Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA 2: LUGHA.

MAAGIZO

  • Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  • Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  • Jibu maswali yote.
  • Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  • Usitoe ukurasa wowote kutoka kwenye kijitabu hiki.
  • Karatasi hii ina kurasa 9 zilizochapishwa.
  • Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
  1. UFAHAMU ( ALAMA 15)
    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuta.

    Ufisadi ni jinamizi ambalo limekuwapo ulimwenguni kote kwa miaka na mikaka. Madhara ya utoaji na ulaji rushwa kwa nia ya kujitajirisha au kupata upendeleo fulani haliwezi kupuuzwa. Ni jambo ambalo li kinyume na maadili au kaida za kijamii. Mojawapo ya madhara ya ufisadi ni kuwepo kwa maendeleo duni nchini. Kudorora kwa maendeleo nchini kumesababishwa na athari hasi mbalimbali za ufisadi. Kutolewa kiasi fulani cha darahima kama hongo ni kiini mojawapo cha kuwapo kwa maendeleo finyu nchini. Hii ni kutokana na ukweli kuwa chirimiri husababisha kupunguzwa kwa kiasi cha fedha za kutekeleza miradi mbalimbali. Si ajabu wafanyakazi wa kutekeleza miradi kukosa kulipwa au kupunjwa kwa kupewa mshahara wa kijingujiko, kukosa kulipwa au hata kulipwa nusu ya mshahara.

    Visa vya ubadhirifu wa pesa zilizotengewa miradi mbalimbali vimeripotiwa katika maeneo tofauti tofauti nchini. Aghalabu, jambo hili hutendwa na wasimamizi wa hazina ya maendeleo. Mathalani, inasikitisha kuwa baadhi ya watumishi wa umma hutumia fedha za maendeleo katika safari humu nchini na hata ughaibuni zisizo na manufaa kwa taifa. Wao hukosa uaminifu na huongozwa na tamaa na ubinafsi uliopita mipaka. Watu hawa hupuuza ukweli kuwa tamaa huja kabla ya mauti. Jambo hili huifanya miradi lengwa kunyimwa pesa zinazohitajika.

    Kutokana na ufisadi, kumekuwa na miradi ya kiwango cha chini. Hii ni kutokana na kununuliwa kwa malighafi ghushi ya kutumiwa viwandani au hata katika ujenzi wa miundombinu. Ukweli ni kuwa miradi inayotekelezwa hudumu katika hali nzuri kwa mwia mfupi tu. Hatimaye ukarabati wa miradi iliyofanywa huanza ; hali inayosababisha matumizi mabaya zaidi ya pesa za umma.

    Aidha, kudinda kwa wafadhili wa miradi mbalimbali kuipa nchi pesa kuanzisha na kuendeleza miradi fulani hutokana na ufisadi. Wahisani hawa huhofia matumizi mabaya ya ghawazi. Matokeo yake huwa kutotekelezwa kwa miradi mikubwa ambayo huweza kuwa kitega-uchumi kwa watu wengi nchini. Kwingineko miradi mingi hukosa pesa za kutosha na kuifanya kutokamilika ipasavyo.

    Isitoshe, kupakwa mafuta viganjani kwa wanaostahili kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa imefikia kiwango kinachohitajika ni sababu nyingine ya maendeleo duni. Ni kutokana na hongo wao huidhinisha kazi duni. Kwa mfano, kuporomoka kwa majengo ambako tumeshuhudia mara kadha na kusababisha vifo kunatokana na utepetevu huu. Watu wengi hupoteza mali huku mchango wa kuleta maendeleo kwa waliolemaa ukiadimika.

    Ni wazi kabisa kuwa kiasi kikubwa cha miradi dhaifu hutokana na chauchau. Serikali pamoja na wananchi wana jukumu kubwa la kuliangamiza janga hili.

