Kiswahili Paper 3 Questions - Maseno Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI

 1. Lazima
  Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali
  Mabibi na mabwana. Siku hii ya leo nina furaha riboribo. Furaha ghaya. Furaha inayoshinda mwanamke aliyepata salama. Mbona nisiwe na furaha na buraha katika jamii hii iliyotuka ikashinda utukufu wenyewe? Jamii hii yetu imedumu kwa miaka na mikaka. Kisa na maana? Umoja wetu. Mshikamano wetu. Undugu wetu. Muungano wetu. Sote twafahamu fika bila chembe chochote cha walakini kwamba umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Nani asiyejua utu ni ubinadamu? Kwamba kinachotutofautisha na hayawani ni utu? Utu imara na dhabiti usiotikisika wala kusukasuka katika mawimbi na dhoruba za aushi. Hakuna adinasi anayeweza kusimama tisti kama mbuyu akiwa pekee. Asiyejua kifai kwamba jifya moja haliinjiki chungu nani?
  1. Tambua kipera hiki cha mazungumzo cha fasihi simulizi. (alama 1)
  2. Huku ukitoa hoja tano, fafanua umuhimu wa kipera. (alama 5)
  3. Bainisha vipengele vya kimtindo vilivyotumiwa kuwasilisha ujumbe. (alama 3)
  4. Unanuia kutumia mbinu ya mahojiano kukusanya habari kuhusu kitanzu hiki.
   Eleza manufaa matano ya kutumia mbinu hii. (alama 5)
  5. Eleza maana ya ngomezi. (alama 1)
  6. Fafanua sifa tano za ngomezi. (alama 5)
 2. SEHEMU B: RIWAYA
  A. Matei: Chozi la Heri
  Jibu swali la 2 au la 3
  “Hajui vipi, lakini moyoni ametia nia, na penye nia bila shaka njia hupatikana. Ataanzia hapa kuyabadilisha maisha yake ya dhiki kuwa ya heri.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
  2. Bainisha vipengele viwili vya kimtindo. (alama 2)
  3. Fafanua sifa sita za mrejelewa. (alama 6)
  4. Kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri eleza jinsi wahusika wanabadilisha maisha yao ya dhiki kuwa ya heri. (alama 8)
 3. “Sijui kama umewahi kujawa na hisia za kukataliwa, ukajihisi kama mkoma aliyesiribwa kinyesi usoni?”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi kwenye dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza namna kukataliwa kunajitokeza katika riwaya. (alama 8)
  4. “Mhitaji siku zote ni mtumwa”. Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri. (alama 6)
 4. SEHEMU C: TAMTHILIA
  P. Kea: Kigogo
  Jibu swali la 4 au la 5
  “… naona watia vyanda kwenye mdomo wa simba – huo ni mchezo hasi.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Fafanua umuhimu wa mbinu ya kimtindo kwenye dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza sifa sita za anayeambiwa maneno haya. (alama 6)
  4. Kwa kurejelea tamthilia onyesha namna kutia vyanda kwenye mdomo wa simba ni mchezo hasi. (alama 8)
 5. “Kuishi ni nini kama si kuabiri katika chombo cha usakaji nafsi na majaliwa? Misimu mingine ikatunyeshea fanaka, na siku pia zikaja za kiangazi cha kadhia, chombo chenye rubani imara huhimili vishindo na hasira ya mawimbi makali. Hata hivyo, mwenye woga wa dhoruba hubakia ufukweni asibanduke, asidiriki katu kuionja shubiri na tamu ya mapambano. Ni lazima kama ibada kuisoma bahari na kusonga mbele kwa mpango, kwa kuwa hatuna budi kuishi. Kuishi kwa kutojali ni muhali, kutakuletea ajali, ajali nayo ilivyo haijali, hasara zake zitakuhasiri. Uwe si mtu tena, bali gofu la mtu linaloishi leo kama kwamba ni mwisho wa maisha. Linaloisifia jana bila kufikiria kesho yake. Linasahau kuwa safari ya kesho hupangwa leo, na jana haitarudi tena. Nasema kwa tashtiti, wa kunikosoa asimame!”
  1. Changanua vipengele vya kimtindo katika kifungu hiki. (alama 10)
  2. Hali duni ya maisha katika jamii huchangiwa pakubwa na viongozi. Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Kigogo. (alama 10)
 6. SEHEMU D: USHAIRI
  Jibu swali la 6 au la 7
  Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  Kindumbwendumbwe cha kandanda
  Ndio mwanzo kasi kimeshika
  Na vumbi kutifuliwa
  Safu ya ushambulizi naona
  Imeanza makali kukosa
  Nalo shinikizo kuelemea upande mmoja
  Kila mtu anashangilia
  Maana
  Hata mvua inyeshapo
  Mkondo wa maji hupenya palipo dhaifu.
  Ni kipindi cha lala salama
  Na si ishara nzuri kwa waliolemewa
  Chenga wanapigwa na kanzu kuvishwa
  Na washangiliaji maelfu
  Sauti wakipaaza na kelele kupiga
  Ni kilele cha wendawazimu
  Wa binadamu kujidhiki na jasho kumwaga
  Kwa kuufukuzia upepo alioutia mateka
  Kwa ngome kuujengea.
