Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA 3:FASIHI

MAAGIZO:

 • Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 • Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 • Jibu maswali manne pekee.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani; Riwaya, Tamthilia, Ushairi na Hadithi Fupi.
 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

SEHEMU YA A : SWALI LA LAZIMA

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  Tabasamu zao

  Nitafakaripo kwa tuo
  Moyo hunitweta na mtetemeko kunivaa
  Wanijiapo na tabasamu
  Ambazo hulinyonga tumaini langu
  Ninahuzunika!

  Wanisalimiapo kwa mikono miwili
  Na chini kuniinamia
  Wakiyakoleza yao matamshi
  ‘’Mzee…ndugu…Salama!Salama!

  Nachukia zao nyendo
  Wanadai kwaa mihemko
  ‘’Lazima tungo kutetea wanyonge’
  Lakini nitazamapo, wenyewe hawasiti

  Mnyonge mkononi kumtia
  Na kwa maguvu kumfikicha
  Haki yake kumhini
  Mtetezi kumfaidi

  Wote sawa sioni tofauti
  Wote hawa sawa
  Na mwanasiasa mwehu
  Ni moto wa jicho
  Wanapotabasamu nachelea kuridhia
  Hutabasamu wadhamiriapo vingine
  Tabasamu zao ni ishara ya maangamizi
  Wanipangiayo kimoyomoyo ,kimyakimya
  Wafurahie kutatarika kwangu
  Kwenye tanuri hii ya Maisha

  Maswali
  1. Tambua wahusika watatu katika shairi hili (alama3)
  2. Eleza sifa mbili za wanaorejelewa katika shairi (alama2)
  3. Tambua nafsi neni katika shairi hili (alama1)
  4. Bainisha toni mbili katika shairi hili (alama2)
  5. Kwa kutoa mifano bainisha vipengele vinne vya kimtindo vilivyotumiwa katika utungo huu (alama 4)
  6. Kwa kutoa mifano eleza mbinu zilizotumiwa na mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (alama2)
  7. Bainisha aina mbili za urudiaji katika shairi (alama 2)
  8. Eleza maana ya mshata na utolee mfano kutoka kwa shairi (alama 2)
  9. Bainisha aina mbili za taswira katika shairi hili (alama 2)

SEHEMU YA B : RIWAYA CHOZI LA HERI
Jibu swali moja katika sehemu hii

 1. Lakini…
  Wewe hushangai?
  Kwani wanawashwa
  na pilipili iliyo
  kwenye uchango wa mwengine?
  Kwani wasitake kukuli
  Kilichotufanya mimi na wewe
  Kuwa marafiki wa kufa kuzikana
  Kwanu wasimulize
  alonirithisha hno mkanja?
  Kwa utu kunipoka
  akanibakishia kaka
  La!
  kiunzi cha mifupa?

  Wali wakifanyani?
  Alipokuja Bwana Mabavu
  Shamba la asili akatwaa
  ati ni yake miliki
  alonunua,
  Si kurithishwa,
  na mkoloni?
  Wali wakiwazani
  alipotuonyesha hati miliki bandia
  nasi mithili ya vifaranga
  waliomwona mwewe,
  tukajikunyata kwa uoga
  tusitoe hata kauli moja
  Kupinga ubahaimu huu?
  Dhiki ya ukosefu ikatutuma
  Kuwa vibarua
  Katika’ lake’ shamba?

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
  2. Tambua mbinu sita za kimtindo zilizotumiwa katika utungo huu (alama6)
  3. Kwa kurejelea utungo mzima fafanua umuhimu wa mnenaji katika kujenga riwaya. (alama10)

   AU
 2. Baba umewahi kumwona mtoto wa miaka hamsini ambaye hajasota…
  Kwa kurejelea riwaya nzima dhibitisha kuwa mtoto anayerejelewa hajasota. (alama20)

SEHEMU YA C: TAMTHILIA YA KIGOGO-
(Jibu swali moja kutoka sehemu hii)

 1. Huwezi kuandamana na wavuvi kama kitoweo hukitaki!
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
  2. Tambua mbinu za kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Fafanua umuhimu wa msemaji kwa kurejelea tamthilia nzima (alama 4)
  4. )Fafanua umuhimu wa mandhari ya Mangweni katika kuendeleza tamthilia ya Kigogo
   (alama10)

   AU
 2. Kwa kurejelea tamthilia nzima ,jadili jinsi mwandishi alivyotumia jazanda (alama 20)

SEHEMU YAD: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

 1. Wako wapi?Wamepuuzwa tu kulee! Futari kwa niaba.Sikukuu kwa niaba.Harusi kwa niaba.
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
  2. Tambua mbinu za kimtindo katika dondoo hili (alama 3)
  3. Fafanua sifa za mnenaji ( alama3)
  4. Jadili maudhui yanayojitokeza katika dondoo kwa kurejelea hadithi nzima (alama5)
  5. Kwa kutoa hoja tano jadili ufaafu wa anwani ya hadithi husika. ( alama5)

   AU
 2. Kwa kurejelea hadithi zifuatazo,jadili changamoto wanazopitia Watoto; (alama 20)
  1. Tulipokutana Tena
  2. Mame Bakari
  3. Ndoto ya Mashaka

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

 1. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.

  Mimi ni Olichilamgwara
  Olichilamgwara mwana mbee wa Ojilong
  Ojilong wa Marukatipe
  Wazee waliposhindwa
  Nilivuka misitu milima na mito
  Ni mimi jabali
  Kipande cha jifya la mama
  Nilipokuwa nalisha mifugo
  Nilisikia baragumu inalia
  Baragumu ya wito
  Mifugo wa mtemi wamechukuliwa
  Nikachukua mkuki wangu
  Wenye kigumba cha mti
  Nikachukua upanga wangu
  Wenye makali kama mmweso wa radi
  Upanga uliopasua pembe za nyati kwa dhoruba moja
  Ndipo nilipofyatuka kasi kama umeme
  Kufumba kufumbua nikawakaribia nduli
  Kusikia vishindo vyangu wakaanza kubabaika
  Kuona kifua changu cha manyoya ya kanga wakatetemeka
  Macho yangu makali kama kaa la moto yalipowatazama wakakimbia
  Mkuki wangu ulipaa kama umeme
  Wote wakalala
  Mifugo wakanifuata…
  Mko wapi vijana
  Mmekuwa kama majivu baada ya moto kuzimika?