    Maswali
    1. Fafanua vikwazo vitano vya maendeleo ya nchi na jamii ( alama 5)
    2. Taja na ueleze mbinu nne za kimtindo ambazo zimetumika katika kifungu (alama 4)
    3. Eleza jinsi washikadau mbalimbali wanavyoonyesha uwajibikaji kwa mujibu wa kifungu hiki. ( alama4)
    4. Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kulingana na muktadha wa matumizi yake kifunguni. ((alama 2)
      1. ghawazi……………………………………………………………………………………………
      2. kupakwa mafuta viganjani………………………………………………………………………..

  2. UFUPISHO (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

    Kiswahili tunasema ni lugha yetu kwa sababu ndiyo lugha ya Kiafrika inayoongewa katika nchi nyingi Barani Afrika. Ni lugha yetu kwa sababu ni lugha asilia mojawapo za Afrika. Siyo lugha iliyoletwa na watu wa nchi za nje kama vile Kiingereza, Kifaransa na Kireno. Uzuri wa Kiswahili sasa ni kuwa kimeenea kote Afrika Mashariki na Kati.

    Wenyeji asilia waliokuwa wakiongea lugha hii tangu awali ni Waswahili. Waswahili hawa hata leo wako na wanaendelea kuitumia lugha hii kama lugha yao ya mama, kama vile Wakikuyu watumiavyo Kikikuyu, Wakamba, Kikamba na Wadigo lugha ya Kidigo. Makao yao Waswahili tangu jadi yanapatikana kaunti za Pwani. Makao yao yameanzia upande wa Kaskazini Mashariki mwa Kenya , na wanapakana na nchi ya Somalia huko. Wameenea katika upwa huo wa Pwani, ikiwemo Lamu, Malindi, Mombasa, Pemba, Unguja, Visiwa vya Ngazija na kuendelea.

    Lugha ya Kiswahili ina lahaja nyingi kulingana na sehemu wanamoishi. Kwa mfano, Waswahili wa Lamu huongea lahaja ya Kiswahili inayoitwa Kiamu. Waswahili wa Mombasa huongea lahaja ya Kimvita. Pemba wanaongea Kipemba, Ngazija lahaja ya Kingazija, Unguja lahaja ya Kiunguja na kadhalika. Kutokana na lahaja hizi na nyinginezo za Kiswahili ambazo hazikutajwa hapo, wataalamu wa lugha walitokea na Kiswahili sanifu. Hiki Kiswahili sanifu ndicho kitumiwacho katika mafunzo ya shule, uandishi wa vitabu na mawasiliano ya kiserikali na kibiashara.

    Nchini Kenya, kwa muda mrefu Kiswahili hakikuthaminiwa kama Lugha ya Kiingereza. Sababu mojawapo ni kuwa Kiswahili hakikufanywa somo la lazima katika rasimu za shule, wala kutahiniwa katika shule za msingi. Hata katika shule za upili, katika kufunzwa na kutahiniwa hakikupewa umuhimu wowote. Kwa ajili hii wanafunzi wengi waliacha kujifunza Kiswahili kama somo. Hali hiyo ilifanya Kiswahili kuonekana kama lugha inayoongewa na wale watu wasio na kisomo ama elimu nyingi. Kwa ajili ya fikira hizi, watu wengi wamekuwa wakikichukia, kukidunisha na kujaribu kuongea Kiingereza kila nafasi inapojitokeza.

    Miaka michache iliyopita, Kiswahili kilianza kutiliwa mkazo katika shughuli zote nchini Kenya. Kwa upande wa msimamo wa nchi lugha hii ilionekana yenye manufaa katika kuleta umoja na kuwaunganisha wananchi wote. Jambo hili ni muhimu kwa maendeleo ya nchi iwayo yote. Umoja huleta maelewano na undugu. Hali hizi mbili zinapokuwapo, amani husambaa nchini mote.

    Tukitazama mfumo wa elimu wa 8-4-4, Kiswahili kimepewa nafasi sawa katika ratiba za shule kama lugha ya Kiingereza. Kiswahili kinatahiniwa kama somo muhimu kuanzia shule ya msingi hadi shule ya upili. Kinyume na enzi za zamani, siku hizi mwanafunzi anayesoma Kiswahili, hata asipofaulu vizuri katika lugha ya Kingereza ana nafasi sawa ya kupata kazi kama wengine.