  Upande mmoja umenywea
  Na kutegemewa kurambishwa
  Ila nitazamapo kwa tuo
  Naona walinda ngome
  Misuli yao bado imara
  Miguu yao bado haijawasaliti
  Mbinu zao bado hazijapata kutu
  Nguvu zao bado hazijanywea
  Hawawezi kushambulia kwa makali
  Lakini ngome yao bado ni tisti.
  “Endeleeni kuimarisha ngome
  Na yao mikwaju kuzuia
  Kipindi cha majeruhi bado kiko mbali
  Wala hiki sidhani kitalala salama
  Karibuni nao wataanza kunywea
  Na tamaa kukata kwa bao kukosa.”
  Nani asiyejua binadamu aliyetamauka
  Dhaifu alivyo kwa tumaini kukosa?
  Nani asiyejua kuwa bao
  Kimiani haliingii pasi ngome kusalitika?
  Tangu lini mechi kushindwa
  Kwa wingi wa mashambulizi?
  Hata ngome imara ni ushindi tosha!
  Najua watasema, “msikize huyo mwendawazimu
  Na kauli zake za kiwendawazimu.”
  Kwangu lililo muhimu ni kusikilizwa
  Maana maisha yenyewe ni wendawazimu.
  Kuna urazini gani kuifukuzilia pumzi
  Kama mtoto mdogo aliyepagawa?
  Kuna urazini gani kurushiana makonde lingoni
  Jasho kumwaga na damu kutoana?
  Na mtu asiye hasimu yako
  Kwa kusingizio cha burudani?
  Kuna urazini gani kujilimbikizia mali
  Ilhali mchapa kazi ananyongwa na njaa?
  Wendawazimu wangu daima unanituma
  Shindano la miereka kushabikia
  Uhayawani huo kushangilia kwa vicheko
  Maana
  Maisha na uhayawani
  Ni kama theluji na barafu
  Kwangu mimi mzaliwa wa hapa jangwani.
  (T. Arege)
  1. Maisha ni wendawazimu na uhayawani. Thibitisha kwa kutoa hoja tano kwenye shairi. (alama 5)
  2. Fafanua mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kuwasilisha ujumbe katika shairi hili. (alama 3)
  3. Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
  4. Bainisha aina mbili za urudiaji katika shairi hili. (alama 2)
  5. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
  6. Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
  7. Huku ukitoa mifano, eleza mbinu mbili ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika ubeti wa tano. (alama 2)
 7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  Ujana wa kisasa!
  Mtu akiwa kijana, hudhania hazeeki
  Mzee akimuona, kwake ni kama kisiki
  Anafikiri ujana, daima haufutiki
  Fahamu kamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  Ukimuona kijana, apita hatikisiki
  Mzee wakipishana, amuona kama dhiki
  Utadhania hapana, uzee haumfiki
  Fahamu kamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  Kuringia uvulana, ukaona iliki
  Na kusahahu kijana, uzee haukingiki
  Kwa kweli hiyo ni lana, nakwambia Ludoviki
  Fahamu kwamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  Huo wako usichana, ukiitwa huitiki
  Unapoitwa kwa jina, na mzee mamluki
  Wamuona ni kichana, hata nywele hazisuki
  Fahamu kamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  Umbo ulivyojazana, usiseme ni bureki
  Nyama hazitakunjana, na ngoziyo sio feki
  Wala haitavutana, mfano wa pulastiki
  Fahamu kamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  Si vyema kumtukana, mzee kwa chukichuki
  Akipita wamguna, useme hahesabiki
  Wewe ni mtu wa jana, hata ukungwi huoki
  Fahamu kamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  Walituambia sana, ujana haushikiki
  Si mwida hutauona, usambe hauponyoki
  Ukiponyoka ni shina, uzee umediriki
  Fahamu kamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  Sifurahi kuoana, ujana ukawa tiki
  Kuna mambo mengi sana, hupitia halaiki
  Amina Rabbi Amina, na Mola akubariki
  Fahamu kamwe hubaki, humo ndani ya ujana
  (Ludovick Mbogholi)
  1. Fafanua kwa kutoa hoja tano mtazamo wa nafsineni kuhusu ujana wa kisasa kwa mujibu wa shairi hili. (alama 5)
  2. Fafanua dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (alama 2)
  3. Eleza aina tatu za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
  4. Bainisha aina tatu za urudiaji zilizotumiwa kwenye shairi hili. (alama 3)
  5. Tambua nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
  6. Eleza umuhimu wa mbinu mbili ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika ubeti wa tano. (alama 2)
  7. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
  8. Andika ubeti wa saba katika lugha nathari. (alama 2)
 8. SEHEMU E: HADITHI FUPI
  A. Chokocho na D. Kayanda (Wah.): Tumbo Lisiloshinba na Hadithi Nyingine
  A. Chokocho: Tulipokutana Tena
  “Ingawa mimi nilikuwa kitoto cha miaka mitano, nilihisi siku ile ilikuwa mbaya kwangu.
  Siku tofauti kabisa katika maisha yangu.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Fafanua umuhimu wa mzungumzaji katika kuijenga hadithi hii. (alama 5)
  3. Eleza namna mbinu ya kinaya inajitokeza katika hadithi ya Shibe Inatumaliza. (alama 5)
  4. Hadithi, Mtihani wa Maisha inahimiza uwajibikaji. Jadili. (alama 6)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions - Maseno Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?