahitaji huduma au msaada wake baadaye.
  • Visa vinaweza kudhihirisha hali zifuatazo;
   1. Mhusika ambaye ameishi mahali kwa muda kisha anapoondoka/ anapofanikiwa anapadharau.
   2. Baada ya kukamilisha masomo, mwanafunzi awadharau walimu, wafanyakazi wa shule au wanafunzi wenzake kisha aibike anaporudi kuchukua matokeo yake.
   3. Mwajiriwa ambaye amefanya kazi katika kampuni fulani kwa muda, kisha anapopata kazi kwingine ajiuzulu kwa dharau. Baadaye patokee jambo linalomhitaji kupata barua kutoka kwa wakuu wa kampuni hiyo, ahasirike kwa kuona aibu kuomba barua.
    Tanbihi: kadiri utungo wa mtahiniwa ipasavyo
 4.  
  • Hii ni insha ya mdokezo wa kutamatisha.
  • Sharti mwanafunzi akamilishe kisa chake kwa maneno haya.
  • Atumie mbinu rejeshi ili kumrejesha mtahini kwenye matukio ya awali.
  • Mtahiniwa akiacha au aongezee neno moja au mawili kwenye mdokezo atakuwa amejibu swali-udhaifu huo uchukuliwe kama kosa ndogo tu la kimtindo.
  • Akikosa kumalizia kwa maneno aliyopewa atakuwa amejitungia swali (D- 0220)
  • Taswira zifuatazo zinaweza kujitokeza;
   1. Mhusika aliyekuwa ameenda ng’ambo kwa shughuli za kimasomo, kikazi au ziara.
   2. Asimulie matukio yaliyofanyika katika nchi alikokuwa kiasi cha kumshurutisha kurejea nyumbani.
   3. Anaweza kusimulia uvamizi wa nchi moja dhidi ya nyingine kama ule wa Urusi dhidi ya Ukraine ambapo wageni wanakimbilia usalama.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lainaku II Joint Mock Examination 2023.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?