    Maswali
    1. Fupisha aya tatu za mwanzo kwa maneno 80. (alama 6, utiririko 1)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Fupisha aya ya nne kwa maneno 40 (alama 5, utiririko 1)
      Matayarisho
      Jibu
    3. Onyesha jinsi mtazamo kuhusu lugha ya Kiswahili ulivyobadilika (maneno 50) ( alama 4)
      Matayarisho
      Jibu

  3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
    1. Unda neno lenye muundo ufuatao: (alama 2)
      1. Irabu ya juu, nyuma + nazali ya ufizi, ghuna + kipasuo cha ufizi, ghuna + irabu ya chini, kati
      2. Kiyeyusho cha mdomo+ irabu ya juu tandazwa + kipua cha midomoni +irabu ya chini
    2. Onyesha muundo wa silabi katika neno lifuatalo: ( alama 1)
      mchwa
    3. Tia shadda katika meneno yafuatayo kuonyesha dhana katika mabano: ( alama 2)
      1. Ala ( kifaa)
      2. Ala! ( kihisishi)
    4. Tunga sentensi katika wakati ujao hali ya mazoea. ( alama 2)
    5. Andika sentensi ifuatayo katika udogo wingi ( alama 2)
      Nyundo za wazee wale zimevunjwa na mwana wake
    6. Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee chenye dhana ya “badala ya” katika ngeli ya U-ZI.  ( alama 2)
    7. Akifisha ili kuonyesha usemi halisi (alama 2)
      tanya ondoka hapa mara moja
    8. Tunga sentensi ukitumia nomino dhahania inayotokana na kitenzi ‘silimu’ ( alama 2)
    9. Eleza matumizi ya mofimu ‘ji’ katika sentensi zifuatazo: (alama 2)
      1. Sauti hiyo inajirudia.
      2. Aliliua jitu hilo kwa mshale dhaifu.
    10. Bainisha sehemu za kiuamilifu za sentensi ifuatayo. ( alama 2)
      Aliwanunulia watoto mkate jana asubuhi.
    11. Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mwalimu aliniambia wataenda kwake kesho.
    12. Onyesha miundo miwili ya nomino katika ngeli ya LI –YA ( alama2)
    13. Chanaganua sentensi ifuatayo kwa kutumia mchoro wa matawi. ( alama 4)
      Huyu ndiye mwizi aliyewaibia watu pesa na atafikishwa mahakamani baadaye
    14. Tunga sentensi ukitumia kishazi tegemezi chenye dhana ya kielezi cha mahali. (alama 2)
    15. Kanusha (alama 2)
      Mwamu wangu alinilea na kunielimisha.
    16. Andika sentensi ukitumia kitenzi – cha katika kauli ya kutendewa. (alama 1)
    17. Onyesha mofimu katika neno ( alama 3)
      Aliowapa
    18. Andika kitenzi kifuatacho katika hali iliyopo mabanoni (alama 1)
      -ja (nafsi ya pili wingi)
    19.            
      1. Kiri ni kwa kukana na ________________ ni kwa nafuu. Na sifu ni kwa___________ (alama 1)
      2. _______________ ni kwa kukubaliana na jambo , simile ni kutaka kitu kinusurike na hongera ni _____________. (alama 1)
    20. Tunga sentensi mojakuonyesha maana tofauti za neno ‘ua’ ( alama 2)

  4. ISIMU JAMII
    “ Maafisa 3 wakana kusaidia mshukiwa wa mauwaji ya watoto kutoroka kituoni.
    Maafisa watatu wa polisi jana walikana mashtaka ya kumsaidia mshukiwa wa mauaji ya watoto 13 kutoroka kutoka kituo cha polisi…”
    1. Huku ukitoa sababu mbili, tambua sajili hii. ( alama 3)
    2. Fafanua sifa zozote saba za sajili hii. (alama 7)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. UFAHAMU
    1. Fafanua vikwazo vitano vya maendeleo ya nchi na jamii ( alama 5)
      1. kutolewa kiasi fulani cha darahimu kama hongo
      2. miradi lengwa kunyimwa pesa zinazohitajika
      3. miradi ya kiwango cha chini
      4. miradi mingi kukosa pesa za kutosha na kuifanya kutokamilika ipasavyo
      5. vifo kutokana na kuidhinishwa kwa kazi duni
      6. hasara – miradi iliyofanywa kuanza kufanyiwa ukarabati baada ya muda mfupi hivyo pesa zaidi kutumika
      7. uharibifu wa mali – wakati majumba yanaporomoka
      8. ulemavu kutokana na ajali za maporomoko ya miradi duni
      9. Wafadhili wa miradi katika nchi hudinda kuipa pesa wakihofia matumizi yake mabaya hivyo miradi mikubwa ambayo inaweza kuwa kitega –uchumi kwa watu wengi nchini inakosa kutekelezwa.
      10. Wanatumia pesa za maendeleo katika safari zisizo na manufaa kwa taifa
      11. ubadhirifu wa pesa za umma na wasimamizi wa hazina ya maendeleo
      12. wasimamizi wa miradi kuidhinisha kazi duni (zozote 5x1)
    2. Taja na ueleze mbinu nne za kimtindo ambazo zimetumika katika kifungu (alama 4)
      1. Sitiari – ufisadi ni jinamizi
      2. Methali – tamaa mbele mauti nyuma
      3. Msemo – kupakwa mafuta viganjani
        - kijungu jiko
      4. Nahau – kupita mipakani/ ulaji rushwa
      5. Takriri/ urudiadi – chauchau (zozote 4x1)
    3. Eleza jinsi washikadau mbalimbali wanavyoonyesha uwajibikaji kwa mujibu wa kifungu hiki. ( alama4)
      1. Viongozi serikalini kukosa kuwalipa wafanyakazi au kuwapuja kwa kuwapa mishahara ya kijungujiko
      2. wasimamizi huwa wabadhirifu wa pesa zilizotengewa miradi mbalimbali.
      3. watumishi wa umma kutumia fedha za maendeleo katika safari zosozo na manufaa kwa taifa.
      4. wasimamizi wa miradi kuidhinisha kazi duni.
      5. wafadhili wa miradi kukosa kutoa pesa kwa kuhofia matumizi mabaya ya fedha hizo.
      6. serikali na wananchi wanakosa kuangazia na kutekeleza miradi dhaifu.
        ( mwanafunzi anaweza kuonyesha kutowajibika au kuwajibika.
    4. Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kulingana na muktadha wa matumizi yake kifunguni. ((alama 2)
      1. ghawazi – pesa/ngwenje
      2. kupakwa mafuta viganjani - kuhongwa

        Usahihishaji
        Makosa ya hijai 6 x ½
        Makosa ya sarufi yasipite ½ ya alama alizopata katika kila kijisehemu

  2. UFUPISHO
    1. Fupisha aya tatu za mwanzo kwa maneno 80. (alama 5)
      • Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayoongewa katika nchi nyingi Barani Afrika.
      • Lugha asilia mojawapo za Afrika
      • Kiswahili kimeenea kote Afrika Mashariki na Kati.
      • Wenyeji asilia waliokuwa wakiongea Kiswahili tangu awali ni Waswahili.
      • Waswahili wanaendelea kutumia Kiswahili kama lugha yao ya mama.
      • Makao ya Wasahili ni kaunti ya Pwani.
      • Kiswahili kina lahaja nyingi kulingana na wanamoishi.
      • Kutokana na lahaja hizi na nyinginezo za Kiswahili wataalamu wa lugha walibuni Kiswahili sanifu
      • Kiswahili sanifu hutumiwa katika mafunzo shuleni, uandishi wa vitabu na mawasiliano ya kiserikali na kibiashara. (Hoja 5)

    2. Fupisha aya ya nne kwa (maneno 40) (alama 4)
      • Kiswahili hakikuthaminiwa kama lugha ya Kiingereza.
      • Kiswahili hakikufanywa somo la lazima katika rasimu za shule
      • Hakikutahiniwa katika shule za msingi wala za upili.
      • Hakikupewa umuhimu wowote. (hoja 4)

    3. Onyesha jinsi mitazamo kuhusu lugha ya kiswahili ulivyobadilika ( maneno 50) ( alama 4)
      • Kiswahili kilianza kutiliwa mkazo katika shughuli zote nchini Kenya.
      • Ilionwa kama lugha yenye manufaa katika kuleta umoja na kuwaunganisha wananchi wote.
      • Kiswahili kimepewa nafasi sawa katika ratiba za shule kama Kiingereza .
      • Kinatahiniwa kama somo muhimu kuanzia shule ya msingi hadi shule ya upili.
      • Mwanafunzi anayesoma Kiswahili, asipofaulu vizuri katika lugha ya Kiingereza ana nafasi ya kupata kazi kama wengine. ( hoja 4)
        KisMEcp2qa2c
        makosa ya hijai – 6x ½
        makosa ya sarufi - 6x ½

  3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
    1. andika maneno yenye miundo ifuatayo: (alama 2)
      1. Irabu ya juu nyuma + nazali ya ufizi ghuna + kipasuo cha ufizi ghuna + irabu ya chini kati
        unda
      2. Kiyeyusho cha mdomo+ irabu ya juu tandazwa + kipua cha mdomoni +irabu ya chini
        wima ( 2x 1)

    2. Onyesha muundo wa silabi katika neno lifuatalo: ( alama 1)
      mchwa
      KKI

    3. Tia shadda katika meneno yafuatayo kuonyesha dhana katika mabano: ( alama 2)
      1. Ala ( kifaa) – ’ala/ ala
      2. Ala! ( kihisishi) - a’ la / ala ( 2x 1)

    4. Tunga sentensi katika wakati ujao hali ya mazoea. ( alama 2)
      1. Wageni watakuwa wakiingia ukumbini kabla ya wenyeji.
        ( kadiria sentensi za mtahiniwa) ( 2/0)

    5. Andika sentensi ifuatayo katika udogo. (alama 2)
      Nyundo za wazee wale zimevunjwa na mwana wake.
      • Vijundo vya vizee vile vimevunjwa na vijana vya. ( 2/0)

    6. Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee chenye dhana ya “badala ya” katika ngeli ya U-ZI. (alama 2)
      • Mwingine unahitajika na sonara.
      • Nyingine zinahitajika na masonara. ( 2/0)

    7. Akifisha ili kuonyesha usemi halisi (alama 2)
      tanya ondoka hapa mara moja
      • ½ Tanya1/2: 1/2Ondoka hapa mara moja!1/2 ( ½ x 4)

    8. Tunga sentensi ukitumia nomino dhahania inayotokana na kitenzi ‘silimu’ ( alama 2)
      Uislamu una imani thabiti mno.

    9. Eleza matumizi ya mofimu ‘ji’ katika sentensi zifuatazo: (alama 2)
      1. Sauti hiyo inajirudia.
        Ji- kirejeshi

      2. Aliliua jitu hilo kwa mshale dhaifu.
        Jitu – ukubwa ( 2x 1)

    10. Bainisha sehemu za kiuamilifu za sentensi ifuatayo. ( alama 2)
      1. Aliwanunulia watoto mkate jana asubuhi.
        • Aliwanunulia – kiarifu
        • Watoto – yambwa tendewa/ shamirisho kitondo
        • Mkate – yambwa tendwa/ shamirisho kipozi
        • Jana asubuhi – chagizo (4x ½ )

    11. Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mwalimu aliniambia wataenda kwake kesho.
      • watu fulani wataenda kwa mwalimu
      • watu fulani pamoja na mwalimu wataenda kwa mtu mwingine (2x1)
      • watu wengine wataenda kwa mwalimu
      • watu wengine pamoja na mwalimu wataenda kwa mwalimu

    12. Onyesha miundo miwili ya nomino katika ngeli ya LI –YA ( alama2)
      • Tunda - matunda – nomino zisizo chukua mofimu ya umoja lakini huchukua ma- katika wingi
      • Jicho – macho – nimono ambazo huchukua mofimu ji – katika umoja na ma- katika wingi

    13. Chanaganua sentensi ifuatayo kwa kutumia mchoro wa matawi. ( alama 4
      KisMEcp2qa3m
    14. Tunga sentensi ukitumia kishazi tegemezi chenye dhana ya kielezi cha mahali. (alama 2)
      • Wakulima wote wamekuwa wakimfuata anakoenda.

    15. Kanusha (alama 2)
      Mwamu wangu alinilea na kunielimisha.
      • Mwamu wangu hakunilea wala kunielimisha. (2/0)

    16. Andika sentensi ukitumia kitenzi – cha katika kauli ya kutendewa. ( alama 1)

    17. Onyesha mofimu katika neno (alama 3)
      aliowapa
      • a – nasfi yatatu umoja / ngeli
        -li- wakati uliopita
        -wa – yambwa/ watendewa
        - p- mzizi
        a- kiishio

    18. Andika kitenzi kifuatacho katika hali iliyopo mabanoni ( alama 2)
      - ja – (nafsi ya pili wingi)
      • Kujeni
        • Shangazi alichwewa akitoka soko. (1/0)

    19.          
      1. Kiri ni kwa kukana na ___ghali__ ni kwa nafuu. Na sifu ni kwa_______kashifu____ (alama 1) ( ½ x2)
      2. ____Hewala___ ni kwa kukubaliana na jambo , simile ni kutaka kitu kinusurike na hongera ni ____kupongeza______. ( ½ x2) (alama 1)

    20. Tunga sentensi moja kuonyesha maana tofauti za neno ‘ua’ ( alama 2)
      • Ua wa shule yetu una ua linalopendeza. ( 2x 0)
        (anaweza kutumia wingi wa ua)

  4. ISIMU JAMII
    “ Maafisa 3 wakana kusaidia mshukiwa wa mauwaji ya watoto kutoroka kituoni.
    Maafisa watatu wa polisi jana walikana mashtaka ya kumsaidia mshukiwa wa mauaji ya watoto 13 kutoroka kutoka kituo cha polisi…”
    1. Huku ukitoa sababu mbili, tambua sajili hii. ( alama 3)
      Sajili ya magazetini/ matangazo
      Sababu – kuwepo kwa anwani/mada yenye mvuto
      - matumizi ya usemi wa taarifa/ lugha ya kuripoti ( sajili 1, sifa 2x1)

    2. Fafanua sifa zozote nyingine saba za sajili hii. (alama 7)
      1. mara nyingi vichwa vya habari havizingatii sarufi – ili kuokoa nafasi katika gazeti/muda
      2. baadhi ya jumbe ya mambo ya kweli – ili kuvutia wasomaji/ wanunuzi/wasikilizaji/mtazamaji
      3. mada/ anwani huwa fupi sana nay a kuvutia- ili kuvutia wateja/ wasomaji wa gazeti/wasikilizaji
      4. lugha inayotumika hutegemea taarifa inayotolewa- kila taaluma ina msamiati wake.
      5. ujumbe huandikwa/husomwa katika aya fupifupi/ kwa muhtasari- ili kuokoa nafasi katika magazeti/muda
      6. lugha yenye kauli/ sentensi ndefundefu- ili kufafanua hoja kikamilifu.
      7. matumizi ya tarakimu badala ya maneno- ili kuokoa nafasi/kusomeka haraka
      8. lugha ya kuvutia – “mwalimu aonja asali”matumizi mengi ya chuku- “ paka amla ndovu”
      9. matumizi ya sitiari/jazanda- ili kutasfidi lugh
      10. matumizi ya lugha rahisi- ili kupasha ujumbe kwa watu wa matabaka yote.
      11. lugha ya maelezo – ili kupasha ujumbe kwa njia nyepese na kueleweka rahisi. (zozote 7x1)
      12. matumizi ya tasfida – ili kuficha ukali
      13. lugha ya picha / michoro – ili ujumbe ueleweke
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest