Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Cekenas Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

QUESTIONS

 1. LAZIMA
  Umekuwa msaidizi wa mbunge wa eneobunge la Mfanisi. Ungependa mbunge huyu apate nafasi ya kuwa mbunge wa eneobunge hili tena. Andika wasifu utakaochapishiwa wanaeneobunge ukieleza mchango wake katika sekta mbalimbali za eneobunge hilo.
 2. Eleza namna wananchi wanavyoonyesha uzalendo kwa nchi yao.
 3. Andika kisa kitakachoafiki maana ya methali: Mwota mchana hukosa mali na wana.
 4. Andika insha itakayoanza kwa maneno yafuatayo.
  Mahakama ilikuwa imejaa furifuri. Jamaa na marafiki walikuwepo. Nilisimama kizimbani. Mashahidi walikuwa wamekamilisha kutoa ushahidi wao. Jaji aliinua uso wake akaniangalia kwa ukali kisha...


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

Swali la 1 (Lazima).

 • Hii ni insha ya wasifu.
 • Sura ya wasifu idhihirike :
 1. Kichwa kinachotaja wasifu.
 2. Wasifu ni wa nani.
 3. Sehemu ya mwili iwe na :
  Sifa, tabia, tajriba ya mbunge.
 4. Maudhui tarajiwa kuhusu mchango  wa mbunge yajitokeze.
  Mchango wa mbunge unaweza kuhusu:
  1. Alivyoshughulikia sekta ya afya katika eneobunge na malengo mapya aliyonayo.
  2. Alivyoshughulikia maswala ya elimu na maono mapya kuhusu elimu.
  3. vitega uchumi k.v kilimo, ufugaji, madini, n.k.
  4. ufisadi utakavyoshughulikiwa.
  5. amani.
  6. utangamano, mawasiliano na uchukuzi.
  7. usalama wa eneobunge.
   Tanbihi- Mwanafunzi asipozingatia sura atolewe alama nne.
   Kuwepo kwa neno wasifu kama anwani/ kwenye anwani kwatosha.

Swali la pili.

 • Hili ni swali la maelezo.
 • Mtahiniwa aeleze majukumu ya mwananchi mzalendo kwa nchi yake.
 • Kila hoja iwe kwa aya yake.

Hoja zifuatazo zinaweza kujitokeza :

 1. Kuheshimu na kuwalinda wanachi wenzake
 2. Kuzingatia haki za wengine k.v kwa kutetea haki za walionyanyaswa na wasioweza kujitetea.
 3. Kuhimiza mshikamano/ umoja wa raia wote. K.m kutobaguana na kukashifu vitendo vya utengano k.v ukabila na mapendeleo.
 4. Kutokandamiza uhuru wa wengine.
 5. Viongozi wazalendo waunde na kuzingatia sera zinazolinda haki ya raia.
 6. Kutunza mazingira na turathi za kitaifa.
 7. Kuchagua  na kupigia kura viongozi waadilifu.
 8. Kupendekeza kuondolewa kwa viongozi waovu na wanaokandamiza haki za raia.
 9. Kupendekeza mabadiliko ya katiba.
 10. Kuhusika katika uundaji wa sera muhimu katikaa uongozi.
 11. Kuhakikisha kuwa katiba imetafsiriwa ipasavyo ili isitumiwe kukandamiza raia.
 12. Kulinda mipaka ya nchi.

Swali la tatu
Andika kisa kitakachoafiki methali hii.

 • Mwota mchana hukosa mali na wana.
 • Methali hii ina maana kuwa anayezembea hukosa mali na asiye na mali hawezi kuwa na familia.
 • Maana ya ndani ni kuwa yeyote asiyetia bidii katika kazi yake atakosa mali na vingine vyote vya kustarehesha na kukamilisha maisha yake.
 • Mwanafunzi asimulie kisa kinachoonyesha mhusika aliyekosa kutia bidii maishani akaishia kukosa vitu alivyotamani katika maisha na kugharamia maish yake kikamilifu. Anashindwa kukidhi mahitaji ya familia yake ipasavyo.
 • Mtahiniwa anaweza kutunga kisa cha mhusika aliyefahamu umuhimu wa kutia bidii na maisha yake yakatengenea: anaipa familia yake starehe za kila aina.

Swali la nne

 1. Hili ni swali la dondoo.
 2. Mtahiniwa aanze kisa kwa maneno aliyopewa.
 3. Mtahiniwa anaweza kusimulia kuhusu mhusika aliyepatikana na hatia, asimulie kuhusu maisha ya jela.
 4. Mhusika aliyepatikana na hatia anaweza akasimuliwa alivyojipata mahakamani.
 5. Mhusika wa kisa anaweza kuwa hana hatia akaachiliwa huru. Asimmulie maisha ya uhuru, uhusiano wake na walionshtaki na walioshuhudia au tahadhari aliyochukua.
 6. Mhusika asiye na hatia anaweza kuelezewa jinsi alivyojipata katika hali hiyo (mahakamani).
 7. Mtahiniwa pia anaweza akasimulia hali kabla ya kushtakiwa na baada ya hukumu katika kisa kimoja.
 8. Mwanafunzi asipoanza kwa dondoo hajapotoka, amepungukiwa kimtindo akadiriwe alivyotimiza matarajio ya swali pamoja na vipengele vingine vya utahini.

USAHIHISHAJI NA UTUZAJI
Mtahini aisome insha ya mwanafunzi kwa kuzingatia.

 1. Maudhui.
 2. Msamiati
  • Tamathali.
  • Visawe.
  • Msamiati usio wa kawaida kimatumizi.
 3. Sarufi.
 4. Hijai/tahajia.
 5. Muundo
  1. sura.
  2. Muundo - Mpangilio wa aya.
   Sura ya kazi.
 6. Mtindo- Upekee wa matumizi ya lugha kwa ubunifu.
 7. Urefu.
  • Maneno chini ya 174 asizidi alama 5.
  • 175-274 nusu – asizidi alama 10.
  • 275-374 robo tatu asizidi alama 15.
  • 375-400 Kamili mwenye ukomavu wa lugha apewe zake.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Cekenas Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?