  Maswali
  1. Tambua kipera ulichokisoma na udhibitishe jibu lako. (alama 2)
  2. Tambua sifa za jamii zinazosawiriwa katika utungo huu (alama 2)
  3. Kwa kutoa mifano bainisha vipengele vinne vya kimtindo vilivyotumiwa na nafsineni (alama 4)
  4. Fafanua sifa nne za kipera hiki (alama4)
  5. Eleza mambo manne ambayo mtendaji wa kipera hiki anaweza kufanya ili kufanikisha utendaji wake. (alama4)
  6. Fafanua mikakati ambayo jamii inaweza kutumia ili kuzuia tungo kama  hizi kufifia. (alama 4)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.          
  1. Mtu mnyonge/ anayenyanyaswa
   - Watetezi wa haki
   - Wanasiasa (3x1)
  2.        
   1. Walaghai – hutabasamu wadhamiriapo vingine
   2. Katili – Tabasamu zao ni ishara ya maangamizi
   3. Wabinafsi – Huhini haki za wanyonge ili kujifaidi
    ( za kwanza 2x1)
  3.      
   1. mnyonge
   2. anayetazama wanyonge wakinyanyaswa
   3. mtetezi wa haki.
    (1x1)
  4.     
   1. Toni ya huzuni – ninahuzunika!
   2. Toni chuki – nachukia
   3. Toni ya kutoridhika – wote hawa sawa!
   4. Toni ya malalamiko.
   5. Toni ya hasira.
    ( hoja za 2x1).
  5.        
   1. Uhuishi - tabasamu kunyonga tumaini, mtetemo kunivaa
   2. urudiaji(takriri) Salama! Salama! Kimya kimya
   3. Istiara(jazanda) – mwanasiasa ni moto wa jicho
   4. Tanuri ya maisha – matatizo (mateso)
   5. Mdokezo – mzee…. Ndugu…
   6. Nidaa – Salama! Salama!
   7. Kinaya – wanaorejelewa wanatabasamu ilhali wanawahini wanyonge haki zao
   8. Usambamba – wote hawa sioni tofauti wote hawa sawa.
    ( Kadiria uhuru wowote wa kishairi km kuboronga sarufi ,inkisari nk.)
    (Zozote 4x 1.)
  6.          
   1. kubananga sarufi – haki yake kumhini – kumhini haki yake
    Mkononi kumtia – nachukia zao nyendo – nachukia nyendo zao
   2. Mazda – maguvu – nguvu
   3. Inksari – nachola – ninachelea
    ( zozote 4x1)
  7.    
   • urudiaji wa maneno – salama kimya kimya
   • urudiaji wa kirai. – wote hawa( vifungu vya maneno)
   • urudiaji wa silabi – na, ngu wa
    kutaja ½
    mfano ½ (Jumla 2)
    (za kwanza 2x1)

  8. Ni mstari ambayo haijitoshelezi kimaana/ haijakamilika kiujumbe m,f
   • Nitafakuripo kwa tuo..
    Kueleza maana 1
    Mfano 1

    Jumla 2
  9.        
   • taswira hisi – ninahuzunika
   • taswira mwendo – wanijiapo
   • taswira mguso – wanisalimiapo
   • taswira oni – nitazamapo
    ( za kwanza 2x1)

 2. CHOZI LA HERI
  1.          
   • msemaji – shamsi/wimbo wa Shamsi
   • msemewa – Ridhaa/ matajiri wanaomtazama
   • anaelekea nyumbani( Kazikeni)
   • Ridhaa anausikiliza wimbo huo akiwa kwake katika Mtaa wa afueni./ Shamsi anajaribu kutoa hisia zake za kutamauka mf. Ukosefu wa ajira, kifo cha babake.
    (4x1)
  2.       
   • maswali ya balagha wewe hushangai?
   • mdokezo lakini …
   • Mdokezo wa methali .. “pili pili iliyo kwenye uchango wa mwengine”
   • Msemo – marafiki wa kufa kuzikazana
   • Inksari – alonirithisha (alionirithisha)
   • Nidaa – La!
   • Kuboronga sarufi – ati ni yake milki – ati ni milki yake
   • Tashbihi – mithili ya vifaranga waliomwona mwewe uhusishi – dhiki ya ukosefu ikatutuma kuwa vibarua ( za kwanza 2x1 = 2)
  3.       
   • kupitia kwa Shamsi maudhui ya umaskini yanakuzwa – umaskini uliwatuma kuwa vibarua.
   • Shamsi anakuza maudhui ya elimu anasema alisoma kwa bidii na kuhitimu elimu ya chuo kikuu
   • Shamsi anawakilisha vijana wanotamauka baada ya kusoma na kukosa ajira. Anajitosa katika unywaji wa pombe haramu
   • Shamsi anakuza maudhui ya utabaka anasema kuna matajiri wanaomtazama wakiwa roshani
   • Kupitia kwake tunapata kuona dhiki wanazopatia wafanyakazi m.f mishahara duni.
    Kutopandishwa vyeo na kufutwa kazi
   • anaonyesha athari za uongozi mbaya ukosefu was chakula dawa n.k
   • Anakuza maudhui ya ufisadi licha ya wao kusoma nafasi za kazi zilitwaliwa na ndugu za wenye vyeo “ viganja huoshana aso mwana aeleke jiwe! Hati miliki babdea
   • anakuza maudhui ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana “Kwani hawakunikabidhi kazi walizoahidi kwenye mabuko?
   • anaendeleza dhamira ya mwandishi ya kuwahimiza wanyonge wazitetee haki zao.Anashangaa kwa nini wazazi wake hawakupinga hatua ya Bwana Mabavi ya kunyakia shamba
   • Kupitia kwake tunapata sifa za babake kama mwenye bidii “ kwa uzee kushika mpini kujisulubu riziki azumbue karo alipe”
   • unyanyasaji
   • ukengeushi
   • Kuendeleza ploti
   • ulevi
   • ubaguzi
    (zozote 10 x 1 = 10)
 3.           
  1. Bado nchi hii inakumbwa na umaskini asilimia kubwa ya raia hawamudu gharama ya matibabu ya kimsingi
  2. vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano kusababishwa na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora
  3. Asilimia kubwa ya wakazi hawawezi hata kumudu kula mara mbili kwa siku njaa – babake Shamsi anakula mizizi mwitu
  4. Watu wengi wanafanya kazi za kijungu jiko
  5. Kampunii za kigeni kuhusishwa katika kuchumbua madini
  6. Mishahara ya wenyeji wanaopata ajira ni duni
  7. Wananchi wahafadhina bado hawajakumbatia uongozi wa mwanamke Bi Mwekevu anaposhinda uchaguzi kunakuwa na vurumai(Ukosefu wa demokrasia)
  8. Kuna ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana walioelimika kama Shamsi asemavyo katika wimbo wake.
  9. Ukabila : Ndoa kati ya kabila tofauti kutoruhusiwa m.f Waombwe na Anyamvua Lucia – na kiriri kang’ata
  10. Nchi ya wahafidhina bado inashuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe – baada ya uchaguzi
  11. Watoto wa nchi hii bado wanakandamizwa m.f ulanguzi wa watoto Dick/mwaliko , ubakaji – Lime mwanaheri
  12. Ndoa za mapema zinazidi kushuhudiwa m.f Pete kuuzwa kwa fungo
  13. Nchi ya wahifadhina bado inakumbatia mila zilizopitwa na wakati, tohara ya wasichana m.f Tuama
  14. Polisi na wanajeshi bado wanatatua mizozo midogo midogo kwa makeke na bunduki. Jambo ambalo limepitwa na wakati k.m Extra – Judicial killings
  15. Mikasa inapotokea nchi hii hungojea vikosi vya kigeni kuja kuwaokoa manusura
  16. Watoto/vijana wa nchi hii kuhusishwa katika biashara haramu m.f ulanguzi wa dawa za kulevya Dick
  17. Bado wananchi hawa wanajihusisha na unywaji wa pombe haramu m.f Shamsi kipanga na wengine kufariki.
  18. Nchi hii haijaweza kupiga vita ufisadi wanaopata kazi kwa njia isiyohalali. Unyakuzi wa ardhi m.f babake Shamsi
  19. Serikali ya nchi hii bado haijaweza kufadhili masomo(elimu) mikopo na ruzuku haitoshi
  20. Utepetevu miongoni wa polisi, hawatimizi jukumu lao la kuwatafuta wanuna wake
   Umulkheri. Walitia juhudi za kuwatafuta katika kaburi la sahau.
  21. Huduma za matibabu ni za hali ya chini Selume analalamikia ukosefu wa vifaa katika kituo cha afya cha umma alichohudumu hapo awali. Wagonjwa wanajifia kwa kukosa huduma za kimsingi.
   ( kadiria hoja zaidi. Zozote 20x1)

 4. Huwezi kuandamana na wavuvi kama kitoweo hukitaki!
  1.          
   1. Msemaji: Ngurumo
   2. Msemewa: Tunu
   3. Mahali : Mangweni kwa Asiya(Mama Pima)
   4. Tunu na Sudi walikuwa wameenda Magweni ili Tunu adhibitishe kuwa aliyemua mila ni Ngurumo na wenzake/ wanaharakati walikuwa wameenda kuwaalika watu katika mkutano ( zozote 4x1)
  2. Nidaa – hutaki! Jazanda(Istiara) wavuvi na kitoweo – walevi na pombe. ( zozote 2x1)
  3. Ni kielelezo cha vijana wanaotumiwa na viongozi kutimiza malengo yao hasi
   • Anatambulisha wanajamii wenye taasubi ya kiume “heri nipigie kura paka wa Majoka kuliko mwanamke
   • Kifo chake kindhihirisha usaliti wa majoka – kimba ni kimba tu”
   • Anawakilisha watu waliopotoka kiamaadili ana uhusiano wa kimapenzi na Asiya mkewe Boza
   • Ametumiwa kuoonyesha ukatili wa viongozi wanaotumia vijana kutekeleza maovu na kuuwa wapinzani wao
   • Ametumiwa kuonyesha jinsi baadhi ya vijana wanavyotekwa nyara kimawazo na kuunga mkono utawala dhalimu
   • Ametumiwa kuonyesha jinsi vijana walivyopotoka kwa kushiriki ulevi bila kujali afya yao
   • Kupitia wimbo wake tunafahamu Tunu hajaolewa.
   • Anajenga tabia za wahusika wengine ( Zozote 4x1)
  4.                 
   • Katika mandhari haya tunafahamishwa kwamba Ngurumo na Tunu walisoma pamoja
   • Katika madhari haya tunafahamu kuwa Siti pia alikuwa akinywa pombe
   • Mandhari haya yanadhihirisha jinsi nafasi ya mwanamke ilivyodhalilishwa katika jamii hii – Ngurumo anasema kama hampi kura yake Majoka heri ampe paka wake lakini si mwanamke
   • Mandhari haya yanakuza maudhui ya ubinafsi – Ngurumo anasema tangu soko lifungwemauzo yao yamekuwa maradufu hivyo basi hapana haja ya soko kufunguliwa
   • Maudhui ya utamaushi yanakuzwa katika mandhari haya – watu wamehamia Mangweni kuuguza majeraha yao baada ya soko kufungwa
   • Maudui ya ufisadi yamekuzwa – mama Pima amepewa kibali cha kuuza pombe haramu na serikali
   • Athari za pombe haramu zimemulikwa katika mandhari haya- vijana wamezikwa na wengine kupofuka
   • Ni katika mandhari haya ambapo Tunu anapata kujua aliyemvamia ni Ngurumo.
   • Ukosefu wa haki pia umemulikwa katika mandhari haya – “Illi uitwe mwizi lazima ushikwe na michuzi au kinofu hapa Sagamoyo”
   • Uhusiano wa kimapenzi kati ya Ngurumo na mama Pima unafichuliwa katika mandhari haya “Keki za uroda”
   • Ujinga wa baadhi ya wahusika kama vile Ngurumo unadhihirika, Hawaelewi na kuwatambua mashujaa halisi ni waliokuwa vitani walikufa kwa ajili yao
    (Zozote 10 x 1 = 10)

 5. Jazanda ni mlinganisho wa vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi
  • Sumu ya nyoka – kurejelea dawa za kulevya au pombe hatari na haramu
  • Maji machafu na harufu mbali sokoni – maovu ya kiutawa uliotokana na utovu wa maadili wa viongozi
  • Keki ya taifa – raslimali za nchi ambazo zinawanufaisha viongozi tu na jamaa zao huku wananchi wa kawaida wakipata mapato duni
  • Wanafunzi kuwa makabeji – Wanafunzi kuathirika akili kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya
  • Kuku na kipanga – kuku ni wanajamii kipanga ni viongozi haki haupatikani kwa urahisi
  • Wingu la kupita na la kutanda – maandamano yanayoendelea
  • Kukata mti kufurusha ndege – ilikuwazuia watu kuandamana, viongozi waangamizwe.
  • Chombo cha usafiri na rubani – uongozi na kiongozi (Uongozi mbaya wa Majoka)
  • Chombo cha babu kutikisa chombo cha Majoka – tofauti zao za kiaadili. Majoka hayuko tayari kubadilika
  • Kisima kilichiingiwa paka na maji yasiyonyweka – uharibifu na maangamizi – kuporomoka kwa uongozi wa Majoka.
  • Mshumaa uwakao – kiongozi anayefaa kuwaletea wengine matumaini na kuwaendeleza
  • Ulaji wa asali ya nyuki- msaada au maafikio ya mtu.Ashua amemkumbuka msaada alioupata awali na kurejea kwa majoka kupata usaidizi Zaidi.
  • Ziwa la damu itiririkayo mikononi damu Majoka aliyomwaga kutokana na mauaji ya kiutawala
  • Ngawa na minyororo iliyomfunga Majoka utabiri wa kuporomoka kwa utawala wake na labda kutiwa gerezani
  • Udongo na mfinyanzi – udongo ni watu dhaifu wa chini . mfinyanzi ni viongozi – wanyonge hawana uwezo wa kupinga viongozi
  • Udhibiti mwendo – njia za kuzuia wanaharakati kama /tunu
  • Kucheza na Simba anayenyonyesha – kufanya kitendo cha hatari
  • Chatu – kikosi cha kutekeleza maovu na mateso
  • Msumari kusema ukweli
  • Kuwaka moto – mambo kuwa mabaya
  • Shamba limekushinda kulima – Sudi – kushindwa kumdhibiti mkewe
  • Panya amejileta mwenyewe kwa paka
   Ashua amejileta ofisini mwa Majoka ambaye amekuwa akimtamani
   Kutia vyanda kwenye mdomo wa Simba kufanya kitendo hatari
  • Jukwaa la mbao na magunia – kuonyesha uduni na umaskini wa watu wa tabaka la chini
  • Pango la joka – eneo hatari – Tunu anatahadharishwa kwenda mkutanoni
  • Kubeba maisha kwa mbeleko – usiyachukulie mambo kwa uzito sana
  • Kujipaka matope – kuharibu sifa – Majoka anahofia kuharibiwa sifa wakati wa maandamano.
   (Zozote 20 x 1 = 20)
 6.           
  1.         
   1. Mnenaji – Mbura
   2. Mnenewa – sasa
   3. Wapi – Nyumbani kwa mzee Mambo
   4. Mzee Mambo alikuwa ameandaa sherehe kwa mtoto wake wa kwanza anaingizwa nasari na wa pili ameanza kuota meno
    ( 4 x1 = 4)

  2. Balagha – wako wapi
   Nidaa – wamepuuzwa tu kulee!
   Urudiaji (takriri) kwa niaba
   Kudumisha sauti – kulee!
   Zozote 3 x1 = 3
  3. Mlafi – alikula chakula kingi
   • Mtetezi wa haki za wanyonge anasema kuwa kula kwa niaba ya maskini ni dharau.
   • Mwenye busara – anaelewa kuwa shibe ilikuwa ikiwamaliza kwa namna mbalimbali m.f magonjwa n.k
   • Mzalendo anawatetea wanyonge wa nchi yake na kuupanda mchele wa kwao Mbeya
   • Ni mweye utu – anataka wananchi pia wale kwa naiba ya viongozi
   • Ni mtambuzi – anatambua kwamba wananchi wanaendelea kukumbwa na dhiki hukuviongozi wakiendela kujifaidi
    Zozote 3 x1 = 3
  4.         
   • tabaka la utawala limejawa na ubinafsi – wanakula kwa niaba yaw engine.
   • Mambo anatumia raslimali ya taifa kuandaa sherehe za watoto wake
   • DJ anapata huduma zote za kimsingi kama maji, umeme bila malipo ilhali maskini hulipia yote
   • DJ anapata dawa za duka lake kutoka kwa bohari ya serikali anasema hajali
   • Mwandishi anasema waliopewa hawapokonyeki
   • Ubinafsi unawamaliza wabinafsi na kuwaletea magonjwa kama saratani, presha n.k
   • Sasa anafurahishwa na tabia yao ya kula kwa niaba ya watu wengine
   • Katika sherehe watu walikula na kurudia tena na tena hadi wengine wakabeba kama Mbura
   • Sasa anasema kuwa walio navyo walikula kwa niaba ya wengine waliopo na watakaozaliwa kwa hivyo kizazi kijacho hakitapata raslimali
   • DJ na wenzake wanachota mabilioni ya serikali katika sherehe
    (Zozote 5 x 1 = 5)

  5. Kwa sababu ya kula watu wamepata magonjwa mbalimbali kama presha…
   • Kwa ajili ya kula wameleta vifo kwa kuuana mabomu, risasi na kunyongana
   • Kula kumewafanya wauane kufikiria kimawazo hivyo basi wanabaki nyuma kiamendeleo
   • Shibe inawamaliza kupitia watu kunyang’anyana vitu vinavyoonekana na visivyoonekana kama haki, heshima, utu na uhuru
   • Waliopo wanakula kwa niaba ya wengine waliopo na watakaozaliwa; watakaozaliwa hawatapata chochote ila matatizo ya kulipia mikopo
   • Mzee mambo anaandaa sherehe zisizo na maana kwa taifa lake. Maandalizi haya yanafanywa kwa kutumia raslimali za umma
   • Kwenye sherehe walikula vyakula vya kila aina, vitamu, vichacho, vikali ana baridi, mchele wa basmati. Plastiki matokeo yake ni maradhi ya kila aina na vifo.
    (za kwanza 5 x 1 = 5)

 7. HADITHI FUPI – TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGE
  1. Tulipokutana Tena
   • Bogoa ananyimwa haki ya kulelewa na wazazi wake na kupelekwa kwa Bi Sinai
   • watoto kukosa mapenzi ya walezi wao. Bogoa anasema kwa Bi Sinai kulikuwa Jehanamu, alitukanwa
   • watoto kunyimwa haki ya elimu. Bogoa hakupata nafasi ya kusoma; anafurahi anapofundishwa Abjadi na Sebu
   • watoto kunyimwa haki ya kucheza Bogoa alikatazwa kucheza na watoto wengine na Bi Sinai
   • watoto kutumikishwa; Bogoa anatumiwa na Bi Sinai kupika maandazi kisha kuyauza shuleni
   • watoto kudanganywa ; Bogoa alidanganywa na babake akikubali kwenda kuishi kwa rafiki yake angekula vizuri avae vizuri na kupelekwa shule. Huu ulikuwa uongo .
   • watoto kutopewa nafasi ya kujieleza. Babake Bogoa anakosa kumsikiliza alipokuwa akijieleza kuwa hakutaka kwenda mjini – Babake anatisha kumchapa
   • watoto kutenganishwa na ndugu zao
   • watoto kutopewa lishe bora; Bogoa alipewa makombo baada ya kila mtu kula; alikula kwenye sufuria wengine wakila sahanini
   • Bogoa anatenganishwa na ndugu zake anapopelekwa kwa Bi Sinai
   • Watoto kukosa mahitaji ya msingi, Bogoa kukosa hata sabuni, mavazi na viatu
    (anatembea miguu safari ndefu bila viatu)
   • kudhulumiwa – kuchomwa

  2. Mamake Bakari
   • Watoto kudhulumiwa kimapenzi Sara anabakwa na janadume anapotoka kudurusu twisheni
   • Watoto kutoaminiwa, Sara anasema kuwa hata angemwambia babake kwamba amebakwa hangemwamini
   • Watoto kufukuzwa shuleni; Sara anasema kwamba angakabidhiwa barua ya kufukuzwa shuleni “Hatufundishi wanawake hapa tunafundisha wasichana”
   • Watoto kutengwa na wenzao, Sara anasema kuwa wanafunzi wengi wangemtenga kama mgonjwa wa ukoma wangebaini kuwa ni mjamzito

  3. Ndoto Ya Mashaka
   • Watoto kuwa mayatima, Mashaka anaachawa na wazazi wake wanapofariki
   • Ajira ya watoto – Mashaka anajihusisha na kazi ya vibarua ili kusaidiana na Biti Kidebe
   • Watoto kulelewa katika mazingira duni – mazingira ni machafu na hapakaliki
   • Wakati wa mvua – watoto wa Mashaka na Waridi wanateseka
   • Watoto kukumbwa na umaskini – watoto wa Mashaka na Waridi wanaishi maisha ya kimaskini, hawana malazi, wanalala katika chumba cha Jirani yao (Chakupewa)
   • Watoto kutenganishwa na wazazi wao waridi anawatenganisha watoto na baba yao wanapoenda Yemeni
    ( Zozote 20x1 = 20)
 8.                           
  1. .   
   • Ni majigambo /vivugo
   • Matumizi ya mimi ni…. (1x2)
  2.       
   • Ni wafugaji – nilipokuwa nalisha mifugo
   • Ni wezi wa mifugo – mifugo wa mtemi wamechukuliwa
   • Wanajihusisha na vita (2x1)
  3.           
   • istiara(sitiari) Ni mimi Jabali
   • Tashbihi – kiasi kama umeme
    • Ulipaa kama umeme
    • Kama mmweso wa radi
   • Mdokezo – mifugo ikanifuata…
   • Swali la balagha – mmekuwa kama majivu baada jua moto kuzimika?
   • Chuku – upanga kupasua pembe za nyati kwa dhoruba moja
   • Msemo – kufumba na kufumbua
   • Urudiaji(takriri) nikachukua mkuki wangu
    • Nikachukua upanga wangu
    • Matumizi ya mishororo mishata m.f wazee waliposhindwa
    • Nilipokuwa nalisha mifugo…
   • Uhuishi – mkuki kupaa
   • Usambamba – nikachukua mkuki wangu , nikachukua upanga wangu
  4.           
   • anayejigamba hutunga kufuatia tukio mahususi katika maisha yake - anakumbuka alivyokomboa mifugo ya Mtemi kutoka kwa wezi.
   • Huwa na matumizi ya chuku
   • Kwa kawaida hutungwa na kughanwa na wanaume
   • Hutolewa kwa nafsi ya kwanza m.f Nikachukua mkuki wangu
   • Anayejisifu huweza kutaja usuli wake wa kinasaba m.f Ochilamgwara mwana mbee wa Ojilong
   • Maudhui makuu ni ushujaa
   • Hutungwa kwa usanii mkubwa – sitiari urudiaji tashbihi n.k
  5.        
   • Avae maleba – mkuki , upanga ngozo
   • Atomie kiimbo na toni kupanda na kushuka kwa sauti yake
   • Atumie miondoko ya mwili
   • Atumie ishara za uso
   • Ashirikishe hadhira kwa kuuliza maswali ya balagha.
    Kadiria hoja zaidi (za kwanza 4 x 1 = 4)
  6.           
   • Kufanya utafiti Zaidi
   • Kuhifadhi kwenye kanda tepu rekodi video n.k
   • Kufunza shuleni
   • Kupanga mashindano kati ya jamii mbalimbali
   • Kuhifadhi katika maandishi
   • Kuhimiza watu kutunga tungo kama hizi.
   • Shere mbalimbali
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest